Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1110 | 1111 | (Page 1112) | 1113 | 1114 | .... | 3272 | newer

  0 0


  0 0

  Ridhione Senga (wa pili kushoto) ambae ni Mwenyekiti wa Madereva wa Daladala wanaofanya shughuli zao katika barabara ya Bugarika-Mzunguko Jijini Mwanza, jana akilalamikia suala la uwepo wa tax bubu linalowasumbua katika shughuli zao.

  Alisema licha ya madereva wa tax bubu wanaobeba abiria kama daladala katika eneo wanalofanyia kazi hususani kubeba abiria wanaoenda na kutoka katika hospitali ya Rufaa ya Bugando kuzuiliwa, bado madereva hao wa tax bubu wameendelea na biashara hiyo kama kawaida.

  Senga alibainisha kwamba hatua hiyo inawaweka katika wakati mgumu katika kutimiza majukumu yao kutokana na kupata hasara kila kukicha ambapo amesema ikiwa itaendelea wataitisha mgomo ili kushinikiza kilio chao kufanyiwa kazi.

  "Sisi tunalipa mapato, lakini jambo la ajabu hawa madereva wa tax bubu ambao hawana leseni ya kubeba abiria wamekuwa ndio wanafanya kazi ya daladala licha ya kupigwa marufuku katika kikao tulichokaa ijumaa iliyopita baina ya Sumatra, halmashauri ya Jiji, Polisi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza pamoja na wawakilishi wengine bila kuwasahau viongozi wa daladala na tax. Kama hali hii itaendelea tutafanya mgomo hapa na hakuna huduma yoyote ya kubeba abiria itakayotolewa".Alisema Senga.

  Ramadhan Idd ambae ni Kaimu Mwenyekiti wa Madereva wa daladala za Bugarika-Muzunguko Jijini Mwanza aliunga mkono hoja ya mwenyekiti huyo na kusema kuwa ikiwa mamlaka husika zitashindwa kutatua suala la tax bubu katika eneo hilo, wao watachukua hatua ya kusitisha huduma ya usafirishaji katika barabara hiyo ya Bugarika-Buzuruga.

  "Hizi tax bubu tunasikia ni za wakubwa na ndiyo maana hawa madereva wanaoziendesha wana jeuri mno. Sisi tunasema haya ni majipu na tunawaomba viongozi wengine wakubwa akiwemo Mhe.Magufuli, waangalie huku Jijini Mwanza maana kuna majipu makubwa ya kutumbua".Alisema Athuman Bin Malick ambae ni mmoja wa madereva wa daladala za Bugarika-Mzunguko Jijini Mwanza.

  Kaptaini Michael Rogers ambae ni Afisa Mfawidhi wa Sumatra Mkoani Mwanza, ameshauri suala hilo kutatuliwa na jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kwa kuwa ndilo lenye jukumu la kukamata vyombo vya usafiri vinavyofanya kazi kwa kukiuka sheria na taratibu zilizoweka na mamlaka husika ikiwemo halmashauri ya Jiji Mwanza ambayo ndiyo inasimamia taratibu la utendaji kazi wa tax.

  Juhudi za kuwatafuta madereva wa tax hizo zinazodaiwa kufanya kazi kinyume cha sheria (tax bubu) bado zinaendelea ili kujua kuzungumzia malalamiko yanayowakabiri.
  Ramadhan Idd ambae ni Kaimu Mwenyekiti wa Madereva wa daladala za Bugarika-Muzunguko akitoa malalamiko yake.
  Athuman Bin Malick ambae ni mmoja wa madereva wa daladala za Bugarika-Mzunguko Jijini Mwanza.
  Kulia ni Kaptaini Michael Rogers ambae ni Afisa Mfawidhi wa Sumatra Mkoani Mwanza akitoa ufafanuzi wake.

  Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo

  0 0
 • 02/01/16--23:30: DIRA YA DUNIA YA BBC SWAHILI

 • 0 0

  Afisa Mkuu wa Fedha wa benki ya Exim Tanzania Bw. Selemani Ponda (katikati) akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati akitoa taarifa ya mapato ya benki hiyo katika kipindi cha mwaka uliopita. Wengine ni NaibuAfisa Mkuu wa Fedha wa benki hiyo Bw. Issa Hamisi (kulia) na Mkaguzi Mkuu wa ndani wa hesabu za benki hiyo Bw. George Binde


  BENKI ya Exim Tanzania imetangaza kupata faida ya sh. bilioni 35.3 (kabla ya kodi) kwa mwaka ulioipita 2015, sawa na ongezeko la faida kwa asilimia 46 ikilinganishwa na mwaka 2014 hatua iliyochagizwa  na ufanisi wa benki hiyo katika usimamizi mizania.

   “Kwa kuangalia hali halisi ya changamoto mbalimbali katika masuala ya kifedha ikiwemo masuala ya riba sambamba na kuporomoka kwa thamani ya shilingi kwa muda wote, mafanikio haya tunayaona kuwa ya kuridhisha,’’ alisema Afisa Mkuu wa Fedha wa benki hiyo Bw Selemani Ponda alipokuwa akitoa ripoti  ya awali (kabla ya ukaguzi) ya benki hiyo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.

  Alisema katika kipindi hicho faida kwenye riba ilikuwa kwa asilimia 28 na kufika sh. Bilioni 73 ikilinganishwa na kiasi cha sh. 57 kilichopatikana katika kipindi kama hicho kwa mwaka uliopita. Ongezeko hilo limechagizwa na mkazo wa benki hiyo katika amana za gharama nafuu, wingi wa matawi ya benki hiyo pamoja na usimamizi mzuri wa mizania.

  Zaidi, tozo mbalimbali za huduma za kibenki katika kipindi cha mwaka ulioipita kiliongezeka kwa asilimia 25 hadi kufikia sh bilioni 50, kutoka sh bilioni 40 kilichopatikana mwaka uliopita.Ongezeko hilo pia lilichagizwa na  faida katika biashara ya kununua na kuuza fedha za kigeni pamoja na mapato mengine ya ada kutokana na ufanisi katika utoaji huduma kwa wateja wakubwa na wale wa kati.

  Jumla ya mapato yatokanayo na uendeshaji yaliongezeka kwa asilimia 29 hadi kufikia sh. Bilioni 95 yakibebwa na ukuaji mkubwa kwenye ada pamoja na kamisheni ambayo ilikuwa asilimia 29 kutoka sh bilioni 24 hadi sh. Bilioni 31 kwa mujibu wa Bw Ponda huku akiongeza kuwa katika kipindi hicho gharama za uendeshaji wa benki hiyo zilikuwa kwa asilimia 20 na kufikia sh. Bilioni 80.

  Benki tanzu zilizopo nje nchini Djibouti na Comoro zimeendelea kufanya vizuri na kuchangia asilimia 4 ya faida tofauti na mwaka jana zilileta hasara kwa ujumla wao. Djibouti imefanya vizuri kulinganisha na mwaka uliopita kwa kupata faida ya Sh bilioni 1.2. “Tunategemea benki hizi tanzu kufanya vizuri zaidi mwaka 2016” aliongeza  mkuu huyo wa fedha.

  Bw Ponda aliongeza kwamba katika kujiongezea mtaji wa biashara na ushirikishaji wa wawekezaji wote nchini (financial inclusion), benki hiyo hivi karibuni ilizindua uuzaji wa dhamana za muda mrefu (hati fungani) ambapo hadi uuzwaji wa hati hizo unafungwa rasmi Disemba 18 mwaka 2015 benki hiyo ilikuwa imefanikiwa kukusanya kiasi cha sh bilioni 19.7 kutokana na mauzo ya hati hizo tofauti na makadirio ya sh. Bilioni 10 iliyokuwa imejipangia kukusanya hapo awali. Benki ya Exim imekuwa taasisi ya kwanza kuzindua dhamana ya muda mrefu ikilenga wawekezaji wadogo, wakati na wakubwa.

  “Pia ni katika mwaka uliopita tumezindua kituo chetu kipya cha  huduma  kwa wateja kwa njia ya mawasiliano ya simu ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha huduma zetu kupitia teknolojia ya mawasiliano,’’

  “Exim tunaahidi kuendelea na muelekeo huu ulio sahihi kwetu na kwa wateja wetu  katika kutimiza malengo yetu. Ripoti hii inaonyesha kuwa mwaka uliopita ulikuwa na mafanikio makubwa na ya kujivunia,’’ alisema Bw Ponda huku akiwapongeza wafanyakazi na wadau wote waliochangia mafanikio hayo.

  0 0

  Leo ni siku ya kuzaliwa ya Saleh Ally, mchambuzi na mwandishi mkongwe wa michezo nchini Tanzania ambaye kwa sasa ni Mhariri Kiongozi wa Magazeti ya Championi yanayomilikiwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd na Mmiliki wa Blog  ya Saleh Jembe.

  Saleh Ally amefanya mengi katika ulimwengu wa michezo na burudani ambapo amesharipoti michuano mbalimbali mikubwa ikiwemo Kombe la Dunia na pia amesafiri katika nchi nyingi za mabara tofauti akifanya kazi hiyo.

  Kazi zake nyingi nzuri zimekuwa hamasa kwa waandishi wengi ambapo amekuwa kioo ‘role model’ kwa wengi wao. Tunamtakia kila la kheri katika maisha yake yote na Mungu ampe baraka nyingi.

  Happy birthday Saleh Ally


  0 0

   Msanii mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Star Mayunga Malini (Kulia) akiongea na wadau wa Sanaa (hawako pichani) mapema wiki hii kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA). Wengine katika picha ni Afisa Habari wa BASATA, Aristides Kwizela (Katikati) na Afisa Sanaa wa Baraza hilo Augustino Makame.
   Msanii Mayunga Malimi akiimba wimbo wake wa Nice Couple sambamba na mkongwe wa muziki wa dansi nchini Kassim Mapili kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa mapema wiki hii.
   Msanii mkongwe wa Sanaa za Maonesho Nkwama Ballanga akimpongeza Msanii Mayunga kwa juhudi zake na kujituma katika kazi anazofanya. Wadau wengi wa Sanaa waliohudhuria kwenye programu ya Jukwaa wiki hii walifurahishwa na juhudi binafsi za Msanii Mayunga.
  Sehemu ya wadau wa Sanaa waliohudhuria programu ya Jukwaa la Sanaa wakimfuatilia kwa makini Msanii Mayunga.  


  WASANII WATAKIWA KUKATAA RUSHWA KWENYE KAZI ZAO
  Wasanii nchini wametakiwa kujituma na kutengeneza kazi za Sanaa zenye ubora na kuachana na dhana ya kutegemea rushwa na hongo katika kuyafikia mafanikio yao kisanaa.
  Wito huo umetolewa mapema wiki hii na wadau wa Sanaa kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa ambayo huandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na kufanyika kwa mwezi mara mbili siku ya Jumatatu kwenye ukumbi wa Baraza hilo.
  Wakizungumza kwa nyakati tofauti wadau hao walisema kwamba kumekuwa na wimbi la wasanii na mameneja wa wasanii kutegemea rushwa za fedha na wengine kufikia hatua kutoa rushwa za ngono ili kufanikiwa kisanaa hasa katika kuvishawishi vituo vya radio na televisheni kucheza nyimbo zao.
  “Ukweli ni kuwa rushwa na hongo zinaendekezwa na wasanii walioshindwa. Msanii anayejitambua hawezi kutoa rushwa ili wimbo wake uchezwe. Lazima wasanii waachane na dhana hii potofu, waelewe kwamba kazi ya Sanaa iliyo bora itapendwa tu na kukubalika na jamii” alisema Nkwama Bhallanga ambaye ni Msanii wa Sanaa za Maonesho.
  Kwa upande wake Katibu wa chama cha wachezesha disko (TDMA) Asanterrabi Mtaki alisema kuwa dhana kwamba wasanii lazima wahonge watangazaji au ma DJs ili nyimbo zao zichezwe ni potofu na ni chanzo cha kutangaza muziki au kazi za Sanaa zisizo bora na kuziacha zile zenye ubora.
  “Kama wimbo wako ni mzuri kwa nini uhonge au utoe rushwa ili uchezwe? Hapa ndipo tatizo la kuendekeza kazi mbovu za Sanaa linapoanzia. Muziki wa wenye fedha na wanaohonga ndiyo unasikika, ule mzuri unaondaliwa na wasanii wasiyo na uwezo haupati nafasi” alisema Mtaki.
  Alitoa wito kwa wasanii kufikiria njia mbadala za kutangaza nyimbo zao hasa kumbi za disko badala ya kutegemea vituo vya radio pekee.
  Awali akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa, Msanii na mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Star Mayunga Malini alisema kuwa wasanii hawana budi kujituma, kutafuta fursa na kuzitumia ipasavyo hasa kwa kutumia muda mwingi kubuni kazi zenye ubora.
  Aliongeza kuwa, wasanii hawana budi kuachana na dhana ya utegemezi na kutegemea fedha na hongo katika kupata mafanikio kwani kazi za Sanaa zikitengenezwa kwa ubora na kwa kuzingatia vigezo vyote zitapendwa na kutuzwa tu.

  0 0

  Kamanda Liberatus Sabas, alipokuwa akifunga Kampeni za ABIRIA PAZA SAUTI, Jijini Arusha,

   Na Vero Ignatus wa Wazalendo 25 Blog, Arusha.
  Jeshi la polisi mkoa wa Arusha limewataka watu wote wanaomiliki silaha kwa njia halali wafike kwenye kituo cha polisi kuhakiki silaha zao na kuzilipia kama inavyostahili na kwa kufuata utaratibu kama sheria inavyoagiza. 
   Hayo yamesemwa na Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas, na kufafanua kwamba kila mwaka huwa kila mwenye silaha anafika polisi na silaha yake na vitabu vyake kwa ajili ya kuihahiki na kuilipia kama inavyostahili. 
  Pia inaangaliwa  kama zipo tuhuma zozote kutokana na matumizi ya silaha hiyo  itasimamishwa kwa ajili ya taratibu zingine na kunyang’anywa hadi hapo jeshi litakapojiridhisha kuwa silaha hiyo matumizi yake ni sahihi ama siyo sahihi 
   Kamanda Sabas amesema utaratibu huu huwa unaratibiwa na makao makuu ya jeshi la polisi kwa ajili ya kuhakiki silaha, ikiwa ni pamoja na kulipia mapato ya serikali ,amewataka watu wanaomiliki silaha wafuate masharti yake kama inavyotakiwa. Amesema sheria inambana kila mtu mara anapotenda kosa ,na kama mtu akiitumia ndivyo sivyo atanyang’anywa silaha kwa kutumia sheria iliyowekwa. 
  Ameongeza kuwa wapo watu ambao wamewatishia silaha wenzao,na wengine kesi zao zipo tayari na zingine zimefutiwa umiliki kwa mujibu wa sheria.
  Kamanda huyo amesema kimsingi kabla mtu hajakabidhiwa silaha ili amiliki, yapo masharti ya kufuata na yapo kwenye kitabu kile cha leseni anachopewa wakati wa umiliki, na kwamba akienda kinyume na  hayo masharti huna sifa ya kumiliki silaha. 
   Kamanda Sabas ametoa anagalizo kwa wamiliki wa silaha na kusema kuwu silaha ya moto siyo kama panga,silaha hiyo ukiifanyia kosa mara moja yaweza kuua mtu au watu hivyo amewataka kuwa makini sana katika ufuatiliaji wa umiliki, pamoja na namna zinavyotunzwa,amesema jeshi la polisi lipo makini kufuatilia kwa ukaribu wakithibitisha silaha haitunzwi kama inavyostahili utanyang’anywa.aidha amesema kwa wazee amabao umri wao umeenda nab ado wanamiliki silaha huwa wanaichukua na kuihifadhi . 
  Amehitimisha kwa kusema kuwa kila , mtu anayetaka kumiliki silaha, lazima kwanza akapitia kwenye kamati za ulinzi na usalama kuanzia kwenye kata, Wilaya, na Mkoa ambako wanamuidhinisha kuwa na silaha afuate masharti na kuitunza silaha isije ikaangukia kwenye mikono ya wahalifu wakaitumia isivyo halali sheria itafuata mkondo wake.
  Silaha huwa zinatakiwa kulipiwa kila mwaka kuanzia mwezi julai hadi septemba ukichelewa kulipia unapigwa penati kwa mujibu wa sheria.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel ameitumia salamu za Rambirambi familia ya Mzee Dellan Tarmo kufuatia kifo cha  kijana wao mpendwa Jovitha Dellan kilichotokea kwa ajali ya gari mkoani Arusha juzi tarehe 31.1.2016.  “Pokea rambirambi zangu za dhati, sote kwa pamoja tumepoteza kijana  mchapakazi, hodari na aliyependa kushirikiana na wenzake katika kazi zake, hakika tutamkumbuka siku zote” Katibu Mkuu amesema.  Katibu Mkuu, Pia amemtumia salamu za pole kwa Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu(KBF) na Wafanyakazi wote wa Bodi ya  Filamu Tanzania.

  “Nimepokea taarifa za kifo cha Jovitha Dellan kwa huzuni kubwa, najua machungu na maumivu mliyonayo kwa kuondokewa na kiungo muhimu katika utendaji wenu, poleni sana,  niko nanyi katika msiba huu mzito kwenu”, amesema Katibu Mkuu huyo.  Katibu Mkuu amesema pamoja na kwamba kifo hakiepukiki, bado ni kitu ambacho kinashtua, kuhuzunisha na kuleta unyonge mkubwa kwa wafiwa katika jamii.

   “Naungana nanyi katika kipindi hiki kigumu kumuombea kijana wetu Jovitha Dellan ili mwenyezi Mungu ampe mapumziko mema ya Milele” Mwenyezi Mungu awatie nguvu, awape uvumilivu na subira katika kipindi hiki”.

  “Niko nanyi katika kipindi hiki kigumu kwa hali na mali, nawaomba msijisikie wapweke” Katibu Mkuu amesema na kuwatakia utulivu na amani katika kipindi hiki cha msiba mkubwa kwa familia.  Marehemu Jovitha Dellan  amefariki juzi tarehe 31 Januari, 2016 mkoani Arusha ambapo alikuwa njiani kurejea kazini jijini Dar es salaam.

            Marehemu Jovitha Dellan anatarajiwa kuzikwa wiki hii mkoani Manyara.

            Jovitha Dellan alikuwa ni Afisa Utamaduni aliyekuwa akifanya kazi katika Bodi ya Filamu Tanzania iliyopo chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

  Mungu ailaze Roho ya Marehemu 
  Jovitha Dellan mahali Pema Peponi - Amina.


  Imetolewa na:

  Idara ya Habari(MAELEZO)

  DSM.
  2 Februari, 2016


  0 0

  Meneja Masoko wa Airtel Bi Anethy Muga akionyesha moja ya tangazo la ongezeko la muda wa masaa ya vifurushi vya Airtel yatosha wakati wa kutangaza muda mpya wa kuisha kwa vifurushi vya Airtel yatosha kwa siku kuwa ni masaa 25. Yaani masaa 24 ya siku ongeza saa moja.

  · Wateja wa Airtel waongezewa muda kufaidi zaidi katika vifurushi vya Airtel Yatosha

  AIRTEL Tanzania imeendelea kutimiza dhamira yake ya kujali wateja wake kwa kuboresha vifurushi vyake vya huduma ya Airtel Yatosha hivyo kuvifanya kuwa bora, vya ushindani na gharama nafuu nchini.

  Akiongea kuhusu kuboreshwa kwa huduma hiyo, Meneja Masoko wa Airtel Bi, Aneth Muga alisema "huduma yetu ya Airtel Yatosha inaendelea kukidhi mahitaji ya Wateja wetu kwani vifurushi tunavyotoa sasa vya Airtel Yatosha vya siku kwa shilingi 500 tumeongeza muda wake wa kutumika zaidi ukilinganisha na vifurushi vingine vinavyotolewa sokoni

  Bi. Muga alisema sambamba na hili vifurushi vya Airtel Yatosha vinamuwezesha mteja kupiga simu kwenda mtandao wowote ule nchini wakati wowote masaa 25 yaani mteja anafaidika na vifurushi hivi kwa masaa 24 na 1 la nyongeza.

  Kikubwa na kizuri zaidi bado pia mteja anapojiunga na vifurushi hivi anapata nafasi ya kuingia kwenye droo ya promosheni yetu kabambe ya Airtel Mkwanjika na kujishindia pesa taslimu hadi sh. Milioni moja"

  Kujiunga na vifurushi mbalimbali vya Airtel yatosha mteja anatakiwa kupiga *149*99# na kisha kuchagua kifurushi kinachokithi mahitaji yake. Airtel yatosha inapatikana katika vifurushi vya siku, wiki au mwezi.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe Angella Kairuki akijibu maswali toka kwa wabunge katika kikao cha 6 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
   Picha na raymond Mushumbusi MAELEZO.


  (Na Raymond Mushumbusi-MAELEZO)
  SERIKALI imejipanga kuborsha zaidi mpango wa kunusuru Kaya masikini nchi ujulikanao kama TASAF kwa awamu ya tatu kwa kutengeneza miundombinu mizuri ya kutambua Kaya zinazolengwa na kuondoa malalamiko ya wananchi kuwa mpango huu umekuwa ni wa Kaya chache na fedha hizo utolewa kwa upendeleo.

  Akijibu swali la Mhe.Magdalena Hamisi Sakaya Mbunge wa Kaliua (CUF) lililouliza ni vigezo gani vinatumika kuondoa Kaya zilizopendekezwa kwenye mradi na kubakiza Kaya chache, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki amesema mpango wa kunusuru Kaya maskini hutambulishwa kijijini na wataalam kutoka Halmashauri husika kwa kusimamiwa na uongozi wa kijiji kisha kuweka vigezo vya Kaya maskini.

  “ Wakusanya taarifa huchaguliwa kutoka miongoni mwa vijana wanaoishi kijijini hapo na kupitia nyumba kwa nyumba kuorodhesha Kaya ambazo zinakidhi vigezo vilivyoanishwa na mkutano wa Kijiji ila bado kuna malalamiko yanayotolewa kuwa Kaya maskini zinaachwa na kupewa Kaya nyingine ambazo sio maskini kwa kuliona tatizo hilo suala hili tunalifanyia uchunguzi na tunaomba watu watoe taarifa ikiwa wataona ukiukwaji wa uorodheshaji wa Kaya zitakazohusika na mpango huu ili hatua ziweze kuchukuliwa dhidi ya yoyote atakaye bainika kufanya hivyo”

  “ Mpaka sasa kutokana malalamiko yaliyojitokeza katika kuorodhesha Kaya maskini zinazotakiwa kuwezeshwa na mpango huu tumewaajibisha watendaji toka Wilaya za Karagwe, Kagera na Kibondo, Kigoma na tuomba kupewa taarifa kwa sehemu yoyote ambapo kutatokea tatizo kama hili na tutachukua hatua mara moja kuokoa fedha zilizotakiwa kwenda kusaidia watu husika” Alisema Mhe Angella Kairuki.

  Aidha Mhe. Angella Kairuki ameongeza kuwa kuna taarifa zinazoenezwa kuwa fedha za mpango wa TASAF Awamu ya Tatu ni fedha za freemasons, taarifa hizo sio za kweli kwani fedha hizi zizantolewa na Serikali ili kusaidia Kaya maskini ili ziweze kujikwamua kiuchumi kwa kuweza kupata Elimu Malazi na chakula bora.

  TASAF ni mpango wa kunusuru Kaya maskini na imekuwa katika awamu tatu mpaka hadi sasa kwa ajili ya kuwezesha Kaya maskini kujikwamua kiuchumi.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
  JESHI LA POLISI TANZANIA.
  TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

  “PRESS RELEASE” TAREHE 02.02.2016.
  · WAZEE WAWILI WAMEUAWA KIKATILI WILAYANI KYELA MKOANI MBEYA KUTOKANA NA IMANI ZA KISHIRIKINA.

  · MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MAPAMBANO JIJINI MBEYA AFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI.

  · MWENDESHA PIKIPIKI AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI ILIYOHUSISHA GARI KUGONGANA NA PIKIPIKI.

  KATIKA TUKIO LA KWANZA:
  WAZEE WAWILI WAKAZI WA KITONGOJI CHA BULINDA WILAYA YA KYELA MKOANI MBEYA WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. GENELI KAPWELA [65] NA 2. RAHABU BUNGULU [70] WALIUAWA KWA KUKATWA NA VITU VYENYE NCHA KALI SEHEMU MBALIMBALI ZA MIILI YAO NA KISHA KUCHOMWA MOTO NA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI.

  MIILI YA MAREHEMU ILIKUTWA KATIKA NYUMBA WALIMOKUWA WAKIISHI MNAMO TAREHE 01.01.2016 MAJIRA YA SAA 08:00 ASUBUHI HUKO KITONGOJI CHA BULINDA, KIJIJI/KATA YA MATEMA, TARAFA YA NTEMBELA WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA.

  KATIKA TUKIO HILO, GENELI KAPWELA ALIUAWA KWA KUTENGANISHWA KICHWA NA KIWILIWILI NA KUKATWA MKONO WA KUSHOTO NA VIUNGO HIVYO HADI SASA HAVIJULIKANI VILIPO NA RAHABU BUNGULU ALIUAWA KWA KUCHOMA NA KITU CHENYE NCHA KALI NA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI.

  INADAIWA KUWA, WANANCHI HAO WALIVAMIA NYUMBA WALIYOKUWA WAKIISHI MAREHEMU KISHA KUWAKATA NA VITU VYENYE NCHA KALI NA BAADA YA KUTEKELEZA MAUAJI HAYO, WATU HAO WALIANGUSHA NYUMBA WALIYOKUWA WAKIISHA AMBAYO ILIKUWA IMEJENGWA KWA MIANZI NA KISHA KUICHOMA MOTO.

  CHANZO CHA TUKIO HILO NI IMANI ZA KISHIRIKINA KWANI MAREHEMU WALIKUWA WANATUHUMIWA KULETA UGONJWA WA KIPINDUPINDU KIJIJI HAPO KWA NJIA ZA KISHIRIKINA. WATU WAWILI WAMEKAMATWA KWA MAHOJIANO KUHUSIANA NA TUKIO HILO AMBAO NI 1. ALIKO MWAMTOBE [47] MKAZI WA MATEMA NA 2. ALISOLOMON MWAMTOBE [49] MKAZI WA KITONGOJI CHA BULINDA. 

  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA KWANI ZINA MADHARA MAKUBWA KATIKA JAMII.

  KATIKA TUKIO LA PILI:
  MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MAPAMBANO ILIYOPO JIJINI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FELISTA MWANSASU [12] AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.949 CVS AINA YA MITSUBISHI FUSO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA NSAJIGWA ALISALA [39] MKAZI WA MBEYA.

  TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 01.01.2016 MAJIRA YA SAA 07:50 ASUBUHI HUKO MAENEO YA MAFIATI, KATA YA MUUNGNANO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA. 

  CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. DEREVA AMEKAMATWA, UPELELEZI UNAENDELEA.

  KATIKA TUKIO LA TATU:
  MWENDESHA PIKIPIKI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ASIFIWE MWANTOBE [25] MKAZI WA TUNDUMA MKOANI MBEYA AMEFARIKI DUNIA BAADA YA PIKIPIKI ALIYOKUWA AKIENDESHA KUGONGANA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 975 CPS AINA YA TATA BUS LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA EMANNUEL ADAM [36] MKAZI WA MBEYA.

  TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 01.01.2016 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI HUKO MAPOROMOKO KATIKA BARABARA YA TUNDUMA/MBEYA, WILAYA MOMBA, MKOA WA MBEYA.

  INADAIWA KUWA, MARA BAADA YA AJALI HIYO PIKIPIKI ALIYOKUWA AKIENDESHA MAREHEMU ILITOROSHWA NA WATU WASIOJULIKANA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA WA BASI AMEKAMATWA NA UPELELEZI UNAENDELEA.

  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUFUATA NA KUHESHIMU SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA KUWA MAKINI KATIKA MATUMIZI YA BARABARA HASA KWA KUFUATA SHERIA ZA BARABARANI.

  Imesainiwa na:
  [AHMED Z. MSANGI – SACP]
  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

  0 0

  LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania bara mzunguko wa 17 unatarajiwa kuendelea kesho Jumatano kwa michezo sita kuchezwa katika viwanja mbalimbali, huku kila timu ikisaka pointi tatu muhimu kwenye msimamo wa ligi hiyo.

  Kesho Jumatano, Simba SC watakua wenyeji wa maafande wa Mgambo Shooting kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, JKT Ruvu watawakaribisha Mbeya City katika uwanja wa kumbukumu ya Karume Ilala, huku Mtibwa Sugar wakicheza dhidi ya Toto Africans katika uwanja wa Manungu – Turiani.

  Jijini Mbeya, Tanzania Prisons watakua wenyeji wa vinara wa ligi hiyo Young Africans katika uwanja wa Sokoine, Wana kimanumanu African Sports watacheza dhidi ya Mwadui FC uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, huku wakata miwa wa Kagera Sugar wakiwakaribisha Majimaji FC katika uwanja wa Kamabarage mjini Shinyanga.

  Alhamisi ligi hiyo itaendelea kwa kuchezwa mchezo mmoja tu, Wagosi wa Kaya Coastal Union watawakaribisha Ndanda FC katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

  Michezo ya viporo ya Azam FC imepangiwa ratiba, mchezo dhidi ya Tanzania Prisons utachezwa Februari 24 uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, huku mchezo dhidi ya Stand United ukichezwa Machi 16 katika uwanja wa Azam Complex.

  0 0


  0 0
 • 02/02/16--05:00: Matukio Bungeni leo.
 •  Naibu Spika Mhe.Dkt Tulia Ackson akiingia Bungeni tayari kuongoza Kikao cha 6 cha Mkutano wa pili wa Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
    Naibu Spika Mhe.Dkt Tulia Ackson akimwapisha Mhe. Balozi Dkt Augustine Maiga.
   Baadhi ya wageni wakifatilia Kikao cha 6 cha Mkutano wa pili wa Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
  Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Kanali Samuel Nzoka (kulia) akipokea moja kati ya mashuka 170 yaliyotolewa juzi na Meneja wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya (NHIF) wa mkoa wa Manyara, Isaya Shekifu (kushoto) kwenye uzinduzi wa uhamasishaji wa kujiunga na mfuko wa afya ya jamii CHF.

  Na Woinde Shizza,Manyara.
  MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Manyara, umekabidhi mashuka 170 kwenye zahanati ya Kijiji cha Engusero na hospitali ya wilaya ya Kiteto kwa ajili ya kutumiwa kujifunika na wagonjwa wanaofika kulazwa.

  Mashuka hayo yalikabidhiwa kwa mkuu wa wilaya hiyo Kanali Samuel Nzoka na meneja wa NHIF wa mkoa huo Isaya Shekifu, kwenye uzinduzi wa uhamasishaji wa kujiunga mfuko wa afya ya jamii (CHF) uliofanyika juzi kijiji cha Engusero.

  Akizungumza wakati akipokea mashuka hayo Kanali Nzoka aliushukuru mfuko huo na kuzitaka kaya za eneo hilo kujiunga na CHF ili wajipatie matibabu kwa mwaka mzima kwani kaya moja yenye watu sita italipia sh10,000.

  Alisema tatizo la ukosefu wa dawa kwenye zahanati, vituo vya afya na hospitalini litamalizika, endapo kaya nyingi zikijiunga na CHF kwani serikali nayo itaweka mkono wake ili kuhakikisha huduma za afya zinaboreshwa.

  Wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo Kanali Nzoka alijitolea sh20,000 kwa ajili ya kuzilipia kaya mbili za watu 12 wa kijiji cha Engusero na Dosidosi na kuungwa mkono na viongozi wanne wa wilaya hiyo waliojitolea sh10,000 kwa kila mmoja.

  Kwa upande wake, Shekifu alisema mwanachama wa CHF atanufaika na huduma zote za afya za msingi za kinga na tiba zitolewazo katika zahanati, kituo cha afya na hospitali ikiwemo huduma za wagonjwa wa kutwa na kulazwa.

  Alitaja huduma nyingine ambazo zitatolewa kwa mwaka mmoja kwa kuchangia sh10,000 ni vipimo vya maabara, upasuaji kulingana na utaratibu uliowekwa na halmashauri husika na wanachama kupata huduma bora ya afya.

  “Pia watapata huduma ya upasuaji kulingana na utaratibu uliowekwa na Halmashauri zinazoendesha mifuko hii zinapata mapato ya tele kwa tele kutoka serikalini ambayo yatatumika kuboresha huduma za afya,” alisema.

  Ofisa uratibu na matokeo wa CHF, Nicholaus Mwangomo alisema mpango huo ulianzishwa kwa sheria namba moja ya mwaka 2001 sura ya 409 ya sheria ya Tanzania toleo la 2002 wa kaya au familia kuchangia gharama za matibabu kabla ya kuugua.

  Mwangomo alisema sababu za kuanzishwa CHF ni kuiwezesha jamii kumiliki huduma za afya zinazowahusu katika maeneo wanayoishi, kuchangia huduma za afya kwa wananchi na kuboresha huduma za matibabu kwa utaratibu rahisi.

  0 0

   Alama zinazotoa tahadhali kwa watumiaji wa barabara hii wakiwa wakiwa wamewekewa tahadhali kwaajili ya kuvunjwa kwa gharofa la Ghorofa 16 lililopo mtaa wa Indra Ghandi jijini Dar es Salaam.
  Mafundi wakiwatoa vyuma kupisha ubomoaji wa jengo la ghorofa 16 lililopo katika mtaa wa Indra Ghandi jijini Dar es Salaam. 
  Jengo la Ghorofa 16 linaloandaliwa kwaajili ya kubomoa.
  Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemteua Bwana Masanja Kungu Kadogosa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), ambako anakwenda kuchukua nafasi ya Mhandisi Elias Mshana ambaye anastaafu hivi karibuni.

  Kabla ya Uteuzi huo Bwana Masanja Kadogosa alikuwa Mkurugenzi Idara ya Mikopo Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB). Uteuzi huo unaanza mara moja.

  Imetolewa na;
  Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
  02 Februari, 2016.  0 0

  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwenye Ofisi ndogo ya CCM Lumumba jijini Dar es salaam leo Februari 02, 2016 wakati Makamu wa Rais alipotembelea katika Ofisi hiyo.
   (Picha na OMR)

  0 0

  The late Mama Bridget Ann Constance Ramadhani

  Today marks exactly one year since she departed from this world. A year spent trying to cope and adjust to a life without her; words cannot express the pain, the sorrow, the emptiness that she left behind.
  The family of the late Mama Bridget Ann Constance Ramadhani (pictured above), mother to Judge Augustino Ramadhani, Mwalimu Henry Ramadhani, Mrs. Maud (Ramadhani)Mzuka, Ms. Mary Ramadhani and Bridget Ramadhani, wishes to express our sincere gratitude  to all our neighbours, relatives, friends and well-wishers who surrounded us with love and care during the difficult period of bereavement.

  We have been deeply touched by all of you who have extended to us immeasurable support both morally and financially. Your acts of kindness and generosity made our burden more bearable. Since we may not be able to mention each one of you by name, we solemnly request each one of you to accept this appreciation note as our humble expression of deep gratitude and special recognition. May God bless you all!

  We have lost a confidant and trusted friend, an anchor of hope and a pillar of advice, dutiful grandmother, caring auntie a nd great mother to the family. Her death has left us with heartaches that no one can heal, but her devoted love leave treasured memories no one can ever steal.

  It is humane to grief over a loss of a loved one. But, it is the Will of God that all mortal bodies are laid aside, when the soul is to embrace the Kingdom of God and enter into real life of eternity. We deeply miss you MAMA.

  Please join us to a year’s thanksgiving mass to be held on 
  Saturday, February 6th, 2016 from 9.00am at Holy Family Church (new church which is under construction), Kimara King’ongo in Dar es salaam.

  MAMA, in God’s hands you rest, in our hearts you will live forever!


  May the Lord continue to rest you in Eternal Peace, Amen!


  0 0


older | 1 | .... | 1110 | 1111 | (Page 1112) | 1113 | 1114 | .... | 3272 | newer