Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1105 | 1106 | (Page 1107) | 1108 | 1109 | .... | 3286 | newer

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI

  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
  JESHI LA POLISI TANZANIA.
  TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

  “PRESS RELEASE” TAREHE 28.01.2016.
  · MTU MMOJA AUAWA KWA KUCHOMWA KISU KUTOKANA NA WIVU WA KIMAPENZI.

  · MWENDESHA PIKIPIKI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI MKOANI MBEYA.

  KATIKA TUKIO LA KWANZA:
  MTU MMOJA MKAZI WA CHILANGA WILAYA YA MBOZI MKOANI MBEYA AITWAYE EMANUEL NZUNDA [55] ALIUAWA KWA KUCHOMWA KISU KICHWANI NA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA MTU AITWAYE MENGO MKISI.

  TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 27.01.2016 MAJIRA YA SAA 23:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA CHILANGA, KATA YA IHANDA, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA. 

  CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI WIVU WA KIMAPENZI, BAADA YA MAREHEMU KUMTUHUMU MTUHUMIWA KUWA NA MAHUSIANO NA MKE WAKE AITWAYE TELEZIA AZIMIO [31] MKAZI WA CHILANGA, AMBAYE AMEKAMATWA KWA MAHOJIANO. 

  INADAIWA KUWA, MAREHEMU BWANA EMANUEL NZUNDA [55] ALIPORUDI NYUMBANI TOKA KAZINI HAKUMKUTA MKE WAKE NA HIVYO KUAMUA KWENDA NYUMBANI KWA MTUHUMIWA NA KUMKUTA MKE WAKE AKIWA NA MTUHUMIWA NA NDIPO UGOMVI UKATOKEA. MAREHEMU ALIFARIKI KUTOKANA NA KIPIGO NA KUTOKWA NA DAMU NYINGI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI KWA UCHUGUZI ZAIDI WA KITABIBU. MTUHUMIWA ALIKIMBIA BAADA YA TUKIO. UPELELEZI UNAENDELEA.

  KATIKA TUKIO LA PILI:
  MWENDESHA PIKIPIKI MKAZI WA MBIMBA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA NELSON MSHEMWA [54] ALIFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI T. 998 DDL AINA YA MITSUBISHI FUSO ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA KENEDY MJELWA [35] MKAZI WA MLOWO.

  TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 27.01.2016 MAJIRA YA SAA 20:00 USIKU HUKO KIJIJI CHA MBIMBA, KATA NA TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA. 

  CHANZO CHA AJALI HIYO NI MWENDO KASI WA GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI T. 998 DDL AINA YA MITSUBISHI FUSO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI. DEREVA WA GARI ALIKIMBIA BAADA YA TUKIO. UPELELEZI UNAENDELEA.

  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUFUATA/KUZINGATIA NA KUHESHIMU SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO DEREVA WA GARI AZITOE ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.

  Imesainiwa na:
  [AHMED Z. MSANGI – SACP]
  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

  0 0


  MWIMBAJI nguli wa muziki wa Injil, Bonny Mwaitege ametoa wito kwa Watanzania kuilipa uzito wa aina yake Tamasha la Pasaka kwa kujitokeza kwa wingi kuhudhuria tukio hilo adhimu duniani.

  Mwaitege alisema Tamasha la Pasaka lina ujumbe wa Mungu hivyo Watanzania wanatakiwa kujitokeza kwa wingi na kumkimbilia M
  ungu katika tamasha hilo.

  “Watanzania tunatakiwa tujitokeze kwa wingi kwa sababu Yesu alikufa na kufufuka, hivyo kuna kuna ujumbe mkubwa kutoka kwa Mungu ambao utawaokoa Watanzania wote,” alisema Mwaitege. 

  Mwaitege alisema kupitia tamasha hilo jamii inaondokana na machafu ambayo yanamchukiza Mungu.

  Naye Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema tamasha la mwaka huu wamejipanga vilivyo kufanikisha matakwa ya jamii kutoka kwa waimbaji wa nyimbo za injili na viongozi wa dini watakaohudhuria tamasha hilo.

  Msama alisema tamasha la mwaka huu wamepanga litaanza Machi 26 hadi 28 hapa nchini, hivyo Watanzania wajiandae na tamasha hilo.

  “Watanzania watarajie tamasha bora ambalo litafikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa jamii, hivyo wajiandae,” alisema Msama.

  0 0

   SHIRIKA la ndege la Etihad limetajwa kuwa Shirika la Ndege la Mwaka wakati wa tuzo za Business Travel 2016. Hafla hii ilifanyika jana usiku katika hoteli ya Grosvenor House iliyopo Jijini London. Tuzo hizi zinatambua makampuni na watu binafsi waliopata mafanikio katika sekta ya biashara ya usafiri na hivyo kuwafanya wastahili kuwania tuzo hizo.

  Tuzo hizi zinazoandaliwa na jarida la Uingereza la Buying Business Travel, huwa na jopo la wataalamu wanaojadiliana na kisha kupiga kura kubaini washindi. Hii ni mara ya kwanza kwa Etihad kushinda tuzo hiyo, hii ikija siku chache tu baada ya shirika la ndege la Etihad kupokea “Tuzo ya Uvumbuzi katika Usafiri” kutoka tuzo za jarida la Globe Travel katika hafla nyingine iliyofanyika wiki iliyopita London.

  James Harrison, Meneja Mkuu wa shirika la Etihad Uingereza, alisema: “Tuzo hii ni ishara ya kutambulika kwa mchango wa Etihad katika sekta ya usafiri wa anga nchini Uingereza. Tunajisikia fahari kubwa sana kutambuliwa katika jukwaa kubwa hivi.”

  “Uingereza ni soko muhimu kwa shirika hili na mwaka huu umekuwa na mafanikio makubwa kwetu kwani tunasherekea miaka kumi tangu tuanze kutoa huduma zetu kati ya jiji la Manchester na Abu Dhabi. Tunategemea kuzindua huduma ya tatu ya kila siku kutoka uwanja wa ndege Heathrow, jijini London, kupitia ndege aina ya A380 ambayo pia ina huduma ya vyumba ya “Makazi”. Zaidi tunalenga kutoa huduma iliyorahisishwa na inayowaunganisha wageni wetu.”

  Shirika la Etihad liliibuka kidedea kutokana na huduma zao za hali ya juu, zikiwemo bidhaa (na vyumba) zilizoingia hivi karibuni sokoni na kuleta mapinduzi katika sekta ya usafiri wa anga. Hii ikiwa pamoja na kutumia ndege aina ya Airbus A380 na Boeing 787 Dreamliners, bila kusahau vyumba ambavyo vilishakuwa vikitumika na Airbus A330/A340 na Boeing 777.

  Mapinduzi haya yametokana na programu ya utafiti na maendeleo iliyoendeshwa katika Kituo cha Uvumbuzi kilichopo Abu Dhabi na kuongozwa na timu ya ubunifu ya Etihad. Shirika la Etihad linapenda kutoa huduma yenye viwango sawa na hoteli kubwa na sehemu nyingine za kitalii kubwa duniani. Etihad wameajiri wafanyakazi wenye ufundi na uzoefu mkubwa haswa katika safari ndefu kwa mfano wahudumu wakuu walipo katika “Makazi” ya ndege ya A380 kwenda London, Wapishi Wa daraja la Kwanza, meneja wa vyakula na Vinywaji katika “daraja la biashara” na wahudumu wa kutunza watoto wakati wa safari. Wahudumu hawa wamehitimu chuo cha kulea na kutunza watoto Norland huko Uingereza.

  Pia shirika la ndege la Etihad lina sehemu ya mapumziko katika viwanja vya ndege wa London Heathrow, Manchester, Frankfurt, Dublin, Paris, Sydney, Washington, D.C. na New York wakati uwanja wa ndege wa Abu Dhabi una sehemu za mapumziko na mapokezi.

  Hivi sasa safari za shirika hili zinafika sita kila siku kwenda Uingereza, zikiwa na huduma za moja kwa moja kufika jijini London kupitia uwanja wa ndege wa Heathrow, jijini Manchester na jijini Edinburgh zilizozinduliwa Juni 8 mwaka jana. Uwanja wa ndege wa Heathrow Jijini London ulipata nafasi ya kuwa kituo cha kwanza kwa ajili ya kuzindua huduma ya ndege za jamii aina ya Airbus A380, ikiwemo huduma ya “Makazi”- ikiwa na vyumba vya kipekee duniani kuwekwa kwenye ndege ya kibiashara yenye ukubwa wa vyumba vitatu huku ndege hii pia ikiwa na vyumba 6 vya “daraja la kwanza”, 70 vya “daraja la biashara” na 415 vya “daraja la uchumi”.

  0 0

  Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano  Mhe. Mhe Eng Godwin Ngonyani akijibu maswali ya wabunge katika kikao cha Bunge la 11linaloendelea Mjini Dodoma. picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO

   
  Serikali imeahidi kuendelea na ujenzi wa barabara katika maeneo tofauti nchini kwa kiwango cha lami ili kutatua adha kubwa ya ubovu wa barabara ulipo katika maeneo mengi nchini.
   
  Hayo yamesemwa leo Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano  Mhe. Eng Godwin Ngonyani akijibu maswali ya wabunge waliouliza kuhusu mpango wa serikali kuboresha barabara zilizopo na kujenga mpya ili kukabiliana na adha ya ubovu wa barabara nchini.
   
  Akijibu swali la Mhe Richard Mganga Ndassa Mbunge wa Sumve (CCM) lililohitaji  ufafanuzi wa serikali ni lini ujenzi wa barabara ya Magu-Bukwimba –Ngudu-Hungumalwa itajengwa kwa kiwango cha lami, Mhe Eng Godwin Ngonyani amesema katika  mwaka wa fedha 2014/15 na 2015/16 serikali ilitenga jumla ya shilling millioni 200 kwa ajili ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 70 na taratibu za kumtafuta Mhandisi Mshauri zinaendelea na baada ya kukamilika kwa usanifu na kupata gharama za mradi huo, Serikali itatafuta fedha za kuanza ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami.
   
  Aidha akijibu pia swali la Mhe Fredy Atupele Mwakibete  Mbunge wa Busokelo (CCM) aliyehitaji kujua ni lini barabara ya Katumba-Mbambo-Tukuyu yenye urefu wa Kilometa 82 inayoanzia Katumba(RDC) kupitia Mpombo,Kandete,Isange,Lwanga, Mbambo (BDC) hadi Tukuyu (RDC) itajengwa kwa kiwango cha lami.
   
  Akijibu swali hilo, Mhe. Eng Godwin Ngonyani amesema kuwa Serikali kupitia  Wakala wa Barabara (TANROADS) kwa kutambua umuhimu wa barabara hii, katika mwaka wa fedha 2009//10 Serikali ilianza maandalizi ya ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami na ambapo upembuzi yakinifu na sanifu wa kina ulikamilika na baadae Serikali iliamua kujenga kilometa 10 ambapo mwezi April,2014 Wakala wa Barabara na kampuni ya CICO ilijenga barabara hiyo kuanzia Lupaso hadi Buseji,Wilayani Busokelo.
   
  Serikali kupiti Wakala wa Barabara (TANROADS) inaendelea na ujenzi wa barabara kwa kiwangocha lami katika Kata, Wilaya na Mikoa mbalimbali nchini  ili kukabiliana na adha ya ubovu wa barabara ambao umesababisha watu kukosa mawasiliano baina ya maeneo.


  0 0


  Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Simiyu, Epaphra Swai (pichani) amefariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es salaam.

  TFF itawajulisha mipango ya msiba na mazishi ya marehemu Epaphra Swai baada ya kukaa na familia ya marehemu na kupanga utaraibu huo.


  Bwana ametoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO

  TAARIFA KWA UMMA

  KUFUNGWA KWA MUDA BARABARA YA MPANDA - KOGA - TABORA
  Tunapenda kutoa taarifa kwa Umma kuwa, Barabara ya Mpanda - Koga - Tabora imefungwa kwa muda kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini zilizosababisha kufurika kwa mto Koga na kufanya daraja la Koga, lililopo mpakani mwa Mikoa ya Katavi na Tabora kutopitika na hivyo kukata mawasiliano ya barabara katika mikoa hiyo.

  Kutokana na kukatika kwa mawasiliano ya barabara kupitia daraja hilo, tunaomba wananchi kusitisha safari kwa kutumia barabara hiyo ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza hadi hapo barabara hiyo itakapofunguliwa mara tu baada ya maji kupungua katika eneo hilo.

  Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imechukua hatua hiyo kwa mujibu wa Kifungu cha 41 (1) cha Sheria ya Barabara Na. 13 ya Mwaka 2007 na Kanuni ya 8 (1) ya Kanuni za Usimamizi za Barabara za Mwaka 2009.

  Wizara, inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza katika kipindi hiki chote.
  Imetolewa na:

  Eng. Joseph Nyamhanga
  KATIBU MKUU (UJENZI)
  28/01/2016

  0 0


  0 0
 • 01/28/16--09:16: Congratulations to Murtaza • 0 0


  0 0


  0 0


  0 0

  Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa Michuzi Blog, Bw. Chalila Chibuda (kushoto) akikabidhiwa na Kaimu Mkuu wa Habari Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Bw. Clarence Nanyaro cheti maalum cha kutambua mchango wa blogu hiyo maarufu duniani namna ilivyoshiriki katika kurusha matangazo, mijadala, habari na michezo iliyoelimisha na kuhamasisha wananchi kujitokeza katika shughuli mbalimbali za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Hafla hiyo ya kukabidhi vyeti kwa vyombo vya habari vilivyofanya vizuri kazi hiyo ilifanyika Makao Makuu ya NEC Dar es Salaam leo.

  0 0

  Gu Xun, Vice President of StarTimes Group (Left) and Jean Jacques Bouya, Minister for Spatial Planning and Delegate-General for Major Projects, Republic of Congo, exchange the contract. Uganda Digital Migration continued to be the topic of discussion, on28thApril2015, Ugandan President Yoweri Kaguta Museveni, the Honourable Jim Muhwezi Katugugu, Minister of Information and State Guidance, and other sectors met with Chairman Pang in Entebbe.The meeting discussed StarTimes’ Public-Private-Partnership proposal with the Uganda government to rollout Digital Migration. President Museveni expressed the importance of Digital Migration for the entire country and urged administrators to enter into further discussions with StarTimes.
  Mr. Pang Xinxing, Chairman of the StarTimes Group and Mr. Museveni, President of Uganda. Zambia. The year kicked off with Pang Xinxing, Chairman of StarTimes Media Group having a very fruitful meeting with Zambian president, Edgar C. Lungu on 31March 2015. The Chairman shared information on StarTimes operations and investment in Zambia, to which President Lungu commented “You are the company that we would like to assist Zambia with rolling out Digital Migration.”
  Mr. Pang Xinxing, Chairman of StarTimes and Mr. Edgar C. Lungu, President of Zambia. China-Africa Media Summit On 1st December 2015, the company co –hosted the China-Africa Media Summit together with Naspers. The event held in Cape Town South Africa at the International Conference Centre. It was organized by the State Council Information Office of the People’s Republic of China (PRC), undertaken by China National Publications Import & Export (Group) Corporation. 
  For more picture  CLICK HIRE.

  0 0

  Mwakilishi wa jamii ya wafanyakazi kutoka Afrika Kusini katika kampuni ya Illovo Tanzania (SATZ) Cathryn Morris akikata utepe wakati wa kukabidhi jengo ambalo ujenzi wake umefadhiliwa na taasisi za (SATZ) waliotoa 5.5, Jenga Women Group milioni 4. Hafla ya kukabidhi ilifanyika Kilombero jana. Jengo hilo litatumika kwa ajili ya maktaba, kuwashauri yatima na watoto washio katika mazingira magumu. 
  Mweka hazina wa kikundi cha Jenga cha Kilombero Candice Roe-Scott akiongea na vikundi ambavyo watafaidika na jengo jipya litakalo tumika kwa kwa ajili ya maktaba, kuwashauri yatima na watoto washio katika mazingira magumu. Jengo hilo lilikabidhiwa kwa vikundi vya kijamii jana, Kilombero.
  Mke wa Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha sukari cha Kilombero Louise Bainbridge akiongea na walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Kilombero, Muungano, Kantui, Ujirani, Lyahira na Mapinduzi (hapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi madawati jana, Kilombero. Katiakti ni Meneja Mkuu wa kiwanda cha sukari cha Kilombero Mark Roe-Scott na kulia ni meneja utawala wa kiwanda cha sukari cha Kilombero Allawi Mdee.

  0 0

  StarTimes Tanzania Vice President, Ms Zuhura Hannif (left) speaks during a press conference in Dar es Salaam yesterday to officially announce the company's “Win a Trip Promotion” a promotion dubbed “Pasua Anga na StarTimes” which starts this January that will see five lucky subscribers heading to Germany in March to watch the Bundesliga matches live. Right is StarTimes Public Relations Manager, Muddy Kimwery. (Photo by our correspondent). --- By Our Correspondent, StarTimes, the leading digital TV operator in the country has officially announced its “Win a Trip Promotion” a promotion dubbed “Pasua Anga na StarTimes” will see five lucky subscribers heading to Germany in March to watch the Bundesliga live. 

   Speaking during a press conference in Dar es Salaam yesterday, The StarTimes Tanzania Vice President, Miss Zuhura Hannif said, The ‘Win a trip promotion’ will be running in five weeks, whereby every week one winner will be announced. “Five lucky subscribers, who have spent at least Tshs 5000 and above to renew their subscription or acquire a StarTimes decoder or Satellite Dish and Decoder automatically enter into a draw to secure an all-expense paid trip to Germany. "Our mission is to give our esteemed and loyal subscribers an experience of their lifetime by sending them to Germany to witness one of the greatest European soccer leagues,” said StarTimes Vice President, Zuhura Hannif. 

   StarTimes, Africa’s leading digital-TV operator covering 80% of the continent’s population, has exclusive rights to broadcast the German Bundesliga, the Italian Serie A and the French League, League One. Under the deal, StarTimes subscribers have the opportunity to watch live matches in every match day from the three exciting leagues, beginning with the Friday night fixture from the Bundesliga. “We have these three leagues exclusive to StarTimes but there is also a lot more for our subscribers to enjoy, including the Tennis tournaments, Boxing and other contents which are in our platform,” she added. StarTimes viewers have the opportunity to watch all the live matches through the company’s sports channels such as Sports Focus, Sports Arena, World Football, Sport Life, and Sport Premium.

  0 0

  flavianmarwa_HeadshotThe African continent is, in many realms, an untapped frontier, and many global business analysts believe that one of those areas is entrepreneurship. “East Africa, in particular, is very green ground for basic entrepreneurship,” says Flavian Marwa, SF ’10. “Here, it’s more important to execute a simple idea well than to come up with an idea that no one has thought of. You don’t have to be a sophisticated technologist to take advantage of this environment.”

  A consultant with the International Finance Corporation (IFC), an arm of the World Bank Group, Marwa uses his insights into the continent to advise the IFC on how African countries can implement policies that stimulate the creation and growth of small and medium enterprises (SMEs). “The idea is to bring in the private sector as much as possible. We know this approach leads to sustainable development. To be effective, however, policies to support SMEs also must address impediments in the value chain of targeted sectors.” Impediments like the skills gap, lack of mentorship, and information asymmetry.

  Marwa says that leaders who are committed to a robust education system—from primary to secondary to university levels—will enable their citizens to develop a keen eye for opportunities and empower them with the skills to launch businesses. He notes that in Tanzania and other East African countries, the IFC is encouraging multinational companies to collaborate with universities to develop curricula that are relevant to what is actually happening in industry.

  Continue reading →

  0 0
  0 0

  Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dr Kamugisha Kazaura (Kushoto) akielezea kuhusu mipango ya kampuni mbele ya Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Faustine Kamuzora (Katikati) na Naibu Katibu Mkuu Dr Mary Sassabo (Kulia) walipotembelea kampuni hiyo. Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dr Kamugisha Kazaura (Kushoto) akielezea kuhusu mipango ya kampuni mbele ya Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Faustine Kamuzora (Katikati) na Naibu Katibu Mkuu Dr Mary Sassabo (Kulia) walipotembelea kampuni hiyo.Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Faustine Kamuzora na Naibu Katibu Mkuu, Dk. Mary Sassabo wakiwa katika kikao na wafanyakazi wa TTCL. Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Faustine Kamuzora na Naibu Katibu Mkuu, Dk. Mary Sassabo wakiwa katika kikao na wafanyakazi wa TTCL.Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Faustine Kamuzora na Naibu Katibu Mkuu, Dk. Mary Sassabo wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TTCL pamoja na baadhi ya maofisa kutoka wizara hiyo. Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Faustine Kamuzora na Naibu Katibu Mkuu, Dk. Mary Sassabo wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TTCL pamoja na baadhi ya maofisa kutoka wizara hiyo.
  Baadhi ya maofisa wa TTCL wakitoa maelezo kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu mawasiliano kwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Faustine Kamuzora na Naibu Katibu Mkuu wake, Dk. Mary Sassabo walipotembelea ofisi za TTCL Dar es Salaam. Baadhi ya maofisa wa TTCL wakitoa maelezo kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu mawasiliano kwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Faustine Kamuzora na Naibu Katibu Mkuu wake, Dk. Mary Sassabo walipotembelea ofisi za TTCL Dar es Salaam.

  0 0

  Kulia ni Mwl.Chacha Heche ambae ni Katibu wa Chadema Mkoani Mara akiongea na wanahabari nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza.

  Na:George Binagi.
  MAHAKA kuu Kanda ya Mwanza jana imeitupilia mbali kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Novemba 25 mwaka jana, katika Jimbo la Tarime Vijijini Mkoani Mara, iliyofunguliwa na aliekuwa mgombea ubunge katika jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Christopher Ryoba Kangoye.


  Katika kesi hiyo, wajibu maombi walikuwa ni Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini Mhe.John Heche (Chadema), Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambapo mtoa maombi alikuwa akiiomba Mahakama kutengua matokeo ya Uchaguzi Mkuu katika Jimbo hilo kwa kuwa haukuwa huru na haki.


  Baada ya Mahakama hiyo kupitia kwa Jaji Lameck Mlacha kusikiliza utetezi wa pande zote, iliamua kuifuta kesi hiyo ambayo ilikuwa ni nambari nne ya mwaka 2015 kutokana na hoja za mleta maombi kuwa na kasoro mbalimbali ikiwemo kutoainisha majina ya waliokuwa wakilalamikiwa kuvuruga uchaguzi Jimboni humo.


  Wakili wa mleta maombi Costantine Mutalemwa pamoja na Wakili wa mjibu maombi Paul Kipeja aliekuwa akisaidiana na Wakili Tundu Lisu katika kesi hiyo, wameelezea kuridhika na maamuzi ya Mahakama hiyo.


  0 0

  Baadhi ya mabango yakiwa yamewekwa na Kamapuni ya TTCL katika maeneo ya makutano ya barabara Mwenge na Kawe jijini Dar es Salaam kuitambulisha bidhaa ya 4G-LTE kwa wateja wa jiji la Dar es salaam. Baadhi ya mabango yakiwa yamewekwa na Kamapuni ya TTCL katika maeneo ya makutano ya barabara Mwenge na Kawe jijini Dar es Salaam kuitambulisha bidhaa ya 4G-LTE kwa wateja wa jiji la Dar es salaam.Baadhi ya mabango yakiwa yamewekwa na Kamapuni ya TTCL katika maeneo ya makutano ya barabara Mwenge na Kawe jijini Dar es Salaam kuitambulisha bidhaa ya 4G-LTE kwa wateja wa jiji la Dar es salaam. Baadhi ya mabango yakiwa yamewekwa na Kamapuni ya TTCL katika maeneo ya makutano ya barabara Mwenge na Kawe jijini Dar es Salaam kuitambulisha bidhaa ya 4G-LTE kwa wateja wa jiji la Dar es salaam.

    KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imeendelea na harakati zake za kimasoko kutambulisha intaneti yake yenye kasi na bora zaidi ya 4G-LTE kwa wateja wa jiji la Dar es salaam ili kuwafikia watanzania walio wengi zaidi. 

   Tangu kuzinduliwa kwa Huduma hii mwishoni mwa mwezi wa Desemba, 2015, wateja wengi wamefurahishwa na huduma hii kutokana na ubora wa intaneti, gharama nafuu ambayo inakidhi mahitaji yao. “Kweli nimeridhishwa na huduma zao, kwa sasa natumia kifurushi cha Oneconnect ambacho napata huduma za data ya 4G na ADSL (fixed modem), hii inanisaidia nikiwa nyumbani na nikirudi nyumbani naendelea kupata huduma kama kawaida kwa bei moja” alisema mteja, Boazi Kaaya. Pichani juu ni baadhi ya akinadada wawakilishi wa Kampuni ya TTCL wakizungumza na wateja barabarani jijini Dar es Salaam kuitambulisha huduma ya 4G-LTE kwa wateja anuai. Pichani juu ni baadhi ya akinadada wawakilishi wa Kampuni ya TTCL wakizungumza na wateja barabarani jijini Dar es Salaam kuitambulisha huduma ya 4G-LTE kwa wateja anuai.Pichani juu ni baadhi ya akinadada wawakilishi wa Kampuni ya TTCL wakizungumza na wateja barabarani jijini Dar es Salaam kuitambulisha huduma ya 4G-LTE kwa wateja anuai. Pichani juu ni baadhi ya akinadada wawakilishi wa Kampuni ya TTCL wakizungumza na wateja barabarani jijini Dar es Salaam kuitambulisha huduma ya 4G-LTE kwa wateja anuai.Pichani juu ni baadhi ya akinadada wawakilishi wa Kampuni ya TTCL wakizungumza na wateja barabarani jijini Dar es Salaam kuitambulisha huduma ya 4G-LTE kwa wateja anuai. Pichani juu ni baadhi ya akinadada wawakilishi wa Kampuni ya TTCL wakizungumza na wateja barabarani jijini Dar es Salaam kuitambulisha huduma ya 4G-LTE kwa wateja anuai.[/caption] Naye, Meneja Masoko wa TTCL, Beda Kinunda amesema kuwa mkakati huu wa kutangaza bidhaa za TTCL 4G – LTE na ADSL ni mkakati endelevu, lengo letu kuwafikia wateja wetu popote walipo katika jiji la Dar es salaam. Tunapenda kuwakaribisha wakazi wa Dar es salaam kutumia huduma zetu za 4G zina ubora, bei nafuu na uhakika muda wote. Pia, TTCL tunauza vifaa vinavyotumia teknolojia ya 4G –LTE ambavyo ni Dongle (modem), Mi-Fi na Routers kwa bei nafuu zaidi.

older | 1 | .... | 1105 | 1106 | (Page 1107) | 1108 | 1109 | .... | 3286 | newer