Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

Meja Jenerali Rwegasira ataka polisi wenye tabia ya kuwabambikizia kesi wananchi wachukuliwe hatua kali

$
0
0
Na Felix Mwagara

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira amewataka viongozi wakuu wa Jeshi la Polisi nchini kuhakikisha wanawachukulia hatua kali askari polisi wenye tabia ya kuwabambikizia kesi wananchi.

Meja Jenerali Rwegasira alisema Jeshi hilo lina sifa nzuri nje ya nchi pamoja na hapa nchini lakini kuna baadhi ya askari wasiowaadilifu wanawaonea wananchi mitaani wasiokuwa na hatia kwa kuwabambikizia kesi ambapo wanalitia doa jeshi hilo.

“Jeshi letu lina sifa nzuri, niliwahi kwenda nchini Kenya nikaambiwa Jeshi la Polisi Tanzania lina maadili kwani hata likimkamata mhalifu linafuata sheria na utaratibu na sio kutumia nguvu kubwa kama yalivyo majeshi mengine,” alisema Rwegazira.

Rwegasira aliongeza kuwa, amefurahishwa sana na utendaji kazi wa jeshi hilo na kutaka kuongeza umakini zaidi ili kuliletea sifa zaidi jsehi hilo na yeye yupo karibu nao katika kuliendeleza jeshi hilo ili liweze kufanya kazi kwa weledi.

Alisema kuwa ni askari wachache mno wenye tabia hiyo ya kuwabambikizia kesi wananchi na kutofuata sheria za jeshi, hivyo kazi ya kupambana na askari hao inawezekana endapo viongozi wa jeshi wakiamua kulifanyia kazi. 

“Utendaji kazi wenu ni mzuri, nawapongeza sana hasa mlivyosimamia uchaguzi mkuu vizuri kwani wananchi wengi walikuwa na wasiwasi kuhusu usalama wao katika kipindi cha uchaguzi, lakini mlisimama imara kuhakikisha uchaguzi unamalizika salama,” alisema Rwegasira.

Hata hivyo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya naye alitoa pongezi kwa jeshi hilo na kuwataka kuyapeleka mahitaji yao katika ofisi ya Katibu Mkuu pamoja na yeye ili waweze kuyafanyia kazi na hatimaye kuliboresha jeshi hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi hilo nchini, IGP Ernest Mangu aliwapongeza Viongozi hao wa Wizara kwa kuwatembelea katika ofisi za Makao Makuu ya Jeshi kwani wamefariji na kuwahakikishia viongozi hao kuwa wamejipanga vizuri katika kulinda usalama wa raia na mali zao na watayafanyia kazi maagizo waliyopewa. 

Katibu Mkuu pamoja na Naibu wake wanamekamilisha ziara yao ya kuzitembelea Idara za Wizara hiyo ambazo ni Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Idara ya Uhamiaji, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), ambapo lengo la ziara hizo ni kujitambulisha kwa viongozi hao pamoja na kujifunza kazi mbalimbali zinazofanywa na idara hizo.

UCHAGUZI WA MBUNGE JIMBO LA KIJITOUPELE, ZANZIBAR WAPANGWA KUFANYIKA MACHI 20

$
0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuutaarifu Umma wa Watanzania kuwa Uchaguzi wa Ubunge katika Jimbo la Kijitoupele – Zanzibar utafanyika mnamo tarehe 20 Machi, 2016.
Uchaguzi wa Mbunge katika Jimbo la Kijitoupele - Zanzibar ni mojawapo ya Majimbo yaliyoahirisha kufanya Uchaguzi tarehe 25 Oktoba, 2015 kutokana na hitilafu kwenye Karatasi za Kura.
Aidha, Tume inapenda kuwataarifu Wananchi kuwa Watendaji (Msimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi) walioteuliwa kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa 2015 ndio watakaosimamia na kufanya shughuli za Uchaguzi huo. Uchaguzi huo wa Ubunge katika Jimbo la Kijitoupele hautakuwa na Kampeni na Wagombea walioteuliwa kushiriki Uchaguzi ulioahirishwa mwezi Oktoba, 2015 ndio watakaoshiriki Uchaguzi huu.

Vituo vilivyotumika katika Uchaguzi wa mwaka 2015 ndiyo vitakavyotumika. Vituo vitafunguliwa saa 1.00 asubuhi na kufungwa saa 10.00 jioni. Watakaoruhusiwa Kupiga Kura tarehe 20/3/2016 ni wale ambao wameandikishwa na majina yao yapo katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la Kituo na waje na Kadi ya Mpiga Kura.

Imetolewa na,
Jaji (Mst.) Damian Z. Lubuva
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
MWENYEKITI
26/01/2016

GEPF WAKARABATI UWANJA WA MPIRA WA KIKAPU WA CHUO CHA POLISI MOSHI NA KUKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO

$
0
0
Mkuu wa kitengo cha masoko kutoka Mfuko wa GEPF Bw Aloyce Ntukamazina akimkabidhi vifaa vya michezo mrakimu wa polisi SP Moses Luvinga.
Timu za mpira wa kikapu kutoka chuo cha polisi moshi pamoja na KCMC zikikaguliwa tayari kwa kucheza mchezo wa kirafiki kuashiria uzinduzi wa kiwanja cha mpira wa kikapu katika chuo cha polisi Moshi.
Pichani baadhi ya wanafunzi wakifuatilia mechi hiyo ya ufunguzi

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

PUBLIC NOTICE: VACANCY AT THE INTERNATIONAL TELECOMMUNICATIONS UNION (ITU) IN GENEVA

$
0
0
The Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA), is quasi-independent Government body established under the Tanzania Communications Regulatory Act No.12 of 2003 to regulate communications and broadcasting sectors in Tanzania, on behalf of International Telecommunications Union ( ITU) a world-wide organization which brings government and industry together to coordinate the establishment and operation of global telecommunication network and services hereby invites applications from suitably qualified Tanzanians to fill the following post available at the ITU Headquarters in Geneva- Switzerland:-

1.     FUNCTIONS: Head, Least Developed Countries Division 
           POST NUMBER:       TD43/P5/585
           Deadline for application submission to TCRA:    4th March, 2016
      Vacancy Notice No. 2P-2016/BDT-PKM/EXTERNAL/P5
      Duty Station: Geneva, SWITZERLAND

Details on duties, responsibilities and qualifications may be accessed on the ITU’s website:                http:www.itu.int/employment/Recruitment/index.html

Email:     itumail@itu.int : Website www.itu.int

Applicants for this post are advised to state their nationality, quote the vacancy notice number and address applications with completed ITU Personal History form (PHF) to the undersigned so as to reach him not later than 04th March 2016 respectively. The post applied for should be clearly marked on top of the envelope.

Deadline for application submissions to TCRA:  04th March 2016

Applications from women are encouraged.

ITU is an equal opportunity employer
Applications should be addressed to:

Director General,
Tanzania Communications Regulatory Authority,
Mawasiliano Towers
20 Sam Nujoma Road
P.O. Box 474,
14414, DAR ES SALAAM

NGOMA AZIPENDAZO ANKAL

JK AKABIDHI REPOTI YA JOPO LAKE KWA BAN KI MOON NAYE AMSHUKURU

$
0
0
Na Mwandishi Maalum, New York 
Mwenyekiti wa Jopo la Ngazi ya juu kuhusu Mwitikio wa Kimataifa wa Majanga ya Kiafya, Rais Mstaafu, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, jana Jumatatu, amemkabidhi Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki Moon, Ripoti ya Jopo lake. 
Mhe. Jakaya Kikwete aliteuliwa na Ban Ki Moon, kuongoza Jopo lililokuwa na wajumbe watano mwezi Aprili 2015. kwa mujibu wa hadidu za rejea Jopo hili lilitakiwa kutekeleza majukumu yake kuanzia mwezi Mei hadi Desemba 2015. 
Akipokea ripoti hiyo, katika hafla fupi iliyofanyika Ofisini kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa . Ban Ki Moon, pamoja na kumshukuru Mwenyekiti wa Jopo Mhe. Jakaya Kikwete pamoja na timu yake, amesisitiza kwamba, mapendezo yaliyotolewa na Jopo hilo yatazingatiwa na kufanyiwa kazi. “ Ninatoa shukrani zangu za pekee na za dhati kwako wewe kama Mwenyekiti kwa uongozi wako , na pia kuwashukuru wajumbe uliofanya nao kazi. Ripoti hii ambayo imesheheni mapendekezo na ushauri itazingatiwa na kufanyiwa kazi”. Amesema Ban Ki Moon 
Akabanisha kwamba, mapendekeo na ushauri uliomo ndani ya Ripoti ya Jopo atauwasilisha pia kwa Shirika la Afya Duniani ( WHO). 
Katibu Mkuu pia amesema Ripoti hiyo itasaidia sana katika kutoa mwongozo kwa Jumuiya ya Kimataifa juu ya namna ya kuimarisha na kuboresha miundombinu ya afya ili iweze kukabiliana na magonjwa ya milipuko. 
Vile vile Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amemhakikishia Mwenyekiti wa Jopo Mhe. Jakaya Kikwete na wajumbe wake kwamba, Ripoti hiyo itawekwa hadharani mapema iwezekanavyo ili Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na makundi mbalimbali ya jamii waweze kuisoma. 
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jopo, Rais Mstaafu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amemshukuru Katibu Mkuu Ban Ki Moon, kwa kumpatia heshima ya kuongoza Jopo hilo, jopo ambalo amesema walifanya kazi kwa ushirikiano wa hali ya juu. 
 Wajumbe wengine wa Jopo hilo walikuwa ni Bw. Celso Amorim ( Brazil), Micheline Calmy ( Switzerland), Marty Natalegawa ( Indonesia) Joy Phumapi ( Botswana) na Rajav Shah ( USA). 
Jukumu kubwa ya jopo hilo kwa mujibu wa hadidu za rejea, pamoja na mambo mengine, lilikuwa ni kutoa mapendekezo ya namna ya kuimarisha mifumo ya kitaifa na kimataifa katika kuzuia na kukabiliana na majanga ya kiafya yakiwamo magonjwa ya mlipuko, ikiwa ni pamoja na kujifunza kuhusu mwitikio wa Jumuiya ya Kimataifa kufuatia kuibuka kwa janga la ugonjwa wa Ebola. 
Katika utekelezaji wa majukumu yake Jopo lilikutana na kufanya majadiliano ya kina na makundi mbalimbali yakiwamo ya wataalamu, wawakilishi wa nchi tatu ambazo ziliathirika sana na ugonjwa wa Ebola ( Liberia, Siera Leone na Guinea),Mashirika ya Kimataifa na Kikanda , Taasisi za Fedha za kimataifa, wahudumu wa Afya, Wasomi , Watafiti, Sekta Binafsi na wataalam wa fani na kada mbalimbali.
Mwenyekiti wa Jopo la Ngazi ya Juu kuhusu Mwitikio wa Kimataifa wa Majanga ya  Kiafya, Rais Mstaafu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Ban Ki Moon Ripoti ya  Jopo lake katika hafla fupi iliyofanyika  Jumatatu  Makao  Makuu ya Umoja wa Mataifa. Kushoto ni Bw. Rajav Shah (USA) na Bw. Marty Natalegawa ( Indonesia) ambao ni  sehemu ya wajumbe wa Jopo hilo.

Rais Dkt. John Magufuli amsimamisha kazi mkurugenzi mkuu wa wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA.

$
0
0

Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue leo jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea na waandishi wa habari jana  jijini Dar es salaam kuhusu uamuzi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kutengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na kumsimamisha kazi ili kupisha uchunguzi wa matumizi ya kiasi cha Sh. Bilioni 179.6 zilizotumika hadi sasa. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, Ikulu Gerson Msigwa.

Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Bw. Dickson Maimu na kumsimamisha kazi ili kupisha uchunguzi wa matumizi ya kiasi cha Sh. Bilioni 179.6 zilizotumika hadi sasa.    
Uamuzi huo wa Rais wa kutengua na kusimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu huyo umetolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam.
Sambamba na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu NIDA, Mhe. Rais Dkt. Magufuli pia amewasimamisha kazi watendaji wanne wa Mamlaka hiyo ambao ni Mkurugenzi wa TEHAMA Joseph Mkani, Afisa Ugavi Mkuu Rahel Mapande, Mkurugenzi wa Sheria Sabrina Nyoni na Afisa Usafirishaji George Ntalima.
Balozi Sefue alisema kuwa Mhe. Rais ameelekeza Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) wafanye ukaguzi maalum wamanunuzi yote yaliyofanywa na NIDA, Mdhabiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) afanye ukaguzi maalum wa hesabu za NIDA ikiwemo “value for money” baada ya kuthibitisha idadi halisi ya vitambulisho vilivyotolewa hadi sasa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB) kujiridhisha na kama kulikuwa na vitendo vya rushwa au la.  

Aidha, Mhe. Rais Dkt. Magufuli amemteua aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenye Serikali ya Awamu ya Nne Mahadhi Juma Maalim kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kuwait kufuatia uamuzi wa Serikali kufungua Ofisi ya Ubalozi katika nchi hiyo rafiki.
Vile vile Rais ameagiza Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa kuwarejesha nyumbani mara moja Mabalozi wawili ambao mikataba yao imeisha na kuwataka Mabalozi hao kukabidhi kazi kwa Afisa Mkuu au Mwandamizi aliyechini yao leo hii.

Mabalozi hao ni Bi Batilda Salha Buriani, aliyeko Tokyo, Japan, Dkt. James Alex Msekela, aliyeko Rome, Italia.
Kwa mujibu wa Balozi Sefue, Rais pia amemrejesha nyumbani Balozi wa Tanzania aliyeko London, Uingereza, Bwana Peter Allan Kallaghe ambaye anarejea Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa ambapo atakapopangiwa kazi nyingine.
Balozi Sefue alisema kuwa hadi sasa vituo vya Ubalozi ambavyo viko wazi ni London nchini Uingereza kufuatia kurejea nchini kwa Balozi Peter A. Kallaghe, Brussels nchini Ubelgiji kufuatia aliyekuwa Balozi, Dkt. Deodorous Kamala kuchaguliwa kuwa Mbunge, Rome nchini Italia, kufuatia kuisha kwa mkataba wa Dkt. James Alex Msekela na Tokyo nchini Japan, kufuatia kuisha kwa mkataba wa Bibi Batilda Buriani. 
Vituo vingine vya Ubalozi ambavyo viko wazi ni Kuala Lumpar nchini Malaysia, kufuatia aliyekuwa Balozi Dkt. Aziz Ponray Mlima kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa na Brasilia nchini Brazil, kufuatia kustaafu kwa aliyekuwa Balozi, Bwana Francis Malambugi.
Wakati huo Balozi Sefue alisema kuwa Rais ametengua uteuzi wa Mhandisi Madeni Juma Kipande kabla hajathibitishwa kwenye cheo cha KatibuTawala wa Mkoa wa Katavi kutokana na utendaji kazi usioridhisha.

UMUHIMU WA TAALUMA YA MANUNUZI NA UGAVI.


IDARA YA UHAMIAJI YAJA NA HATI MBILI ZA MUDA MFUPI KWA WAGENI.

$
0
0
NAIBU Kamishna wa Idara ya Uhamiaji, Abbas Irovya, akizungumza na waandishi wa habari  kuhusu idara hiyo kuanza kutoa hati kwa wageni wanaoingia nchini kwa shughuli za muda mfupi, Makao Makuu ya Uhamiaji, Dar es Salaam leo. Kulia ni Ofisa Vibali vya ukazi wa idara hiyo, Philon Kyetema. 

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
IDARA ya Uhamiaji imeanzisha hati mbili ambazo zitatumika kwa wageni wanaoingia na wanaotoka nje na kuondokana hati ya awali ya muda mfupi (CTA).

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Msemaji Mkuu Idara ya Uhamiaji, Naibu Kamishina Abbas Irovya amesema kuwa hati ya kwanza ni ile ya muda atayeingia nchini kwa muda usiozidi siku 90 na baada hapo anatakiwa kurudi alikotoka.

Naibu Kamishina, Irovya amesema kuwa wanaoingia kwa ajili ya kutoa utalaam wafanye hivyo kwa kuwa na hati hiyo na sio kuwa na ajira katika sehemu hizo.

Amesema hati pili ni ile ile katika nchi zilizoingia makubaliano ya kutomia viza watatumia ya muda mfupi kwa kukaa kwa muda huo.

Aidha ameesema wananchi watambue kuwepo kwa huduma hiyo ikiwa na kutoa ushirikiano pale wanapowaona watu ambao wanatumia hati ya muda lakini wanaendelea.

Irovya amesema hati hizo mbili hazihusiani kwa wale wanaoingia nchini kwa kutafuta ajira na wakitaka kufanya hivyo wanatakiwa kuomba kibali cha kazi kutoka idara ya kazi.

MAJALIWA ATOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MWANASHERIA WA BUNGE

$
0
0
 Baadhi ya waombolezaji walioshiriki katika ibada ya kumwombea aliyekuwa Mshauri Mkuu wa Masuala ya Sheria wa Bunge, maerehemu Oscar Mtenda iliyofanyika nyumbani kwake mjini Dodoma Januari 26, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Mshauri Mkuu wa Masuala ya Sheria wa Bunge, marehemu Oscar Mtenda nyumbani kwa marehemu mjini Dodoma Januari 26, 2016. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwapa pole wafiwa baada ya kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Mshauri Mkuu wa Masuala ya Sheria wa Bunge, marehemu Oscar Mtenda nyumbani kwa marehemu mjini Dodoma Januari 26, 2016. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MPAKA WA KENYA NA TANZANIA KUIMARISHWA.

$
0
0

Maafisa wa serikali za Kenya na Tanzania, waliokutana mjini Naivasha, nchini Kenya, Januari 18 – 22 mwaka huu, wameazimia kutekeleza uimarishaji wa mpaka wa nchi hizo, unaokadiriwa kufikia kilometa 760, kwa awamu.

Kiongozi wa ujumbe wa serikali ya Tanzania kwenye mazungumzo hayo, Bw. Justo Lyamuya, amesema zoezi hilo linatarajiwa kuanza Aprili mwaka kuu na kipande cha Ziwa Victoria mpaka Ziwa Natron (kilometa 238).

Akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. John Haule, jijini Nairobi mwishoni mwa juma, Bw. Lyamuya, ambaye ni Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, alisema utekelezaji wa mradi huo utategemea upatikanaji wa fedha zinazokadiriwa kufikia dola za Kimarekani milioni 4.68 (Shilingi bilioni 5.13), gharama ambayo itagawanwa na serikali za Kenya na Tanzania.

Mpaka wa Kenya na Tanzania unaanzia pembezoni mwa Ziwa Victoria na kuishia Bahari ya Hindi eneo la Vanga.

MATUKIO MBALIMBALI BUNGENI MJINI DODOMA.

$
0
0
Spika wa Bunge Job Ndugai (kulia)  akimwapisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa  , bungeni mjini Dodoma Januari 26, 2016. 
 Spika wa Bunge Job Ndugai (kulia)  akimwapisha Waziri wa  Fedha na Mipango, Dkt.Philip Mpango, bungeni mjini Dodoma Januari 26, 2016.
  Wabunge wakisikiliza hoja mbalimbali bungeni mjini Dodoma Januari 26, 2016.
  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MWESIGWA AFUNGUA KOZI YA NGAZI YA JUU KWA WANAWAKE

$
0
0

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Mwesigwa Selestine leo amefungua kozi ya ngazi ya juu ya ukocha kwa wanawake (High Level Coaching Course) iliyoandaliwa na TFF kwa kushirikiana na FIFA.

Akiongea na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa kozi hiyo, Mwesigwa amewataka washiriki wa kozi hiyo kuzingatia mafunzo hayo na kuitumia vyema fursa hiyo adimu waliyoipata.

Mwesigwa amewataka washiriki kuhakikisha kozi hiyo ya siku tano, inawasaidia na kwenda kuwa walimu wa mpira wa miguu kwa wanawake, na kuongeza mwamko kwa wanawake wengi kuupenda na kuucheza mpira wa miguu.

Aidha Mwesigwa, amewataka washiriki wa kozi hiyo kuzingatia maelekezo ya mkufunzi, nidhamu ya ndani na nje ya uwanja kwani imekua ni bahati nzuri kwao kupata nafasi ya kushiriki kozi hiyo ya ngazi ya juu.

Naye mkufunzi wa kozi hiyo anayetambulika na FIFA/CAF, Sunday Kayuni amesema atatumia uwezo wake wote kuhakikisha washiriki wa kozi hiyo wanajifunza na kuelewa vizuri mafunzo yake, ili waweze kuwa walimu wazuri watakapokwenda kuanza kufundisha.

Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Wanawake ya TFF, Amina Karuma ameishukuru TFF kwa kuendesha kozi hiyo na kusema kupatikana waalimu wengi wa kike kutaongeza mwamko wa wanawake kuucheza mpira wa miguu.

Jumla ya washiriki 25 wanashiriki kozi hiyo kutoka mikoa mbalimbali nchini ambao ni Fatuma Omary, Esther Chabruma, AMina Mwinchum, Sweetie Charles, Pendo John, Berlina Mwaipungu, Mariam Mchaina, Elizabeth Sokoni, Sophia Mkumba, Marry Masatu, Aziza Mbwele, Fadhila Yusuph.

Wengine ni Veneranda Mbano, Mariam Aziz, Hilda Masanche, Chichi Mwidege, Sophia Edward, Asha Rashid, Fatuma Khatibu, Neema Sanga, Hindu Muharami, Tatu Malogo, Komba Alfred, Veroinca Ngonyani, Judith nyatto na Ingfridy Kimaro.

STIKA ZA KUTOKOMEZA MAUAJI KWA WATU WENYE UALBINO ZA ZINDULIWA JIJINI DAR LEO.

$
0
0
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna, Simon Sirro, akizungumza na wadau mbalimbali juu ya kufanikisha uzinduzi wa Stika maalumu yenye ujumbe wa kutokomeza mauaji ya watu wenye Albinism,leo jijini Dar es Salaam.
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna, Simon Sirro, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Stika maalumu yenye ujumbe wa kutokomeza mauaji ya watu wenye Albinism jijini Dar es Salaam,kulia ni Mwenyekiti wa Albino Enteprises of Dar es Salaam Michael Lugendo.
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna, Simon Sirro, akupokea tuzo kutoka kwa Mwenyekiti wa Albino kutoka Enteprises of  Dar es Salaam, Michael Lugendo leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii.

SIMU TV: UCHAMBUZI WA HABARI TOKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI January 26, 2016.


DIRA YA DUNIA JUMANNE 26.01.2016

Eng. George Isai Sambali appointed Acting Director General of Tanzania Airports Authority (TAA).

$
0
0
The Minister for Works, Transport and Communication, Prof. Makame Mbarawa has appointed Eng. George Isai Sambali (51), Acting Director General  of Tanzania Airports Authority (TAA).

According to the Permanent Secretary, Ministry of Works, Transport and Communication, (Transport Sector), Dr. Leornard Chamuliho, the appointment is effective 20th January, 2016.

Eng. Sambali takes over from the late Eng. Suleiman S. Suleiman who passed away on 18th January, 2016 while doing swimming exercises at Ferry-Kigamboni area within the city of Dar es Salaam.

Born in 1965 in Tabora region, Eng. Sambali holds Masters Degree of Science in Transportation Engineering (Transport and Road) from Netherlands that he attained in 2001 and BSc. Civil Engineering from the University of Dar es Salaam (UDSM) attained in 1995.

 He has attended numerous local and international trainings in civil aviation and in 2015 was awarded a Post- Graduate Diploma in International Airports Professionals (AIP) under AMPAP program in Canada.

Also he holds a Diploma in Airport Engineering from Nanyang Technical University in Singapore and is a graduate of Airport Management Professional Accreditation Programme (AMPAP) under ICAO and ACI. He also holds a Diploma in Airports Executive Leadership from Concord University in Canada.

Eng. Sambali who was employed by TAA in 2001 as a Manager - Design, Planning and Evaluation is registered with several professional bodies including the Engineers Registration Board (ERB), Institute of Engineers Tanzania (IET) and Forum for Rural Transport Development (IFRTD).

In 2012 he was appointed Acting Director of Engineering and Technical Services (DETS) and later from 2013 was working as Advisor to the TAA Director General up to 2015 when he became Acting Director of Julius Nyerere International Airport (JNIA), the post he held until January 20, 2016 when appointed the Acting Director General of TAA.

Before joining TAA, Eng. Sambali worked as a Research Fellow on urban transport at the University of Dar es Salaam. 


ISSUED BY THE LEGAL AND 
PUBLIC RELATIONS UNIT  – TAA


20th JANUARY, 2016

CHAMA CHA WAENDESHA BODABODA JIJINI ARUSHA CHAIOMBA SERIKALI KUONDOA UTATA ULIOPO KATI YAO NA WAENDESHA PIKIPIKI ZA KAWAIDA.

$
0
0
 Waendesha pikipiki wakiwa mbele ya ofisi ya Mkuu wa mkoa.
Na Vero Ignatus , Arusha.
Chama cha waendesha bodaboda Jijini Arusha ( UWAPA) chaiomba serikali kutatatua utata uliopo kati ya waendesha bodaboda na waendesha pikipiki za kawaida kwa kuwawekea alama maalumu ambayo itawatambulisha, hii ni kutokana na maandamano ambayo yamefanyika siku ya tar 25./1 /2016 kwani ni kinyume kwakuwa chama hakina taarifa yeyote kuhusu maandamano hayo. 
 Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa UWAPA bwana Godlight Rugemalila ambapo amesema ametoa taarifa polisi kutokana na maandamano hayo na amesema jambo walilolifanya siyo sahihi kwa hao walioratibu maandamano hayo ,na amewataka waendesha bodaboda wote kama kuna jambo lolote watalipata ofisini wafuate utaratibu wasikurupuke.
 Amesema kuwa yapo makundi ya aina mbili kwa waendesha bodaboda,kundi la kwanza ni walimesajiliwa na UWAPA hawana vituo maalum , kundi la pili ni waendesha pikipiki za kawaida hawa hawajasajiliwa na idadi yao ni kubwa ambao huwaharibia wale ambao wanafanya biashara halali ya kubeba abiria 
 Amesema kuwa wao kama UWAPA hawajapanga maandamano walipata taarifa kutoka kwa watu binafsi na walishtushwa kusikia kuna maandamano hayo na ameongeza kuwa wanaendelea kufanya utafiti kwa kushirikiana na jeshi la polisi ili kufahamu ni wakina nani wanahusika kuratibu maandamano hayo.
Amewataka waendesha bodaboda wafuate sheria za usalama barabarani kama zinavyoelekeza, wawe na leseni, wavae kofia ngumu ,wapaki kwenye vituo vilivyosajiliwa.
Pia amewashauri abiria wanaotumia usafiri huo wachukue bodaboda zilizopo kwenye vituo kwani akipata tatizo lolote ni rahisi yeye kusaidika tofauti na akichukua pikipiki ambayo ameiona barabarani inapita utakosa pa kupeleke malalamiko yako maana kila kituo kina kiongozi. 
 Ameainisha waendesha bodaboda waliosajiliwa na wanaotambulika hadi sasa jumla yao ni 2950 ,vituo vilivyosajiliwa 144 na vituo bubu ambavyo bado na vinatazamia kupata usajili ni 55. 
Hivyo amewataka waendesha pikipiki wote wajisajili kwenye chama hii ni kwa faida yao maana watatambulika watasaidika mara wapatapo tatizo na hii itawaepusha kuingia kwenye lawama za mara kwa mara kuwa waendesha pikipiki ni wakwapuaji na wanatumika kwenye matukio ya uhalifu.
 Amehitimisha kwa kusema kuwa UWAPA ni umoja wa wawaendesha bodaboda jijini Arusha na umoja huu ulisajiliwa marchi 2012 na unatambulika kiserikali, lengo ni kuwaleta pamoja waendesha bodaboda na huwa wanapatiwa mafunzo na RTO chini ya kitengo cha usalama barabarani Amewataka wananchi wafahamu kuwa wapo waendesha bodaboda hawa wanapaki maeneo yaliyoidhinishwa na ni vituo halali na waendesha pikipiki ni yeyeote yule unayeweza mchukua barabarani hana kituo. 
Maandamano hayo yalifanyika kuelekea kwa mkuu wa mkoa wa Arusha wakiwa na madai ya wakimtaka mkuu huyo wa mkoa atoe tamko kuhusu kusumbuliwa kwao na askari wa usalama barabarani .

VYAMA VYA SIASA VYAASWA KUSHIRIKI UCHAGUZI WA ZANZIBAR

$
0
0
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Mhe.Jaji Francis Mutungi (pichani)mameviasa Vyama vya Siasa kushiriki chaguzi zinazotangazwa na tume za uchaguzi nchini ikiwemo uchaguzi wa Machi 20, mwaka 2016 uliotangzwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).
 Kwa mujibu wa barua iliyotolewa  kwa vyama hivyo leo na kusainiwa na  Jaji Mutungi  ilieleza kwamba,  kimsingi Sheria ya Vyama Vya Siasa Sura ya 258 inasisitiza vyama vya siasa kushiriki katika chaguzi zote zinazotangazwa na tume za uchaguzi ili kufikia malengo yake ya kushika dola.
“Katika nchi kidemokrasia na kwa chama cha siasa kinachoamini misingi ya kidemorasia ya vyama vingi vya siasa, hakuna njia mbadala kwa chama cha siasa kufikia malengo yake zaidi ya kushiriki uchaguzi.
“Ni wajibu wa kila chama cha siasa nchini  kama wakala wa kukuza demokrasia, utawala wa sheria na amani ya nchi, kuwa wa kwanza kutii matamko ya kisheria yanayotolewa na mamlaka  husika . 
"Kama kuna chama cha siasa hakiridhiki au kimekwazwa kwa njia moja au nyingine na suala lolote kuhusu masuala ya uchaguzi, njia stahiki na inayonyesha ukomavu wa kisiasa si kuhamasisha kugomea uchaguzi, bali ni vema kikafuata utaratibu uliowekwa katika sheria za uchaguzi,” alisema Jaji Mutungi.
Aidha Msajili huyo amesema kwa mujibu wa Sheria za Nchi bado ni suala la hiari kwa chama kushiriki uchaguzi lakini utashi huo wa hiari unaenda sanjari na umuhimu wa kila chama kushiriki kila uchaguzi unaotangazwa na tume ya uchaguzi.
“Hivyo ni muhimu basi kila chama cha siasa kuelewa kuwa,uchaguzi ni kipimo cha uhai wa chama cha siasa. Chama cha siasa kisiposhiriki uchaguzi kinaua uhai wake katika mtazamo wa harakati za kisiasa,” alisisitiza.
 
Aliongeza kwamba hivi sasa, mfumo wa demokrasia ya vyama vingi na vyama vya siasa vimeimarika, hivyo sio vyema kwa chama cha siasa kujirudisha nyuma au kujiua kisiasa kwa kutoshiriki uchaguzi wakati kina uwezo wa kufanya hivyo.

TANZANIA YAUTAKA UMOJA WA MATAIFA KUZINGATIA MISINGI ILIYOJIWEKEA

$
0
0
Mwakilishi wa  Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi akizungumza wakati wa  Mkutano wa Bodi za Mashirika na  Mifuko ya Umoja wa Mataifa  siku ya jumatatu, ambapo pamoja na mambo mengine ameutaka Umoja wa Mataifa kutekeleza majukumu yake  kwa  kuzingatia misingi iliyojiwekea na pia kutowapa  nafasi  watendaji  wenye ushabiki na  wanaoweka mbele maslahi binafsi. Walioketi nyuma ni  Maafisa wa Uwakilishi  Bw. S. Shilla  na Bi, Lilian Mkasa
Na   Mwandishi Maalum, New  York

Wakati  Tanzania ikipongeza, kusifu na kushukuru uhusiano na ushirikiano wake na Umoja wa Mataifa kupitia  Mifuko  na Mashirika yake ya  Maendeleo,  imeutaka pia Umoja  huo kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia, kanuni, taratibu, sheria na misingi iliyojiwekea ili iendelee  kujijenga heshima.

 Hayo yameelezwa jana jumatatu na  Mwakilishi wa  Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa  Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, wakati  wa mkutano wa Bodi   za   Mashirika ya  Umoja wa  Mataifa UNDP, UNFPA na  UNOPS.    Tanzania ni mjumbe wa  Bodi  katika Mashirika hayo.

 Katika  siku ya kwanza ya  mkutano ,  mkutano uliofunguliwa na Mtendaji Mkuu wa UNDP, Bi Helen Clark,    Balozi  Manongi  amesisitiza kwamba,   ili  Umoja wa Mataifa  uendelee kujijenga heshima na  kuheshimika,  unapashwa kutoruhusu watendaji  wenye ajenda na maslahi binafsi kufanya kazi katika  Mashirika ya Umoja wa  Mataifa.

“ Umoja wa Mataifa  wakati wote  umekuwa sehemu na  mdau mkubwa katika uimarishaji  na ujenzi wa  utawala  bora katika nchi nyingi , Tanzania  ikiwamo. Wajibu wa Umoja wa Mataifa utabaki kuwa  halali na wenye nguvu  endapo wale ambao wamepewa  dhamana ya kutenda kwa niaba yake watatambua na kuheshimu imani na  wajibu uliotukuka ambao wamepwa kuutekeleza ” akasisitiza Balozi Manongi

Akaongeza kwamba, mashabiki  hawapaswi kupewa nafasi, wala kuvumiliwa na kuwa sehemu ya miongoni mwa watendaji wa chombo hicho wasipewe nafasi,  wala wasivumiliwe  kuwa miongoni mwa watendaji wa chombo hicho.

Akizungumzia kuhusu  rasimu  ya  Taarifa ya  Mpango wa Utekelezaji  kuhusu  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Country report) kwa kipindi cha 2016-2021) ambayo imewasilishwa mbele ya Wajumbe wa Bodi wa UNDP,  Balozi Manongi amesema,  mapendekezo  yaliyomo kwenye  rasimu na ambayo imeshirikisha wadau mbalimbali  inajumuisha mawazo na mapendekezo kutoka pande zote za  Muungano na imetokana na misingi ya ushirikiano kati ya UNDP na Serikali ya Tanzania.

Vile vile akasema rasimu  hiyo imejumuisha vipaumbele vinavyoainishwa  katika Dira ya  Taifa ya 2025 kwa upande wa Tanzania Bara ,  Dira ya  2020 kwa upande wa  Zanzibar,  mkakati wa  kupunguza umaskini kwa pande zote za Muungano  pamoja  na Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano.

“ Tunaishukuru UNDP- Ofisi ya Tanzania kwa ushirikiano wake katika utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo ikiwano mikakati ya  kupunguza umaskini, ushirikiano huu   umekuwa mzuri ingawa unachangamoto zake” akasisitiza Balozi Manongi

Akaeleza kwamba, kutokana  na umuhimu wa mwaka huu wa 2016 ambao pamoja na mambo mengine  ni  kuanza kwa utekelezaji wa Agenda ya Maendeleo Endelevu ( Agenda 2030) Tanzania itaendelea kushirikiana  kwa  karibu na  UNDP katika utekelezaji wa  Agenda hiyo huku mkazo ukiwa ni katika  kupungua ama kuondoa umaskini   uliokithiri kwa makundi ya mbalimbali ya  jamii  hususani wanawake.

Akasema , Serikali imejipanga vema katika utekelezaji wa mipango mbalimbali inayolenga katika kuboresha maisha  ya wananchi  wake. Ikiwa ni pamoja na  kutatua tatizo la uhamaji wa  wananchi wake  kutoka  vijijini na kwenda katika miji mikuu hususani vijana kwa lengo la kutafuta ajira na hali bora  ya maisha.

Akasema kuwa wajibu au  madhumuni  ya msingi   UNDP ni kupunguza umaskini, ni kwa sababu hiyo Tanzania ingependa kuiona UNDP ikijielekeza zaidi katika jukumu lake hilo la msingi kama  inavyoelekezwa katika  maazimio  mbalimbali ya Baraza Kuu la Umoja wa  Mataifa.

Kwa upande wa ukusanyaji na uchambuzi wa takwimu zinazohusu maeneo  mbalimbali,  Balozi Manongi amesisitiza kwamba  UNDP inapashwa kufanya kazi kwa karibu na kwa ushirikiano na  Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kile alichosema ndicho chombo cha serikali chenye dhamana juu ya  masuala yote  yahusuyo takwimu.

Na kwa sababu hiyo akasema Tanzania inaridhishwa na taarifa ya kwamba UNDP itashirikiana na  Ofisi  hiyo ya Taifa ya  Takwimu katika Nyanja mbalimbali zikiwamo za uwezeshaji kwa lengo  la kusaidia katika  uhuishaji wa takwimu.


Aidha  Tanzania  imesisitiza kuhusu  umiliki  katika uendeshaji na usimamizi wa miradi ya maendeleo pamoja na kiushauri   UNDP kuhakikisha kwamba fedha zinazotengwa kwaajili ya   miradi ya maendeleo zinakwenda kufanya kazi iliyokusudiwa na si vinginevyo. 

Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images