Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

mafunzo ya namna ya kutumia mizani za kisasa Weigh in Motion ili kudhibiti magari yanayozidisha uzito Mkoani Morogoro.

0
0
 Ofisa wa Mizani wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS)  kutoka Mkoa wa Iringa akitoa mada katika mafunzo ya namna ya kutumia mizani za kisasa Weigh in Motion ili kudhibiti magari yanayozidisha uzito Mkoani Morogoro.
 . Magari yaliyokamatwa baada ya kuzidisha uzito yakiwa yamezuiliwa katika Mizani ya Vigwaza kwa hatua zaidi za kisheria.
 Eng. Japhet Kivuyo kutoka (TANROADS) Makao makuu akifafanua jambo katika mafunzo ya namna ya kutumia mizani za kisasa Weigh in Motion ili kudhibiti magari yanayozidisha uzito Mkoani Morogoro,Kulia ni Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira Wizara ya Ujenzi Eng.Julius Chambo na kushoto ni Mkurugenzi msaidizi wa Usalama na Mazingira Eng.Joyce Mbunju.

 Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira Wizara ya Ujenzi Eng.Julius Chambo (Wakwanza Kulia) akifafanua mada katika mafunzo ya namna ya kutumia mizani za kisasa Weigh in Motion ili kudhibiti magari yanayozidisha uzito Mkoani Morogoro.


 Mashine inayoonyesha uzito wa magari yakiwa yanapimwa katika Mizani ya  Static Weighbridge katika Mizani mpya ya Vigwaza Mkoani Pwani ambayo huondoa malalamiko ya gari kuzidishiwa uzito.



TEASER YA JOTO LA ASUBUHI LA 93.7EFM ALHAMISI JANUARY 21, 2016

NO BAN ON MINISKIRTS BY PRESIDENT MAGUFULI - TANZANIA GOVERNMENT

0
0
PRESS RELEASE

The Ministry of Foreign Affairs, East African, Regional and International Cooperation of the United Republic of Tanzania has noticed, with serious concern and disapproval, a grossly distorted report in the Kenyan Standard newspaper, purporting that H.E. President John Pombe Magufuli has banned the wearing of miniskirts in Tanzania.

Unfortunately, the false report, appearing in the daily newspaper's 'MondayBlues' gossip page on 18th January 2016, was taken for factual and circulated widely by other outlets and the social media in Kenya and beyond.The ministry deplores the casual manner in which the Standard handled the hearsay report and the reckless, totally unwarranted attribution of the imaginary 'ban' to the Tanzania Head of State.

While it appreciates the enthusiastic, positive reviews of H.E. President Magufuli's performance in the Kenyan and international media, the Ministry of Foreign Affairs takes strong exception at irresponsible distortions and misreporting, such as the one on miniskirts.

There is no doubt that H.E. President Magufuli and his government are strong proponents of decent dressing, but the ministry wishes to put the record straight that the President has not issued any ban on miniskirts for any reason.

The ministry understands that as a mainstream newspaper, the Standard is obliged to observe the highest standards of journalism, central of which is respect for facts and accurate reporting.

The ministry trusts that the distortion in question was inadvertent, not a malicious attempt to undermine the new administration in Tanzania, and that the Standard will show good faith by at least retracting the wrong information fed to its readers.

-Ends-

Issued by:

Government Communication Unit,

Ministry of Foreign Affairs, East African, Regional and International Cooperation.


Dar es salaam, January 20, 2016

Warning for heavy rains/Tahadhari ya mvua kubwa 20/01/2016 - 21/01/2016.

RAIS DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA MAREHEMU LETICIA NYERERE

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Rais mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho  Kikwete nyumbani kwa Baba wa Taifa  Msasani Dar es salaam wakati wa kuaga mwili wa aliyekua Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Marehemu Leticia Nyerere aliyefariki mwishoni mwa wiki Nchini Marekani alikokuwa akitibiwa leo Januari 20, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na waombolezaji wakati wa kuaga mwili wa aliyekua Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Marehemu Leticia Nyerere aliyefariki mwishoni mwa wiki Nchini Marekani alikokuwa akitibiwa leo Januari 20, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiweka saini katika kitabu cha maombolezo wakati wa kuaga mwili wa aliyekua Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Marehemu Leticia Nyerere aliyefariki mwishoni mwa wiki Nchini Marekani alikokuwa akitibiwa leo Januari 20, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitoa heshima zao za mwisho  wakati wa kuaga mwili wa aliyekua Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Marehemu Leticia Nyerere aliyefariki mwishoni mwa wiki Nchini Marekani alikokuwa akitibiwa leo Januari 20, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimfariji mume wa marehemu Bw. Madaraka Nyerere wakati wa kuaga mwili wa aliyekua Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Marehemu Leticia Nyerere aliyefariki mwishoni mwa wiki Nchini Marekani alikokuwa akitibiwa leo Januari 20, 2016. Kulia ni Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimfariji Mama Maria Nyerere wakati wa kuaga mwili wa aliyekua Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Marehemu Leticia Nyerere aliyefariki mwishoni mwa wiki Nchini Marekani alikokuwa akitibiwa leo Januari 20, 2016. Kulia ni Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere.

NEWS ALERT: JPM AMSIMAMISHA KAZI KAMISHNA MKUU WA UHAMIAJI

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewasimamisha kazi Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Bwana Sylvester Ambokile na Kamishna wa Uhamiaji anayeshughulikia Utawala na fedha Bwana Piniel Mgonja   ili kupisha uchunguzi, kufuatia dosari alizozibaini Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mheshimiwa Charles Kitwanga alipotembelea Idara ya Uhamiaji hivi karibuni.

MAKALA YA SHERIA: NJIA TANO ZA MWEKEZAJI ASIYE MTANZANIA KUPATA ARDHI

0
0
Na  Bashir  Yakub .

Kupitia  makala  haya  wako  Watanzania ambao wanao  marafiki  wa  kigeni, wanao wafanyabiashara  wenzao  wa  kigeni,  ndugu  wa  kigeni, na  wengine  wanahisa  wenzao  katika  makampuni  mbalimbali  ambao  wangependa   wenzao   hao  wapate  ardhi  ya  uwekezaji  Tanzania.  Makala  haya  ni  nafasi  kwao  kujua  mambo  ya  msingi  ya  awali  kuhusu  namna  ya  kupata  ardhi   kwa  hao  wageni.

Aidha mara  kadhaa  makala  yetu  yameeleza   taratibu  mbalimbali  ambazo   Mtanzania  huweza  kupitia  ili  kupata  haki  ya  kumiliki  ardhi. Sanjari  na  hilo   imeelezwa  mara nyingi pia  namna  nzuri  ya kuweza   kupata  ardhi  huku  ukiepuka  migogoro  ambayo  huwaingiza  wengi  katika  hasara  ikiwa  ni  pamoja  na  kuwapotezea  muda. 

 Iliwahi  kuelezwa  hapa  kuwa  Mtanzania  anaweza kupata ardhi  kwa  kununua,  kurithi, kuzawadiwa,  njia ya  fidia,  na kwa  kutwaa  eneo  lisilo  na  mmiliki.     

Hii ni  kwa raia  wa  Tanzania.  Yumkini raia    wasio  watanzania  nao  wanazo  haki  zao  katika   ardhi  yetu. Raia  wasio  Watanzania  wanaweza  kupatiwa  ardhi  kwa ajili  ya  matumizi. Kubwa  kwao  hupatiwa ardhi  kwa  ajili  ya  uwekezaji   kwa  manufaa  ya  taifa. 

 Kupitia  hili  zipo  namna  tano  ambazo  raia wasio  Watanzania  wanaweza  kupitia  hadi kupatiwa  ardhi.

1.SHERIA  ZINAZOWARUHUSU  WAGENI  KUPATIWA  ARDHI.
Sheria  kuu  inayowaruhusu  raia  wa  kigeni  kupatiwa  ardhi nchini  ni  sheria  namba  4   sheria  ya  ardhi  ya  mwaka  1999.  Kifungu  cha  19( 2 )  cha  sheria  hii  kinasema  kuwa  mtu  au  kikundi  cha  watu  ambacho  kimejiunga  kama  kampuni  au   bila  kampuni  ambacho  wahusika  wake  ni  raia  wa  kigeni  wanaweza  kupata  haki  ya  kumiliki  ardhi  kwa  ajili  ya  uwekezaji. 

Sheria  nyingine   inayotoa  mwongozo   kwa  raia  wa  kigeni  kupata ardhi  Tanzania  ni   sura  ya  38 sheria  ya   uwekezaji  ya  mwaka  1997. Sheria    hii  hueleza  namna  ya  kumpatia mwekezaji  ardhi,  matumizi,  na  muda  wa  mwekezaji  mgeni  kutumia  ardhi  hiyo.

NGOMA AZIPENDAZO ANKAL


Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kimetiliana saini mkataba wa makubaliano wa mashirikiano na Chuo Kikuu cha Komoro

0
0
Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kimetiliana saini mkataba wa makubaliano juu ya mashirikiano na Chuo Kikuu cha Komoro mjini Moroni katika hafla maalum iliyofanyika tarehe 19 Januari, 2016 na kuhudhuriwa na uongozi wote wa Chuo Kikuu cha Komoro, Balozi wa Komoro nchini Tanzania Dkt. Ahmada El Badaoui Mohamed na Mwakilishi wa Balozi wa Tanzania nchini Komoro, Bw Mudrik Ramadhan Soragha. 
 Makubaliano kati ya vyuo hivi ni moja ya matokeo ya ziara ya nchini Komoro ya Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliyoifanya hivi karibuni.
Profesa Idris Rai, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) na Dkt Said Bourhani, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Komoro wakisaini Mkataba wa makubaliano ya mashirikiano baina ya vyuo vyao.

SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUTOKA CCM CALIFORNIA.

0
0
Chama cha mapinduzi- Tawi la California, tunapenda kutoa salamu za pole zilizojaa masikitiko makubwa kwa familia na ndugu wa Marehemu wa Mwenyekiti wa Tawi la CCM la DMV Mzee George Sebo. 
Pia tunapenda kutoa pole kwa uongozi wa chama wa tawi la DMV kwa kuondokewa na kiongozi wao mahili. Lakini pia tunapenda kutoa pole kwa watanzania wote wa DMV na wengine wote waliomjua marehemu.

Tumesikitishwa na kuguswa sana na huu msiba hasa kwa kumjua marehemu kwa ukaribu sana, kwa mapenzi yake kwa watu wote na nchi yake. Wengi wetu huku northern California wanaccm na wasio wanaccm tunamjua marehemu kwa ukaribu kwani alikuwa akitutembelea huku mara kwa mara na kuna kipindi yeye na mke wake walikuwa wanachama wa jumuiya yetu ya watanzania waishio hapa bay area. 
Hivyo ni mtu wetu tunafahamu fika.

Kama chama tutamkumbuka sana kwa kuwa mzee wa ushauri katika chama chetu na matawi yetu hapa Marekani. Tutayazingatia yale yote aliyotuachia na kuyafanyia kazi.


Tunaomba mungu wa rehema aiweke 
roho yake mahala pema peponi. 
AMINA


Erick Byorwango


Karibu-Tawi la California.

Wadau wakutana kujadili njia mahususi za kuboresha mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kwenye majiji

0
0
Wadau wa mazingira kutoka idara na wizara mbalimbali za serikali na mashirika binafsi wamekutana Januari 20, 2016 kujadili njia mahususi za kuboresha mazingira na kukabilaiana na athari za mabadiliko ya tabianchi kwenye majiji

Majadiliano hayo ni hatua moja wapo ya uanzishwaji wa mfuko wa Mfuko wa Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi ukiwa na lengo la kukusanya pesa za kukabiliana na changamoto za mazingira na mabadiliko ya tabianchi katika Manispaa ya Ilala

Mradi huo unafanywa kwa ushirikiano wa Manispaa ya ilala na ForumCC
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu Rais, Ngosi Mwihava akifungua mkutano huo wa wadau ambao umewashirikisha pia watendaji wa serikali na mashirika yasiyo ya serikali kutoka katika wizara na idara mbalimbali,  kwa lengo la kujadili kwa pamoja namna ya kushirikiana na kupata njia ya pamoja ya kuboresha mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi zikiwemo mafuriko, magonjwa na uharibifu wa miundombinu.
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu Rais, Ngosi Mwihava (katikati) akiwa na viongozi wa Forumcc wakati wa mkutano huo, kuanzia kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia Mabadiliko ya Tabianchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Richard Muyungi, Mkurugenzi wa Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Julius Ningu wakati kuanzia kulia ni Afisa Miradi Forumcc, Fazal Issa na Mwenyekiti wa bodi ya forumcc, Yusta Kibona
Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Dr. Julius Ningu akifafanua jambo wakati wamkutano huo.

DAWASCO YATANGAZA KUZIMA KWA MTAMBO WA MAJI WA RUVU CHINI KWA SIKU MBILI

0
0
Afisa Uhusiano wa Shirika la Maji Safi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO), Everlasting Lyaro, akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya kuzimwa kwa Mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Chini kwa wastani wa Saa 48 kwa siku za Jumamosi 23/01/2016 na Jumapili 24/01/2016 

Mtambo wa Ruvu Chini utazimwa ili kuruhusu Mkandarasi Kuunganisha bomba Jipya na Bomba la zamani katika tanki la Maji Wazo- Tegeta. Zoezi hili linaashiria kuanza kukamilika kwa upanuzi wa Mtambo wa Maji wa Ruvu Chini ambapo Shirika linakusudia kuzalisha Maji mapya toka kiwango cha sasa cha cubic za ujazo 182,000 hadi cubic 270,000 kwa siku kuanzia mwezi Februari 2016 na Kuondoa kabisa tatizo la Maji kwa maeneo yanayohudumiwa na Mtambo wa Ruvu Chini.

Kuzimwa Kwa mtambo wa Ruvu Chini kutapelekea maeneo yafuatayo katika Jiji kukosa Maji:
. MJI WA BAGAMOYO VIJIJI VYA ZINGA, KEREGE NA MAPINGA, BUNJU, BOKO, TEGETA, KUNDUCHI, SALASALA, JANGWANI, MBEZI BEACH NA KAWE.
Maeneo Mengine ni : MLALAKUWA, MWENGE, MIKOCHENI, MSASANI, SINZA, KIJITONYAMA, KINONDONI, OYSTERBAY, MAGOMENI, UPANGA, KARIAKOO, CITY CENTRE, ILALA, UBUNGO MAZIWA, KIGOGO, MBURAHATI, HOSPITALI YA RUFAA MUHIMBILI, BUGURUNI, CHANGOMBE NA KEKO.

WANANCHI MNASHAURIWA KUHIFADHI MAJI NA KUYATUMIA KWA MATUMIZI YA LAZIMA.

Wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 022-2194800 au 0800110064 (BURE)
DAWASCO INAWAOMBA RADHI WANANCHI KWA USUMBUFU UTAKAOJITOKEZA.

IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
DAWASCO-MAKAO MAKUU

SIMU TV: MAPITIO YA MAGAZETI LEO

AIRTEL YAZINDUA DUKA KARIAKOO MSIMBAZI

0
0
Airtel Tanzania imezingua duka la Airtel Xpress mtaa wa msimbazi, Kariakoo Dar es Salaam ikiwa ni moja ya mipango yake ya kusogeza huduma zake karibu zaidi na wateja wake.

Kuzinduliwa kwa duka la kariakoo Airtel Xpress inaongeza idadi ya maduka kuongezeka kufatia uzinduzi wa dula jipya la kisasa lililoko Morocco Dar es salaam ulifanyika wiki iliyopita.

Katika uzinduzi wa duka la Airtel XPress kariakoo mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Adriana Lyamba alisema, kufunguliwa kwa duka la Airtel Xpress kariakoo itawawezesha wateja wa Airtel na wafanya biashara wa Kariakoo, Ilala, Magomeni kupata huduma zetu kwa ukaribu zaidi kama kujipatia simu za kisasa na kwa bei nafuu. Tunaimani kufunguliwa kwa duka hili hapa kutatasaidia kupata huduma kwa uharaka na ubora zaidi.

“Airtel tumejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja wetu zaidi ya milioni 10 nchi nzima. Kipaumbele chetu ni kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma kiurahisi zaidi na kwa ufanisi wakati wote na hili limejidhihirisha leo kwa kufungua duka la Airtel Xpress”, aliongezea Adriana

Baadhi ya huduma zitakazotolewa kwenye duka la Kariakoo ni pamoja na Airtel Money, kusajili laini, huduma za internet na huduma zetu nyinginezo.

Pamoja na duka jipya lililozinduliwa kariakoo pia Airtel inamaduka sehemu mbalimbali katika mkoa wa Dar es Salaam kama Airtel Morroco, Mlimani City, J Mall, Buguruni Airtel inatarajia kufungua maduka zaidi ifikapo Juni 2016 yatakayotoa huduma sambamba na mawakala wake Zaidi ya 80,000 nchi nzima.
Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Adriana Lyamba, akikata utepe wakati wa uzinduzi wa duka jipya la Airtel Express lililopo Kariakoo mtaa wa msimbazi, Dar es Salaam, akishuhudia ni wakala mkuu wa Airtel kutoka Celnet, Bwana Kalpesh Bandar.
Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Adriana Lyamba (katikati), akiangalia simu aina ya Bravo Z10 wakati wa uzinduzi wa duka jipya la Airtel Express lililopo kariakoo mtaa wa msimbazi, Dar es Salaam. Akitoa maelezo kuhusu simu hiyo ni Afisa mauzo wa Airtel , Meshack Joseph (kwanza kulia) , akishuhudia kulia ni Meneja Mauzo wa Airtel, James Moilo.
Afisa mauzo wa Airtel , Meshack Joseph (kwanza kulia) akitoa maelezo kuhusu simu mbalimbali za smartphone zinazopatikana katika duka jipya la Airtel Express Kariakoo wakati wa uzinduzi wa duka hilo jipya lililopo Kariakoo mtaa wa msimbazi, Dar es Salaam. Pichani ni Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Adriana Lyamba (katikati) akiwa na wateja pamoja na wafanyakazi wa Airtel

NGOMA AZIPENDAZO ANKAL


Mkutano wa Utaratibu wa Upangaji Taarifa Wafunguliwa jijini Dar

0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais, Dk. Julius Ningu akizungumza na Wajumbe wa Mkutano wa Utaratibu wa Upangaji Taarifa (Clearing House Mechanism) kuhusu Viumbe Hai, wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Taasisi ya Utafiti wa Dawa (NIMR), jijini Dar es salaam leo. (Picha na OMR).
Sehemu ya Washiriki wa Mkutano wa Utaratibu wa Upangaji Taarifa (Clearing House Mechanism) kuhusu Viumbe Hai, wakimsikiliza kwa makini mtoa mada wa Mkutano huo, Bwana Maskati Maliwanga (hayupo pichani).

Washiriki katika Mkutano wa Utratibu Upangaji Taarifa (Clearing House Mechanism) kuhusu Viumbe Hai wakiwa katika picha ya pamoja.

MWANASAIKOLOJIA ANTI SADAKA AWAFUNDA WANAWAKE WA JIJI LA MWANZA

0
0
Mwanasaikolojia Anti Sadaka akitoa Mada kwenye Mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Mkoa wa Mwanza yanayoendesha na  Taasisi ya Manjano foundation yanaoendelea kwenye ukumbi wa Rocky city Jijini Mwanza.

Mwanasaikolojia Anti Sadaka amewafunda wanawake wa Mkoa wa Mwanza wanaoshiriki mafunzo ya ujasiriamali ya kujikita katika biashara ya Vipodozi vya LuvTouch Manjano. Mafunzo hayo yanaendeshwa  na wataalamu kutoka taasisi ya Manjano  Foundation  yanayoendelea Jijini Mwanza kwa wiki nzima. Anti Sadaka amewataka wanawake hao kujitambua kwa lengo la kufikia malengo yao waliojiwekea. Akieleza zaidi katika semina hiyo amewataka wanawake hao kujitambua wao ni nani  wana nafasi gani kwenye jamii inayowazunguka, kufanya kazi kwa bidii na kudumisha nidhamu yao kwa kila wakifanyacho kwa lengo la kufikia malengo yao.
Wanawake wa Mkoa wa Mwanza wakifuatilia kwa amkini Mada zilizokuwa zinaendeshwa   kwenye Mafunzo hayo.
Pia amewaasa wanawake walioshiriki mafunzo hayo mkoani Mwanza kuchangamkia FURSA zinazowazunguka mapema iwezekanavyo. Alisisitiza umuhimu wa usafi wao binafsi na mazingira yao ya kazi kupewa kipao mbele kwa sababu usafi humlinda mteja asipate breakout ya ngozi yake na kuridhika na huduma yake yaani "Smart You & Environment."
Semina hiyo inawanufaisha wanawake wa Mwanza kwa lengo la kuwaongezea kipato na pia kuweza kujiajiri ili kujikwamua na tatizo la ukosefu wa ajira. Baada ya washiriki kupata mafunzo ya biashara na urembo watapatiwa  MIKOPO kutoka Taasisi ya Manjano  Foundation  kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano. 
Mwanasaikolojia Anti Sadaka Akiwa katika Picha ya Pamoja na wanawake wa Mkoa wa Mwanza waliojitokeza  kwenye Mafunzo ya Ujasiriamali  yanayoendeshwa  na Taasisi ya Manjano Foundation.
Washiriki wa mafunzo hayo  wameushukuru uongozi wa Taasisi ya Manjano  Foundation kwa kuwakumbuka na kuwaletea Mradi huo jijini Mwanza. Wakieleza zaidi wamesema kwa muda mrefu wamekuwa na hamu ya kujua zaidi kuhusu matumizi sahihi ya vipodozi lakini walikosa elimu hiyo ya kuwa Makeup Artists.

Kikao cha kwanza cha kamisheni ya kukabiliana na maafa chakutana zanzibar

0
0
Kikao cha kwanza cha Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar chakutana chini ya mwenyekiti wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ofisini kwa Vuga Mjini Zanzibar.
Balozi Seif akikiongoza Kikao cha Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar akisaidiwa na Makamu Mwenyekiti wake kulia, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Moh’d Aboud Moh’d.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Nd. Ali Juma Hamad aliyesimama akitoa Muhtasari wa Sheria ya Kamisheni hiyo kwenye Kikao cha kwanza Wajumbe wa Kamaisheni hiyo.

Muhimbili Yapokea Msaada wa Mashine maalum kwa Watoto

0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imepokea msaada wa mashine moja ya kumsaidia mtoto kupumua Ventilator Machine yenye thamani ya Shilingi Milioni 17. Msaada huo umetolewa na Human Walfare Trust kwa ajili ya Idara ya magonjwa ya dharura na ajali katika hospitali ya Taifa Muhimbili.

Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya Human Walfare Trust , Bwana Dipak Vassa amesema lengo ni kuendelea kusaidia sekta ya afya mbapo wanataraji kuipanua zaidi idara ya magonjwa ya dharura na ajali kwenye hospitali hiyo.

Mipango mingine ni kutengeneza uwanja maalumu wa kuchezea ili watoto wenye matatizo ya Saratani ambao wanapatiwa matibabu MNH wautumie uwanja huo na pia kutoa usafiri wa basi kwa ajili ya kuwapeleka Ocean Road.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Mseru amewashukuru Human Walfare Trust kwa msaada huo na kuahidi kuutumia vema kwa lengo lililokusudiwa.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Mseru akipokea msaada wa mashine ya kuwasaidia watoto kupumua ambayo imetolewa na Human Walfare Trust kwa ajili ya Idara ya Magonjwa ya Dharua na Ajali hapa MNH.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Mseru akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakuu wa Idara na wawakilishi kutoka Human Walfare Trust ambao wametoa msaada wa mashine ya kusaidia watoto kupumua (Ventilator Machine). Picha kwa Niaba ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)

NMB na John Deere wasaini makubaliano Kusaidia Wakulima Nchini

0
0
Kampuni maarufu kwa uuzaji wa matrekta duniani ya John Deere imeingia makubaliano na benki ya NMB ili kutoa mikopo nafuu kwa wakulima wanaochipukia nchini yenye nia ya kuwarahisishia kupata vifaa vya kilimo.

Makubaliano hayo yatarahisisha upatikanaji wa vifaa kazi kama matrekta kutoka kampuni ya John Deere kupitia wakala wao wa hapa nchini – LonAgro ambao husambaza matrekta kwaajili ya shughuli za kilimo.

Kupitia makubaliano hayo yaliyoingiwa leo jijini Dar es Salaam, nje ya kurahisisha upatikanaji wa vifaa vya kilimo, pia kampuni ya John Deere itatoa mafunzo ya jinsi ya kutumia vifaa hivyo hayo pamoja na mafunzo ya biashara ya kilimo kwa wanunuzi wa vifaa hivyo.
Mkurugenzi wa John Deere kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara - Antois van der Westhuizen amesema kuwa mikopo hiyo ya matrekta itakayotolewa na NMB kwa kushirikiana na kampuni yake  ina lengo la kuinua wakulima wadogo kubadirisha kilimo kutoka kilimo cha mazoea kuwa kilimo endelevu chenye kutumia vifaa vya kisasa kama matrekta ya kulimia, kuvuna na pia kusafirisha mazao.

“kwa kutambua umuhimu wa wakulima wadogo katika nchi za Afrika, John Deere kwa kushirikiana na NMB tunategemea kuweka mifumo itakayowawezesha wakulima wadogo ili kuleta ufanisi katika shughuli nzima za kilimo. Ufanisi katika manunuzi ya pembejeo, uzalishaji na pia matumizi ya teknolojia za kisasa (mbegu, mbolea na hata vitendea kazi - Mashine) na pia ufanisi katika kutafuta masoko ya mazao shamba yao.” 

Alisema van der Westhuizen na kuongeza kuwa John Deere inaelewa kuwa wakulima wadogo wanaweza wasimudu uwekezaji wa tekinolojia na ndio maana wapo NMB kusaidia kuwapa mikopo itakayowawezesha kununua vifaa hivyo.

Uwezeshaji kutoka kwenye taasisi ya fedha utasaidia wakulima wengi kumudu upatikanaji wa vifaa muhimu vya kilimo kulingana na tekinolojia za kisasa za kilimo na hivyo kusaidia kuboresha shughuli za wakulima mashambani, kuongeza mavuno na pia kuongeza kipato cha kaya moja moja.

“malengo makubwa ya John Deere ni kusaidia wakulima wadogo na wanaochipukia kufanya kilimo kama biashara na kukuza shughuli hizo mpaka kufikia kuwa wajasiliamali wakubwa watakaosaidia wakulima wadogo kupitia vifaa vyao vya kilimo kama matrekta ya kulimia na kuvuna kupitia mtindo wa mkataba.” Aliongeza  van der Westhuizen

Akiongea baada ya kuweka saini makubaliano jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha wateja wakubwa wa NMB – Filbert Mponzi alisema kuwa benki inatambua umuhimu wa sekta ya kilimo katika ukuaji wa uchumi wa nchi na hivyo kuchukua hatua madhubuti ya kuingia makubaliano na makampuni na pia kubuni bidhaa zinazolenga kuboresha sekta ya kilimo.

“upatikanaji wa mikopo, siku za nyuma ulikuwa ni kikwazo kikubwa katika maendeleo ya kiilimo, makubaliano haya yanakuja kuleta suruhisho muhimu kabisa kwa wakulima kuanza kumudu gharama za ununuzi wa vifaa muhimu vinavyoendana na tekinolojia ya leo katika kilimo.” Alisema Bwana Mponzi.

NMB tumewafikia zaidi ya wakulima wadogo 600,000 kwa kusaidia mitaji kwaajili ya uzalishaji wa mazao ya kilimo, pia tunasaidia wakulima wakubwa ili waweze kukua zaidi. Katika mipango ya benki ya uwajibikaji kwa jamii, tunatoa elimu kwa wajasiliamali kupitia mafunzo mbalimbali ya kibiashara na hivyo kuwawezesha kwa maarifa na uelewa jinsi ya kutunza fedha na pia kukuza mitaji. 

Kampuni ya John Deere inaamini kuwa wakulima wanaochipukia kwa kutumia mashine ambazo zinawawezesha kufanya kilimo cha kisasa kwa kupitia mafunzo maalumu, wanaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa hazina ya chakula duniani. Wanaamini kuwa wakulima wadogo na wanaochipukia kwa kutumia vifaa vya uhakika na mafunzo watachangia sana kuongezeka kwa mavuno na uzalishaji kukua mara dufu katika mtiririko mzima wa mzunguko wa kilimo nchini.

LonAgro, kama mawakala waliosajiliwa na John Deere nchini, wanaamini kuwa suruhisho la zana za kilimo na mashine ndilo suruhisho pekee katika kukabiliana na upungufu wa chakula duniani.

Mkurugenzi wa LonAgro Tanzania Lukas Botha alisema kuwa “Kupitia makubaliano kati ya NMB na John Deere, wakulima wana uhakika wa kupata nyenzo muhimu na kufanya ukulima kwa tekinolojia kisasa kuwezekana na pia wana uhakika wa kupata ushirikiano mkubwa kutoka LonAgro na kufanya mashirikiano endelevu.”
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images