Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1097 | 1098 | (Page 1099) | 1100 | 1101 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad,akisalimiana na Baba mzazi wa marehemu Bi. Asha Bakari Makame, alipofika kwenye msiba huo Jang'ombe mjini Zanzibar.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad,akimfariji Mama mzazi wa marehemu Bi. Asha Bakari Makame, alipofika kwenye msiba huo Jang'ombe mjini Zanzibar.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad,akibadilisha mawazo na Baba mzazi wa marehemu Bi. Asha Bakari Makame, pamoja na kaka yake Bw. Mbarouk Makame (mwisho kushoto), alipofika kwenye msiba huo Jang'ombe mjini Zanzibar. (Picha na Salmin Said, OMKR)

  0 0
  0 0


  Jumuiya ya wanarugambwa (Rugambwa Girls Foundation) wanayo furaha kukualika kwenye mkutano wa pamoja utakaofanyika tarehe 23 Januari, 2016 kuanzia saa 7 mchana, Leaders Club, Dar es Salaam.
  Ukiwa kama mdau wa Rugambwa Sekondari: mwanafunzi, mwalimu, mtumishi wa aina yoyote aliyewahi kupita Rugambwa Sekondari pamoja wanafunzi wote waliosoma shule rafiki za Rugambwa (Ihungo, Kahororo, Bukoba Sekondari, Nyakato, Ntugamo Seminari, n.k. tunakualika kushiriki.
  Lengo ni kukutana kubadilishana mawazo na kupeana mikakati jinsi ya kupata fedha kwa ajili ya kufanikisha jubilee ya miaka 50 ya Rugambwa Sekondari itakayofanyika, Machi 2016 pamoja na ukarabati na uboreshaji wa shule hiyo.
  Atakayesikia au kusoma tangazo hili amfahamishe na mwingine.
  Kwa maelezo zaidi wasiliana na:
  Rugambwa Girls Foundation

  0 0


  0 0

  Ofisa Tehama wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ernest Masaka (katikati), akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu mamlaka hiyo, kutumia mfumo wa kielektroniki kupokea na kushughulikia malalamiko ya wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utafiti, Tathimini na Sera wa SSRA, Ansgar Mushi na kulia ni Ofisa Uhusiano wa SSRA, Agnes Lubuva. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com) 
  Ofisa Tehama wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ernest Masaka, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu mamlaka hiyo, kutumia mfumo wa kielektroniki kupokea na kushughulikia malalamiko ya wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii. 
  Ofisa Tehama wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ernest Masaka (katikati), akitoa taarifa kuhusu mamlaka hiyo, kutumia mfumo wa kielektroniki kupokea na kushughulikia malalamiko ya wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii.

  0 0

  Balozi wa Norway nchini Tanzania ,Hanne -Marie Kaarstad akiweka saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye Kituo cha kuzalisha umeme na kutoa mafunzo cha Kikuletwa ambacho nchi yake imetoa dala za Marekani milioni 5 kwaajili kukifufua kwaajili matumizi ya Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)

  Kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro,Anthony Mtaka,Balozi wa Norway nchini Tanzania ,Hanne -Marie Kaarstad na Mkuu wa Chuo cha UfundiArusha(ATC),Dk Richard Masika wakikagua vyanzo vya maji eneo la Chemka vitakavyotukika kuzalisha umeme na kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa fani ya Uandisi Umeme wa Chuo hicho.

  Mhandisi wa Umeme katika Chuo cha Ufundi Arusha,Merchior Urbanus(kushoto)akimwelekeza jambo Balozi wa Norway wakati akitembelea eneo la Kikuletwa.

  Balozi wa Norway nchini Tanzania ,Hanne -Marie Kaarstad akifurahia madhari ya Kituo cha Kikuletwa, amehaidi kuendelea kusaidia sekta ya nishati hapa nchini. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dar es Salaam leo asubuhi wakati akitoa mwito kwa wananchi hasa wa Wilaya ya Kinondoni na maeneo mengine ya jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kupimwa maradhi ya moyo bure katiza zoezi litakalofanywa na madaktari kutoka taasisi hiyo litakalofanyika viwanja vya leaders kesho kutwa January 23, 2015. Kushoto ni Meneja wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Salome Kassanga na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Profesa Mohamed Janabi.
  Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Profesa Mohamed Janabi (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
  Meneja wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwe, Salome Kassanga (kushoto), akimuelekeza jambo DC Makonda. Katikati ni Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Moyo wa Taasisi hiyo, Dk.Peter Kisenge.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Mwili wa Marehemu ukiteremshwa katika ndege kwa ajili ya maandalizi ya mazishi kesho saa nne asubuhi Jangombe Zanzibar.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akizungumza na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Pandu Amaer Kificho na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Mohammed Aboud wakiwa uwanja wa ndege Zanzibar wakisubiri kuwasili kwa mwili wa marehemu
  Ndugu na Jamaa wa Marehemu wakiwa na Viongozi wa Serikali na Chama wakisubiri kuupokea mwili wa Marehemu Uwanja wa Ndege wa Zanzibar leo jioni
  Mwili wa Marehemu ukishusha katika gari baada ya kupokelewa katika uwanja wa ndege wa Zanzibar wakiubeba wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege Zanzibar. 

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Na Raymond Mushumbusi Maelezo

  Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ametunukiwa Shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa wa mahusiano ya kimataifa Leo Jijini Dar es Salaam katika mahafaliya 30 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania.

  Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amesema amefarijika sana kutunukiwa shahada hiyo ya heshima itolewayo na Chuo kikuu Huria Tanzania kwa watu ambao wametoa mchango katika maendeleo katika jamii kupitia nafasi zao kiutendaji.

  “Naipokea heshima hii toka Chuo Kikuu Huria Tanzania kwa moyo mmoja kwani wameona mchango ambao nimeutoa nilipokuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Awamu ya Nne hivyo basi nitaendeleza mahusiano na ushirikiano kimataifa”.Alisema Mhe. Dkt Kikwete.

  Mbali na Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kuna baadhi ya maraisi na wakuu mbalimbali duniani waliwahi kupata Shahada za heshima toka Chuo Kikuu Huria Tanzania ambao ni Rais wa Awamu ya kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Awamu ya tatu Benjamin William Mkapa, Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini Hayati Nelson Mandela na Dkt Koichiro Mastuura Mkurugenz iwa UNESCO.

  Chuo kikuu Huria cha Tanzania kimetoa jumla ya wahitimu 69 wawili Shahada maalum na 67 ni Shahada, Stahahada na Astashahada, ambapo Shahada ya uzamivu ni wahitimu watatu, Shahada ya uzamili ni wahitimu 20, Shahada wahitimu 22,Stashahada wahitimu 15 na Astashahada wahitimu 6.

  Tangu kuanzishwa kwa Chuo Kikuu Huria Tanzania mwaka 1992 jumla ya wahitimu 25,908 wametunukiwa Shahada mbalimbali na haya ni mahafali ya 30 tangu chuo kuanzishwa.
  Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ( Kulia) akifatilia kitabu cha mahafali ya 30 ya Chuo kikuu Huria Tanzania yaliyofanyika Jijini leo Dar es Salaam. kushoto ni Prof Suh Chae-Hong Rais wa Chuo cha Chosun kilichopo Korea ya Kusini.
  Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania Dkt Asha Rose Migiro akifungua rasmi mahafali ya 30 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania Dkt Asha Rose Migiro akimtunuku Shahada ya ya heshima ya udaktari wa falsafa ya mahusiano ya kimataifa Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe Dkt Jakaya Mrisho Kikwete katika maafali ya 30 ya Chuo kikuu Huria Tanzania yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.


  0 0
 • 01/21/16--19:00: NGOMA AZIPENDAZO ANKAL
 • Diamond Platnumz - Mbagala

  0 0


  Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa katika picha ya pamoja na wazee wa Pwani waliokuwa naye bega kwa bega katika harakati za kudai Uhuru. Kutoka kushoto na sehemu aliyokuwa anaishi ni Abdallah Shomari (Tandamti No. 3), Nassoro Kalumbanya (Simba), Said Chamwenyewe (Aggrey/Congo), Mtoro Ally (Muhonda), John Rupia (Misheni Kota),Julius Nyerere (Pugu Sekondari), Said Chaurembo (Congo/Mkunguni), Jumbe Tambaza (Upanga), Sheikh Suleiman Takadir (Mafia/Swahili)


  Dossa Aziz (Mbaruku/Somali Kipande), Mshume Kiyate (Tandamti). Juma Sultani (Kitchwele Karibu na Kanisa Dogo), Maalim Shubeti (Masasi/Likoma), Rajab Simba (Kiungani), Waziri Mtonga (Kilosa 18, Ilala), Mwinjuma Mwinyikambi (Mwananyamala) , Makisi Mbwana (Aggrey/Congo), Usia Omari (Sungwi, Kisarawe), Sheikh Issa Nasir (Bagamoyo).

  0 0

   Mkurugenzi Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Mick Kiliba (kushoto) akitoa ufafanuzi wa Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma kwa Mwandishi wa Habari kutoka MiniBuzz Tv Bi. Hadija Mzee wakati wa mahojiano yaliyofanyika ofisini kwake jijini Dar es salaam jana.
  Mkurugenzi Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Mick Kiliba (kulia) akisikiliza swali la Mwandishi wa Habari kutoka MiniBuzz Tv Bi. Hadija Mzee wakati wa mahojiano kuhusiana na masuala ya kiutumishi yaliyofanyika ofisini kwake jijini Dar es salaam jana.

  0 0  0 0

   WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto. Umy Mwalimu (kulia), akihutubia wakati akizindua rasmi duka la Dawa la MSD mkoani Mwanza jana ambalo liko ndani ya Hospitali ya SekouToure, nakufanya maduka ya MSD yaliyofunguliwa baada ya agizo la Rais Dk. John Magufuli kufikia mawili baada ya lile la Muhimbili lililofunguliwa mwaka jana mwishoni. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu na katikati ni Mwenyekiti wa Bodi MSD, Profesa Idrisa Mtulia.
    WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto. Umy Mwalimu (kushoto), akiwa na viongozi mbalimbali wa MSD wakati wa uzinduzi wa duka hilo.
    
  Na Dotto Mwaibale
  WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto. UmyMwalimu amezindua rasmi duka la Dawa la MSD mkoani Mwanza ambalo liko ndani ya Hospitali ya SekouToure, nakufanya maduka ya MSD yaliyofunguliwa baada ya agizo la Rais Dk. John Magufuli kufikia mawili baada ya lile la Muhimbili lililofunguliwa mwaka jana mwishoni.
  Katika hotuba yake ya uzinduzi wa duka hilo, ameipongeza MSD kwa hatua hiyo nzuri ya kufungua maduka ili kuwawezesha wananchi kupata dawa, na kuitaka MSD kukamilisha ufunguzi wa maduka mengine mawili yaliyosalia katika mikoa ya Arusha naMbeya, kwani hicho ni moja ya kipaumbele katika uongozi waserikali ya awamu yaTano.
  Waziri huyo ameeleza kuwa Wizara yake imejiwekea malengo ya upatikanaji wa dawa nchini kutoka asilimia 70 kwa sasa kufika hadi asilimia 95.
  Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu alisema maduka mawili ya Arusha naMbeya yamemekamilika, na yanatarajia kufunguliwa hivi karibuni, na kwamba kwa  mikoa mingine wameshafanya  mawasiliano  na kwamba tayari MSD imefanya mazungumzo na viongozi wa mikoa Ruvuma, Rukwa, Singida, Dodoma, Geita, Kagera na Iringa kufungua maduka yao ya dawa ambapo MSD itawauzia dawa.
  “Tutakachofanya, sisi (MSD) utawapa  utaalamu na  kuwawezesha utaalamu wa uendeshaji maduka hayo” alieleza Bwanakunu.


  0 0


   Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji  FC Chenjelai John akimuelekeza Mwanafunzi Enea Gerald wa shule ya Sekondari Temeke jinsi ya kukabiliana na moto ukiwa katika hatua ya awali tarehe 20 Januari 2016. Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limeamua kuwekeza katika utoaji wa elimu ya majanga ya moto kwa watoto wadogo na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ili kutengeneza jamii yenye ufahamu na utayari wa kukabiliana na majanga ifikapo mwaka 2025.

  Kijue kifaa kinacho weza kung’amua moshi kutoa taarifa;Kinaitwa smoke detector kina uwezo wa kung’amua moto kwa kupitia moshi kisha kupiga king'ora. Kifaa hiki kina patikana katika maduka yanayouza vifaa vya kuzimia moto na bei yake ni ya kawaida sana. Hakizimi moto kazi yake ni kutoa taarifa ili wewe mwananchi ujue mapema kabla moto hauja samba na kuleta madhara makubwa. 

  Ili kifaa hiki kikusaidie lazima uwe na mtungi wa kuzimia moto wa huduma ya kwanza sambamba na kutoa taarifa kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kupiga namba ya dharura 

  0 0

  Mwanasaikolojia Anti Sadaka akitoa Mada kwenye Mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Mkoa wa Mwanza yanayoendesha na  Taasisi ya Manjano foundation yanaoendelea kwenye ukumbi wa Rocky city Jijini Mwanza.
  Mwanasaikolojia Anti Sadaka amewafunda wanawake wa Mkoa wa Mwanza wanaoshiriki mafunzo ya ujasiriamali ya kujikita katika biashara ya Vipodozi vya LuvTouch Manjano. 
  Mafunzo hayo yanaendeshwa  na wataalamu kutoka taasisi ya Manjano  Foundation  yanayoendelea Jijini Mwanza kwa wiki nzima. Anti Sadaka amewataka wanawake hao kujitambua kwa lengo la kufikia malengo yao waliojiwekea. Akieleza zaidi katika semina hiyo amewataka wanawake hao kujitambua wao ni nani  wana nafasi gani kwenye jamii inayowazunguka, kufanya kazi kwa bidii na kudumisha nidhamu yao kwa kila wakifanyacho kwa lengo la kufikia malengo yao.
  Wanawake wa Mkoa wa Mwanza wakifuatilia kwa amkini Mada zilizokuwa zinaendeshwa   kwenye Mafunzo hayo.
  Pia amewaasa wanawake walioshiriki mafunzo hayo mkoani Mwanza kuchangamkia FURSA zinazowazunguka mapema iwezekanavyo. Alisisitiza umuhimu wa usafi wao binafsi na mazingira yao ya kazi kupewa kipao mbele kwa sababu usafi humlinda mteja asipate breakout ya ngozi yake na kuridhika na huduma yake yaani "Smart You & Environment."
  Semina hiyo inawanufaisha wanawake wa Mwanza kwa lengo la kuwaongezea kipato na pia kuweza kujiajiri ili kujikwamua na tatizo la ukosefu wa ajira. Baada ya washiriki kupata mafunzo ya biashara na urembo watapatiwa  MIKOPO kutoka Taasisi ya Manjano  Foundation  kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano. 
  Mwanasaikolojia Anti Sadaka Akiwa katika Picha ya Pamoja na wanawake wa Mkoa wa Mwanza waliojitokeza  kwenye Mafunzo ya Ujasiriamali  yanayoendeshwa  na Taasisi ya Manjano Foundation.
  Washiriki wa mafunzo hayo  wameushukuru uongozi wa Taasisi ya Manjano  Foundation kwa kuwakumbuka na kuwaletea Mradi huo jijini Mwanza. Wakieleza zaidi wamesema kwa muda mrefu wamekuwa na hamu ya kujua zaidi kuhusu matumizi sahihi ya vipodozi lakini walikosa elimu hiyo ya kuwa Makeup Artists.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ametangaza wajumbe wa kwanza wa jopo la ushauri la ngazi ya juu kuhusu afya ya mama na mtoto  #Everywomaneverychild.
  Jopo hilo la watu  12 litakuwa na wenyeviti wanne akiwemo Rais mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete, na Waziri Mkuu wa Ethiopita Hailemariam Desalegn. Wengine ni Rais wa Chile Michelle Bachelet na Rais wa zamani wa Finland Tarja Halonen.
  Ban amesema jopo hilo litamshauri jinsi ya kusaidia kuonyesha uongozi katika masuala ya afya ya wanawake, watoto na vijana barubaru wakati huu ambapo dunia inahama kutoka malengo ya maendeleo ya milenia kuanza kutekeleza malengo endelevu, SDGs.
  Wenyeviti hao watafanya kazi wawili wawili kwa kipindi cha mwaka mmoja mmoja wakipokezana na jopo litakuwa na linakutana mara mbili kwa mwaka.
  Mkakati wa kimataifa wa afya ya wanawake, watoto na barubaru pamoja na kutoa mwelekeo kupitia afya ya mama na mtoto ili kumaliza vifo vya makundi hayo vitokanavyo na magonjwa yote yanayozuilika ifikapo mwaka 2030, pia unalenga kuhakikisha ustawi wao katika utekelezaji wa SDGs.

  0 0
 • 01/21/16--23:00: DIRA YA DUNIA YA BBC SWAHILI

 • 0 0

  Watu wangu wa zamaniii!!!, haya hayawi sasa yamekuwa, JD's Entertainment inakuletea The Legend's Family 2016 Tour.

  Na sasa siyo isumba tena bali safari itaanza Ijumaa hii ya terehe 22/01 ndani ya Rhapsody - Viva Tower DSM, iliyoko pembeni ya Puma Petrol Station karibu na .... zamani Movenpick Hotel; na Jumamosi ya tarehe 23/01 mzigo unahamia New Brake Point Kinondoni Road.

  Mtamboni kama kawa kama dawa ni DJ JD aka The Legend along side DJ Fast Eddie aka The Sniper. Kiingilio ni shillingi 10,000/-tu na milango itakuwa wazi kuanzia saa tatu usiku. Karibu  tucheze tufurahi na tukumbuke wakati muziki ulipokuwa ukiitwa muziki.

  Kwa maelezo zaidi juu ya The Legends Family  2016 Tour na The Legend Family t-shirt na cds zake,  follow instagram @djjdakathelegend facebook @ dj jd, whatsapp/text au piga 0784331249,
  The Legend Family Twenty Sixteen ndio habari ya mjini.

  0 0

  Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi wa Arusha Mjini wakati akipita Barabarani kuelekea Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli ambako pamoja na mambo mengine kesho tarehe 23 Januari, anatarajiwa kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli kundi la 57/15.
  Amiri Jeshi Mkuu,Rais Dkt Magufuli akiwasikiliza wananchi kwa makini alipopita maeneno ya Sanawali kuwasalimia wakati akielekea Wilayani Monduli.
  Baadhi ya Wananchi wa Maeneo ya Sanawali wakishangilia ujio wa Rais John Pombe Joseph Magufuli,alipokuwa akielekea Wilayani Monduli mapema leo asubuhi.
  Rais Magufuli akiwa amevalia sare za kijeshi amesimamishwa na kuwasalimu wananchi katika maeneo ya SANAWALI, TEKNIKO, NGARENALO, MBAUDA, MAJENGO na KISONGO

older | 1 | .... | 1097 | 1098 | (Page 1099) | 1100 | 1101 | .... | 3278 | newer