Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1094 | 1095 | (Page 1096) | 1097 | 1098 | .... | 3278 | newer

  0 0


  0 0

  Na  Bashir  Yakub. 

  Tunapozungumzia mgogoro  wa ardhi  tunazungumzia mgogoro  katika  viwanja, mashamba, nyumba  na  majengo. Wengi  wetu  tunapokutwa  na  migogoro  ya  ardhi  hukimbilia  mahakama  za  wilaya  au  mahakama  kuu  ya  ardhi. Lakini  tunasahau  kuwa  lipo  baraza  la  ardhi  la kata  ambalo  baadhi  ya  migogoro  haifai  kwenda  huko  wilayani  au  mahakama  kuu kabla  ya  kupitia  hatua  hiyo.  Makala  yataeleza  kuhusu  baraza  la  ardhi  la  kata  na  mashauri  yanayotakiwa  kuanzia  hapo. 

  1.NGUVU  YAKE  NI  KATIKA  KATA  TU.
  Baraza la  ardhi  la  kata  ni  mahakama  ya  ardhi  katika  kata husika . Hii  ni  kwa  mujibu  wa kifungu  cha  10 ( 1 )  cha  sheria  ya  mahakama  za  usuluhishi  wa  migogoro  ya ardhi.   Baraza  hili mipaka  yake  ni  katika  kata  husika  kwa maana  ya kuwa  mipaka  ya  kata ndio  mamlaka  yake  kijiografia. 

  Kwa  maana hii  kila  kata   hutakiwa  kuwa na  baraza  lake  la  usuluhishi  wa  migogoro  ya  ardhi . Baraza la  ardhi  la  kata  fulani  haliwezi  kuvuka  mipaka  na  kwenda  kuamua  mgogoro  wa  ardhi  wa  kata  nyingine. 

  2.  JE  INATAKIWA  WAAMUZI  WANGAPI  KATIKA  BARAZA.
  Unapokuwa  na mgogoro  katika  baraza  hili  ni  muhimu  kujua  ni  watu  wangapi  wanatakiwa  kuamua  mgogoro  wako. Mara    kadhaa  hasa  huko  vijijini  waamuzi  katika  mabaraza  haya  wamekuwa  wakijikalia  tu  na kutoa  maamuzi  pasi na  kuzingatia akidi. Unapaswa  kujua  kuwa  kuna  akidi  maalum  ya  kisheria na  hivyo  kabla  ya kuamuliwa  mgogoro  wako  ni  vyema    ukahoji  akidi  hasa  ikiwa  haijatimia. 

  Kifungu  cha 14( 1 ) kinasema  kuwa  vikao   vya  usuluhishi vya  baraza   vitakaliwa  na  wajumbe  wasiopungua  watatu  huku  mmoja  akitakwa  kuwa  mwanamke.  Hii  ni  akidi  ya  kisheria  na  hivyo  yafaa  ujue  kuwa  unayo  haki  ya  kuhoji  ikiwa  akidi  hii  haijatimia.  Ni  muhimu  kutoruhusu  kikao  kuendelea  ikiwa  akidi  haijatimia  kwakuwa  maamuzi  yatakayotolewa  na akidi  pungufu  kisheria yatakuwa  batili. Kwahiyo  hata  kama  umeshinda  ushindi  wako  utakuwa  ni  kazi  bure.


  0 0

   Askari wakiwahoji waendesha pikipiki (wa pili na watatu kulia) waliogongana katika Barabara ya Morocco eneo la Bonde la Mkwajuni, Dar es Salaam. Nawote wamekimbizwa katika Hospitali ya Mwananyamala na watatu kulia mkono inadaiwa umevunjika kwa juu ya maungio ya kiganja cha mkono wa kushoto na mguu wakushoto kuwa na maumivu makali na wapili kulia maumivu ya mguu (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
   Mmoja wa Dereva wa Pikipiki (wakwanza kulia) akikabidhi nyaraka zake kwa Askari na alikuwa akienda kupata matibabu katika Hospitali ya Kairuki na kukimbizwa wote wawili katika Hospitali ya Mwananyamala
  Dereva akitoa maelezo kwa Askari waliokua katika Bonde la Mkwajuni   0 0

  Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, akizungumza na waandishi wa habari, Makao Makuu ya shirika hilo, Dar es Salaam leo, kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu utendaji wa shirika kwa mwaka uliopita na mipango ya shirika kwa mwaka 2016, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Posta barani Afrika. yanayoadhimishwa Januari 18 ya kila mwaka. Kushoto ni Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara za Shirika, Janeth Msofe na kulia ni Meneja Mkuu Rasilimali za Shirika, John Lukonge. 

  Mkuu wa Uhusiano Shirika la Posta Tanzania (TPC), Wilfred Miigo, akitoa utambulisho wakati wa maadhimisho ya Siku ya Posta Barani Afrika leo jijini Dar es Salaam. Katikati waliokaa ni Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika hilo, Fortunatus Kapinga, kushoto ni Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara za Shirika, Janeth Msofe na kulia ni Meneja Mkuu Rasilimali za Shirika, John Lukonge.
  Kaimu Meneja Shughuli za Biashara za Fedha, Mourus Obwana, akijitambulisha wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika maadhimisho ya Siku ya Posta Barani Afrika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Barua na Logistik, Fadya Zam na kulia ni Meneja Mifumo ya Mawasilano, David Mtake.


  0 0

  Tanzania ni miongoni nchi chake katika bara la Arfica  iliojaaliwa kuwa na vivutio vingi vya utalii.Tofauti na nchi nyengine nyingi za Africa na hata dunia kwa ujumla.miongoni mwa vivutio hivo vya utalii nchini Tanzania ni mbuga za wanyama.

  Katika mkoa wa Iringa ambao unapatikana nyanda za juu kusini mwa Tanzania umejaliwa kuwa na mbuga ya wanyama ‘Ruaha Nationa park’mbuga hii ipo magharibi mwa Iringa katika kijiji cha tunga malenga kata ya Idodi kilimota 128 kutoka Iringa mjini.

  Mbuga hii ni ya kipekee yenye wanyama wa kila aina na adimu kupatikana kuonekana sehemu nyengine ulimwenguni wanyama hao ni kama vile ‘kadu’ni aina ya wanyama ambao kisura wameshabihiana sana na swala lakini sio swala na ndio maana mwandishi wa makala hii anasema mbuga hii ni ya kipekee, Kijografia mbuga hii ya Ruaha imepakana na mikoa kadhaa ya Tanzania,miongoni mwa mikoa hio ni singida,Dodoma,mbeya na ina ukubwa wa kilomita za mraba 1300.
  mwandishi wa makala hii Muhamed Khamis akizungumza na chifu wa kabila la kimasai katika kata ya idodi wilaya ya Iringa vijijini Chif Lameck mtemisika.
  Wakaazi wa kijiji cha karibu na eneo hili’tungamalenga’wameleza kusikitishwa kwao licha ya uwepo wa kivutio kikubwa cha wageni lakini kwa upande wao wanaeleza hawafaidiki na lolote lile kupitia mbuga hio.

  Kwa nyakati tofauti wakizungumza na mwandishi wa makala haya walisema uwepo wa mbuga hio kwao ni kama mzigo kwani haina faida kwao,bali ni  hasara inayotokana na wanyama hao kwa vipando vyao mashambani.


  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watanzania waishio Botswana baada ya kuhudhuria mkutano wa SADC mjini Gaborone Januari 18, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Watanzania waishio Botswana baada ya kuhudhuria mkuatano wa SADC mjini Gaborone Januari 18, 2016.
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Watanzania waishio Botswana baada ya kuhudhuria mkutano wa SADC mjini Gaborone Januari 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

   The oil price has been on a free fall in the past couple of months, hitting an historic low last Friday. For the first time in 12 years, oil prices tumbled below $30 as the fear for China’s economic slow down, US dollar strength and steady oil reserves, disagreement among OPEC nations and the expected Iranian’s return into the global oil market has gripped the financial markets with fear, which has sent oil prices plummeting. 

  Oil has recorded more 70% price drop in one year; A significant drop from 2014, peak when prices reached $112 a barrel. There are all indications that prices could hit below $20 a barrel before the end of first quarter of 2016. The drastic and sharp drop in oil prices currently rattling the financial markets, is a combination of many factors, among which, the China’s economic slow down and the US energy policy shift plays a significant role.

  As the US moves towards energy self sufficiency; it has been boosting its crude stockpiles (reserves) and upping its domestic oil production. This move has left her traditional suppliers such as Venezuela, Nigeria, Iraq Saudi Arabia etc, in the cold with millions of barrels of crude oil without buyers. 

  China’s dismal economic news is contributing greatly in the current oil price slump. As recently as 2012, China was a red-hot economy, growing at 10%, with consumption of oil at 10.8 million barrels per day. However, today, its oil consumption has dropped by whopping 397,000 barrels per day. A drop that has partly been driven by the economic slowdown or declining industrial productivity, with projection of 6.5% growth this year, the lowest in 25 years. 

  The United States dollar plays an essential role in the pricing of commodities such as gold and oil in the global markets. With US economy steadily recovering from the 2008-2009 financial meltdown, the US dollar has equally been strengthening in value against most other currencies, and since oil is traded in US-dollar, the rising dollar has been reflected by a fall in value of oil relative to the US dollar. 

  Iran, which has the world’s fourth-largest oil reserves, is also expected to return, and is expected to pump an additional half-million barrels a day into international markets very soon, after the United States and other western powers lift sanctions against its oil exports, and this is likely to send oil prices diving deeper 

  The Vienna based oil cartel, OPEC, seems to be in disarray, as its members do not seem to agree on methodologies to control the oil output. While Nigeria, Angola and other hard-hit by the price drop are pressing for oil production cut, Saudi Arabia, Kuwait, Qatar and the UAE would not agree to reduce their production. And without unanimous agreement, oil prices could only keep on falling

  Oil-price collapse is rippling throughout the world. Russia, an oil-exporting country has been one of the first major casualties’. With oil prices slumping and sanctions painfully biting the country over its actions in Ukraine, Its currency (rubble) value has fallen by 9.7% in the last ten months. Last week, Russia conceded to economic difficulties and announced a 10% budget cut in light of the falling oil prices.

  Nigeria, one of Africa’s major oil producers is on catastrophic economic edge, and could possibly see economic implosion and unrest; citizens taking to the streets in protest of economic hardship, following the massive budget shortfalls caused by the tumbling oil prices. Nigeria 2015 budget passed when price of oil was around $53 per barrel, while 2016 budget was assumed when price of oil was above $38 per barrel last December.  

  In short, Nigeria is a troubled economy on the brink of a recession. Matters are expected to worsen if India, one of her largest customers decides to buy oil from her neighbor Iran, who has been re admitted into the international oil trade following the lifting of economic sanctions on Iran by the United States.

  One man’s loss many a times, not all the time, is another man’s gain. In contrast to the widespread fear and panic in oil exporting countries, oil-importing countries should be in celebratory moment by seizing the opportunity provided oil-price drop. Both Tanzania’s motorists and policy planners will benefit from the historically low oil prices. While Tanzania’s motorists will benefit at the pump by paying less for their gasoline, country’s economic-policy planners should work on re-distribution of resources realized in the form of low oil prices to tame the inflation.

  Drop in energy prices, will enable importing countries (Tanzania inclusive) to reduce fuel subsidies, and thus relieving the government of heavy financial burden.  Low oil price for that matter is more of a tax cut or stimulus incentive to the government of Tanzania. Savings realized from low oil prices should be spent on other critical projects to foster the country’s economic growth as well as taming the inflation.

  The government of Tanzania could invest cash savings realized from low oil prices into alternative sources of energy, into education, healthcare or into geographic areas where infrastructure has been neglected or where manufacturing and jobs have dried up.

  Mungu Ibariki Tanzania
  John Mashaka
  Mashaka.john@yahoo.com

  0 0


  0 0

   
   Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Jordan Rugimbana kwa niaba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto amezindua rasmi kampeni ya kitaifa ya uhamasishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii ( CHF) katika kata ya Nyangamara iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Vijijini.

  Katika uzinduzi huo ulioratibiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa kushirikiana na Halmashauri ya Lindi Vijijini kaya zipatazo 261(sawa na wanufaika 1,566) zilisajiliwa papo hapo katika CHF kwa mchango wa Shilingi 10,000 kwa mwaka. Pia Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Nawanda alihamasisha viongozi mbalimbali wa Mkoa huo ambao hawakuwepo ambapo zilichangwa fedha kwa ajili ya kaya 2,060 za watu wasio na uwezo ili waandikishwe katika CHF.

  Katika uchangiaji huo Mh. Waziri Mkuu ambaye ni Mbunge wa Ruangwa alichangia usajili wa kaya 900 ambapo Mkuu wa mkoa wa Lindi Mh. Rugimbana alichangia kaya 100, RAS Lindi - kaya 100, DC Lindi - kaya 50, NHIF kaya 300, Mh. Waziri wa Habari na Mbunge wa Mtama - kaya 300, Mh. Lalinda Mbunge wa Viti maalum CUF - kaya 50, Mh. Hamida viti maalum CCM - kaya 60, Mh. Hamid Bohali Mbunge wa Mchinga - kaya 100, Mh. Kaunje Mbunge wa Lindi - kaya 100.
  Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Lindi akikabidhi kadi ya CHF kwa mnufaika mpya wa CHF Bw. Hassan Namangaya wakati wa Uzinduzi. 

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa CHF Bw. E. Mikongoti alisema mkoa wa LIndi una wanufaika 89,836 wa CHF ambayo ni asilimia 6.6 ya wana Lindi. Alihimiza Mkoa kuifanya CHF kuwa agenda katika utekelezaji mkoani hapo lakini pia kutumia vema fedha za uchangiaji ili kuboresha huduma za afya ili kuvutia wengi zaidi kujiunga na Mfuko huo. 

  Wakati akiwasilisha ripoti ya CHF mkoa wa Lindi, Mganga Mkuu wa mkoa Dk. Sonda alisema Lindi imefanikiwa kupata malipo ya Tele kwa Tele ya CHF ya SHilingi 109,436,000 kwa mwaka 2015 ambazo ni mchangi mkubwa katika kuboresha afya mkoani humo. Hata hivyo aligusia kusema bado wana changamoto ya hamasa ya watendaji kuhusu CHF.


  0 0  Airtel Mkwanjika tayari imeshawazawadia jumla ya watanzanzia 100 tangu ilipozinduliwa ambapo jana washindi wengine watatu kati ya saba wa Airtel toka mikoa ya Singida,Dodoma na Tabora, wamevuna fedha katika boxi la promosheni ya 'Airtel Mkwanjika' wakati Boxi la Mkwanjika lilipofika mkoani Dodoma kwa lengo la kuwazawadia washindi wake wa kanda ya Kati.

  Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando alisema hayo katika  droo iliyochezeshwa  mjini Dodoma jana kwa wateja  wa kanda  ya kati ambapo wateja wanne wameshindwa kufika licha ya kuambiwa watagharamikiwa kila kitu ikiwemo nauli, chakula na malazi ili waweze kufika kujizolea fedha lakini wamekuwa hawaamini na kuhofia kuwa inawezekana ni matapeli.
  Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akikabidhi shilingi 790,000 bw, kwa Elias Makani mshindi wa Airtel Mkwanjika ikiwa ni zawadi yake aliyojizolea katika boxi la Airtel Mkwanjika mkoani Dodoma jana, anaeshudia katikati ni Afisa Masoko kanda ya Kati bw, Hendrick Bruno. Promosheni ya Airtel Mkwanjika bado inaendelea ambapo hadi sasa tayari Airtel imeshawanyakua washindi 100 na kuwazawadia pesa taslim kila mmoja.

  "leo wateja wa Singida,Dodoma na Tabora,  ni zamu yenu kujizolea mapesa ya Airtel Mkwanjika, pia natoa wito kwenu wateja wa airtel mnapopigiwa simu za ushindi kwa namba ya Airtel 0683-442244 kutoa ushirikiano kwakuwa droo hiyo haina tozo ya aina yoyote laisema mmbando”.

  Mmbando alisema Airtel imetenga kiasi cha sh.milioni 300 kwaajili ya wateja wa Airtel na kila mmoja anaweza kushinda na mteja anachotakiwa kufanya ni kujiunga na kifurushi chochote cha yatosha au kuongeza salio kwa kutumia vocha na kuingizwa moja kwa moja kwenye droo ya siku bila makato yoyote.
  Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akikabidhi shilingi 910,000 kwa Bi Devota Fongonyo mshindi wa Airtel Mkwanjika ikiwa ni zawadi yake aliyojizolea katika boxi la Airtel Mkwanjika mkoani Dodoma jana, anaeshuhudia kulia ni mtangazaji wa kipindi cha mkwanjika Bw Godfrey Rugalabamu (gala B). Promosheni ya Airtel Mkwanjika bado inaendelea ambapo hadi sasa tayari Airtel im

  Alisema kila siku wateja wanne wa airtel wanavuta mkwanja katika promosheni hiyo na huchezeshwa kila baada ya siku saba za wiki na kutoa washindi 28.

  Alibainisha bado zaidi ya wateja 200 kushindaniwa  kwenye bado droo tisa zilizobaki ambazo zitawapa  fursa wateja wanne wa airtel kila siku kushinda kila mmoja hadi sh.milioni moja.

  Wakizungumza mara baada ya kujiokotea fedha katika droo hiyo, mshindi wa kwanza mkazi wa Dodoma,James Ryoba matiku, alisema ameweza kujipatia Shilingi laki tisa na elfu kumi ambazo zitamsaidia kuongeza mtaji katika biashara zake za nguo.

  Kwa upande wake, Mkazi wa Tabora, Devota Fongonyo, alisema awali alipopigiwa simu ya ushindi hakuamini na kuona kuwa ni matapeli lakini baada ya siku nne alipigiwa tena na akubali kufika Dodoma huku akiwa na hofu.

  Alisema katika droo hiyo amejipatia kiasi cha shilingi laki tisa na elfu thelasini ambazo zitamsaidia kulipa ada za watoto wake.


  Naye Mkazi wa Kongwa, Elias Makani, alisema amejipatia kiasi cha shilingi laki Saba na elfu tisini ambazo zitamsaidia katika shughuli zake za kilimo.
  Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando na mtangazaji wa kipindi cha mkwanjika Bw Godfrey Rugalabamu (gala B) wakwanza kushoto wakisaidiana kuhesabu hela na mshindi wa promosheni ya Airtel Mkwanjika mkoani Dodoma bw Rioba Matiku ikiwa ni zawadi yake aliyojizolea katika boxi la Airtel Mkwanjika mkoani Dodoma jana, Promosheni ya Airtel Mkwanjika bado inaendelea ambapo hadi sasa tayari Airtel imeshawanyakua washindi 100 na kuwazawadia pesa taslim kila mmoja.
  Afisa Masoko kanda ya Kati bw, Hendrick Bruno na Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando wakisaidiana kuhesabu hela na mshindi wa promosheni ya Airtel Mkwanjika mkoani Dodoma bw Rioba Matiku (wapili toka kushoto) pamoja na mtangazaji wa kipindi cha mkwanjika Bw Godfrey Rugalabamu (gala B) kulia ikiwa ni zawadi yake aliyojizolea katika boxi la Airtel Mkwanjika mkoani Dodoma jana, hadi sasa tayari Airtel imeshawanyakua washindi 100 na kuwazawadia pesa taslim.

  0 0

  Shehena kubwa ya Bidhaa Haramu ikiwemo Matairi,sukari,mafuta ya kupikia imekamatwa Bandari bubu Tanga kutokea Zanzibar. Operesheni hiyo imefanywa na Polisi 100 wakishirikiana na vyombo mbalimbali vya ulinzi na Usalama.
  Vyombo vilivyohusika katika usafirishaji wa shehena hiyo vyote vimetaifishwa. Walikuwa wanakwepa Kodi. 


  0 0

  Meneja wa Mradi wa Kansa ya Shingo ya Kizazi wa UMMATI, Jeremiah Makula akizungumza wakati wa utoaji tuzo kwa wadau wa mradi wa kansa ya Shingo ya Kizazi iliyofanywa, PSI Tanzania, Marie Stopes pamoja na UMATI iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Kanda Kusini Mwa Afrika, Ulla Muller akizungumza wakati wa utoaji tuzo kwa wadau wa mradi wa kansa ya Shingo ya Kizazi iliyofanywa, PSI Tanzania, Marie Stopes pamoja na UMATI iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Wakurugenzi wa Mashirika yaliyokuwa na Mradi wa Kansa ya Shingo ya Kizazi pamoja na wawakilishi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakifatilia maada wakati wa mkutano wa utoaji wa tunzo kwa wadau wa mradi iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

  Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii 
  WADAU wa wanaoshughulika na kansa ya shingo ya kizazi kwa wanawake ni wachache ikilinganishwa na mahitaji yaliyopo nchini kwa tatizo hilo. 

  Akizungumza katika mkutano wa wadau waliokuwa wakifanya Mradi wa Kansa ya Shingo ya Kizazi na Kinga kwa wanawake dhidi ya kansa hiyo, Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Neema Rusibamayilla amesema serikali inatambua juhudi za wadau ambao wamekuwa wakifanyia wanawake juu ya kinga ya kansa ya shingo ya kizazi. 

  Amesema serikali itaendelea kushirikiana wadau mbalimbali katika kukabili tatizo la kansa ya kizazi ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wanawake kujitokeza kupima afya zao na inapotokea na tatizo hilo kushughulikiwa kwa haraka. 

  Neema amesema serikali itaendelea kutoa ushirikiano zaidi kwa pale inapohitajika katika kukabili tatizo la kansa ya shingo ya kizazi kutokana na serikali peke yake haiwezi kushugulikia matatizo kwa wakati mmoja. 

  Nae Mkurugenzi Mtendaji wa UMATI, Lulu Ng’wanakilala amesema kansa ya kansa ya shingo ya kizazi inaua hivyo ni lazima wanawake kupima mara kwa mara kabla tatizo halijawa kuwa kubwa. 

  Amesema wadau wanaoshughulika na kansa hiyo ni wauchache ikilinanishwa na tatizo lilopo hasa katika maeneo ya vijijini ya kuwa na wanawake wengi ambao hawajafikiwa kwa kupima au kupata huduma hiyo. 

  Kwa upande wa Mkurugenzi Mkazi wa Marie Stopes ,Anil Tambay akiwakilisha wadau walikuwa katika mradi huo amesema mafanikio walioyapata katika mradi huo ni kwa kusaidia wanawake uhai katika utoaji wa tiba ya kansa ya shingo ya kizazi.

  0 0

  Hayati Padre Calisti Nauli Nyambo(pichani) ni mtoto wa tatu wa Familia ya hayati Baba Laurenti Ngasamiaku Nyambo na Mama Augustina Ngambakiha Msaki, alizaliwa tarehe 17/5/1939, katika Kijiji cha Kwamare Kirua Vunjo. Ndugu zake wa kuzaliwa ni Clementina, Martina, Beda, Damas, Adela, Eligi, Flora, Hilda, Domitila na Mary. Calisti alibatizwa na kupokea Sakramenti ya Ekaristi na Kipaimara katika Parokia ya Kirua.  

  ELIMU YA MSINGI
  Mwaka 1948 hadi 1953 alisoma katika Shule ya Msingi Iwa hadi darasa la sita. Kwakuwa wakati ule shule ya msingi Iwa ilikua na darasa la kwanza hadi la sita tu, Calisti aliendelea na masomo ya darasa la saba kule milimaniUsambara mwaka 1954 katika shule ya Msingi Gare. Mwaka 1955 aliendelea na masome ya darasa la nane katika Shule ya Msingi Kichwele (au Uhuru) katika Jimbo Kuu la Dar-es-Salaam.  

  ELIMU YA SEKONDARI
  Mwaka 1956-1957 Calisti aliendelea na masomo kidato cha kwanza na cha pili katika Shule ya Sekondari Umbwe.Alifuzu vizuri masomo yake akachaguliwa kujiunga na kidato cha tatu na cha nne katika Shule ya Sekondari yaPugu Dar es Salaam 1958 hadi 1959.

  WITO WA UPADRE
  Calisti aliongozwa na Roho Mtakatifu alijisikia kuitwa na kuvutwa na wito wa Upadre. Akaomba kujiunga na masomo ya Seminari kupitia Jimbo Katoliki Moshi. Mwaka 1960 hadi 1962 alijiunga na Seminari Kuu ya Kibosho.

  Baada ya kuhitimu masomo ya Falsafa, aliamua kukatiza masomo na malezi ya Seminari. Akaajiriwa kufanya kazi Benki na Serikalini. Kutokana na nguvu ya wito wa Upadre fedha za mshahara hazikutosheleza dhamira na malengo ya maisha yake ya kupenda kumtumikia Mungu.  Hivyo aliamua arudi Seminari kuendelea na safari yawito wa Upadre.

  Akaomba kujiunga na Jimbo Kuu la Dar-es-Saam. Mwaka 1966 alipelekwa kusoma Teolojia katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Paulo, Kipalapala Tabora. Mwaka 1969 alihitimu masomo na malezi ya seminari akapewa Ushemasi na mwaka huo huo tarehe 14 December 1969 akapewa sacramenti ya daraja la upadre na Mwadhama Cardinal Laurian Rugambwa na akawa padre wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam.

  UTUME WA UPADRE
  Kwa muda wa miaka tisa alifanya utume katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Alianza kama paroko msaidizi nabaadaye paroko katika parokia kadhaa za Jimbo Kuu la Dar es salaam. Tangu mwaka 1973 hadi 1976 aliteuliwa na  Mwadhama Kardinali Rugambwa kuwa Vikari  wa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es salaam. Kutoka Dar Es Salaam alifanya utume pia katika Jimbo Kuu la Arusha kwa muda mfupi kisha Mhashamu  Askofu Denis wa Jimbo la Arusha akamtuma Marekani kwa masomo ya Chuo Kikuu.

  MASOMO YA CHUO KIKUU
  Mwaka 1978 alienda Marekani akasoma katika Chuo cha Majesuiti kilichoko Berkeley, California, akatunukiwa Master Degree ya Teolojia mwaka 1982. Alipenda bado kujiendeleza ndipo alipoenda katika Jiji la Washington DC akasoma katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Amerika (Catholic University of America) na akafuzu vizuri akatunukiwa Master of Arts Degree in Religious Education mwaka 1987.

  UTUME NCHINI MAREKANI
  Padre Nyambo alikuwa padre wa kwanza mwafrika kufanya kazi katika jimbo la St. Petersburg, Florida, Amerika. Alianza kwa kufanya utume wakati wa kiangazi (Summer holidays) katika parokia ya Mt. Joseph 1982 na Parokia ya Utatu Mtakatifu (Blessed Trinity) mwaka 1986-1987.
  Askofu wa jimbo la St. Petersburg alifurahiwa na kuridhika na maisha na utendaji wa Padre Nyambo ndipo akampa utume kamili kama wakili paroko katika parokia moja katika jiji la Tampa, Florida mwaka 1988-1991. Wakati huo huo alikuwa Mkurugenzi wa jimbo wa utume wa Wakatoliki Waamerika Weusi katika jimbo la St. Petersburg.

  Mwaka 1992-1993 alikuwa Paroko Kiongozi wa parokia ya Mt. Peter Claver Tampa. Kwa kuwa alifanya utume wake vizuri alipewa cheo cha Uparoko tangu mwaka 1993-1997.

  Kwa muda wa miaka sita alikuwa Paroko katika Parokia ya Mt. Joseph St Petersburg, yaani, tangu mwaka 1997 hadi 2003. Mwaka huo huo wa 2003 alikuwa Paroko wa Parokia ya Watakatifu Wote (All Saints Parish) hadi mwaka 2013 alipostaafu kisheria.

  Pamoja na majukumu ya uparoko na ya Kijimbo, Padre Nyambo alikuwa raisi wa utume wa Waamerika Weusi Wakatoliki katika Mkoa wa Florida.  

  Alikuwa pia Mjumbe katika Bodi ya Kitaifa ya Wakleri Waamerika Weusi. Padre Nyambo alikuwa pia ni Raisi Mwanzilishi wa Wakatoliki Wakleri Weusi na Umoja wa Mashirika ya Kidini Amerika. Alikuwa pia Mwakilishi wa Kitaifa wa Utume wa Walei Amerika, Mshauri wa Kitaifa wa Shirikisho la Kitume la Watanzania kule Amerika, Mjumbe wa Bodi katika Ofisi za Utume wa Kichungaji kwa Wahamiaji, Wakimbizi na Wasafiri.

  Mwaka 2008 alitunukiwa tuzo ya heshima ya askofu mkuu Silvano Tomas kutokana na majitoleo na kazi nzuri kwa wahamiaji. Mwaka 2012 alitunukiwa tuzo ya mtumishi wa Kristu kutoka kwa Congress ya Kitaifa ya Wakatoliki Weusi wa Amerika.

  WASIFU WA PADRE KALIST NYAMBO
  Padre Kalist alikuwa mtu wa watu. Aliwapenda watu na hasa watu wa taifa lake. Alipenda na kuheshimu nyumbani alikozaliwa, alikokulia, kanisa alikobatizwa, kupata komunyo na kipaimara na shule Msingi ya Iwa alikosoma hadi darasa la sita. Ni miaka michache tu iliyopita alijenga vyumba vipya vya madarasa na vyoo katika shule ya Iwakama shukrani upendo kwa watu wa Kirua.
  Alipenda na kutamani sana kuona maendeleo mazuri ya taifa letu. Alipenda kufadhili miradi ya maendeleo hususan elimu na afya. Watu wote waliomfahamu na kumtembelea kule Marekani watashuhudia alivyokuwa akishirikiana vizuri na watu wote na hasa watanzania aliowafahamu kule Marekani. Alikuwa mchapakazi na mwenye furaha kila wakati.

  UGONJWA NA KIFO
  Mwishoni mwa Mwaka jana, masaa machache kabla ya mwaka mpya Padre Calist Nyambo alishikwa na ugonjwa wa kiharusi akiwa nyumbani kwake akiwa anajiandaa kwenda kufanya Ibada kesho yake ambapo alipelekwa Hospitali kwa matibabu zaidi huko nchini Marekani lakini jitihada za Madaktari Bingwa za kuokoa uhai wake hazikuzaa matunda. Ilipofika tarehe 3 Januari, 2016 Mungu aliyempenda sana Padre Calist Nyambo alimwita kwake akamshikirishe furaha za Ufalme wake.

  Ndugu wa marehemu na wanaukoo wote wa Nyambo wanatoa shukrani za kipekee kwa Uongozi wa Diocese ya St. Petersburg, Askofu Amani wa Moshi, Paroko, Watanzania wote wanaoishi USA pamoja na Madaktari kwa namna walivyoshiriki kwa hali na mali katika kufanikisha kuokoa maisha ya mpendwa wetu. Mungu awajalieni wingi wa Baraka na hasa afya ya roho na mwili. Asanteni sana. Taratibu za kuusafirisha Mwili wa Padre Calisti kutoka nchini Marekani kuja nchini Tanzania zinafanyika ambapo mazishi yanatarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii katika Kanisa Katoliki Kirua Iwa, Diocese ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

  Raha ya milele umpe ee Bwana na mwanga wa milele umwangazie. Ampumzike kwa amani. Amina.

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Generali Gaudence Milanzi (kulia) akizungumza na viongozi wa Kundi la Washirika wa Maendeleo katika sekta ya Mazingira, Maliasili na Mabadiliko ya Tabia Nchi (Development Partners Group on Environment, Natural Resources and Climate Change (DPG-E) walipoonana leo tarehe 19 Januari, 2016 katika ukumbi wa Selous uliopo makao makuu ya Wizara hiyo Mpingo House. Kundi hilo liliomba kuonana na Katibu Mkuu huyo kwa ajili ya utambulisho na kujadili mambo muhimu ya maendeleo katika sekta hiyo.
   
  Bi. Lena Thiede (kushoto) kutoka ubalozi wa Ujerumani ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Shirikisho la Kikanda Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kutoka Kundi la Washirika wa Maendeleo katika sekta ya Mazingira, Maliasili na Mabadiliko ya Tabia Nchi (DPG-E) akizungumza katika kikao hicho ambapo alielezea kazi ya Kundi hilo kuwa ni kuandaa mijadala maalum ya kisera na Serikali pamoja na wadau wengine wa maeneo husika, kuratibu miradi na mipango ya kundi hilo na kuhamasisha mawasiliano na utetezi wa pamoja baina yake na Serikali na wadau wengine katika sekta hizo. Katikati ni Bi. Clara Makenya kutoka UNEP ambaye ni Mratibu wa Kitaifa wa Kundi hilo na Bw. Steven Nyagondi Sekretarieti ya Kundi hilo. 
   
  Bwana Bernad Lubogo (kulia) Afisa Mipango Wizara ya Maliasili na Utalii akichangia jambo katika kikao hicho, Wengine ni Bi. Bertha Nyange (Katikati) Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mipango na Bw. Joseph Sendwa Afisa Utalii Wizara ya Maliasili na Utalii.
  Baadhi ya washiriki wa kikao hicho kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.
  (Picha na Hamza Temba - Kitengo cha Mawasiliano Serikalini - Wizara ya Maliasili na Utalii)

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wapili kushoto) akiwasili Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya kikazi. Wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Hassan Simba, kulia ni Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali, Pius Nyambacha. Katika hotuba yake, Rwegasira alilipongeza jeshi hilo kwa utendaji wa kazi mzuri na kulitaka liongeze kasi zaidi katika ukusanyaji wa mapato.
  Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali, Pius Nyambacha (kulia) akitoa taarifa ya utendaji wa Jeshi lake kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati) wakati Katibu Mkuu huyo alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake, Rwegasira alilipongeza jeshi hilo kwa utendaji wa kazi mzuri na kulitaka liongeze kasi zaidi katika ukusanyaji wa mapato. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Hassan Simba.


  0 0


  0 0


  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. 
  KUHUSU UPOTOSHWAJI WA TAARIFA ZILIZOANDIKWA NA GAZETI LA MWANAHALISI KUHUSIANA NA UCHAGUZI WA UBUNGE JIMBO LA  KIJITOUPELE


  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), inapenda kutaarifu Umma na Watanzania kwa ujumla kuwa Jimbo la Kijitoupele lililoko  Zanzibar ni miongoni mwa Majimbo hamsini(50) ambayo yalitegemewa kufanya uchaguzi mkuu tarehe 25, oktoba,2015. 

  Hata hivyo Jimbo hilo halikufanya uchaguzi wake wa Mbunge kutokana na hitilafu katika karatasi za kupigia kura badala Wapiga kura walishiriki katika kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano.


  Tume imefikia uamuzi wa kutoa ufafanuzi huu kutokana na taarifa iliyochapishwa na gazeti la MwanaHalisi toleo l Na.322 la Januari 18, 2016 katika ukurasa wake wa mbele likidai  “ NEC YAIBUA MAPYA” Habari hii si sahihi na inalenga kuupotosha umma na kuleta uchochezi miongoni mwa Wananchi.


  Kwa ujumla maelezo yote yaliyopo katika taarifa hiyo yanaeleza kwamba, Tume imeanzisha Jimbio jipya, kwa mujibu wa taarifa ya gazeti husika ni Jimbo la Kijitoupele – Zanzibar.


  Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda inasisitiza kuwa taarifa zilizotolewa na Gazeti la MwanaHALISI siyo za kweli, ni za uongo, uzushi, uzandiki na uchochezi. Kufuatia taarifa hiyo,Tume inapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:

  •          Tarehe 13 Julai, 2015 Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitoa taarifa kwa Vyombo vya Habari ikionesha Orodha ya Majimbo yatakayofanya uchaguzi wa Mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na Jimbo la Kijitoupele lipo katika Orodha hiyo. Taarifa hii ipo katika tovuti ya Tume.


  0 0


  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiambatana pamoja na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Elimu cha Kumbu kumbu ya Dr. Abdulrahman Al – Sumait wakiingia kwenye uwanja kwa ajili ya Mahfali ya 15 ya chuo hicho hapo Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Kulia ya Balozi Seif ambae alimuwakilisha Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein kwenye Mahafali hayo ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Hicho Dr. Abdulrahman Al - Muhailan na kushoto ya Balozi Seif ni Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho Profesa Hamed Rashid Hikmany.
   Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Elimu cha Kumbu kumbu ya Dr. Abdulrahman Al – Sumait wakiingia kwa maandamano kwenye uwanja kwa ajili ya kupewa stashahada zao.
    Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Elimu cha Kumbu kumbu ya Dr. Abdulrahman Al – Sumait, Dr. Abdulrahman Al – Muhailan akitoa salamu kwenye mahafali ya 15 ya chuo hicho hapo chukwani.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh:Abbas Kandoro akizungumza na Waandishi wa Habari hawapo Pichani nje ya Ukumbi wa Mkapa uliopo Sokomatola Jijini Mbeya katika Semina ya Wadau wa Elimu wa Mkoa wa Mbeya na Mkowa wa Katavi ambao wamekutana leo kuzungumzia juu ya Mbinu ambazo wanazitumia Mkoa wa Katavi kufanikiwa kufaulisha Wanafunzi kwa Asilimia kubwa kulinganisha na Mkowa wa Mbeya na Mikoa mingine.
  Kutoka Kushoto ni Afisa Elimu Mkoa wa Mbeya Ndugu,Charles Mwakalila na Afisa Elimu Mkoa wa Katavi Ndugu,Helenest Hinju akizungumza na Wadau wa Elimu Mkowa wa Mbeya na Katavi hawapo Pichani katika Semina ya Wadau wa Elimu iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Mkapa Jijini Mbeya.
  Baadhi ya Wadau wa Elimu Mkowa wa Mbeya na Katavi wakisikiliza kwa makini Semina hiyo ya siku mbili juu ya Mbinu za Ongezeko la ufauru kwa Dalasa la Saba Mkoa wa Mbeya.
  PICHA NA MR.PENGO GLOBU YA JAMII MBEYA.

older | 1 | .... | 1094 | 1095 | (Page 1096) | 1097 | 1098 | .... | 3278 | newer