Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110126 articles
Browse latest View live

MBINU ZA KISASA ZA KUPAMBANA NA MAFURIKO JIJINI DAR ES SALAAM


WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AONGOZA MKUTANO WA WABUNGE MJINI DODOMA LEO

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua mkutano wa wabunge, bungeni mjini Dodoma Januari 22, 2016.  Kulia ni Spika wa Bunge Job Ndugai na kushoto ni Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kahilillah.
 Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, Nenelwa Mwihambi akitoa mada katika mkutano wa wabunge ulioongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, buneni mjini Dodoma Januari 22, 2016. Watatu kulia ni Spika wa Bunge Job Ndugai na kulia ni Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashilillah
 Spika wa Bunge Job Ndugai akizungumza kumkaribisha Mwenyekiti wa Mkutano wa Wabunge, Waziri Mkuu, Kassim Majliwa kufungua mkutano huo bungeni mjini Dodoma Januari 22, 2016. Kulia ni Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilillah. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

ASHANTI YAONDOLEWA KOMBE LA SHIRIKISHO

$
0
0

Kikao cha Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kilichoketi jana na kupitia taarifa mbalimbali za michezo ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) mzunguko wa pili, kimeiondoa klabu ya Ashanti United kwenye michuano hiyo na nafasi yake kuchukuliwa na klabu ya Africa Lyon.
Katika kikao hicho kamati ilipokea malalamiko ya klabu ya Africa Lyon dhidi ya Ashanti United kwa kumchezesha mchezaji Enock Balagashi kwa jina la Awesu Abdu katika mchezo namba 3, uliochezwa tarehe 15 Disemba, 2015 na Ashanti kuibuka na ushindi kwa mikwaju ya penati.
Kamati imejiridhisha baada ya kupitia taarifa ya mchezo huo, na kubaini klabu ya Ashanti United ilifanya udanganyifu wa kumtumia mchezji huyo kwa jina la mchezaji mwingine, huku ikitambua kuwa kufanya hivyo ni makosa na mchezo huo ulikuwa ukionyeshwa moja kwa moja kwenye kituo cha luninga cha Azamtv.
Kwa mujibu wa Kanuni no. 41 (12) ya uthibiti wa viongozi kufungiwa miezi 12, Kamati imemfungia Katibu Mkuu wa klabu ya Ashanti kutojihusisha na masuala ya mpira wa miguu kwa kipindi cha miezi 12.
Aidha Kamati pia kwa kutumia kanuni ya 37 (15) ya udhibiti wa wachezaji, mchezaji Enock Balagashi amefungiwa kwa kucheza mpira kwa kipindi ch amiezi 12 na faini ya shilingi laki tatu (300,000).
Kamati imevitaka vilabu vya ngazi zote nchini kuheshimu vipindi vya usajili kwa kufanya usajili wa wachezaji watakaowatumia, na kuheshimu kanuni na taratibu zinazoendesha michuano inayoandaliwa na TFF.
Africa Lyon watacheza dhidi ya Azam FC mznguko wa tatu siku ya Jumatatu katika Uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.

INTRODUCIN DHAMANA YA HAKI BY YUZZO

Balozi Haule akutana na Balozi wa Hungary jijini Nairobi

$
0
0
 Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. John Michael Haule akizungumza na Balozi wa Hungary Mhe. Laszlo Mathe jiji Nairobi. Serikali ya Hungary imetoa nafasi 30 za masomo kwa Tanzania kwa miaka mitatu kuanzia mwaka huu. Wawakilishi hao wa Nchi pia alizungumzia ushirikiano wa kiuchumi, ambapo Hungary imeahidi kushawishi wawekezaji kuanzisha miradi ya ubia ya viwanda itakayosisitiza uhamishaji wa teknolojia kwa Tanzania
Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. John Michael Haule akiagana na Balozi wa Hungary Mhe. Laszlo Mathe baada ya mazungumzo yao jijini Nairobi.

YAnga isitarajie mteremko keshokutwa - Friends Rangers

$
0
0

UONGOZI wa klabu ya Friends Rangers, umesema klabu ya Yanga isitarajie mteremko katika mchezo wao wa kutania kombe la FA, utakaofanyika keshokutwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. 
 Ofisa habari wa klabu hiyo Asha Kigundula, alisema licha ya kujua wanacheza na timu inayoongoza Ligi Kuu, wao wamejipanga kushinda mchezo huo. 
 Kigundula alisema kuwa tayari kikosi chao kipo kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo wa mzunguko wa tatu wa michuano hiyo. 
Alisema Yanga isiwadharau na kuona wanacheza na timu ndogo inayocheza Ligi Daraja la kwanza wao wanaingia kamili kupata matokeo mazuri ya ushindi. 
 Kigundula alisema Yanga isiifananishe timu yao na timu iliyoifunga mabao 5-0, hivyo kwao wanakuja kamili kuhakikisha wanaitoa na kuendelea katika hatua inayoufuata. 
 "Tumejipanga kushinda hivyo Yanga ifute ndoto za kutufunga kwa sababu juzi ilipata ushindi wa mabao mengi, wameifunga timu ambayo ilipanda kizengwe wasubili waone tutakachowafanya"alisema Kigundula
Hata hivyo Kigundula amewataka mashabiki wa timu hiyo wajitokeze kwa wingi katika mchezo wao ili waweze kuwapa hali zaidi wachezaji wao wacheze kwa kujiamini.

WAFANYAKAZI WA MIZANI NCHINI WAASWA

$
0
0
Wafanyakazi wa Mizani hapa nchini wametakiwa kufanya kazi kwa uwazi, uadilifu, na weledi ili kuzingatia sheria zinazoongoza sekta hiyo na hivyo kutenda haki kwa wasafirishaji wote na kujenga taswira nzuri kwa taasisi hiyo. 
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Julias Chambo katika mafunzo kwa maofisa waendesha mizani hapa nchini yanayofanyika mjini Morogoro. 
“Sasa tubadilike tujenge taswira njema katika sekta ya mizani kwa kuepuka vitendo vya rushwa kwa kufanya kazi kwa uwazi na kulinda barabara zetu”, amesema Eng. Chambo. 
Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uelewa wa pamoja watumishi wote wa mizani nchini juu ya utelekelezaji wa majukumu yao na kupunguza malalamiko yasio na msingi katika sekta hiyo muhimu kwa uchumi wa nchi. 
Naye mkuu wa mizani wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Eng Lucian Kilewo amewataka watumishi wa mizani kutumia elimu walioipata katika kutekeleza majukumu yao na kuipeleka kwa wenzao ili sekta hiyo ipate mabadiliko yanayoendana na wakati wa sasa.
“Mafunzo haya yataendelea mara kwa mara ili kuhakikisha mnakuwa na uelewa wa pamoja katika kuimarisha sekta ya mizani nchini na kuiwezesha kufanyakazi kwa tija na kulinda barabara zinazojengwa kwa fedha nyingi”. amefafanua Eng. Kilewo. 
Mkurugenzi wa matengenezo (TANROADS) Eng. Joseph Lwiza amesema Wakala wa Barabara nchini wamejipanga kutatua changamoto zinazojitokeza katika vituo vya mizani nchini kote na kuwa na mfumo mmoja utakaowezesha kazi zinazofanywa katika mizani kuonekana moja kwa moja makao makuu ya TANROADS na Wizarani ili kuimarisha uwazi na kudhibiti rushwa. 
Wataalam hao wa mizani pia wametembelea mizani zinanopima uzito wa magari katika mwendo weigh in motion katika eneo la Mikese na Vigwaza na kujionea mfumo huo unavyofanya kazi na kupunguza msongamano wa magari. 
Takriban mizani 70 zinapima uzito wa magari hapa nchini tatu zikiwa za magari yanayopimwa yakiwa katika mwendo, 29 mizani za kuhamisha-mobile na 41 mizani za kudumu –fixed ambapo nia yake ni kuhakikisha magari yababeba uzito unaokubalika ili kulinda barabara.
 Maofisa uendeshaji mizani nchini wakifuatilia mada katika mafunzo ya kujengewa uelewa wa pamoja mjini Morogoro.

Mkuu wa Mizani Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng.Lucian Kilewo akifafanua jambo katika mafunzo ya  kuwajengea uelewa wa pamoja maafisa uendeshaji wa Mizani yanayofanyika mjini Morogoro.Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa matengenezo wa TANROARDS Eng.Joseph Lwiza akifuatiwa na Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng.Julius Chambo na Kaimu Mkurugenzi msaidizi Eng.Joyce Mbunju.

CLUB ROUGE @ HYATT IS ONLY PLACE TO BE THIS SATURDAY


Watumishi NEC wapongezwa kwa kufanikisha Uchaguzi Mkuu 2015

$
0
0
 Afisa Ushirika toka Manispaa ya Ilala Bi. Mihayo Malunde akielezea umuhimu wa Watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuanzisha kikundi cha akiba na mikopo (SACCOS) wakati wa kikao kazi kilichofanyika mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

 Afisa Ufuatiliaji toka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bw.  Ambrose Manyanda akielezea mafao mbalimbali yanayotolewa na mfuko huo kwa watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) hawapo pichani,  wakati wa kikao kazi kilichofanyika mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva akiongea na watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakati alipokwenda kuwashukuru na kuwapongeza watumishi wa tume hiyo kwa kuweza kufanikisha zoezi la uchaguzi kwa mafanikio makubwa mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

 Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Ramadhan Kailima (aliyesimama) akifurahia jambo na watumishi wa tume hiyo wakati  Wajumbe na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi  walipokwenda kuwashukuru na kuwapongeza watumishi wa tume hiyo kwa kuweza kufanikisha zoezi la uchaguzi kwa mafanikio makubwa
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Ramadhan Kailima (aliyesimama) akiwakaribisha wajumbe na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi wakati Wajumbe hao na Mwenyekiti walipokwenda kuwashukuru na kuwapongeza watumishi wa tume hiyo kwa kuweza kufanikisha zoezi la uchaguzi kwa mafanikio makubwa. 

Picha zote na Eliphace Marwa -Maelezo

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA ASHIRIKI DUA MAALUM YA KUMUOMBEA MAKAMU MWENYEKITI WA UWT CCM TAIFA KWENYE MAZISHI YALIYOFANYIKA LEO

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kulia, Mama Salma Kikwete katikati, Mama Mwanamwema  Shein kushoto na Wananchi wa Zanzibar, wakiwa katika Dua ya Pamoja ya kumuombea aliyekua Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa (UWT) Marehemu Asha Bakari Makame iliyofanyika leo Januari 22,2016 nyumbani kwao Jang’ombe kabla ya mazishi yake yaliyofanyika katika kijiji cha Kianga Wilaya ya Magharibi Unguja.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kulia akimfariji Mama Mzazi wa aliyekua Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa (UWT) Marehemu Asha Bakari Makame, Bibi Mwanajuma Faki (90) wakati wa Dua maalum iliyofanyika leo Januari 22,2016 nyumbani kwao Jang’ombe Zanzibar, Mhe. Asha amezikwa leo kijijini kwake Kianga Wilaya ya Magharibi Unguja.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kulia, Mama Salma Kikwete katikati, Mama Mwanamwema  Shein kushoto na Wananchi wa Zanzibar, wakiwa katika Dua ya Pamoja mbele ya Jeneza lenye Mwili wa aliyekua Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa (UWT) Marehemu Asha Bakari Makame iliyofanyika leo Januari 22,2016 nyumbani kwao Jang’ombe kabla ya mazishi yake yaliyofanyika katika kijiji cha Kianga Wilaya ya Magharibi Unguja. Picha na OMR

Spika Rebecca Kadaga (Mb) wa Uganda afunga Warsha ya siku mbili ya Sekretarieti ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Jijini Dar es Salaam

$
0
0

Spika Rebecca Kadaga (Mb) wa Uganda afunga Warsha ya siku mbili ya Sekretarieti ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya Wajumbe wa Sekretarieti ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika kutoka nchi mbalimbali za Afrika wakichangia mada katika Warsha kuhusu ushirikishwaji wa wanawake katika ngazi za maamuzi wakati wa siku ya ufungaji warsha hiyo iliyofanyika Jijini Dar es Salaam 21-23 Januari, 2016. 
Picha zote na habari na Benedict LiwengaSPIKA wa Bunge la Uganda, Mhe. Rebecca Kadaga (Mb), ambae pia ni Mwenyekiti wa CWP Kimataifa amezihasa nchi Wanachama wa Sekretarieti ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika kuendelea kuwathamini wanawake kwa kuwapa vipaumbele vya ushiriki katika ngazi za maamuzi pamoja na kuwaenzi wanawake waliotoa mchango wa maendeleo ya nchi zao.Spika Kadaga ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati akifunga rasmi Warsha ya siku mbili iliyohusu kujadili ushiriki wa wanawake katika ngazi za maamuzi ili kubuni mbinu na mikakati ya kuongeza idadi ya Wanawake katika ngazi za siasa na kijamii.Mhe. Kadaga ameeleza kuwa, nchi Wanachama hazinabudi kuthamini mchango mkubwa wa wanawake katika masuala ya kijamii pamoja na kisiasa, hivyo kuna haja ya kuwaenzi kwa kutunza nyaraka zao muhimu ikiwemo kuwaendeleza wanawake kielimu ili kuweza kuleta maendeleo katika nchi husika.“Ni vema tukaaangalia mchango mkubwa unaotolewa na Wanawake katika nchi zetu hususani katika masuala ya kijamii pamoja na kisiasa, basi  nchi zetu hazinabudi kuwajali kwa kuwashirikisha katika ngazi zote muhimu ili kuwe na usawa kati ya wanawake na wanaume, lakini pia kuna haja ya jamii husika kuwaelimisha wanawake hawa ili waweze kuleta mchango mkubwa katika jamii zetu”, alisema Spika Kadaga.Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya CPA Kanda ya Afrika, Mhe. Lindiwe Maseko (Mb) kutoka Afrika Kusini, amezidi kuipongeza Tanzania katika hatua nyingine kwa kujali haki na usawa katika masuala ya kisiasa ambapo pia ameimwagia sifa kwa uchaguzi uliopita wa mwaka 2015 kuwa wa huru na haki na kuzitaka nchi nyingine za Afrika kufanya chaguzi zake kuiga mfano huo.Kwa upande wao Wajumbe wa Warsha hiyo wameendelea kujadili masuala mbalimbali ambayo yanaweza kuleta mabadiliko katika jamii kwa kuhakikisha kuwa wanawake wanapewa fursa sawa na wanaume katika masuala ya kisiasa na kijamii ambapo msisitizo mkubwa unaotolewa katika warsha hiyo ni ‘ushiriki wa wanawake katika ngazi za maamuzi’.Sambasamba na hilo, suala la kuwashirikisha wanawake kwa njia ya Vyombo vya habari na mitandao ya kijamii limezungumziwa katika warsha hiyo ambapo msisitizo umetolewa wa kutumia mitandao hiyo kwa njia ya kuelimisha umma juu ya nafasi ya mwanamke katika ngazi za maamuzi ambapo endapo ikitumiwa vema inaweza kuleta usawa katika jamii.Nchi zilizoweza kushiriki katika Warsha hiyo ni Tanzania, Uganda, Kenya, Ghana, Nigeria, Zambia, Mauritus pamoja na Afrika Kusini.


Mazishi ya marehemu Bi. Asha Bakari Makame yaliyofanyika leo asubuhi katika makaburi ya Kianga Wilaya ya Magharibi Unguja

$
0
0
Viongozi mbali mbali wakishiriki mazishi ya marehemu Bi. Asha Bakari Makame yaliyofanyika leo asubuhi katika makaburi ya Kianga Wilaya ya Magharibi Unguja. Miongoni mwa viongozi hao ni pamoja na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Pili Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohd Gharib Bilal na Spika wa BLW Mhe. Pandu Ameir Kificho. 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiitikia dua baada ya kumsomea hitma Marehemu Asha Bakari Makame iliofanyika katika Masjid Noor-Muhammad kwa Mchina Unguja 
WANANCHI wakishiriki katika dua ya kumuombea marehemu Asha Bakari Makame katika Masjid Noor-Muhammad kwa mchina.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiweka udongo kaburini
Makamu wa Rais Mstaafu Dkt Mohamed Gharib Bilal akiweka udongo kaburini
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe Maalim Seif Shariff Hamad akiweka udongo kaburini. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Serikali kuendelea kutoa elimu ya Uzalishaji na matumizi endelevu ya rasilimali

$
0
0
Hassan Silayo-MAELEZO 
 Serikali kuendelea kutoa elimu ya Uzalishaji na matumizi endelevu ya rasilimali kwa wananchi ili waweze kunufaika na rasilimali zote zilizopo katika maeneo yao kote nchini. 
 Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam na Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) Bw.Carlos Mbuta wakati wa mkutano na vyombo vya Habari ikiwa ni moja ya mikakati ya Serikali katika kuelimisha umma kuhusu matumizi sahihi ya rasilimali ikiwemo ardhi. 
Akifafanua Mbuta amesema kuwa Elimu hiyo itawasaidia wananchi kungamua na kufanya maamuzi sahihi pale wanapotaka kutumia rasilimali zilizopo katika kujiletea maendeleo.
 ’Elimu ya mazingira imejumuishwa katika mitaala ya shule zetu hapa nchini ili kujenga uelewa kuhusu matumizi sahihi ya rasilimali alisisitiza Mbuta Akizungumzia faida za Elimu ya Mazingira kutlowa mashuleni mbuta alibainisha kuwa itasaidia kujenga kizazi chenye uelewa na uwezo wa kutumia rasilimali zilizopo kwa kuzingatia sheria na kanuni.
 Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mipango Miji kutoka Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. George Pangawe alitoa wito kwa wananchi kufuata taratibu zote za kisheria pale wanapotaka kuendeleza Kipande chochote cha ardhi. 
 Aliongeza kuwa Serikali kupitia Wizara yake inasimamia matumizi sahihi ya uendelezaji wa ardhi na kuwataka wananchi kuunga mkono juhudi za Serikali katika kusimamia Sheria na Kanuni zinazosimamia Sekta ya ardhi. 
 Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Mazingira pamoja na Halmashuri zote nchini zimekuwa zikisisitiza kuhusu elimu ya uzalishaji na matumizi endelevu ya rasilimali ili ziweze kuwanufaisha wananchi.
 Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mipango Miji kutoka Wizara ya Ardhi,|Nyumba na Maendeleo ya Makazi George Pangawe akizungumza na Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) kuhusu wananchi kuzingatia sheria na kanuni za mipango miji  nchini pale wanapotaka kuendeleza ardhi kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Mazingira Carlos Mbuta na kulia ni Mkuu wa Idara ya Mipango Miji, Ardhi na Mazingira Manispaa ya Kinondoni Bi. Juliana Letara

 Mkuu wa Idara ya Mipango Miji, Ardhi na Mazingira Manispaa ya Kinondoni Bi. Juliana Letara akisisitiza jambo kwa Waandishi wa Habari  Jijini Dar es Salaam kulia niMsaidizi Idara ya Mipango Miji kutoka Wizara ya Ardhi,|Nyumba na Maendeleo ya Makazi George Pangawe na kushoto ni 
Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Mazingira Carlos Mbuta

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

$
0
0

SIMU.TV: Mbio za Kilimanjaro marathon zimezinduliwa rasmi mkoani Moshi ambapo wanariadha zaidi ya elfu 7 wanatarajiwa kushiriki; https://youtu.be/ysQLaLMk_N
 SIMU.TV: Mamlaka ya chakula na dawa nchini TFDA, imeanza kutoa elimu ya usalama wa chakula kwa wanafunzi ili kuboresha afya zao: https://youtu.be/3-6jWGcB49A
 SIMU.TV: Wizara ya mambo ya ndani inakabiliwa na changamoto ya msongamano wa wafungwa na kuruhusu adhabu ya vifungo vya nje: https://youtu.be/nQA43X1le_c
 SIMU.TV: Mpango wa serikali ya awamu ya tano wa kutoa elimu bure umewezesha kuongezeka kwa idadi kubwa ya wanafunzi wanaoandikishwa:https://youtu.be/xoB_pGX6j4Q
 SIMU.TV: Jopo la wafanyakazi wa wizara ya habari kutoka nchini china wamewasili nchini Tanzania kwa ajili ya kubadilishana uzoefu: https://youtu.be/SKVHm_ARebU
 SIMU.TV: Fahamu mambo mengi kutoka kwa wakazi wa mkoa wa Manyara wakikujuza jinsi wanavyokabiliwa na baa kubwa la njaa https://youtu.be/LlldgAuKt84
 SIMU.TV: Jifunze mengi kutoka kwa Mkurugenzi wa elimu ya ulipaji kodi kutoka TRA, akikuelimisha kuhusu suala la ulipaji kodi: https://youtu.be/S8_KFLTlk-U
 SIMU.TV:  Yajue mengi kutoka kwa Katibu mkuu wa jumuiya za serikali za mitaa akikujuza kuhusu Kuelekea mkutano wa 32 wa serikali za mitaa:https://youtu.be/4Tv6_MooNkA
 SIMU.TV: Fahamu mengi kutoka kwa wakala wa afya mahala pa kazi OSHA, Wakikujuza kuhusu sheria za usalama na afya kwa wafanyakazi: https://youtu.be/8vZP9BdoLZc

AGONGA MAGARI MAWILI, PIKIPIKI NA MAMA MUUZA UJI JIJINI MBEYA..


BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 22.01.2016

SIMU TV: UCHAMBUZI WA HABARI TOKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI January 22, 2016.

introducing Karanga by Cosmoo Mnyamwezi

NGOMA AZIPENDAZO ANKAL

EAC SECRETARY GENERAL RECEIVES CREDENTIALS FROM FINNISH AMBASSADOR

$
0
0
cid:image001.png@01D154FC.4DC0AE60
East African Community
  The East African Community Secretary General, Amb. Dr. Richard Sezibera, today received credentials from the Ambassador Extraodinary and Plenipotentiary and Permanent Representative of Finland to the EAC, H.E. Pekka Hukka. 
Speaking at the function, Amb. Hukka said that his appointment was out of his government’s commitment to deepen its cooperation with the EAC, noting the significance of regional integration not only for East Africans, but as an important source of growth for the continent as well. 
Expressing his gratitude to the Finnish Government for her dynamic support to the EAC, the Secretary General shed light on the region’s increased market size, which has led the Community to expand on cross-border production chains. 
Finland is a regular contributor to the Partnership Fund, a basket fund which enables the Community to make significant achievements in various sectors.

 H.E. Pekka Hukka, Ambassador Extraodinary and Plenipotentiary and Permanent Representative of Finland to the EAC, listening in to updates on regional integration from EAC’s Secretary General Amb. Dr. Richard Sezibera.
H.E. Pekka Hukka, Ambassador Extraodinary and Plenipotentiary and Permanent Representative of Finland to the EAC, in a group photo with EAC’s Secretary General Amb. Dr. Richard Sezibera and other members after presenting his credentials.
Viewing all 110126 articles
Browse latest View live




Latest Images