Na Mugishagwe Zablon
Ingawa dunia inataja nchi nyingi kusgindwa kufikia malengo ya milenia klushindwa kutimiza bWasichana na wanawake nchini wametakiwa kuchangamkia fursa zinazojitokeza katika taasisi mbalimbali ikiwa ni pamoja na za Chama cha Skauti wa Kike (Girl Guide) ili kupambana na mambo ambayo yanachangia ukatili kwa wanawake.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Msichana anaweza kuzuia ukatili dhidi ya Wanawake’, Mratibu wa kampeni hiyo, Agnes Fivao alisema wasichana kwa nafasi yao wanaweza kudhibiti hali hiyo kwa kuwa viungo baina yao na wanajamii wengine.
“Wewe Girl Guide au msichana mwingine yeyote, unafanya nini kuwasaidia wenzako wanaokuzunguka ambao hawaendi shule, wanaotumikishwa katika ajira mbaya, una nafasi ya kuwaunganisha, kufikiri mbali zaidi, kuwa na mtazamo wa kudunia katika kile kinachowakabili” alisema.
Alibainisha kuwa ulimwengu bado unakabiliwa na changamoto kubwa ya tohara kwa wasichana na wanawake, biashara ya binadamu hususan watoto wa kike na wasichana wataweza kupambana nayo kwa kutoa taarifa, kupaza sauti na kuwaelimisha wengine.
“Mnatakiwa kuwa sauti yao na skauti wa kike ni walinzi wa wanawake wenzao” alisema na kuongeza kuwa wasichana na wanawake wanatakiwa watambue kuwa wanatakiwa kupiga hatua zaidi kimaendeleo kutoka katika kujiongoza hadi kuongoza wengine. Awali aizungumza wakati wa uzinduzi huo ambao uliambatana na maadhimisho ya kila mwaka toka 1926 ya muanzilishi wa skauti ulimwenguni Lord Robert Baden-Powell, Mkufunzi wa Girl Guide mkoa wa Dar es Salaam, Margareth Olumbe alisema watafanya shughuli mbalimbali za kijamii kuanzia sasa hadi siku ya kilele 22 Februari mwaka huu 2016.
“Tutafanya usafi na shughuli zingine za kijamii, kuanzia ngazi ya Taifa hadi wilaya, kutoa huduma katika vituo vya wasiojiweza, Hospitalini na kwingineko” alisema na kuongeza kuwa kauli mbinu ya mwaka huu ni kuwaunganisha wasichana na wanawake milioni 12 ulimwenguni ifikapo 2020.
Dunia bado inakabiliwa na changamoto ya kushindwa kufikia lengo namba tatu la milenia kuelekean 2015 linalotaka Usawa wa Kijinsia na kwa Wanawake na kazi ya ziada inahitajika kufanyika ili kupata uwiano huo ikiwa ni pamoja na wasichana na wanawake kujisimamia wenyewe badala ya kusubiri njia zingine.
Kamishna wa Chama cha Skauti wa Kike (Girl Guide), Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Shaba akizungumza wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya kuanzishwa taasisio hiyo ulimwenguni katika hafla ilioyofanyija jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mkufunzi wa mafunzo, Margreth Olumbe.
Mwenyekiti wa Chama cha Maskauti wa Kike, Sawi Dath (kushoto) na mkufunzi wa mafunzo wa chama hicho, Margareth Plumbe wakiimba nyimbo za hamasa wakati wa uzinduzi wa maadhimuisho ya chama hicho ya kila mwaka, jijini Dar es Salaam,
Waasisi na wanachama wa Chama cha Maskauti wa Kike, wakizindua maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwa muasisi wa chama hicho ulimwenguni, Lord Robert Baden-Powell jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Chama cha Maskauti wa Kike, Sawi Dath (kushoto) na mkufunzi wa mafunzo wa chama hicho, Margareth Plumbe wakiimba nyimbo za hamasa wakati wa uzinduzi wa maadhimuisho ya chama hicho ya kila mwaka, jijini Dar es Salaam.