Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110020 articles
Browse latest View live

KUTOKA MAKTABA: LIGI KUU YA KANDANDA YA VODACOM UWANJA WA UHURU MIAKA 5 ILIYOPITA


OFISI YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS ZANZIBAR YAKABIDHI VIFAA TIBA

$
0
0
Na Hassan Hamad (OMKR)
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, imeikabidhi Wizara ya Afya vifaa vya maabara vyenye uwezo wa kubainisha dawa za kulevya.

Akikabidhi vifaa hivyo kwa Naibu Katibu wa Wizara ya Afya, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dkt. Omar Dadi Shajak (pichani) , amesema kuna umuhimu wa kuvitunza na kuvitumia vifaa hivyo kwa njia zilizo sahihi, ili viweze kuleta tija katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya nchini.
Ametoa wito kwa jamii hasa wadau wakuu wanaohusika na mapambano dhidi ya dawa za kulevya kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuhakikisha kuwa mapambano hayo yanafanikiwa.
Amesema Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kupitia Tume ya Kuratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya Zanzibar, itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo ili kusaidia upatikanaji wa vifaa vya kisasa katika kufanikisha mapambano hayo.
Amelishukuru Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na dawa za kulevya na uhalifu duniani (UN ODC) kwa kutoa vifaa hivyo vya dawa, na kuwaomba washirika wengine wa maendeleo kusaidia juhudi hizo.
Mapema akipokea vifaa hivyo katika hafla iliyofanyika Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Migombani, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bi. Halima Maulid Salum, ameishukuru Ofisi hiyo kwa jitihada zake inazochukua katika kukabiliana na dawa za kulevya, na kuahidi kuvitumia vifaa hivyo kwa uangalifu mkubwa.
Nae Mkemia Mkuu wa Serikali Zanzibar Dkt. Slim Rashid Juma, amesema vifaa hivyo vitasaidia na kurahisisha uchunguzi wa dawa za kulevya, na kuweza kutofautisha kwa haraka baina ya dawa hizo na kemikali.
Amesema matarajio ya maabara yao ni kuwa na vifaa vya kisasa kwa ajili ya kurahisisha na kuwezesha kufanya uchunguzi wa aina zote za dawa za kulevya, kwa lengo la kuondosha usumbufu wa kusafirisha sampuli kwenda Tanzania Bara.                                                                                              

Hon Dr Susan Kolimba sworn in as EALA NEW MEMBER

$
0
0
Hon Dr Susan Kolimba (centre) is ushered into the House by Hon Angela Kizigha (right) and Hon Shyrose Bhanji.
Hon Dr Susan A. Kolimba takes the Oath of Allegiance to the Assembly assisted by the Senior Clerk Assistant, Stephen Mugume as Hon Angela Kizigha and Hon Shyrose Bhanji.
CONGRATULATIONS: EALA Speaker, Rt. Hon Daniel Kidega welcomes and congratulates the Deputy Minister for Foreign Affairs, East African, Regional and International Co-operation.

EALA has this afternoon sworn in Hon Dr Susan Alphonce Kolimba, the Deputy Minister for Foreign Affairs, East African, Regional and International Co-operation in the United Republic of Tanzania, as an Ex-Officio Member.  The Oath of Allegiance to the House was administered by the Clerk of EALA, before the EALA Speaker, Rt. Hon Daniel F. Kidega.
Hon Dr.Kolimba took the oath in accordance with Rule 5 of the Rules of Procedure of the Assembly. The Rules of Procedure say in part that: “No Member can sit or participate in the proceedings of the House until the Oath or Affirmation of Allegiance to the Treaty is taken”.
Rule 5(5) specifically states that “when a Member first attends to take his or her seat other than at the first sitting of a new House, he or she shall be brought to the table by two Members and presented by them to the Speaker who shall then administer the Oath or Affirmation of Allegiance”.
The EAC Treaty under Article 48 provides that the Assistant Minister, Deputy Minister of Minister of State may only participate in the meetings of the Assembly when the substantive Minister responsible for East African Community Affairs is unable to participate.
The Deputy Minister was ushered into the House by Hon Angela Kizigha and Hon Shyrose Bhanji.
In her maiden speech, Hon Dr. Kolimba who immediately assumes the Chair of the EAC Council of Ministers, assured the House that the United Republic of Tanzania is fully committed to the ideals of integration and of her intention to ensure the objectives of the Community are realised.
Hon Dr Kolimba, was appointed Deputy Minister by President John Pombe Magufuli in the cabinet named in December 2015.
Prior to her appointment, Hon Dr. Kolimba rose through the ranks of the academic world to become Dean, Faculty of Law at the Open University of Tanzania, a position she held from 2010 to late 2015.  Dr Kolimba, whose background is entrenched in law, taught in the institution for a number of years and also served in various administrative capacities.
Hon Dr. Kolimba holds a Ph.D. in Law from the Russian Peoples’ Friendship University, Moscow and a Master’s degree from the same institution.

HABARI TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

Mpaka wa Kenya na Tanzania Kuimarishwa

$
0
0
Maafisa wa serikali za Kenya na Tanzania waliokutana mjini Naivasha, nchini Kenya, Januari 18 – 22 mwaka huu, wameazimia kutekeleza uimarishaji wa mpaka wa nchi hizo, unaokadiriwa kufikia kilometa 760, kwa awamu. 
 Kiongozi wa ujumbe wa serikali ya Tanzania kwenye mazungumzo hayo, Bw. Justo Lyamuya, amesema zoezi hilo linatarajiwa kuanza Aprili mwaka kuu na kipande cha Ziwa Victoria mpaka Ziwa Natron (kilometa 238). 

 Akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. John Haule, jijini Nairobi mwishoni mwa juma, Bw. Lyamuya, ambaye ni Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, alisema utekelezaji wa mradi huo utategemea upatikanaji wa fedha zinazokadiriwa kufikia dola za Kimarekani milioni 4.68 (Shilingi bilioni 5.13), gharama ambayo itagawanwa na serikali za Kenya na Tanzania. Mpaka wa Kenya na Tanzania unaanzia pembezoni mwa Ziwa Victoria na kuishia Bahari ya Hindi eneo la Vanga.
Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. John Haule(katikati) akiwakaribisha chakula cha jioni jijini Nairobi, wajumbe walioiwakilisha serikali ya Tanzania kenye mazungumzo ya mpaka na Kenya, yaliyofanyika Naivasha.

Mhe. Balozi Haule (wa tatu kulia) katika picha ya pamoja na wajumbe hao na baadhi ya maofisa wa ubalozi wa Tanzania Nairobi. Anayemfuata ni Bw. Justo Lyamuya, Kiongozi wa ujumbe


TEASER YA JOTO LA ASUBUHI LA 93.7 EFM ALHAMISI JANUARY 28, 2018 KUANZIA SAA 12 ASUBUHI

IDADI YA RAIA WA EPHIOPIA WALIOKAMATWA MJINI IRINGA WAFIKIA 12, MCL YATOA UFAFANUZI DHIDI YA KUHUSISHWA

$
0
0
Idadi ya Raia wa kigeni kutoka nchini Ephiopia waliokuwa wakisafirishwa na Gari la magazeti la kampuni ya Mwananchi Communication Ltd yafikia 12 baada ya wengine 4 kukamatwa Jioni wakiwa Eneo la Kibwabwa  mjini Iringa wakiwa wamefichwa porini.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Iringa Peter Kakamba amesema kuwa tayari ametuma usafiri kwenda kuwabeba Raia hao ambao wanadai walishushwa katika gari hilo aina ya Hiace ili kuvuka eneo la ukaguzi wa Magari ( check pointi)  kijiji cha Igumbilo nje kidogo ya mji wa Iringa.

Wakati huo huo Kampuni ya Mwananchi Communication Limited (MCL)  imetoa ufafanuzi kuhusiana na kuhusishwa na kadhia hiyo. Soma zaidi:

Kufuatana na taarifa ya Jeshi la polisi mkoa wa Iringa kukamata gari la kampuni ya Okanda lenye usajili namba T745 DED Toyota Hiace inayosafirisha magazeti ya MCL jana tarehe 27 Januari 2016 asubuhi likiwa linadaiwa kubeba WAHAMIAJI HARAMU. Tunapenda kutoa maelezo yafuatayo:

•         MCL haijawahi kufanya, haifanyi na hivyo haihusiki kwa hali yoyote katika tukio hili. Watuhumiwa (madereva) wanaodaiwa kuhuhusika na tukio hili si wafanyakazi wa Mwananchi Communications Limited bali ni wa Okanda kampuni ambayo imeingia kandarasi na MCL kusafirisha magazeti yake kutoka Dar es Salaam kwenda Mbeya

•         MCL itaendelea kufanya kazi za biashara yetu ya habari kwa uadilifu na weledi wa hali ya juu.
•         MCL inaangalia uwezekano wa kuchukua hatua kali zaidi dhidi ya mkandarasi  ikiwepo kusitisha mkataba.
•         Tunawapa pole wasomaji wetu wote na umma kwa ujumla kwa usumbufu mlioupata kutokana na habari za tukio hili

Francis Nanai
Mkurugenzi Mtendaji – MCL

ufafanuzi kuhusu uamuzi wa kutorusha matangazo ya moja kwa moja ya majadiliano ya Bunge.

$
0
0
Huu ni uchambuzi wa Habari toka vituo mbalimbali vya Televisheni January 27, 2016.
Serikali imetolea ufafanuzi kuhusu uamuzi wa kutorusha matangazo ya moja kwa moja ya majadiliano ya Bunge.

yale yaleeeee... baada vya uongo wa kupigwa marufuku vimini, watani wa jadi waendeleza libeneke la taarifa zisizo za kweli

$
0
0
Kumekuwepo na habari za uongo na potofu katika mtandao wa jamii wa www.kenya-today.com kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli atazuru Kenya kuhudhuria kumbukumbu ya marehemu Mhe. Jaramongi Odinga na Fidel Odinga Jumamosi hii. 
Inasikitisha kuona kwamba mwandishi wa Kenya anachukua nafasi ya Mwandishi wa habari wa Rais wa Tanzania kwa kuwa na  ratiba ya Mhe. Rais wa Tanzania kuliko waTanzania wenyewe. 
Haijulikani ni nini has nia ya mtandao huo, lakini ukweli ni kwamba ratiba hiyo ni batili na ya uongo uliotukuka. Hawa watani wetu wa jadi wana lao jambo!  Wapuuzeni. Taarifa hiyo si ya kweli.

Kuona habari hio ya uongo BOFYA HAPA

NGOMA AZIPENDAZO ANKAL

DIRA YA DUNIA YA BBC SWAHILI KUTOKA LONDON

KIVUKO CHA MTO KILOMBERO CHAZAMA,ABIRIA ZAIDI YA 29 WAOKOLEWA

$
0
0

Kivuko cha mto Kilombero mkoani Morogoro kimezama kikiwa na abiria zaidi ya 30 na magari yapatayo matatu

Habari kutoka Kilombero zilizothibitishwa na mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Bw. Leph Gembe zinadai kuwa ajali hiyo imetokea jana Majira ya saa 1 usiku wakati kivuko hicho kikitokea Ulanga.

Alisema kuwa Jumla ya watu zaidi ya 30 ndio walikuwepo katika kivuko hicho na kuwa jitihada za uokoaji zilifanyika na watu zaidi 29 waliokolewa

Alisema chanzo cha ajali hiyo ni upepo Mkali na mawimbi makali yaliyopelekea kivuko hicho kuzama na kuwa hadi sasa bado taarifa kamili kupatikana na pindi atakapopata habari kamili atazitoa

Mkuu huyo alisema kwa sasa yupo jijini Dar es Salaam kwa matibabu.
Muonekano wa Misingi ya Daraja la Mto huo, huku kivuko kilichozama kikionekana kulia.

Wakabidhiwa jengo la mafunzo na madawati Kilombero

$
0
0
Mwakilishi wa jamii ya wafanyakazi kutoka Afrika Kusini katika kampuni ya Illovo Tanzania (SATZ) Cathryn Morris akikata utepe wakati wa kukabidhi jengo ambalo ujenzi wake umefadhiliwa na taasisi za (SATZ) waliotoa 5.5, Jenga Women Group milioni 4. Hafla ya kukabidhi ilifanyika Kilombero jana. Jengo hilo litatumika kwa ajili ya maktaba, kuwashauri yatima na watoto washio katika mazingira magumu. 
Mweka hazina wa kikundi cha Jenga cha Kilombero Candice Roe-Scott akiongea na vikundi ambavyo watafaidika na jengo jipya litakalo tumika kwa kwa ajili ya maktaba, kuwashauri yatima na watoto washio katika mazingira magumu. Jengo hilo lilikabidhiwa kwa vikundi vya kijamii jana, Kilombero
Mke wa mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha sukari cha Kilombero Louise Bainbridge akiongea na walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Kilombero, Muungano, Kantui, Ujirani, Lyahira na Mapinduzi (hapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi madawati jana, Kilombero. Katiakti ni Meneja Mkuu wa kiwanda cha sukari cha Kilombero Mark Roe-Scott na kulia ni meneja utawala wa kiwanda cha sukari cha Kilombero Allawi Mdee.

Serikali yasema haijafuta vipindi vya Bunge TBC

$
0
0
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO

Serikali imetolea ufafanuzi kuhusu taarifa za upotoshaji kwa umma kuwa imefuta vipindi vya shughuli za Bunge kuoneshwa katika televisheni ya Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) kama zisemazo taarifa zilizozagaa mitaani.

Hayo yamesemwa Mjini Dodoma na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Mose Nnauye wakati akiongea na wananchi moja kwa moja kupitia vyombo mbalimbali vya habari nchini kutolea ufafanuzi taarifa za upotoshaji juu ya TBC kufuta vipindi vya matangazo ya vikao vya Bunge.

Mhe.Nape Moses Nnauye amesema Serikali haijafuta vipindi vya Bunge bali ilichofanya ni kubadilisha muda wa kurusha vipindi hivyo kutoka muda wa mchana na kuviweka usiku kwa lengo la kupunguza gharama za kurusha moja kwa moja matangazo hayo ya Bunge na pia  kuwapa fursa wananchi zaidi kuangalia na kufatilia yanayoendelea Bungeni kwa kuwa muda wa usiku watu wengi wanakuwa wamesharejea kutoka katika shughuli zao za ujenzi wa taifa.

Ameongeza kuwa Serikali imechukua uamuzi wa busara katika hili kwani TBC imekuwa ikitumia Sh Billion 4.2 kwa mwaka kama gharama za urushaji wa moja kwa moja wa matangazo hayo , hivyo itasaidia katika kubana matumizi ya shirika hilo kwani fedha hizo hazipo katika bajeti ipewayo shirika bali ni fedha za ndani zinazokusanywa na shirika hilo
.
Aidha amesema kuwa sio kitu kigeni kwa Bunge kutotangazwa moja kwa moja kwani kuna baadhi ya mabunge katika nchi nyingine urekodiwa na kurushwa baadae kama kipindi maalum cha Bunge,amezitaja baadhi ya nchi hizo kuwa ni New Zealand, India, Malawi, Lesotho, Uingereza na Singapore.

Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) lilianza kurusha matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2005 ila baada ya Serikali  kukaa na kujadili kwa kina kuhusu gharama za urushaji wa matangazo hayo moja kwa moja ikaamua kubadili mtindo wa urushaji wa matangazo hayo kutoka matangazo ya moja kwa moja kwa siku nzima kwenda kwenye mfumo wa kuyarekodi na kuyarusha katika kipindi cha LEO KATIKA BUNGE.

MRADI MANJANO DREAM MAKERS WA KUKWAWEZESHA MANAWAKE WAJASIRIAMALI WAINGIA ZANZIBAR

$
0
0
 Mradi wa Kuwawezesha wanawake Kupitia Tasinia ya Urembo ujulikanao kama Manjano Dream-Makers waingia Zanzibar. Wataalamu kutoka Taasisi ya Manjano Foundation wataendesha mafunzo kuanzia tarehe  1 February 2016 kwenye ukumbi wa  Mtoni Marine Hotel Zanzibar. 
Wanawake 30 wa Zanzibar watanufaika na mafunzo ya ujasiriamali kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano. Wanawake wakazi wa Zanzibar wanaopenda kunufaika na mradi huo  wanaombwa kwenda kwa usaili na kujiandikisha siku ya Jumamosi tarehe 30 January 2016 kuanzia saa tatu asubuhi kwenye hoteli ya Mtoni Marine mjini Zanzibar.
Mafunzo yana lengo la  kumsaidia mjasiriamali mwanamke kujikwamua. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya biashara namna ya kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika mpangilio wa biashara ikiwemo matumizi sahihi ya rasilimali muda, kutokufuja fedha, muda na pia namna ya kujitunzia akiba itokanayo na biashara yake. 

Awamu ya pili itahusu kuwafundisha jinsi ya kupamba harusi na matumizi sahihi ya vipodozi vya LuvTouch Manjano. Baada ya wanawake hawa kuhitimu mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation inatoa mikopo bila riba kwajili ya kuwawezesha kuanzisha biashara wakiwa chini ya uangalizi maalum wa Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha kila mhitimu wa mafunzo haya anapiga hatua na kuweza kujitegemea .
Wasiliana nasi kwa Simu namba +255 759413234

Wananchi wa Kiteto Mkoani Manyara wahamasika kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF)

$
0
0
 Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoani Manyara, Isaya Shekifu akizungumza kwenye Kijiji cha Engusero Wilayani Kiteto, wakati wa uzinduzi wa uhamasishaji wa kuchangia mfuko wa afya ya jamii (CHF) ambapo kila kaya yenye watu sita wanachangia sh10,000 na kupatiwa matibabu kwa mwaka mzima.
 Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara, Kanali Samuel Nzoka akizungumza kwenye kijiji cha Engusero, wakati wa uzinduzi wa uhamasishaji wa kaya kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) ambapo katika uzinduzi huo Kanali Nzoka alizichangia kaya mbili za watu 12, shilingi 20,000 ambazo zitapatiwa matibabu kwa mwaka mzima pindi wakiugua.
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara, Kanali Samuel Nzoka (kulia) akipokea moja kati ya mashuka 170 yaliyotolewa na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wa Mkoa huo Isaya Shekifu (kushoto) kwenye uzinduzi wa uhamasishaji wa kaya kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) ambapo kwenye wilaya hiyo ulizinduliwa katika kijiji cha Engusero.

WAKAZI wa Wilaya ya Kiteto, Mkoani Manyara, wametakiwa kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) ili waweze kupatiwa matibabu kwa kuchangia sh10,000 na kupatiwa matibabu mwaka mzima kwa kaya yenye watu sita.

Akizungumza kwenye kijiji cha Engusero wakati wa uzinduzi wa uhamasishaji wa kaya kujiunga na CHF, mkuu wa wilaya hiyo Kanali Samuel Nzoka alisema kaya nyingi zikijiunga ndiyo upatikanaji wa dawa unakuwepo.

Kanali Nzoka alisema tatizo la ukosefu wa dawa kwenye zahanati, vituo vya afya na hospitalini litamalizika, endapo kaya nyingi zikijiunga na CHF kwani serikali nayo itaweka mkono wake ili kuhakikisha huduma za afya zinaboreshwa.

Wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo Kanali Nzoka alijitolea sh20,000 kwa ajili ya kuzilipia kaya mbili za watu 12 wa kijiji cha Engusero na Dosidosi na kuungwa mkono na viongozi wanne wa wilaya hiyo waliojitolea sh10,000 kwa kila mmoja.

Kwa upande wake, Ofisa uratibu na matokeo wa CHF, Nicholaus Mwangomo alisema kila kaya wilayani humo inapaswa kuchangia sh10,000 za gharama za matibabu ili watibiwe kwa kadi na kuachana na mtindo wa kutibiwa kwa fedha.

“Kaya moja ikilipa sh10,00 inapatiwa matibabu kwa mwaka na isipougua inakuwa imewachangia wenzao watakaougua, kwani hata kwenye bima za magari na pikipiki wasiopata ajali wanawachangia waliopata majanga,” alisema Mwangomo.

Meneja wa mfuko wa Taifa wa Bima ya afya (NHIF) wa mkoa wa Manyara, Isaya Shekifu alisema mwanachama wa CHF atanufaika na huduma zote za afya za msingi na kinga na tiba kwa zahanati, kituo cha afya na hospitali.

Hata hivyo, ili kudhihirisha kauli mbiu ya awamu ya tano ya hapa kazi tu, Shekifu alikabidhi mashuka 170 ya kujifunika wagonjwa ambapo mashuka 20 yalitolewa kwenye zahanati ya Engusero na mashuka 150 kwa hospitali ya wilaya ya Kiteto.

Shekifu alitaja baadhi ya huduma zinazotolewa ni vipimo vya maabara, wagonjwa wa kutwa na kulazwa, upasuaji kulingana na utaratibu uliowekwa na halmashauri husika na wanachama kupata huduma  bora ya afya kwa mwaka.

“Pia watapata huduma ya upasuaji kulingana na utaratibu uliowekwa na Halmashauri zinazoendesha mifuko hii zinapata mapato ya tele kwa tele kutoka serikalini ambayo yatatumika kuboresha huduma za afya,” alisema.

Hata hivyo, ili kudhihirisha kauli mbiu ya awamu ya tano ya hapa kazi tu, Shekifu alikabidhi mashuka 170 ya kujifunika wagonjwa ambapo mashuka 20 yalitolewa kwenye zahanati ya Engusero na mashuka 150 kwa hospitali ya wilaya ya Kiteto.

TANGAZO LA ZABUNI YA UNUNUZI WA KIWANJA No. C/R 326/43 KIJITONYAMA KILICHOKO KARIBU NA SHULE YA MSINGI MWENGE BARABARA YA ALLY HASSAN MWINYI MKABALA NA TAASISI YA ELIMU.

MCHEKESHAJI KUTOKA KENYA, ERIC OMONDI AWASILI JIJINI DAR LEO TAYARI KWA LIVE SHOW KESHO.

$
0
0
MWIGIZAJI na mchekeshaji wa nchini Kenya, Eric Omondi amewasili mchana huu jijini Dar leo akiwa na kikosi kazi chake wakiwa tayari kwa 'LIVE SHOW' kesho katika ukumbi wa mikutano wa Marqee uliopo hoteli ya Hyatt jijini Dar es Salaam.
Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Omondi akiwa na kikosi kazi chake wakiwasili katika jengo la Alosco Tower lililopo Lumumba jijini Dar es Salaam leo.

Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Omondi akiwa katika pozi na bango la GSM Media leo alipo wasili jijini Dar es Salaam kwaajili ya 'LIVE SHOW' itakayofanyika kesho katika hoteli ya Hyatt katika ukumbi wa Marqee jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Omondi akiwa na Meneja Mkuu wa GSM Media, Deo Ndejembi (katikati) na Dj wa mchekeshaji huo, wakiwa katika ofisi cha GSM Media leo mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam.
Meneja Mkuu wa GSM Media, Deo Ndejembi na Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Omondi wakiwa katika picha na kikosi kazi cha mchekeshaji huyo ambapo 'LIVE SHOW' itakayofanyika kesho jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

RAIS DKT MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA NAIBU GAVANA WA BENKI KUU YA TANZANIA

Waziri Mkuu majaliwa BUngeni leo mjini Dodoma

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wabunge kwenye viwanja vya Bunge jini Dodoma Januari 28, 2016. Kutoka kushoto ni Jumanne Kishimba wa Kahama, Edwin Ngonyani wa Namtumbo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Hussein Amar wa Nyangwhale, Prosper Mbene wa Morogoro Kusini na Joseph Kalanda wa Sikonge. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akijibu maswali Bungeni mjini Dodoma Januari 28, 2016
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba, Bungeni Mjini Dodoma, Januari 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Viewing all 110020 articles
Browse latest View live




Latest Images