Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live

Open Sanit, MSA brings safety guard products in Tanzania

$
0
0

MSA Segment Leer for Sub Saharan Africa Mbuwa Ngomani (left) gives a special gift to Junaco Angela Limited Human Resource Angela Rwehumbiza at the ceremony, on the centre of the picture is Open Managing Director Octavian Mshiu. PhotoS BY Nicco Mediatz
This is the group picture of the people that attended the seminar at Sea Cliff hotel in Dar es Salaam

Iist from the left is The Open Sanit General Manager Mr Baraka Mwakatumba in a photo with his fellow workers at the seminar in Sea Cliff Hotel
Annastazia KIlonda working with Open Sanit as Public Relations 

Dustan Biyengo from Tanzania Ports Authority sows the attendants of the seminars on how to wear protected helmet when they are at work places
By Nicco Mediatz Reporter

Open Managing Director Octavian Mshiu.
TANZANIA companies have now not to be worried on safety of their workers when they are at work places since the joint venture of the Open Sanit from Tanzania who joins with a South African firm MSA for the sake of bringing safety guards products in Tanzania to ensure that workers are working safely at work places without ‘accidents’ that may happened without having protective gears.

The joint venture has brought in to Tanzania the health safety guards products services such as uniforms, security wears, safety and security boots, protective gears, embroidery, printing and tents and tarpaulins.

Speaking yesterday at Sea Cliff Hotel in Dar es Salaam after launching the safety products, open Sanit Managing Director Octavian Mshiu said that all of their products are made in house or finished and other specialized services which requires international accreditations such as ISO ,SABS are made through international partners such as MSA, Beier Safety, SACLA.

Mshiu added that the aim of bringing the safety product in the country is to make sure that the when people are at work are supposed to be safe so as ensure safeness at work
He also give an advice to some of the companies in Tanzania which do not provide to their workers boots or safety gears when they are at work places and urged them that they must give them such protectors in order to make sure that they are in safe hands when they at work.

For his part, MSA Managing Director Mbuwa Ngomani said that the safety guard properties will help workers to be confortable and working without fearing of the accidents.
Ngomani also said that the move will assures the workers security and increase the workers ability of doing work.

‘‘The companies in Tanzania have to understand the importance of the safety guards products as to secure their workers when they are at work places, ’’he said
Open Sanit Companies are dedicated to quality, efficiency, and timely deliveries, we believe in professionalism and we work as teams which have earned us a place for two consecutive years now in TOP 100 MIDE SIZED Companies in both year 2011 and 2012.

Our 180 staffs [both permanent and casual] have been touched in a special way with these achievements and altogether have agreed to keep the dreams and spirits high understanding the challenges ahead of us.

AIPS yaahidi kusaidia mafunzo kwa waandishi wa habari za michezo wa Tanzania

$
0
0
CHAMA cha Kimataifa cha Waandishi wa Habari za Michezo (AIPS),kimeahidi kusaidia masuala mbalimbali yahusiyo mafunzo kwa waandishi wa habari za michezo wa Tanzania.

Rais wa AIPS,Gianni Merlo raia wa Italia aliwapa fursa viongozi wa vyama vya waandishi wa habari za michezo wa Afrika kuwasilisha changamoto mbalimbali zinazovikabili vyama vyao, lakini kati ya hizo changamoto waitaje moja ambayo wanataka AIPS isaidie kuwapa msaada.

Tunashukuru Merlo kwanza alivutiwa sana na namna Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kinavyofanya kazi zake na ushiriki wake wa mikutano ya Dunia mara kwa mara, hali ambayo aliahidi yeye binafsi kusaidia chama chetu kuboresha masuala ya kimsingi.

Kubwa ambalo AIPS baada ya kuelezwa imesema italipangia utaratibu ni suala la mafunzo kwa waandishi wa habari chipukizi na wanawake kwani hayo ni baadhi ya mambo ambayo wenyewe wanayatilia mkazo na hasa baada ya kujulishwa kuwa kuna wanahabari zaidi ya 50 wanawake hapa nchini wanaofanya kazi kwenye masuala ya michezo.

Hata hivyo ingawa TASWA iliomba isaidiwe mafunzo kwa wanachama wake wote kwa kupatiwa wataalamu hasa wakati huu ambao kuna changamoto kubwa ya teknolojia ya habari na mawasiliano, lakini AIPS imesema kwa mwaka huu uwezo wake ni kwa waandishi wa habari za michezo chipukizi kupitia programu inayoandaliwa na AIPS.

Lakini Rais wa AIPS aliutaka ujumbe wa Tanzania utakapokuwa umerudi nyumbani umuandalie mikakati hiyo kwa mafunzo ya wanawake ili ikiwekezekana yafanyike kwa awamu katika kipindi cha miezi 18 kutegemea na idadi ya wahusika na pia gharama zenyewe.

Nchi wanachama 103 duniani zikiwemo nchi 24 za Afrika zilihudhuria mkutano huo uliomalizika juzi Sochi, Urusi, ambapo pia ulifanyika uchaguzi wa viongozi wa AIPS watakaokuwa madarakani kwa miaka minne ijayo, ambapo Merlo alipita bila kupingwa.

Mkutano Mkuu wa AIPS ambao ni wa 76 ulimalizika juzi, ambapo kulikuwa na kikao cha makatibu wakuu wa kila nchi kilichoendeshwa na Katibu Mkuu wa AIPS, Roslyn Morris ambapo Tanzania iliwakilishwa na Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando na huko pia suala la tuzo mbalimbali zinazotolewa na wanahabari zilizungumzwa kwa kina.

Pia kulifanyika kikao cha marais wa AIPS wa mabara na baadhi ya viongozi wa vyama vya wanahabari wa michezo wa Afrika kilichokuwa chini ya Merlo, ambapo nilidhuria na ajenda kubwa ilikuwa suala la rushwa kwenye michezo na mambo ya upangaji wa matokeo wa mechi mbalimbali.

Baada ya mkutano huo, wakati ujumbe wa Tanzania ukiwa njiani kurejea nyumbani ulipitia jijini Moscow, Urusi na kuzungumza masuala mbalimbali na Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Jaka Mwambi.

Kwa ujumla mkutano ulikuwa na manufaa makubwa kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla, ambapo masuala mengine mengi yaliyojitokeza kwenye mkutano huo ikiwemo namna ya mafunzo hayo yatakavyofanyika tutayazungumza Jumatano ijayo kwenye mkutano na wanahabari utakaofanyika ukumbi wa City Sports Lounge, Dar es Salaam saa tano asubuhi.

TASWA ni mwanachama hai wa AIPS yenye makao yake makuu Lausanne, Uswisi, ndiyo sababu kila mwaka tumekuwa tukishiriki mikutano hiyo tangu tulipoingia madarakani mwaka 2010.Mwaka 2011 tulishiriki Mkutano Mkuu wa AIPS uliofanyika Seoul Korea, Korea Kusini na tuliwakilishwa na Makamu Mwenyekiti, Maulid Kitenge na Katibu Msaidizi, George John

Pia tulishiriki Mkutano Mkuu wa AIPS uliofanyika Innsbruck, Austria Januari mwaka jana, ambapo Katibu Mkuu, Amir Mhando alihudhuria.

Nawasilisha.

Juma Pinto
Mwenyekiti, TASWA
21/04/2013

MKUTANO WA TUICO MOROGORO WAFANYIKA MKOANI MOROGORO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhandisi Stella Manyanya, akilakiwa na baadhi ya viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri, TUICO, katika ukumbi wa Midland Inn, Morogoro jana, muda mfupi kabla ya hafla ya kumtunuku cheti cha uanachama wa heshima ndani ya chama hicho, kama ishara ya kuenzi mchango wake.
Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere, Profesa Issa Shivji, kushoto, akilakiwa na baadhi ya viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri, TUICO, katika ukumbi wa Midland Inn, Morogoro jana, muda mfupi kabla ya hafla ya kumtunuku cheti cha uanachama wa heshima ndani ya chama hicho, kama ishara ya kuenzi mchango wake.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri, TUICO, Omary Ayub Juma wa kwanza kulia, akiimba wimbo wa mshikamano muda mfupi kabla ya kuanza hafla ya kuwatunuku vyeti vya heshima baadhi ya wanachama wake wastaafu kama ishara ya kuenzi mchango wao ndani ya chama, (katikati) ni Katibu Mkuu wa Chama hicho, Boniface Nkakatisi.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF, Crescentius Magori, akitoa mada mbele ya Wajumbe wa Baraza Kuu la TUICO, (hawapo pichani) Morogoro jana, pamoja na mambo mengine alisisitiza kuwa Mfuko huo tofauti na mifuko mingine hutoa mafao ya moja kwa moja kwa mwanachama husik bila kupitia kwa mwajiri wake, na kwamba Pensheni hutolewa kulingana na hali ya maisha kwa wakati huo.Picha na Samuel Lyimo.

MTANANGE KATI YA WAFANYAKAZI WA NSSF NA WADAU WA GYMKHANA

$
0
0
 Kikosi Kamili cha timu ya soka ya Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mcherzo wa na Gymkhana jijini Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka sare ya mabao 3-3
Kikosi cha timu ya soka ya Gymkhana.
Mshambuliaji wa timu ya soka ya NSSF, Patrick Gandye akiwania mpira huku akizongwa na beki wa timu ya  Gymkhana,  Hayssam Srour.
 Clementi Sanga akiambaa na mpira huku akifuatiliwa kwa karibu na mchezaji wa NSSF, Kitwana Kidatu.
 Baadhi ya wafanyakazi wa NSSF wakifuatilia mchezo huo.

Tamasha la Exel with Grand Malt lazinduliwa jijini Dar

$
0
0

Meneja masoko wa kampuni ya bia Tanzania (TBL), Fimbo Buttala akizungumza na wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya mkoa wa Dar es salaam kwenye Tamasha la uzinduzi wa kampeni ya kinywaji cha Grand Malt ya kuwashindanisha wanafundi ili kuweza kujinyakulia zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja fedha taslimu ijulikanayo kama Exel with Grand Malt, tamasha hilo lilifanyikia katika viwanja vya chuo kikuu Arthi mkoani Dar es salaam jana.
Mratibu wa tamasha la Exel With Grand Malt,Victor Ndunguru akiongoza ujumbe wa kukagua timu za mpira wa miguu za Chuo kikuu DUCE na chuo kikuu cha Dar es salaa kwenye bonanza hilo lililoshirikisha wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya mkoa wa Dar es salaam kwenye Tamasha ka uzinduzi wa kampeni ya kinywaji cha Grand Malt ya kuwashindanisha wanafunzi ili kuweza kujinyakulia zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja fedha taslimu ijulikanayo kama Exel with Grand Malt,Timu ya chuo kikuu Dar Es Salaam ilishinda kwa 3-1 tamasha hilo lilifanyikia katika viwanja vya chuo kikuu Arthi mkoani Dar es salaam
Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Joh Makini akiwapagawisha wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya mkoa wa Dar es salaam kwenye Tamasha ka uzinduzi wa kampeni ya kinywaji cha grandmalt ya kuwashindanisha wanafundi ili kuweza kujinyakulia zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja fedha taslimu ijulikanayo kama Exel with grandmalt, tamasha hilo lilifanyikia katika viwanja vya chuo kikuu Arthi mkoani Dar es salaam. 

APRIL NIGHT SKIES OVER TANZANIA

TRL KUANZA TENA HUDUMA YA TRENI YA JIJI KESHO JUMATATU APRILI 22, 2013

$
0
0
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania –TRL unafuraha kuwataarifu wateja wake na wananchi kwa ujumla kuwa huduma ya usafiri wa treni ya Jiji ambao ulikuwa umesitishwa kwa wiki tatu zilizopita kuanzia Machi 24, 2013, itaanza tena hapo kesho Aprili 22, 2013.

Kuanza tena kwa huduma hiyo kumetokana na kukamilika kwa kazi ya ukarabati wa awali wa eneo la tuta la reli Tabata Mwananchi lililokuwa limeathiriwa na mvua kubwa hapo Machi 24, 2013. 

Wahandisi wa Kampuni Hodhi za Mali na Uendelezaji wa Miundombinu ya Reli-Rahco walikabidhi eneo hilo kwa Wahandisi wa TRL hapo mchana Aprili 19, 2013. Halikadhalika ukarabati wa kuimarisha eneo hilo utaendelea kufanywa na Rahco.

Kwa mujibu wa ratiba ya treni ya jiji safari hizo zitaanza kama kawaida hapo kesho saa 12:30 asubuhi kutoka kituo cha Ubungo Maziwa na kuishia Kituo cha Reli cha Dar es Salaam ambapo huduma ya awamu ya kwanza itamalizika kama kawaida saa 5 asubuhi. 

Aidha awamu ya jioni itaanza saa 10 kutokea Kituo cha Reli Dar kwenda Ubungo Maziwa kupitia vituo saba vikiwemo Kamata, Buguruni Bakhresa, Buguruni kwa Mnyamani, Tabata Matumbi, Tabata Mwananchi , Mabibo na kuishia Ubungo Maziwa. Huduma ya jioni humalizika saa 4 usiku.

Hakuna mabadiliko ya nauli kila mtumiaji wa huduma atatakiwa kulipia Shilingi 400 kwa mtu mzima na watoto na wanafunzi Shilingi mia moja kwa safari moja.

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,
Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu.
Dar es Salaam,
Aprili 21, 2013

Balozi Kamala akutana na Rais wa Jumuiya ya Ulaya

$
0
0
Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Kamala akiwa katika mazungumzo na Rais wa Jumuiya ya Ulaya Mhe. Herman Van Rompuy,alipomtembelea ofisini kwake hivi karibuni.

Kinana na nape waiteka morogoro katika mkutano wa kuhitimisha ziara yao mkoani humo leo

$
0
0

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, nape Nnauye wakiingia katika Uwanja wa Mkutano wa hadhara wa Kiwanja cha Ndege, mjini Morogoro, leo
 Baadhi ya maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa CCM kwenye Uwanja wa Kiwanja cha Ndege wa mjini Morogoro, wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipowasili Uwanjani hapo
 Umati ukiwa umefurika kwenye mkutano wa CCM uliofanyika leo April 21, 2013 kwenye uwanja wa Kiwanja cha Ndege wa mjini Morogoro
 katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia umati wa wananchi katika Uwanja wa Uwanja wa Ndege (zamani sabasaba) mjini Morogoro leo, Aprili 21, 2013, ikiwa ni hitimisho la ziara yake ya siku nane aliyofanya katika wilaya zote, mkoani Morogoro. (Picha na Bashir Nkoromo)
Msanii wa muziki wa kizazi kipya ajulikanae kw jina la Abdul Nasib a.k.a Diamond akitumbuiza jukwaani jioni ya leo kwenye hitimisho la mkutano wa chama cha CCM,uliofanyika kwenye uwanja wa Ndege (zamani sabasaba),Mkoani Morogoro.Uongozi wa Chama hicho ukiongozwa na Katibu Mkuu wake,Ndugu Abdulrahman Kinana wamefanya ziara ya kutembelea wilaya zote saba za mkoa huo kukagua uhai wa chama na maendeleo ya miradi mbalimbali.PICHA ZAIDI BOFYA HAPA KWA UHONDO ZAIDI.

SHEREHE ZA MIAKA 49 YA MUUNGANO WA TANZANIA Mjini Koloni, Ujerumani Jumamosi 27.04 .2013

$
0
0

Mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania nchini Ujerumani Bw. Mfundo Peter Mfundo (pichani) anayofuraha kubwa kuwakaribisha watanzania na marafiki  wa Tanzania kutoka pembe mbali mbali za Dunia katika maadhimisho ya Sherehe Ya Muungano wa Tanzania Bara na Visiwani, zitakazofanyika mjini Koloni hapa ujerumani.siku ya juma mosi Tarehe 27.04.13 kuanzia saa :08:00 za mchana  hadi usiku wa manane.

Katika sherehe hio ambayo  imedhaminiwa na Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU) kushirikiana na culture center ya sarakasi. Die Zirkus Fabrik,  kutakuwa na maonyesho ya bidhaa za Tanzania,  na atakayependa anaweza pia kununua bidhaa hizo. Ngoma za asili kutoka TanzaniaMwanamuziki Kongwe Bi.Tabia Mwanjelwa naye atakuwepo,  Msanii wa Bongo Flava Shah Smooth mwenye maskani yake  Dublin,. Kikundi cha Sarakasi kitafanya mavitu yake Live ! na  mwisho watanzania na wageni wote watapata Fursa ya Kuduarika na midundo  kutoka Tanzania kupitia DJ Sudi Mnete wa DW.
Akihojiwa na vyanzo vyetu vya habari mwenyekiti Bw Mfundo Alisema, Madhumuni ya sherehe hiyo sio tu kusherehekea siku kuu ya muungano pekee, bali ni kutimiza moja ya maazimio ya UTU la kuwakutanisha Watanzania wanaoishi nchini humo na kutangaza utamaduni wetu wa Tanzania kwa wenyeji wetu hapa Ulaya. Aliendelea kufafanua kwamba moja ya Agenda ya UTU ni kuhakikisha Watanzania wanaoishi nchini Ujerumani wanakuwa pamoja kwa hali zote, wanashirikiana kwa karibu na kusaidiana. Aidha  pia kuhakikisha wasanii wanaoisha hapa ujerumani wanatangaza kazi zao hadharani na wanazitumia kazi hizo kujipatia manufaa zaidi.Hivyo katika sherehe hii (UTU) imealika wasanii mbali mbali kuja kuonyesha kazi zao. Mwenyekiti alimaliza kwa kuwashukuru wasanii na watanzania ambao tayari wameshajiandikisha kushiriki katika sherehe hiyo kubwa Mjini Koloni,
Umoja ni Nguvu!
KARIBUNI SANA MJINI KOLONI

Kilaji cha Redd's chapambisha shindano la Redds Miss Arusha City Centre 2013.

$
0
0
 Warembo wa shindano la kumtafuta mshindi wa shindano la Redd's Miss Arusha City Centre wakiwa katika mazoezi ya pamoja kujiandaa na shindano lao ambapo jumla ya warembo ishirini na mbili wanatarajiwa kupanda ukumbini kumtafuta mshindi mmoja

Young and Dynamic Mayor graces cover of MAN MAGAZINE

Rais Kikwete akagua Ujenzi Nyumba za Waalimu Mboga Sekondari

$
0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ujenzi wa nyumba za waalimu katika shule ya Sekondari ya Mboga, iliyopo kata ya Msoga wilayani Bagamoyo le
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimwelekeza  jambo Diwani wa Kata ya Msoga Bwana Mohamed Mzimba wakati Rais alipotembelea shule ya Sekondari ya Mboga,kata ya Msoga wilayani Bagamoyo leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mboga kata ya Msoga leo wakati Rais alipotembelea shule hiyo leo kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba za waalimu shuleni hapo. Picha na Freddy Maro

OFID YATOA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 18.42 KUSAIDIA MRADI WA MAJI MKOANI MANYARA

$
0
0
Serikali ya Tanzania yasaini mkataba wa jumla ya dola za kimarekani milioni 16 kusaidia mradi wa maji Orkesumet mkoani Manyara. Mkataba huo umesainiwa  leo kati ya Serikali ya Tanzania na OPEC Fund For International Development (OFID) wakishirikiana na BADEA. OPEC wametoa milioni 8 na BADEA wametoa milioni 8. Ili kufanikisha mradi huu Serikali ya Tanzania itatoa dola za kimarekali milioni 2.42, Hivyo kufanya mradi huu kufikia jumla ya dola za Kimarekani milioni 18.42.
 Waziri wa Fedha Dkt. Wiliam Mgimwa akisaini mkataba wa maji ambao utawasaidia wananchi ya Manyara.
 Waziri wa Fedha Dkt Wiliam Mgimwa akipokea mkataba kutoka kwa mchumi wa Wizara ya Fedha Bw. Patrck Pima.

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa akibadilishana mkataba na Mkurugenzi  wa OFID kushoto ni Katibu wa Waziri wa Fedha Bw. Omar Khama akiwasikiliza wafanyakazi wa OFID.

Nyumba za bei nafuu za shirika la nyumba la taifa kigamboni

$
0
0
Nyumba hizi  ambazo tayari zote zimeshauzwa (BOFYA HAPA), ziko  eneo la Kibada. Kigamboni Housing Estate ipo Kigamboni katika eneo linalofikika kirahisi, kilomita 17 kutoka Feri. Kigamboni Housing Estate ni mradi wa nyumba 182 zilizopangwa kwa kuzingatia vigezo vya miji ya kisasa yenye huduma za msingi zikiwemo sehemu za kuchezea watoto na shughuli mbalimbali za jumuiya, barabara pana inayotoa fursa kwa watembea kwa miguu na baiskeli kuwa huru vilevile, imezingatia nafasi ya miundombinu kama vile mitaro na umeme.

Kwa mujibu wa tovuti ya shirika hilo, Nyumba hizi zenye vyumba kati ya viwili na vitatu ni mwanzo tu wa miradi mbalimbali inayoendelea nchi nzima. Uzinduzi wa Mradi huu ni chachu na dhamira ya Shirika la Nyumba la Taifa kuhakikisha watanzania wanapata nyumba bora na za kisasa vile vile zikiuzwa kwa bei nafuu. Wanunuzi wa nyumba hizi wataishi kwenye maeneo kwa kuzingatia mfumo wa hati pacha (Unit titles Act 2008). Mfumo huu utawawezesha wakazi kuishi katika utaratibu wakiongozwa na sheria hiyo ambayo imeundwa kulinda maslahi ya kila mnunuzi.

Katika mradi wa Kigamboni Housing Estate, nyumba ya vyumba vitatu ina ukubwa wa 70m² huku nyumba ya vyumba viwili ikiwa na ukubwa wa 56m², ambapo Kila nyumba inajitegemea ikiwa na eneo kubwa kwa ajili ya matumizi binafsi ya wakazi ikiwa ni pamoja na maegesho ya magari hadi matatu.

Sensei Rumadha Fundi aka Romi (3rd Dan black belt) mtaalamu wa kujivunia

$
0
0
 Tunapozungumzia watanzania waliozaliwa na vipaji na kufanikiwa kuvipigania na kuviendeleza vipaji hivyo hadi kufikia kiwango cha kimataifa jina la Sensei Rumadha Fundi aka Romi  (pichani) hatuwezi kulikwepa. Yeye  ni Mtanzania mwenye makazi yake huko Texas, nchini Marekani. 
Kabla ya kujikita huko Romi  alikuwa moja ya wanafunzi wa karate pale Zanaki jijini Dar es salaam chini ya mwalimu wake Sensei Natambo Guru Kamara Bomani (RIP), akiwa mmoja wa vijana wadogo wateule wa mwalimu huyo aliyebuni kundi maalumu la vijana hodari wa mchezo huo, kwa jina Bomani Brigade.

Baada ya hapo Sensei Rumadha akaenda kwa mafunzo zaidi huko Okinawa nchini Japan, Sweden na Denmark. Pia akachaguliwa kwenda nchini India kwa mafunzo ya kuwa mtaalamu wa Yoga.

Kwa vipaji hivi vya Karate na Yoga, Sensei Rumadha Fundi anaiwakilisha Tanzania kuwa nchi ya wenye vipaji, akiwa  ni mwalimu wa karate na yoga mwenye utalaamu na upeo wa hali ya juu sana na mwenye nidhamu.

Sensei Rumadha ni  mmoja wa walimu wa Kitanzania wa karate ambao wanafanya vizuri katika fani hii  ughaibuni. Ni matumaini yetu wahusika katika sekta ya michezo hasa upande wa mapambano kama ngumi, kick boxing, judo na kadhalika  wataangalia uwezekano wa kupata mchango wao ambao unaweza kusaidia katika kuboresha wanamichezo wetu kufikia kiwango cha kimataifa na kuliletea sifa taifa letu.
Sensei Rumadha Fundi 'Romi' (3rd Dan black belt),  akiwajibika katika semina ya karate katika Dojo ya Sugarland, Texas, nchini Marekani katika semina ya walimu wa karate (ma-sensei)  chini ya uongozi wake Sensei Ramon Veras (7th Dan), wa Traditional Okinawan Goju Ryu Karate-Do.

Ngoma azipendazo Ankal

$
0
0
Jabali la Muziki Marijani Rajabu na Dar International walikuwa hawashikiki enzi hizo. Sikiliza ngoma hii ya 'Ndoa ya Mateso'

Miss Tabata kufanyika Mei 31

$
0
0
Miss Tabata na Ilala 2012 Noela Michael 

Shindano la kumsaka mrembo wa Tabata, Miss Tabata 2013, litafanyika Mei 31 katika ukumbi wa Da’ West Park, Tabata.
Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga amesema kuwa shindano hilo litakuwa ni ya aina yake kulinganisha na mashindano ya miaka ya nyuma kwani mwaka huu wamemejitokeza warembo wazuri zaidi.
 “Warembo wazuri wamejitokeza zaidi kuliko mashindano ya tuliyowahi kuyafanya nyuma. Tutakuwa na burudani nyingi kutoka nje na ndani ya nchi,” alisema mratibu huyo wa Bob Entertainment na Keen Arts.
Warembo watakaoshiriki kwenye shindano wanaendelea na mazoezi kila siku katika ukumbi wa Da’ West Park.
Warembo hao ni Pendo Judica Moshi (20), Madgalena Bhoke (21), Kabula Juma Kibogoti (20), Queen Eliakim Masha (19), Upendo Dickson Lema (22), Martha Gewe (19), Zilpha Christopher (19), Hidaya David (22), Aneth Ndumbalo (19), Amina Ally (18), Dorice Mollel (22), Eunice Nkoha (19), Kazunde Kitereja (19),  Angela Fradius (19), Domina Soka (21), Rehema Kihinja (20), Glory Jigge (18) na Sophia Claud (21).
Wengine ni Lilian Mpakani (19), Lilian Msanchu (19), Rita Frank (20), Pasilida Mandali (21), Rafhel Mussa (19), Jasmin Damian (18), Angelina Mkinga (19), Mercy Mwakasungu (20), Tunu Hamis (19), Brath Chambia (23), Ray Issa (22), Shamim Abass (22) na Shan Abass (22). 
Kapinga aliwaomba warembo wenye sifa kuendelea kujitokeza ili waweze kupata wawakilishi bora katika shindano la Kanda ya Ilala.
"Bado milango iko wazi, mrembo yoyote anayejiamini kwamba ana vigezo anakaribishwa. Tunataka shindano la mwaka huu liwe na ushindani zaidi,” mratibu huyo aliongeza.
Warembo 10 watachaguliwa kushiriki mashindano ya Miss Ilala na baadaye Miss Tanzania.
Anayeshikilia taji la Miss Tabata kwa sasa Noela Michael ambaye pia ni Miss Ilala.
Waliyojitokeza kudhamini shindano hilo ni Fredito Entertainment, CXC Africa, Brake Point na Saluti5.

Taswira za Komba Discotheque ya Bwawani hotel, Zanzibar

$
0
0
 Komba disco katika hoteli ya Bwawani huvuta wapenzi wengi wa muziki kila weekend
 Ndani ya Komba Disco panapendeza

Zanzibar by night

$
0
0
Ni sehemu za Shangani na muda ni saa tisa alfajiri na mtaa uko kimyaaaa. Ngoja pakuche.....
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live




Latest Images