Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110089 articles
Browse latest View live

Ziara ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Profesa Makame Mbarawa Kukagua miradi inayotekelezwa na Wizara hiyo

$
0
0
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Profesa Makame Mbarawa akiweka saini kwenye kitabu cha kumbukumbu mara alipowasili Mkoani  Mtwara  kwa Ziara ya Kukagua miradi inayotekelezwa na Wizara hiyo,kulia ni Mkuu Mkoa wa Mtwara Bi.Halima Dendegu na kushoto ni Katibu Mkuu sehemu ya Mawasiliano Prof.Faustin Kamuzora.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Profesa Makame Mbarawa akikagua Mitambo ya Mawasiliano ya TTCL Mkoani Mtwara kulia ni  Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Dkt.Kamugisha Kazaura na wadau wengine wa mawasiliano.

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Profesa Makame Mbarawa akizungumza na baadhi ya abiria wanaotumia kivuko cha Mv.Mafanikio kabala ya kuanza kwa safari kutoka Msangamkuu kwenda Msemo.

 Mojawapo ya Meli kubwa zinazotia nanga katika bandari ya Mtwara ikiwa tayari kwa kupakua mzigo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

MWILI WA MAREHEMU LETICIA NYERERE WAWASILI JIJINI DAR ES SALAAM MAZISHI YAKE KUFANYIKA BUTIAMA MKOANI MARA KESHO KUTWA

$
0
0
 Askari wa Bunge wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mara, Leticia Nyerere aliyefariki nchini Marekani alikokuwa akitibiwa mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam leo jioni. Mwili huo kesho utaagwa nyumbani kwa Mwalimu Nyerere Msasani  kabla ya kusafirishwa kwenda Butihama mkoani Mara kwa mazishi yatakayofanyika keshokutwa.
 Mwili huo ukiingizwa kwenye gari maalumu katika uwanja huo.
 Ndugu jamaa na marafiki wakijadiliana jambo wakati wa kuupokea mwili huo.
 Ndugu, jamaa, marafiki na watoto wa marehemu wakisubiri kuupokea mwili wa mpendwa wao.
 Mume wa marehemu, Madaraka Nyerere akizungumza na wanahabari baada ya kuupokea mwili huo uwanjani hapo.
Mtoto wa marehemu (kulia), akifarijiwa na mmoja wa ndugu wakati wakienda kupanda gari kabla ya kuondoka uwanjani hapo.
Picha na Dotto Mwaibale

SIMU TV:UCHAMBUZI WA HABARI TOKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI

RAIA WA UJERUMANI AITELEKEZA FAMILIA YAKE HOTELINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Raia wa Ujerumani (kulia) ambaye jina lake halikupatikana mara
moja, ametiwa na mbaroni na Jeshi la  Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa tuhuma za kutaka kuitoroka  familia yake katika  Hoteli ya Cate Dar es Salaam. Raia huyo alikuwa nchini na mkewe mwenye asili ya Afrika katika kipindi cha msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka. Alijaribu kumtoroka mkewe na mtoto (4) na kuwaacha wakidaiwa deni la sh. 315,000 baada ya kile kilichodaiwa kuzuka ugomvi baina yao.

 Mtoto wao (4) akisaidiwa kupandishwa katika Gari




 Raia wa Ujerumani huyo akitaka kuruka toka katika Gari la Polisi
 Mke wa Raia wa Ujerumani wa pili kulia akiwa anaingia katika Gari kuelekea katika Kituo cha Polisi cha Msimbazi Dar es Salaam na wapili kulia ni kaka wa mwanamke wa Raia wa Ujerumani
Wananchi wakifuatilia kwa karibu tukio hilo

Muujiza wa Kupandikizwa kwa Ubongo (Bone Marrow) Ulivyobadilisha Maisha

$
0
0
Mara nyingi watu kutoka nchi zilizoendelea waishio na tatizo la damu na upungufu wa kinga mwilini huishi, tofauti na nchi zinazoendelea ambazo zinakumbana na uhaba wa huduma ya kupandikiza uboho.

Huduma za kisasa na bora za kupandikiza uboho katika nchi zinazoendelea kama Tanzania bado ni tatizo; kusubiria huduma bora katika nchi hizi zinazoendelea, inaendelea kuhusiana na hali mbaya ya kiafya na vifo. Hii ni kutokana na ripoti mpya za kiafya. Kutokana na takwimu za mwaka 2012, ni nchi tatu tu za kiafrika ambazo ni Misri, Afrika kusini na Nigeria ambazo zina hospitali zenye uwezo wa kupandikiza uboho.
Muanzilishi na Mwenyekiti wa Apollo Hospitals Dkt. Prathap .C. Reddy.

Upandikizi wa uboho ni njia mpya ya kisayansi na udaktari katika kutibu matatizo na maradhi kama Leukimia, kuvimba kwa seli (Lymphoma), saratani katika seli nyeupe (Multiple myeloma), sicko seli anaemia, kuharibika kwa uboho (Aplastic anaemia), Thalassemia, ukosefu wa seli nyeupe (Congenital neutropenia), na upungufu wa kinga za mwili. Matatizo maalum kama ya uvimbe na ulemavu wa kurithi kama Thalassemia pia umepatiwa ufumbuzi mzuri kupitia matibabu haya.

Upandikizwaji wa uboho na seli za mfumo wa kati wa damu ni mfumo unaorudisha seli katika shina la mfupa zilizoharibiwa kwa matumizi makubwa ya mionzi ya kuulia saratani na mionzi mingine pia. Baada ya kupatiwa tiba kwa dozi yenye nguvu ya dawa za saratani na mionzi, mgonjwa huwa anatengeneza shina bora la seli, zinazo safiri kwenye uboho na kuanza kutengeneza seli mpya za damu.

BALOZI WA NORWAY HAPA NCHINI AWATUNUKU WAHITIMU CHUO CHA UFUNDI ARUSHA

$
0
0
Balozi wa Norway nchini Tanzania,Hanne -Marie Kaarstad ambaye alikua mgeni rasmi katika Mahafali ya Saba ya Chuo chaUfundi Arusha (ATC) akiwatunuku Vyeti,Stashahada na Shahada wahitimu katika fani za Uandisi Umwagiliaji,Umeme,Ujenzi,Mawasiliano Anga ,Mitambo na Kompyuta Januari 16,2016.
Baadhi ya wahitimu wa fani ya Uandisi Mitambo wakifurahia mara baada ya kutunukiwa Stashahada zao.
Wahitimu wakifatilia kwa makini hotuba mbalimbali.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MAKALA SHERIA: JE INAWEZEKANA HATI KUWA NA MAJINA YA WANANDOA WOTE ?.

$
0
0
Na Bashir  Yakub. 

Hakimiliki  katika  masuala  ya  ardhi  huhusisha  umiliki  wa ardhi  zenye hati. Umiliki huu  hutoa  wajibu  na haki  fulani  kwa mmiliki  katika  ardhi husika. Si  rahisi  kudai  una  hakimiliki  katika  ardhi kama  hauna  hati.  

Aidha  tumezoea  kuona  hati  zilizo  na  jina  la  mtu  mmoja mmoja. Hii  ni  hata  kwa  wanandoa ambao  hudai   mali  husika zinatokana  na  jasho lao wote. Lakini  je  unajua  kuwa  inawezekana   hati miliki  ikawa  na  majina  ya wanandoa  wote  badala  ya  kuwa  na  jina la mmoja tu hasa   baba   ambao  ndio  wengi  hupenda  majina  yao  yaonekane  hapo ?.  Jambo  hili  linawezekana na  linaruhusiwa.

1.HAKIMILIKI  YA  PAMOJA  KUONDOA  MGOGORO.
Kutokuelewana  ambako  mara  kadhaa  hutokea  baada  ya  kifo  cha  mmoja  wa  wanandoa  kwaweza   kuondolewa  na  umiliki  wa  ardhi  wa  pamoja. Ikiwa una  wasiwasi  juu  ya  mustakabali  wa  mali  hasa  ardhi  huko  mbeleni  ni  vema  basi  ukachukua  hatua  hii  ya  kusajili  kwa umiliki  wa  pamoja. 
Kama kiwanja/ nyumba  ina  hati  yenye majina mawili  la baba na  mama halafu mmoja  wao  akafariki itakuwa   ni  vigumu  ndugu  au  mwingine  yeyote  mwenye  nia  mbaya kudai  umiliki  wa kiwanja/nyumba hiyo. 

Lakini hali  itakuwa  tofauti iwapo  hati  ina  jina  la  mmoja  na  huyohuyo mmoja  ndiye  aliyefariki. Pale  pote  ambapo  ndugu  walidhulumu  mali  za  marehemu  hasa  ardhi  ni  pale  ambapo  kuna jina  la mmoja.

Mara  nyingi  fitina  huingia pale penye  mwanya  wa  kufanya  hivyo. Si  rahisi  fitina kuingia  pasi na  mwanya. Kuweka majina  ya  wanandoa wote  kwenye  hati  za  ardhi  ni  hatua  ya  kuziba  mwanya  wa  fitina. Itawezekanaje  ndugu au mwingine  mwenye  nia  ovu kudai umiliki  wa  ardhi  ya  marehemu huku  akijua  kuwa  hati   inalo  jina  la  mke  pia.  Si  rahisi  hata   kidogo. 

Lakini  pia  umiliki  wa  pamoja  huondoa  mgogoro  pale  panapo  talaka. Swali  la  je  mwanandoa  fulani  amechangia  chochote  katika  kupatikana  kwa  mali  huwa  halipo  ikiwa  majina  yote  mawili  ya  wanandoa  yameonekana  kwenye  hati. 

NGOMA AZIPENDAZO ANKAL


DIRA YA DUNIA YA BBC SWAHILI

Jumuiya ya Veterani wa Umoja wa Vijana Zanzibar (Young Pioneers) yazinduliwa

$
0
0
Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee akiwahutubia Veterani wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Young Pioneers wakati wa Uzinduzi wa Jumuiya hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa ZSSFKiwanja cha Watoto Kariakoo Zanzibar. na kutangaza Fedha zilizopatika katika harambee aliyoiazisha kwa ajili ya kukuza Mfuko wa Jumuiya hiyo Jumla ya Shilingi Milioni 9,724,000/= zimepatika ikiwa Fedha Taslimu Shs 3.874,500 na Ahadi Shs.5,850,000/=.
 Katibu Mkuu Wizara ya Ustawi wa Jamii Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto Mhe Asha Ali Abdalla akizungumza wakati wa hafla hiyo ya Uzinduzi wa Jumuiya ya Veterani ya Umoja wa Vijana wa Young Pioneers, katika Ukumbi wa ZSSF Kiwanja cha Watoto Kariakoo Zanzibar.
Veterani wa Young Pioneers Makame Haji Makame (Cairo) akihamasisha kwa kuimbi wimba za Vijana za wakati huo wa kuhamasisha vijana katika kujenga taifa wakati wa uzinduzi wa Jumuiya hiyo katika ukumbi wa uwanja wa watoto kariakoo Zanzibar, kabla ya kuaza kwa kongamano la Jumuiya hiyo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

TANZANIA WILL NEVER BENEFIT FROM LOW OIL PRICES.............. A RESPONSE TO JOHN MASHAKA DEBATE

$
0
0
Ankal Michuzi,

First and foremost, I must compliment our brother, learned colleague and our superstar, John Mashaka for his extra ordinary brilliance in articulating some issues we see so difficult to touch. While we may try to argue as much as we can, the truth of the matter is, John Mashaka is another level of intellect, John is a genius as some describe him, and few will dispute that

I am a PhD student at the University of Melbourne Australia, specializing in Macro Economics. I read with lot of interest John Mashaka’s analysis on the fall of oil price in the commodity markets, its impact and opportunity for Tanzania.

While I do agree with John on many aspects, and support his arguments by 100%,  I would like to challenge him to be forthcoming. He was very diplomatic in his writing and never touched on the root cause of the problem.  Why the oil price never change in Tanzania, despite the fall of the global prices.

John never told Tanzanians that, Petroleum price in Tanzania would never change because Tanzania doesn’t have refinery. It buys refined petroleum products from the middle East. John knows very well that, there is a an international cartel that controls oil trade.

These corrupt officials are making billions of dollars on petro-chemicals, and do not like to lower prices and therefore fixing it all the time in Tanzania. The same cartel and the corrupt officials within the regulatory body, ensures prices aren’t changed despite the drop from the world markets. Therefore drivers in Tanzania would never enjoy low prices. Oils price started dropping in 2014. Today as John said, it has dropped by 74% yet in Tanzania oil has dropped by only 2%, and that was after pressure from the public. 

Tanzania tax on petrol is too high, and the government cannot expect the economy to grow this commodity is unaffordable

EWURA would claim that, they are selling old stock of Petrol and Diesel. That is not true, because basically an old stock only lasts for 30 days before a new stock comes in IN Tanzania. from 2014 Until today, they have the old stock?  President Magufuli must deal with EWURA. It is this EWURA pushing inflation higher, sabotaging the Economy, and therefore the country will never enjoy low prices of oil.

SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MWENYEKITI WA CCM TAWI LA DMV MAREKANI

$
0
0
Napenda kuchukua fursa hii kutuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha ghafla cha mwenyekiti wa Tawi la CCM DMV ndugu George Sebo kilichotokea tarehe 18 Januari 2016, Jumatatu asubuhi katika Hospitali ya Prince George Maryland, nchini Marekani. 

Kwa kweli kifo hiki cha ghafla tumekipokea kwa mshtuko mkubwa na majonzi Watanzania wote tunaoishi hapa Marekani, kwani George Sebo alikuwa ni mtu mkarimu kwa watu wote bila kujali tofauti zozote za kiitikadi. 

Nachukua  fursa hii kwa niaba ya Wanachama na wapenzi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tawi la Washington DC Kumpa pole mke wa Marehemu mama Grace Mgaza, Ndugu, Jamaa, Marafiki pamoja na wanachama wote wa CCM kwa msiba huu mkubwa.

Tupo pamoja katika kipindi hiki kigumu cha Maombolezo.

Mungu ailaze Roho ya Marehemu GEORGE SEBO Mahali pema Peponi, AMIN.
Mwenyekiti wa Chadema DMV
Kalley Pandukizi

SIMU TV: MAPITIO YA MAGAZETI LEO

CHF YAKUBALIKA KAMA SULUHISHO LA MATIBABU NYEGENDI MKOANI LINDI

$
0
0
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa kishirikiana na Halmashauri ya Lindi Vijijini wameendelea na kampeni ya uhamasishaji wa wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii CHF katika kata ya Nyangedi.

Katika uhamasishaji huo uliongizwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Nawanda kaya 70 zilijiunga papo hapo kwa kuchangia Shilingi 10,000 kwa kaya hivyo jumla ya Shilingi 700,000 zilikusanywa.

Aidha Mh. Nawanda alimwagiza Mganga Mkuu wa Wilaya kuhakikisha hakuna upungufu wa dawa katika kituo hicho na endapo litatokea hilo wananchi wamjulishe mapema. 

Pia aliwakumbusha maagizo ya Mkuu wa Mkoa kwamba wasiojiunga na CHF watalipia Sh. 10,000 kwa matibabu kila wanapoenda kutibiwa kama hawaoni umuhimu wa kuchangia 10,000 kwa kaya kwa mwaka mzima na wakatibiwa kwa kadi. 

Alimaliza kwa kuwahimiza watu kufanya kazi kwa bidii ili waweze kutimiza mahitaji yao kama afya kwani fursa za uzalishaji zipo.Uhamasishaji wa CHF unaendelea katika kata mbalimbali za Lindi katika wiki hìi na baada ya hapo katika Halmashauri mbalimbali nchini.
naw1
Wananchi wa Kata ya Nyengedi Lindi wakimsikiliza Mh. Nawanda DC wa Lindi akiwaelimisha umuhimu wa CHF katika kampeni ya uhamasishaji unaofanywa na NHIF kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya hiyo
naw2
Mkuu wa wilaya ya Lindi Mh. Yahya Nawanda akiwasikiliza akisikiliza kwa makini hoja za wana Nyengedi ili kupata mrejesho wa huduma za afya katika kata hiyo. wakati alipokuwa akiwaelimisha kuhusu umuhimu wa huduma za CHF katika kampeni ya uhamasishaji inayofanywa na NHIF kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya hiyo
naw3
Mkuu wa wilaya ya Lindi Mh. Yahya Nawanda akisisiztiza jambo wakati NHIF ilipozindua kampeni hizo katika wilaya ya Lindi mkoa wa Lindi kulia ni Mkuu wa mkoa huo Mh. Jordan Lugimbana na kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Ali Mtopa na Eugine Mikongoti Mkurugenzi wa wa Huduma na Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii Tanzania, NHIF

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

EALA TO HOLD PLENARY IN ARUSHA NEXT WEEK …regional legislators gear up for a busy two week period

$
0
0
East African  Legislative  Assembly
The East African Legislative Assembly (EALA) shall hold its sitting in Arusha, Tanzania, next week. The Forth Meeting of the Fourth Session of the Third Assembly takes place from Monday, January 24th, 2016 to Friday, February 5th 2016.
The Assembly is to be presided over by the Speaker, Rt. Hon Daniel F. Kidega. Top on the agenda during the two week period is debate on the EAC Disaster Risk Reduction and Management Bill, 2013, as well as reports emanating from various Committees following deliberations with key stakeholders in the integration process.
The Objective of the Disaster Risk Reduction and Management Bill, 2013 is to provide a legal framework at regional and national level for timely intervention in disaster situations and to protect the people and the natural environment affected by disaster through comprehensive disaster risk reduction and management. 
The Bill which was due for the 3rd reading at the 4th meeting of the 2nd Session in Kampala, Uganda in January 2014, was adjourned following a request by the Chairperson of the Council of Ministers, citing the need to consult the relevant provisions of the Treaty and to allow for pursuit of the ratification of the EAC Protocol on Peace and Security.  The said Protocol among other objectives, provides for co-operation in DRR management and crisis response.
Earlier in August 2013, the EAC Council of Ministers moved a Motion seeking to take over the Bill from the original mover, Hon Patricia Hajabakiga, make appropriate amendments and initiate its re-introduction as a Council of Ministers’ Bill.  The move was preceded by a sitting of the Sectoral Council on Environment to give policy direction to the said Bill.
The issue of the humanitarian situation in the Republic of Burundi is also expected to be a matter of discussions at EALA should the Regional Affairs and Conflict Resolution Committee complete and present its Report on the Petition by the Pan-African Lawyers Union (PALU) concerning the political situation in Burundi.  
 Last week, the Committee held a public hearing workshop in Arusha where it listened to the PALU petition as well as to the contributions by other stakeholders comprising of the representatives of Civil Society Organisations and the opposition parties in Burundi.   The Committee is expected to listen to representatives of the Government of Burundi on January 25th, 2016, who requested to be considered to appear before it after January 18th, 2016. Thereafter, it will retreat to prepare its report to the Assembly for debate.
The House is further expected to consider a report of the General Purpose Committee on a petition on work and residence permits supplicated by the East African Trade Union Confederation (EATUC) and the East African Employers Organisation (EAEO).  The petition amongst other things, states the desire of workers and employers to see the Common Market Protocol fully implemented to enhance productivity.
In March 2015, the EATUC/EAEO presented a petition to the Speaker of EALA in which it made 17 prayers including the harmonization of the standards and processes of acquiring permits as well as the future amendment of annex 2 of the Common Market Protocol to put in place a roadmap for free movement of workers.    
The petitioners further call for standardization of the processes of issuance of work permits, pending their eventual removal in the long-run.  The General Purpose Committee has since met with the employers and prepared its report which is to be debated by the House.
The House will also receive and debate on the report of the Committee on General Purpose on the EAC Annual Report as well as a Report of the Committee on Legal Rules and Privileges on a resolution moved under Rule 30 (J) of the Assembly Rules of Procedure on a matter of privileges arising from a threat of tenure of office of Members. 
EALA Sittings are held under the principle of rotation in line with Article 55 of the EAC Treaty. EALA held its last Sitting in November 2015 in Kigali, Rwanda.

TTCL KUREJEA KUWA MALI YA UMMA KWA ASILIMIA 100.

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Makame Mbawara (wapili kulia) akitoa maekekezo kwa Viongozi wa TTCL katika ziara yake Mkoani Mtwara juzi.     Wafanyakazi wa TTCL Mtwara katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Prof. Tolly Mbwette na Ofisa Mtendaji Mkuu wao, Dk. Kamugisha Kazaura. Ofisa Mtendaji Mkuu wao, Dk. Kamugisha Kazaura (wa kwanza kushoto) akizungumza kwenye ziara ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Makame Mbawara mkoani Mtwara juzi. Mazungumzo kati ya Wafanyakazi wa TTCL Mtwara katika mkutano na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Makame Mbawara alipofanya ziara yake.

 SERIKALI ipo katika hatua za mwisho za kuilipa kampuni ya Bharti Airtel ili kurejesha umiliki wa asilimia 100 katika Kampuni ya Simu Tanzania, TTCL. 

Uamuzi huo unaotarajiwa kutekelezwa kabla ya mwisho wa mwezi huu utaiwezesha TTCL kurejesha hisa zake 35% zilizonunuliwa na Airel mwaka 2001 na kuifanya Bharti Airtel kuwa mbia mwenza katika Kampuni hiyo. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof Makame Mbarawa ametangaza uamuzi huo Jumatatu hii Mkoani Mtwara alipotembelea Ofisi za TTCL Mkoa wa Mtwara, kukagua mitambo na miundo mbinu ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano.

 "Serikali imesikia kilio cha muda mrefu cha Watanzania na wadau wote wa TTCL kuhusu kuondoka kwa mbia mwenza Kampuni ya Bharti Airtel. Ubia huu wa TTCL na Bharti Airtel utahitimishwa Rasmi kabla ya mwisho wa mwezi huu. Tumefanya majadiliano ya kutosha, tumekubaliana kuwa Serikali iilipe Bharti Airtel sh bilioni 14.9 ili kurejesha hisa za 35% za TTCL na kuifanya Kampuni hii ya TTCL kuwa mali ya Umma kwa 100%. 

Tutatumia fedha za Mapato ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ili kukamilisha utaratibu huu. Naiagiza Bodi na Menejimenti ya TTCL kufanya kazi kwa bidii na Ufanisi Mkubwa na kusimamia kikamilifu shughuki za TTCL ili kutimiza jukumu lake kwa Umma.

 Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Prof. Tolly Mbwette amesema, kukamilika kwa mchakato huu ni hatua muhimu sana kwa Uhai na ufanisi wa TTCL na kusisitiza kuwa, mpango wa mageuzi ya kibiashara wa kampuni hiyo sasa utatekelezeka kwa kasi kubwa baada ya hatua hii.

 Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura amesema, jitihada kubwa za TTCL sasa zitaelekezwa katika kuboresha huduma kwa kutumia fedha za ndani na Mikopo ya wadau wa kibiashara ili kuiwezesha kampuni kuendelea kuwa kiongozi katika utoaji wa huduma bora na nafuu katika soko la Mawasiliano nchini.

 Hivi karibuni, TTCL imezindua huduma za Mtandao wenye kasi zaidi wa 4G LTE na kuimarisha ubora wa huduma zake za data na sauti. Aidha, TTCL na Benki ya TIB zimeingia makubaliano ya mkopo wa fedha na dhamana za Benki utakaoiwezesha TTCL kupata fedha dola za Marekali milioni 329 ili kuingiza mitambo mipya ya kisasa itakayo boresha huduma zake ikiwa ni pamoja na kuanzisha huduma ya miamala ya fedha kwa njia ya mtandao.

NHIF Yakabidhi Kadi za Matibabu kwa Wanachama wa TBN.

$
0
0
Meneja wa Mfuko wa Afya ya Jamii, Slivery Mgonza akimkabidhi Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii (Bloggers-TBN) kadi za Bima ya Afya kwa baadhi ya wanachama wa TBN. Meneja wa Mfuko wa Afya ya Jamii, Slivery Mgonza akimkabidhi Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii (Bloggers-TBN) kadi za Bima ya Afya kwa baadhi ya wanachama wa TBN. Kushoto ni Ofisa wa Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa, Nicholaus Mwangomo. Meneja wa Mfuko wa Afya ya Jamii, Slivery Mgonza akimkabidhi Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii (Bloggers-TBN) kadi za Bima ya Afya kwa baadhi ya wanachama wa TBN. Kushoto ni Ofisa wa Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa, Nicholaus Mwangomo.

RAIS MHESHIMIWA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKIONESHA UMAHIRI KATIKA USHONAJI.

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akionesha umahiri wake wa kushona kama inavyoonekana katika picha.
 Picha na IKULU.

INTRODUCING MRISHO MPOTO'S NEW HIT "SIJONJE" Feat. BANANA ZORRO AND FARIDA KATUNGAYE

$
0
0
WIMBO : SIZONJE
MRISHO MPOTO Feat. BANANA ZORRO AND FARIDA KATUNGAYE
WAITE RECORDS
PRODUCER : ALLAN MAPIGO

PIA MRISHO AMEINGIA KWENYE MASHINDANO YA KORA (KORA AWARDS) KIPENGELE CHA MWANAMUZIKI BORA WA KIUME WA NYIMBO ZA ASILI (BEST TRADITIONAL MALE ARTIST) KUPITIA WIMBO WAKE WA "WAITE"
KURA ZITAANZA KUPIGWA KESHO TAREHE 20/1/2016,
JINSI YA KUPIGA KURA
ANDIKA: KORA 67
TUMA KWENDA: +248984000

MWISHO WA KUPIGA KURA NI SIKU
YA TUZO ZENYEWE, MWEZI MARCH!

RAIS DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI AKIONESHA UMAHIRI WAKE WA KUSHONA

$
0
0
 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akionesha umahiri wake wa kutumia Cherahani na kushona nguo za wafanyakazi wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kuvifahamu vitengo mbalimbali na watumishi wake wa  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 20, 2016 
 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kushona kwa ustadi wa hali ya juu
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimalizia moja ya nguo za wafanyakazi wa Ikulu.
Viewing all 110089 articles
Browse latest View live




Latest Images