Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1099 | 1100 | (Page 1101) | 1102 | 1103 | .... | 3272 | newer

  0 0  SIMU.TV: Niyonzima aanza kazi na vigogo wa msimbazi viroho kwatu pata dondoo za magazeti hapa: https://youtu.be/4fkYnXxHIR8 
   SIMU.TV: Marudio uchaguzi Zanzibar Machi 20. Magufuli atinga ngome ya Lowassa kijeshi. Wasomi walaumiwa sakata la Zanzibar; https://youtu.be/1LOdcwETk1Y  
   SIMU.TV: Kamati ya bunge kizaazaa. Kivuli cha Lowasa chatesa bunge. Asha Bakari azikwa. Waziri awachimba mkwara wakurugenzi; https://youtu.be/xUbPAtwZLjM 

  0 0


   


  EAC logo

    The Federal Republic of Germany signed an intergovernmental agreement with the East African Community (EAC) to support the economic integration, regional health facilities and water resource management. Germany signed a total of 37 million euros in grants to the EAC for 2016-2018, highlighting the strong commitment to support the integration process in East Africa.   

  ·         10 million euro in financial assistance will be invested in the establishment of a regional network of reference laboratories for communicable diseases. With this project, the German Government responds to a request for support from the EAC for the prevention and control of epidemic outbreaks in the region. Another 10 million euros in financial assistance will be used for Integrated Water Resource Management of Lake Victoria aiming at improving water provision and management of water resources. Both projects will be implemented by KfW development bank.

  ·         17 million euros in technical assistance will be made available to further support of the economic integration process, including a contribution to the EAC partnership fund. The programme is focusing on institutional strengthening of the EAC Secretariat and on supporting the implementation of the Customs Union, Common Market Protocols and Monetary Union. This includes the elimination of Non-Tariff Barriers such as tax harmonisation as well as Mutual Recognition Agreements for qualifications. At the same time Germany will support the EAC in promoting private investment especially in the pharmaceutical sector, including the establishment of a regional quality infrastructure for the pharmaceutical sector. These projects will be implemented by GIZ and PTB – German Metrology Institute.

  During the signing ceremony, Amb. Dr. Richard Sezibera, the EAC Secretary General, thanked the German government for her continued support to the Integration Agenda especially at a time when integration facing challenges across the world. He said this particular financing agreement comes at the right time when the Community is finalising its New Vision 2050. 

  Mr. John Reyels, Chargé d` Affaires of the German Embassy Dar es Salaam, said: “Our support underlines the importance we give to the East African Community. The EAC is a role model and pace-setter in Africa and we are proud working closely with you in order to contribute to the well-being and prosperity of the citizens of this region.”

  Since cooperation began in 1998 the total volume of German support to the EAC amounts to almost 213 million euro. Germany also has substantial bilateral cooperation with all five EAC Partner States.

   Mr. John Reyels, Chargé d` Affaires of the German Embassy Dar es Salaam, signing the intergovernmental agreement with the EAC’s Secretary General Amb. Dr. Richard Sezibera.
  Mr. John Reyels, Chargé d` Affaires of the German Embassy Dar es Salaam, in a group photo with EAC’s Secretary General Amb. Dr. Richard Sezibera and other members after the signing ceremony of the intergovernmental agreement between Germany and the EAC.

  0 0


  Leo ni Hepi Besdei  ya kuzaliwa mdau wa 
  Libeneke Alhaj Mohammed Mbilili.
  Happy Birthday Mdau.

  0 0

  Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na wananchi wa Arusha Mjini wakati akipita kuelekea Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli ambako pamoja na mambo mengine jana kafunga zoezi la Onesha Uwezo Medani na  leo  anatarajiwa kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli kundi la 57/15.
  Amiri Jeshi Mkuu,Rais Dkt Magufuli akiwasikiliza wananchi kwa makini alipopita maeneno ya Sanawali kuwasalimia wakati akielekea Wilayani Monduli.
  Baadhi ya Wananchi wa Maeneo ya Sanawali wakishangilia ujio wa Rais John Pombe Joseph Magufuli,alipokuwa akielekea Wilayani Monduli mapema jana  asubuhi.
  Rais Magufuli akiwa amevalia sare za kijeshi amesimamishwa na kuwasalimu wananchi katika maeneo ya SANAWALI, TEKNIKO, NGARENALO, MBAUDA, MAJENGO na KISONGO


   Umati mkubwa uliojitokeza katika eneo la Mianzini Mkoani Arusha

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini General Davis Mwamunyange wakati wa ufungaji wa zoezi la Onesha Uwezo Medani lililofanyika Monduli nje kidogo ya Jiji la Arusha.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini General Davis Mwamunyange wakati akielekea kupewa maelezo ya zoezi zima la Onesha Uwezo Medan.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya Maafisa wa jeshi katika tukio hilo la Ufungaji.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kwenye uwanja wa maonesho akiwa pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi (kulia) na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini General Davis Mwamunyange (wa pili kulia).
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Ntibenda, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange  na Maafisa wa ngazi za juu wa Jeshi mara baada ya kufunga zoezi la Onesha Uwezo Medani Monduli Mkoani Arusha.
  Kwa habari na picha zaidi BOFYA HAPA  0 0


  0 0

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akizungumza na raia wa China wanaoishi nchini, katika sherehe yao ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake, Waziri Kitwanga alisema Tanzania inatambua ushirikiano mzuri wa miaka mingi uliopo kati yake na China, hivyo raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi nchini, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni, kamwe haitagusa wenye vibali halali.

   Kaimu Balozi wa China nchini, Zhang Biao akizungumza katika sherehe ya raia wa China wanaoishi nchini ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam, kabla ya kumkaribisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (hayupo pichani) kuja kuzungumza na mamia ya wachina hao waliohudhuria sherehe hiyo. Katika hotuba yake, Waziri Kitwanga alisema Tanzania inatambua ushirikiano mzuri, wa miaka mingi uliopo kati yake na China, hivyo raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi Tanzania, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni nchini, kamwe haitagusa wenye vibali halali.

   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick akimpongeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto), kwa kutoa hotuba nzuri iliyowafafanulia wachina waishio nchini kuwa Serikali ya Tanzania inawajali na inatambua umuhimu wa ushirikiano wao uliodumu kwa kipindi cha miaka mingi, hivyo raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi Tanzania, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni nchini, kamwe haitagusa wenye vibali halali. Wachina waishio nchini jana walifanya sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip na kuhudhuriwa na mamia ya wachina hao.  Kulia ni Kaimu Balozi wa China nchini, Zhang Biao
   Raia wa China wanaoishi nchini wakishindana kula Tunda aina ya Tikiti wakati wa Sherehe yao ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam. Katika Sherehe hiyo ambayo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (hayupo pichani) alikuwa mgeni rasmi ilihudhuria na mamia ya raia hao wa China. Hata hivyo, Waziri Kitwanga alisema raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi Tanzania, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni nchini, kamwe haitagusa wenye vibali halali.

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akiwapongeza raia wa China walioshinda mchezo wa bahati nasibu walioucheza katika sherehe yao ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam. Waziri Kitwanga katika hotuba yake alisema nchi yake inatambua ushirikiano mzuri wa miaka mingi uliopo kati yake na China, hivyo raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi nchini, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni, kamwe haitagusa wenye vibali halali.

   Kikundi cha Karate kinachoongozwa na raia wa China wanaoishi nchini kikitoa burudani katika sherehe yao ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (hayupo pichani) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo, katika hotuba yake alisema nchi yake inatambua ushirikiano mzuri wa miaka mingi uliopo kati yake na China, hivyo raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi nchini, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni, kamwe haitagusa wenye vibali halali. 

  Sehemu ya raia wa China wanaoishi nchini, wakimsikiliza kwa makini, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba yake kwa Wachina hao katika sherehe yao ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam jana. Waziri Kitwanga katika hotuba yake alisema nchi yake inatambua ushirikiano mzuri wa miaka mingi uliopo kati yake na China, hivyo raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi nchini, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni, kamwe haitagusa wenye vibali halali. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


  0 0

  Basi la Kampuni ya BM linalofanya safari zake kati ya Dar es salaam - Morogoro, limepata ajali usiku wa kuamkia leo katika eneo la Mikese Mkoani Morogoro, na kupelekea watu wawili kupoteza maisha na wengine 43 kujeruhiwa. Basi hilo liligongana na gari lingine na kutumbukia kwenye Korongo.

  Chanzo cha ajali hiyo, inadaiwa ni mwendo kasi wa Basi hilo uliopelekea kushindwa kusimama baada ya kukuta Lori lililokuwa limeharibika na kuegeshwa pembeni, huku upande mwingine kukiwa na Lori lingine likipita.
  Basi la Kampuni ya BM linavyoonekana baada ya kupata ajali hiyo.


  0 0

  Baadhi ya Maafisa wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Mbeya, wakiongoza shughuli ya Mazishi ya aliyekuwa mkurugenzi wa michezo Jeshi la Magereza Tanzania na Kocha wa zamani wa kikosi cha Tanzania Prison, Marehemu Hassan Mlwilo, yaliyofanyika kwenye kijiji cha Mabanda wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya leo.
  Baadhi ya waombolezaji wakishiriki kwenye Mazishi ya aliyekuwa mkurugenzi wa michezo Jeshi la Magereza Tanzania na Kocha wa zamani wa kikosi cha Tanzania Prison, Marehemu Hassan Mlwilo, yaliyofanyika kwenye kijiji cha Mabanda wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya leo.

  0 0

  msitu
  Na. Ahmad Mmow, Nachingwea.

  Baadhi ya wananchi na viongozi wa kijiji cha Ngunichile, wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi. Wameiomba serikali kuharakisha na kukamilisha mchakato wa uvunaji wa msitu wa kijiji hicho.

  Wananchi na viongozi hao waliyasema hayo mbele ya timu ya waandishi wa habari na maofisa wa Mtandao wa jamii wa usimamizi wa misitu (MJUMITA) waliokwenda kijijini hapo juzi ili kuona mafanikio na changamoto za uhifadhi misitu.

  Wakizungumza na Ripota wetu, walisema urasimu ambao hawaujui unatokana nanini, umesababisha uvunaji wa mazao ya misitu kwenye msitu waliohufadhi uchelewe kuanza.

  Bakari Lilombo aliyejitambulisha ni mwanajamii, alisema kutoanza uvunaji wakati miti imefikia umri wa kuvunwa kunasababisha baadhi ya wananchi kukatatamaa kutokana na kutoona manufaa ya msitu huo."Uvunaji ungeanza ungeingiza mapato ambayo yangetumika kununua zana za kilimo na kujenga visima vya  vya maji, lakini kwa hali hii tunakata tamaa,"alisema Bakari.

  Mzee Hamis Malombe mwanajamii, alisema matarajio ya wananchi nikunufaika na mapato ya mazao ya msitu huo wenye hekta 1800, kupitia huduma za jamii. Hata hivyo wananchi wanakata tamaa na matarajio yao yameanza kutoweka.  Bi Maua Ntila, ambae ni mjumbe waserikali ya kijiji hicho, alisema mapato ambayo yangetokanana mauzo mazao ya msitu huo yangeweza kutumika kuchimba visima na kuboresha zahanati. Jambo ambalo lingekuwa ni ukombozi kwa akinamama wakazi wa kijiji hicho.


  Hatahivyo hadi sasa hawajaanza uvunaji, ingawa walitaraji uvunaji ungekuwa umeanza tangu mwaka jana. Kwa upande wake, ofisa mtendaji wa kijiji hicho, Selemani Soya, alisema hatua za awali za maandalizi ya uvunaji zilishafanyika.

  Ofisi ya mkurugenzi wa wilaya ya Nachingwea iliwahaidi wangeanza uvunaji mwaka jana mwezi novemba, hata hivyo hadi sasa hawajaanza kuvuna."Tunapata shida ya kupambana na wavunaji haramu,maana maeneo mengi hayana miti"kwahiyo eneo lenye miti ni msitu huu, kama tungeanza uvunaji naamini wangeogopa na tungekuwa na nafuu sana,"alisema Selemani.

  Akijibu malalamiko hayo kwaniaba ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Nachingwea. Ofisa misitu wa halmasiauri hiyo, Paiton Kamnana, alisema uvanaji umechelewa kuanza kwasababu kutokamilika baadhi ya taratibu, nyaraka na nyundo.

  Hata hivyo maandalizi yote yamekamilika, kwahiyo muda si mrefu uvunaji utaanza.
  "Nyaraka zilishafuata wizarani,nyundo imeshapatikana pia.Ilikuwa jambo lisilowezekana kuanza uvunaji kabla ya kuwapa plan(mpango)".

  Utunzaji wa msitu huo nimatokeo ya elimu iliyotolewa na mashirika yasiyo kiserikali ikiwamo Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania(MJUMITA) kupitia mradi wa kampeni ya mama misitu kwa kushirikiana na serikali.

  0 0

   Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Iramba Mashariki, Mhe. Allan Kiula kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Januai 23, 2016.
   Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Cecilia Daniel Paresso kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Januai 23, 2016.
  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Azza Hillal  Hamad kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Januai 23, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  IMG-20160123-WA0051
  Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na wafanyabiashara wa eneo la Msalato lililopo mkoani Dodoma sehemu ambayo inatumika kufanyia mnada wa nyama choma ikiwa ni moja ya ziara zake kufatilia hali ya ugonjwa wa kipindupindu katika maeneo mbalimbali ya nchi, akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya hiyo, Dkt. Jasmine Tiisekwa (mwenye skafu shingoni) pamoja na Afisa Afya Mkuu wa Manispaa ya Dodoma Bw. Alek Barakena (mwenye suti nyeusi).

  Na Rabi Hume, Modewjiblog
  Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu ametembelea eneo la Msalato lililopo mkoani Dodoma sehemu ambayo inatumika kufanyia mnada wa nyama choma ikiwa ni moja ya ziara zake kufatilia hali ya ugonjwa wa kipindupindu katika maeneo mbalimbali ya nchi.
  Baada ya kutembelea mnada huo, Mhe. Ummy aliwataka wananchi wa eneo hilo kutambua kuwa bado ugonjwa wa kipindupindu upo na unaendelea kusambaa maeneo mbalimbali ya nchi hivyo ni wajibu wao kama wananchi kuweka mazingira yao katika hali ya usafi ili kutokomeza uonjwa huo.
  Aidha ili kuzidi kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu, Waziri Ummy ameagiza kuendelea kutekelezwa kwa agizo la Mkuu wa Wilaya hiyo, Dkt. Jasmine Tiisekwa ambaye aliagiza kusimamishwa kwa shughuli za kuuza nyama nyoma katika eneo hilo la Msalato mpaka uongozi wa wilaya hiyo utakapojiridhisha kuwa ugonjwa wa kipindupindu umetoweka mkoani Dodoma.
  “Kipindupindu kimesambaa sehemu nyingi nchini ikiwepo hapa Dodoma na hivyo naagiza katazo la Mkuu wa Wilaya, Dkt Jasmine Tiisekwa liendelee kuwepo hadi ugonjwa wa kipindupindu uishe Dodoma na niwajibu wa kila mwananchi kuhakikisha kipindupindu kinakwisha,” alisema Waziri Mhe. Ummy.
  Pamoja na hayo pia Waziri huyo wa Afya ameutaka uongozi wa Manispaa ya Dodoma kufanya kikao cha pamoja na wafanyabiashara hao wa nyama choma ili kuona ni jinsi gani wanaweza kuendelea na biashara zao huku wakizingatia kanuni za usafi wa afya na mazingira bila kusababisha kuzidi kusambaa kwa kipindupindu.
  IMG-20160123-WA0050
  Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akifafanua jambo kwa wafanyabiashara wa eneo hilo.
  IMG-20160123-WA0045
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akitoa maagizo ya wafanyabiashara hao kusitisha shughuli zao mara moja katika eneo hilo la Msalato mpaka uongozi wa wilaya hiyo utakapojiridhisha kuwa ugonjwa wa kipindupindu umetoweka mkoani Dodoma.
  IMG-20160123-WA0043IMG-20160123-WA0044
  Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili kushoto), Mkuu wa Wilaya hiyo, Dkt. Jasmine Tiisekwa (wa tatu kulia) na Afisa Afya Mkuu wa Manispaa ya Dodoma Bw. Alek Barakena (kushoto) wakisikiliza hoja kutoka kwa mmoja wa wafanyabiashara wa eneo hilo (hayupo pichani).
  IMG-20160123-WA0046
  Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akisikiliza hoja kutoka kwa mmoja wa wafanyabiashara wa eneo la Msalato lililopo mkoani Dodoma sehemu ambayo inatumika kufanyia mnada wa nyama choma ambaye jina lake halikupatikana alipofanya ziara ya katika eneo hilo.

  0 0

  Yamoto Band waliweka Kambi ya Siku 3 katika jiji la Tanga wakiwa wanashoot video ya wimbo wao Mpya ambao unaitwa MAMA na Director Pablo, Video ya wimbo huo inatarajiwa kuachiwa mapema wiki ijayo. Kiongozi wa Yamoto Band Aslay amesema kuwa wameamua kwenda kufanya Video hiyo Tanga ili Kubadirisha Mazingira na pia kuleta Utofauti na Video zingine ambazo tayari wameshazifanya, Lakini pia aliwaomba mashabiki kupokea kazi hiyo ambayo inatoka hivi Karibu kwani niwimbo Mzuri wenye maneno mazuri kuhusu Mama maana kila mmoja amezaliwa na Mama.

  0 0
 • 01/23/16--19:00: NGOMA AZIPENDAZO ANKAL

 • 0 0
  0 0

  STAR TV 
  Lowassa, Maalim Seif waishika Zanzibar, CUF Zanzibar watoa tamko. Kwa habari zaidi fuatilia uchambuzi wa magazeti hapa;  https://youtu.be/DefGw875Hi8 
  TBC 
  Wabunge viti maalum ruksa udiwani, mashangigi 3 ya serikali yaibwa, Paulsen mshahara milioni 33 Simba.Tazama uchambuzi wa magazeti; https://youtu.be/4_dooVvZIuk 
  AZAM TV 
  Shikamoo Yanga, Simba mbele kwa mbele FA na Liverpool yapiga mtu goli 5. Kwa undani zaidi fuatilia uchambuzi wa magazeti hapa;  https://youtu.be/eGEVIV76EoI


  0 0

  Vijana katika manispaa ya Morogoro wametakiwa kutumia fursa mbalimbali zinazotolewa na wadau wa sekta za maendeleo ili kufikia malengo yao ya kiuchumi. 
   Akiongea wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya wiki sita ya ujasiriamali chini ya programu ya Kijana Jiajiri, Mkuu wa mkoa huo, Dkt. Rajabu Rutengwe amesema mpango huo ni moja ya fursa ambazo zinatakiwa kuchangamkiwa ili kujenga uwezo wa vijana katika manispaa hiyo. 
   Kijana Jiajiri ni program ya kukuza na kuendeleza ujasiriamali kwa vijana wa Tanzania wenye umri wa miaka 18-35. Inatekelezwa na Taasisi ya Kuendeleza Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC) kwa kushirikiana na Taasisi ya kuendeleza Vijana ki-biashara ya Uingereza (YBI) na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC). 
   “Hii ni fursa kubwa sana, vijana wanatakiwa kutilia mkazo mafunzo kama haya,” alisema Dkt. Rutengwe. Amesema vijana wengi wanaingia katika biashara pasipo kuwa na uelewa mpana wa kufanya biashara na kutambua namna ya kukabiliana na ushindani wa masoko. “Kwa bahati nzuri programu kama hizi zinahudhuriwa na wafanya biashara waliofanikiwa, hivyo wanawatia moyo kwa kutoa ushuhuda wao wa mafanikio,” aliongeza. 
   Aliiomba TECC kutoishia katika manispaa ya Morogoro na badala yake waende katika manispaa nyingine za mkoa huo ili kuwajengea uwezo vijana wengine katika ufanyaji biashara na swala zima la kujiajiri. 
   Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa alisema programu hiyo ni muhimu sana kwa kuwa malengo yake ni kuwalea vijana kuelekea kwenye ajira zao binafsi. “Baada ya mafunzo haya, vijana hawa watapata malezi ya mwaka mmoja, kila kijana ataunganishwa na mfanyabiashara mzoefu ili amuongoze,” alisema. 
   Alisema mara baada ya malezi hayo vijana wataweza kupatiwea mikopo kupitia dhamana ya serikali ili waweze kufanya biashara zao kwa uhakika zaidi. Mkurugenzi Mtendaji wa TECC, Bw. Sosthenes Sambua alisema mpaka sasa wameshafundisha takribani vijana 260 na tayari wameshawatafutia walezi. 
   “Tumeshafanya mafunzo haya katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Dar es Salaam kwa mafanikio makubwa,” alisema Sambua. Alishukuru uongozi wa manispaa hiyo kwa kuhamasisha vijana ambao walijitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo. 
   “Vijana wameuliza maswali ya msingi sana,” aliongeza. Mmoja wa vijana, Bi. Winfrida Kimaro ameishukuru taasisi hiyo kwa kuwapelekea programu hiyo katika mkoa wao na amewaomba waendelee katika kuwafikia vijana wengi zaidi ili kupunguza tatizo la ajira nchini.
   “Vijana wengi bado tuna mawazo ya kuajiriwa, hivyo mafunzo haya yatatutoa katika dhana ya kuajiriwa na kufikiria kujiajiri zaidi,” alisema. Kwa mkoa wa Morogoro mafunzo yamedhaminiwa na benki ya Barclays.
   Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Rajabu Rutengwe akimkabidhi fomu mmoja wa vijana aliyehudhuria uzinduzi wa programu ya kijana Jiajiri mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Beng’i Issa. Programu hiyo ya kukuza na kuendeleza ujasiriamali kwa vijana wa Tanzania inatekelezwa na Taasisi ya Kuendeleza Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC) kwa kushirikiana na Taasisi ya kuendeleza Vijana ki-biashara ya Uingereza (YBI) na NEEC.
   Vijana wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Rajabu Rutengwe wakati wa uzinduzi wa programu ya kijana jiajiri mkoani hapo mwishoni mwa wiki. Programu hiyo ya kukuza na kuendeleza ujasiriamali kwa vijana wa Tanzania inatekelezwa na Taasisi ya Kuendeleza Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC) kwa kushirikiana na Taasisi ya kuendeleza Vijana ki-biashara ya Uingereza (YBI) na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).
   Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dkt. Rajabu Rutengwe akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa programu ya kijana Jiajiri mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki. Programu hiyo ya kukuza na kuendeleza ujasiriamali kwa vijana wa Tanzania inatekelezwa na Taasisi ya Kuendeleza Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC) kwa kushirikiana na Taasisi ya kuendeleza Vijana ki-biashara ya Uingereza (YBI) na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).
  Vijana wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Rajabu Rutengwe wakati wa uzinduzi wa programu ya kijana jiajiri mkoani hapo mwishoni mwa wiki. Programu hiyo ya kukuza na kuendeleza ujasiriamali kwa vijana wa Tanzania inatekelezwa na Taasisi ya Kuendeleza Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC) kwa kushirikiana na Taasisi ya kuendeleza Vijana ki-biashara ya Uingereza (YBI) na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).

  0 0


  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Charles Kitwanga amesema zoezi linaloendelea sasa la kukamata raia wa kigeni wanaoishi na kufanya kazi hapa nchini bila vibali halitawagusa wageni wenye vibali halali. 
  Mheshimiwa Kitwanga ameyasema haya mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na jumuiya ya raia toka nchini China wakati wa sherehe zilizoandaliwa na raia hao katika Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam. 
  Katika sherehe hizo ambazo ziliandaliwa mahsusi kuukaribisha mwaka Mpya wa Kichina, Mheshimiwa Kitwanga alisema uhusiano wa Tanzania na China ulianzishwa na marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Kiongozi wa China, marehemu Mao Zedong zaidi ya miaka hamsini iliyopita. 
  Amesema uhusiano huo umeendelea kuimarishwa hadi katika nyanja za kiuchumi ambapo hadi sasa kuna zaidi ya Kampuni 500 za Kichina ambazo zinafanya shughuli za kibiashara hapa nchini ambazo zimetoa zaidi ya nafasi 100,000 za kazi kwa Watanzania. 
  Mheshimiwa Kitwanga alitumia fursa ya sherehe hizo kuwahakikishia wawekezaji wote waliopo hapa nchini kuwa Serikali ya Tanzania italinda biashara zao kufuatana na sheria za nchi. 
  Kuhusu zoezi linaloendelea hapa nchini la kukamata wageni ambao wanaishi na kufanya kazi bila vibali halali alisema kumekuwa na taarifa za uzushi zinazoenezwa hapa nchini na nje ya nchi kuwa Serikali ya Tanzania inawafukuza wageni kwa vile haihitaji raia wa kigeni hapa nchini. 
  Amesema taarifa hizo ni za uongo zinazolenga kuichafua Tanzania katika jumuiya ya kimataifa na kusema raia wa kigeni wanaokamatwa ni wale tu wasio na vibali halali vya kuishi na kufanya kazi hapa nchini. 
  Amesema zoezi hilo ni la kawaida na linafanywa kufuatana na Sheria za Uhamiaji lakini halitawahusu wageni wenye vibali halali vya kufanya kazi na kuishi nchini. 
  Kati ya mwaka 2014 na Januari 2016 Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imetoa vibali vya ukaazi kwa jumla ya wageni 40,765 toka mataifa mbalimbali na idadi hiyo inaendelea kuongezeka siku hadi siku. 
  Wageni waliofukuzwa kwa sababu mbalimbali mwaka 2015 ni 1,642.


  Aidha, kati ya 08 Desemba, 2015 na 14 Januari, 2016 raia wa kigeni waliokamatwa kwa kuishi na kufanya kazi nchini bila vibali halali ni kama ifuatavyo:


  1.Burundi 284

  2.Kenya 26

  3.Uganda 13

  4.Somalia 7

  5.Ethiopia 157

  6.DRC 34

  7.China 285

  8.India 41

  9.Zambia 40

  10.Nigeria 08

  11.Lebanon 01

  12.Ivory Coast 10

  13.Madagascar 05

  14.Malawi 27

  15.Korea 09

  16.Zimbabwe 01

  17.Ghana 01

  18.Rwanda 03

  19.Afrika Kusini 01

  20. Wenye uraia wa utata 11.  Kati ya hawa, wengine wamemepelekwa katika kambi za wakimbizi, hasa raia waliotokea Burundi, wengine wamepewa amri ya kuondoka nchini na wengine kesi zao ziko katika hatua mbalimbali mahakamani.


  0 0

   Mafundi Wa Shirika la Maji Safi na Nakitaka Dar es salaam, wakiendelea na kazi ya ukarabati wa Bomba la Maji la Wazo - Tegeta, uliopelekea kukosekana kwa Maji katika maeneo mengi ya Jiji la Dar es salaam.

  0 0

   Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Majeshi Nchini Jenerali Davis Mwamunyange wakati alipowasili katika chuo cha Maafisa wa Kijeshi Monduli Mkoani Arusha kwa ajili ya kuwatunuku Kamisheni Maafisa wapya wa Jeshi kwa cheo cha Luteni Usu, anayetazama katikati ni Mkuu wa Chuo hicho Meja Jenerali Paulo Peter Massao. 
   Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipungia mkono wananchi wakati akiwasili kwenye viwanja vya Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli kwa ajili ya kuwatunuku Kamisheni Maafisa wapya wa jeshi kwa cheo cha Luteni Usu.

   Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipigiwa wimbo wa Taifa kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi katika viwanja vya Chuo hicho.

   Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya
   Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia gwaride lililokuwa likipita mbele yake  kutoa heshima.
   Gwaride la Wahitimu likipita kutoa heshima mbele ya mgeni rasmi  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


older | 1 | .... | 1099 | 1100 | (Page 1101) | 1102 | 1103 | .... | 3272 | newer