Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1101 | 1102 | (Page 1103) | 1104 | 1105 | .... | 3285 | newer

  0 0

  SHIRIKISHO la Riadha Tanzania(RT) limeandaa mbio fupi kwa ajili ya kuhitimisha siku 100 za rais Dk.John Pombe Magufuli kuwa Ikulu zitakazotimua vumbi jumamosi hii januari 30 mwaka huu mjini Dodoma.

  Mbio hizo zimepewa jina maalumu la Dodoma ‘hapa kazi tu’ Half Marathon ambazo zitashirikisha washiriki mbali mbali wakiwamo waheshimiwa wabunge,mawaziri,wanafunzi,walemavu na wanariadha wakongwe nchini.Akizindua mbio hizo mjini Moshi mwishoni mwa wiki zinazodhaminiwa na Kampuni ya JSM,Rais wa shirikisho hilo,Anthony Mtaka alisema kuwa lengo la kuanzishwa kwa mbio hizo ambazo zimeandaliwa na kuendeshwa na shirikisho hilo ni kufufua michezo hapa nchini.

  Pia alisema mbio hizo zitatumika kwa ajili ya kumpongeza Rais Dk.John Pombe Magufuli kutimiza siku 100 tangu aingie maradakani ambazo zitakuwa februari 14 mwaka huu.Kwa mujibu wa rais huyo wa RT,mbio hizo zimegawanywa katika makundi matatu ambako mbio za kwanza ni za kilomita 2.5 ambazo zitashirikisha wabunge,mawaziri,walemavu,wanafunzi ,wazee na watu mbalimbali.

  Mbio za kilomita 5 ambazo ni za kujifurahisha zitashirikisha wakimbiaji wote na mbio za nusu marathon ambazo zitakuwa ni mbio za ushindani washindi watapata zawadi .Akitangaza zawadi kwa washindi,Mtaka alisema mshindi wa kwanza kwa upande wa wanaumme na wanawake atapata zawadi ya piki piki yenye thamani ya sh,Milioni 2.8,mshindi wa pili akipata bati 100,wa tatu bati 40,mshindi wa nne akipata sh,200,000 huku mshindi wa tano akiondoka nash,100,000.

  Mshindi wa sita hadi wa kumi watapata kifuta jasho cha sh,50,000 kila mmoja huku waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa ndiye atayakuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mbio hizo na atashiriki mbio za kilomita 2.5.Wanafunzi waatakaopenda kushiriki mbio hizo watasajiliwa kwa sh,500,huku vwasio wanafunzi wakisajiliwa kwa sh,1,000 na wingine ambao hawakutajwa ni kundi gani wakisajiliwa kwa sh,5,000 na fedha hizo kwa mujibu wa Mtaka zitasaidia kambi ya wanariadha watakaoshiriki michuano ya Olimpiki.

  Uzinduzi huo pia ulitumika kuwatambulisha wanariadha wawili ambao wamekidhi vigezo vya kushiriki michuano ya Olimpiki itakayofanyika nchini Brazil mapema mwezi Agosti mwaka huu ambako nchi zaidi ya 216 kutoka kila kona ya dunia zitashiriki

  Wanariadha hao ni Alphonce Felix ambaye ana wastani wa muda wa kukimbia wa saa 2:12.01 na Said Makula ambaye muda wake wa kukimbia ni saa 2:13.27 na watatumia mbio hizo mjini Dodoma kama majaribio yao ya kitaifa kati ya majaribio sita ya kitaifa kabla ya kwenda Brazil.

  Julai 6 mwaka jana,Felix alishiriki mbio za Gold Coast Marathon nchini Australia na kumaliza nafasi ya sita huku Makula akishiriki mbio za Casablanca Marathon oktoba 25 mwaka jana na kumaliza katika nafasi ya nne.

  Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania ,Anthony Mtaka akiwa na Mwe3nye3kiti wa Chama cha riadha mkoa wa Kilimanjaro,( KAA) Liston Methacha wakati wa uzinduzi rasmi wa mbio za Dodoma Hapa Kazi tu Half Marathoni 2016 zinzotarajia kufanyika January 30 mwaka huu mjini Dodoma.
  Baadhi ya wadau wa Riadha wakifuatiia mkutano wa uzinduzi wa Mbio za Dodoma Hapa kazi tu Half Marathon 2016 uliofanyika katika Hotel ya Nyumbani mjini Moshi. 


  0 0
   Mhandisi George Sambali.


   WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Profesa Makame Mbarawa amemteua aliyekuwa Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Mhandisi George Sambali kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo,  Mhandisi Suleiman S. Suleiman. 


  Mhandisi Suleiman alifariki dunia tarehe 18 Januari, 2016 wakati akipelekwa katika hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam baada ya kuishiwa nguvu ghafla akiwa  katika  mazoezi ya kuogelea katika eneo la  Feri, jijini Dar es Salaam.


  Akitangaza uteuzi huo kwa niaba ya Waziri  Mbarawa mbele ya Menejimenti ya TAA Jumatano tarehe 20 Januari, 2016 katika Ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka hiyo kwa niaba ya Mh. Waziri,  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Sekta ya Uchukuzi,  Dkt. Leonard Chamuliho,alisema uteuzi wa Mhandisi Sambali umeanza rasmi tarehe 20 Januari, 2016.


  Mhandisi George Sambali alizaliwa mwaka 1965, mkoani Tabora na ana shahada ya Uzamili ya Sayansi Uhandisi Uchukuzi na Barabara (MSc. Transportation (Transport & Road) Engineering, aliyoipata mwaka 1999- 2001 nchini Uholanzi.


  Mhandisi Sambali alihitimu shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Uhandisi Ujenzi  (BSc.Civil Engineering) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka 1995 .


  Mhandisi Sambali pia amepata mafunzo na kozi mbalimbali za masuala ya anga kutoka katika  vyuo vya hapa nchini na nje ya nchi, ikiwemo  Stashahada ya Uongozi wa Viwanja vya Ndege (Certificate in Airport Executive Leadership) mwaka 2014 huko Montreal, Canada.


  Pia mwaka 2015 alitunukiwa Stashahada ya Wataalamu wa Kimataifa wa Viwanja vya ndege (Post-Graduate Diploma in International Airports Professionals (AIP) chini ya AMPAP nchini Canada.Mhandisi Sambali aliajiriwa na TAA mwaka 2001 kama Meneja Mipango, Usanifu na Uthamini (Manager Design, Planning and Evaluation) na mwaka 2012 aliteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uhandisi na Ufundi.


   Mwaka 2013, Mhandisi Sambali aliteuliwa kuwa Mshauri Maalum wa Mkurugenzi Mkuu kabla ya mwishoni mwa mwaka jana kuteuliwa tena kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha  Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).


  Mhandisi Sambali ni mwanachama kwenye vyama mbalimbali vya kitaaluma kikiwemo cha Wataalamu wa Kimataifa wa Viwanja vya Ndege chini ya Baraza la  Viwanja vya Ndege Duniani (ACI) na Shirika  la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO).


  Pia Mhandisi Sambali ni Mjumbe wa Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET); Mjumbe katika Jukwaa la Kimataifa la Uendeshaji wa Uchukuzi Vijijini (IFRTD); na Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB).


  IMETOLEWA NA KITENGO CHA SHERIA NA UHUSIANO –TAA Januari 25, 2016  0 0

                           Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora , Angela                   Kairuki akiteta na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Ashatu                                                      Kijaji bungeni mjini Dodoma Januari 25, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Songwe, Philip Mulugo kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Januari 25, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wazee kutoka jimbo la Chemba Ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Januari 25,2016. Kushoto kwake ni Mbunge wa Chemba Juma Nkamia. 

   (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0


  Na Jacquiline Mrisho MAELEZO

  Halmashauri ya Manispaa ya Ilala yapiga marufuku uuzwaji holela wa bidhaa katika soko la Buguruni unaochafua mazingira ya soko na kuhatarisha afya za walaji.

  Hayo yamesemwa leo na Afisa Habari wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala David Langa wakati akifafanua kuhusu kero ya wauzaji holela wanaopanga bidhaa chini katika soko la Buguruni.

  “Bidhaa zinazopangwa chini katika soko la Buguruni sio rasmi na hakuna utaratibu unaoruhusu wauzaji kufanya biashara hiyo, hivyo natoa tahadhari kwa wale wote wenye tabia hiyo kuwa ni marufuku kufanya biashara ya kupanga bidhaa chini na sio kwa soko la Buguruni tu ila katika masoko yote yaliyopo katika manispaa yetu” Alisema Langa

  Afisa langa amesema kuwa wapo maaskari wanaolinda na kuthibiti uuzwaji holela wa bidhaa katika soko hilo ila wauzaji wamekuwa wakifanya mchezo wa kuwavizia maaskari pindi wanapoondoka ndipo wanapanga bidhaa zao.

  Ameongeza kuwa suala hili limekuwa sugu katika masoko mengi na njia ya kukabiliana na changamoto hii ni kuongeza askari wengi watakaokaa muda wote ili waweze kukabiliana na wauzaji holela.

  Aidha Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa kushirikiana na Maafisa Afya inafatilia kwa karibu masoko yote ili kufatilia kama wauzaji wanazingatia kanuni za afya kwa kuweka mazingira safi ili kuokoa afya za walaji.

  Uchafu wa mazingira katika masoko ya Jiji la Dar es Salaam umekithiri na imekuwa ni tatizo sugu lakini Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imejipanga kupambana nalo ili kuondoa uwezekano wa kutokea kwa magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu.

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano sehemu ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga amesema daraja la Kigamboni litaanza kutumika kuanzia Machi mwaka huu.

  Akizungumza mara baada ya kukagua hatua za ujenzi wa daraja hilo Eng. Nyamhanga amemtaka msimamizi wa ujenzi huo kuhakikisha hatua ya ujenzi iliyobaki inakamilika katikati ya mwezi februari na kuanza kazi mwanzoni mwa mwezi Machi.

  “Hakikisheni Machi mosi magari yaanze kupita rasmi kwenye daraja hili na hivyo kufungua ukurasa mpya kwa wakazi wa Kigamboni ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na msongamano katika eneo la Magogoni”, amesema Eng. Nyamhanga.

  Eng. Nyamhanga amesisitiza kuwa Serikali inaangalia uwezekano wa kuunganisha daraja la Kigamboni na barabara ya Charambe,Mlandizi hadi Chalinze ili kupunguza msongamano wa magari katikati ya Jiji.

  Amemtaka meneja wa mradi wa ujenzi wa daraja hilo toka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eng. John Msemo kuhakikisha anatafuta Wakala makini atakayesimamia na kuendesha mradi huo.

  Daraja la Kigamboni lenye urefu wa mita 680, unasimamiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano linatarajiwa kuishi zaidi ya miaka 100 na kuwa na uwezo wa kupitisha mizigo ya tani 56 zinazokubalika katika nchi za jumuiya ya madola.

   Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sehemu ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga (wa nne kushoto), akitoa maelekezo kwa Msimamizi na Meneja Mkuu wa mradi wa ujenzi wa daraja la kigamboni kutoka mfuko wa Hifadhi ya jamii (N.S.S.F) Mhandisi John Msemo (wa kwanza kushoto) wakati wa ziara ya kushtukiza iliyofanywa na Katibu huyo kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo. 
   Msimamizi na Meneja Mkuu wa mradi wa ujenzi wa daraja la kigamboni kutoka mfuko wa Hifadhi ya jamii (N.S.S.F) Mhandisi John Msemo, akimuonesha Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sehemu ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga (wa kwanza kulia)  sehemu ya kipande cha km 1.5 kilichopo upande wa Kigamboni kwa ajili ya upanuzi wa daraja hilo.
   Mwonekano wa Ofisi za Daraja la Kigamboni zitakazotumiwa na wasimamizi wa daraja hilo linalotarajiwa kuanza kazi rasmi mwezi Machi mwaka huu.
   Lango la kuingilia daraja la Kigamboni linavyoonekana, pembeni ni ofisi za huduma mbalimbali zitakazokuwa zinatolewa darajani hapo.
  Sehemu ya juu ya daraja la Kigamboni, likiwa katika hatua za mwisho za ujenzi wake.
  IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO


  0 0

   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam kuhusu uamuzi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  kuwarejesha nyumbani mara moja Mabalozi wawili 


  2.0 Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa

  2.1 Aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenye Serikali ya Awamu ya Nne, Mhe. Mahadhi Juma MAALIM ameteuliwa kuwa Balozi wa kwanza wa Tanzania nchini Kuwait, kufuatia uamuzi wa Serikali kufungua Ofisi ya Ubalozi katika nchi hiyo rafiki.

  2.2 Rais ameagiza Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kanda na Kimataifa kuwarejesha nyumbani mara moja Mabalozi wawili ambao mikataba yao imeisha. Leo hii Mabalozi hao wanatakiwa kukabidhi kazi kwa Afisa Mkuu au Mwandamizi aliye chini yao. Mabalozi hao ni:

  2.2.1 Bi Batilda Salha BURIANI, aliyeko Tokyo, Japan

  2. 2.2 Dkt. James Alex MSEKELA, aliyeko Rome, Italia.

  2.3 Rais amemrejesha nyumbani Balozi wa Tanzania aliyeko London, Uingereza, Bwana Peter Allan KALLAGHE. Anarejea Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa atakapopangiwa kazi nyingine.

  2.4 Kwa maana hiyo, vituo vya Ubalozi vifuatavyo viko wazi:

  2.4.1 London, kufuatia kurejea nchini kwa Balozi Peter A. KALLAGHE

  2.4.2 Brussels, kufuatia aliyekuwa Balozi, Dkt. Deodorous KAMALA kuchaguliwa kuwa Mbunge.

  2.4.3 Rome, Italia, kufuatia kuisha kwa mkataba wa Dkt. James Alex MSEKELA.

  2.4.4 Tokyo, Japan, kufuatia kuisha kwa mkataba wa Bibi Batilda BURIANI

  2.4.5 Kuala Lumpar, Malaysia, kufuatia aliyekuwa Balozi, Dkt. Aziz Ponray MLIMA, kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa.

  2.4.6 Brasilia, Brazil, kufuatia kustaafu kwa aliyekuwa Balozi, Bwana Francis MALAMBUGI.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Advanced Security, Juma Ndambile ambaye pia ni meneja wa bondia Francis Cheka akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari baada ya bondia huyo kurejea akitokea nchini Zambia. Kushoto ni bondia Francis Cheka.
  Bondia Francis Cheka akizungumzia kambi yake ya wiki mbili nchini Zambia ambayo imemjengea stamina, kupata mbinu mpya na jinsi ya kujilinda. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Advanced Security, Juma Ndambile ambaye pia ni meneja wa bondia huyo.
  Meneja Msaidizi wa bondia Francis Cheka akifafanua kwa kina jinsi bonia huyo alivyofanya mazoezi nchini Zambia. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Advanced Security, Juma Ndambile ambaye pia ni meneja wa bondia Francis Cheka.


  Dar es Salaam. Bondia maarufu wa ngumi za kulipwa nchini, Francis Cheka amerejea nchini kutoka Zambia na kusema Mserbia Geard Ajetovic aiandae kupokea kipigo kikali katika pambano lao la mabara la uzito wa super middle la Shirikisho la Masumbwi ya Kulipwa Duniani (WBF).

  Cheka na Ajetovic watapambana kwenye viwanja vya Leaders Club Februari 27 katika pambano lililoandaliwa na kampuni ya Hall of Fame Boxing and Promotion.Akizungumza jana, Cheka alimpongeza meneja wake, Juma Ndambile wa Kampuni ya Advanced Security Limited kwa kumwezesha kuweka kambi nje ya nchi ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya mchezo huo kwa upande wake.

  Alisema kuwa Ndambile na kampuni yake imeonyesha kuwa wanajali na wanamalengo makubwa ya kumwendeleza kutokana na ukweli kuwa amekaa katika kambi ya kisasa yenye mabondia na makocha wazuri nchini Zambia.

  “Kwanza naishukuru kampuni ya Advanced Security Limited kwa kufanikisha kambi hii, nimejifua vya kutosha nchini Zambia, mazoezi yalikuwa magumu na yalihitaji uvulivu mkubwa, kwa kutambua lengo langu ni nini, nilifanya kwa juhudu zote na sasa nipo tayari kwa pambano, hata kesho (leo) nipo tayari kwa bondia yoyote duniani,” alisema Cheka.

  Alisema kuwa kutokana na siku kuwa nyingi, ataendelea na mazoezi hapa hapa nchini huku akisubiri mipango mengine ya meneja wake kwa upande wa maandalizi.Meneja wa Cheka, Juma Ndambile ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Advanced Security Limited alisema kuwa lengo la kampuni yao ni kufanya mapinduzi na kuleta maendeleo katika mchezo wa ngumi za kulipwa hapa nchini.

  Ndambile alisema kuwa Cheka ni bondia mwenye kipaji na hakuwa tayari kuona kipaji hicho kinapotea na kuchukua jukumu la kumwendeleza. “Mimi na kampuni yangu tuna mipango ya kuwamiliki mabondia wengi hapa nchini, kama ilivyo kwa Cheka, nao watapata fursa ya kufanya mazoezi nje ya nchi na kupata mapambano ya kimataifa ya ubingwa ili kuiletea sifa taifa,” alisema Ndambile.

  Alisema kuwa wanataka kutumia vizuri fursa waliyopewa na WBF ambayo inamtaka Cheka ashinde pambano hilo ili aweze kuwania ubingwa wa Dunia hapa hapa nchini.

  0 0


  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
  TAMKO KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI LILILOTOLEWA NA MHE. UMMY MWALIMU (MB); WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, TAREHE 25 JANUARI 2016

  Ndugu Waandishi wa Habari,
  Wizara yangu inaendelea kutoa taarifa ya wiki kwa umma kuhusu mwenendo wa ugonjwa wa kipindupindu hapa nchini. Hadi kufikia tarehe 24 Januari 2016, jumla ya watu 14,608 wameugua ugonjwa huo, na kati yao watu 228 wamepoteza maisha kwa ugonjwa huu. Njombe, Ruvuma na Mtwara ndiyo Mikoa pekee ambayo haijawahi kuripoti mgonjwa yoyote wa kipindupindu, tangu mlipuko huu uanze mnamo mwezi Agosti mwaka huu.

  Kwa mujibu wa Takwimu za kuanzia tarehe 18 hadi 24 Januari 2016, ni kuwa jumla ya Mikoa ambayo imeripoti kuwa na wagonjwa ni 15 ambapo idadi ya wagonjwa 524 na vifo 10 vimeripotiwa. Idadi ya wagonjwa walioripotiwa wiki hii imepungua ukiliinganisha na idadi ya wiki iliyoishia tarehe 17 ambapo kulikuwa na wagonjwa 621 na vifo 14 ambalo ni punguzo la asilimia (16%). Mkoa wa Morogoro badoumeendelea kuripoti idadi kubwa zaidi ya wagonjwa ukilinganishwa na Mikoa mingine, (Manispaa ya Morogoro 89, Halmashauri ya Morogoro 36, Mvomero 17), ukifuatiwa na mikoa ya Mwanza (Ukerewe 36, Nyamagana 19 na Ilemela 13), Simiyu (Bariadi DC 29 na Bariadi municipal 23), Manyara(Simanjiro 48), Mara (Musoma Manispaa 11, Musoma DC 8, Rorya 8 na Butiama 8), Geita(Geita DC 21 na Geita TC 6)  na Mbeya (Kyela 26). 

  Mikoa mingine ambayo bado pia imeendelea kuripoti wagonjwa ni pamoja naDodoma (Wagonjwa 22), Arusha (21), Tabora (18), Singida (18), Lindi (12), Rukwa (7), Kilimanjaro (6) na Kagera (2).

  Ndugu Waandishi wa Habari,
  Mwanzoni mwa mwezi Januari mwaka huu, Wizara yangu kwa kushirikiana na wadau ilituma timu ya jopo la wataalam kutoka ngazi ya Taifa kwenda kusaidiana na wataalam waliopo katika ngazi ya mkoa na halmashauri katika mikoa 7 iliyokuwa inatoa taarifa ya kuwa na  wagonjwa wengi zaidi. Mikoa hiyo ni Arusha, Manyara, Mwanza, Simiyu, Singida, Mara na Morogoro. Mafanikio ya kazi iliyofanywa na Jopo hilo yameanza kuonekana kwani katika Mikoa hiyo saba idadi ya wagonjwa wa kipindupindu imeanza kupungua. Pamoja na mafanikio hayo zipo changamoto ambazo timu hizo ilizibaini kuwepo ambazo zinachangia kulegalega kwa juhudi za kupambana na Kipindupindu nazo ni;

  1. Kuwepo na idadi ndogo ya kaya ambazo zinamiliki na kutumia vyoo bora hususani katika maeneo ambayo yameathirika zaidi na ugonjwa huu.
  2. Kutokuwepo kwa miundombinu stahiki ikiwemo vyoo na maji katika Maeneo ya mikusanyiko kama masoko na minada kutokuwa na
  3. Wananchi kutokutii sheria zilizopo kwa kuendelea kuuza chakula bila kuzingatia kanuni za afya na kuuza matunda yaliyokwisha katwakatwa maeneo yasiyo salama.
  4. Utiririshaji wa maji taka kwenye vyanzo vya maji, pamoja na kujisaidia maeneo ya wazi na pembezoni karibu na vyanzo vya maji.
  5. Kuwepo kwa idadi ndogo ya watu wanaopata maji safi na salama ya kunywa. Aidha utakasaji wa maji katika ngazi ya kaya kwa kuyachemsha au kwa kutumia vidonge vya kutakasia bado ni changamoto kubwa.
  6. Wagonjwa wa Kipindupindu kuchelewa kufika Kambi za Matibabu.
  HABARI ZAIDI SOMA HAPA

  0 0

   Jengo refu lilojengwa chini ya kiwango lililopo katika mtaa wa Indiraghandi jijini Dar,kama lionekanavyo pichani.
   Sehemu ya jengo ambayo inaonekana imepasuka.Picha na Emmanue Massaka wa Globu ya jamii
  Waziri wa Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiwaagiza Watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na Shirika la Nyumba la Taifa kubomoa jengo refu lilojengwa chini ya kiwango lililopo katika mtaa wa Indiraghandi ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa.

  WAZIRI wa Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amewaagiza watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na Shirika la Nyumba la Taifa kubomoa jengo refu lilojengwa chini ya kiwango lililopo katika mtaa wa Indiraghandi ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa.

  Lukuvi ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam kabla ya kuelekea kwenye ziara fupi katika Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani ambapo nako pia amebaini matatizo mbalimbali katika sekta  ya Ardhi.

  “Miezi sita iliyopita Rais Mstaafu alikuja hapa akaagiza jengo hili libomolewe na nyie mkajiridhisha kweli lafaa kubomolewa sasa inakuwaje mpaka leo linaendelea kuwepo, hivyo naagiza mfanye haraka jengo hili ndani ya mwezi mmoja taratibu za ubomoaji ziwe zimeanza ili kulinusuru taifa kuingia katika janga jingine.”alisema Waziri Lukuvi.

  Akiwa bagamoyo waziri Lukuvi alibaini katika Wilaya ya Bagamoyo upotevu wa viwanja  vya wanachi ambavyo walitakiwa kupewa katika eneo la ukuni ambapo vimetoweka 

  Mara baada ya kupata taaarifa hiyo mmoja wa wakaazi wa bagamoyo ambaye alitoa malalamiko juu ya viwanja hivyo mbele ya mkutano wa hadhara na kutaja kuwa Halmashauri ilichukua kiasi cha pesa kuanzia laki sita kwa kila mtu mwaka 2005 na kuahaidi kuwapatia viwanja lakini mpaka leo hawajapewa.

  Mara baada ya kupata taarifa hiyo waziri Lukuvi aliwagiza watendaji wa wilaya hiyo ndani ya miezi sita wawe wamewapatia wakazi hao viwanja hivyo.

  0 0


  DIASPORA COUNCIL OF TANZANIANS IN AMERICA PRESIDENT DR. NDAGA MWAKABUTA. NDANI YA LONGA NA VIJIMAMBOBLOG.

  0 0

  Wakili wa upande wa walalamikaji (waliobomolewa )Abubakari Salim akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya kuahirishwa kwa kesi ya Bomoabomoa kwa Wakazi wanaoishi maeneo ya mabondeni mpaka January 26 mwaka huu ambapo hukumu itatolewa rasmi.
  Wananchi wakimsikiliza Wakili wa upande wa walalamikaji (waliobomolewa )Abubakari Salim leo baaada ya kuahirishwa kwa kesi ya Bomoabomoa,katika Mahakama Kuu,Kitengo cha Ardhi jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanue Massaka wa Globu ya jamii

  0 0

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro (katikati) akifungua mafunzo kwa timu ya ukusanyaji taarifa za tathmini ya kazi (hawapo pichani) kwenye ukumbi wa jengo la Maendeleo ya Jamii Dar es Salaam mapema leo. Kulia kwake ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma Bibi Tamika Mwakahesya na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu wa Maendeleo ya Jamii, Bwana James Kibamba.
   Katibu Mtendaji wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Bibi Tamika Mwakahesya (kulia) akimkaribisha Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro (katikati) kufungua mafunzo kwa  timu ya ukusanyaji taarifa za tathmini ya kazi kwenye ukumbi wa jengo la Maendeleo ya Jamii Dar es Salaam mapema leo. 
   Timu ya washiriki wa ukusanyaji taarifa za tathmini ya kazi wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) alipokuwa akifungua mafunzo ya ukusanyaji taarifa za tathmini ya kazi kwenye ukumbi wa jengo la Maendeleo ya Jamii Dar es Salaam mapema leo.
  Picha ya pamoja

  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Dkt. Larean Ndumbaro amewataka Watumishi watakaoshiriki zoezi la ukusanyaji taarifa za tathmini ya kazi kufanya kazi hiyo kwa uadililifu mkubwa ili kuweza kupata tathmini sahihi ya mishahara ya watumishi wa umma nchini kulingana na majukumu waliyonayo. 

  Katibu Mkuu aliyasema hayo alipokuwa akifungua mafunzo ya ukusanyaji taarifa za tathmini ya kazi yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Maendeleo ya Jamii jijini Dar es Salaam.

  Dkt. Ndumbaro alisema kuwa kazi ya ukusanyaji taarifa za tathmini ya kazi ni kubwa hivyo inahitaji umakini wa hali ya juu.“kama nilivyoeleza hapo awali kwamba kazi hii itawahusu watumishi wa umma wote, ni dhahiri kwamba  mtakutana na watu wa kada, taaluma, uelewa na matarajio tofauti ambapo mtalazimika kutumia weledi wenu wa mahusiano na mawasiliano (interpersonal and communication skills) katika kufanikisha kazi hii kwa ufasaha,” Dkt. Ndumbaro alisisitiza.

  Amewataka washiriki kuwa wasikivu na wepesi wa kuelewa mafunzo haya kwani lengo si kuwapa ujuzi wa kufanya kazi hii peke yake bali kuwajengea uwezo katika kumudu mazoezi kama haya kwa siku za baadae. 

  “Nitafurahi endapo miongoni mwenu mtatokea wataalam wa kuendesha zoezi kubwa kama hili siku za usoni kama wataalam waelekezi (Consultants),” Dkt. Ndumbaro aliongeza.

  Aidha, amemtaka Mtalaam Mwelekezi kufuatilia kwa karibu utendaji wa kila mshiriki ili kuhakikisha kwamba ameelewa, ameshiriki kikamilifu na kuwa anaweza kuaminiwa siku za baadae kuwa sehemu ya kazi kubwa kama hii. 

  Zoezi hili ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Malipo ya Mishahara na Motisha katika Utumishi wa Umma ya mwaka 2010 ambayo imetokana na juhudi za Serikali za muda mrefu katika kuboresha mishahara na masilahi ya watumishi wa umma. 

  Zoezi la Tathmini ya Kazi sio zoezi jipya katika utumishi wa umma kwani zoezi la aina hii lilifanyika mwaka 1998 – 2000 ingawa halikuhusisha utumishi wa umma wote. Zoezi la sasa litapima uzito wa kazi katika utumishi wote wa umma kama ulivyoainishwa katika Hati maalum iliyoanzisha Bodi.Zoezi hili linajumuisha watumishi wa umma katika taaluma mbalimbali kutoka katika maeneo ya pembe zote za Tanzania.

  Akitoa maelezo ya awali, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Bibi Tamika Mwakahesya alisema katika mwaka 2013/14 Bodi ilifanya utafiti ili kubaini hali ya mishahara na masilahi katika utumishi wa umma.

  Katika utafiti huo, ilibainika kuwepo kwa tofauti kubwa sana za mishahara na masilahi katika utumishi wa umma hata kwa kazi zinazofanana. Baada ya utafiti huo ilionekana kuwepo umuhimu wa kuendesha zoezi la Tathmini ya Kazi kama njia ya kubaini uzito wa kazi ambalo maandalizi yake yalianza mwaka 2014/15.

  Zoezi hili, tofauti na zoezi lililokuwa limetangulia, linazishirikisha tumishi zote za umma kama zilivyoelezwa kwenye Hati ya kuanzishwa kwa Bodi na limekusudia kujenga uwezo wa watumishi wa umma. 

  Bodi itaendesha zoezi hili kwa kumtumia Mtaalam Mwelekezi, ambaye ni Kampuni ya Deloitte Consulting Ltd ambaye ametakiwa kufanya kazi na watumishi 70 kutoka kwenye utumishi wa umma ambao watapatiwa mafunzo ya nadharia na vitendo, atawasimamia kukusanya na kuchambua taarifa na mwisho kwa wale ambao watakuwa wametimiza wajibu wao ipasavyo, kwa kushirikiana na Bodi, watatunukiwa Hati Maalum za Ushiriki (Certificate of Participation) na kuingizwa kwenye kumbukumbu za Serikali. Zoezi hili linatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 15 kuanzia mwezi Oktaba 2015.   

  0 0


  Rais Dk. John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Maimu (pichani) kuanzia leo.

  Aidha, baada ya utenguzi huo, Maimu amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi, pamoja na wafuatao. Mkurugenzi wa Tehama, Joseph Makani, Ofisa Ugavi Mkuu, Rahel Mapande, Mkurugenzi wa Sheria, Sabrina Nyoni na Ofisa Usafirishaji, George Ntalima.

  Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akifafanua moja ya swali lililoulizwa kutoka kwa mmoja Waandishi wa habari (hayupo pichani) kuhusiana na suala zima la kusimamishwa kwa Mkurugenzi wa NIDA,katika mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam mapema leo, kuhusu uamuzi wa Rais Magufuli kutengua uteuzi wa Mkurugenzi wa NIDA, Dickson Maimu.
  Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akizungmza katika mkutano na waandishi wa habari, Ikulu Dar es Salaam leo, kuhusu uamuzi wa Rais Magufuli kutengua uteuzi wa Mkurugenzi wa NIDA, Dickson Maimu.Picha Michuzi Jr-MMG 

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
  RAIS Dk.John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA),Dickson Mwaimu kwa ajili kupisha uchunguzi wa sh. Bilioni 179.6 zilizotolewa kwa ajili ya vitambulisho.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mkuu Kiongozi , Balozi Ombeni Sefue amesema kutengua uteuzi huo ikiwa ni pamoja na baadhi ya watendaji wa vitambulisho vya taifa kusimamishwa kazi ambao ni Mkurugenzi wa Tehama ,Joseph Makani , Afisa Ugamvi Mkuu, Rahel Mapande ,Mkurugenzi wa Sheria, Sabrina Nyoni ,pamoja na Afisa Usafirishaji ,George Ntalima.

  Balozi Sefue,amesema kuwa kutengua uteuzi huo unatokana na kuwepo kwa malalamiko ambayo yamemfikia Rais juu ya wananchi kukosa vitambulisho vya taifa huku kukiwa na fedha ya Sh.Bilioni 179.6 zikiwa zimetumika .

  Rais Dkt Magufuli ameitaka Taasisi ya Kupambana na Rushwa (Takukuru) ifanye uchunguzi kama kuna vitendo vya rushwa vimefanywa ,amezitaka taasi ya Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),Mamlaka ya Manunuzi (PPRA) kufanya uchunguzi wa manunuzi yote yaliyofanywa na NIDA.

  Amesema katika uchunguzi huo CAG ifanye uchunguzi na kuangalia vitambulisho vya taifa kama vinaendana na fedha iliyotumika ya sh.bilioni 179.6.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

  Simu: 255-22-2114512, 2116898
  E-mail: press@ikulu.go.tz
  Tovuti : www.ikulu.go.tz              

  Faksi: 255-22-2113425
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amempongeza Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mheshimiwa Ban Ki-moon kuunda jopo la watu mashuhuri watakaomshauri juu ya namna bora ya kuendeleza na kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu hususani katika afya ya uzazi ya Mama na mtoto.

  Jopo hilo la watu mashuhuri linaongozwa na wenyeviti wenza ambao ni Rais wa Chile Mheshimiwa Michelle Bachelet na Waziri Mkuu wa Ethiopia Mheshimiwa Hailemariam Desalegn, huku Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete na Rais Mstaafu wa Finland Mheshimiwa Tarja Halonen wakiteuliwa kuwa wenyeviti mbadala.

  Katika Pongezi hizo Rais Magufuli amesema kuteuliwa kwa Rais Kikwete kuwa miongoni mwa jopo la kumshauri Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kumeijengea heshima Tanzania na kumechochea matumaini ya mafanikio ya kukabiliana na changamoto za afya ya mama na mtoto hususani kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania.

  Rais Magufuli ameahidi kuwa serikali yake ya awamu ya tano itatoa ushirikiano katika kutimiza malengo ya maendeleo endelevu ambayo jopo hilo litamshauri Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ikiwemo katika kuimarisha afya ya uzazi wa mama na mtoto.

  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Dar es salaam
  25 Januari, 2016

  0 0


  0 0

   Mwanaharakati wa Haki za Binadamu, Rebeca Gyumi akizungumza jambo na Wakili wakujitegemea, Jebra Kambole baada ya kutoka Mahakama Kuu ambako wamefungua hauri la Kikatiba la kupinga sheria ya ndoa kifungu cha 13 na 17 vinavyoruhusu mtoto wa kike chini ya miaka 18 kufunga ndoa.
   Mwanaharakati wa Haki za Binadamu, Rebeca Gyumi akizungumza na Waandishi wa Habari nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania baada ya kutoka Mahakamani hapo ambapo wamefungua shauri la Kikatiba la kupinga sheria ya ndoa kifungu cha 13 na 17 vinavyoruhusu mtoto wa kike chini ya miaka 18 kufunga ndoa, ambapo wameona hiyo ni kumnyima mtoto wa kike haki yake ya msingi katika jamii. 
  Wakili wakujitegemea, Jebra Kambole kizungumza na Waandishi wa Habari nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania baada ya kutoka Mahakamani hapo ambapo wamefungua shauri la Kikatiba la kupinga sheria ya ndoa kifungu cha 13 na 17 vinavyoruhusu mtoto wa kike chini ya miaka 18 kufunga ndoa, ambapo wameona hiyo ni kumnyima mtoto wa kike haki yake ya msingi katika jamii.

  Na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
  VIFUNGU vya sheria ya ndoa vinavyoruhusu mtoto wa kike kuolewa chini ya miaka 18 vyapingwa mahakama kuu leo jijini Dar es Salaam.

  Vipengele vinavyopingwa ni kifungu cha sheria cha 13 na 17 vya sheria ya ndoa (CAP 29 R.E 2002), sheria inayotoa mwanya kwa mtoto wa kike kuolewa akiwa na miaka 14 kwa kibali cha mahakana na miaka 15 kwa ridhaa ya wazazi ambayo ni kinyume na ibara ya 13, 12 na 18 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 19977 zinazotoa haki ya usawa mbele ya sheria kutokubaguliwa, kuheshimu utu wa mtu na uhuru wa kujieleza.

  Kesi ya kupinga vifungu  vya sheria ya ndoa vinavyoruhusu mtoto wa kike kuolewa chini ya miaka 18  ni keshi ya kikatiba yenye namba tano ya mwaka 2016 iliyofunguliwa na Mwanaharakati wa haki za binadamu, Rebeca Gyumi na kusimamiwa na wakili Jebra Kambole wa Law Guards Advocate.

  Akizungumza na waandishi wa jijini Dar es Salaam leo Mwanaharakati wa Haki za Binadamu, Rebeca Gyumi  ameomba mahakama kuu kufutia mbali vifungu vya sheria hivyo na kupandisha umri wa chini wa kuoa  kwa wanaume na kuolewa kwa wanawake kuwa ni miaka 18.

  Aidha Rebeca amesema kuwa  ndoa za utotoni kwa wasichana ni ukiukwaji wa haki za binadamu pia kuzaa kwa msichana akiwa na umri mdogo ni chanzo kikubwa cha matatizo ya Fistula na vifo vingi vya wajawazito.

  0 0


  0 0


  Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi katibu mkuu wa Ambassador FC, Bakari Khalid kwa ajili ya maandalizi ya ligi daraja la pili mkoa wa Shinyanga. 
  Baadhi ya wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi katika hafla ya makabidhiano ya hundi kwa timu ya Ambassador kwa ajili ya maandalizi ya ligi daraja la pili mkoa wa Shinyanga.
  Vikosi vya timu za Buzwagi fc na Ambassador vikiwa katika maandalizi wakati wa ukaguzi kabla ya kuanza kwa mhezo.

  0 0


  0 0

  Uongozi wa Benki ya Walimu Tanzania (MCB) umekanusha vikali taarifa iliyotolewa katika mtandao wa ZOOM Tanzania na mitandao mingine ya kijamii ikidai kuwa benki hiyo iko katika mchakato wa kujaza nafasi 120 za ajira.

  Taarifa hiyo iliyoanza kutolewa Ijumaa tarehe 22, 2016 inadai kuwa MCB imetafuta wataalamu washauri katika sekta ya benki wanaojulikana kama Quality Service Consultants kusimamia swala zima la ajira hizo na mafunzo katika muda wa miezi sita.

  Imesema kuwa baada ya hapo, wale watakaofaulu wataajiriwa na benki hiyo na kuendelea na mafunzo kwa vitendo chini ya uangalizi wa wataalamu.

  Pia taarifa hiyo iliyotolewa na mtu aliyejiita Christopher Mwakingwe ilidai kuwa benki hiyo inatafuta wazoefu na wenye bidii ambao wako tayari kufanyakazi katika mazingira shindani na kwenye matawi ya benki hiyo yanayoanzishwa nchini pote.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Afisa Mkuu Mtendaji wa benki hiyo, Bw. Ronald Manongi alisema taarifa hiyo ni ya uongo na yenye lengo la kupotosha umma.

  “Benki haijawahi kutoa tangazo kama hilo wala kutafuta mtaalam mshauri kufanya kazi hiyo kwa niaba yetu,” alisema Bw. Manongi.

  Alitoa tahadhari kwa wananchi kutoomba kazi hizo kwani hazipo.

  “Tunaitaka kampuni hiyo kukanusha taarifa hiyo kupitia mitandao waliyotumia ndani ya siku tatu kuanzia leo na kueleza chanzo cha taarifa hizo au wachukuliwe hatua za kisheria na benki,” alisema Bw. Manongi.

  Benki hiyo pia imeitaka Quality Service Consultants kueleza ni mara ngapi wameshatoa taarifa kama hiyo siku za nyuma na watu wengine wanaoshirikiana nao kuchapisha taarifa za uongo zenye nia ya kupotosha umma.

older | 1 | .... | 1101 | 1102 | (Page 1103) | 1104 | 1105 | .... | 3285 | newer