Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

NGOMA AZIPENDAZAO ANKAL


WAZIRI MBARAWA AWATAKA MAKANDARASI MKOANI MTWARA KUKAMILISHA MIRADI YA UJENZI WA BARABARA KWA WAKATI

$
0
0
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amewataka makandarasi wanaojenga barabara za Mangaka-Mtambaswala KM 62.7 na Mangaka-Nakapanya Km 70,5 kukamilisha ujenzi huo ifikapo Juni mwaka huu.

Amewataka makandarasi hao kuongeza rasilimali watu na vifaa ili ujenzi huo ukamilike kama ilivyopangwa katika mkataba wa ujenzi wake.

“Hakuna muda utakaoongezwa nataka miradi yote miwili iwe imekamilika ifikapo juni mwaka huu tena iwe kwenye ubora unaowiana na thamani ya fedha,”amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Barabara hizo ambazo ujenzi wake kwa kiwango cha lami ulianza mwaka 2014 zitafungua fursa za kiuchumi mkoani Mtwara ikiwemo kuiunganisha Tanzania na Msumbiji kwa lami kupitia daraja la umoja lililoko Mtambaswala.

Akizungumza katika ziara hiyo Meneja wa Wakala wa Barabara TANROADS mkoa wa Mtwara Eng. AISHA SALIM amesema hawata kubali maombi yoyote ya kuongeza muda wa ujenzi wa barabara hizo ambapo ujenzi wa barabara ya Mangaka –Mtambaswala Km 62.7 unatarajiwa kukamilika mwezi Mei na ule wa Mangaka-Nakapanya KM 70.5 ukitarajiwa kukamilika mwezi julai mwaka huu.

Mapema Prof. Mbarawa alikagua hali ya barabara wilayani Ruangwa,Nachingwea na Masasi na kusisitiza kuwa ujenzi wa barabara na madaraja katika wilaya hizo utaendelea katika kipindi kifupi baada ya Serikali kuanza kutoa fedha kwa miradi inayotumia fedha za Mfuko wa Barabara (RFB).

Waziri Mbarawa yuko katika ziara ya mikoa ya lindi na mtwara kukagua miradi ya Barabara,Mawasiliano na Bandari ili kuona ufanisi uliopo katika sekta hizo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Profesa Makame Mbarawa akipokea taarifa ya Ujenzi wa barabara ya Mangaka-Mtambaswala (KM 62.7), kutoka kwa Mhandisi Mkazi Anold Msengezi (Katikati) anayesimamia ujenzi wa barabara hiyo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Wa kwanza kulia) akipokea taarifa ya Ujenzi wa barabara ya Mangaka –Nakapanya (KM70.5) kutoka kwa Mhandisi mkazi Dkt.Chaurasia inayojengwa na kampuni ya Jiangxi Geo Engineering (Group) Cooperation ya China.
Sehemu ya barabara ya Mangaka –Mtambaswala (KM 62.5) ambayo Ujenzi wake unaendelea kwa kiwango cha lami.

JAMES KATORO AWASHUKURU WAKAZI WA KATA YA KAYENZE MANISPAA YA ILEMELA KWA MAAMUZI YAO

$
0
0
Wazee wakimsimika James Katoro baada ya kuchaguliwa kuwa Diwani wa Kata ya Kayenze katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza.

Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG 



Katoro alichaguliwa kuwa diwani wa Kata hiyo katika uchaguzi uliofanyika Novemba 25,2015 kupitia Chama cha Mapinduzi CCM. Tukio hili limejiri jana katika Mkutano wa hadhara wa CCM kuwashukuru wakazi wa Kata hiyo kwa kumchagua Katoro kuwa diwani wa Kata hiyo.
Wazee wakimsimika James Katoro baada ya kuchaguliwa kuwa Diwani wa Kata ya Kayenze katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza. 
Mchungaji Elias Lutalamamila (wa pili kulia) kwa niaba ya viongozi wa dini akimsimika James Katoro baada ya kuchaguliwa kuwa Diwani wa Kata ya Kayenze katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza. 

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

WAZIRI MKUU, MAJLIWA AMWAKILISHA RAIS MAGUFULI MKUTANO WA SADC GABORONE

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wa Botswana, Bw. Tshenolo Mabeo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sir Seretse Khama uliopo Gaborone Januari 17, 2016. Majaliwa amemwakilisha Rais John Magufuli katika Mkutano wa SADC.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Katibu Mtendaji wa SADC,Dkt, Srergomena Tax mjini Gaborone ambako Mheshimiwa Majaliwa anamwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano wa SADC Januari 17, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TMAA YAKAMATA MADINI YAKITOROSHWA JNIA

$
0
0
Teresia Mhagama na Mohamed Saif

Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege na Usalama wa Taifa wamekamata madini yenye thamani ya jumla ya shilingi milioni 11.2 ambayo yalikuwa yakitoroshwa kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA). 

Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano  wa  TMAA, Mhandisi Yisambi Shiwa ambapo alieleza kuwa raia mmoja wa kigeni na mwingine wa Tanzania walikamatwa wakiwa na madini hayo bila kuwa na kibali chochote cha usafirishaji kama ambavyo Sheria ya Madini ya mwaka 2010 inavyoelekeza.

“ Raia huyu wa kigeni ambaye jina lake linahifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi kwani tayari ameshafunguliwa kesi mahakamani, alikuwa anasafiri kwenda mji wa Bangkok Thailand na alikamatwa akiwa na madini ya aina mbalimbali ikiwemo almasi, aquamarine, sapphire, green tourmaline, quartz na rhodolite,” alisema Mhandisi Shiwa.

 Aidha, Mhandisi Shiwa alisema kuwa katika tukio la pili mtuhumiwa mwingine raia wa Tanzania ambaye alikuwa anasafiri kwenda Ujerumani alikamatwa akiwa na madini mbalimbali ikiwemo amethyst, moonstone cabochon, rulilated quartz (cabochon), rulilated quartz(faceted), chrysoprase, green tourmaline, rubi, red garnet, green quartz, zircon na rhodolite na kufikishwa katika vyombo vya Dola.

Alisema kuwa katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai mwaka 2015 hadi Januari 13 mwaka huu kumekuwepo na jumla ya matukio 14 ya utoroshaji madini ambapo madini yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 1.4 (zaidi ya Shilingi Bilioni 3.2) yalikamatwa na wakaguzi wa Wakala kupitia Madawati ya Ukaguzi yaliyopo katika viwanja vya ndege vya Dar es Salaam (JNIA), Kilimanjaro (KIA) na Mwanza ambapo yote yalitaifishwa na Serikali. 

Mhandisi Shiwa ametoa rai kwa Umma kujiepusha na shughuli za utoroshaji na biashara haramu ya madini kwani hatua kali zitaendelea kuchukuliwa kwa yeyote atakayebainika au kukamatwa akijihusisha na shughuli hizo ikiwemo kutaifisha madini yaliyokamatwa.

Vilevile Mhandisi Shiwa alisema kuwa  Serikali kupitia  Wizara ya Nishati na Madini inatoa motisha kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa kwa Kamishna wa Madini ama Wakala za utoroshaji/magendo na biashara haramu ya madini ambazo zitawezesha ukamataji wa madini, atazawadiwa fedha taslimu ambazo ni asilimia 5 ya thamani ya madini yatakayokamatwa na kunadiwa.

JANET MWENDA NA MARAFIKI ZAKE WA "MENTORING AND NETWORKING" WATOA MSAADA KWA KITUO CHA WATOTO WETU TANZANIA

$
0
0
Bi. Janet Sosthenes Mwenda (wa pili kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania, Bw. Evans Tegete moja ya vitu vilivyowasilishwa kwenye kituo hicho ndoo ya sabuni ya unga. Kushoto ni Muhamasishaji na mchangishaji fedha wa “Mentoring and Networking”, Bi. Mary Sanga na wengine wanaoshuhudia ni watoto wa kituo hicho. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).


Mmiliki na Mwendeshaji wa kipindi cha ‘Ongea na Janet’ Bi. Janet Sosthenes Mwenda ambaye pia ni mmiliki wa programu maalum ya vipindi vya watoto katika kutoa elimu katika televisheni kiitwacho ‘Tuwalinde Watoto Wetu’ kwa kushirikiana na marafiki zake wa kundi la “Mentoring and Networking” kupitia mitandao ya kijamii wametoa misaada mbalimbali ya vyakula na vinywaji kwa kituo cha Watoto Wetu Tanzania.

Akizungumza wakati wa kutoa misaada hiyo mapema jana 17 Januari, wakati wa tukio hilo lililofanyika kwenye kituo hicho kilichopo Kimara jijini Dar es Salaam, Janet Mwenda ambaye aliambatana na baadhi ya marafiki zake hao wa “Mentoring and Networking” wameweza kutoa misaada hiyo ya vyakula, vinywaji ambavyo vitasaidia kituo hicho.

“Kwa kuja hapa kutoa msaada huu ni kutokana na kuguswa na hali ya watoto wanaolelewa hapa na kwingineko kote. Naamini msaada huu utasaidia watoto wetu hapa kituoni naamini kwa hiki kidogo kitasaidia kwa siku kadhaa” alieleza Janet Mwenda.

Janet Mwenda ameongeza kuwa, amekuwa akifikiria zaidi kutoa misaada hivyo kufika hapo ni kutokana na kuguswa kwake kwa muda mrefu na amekuwa pia akitembelea kituo hicho kipindi cha nyuma hivyo kuwa miongoni mwa wanafamilia.

TANZIA

$
0
0
Mwandishi wa Kitabu cha "Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe" na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Edwin Semzaba amefariki dunia jana jioni. Taarifa kamili itawajia baadae.

TANZIA: GEORGE SEBO MWENYEKITI WA CCM DMV HATUNAE TENA

$
0
0
Aliyekuwa Mwenyekiti tawi la CCM DMV 
 Ndg. George Sebo enzi za uhai wake.
mwenyekiti wa CCM DMV  Ndg. George Sebo  amefariki Dunia muda si mrefu Katika hospitali ya  Prince George's Hospital Center, Maryland, Marekani. Taarifa zaidi zinakujia hivi punde.

MISA YA KUMBUKUMBU YA MAREHEMU LETICIA NYERERE

$
0
0
Misa ya kumbukumbu ya marehemu Leticia Nyerere iliyofanyika siku ya Jumamosi January 16, 2016 katika kanisa la Mt. Edward Baltimore, Maryland na kuhudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki kutok kila kona ya Marekani. Mwili wa marehemu Leticia Nyerere unatarajia kufika Tanzania kesho Jumanne January 19, 2016 na utaagwa Dar es Salaam na mazishi yake yanatarajiwa kufanyika Butiana. Picha na Iska Jojo.
Wana familia wakifuatilia misa ya kumbukumbu ya marehemu Leticia Nyerere iliyofanyika siku ya Jumamosi January 16, 2016 katika kanisa la Mt. Edward Baltimore, Maryland nchini Marekani. Kutoka kushoto ni Bi. Kijogoo kutoka Arizona,,Margareth Mageni na ,Flora Mageni
Wanafamilia wakiwemo watoto wa marehemu kutoka kushoto ni Julius Nyerere, Helena Nyerere na Julia Nyerere kulia ni Edlaila  Nyerere ambaye ni wifi wa marehemu kutoka Atlanta jimbo la Georgia nchini Marekani  wakifuatilia misa ya kumbukumbu ya mpendwa mama yao Leticia Nyerere aliyeaga Dunia siku ya Jumapili January 10, 2016 katika hospitali ya Jumuiya ya Madaktari iliyopo Lanham, maryland nchini Marekani.

Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi akitoa mkono wa pole kwa mume wa marehemu Madaraka Nyerere kwenye misa ya kumbukumbu  ya marehemu Leticia Nyerere iliyofanyika siku ya Jumamosi January 16, 2016 katika kanisa la Mt. Edward Baltimore, Maryland na kuhudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki

Balozi Wilson Masilingi akiongea machache na kutoa pole kwa wafiwa.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman Said azikwa leo jijini Dar

$
0
0
 Sehemu ya Waombolezaji wakiwa wamebeba Jeneza lenye mwili wa aliekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman Said Suleima, wakati wakiwasili kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam leo kwa ajili ya mazishi.
Sehemu ya Waombolezaji wakiwa kwenye Mazishi ya aliekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman Said Suleima, yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es salaam.

SIMUTV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

$
0
0

SIMU.TV:  Burundi kuwekwa kitimoto na kamati ya jumuiya utatuzi wa migogoro ya jumuiya ya  Afrika mashariki tarehe  25 kujadili; https://youtu.be/8Y8ogiUZjGQ
 SIMU.TV:  Wakazi wa Malami Tabora wamtumia salamu waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mh.Lukuvi  juu ya migogoro ya ardhi mkoani humo;https://youtu.be/nB1gxdsx9Js
 SIMU.TV:  Jeshi la polisi kuendelea kutoa elimu ya usalama wa barabarani sambamba na ukaguzi wa magari na vyombo vya moto; https://youtu.be/d8VhATK9f_w
 SIMU.TV:  Baada ya kaulimbiu ya rais Magufuli ya elimu bure kuanza kutekelezwa nchini, wadau wa elimu wamepata chachu ya kuanza kuboresha   miundombinu ya shule; https://youtu.be/V9W1x07G3m8
 SIMU.TV:  Wafanyakazi wa vikundi vya kujitolea katika manisapaa Zanzibar wapaza sauti zao kwa Mh. Haji Kheri juu ya changamoto katika kazi zao;https://youtu.be/svCwuqs1uzU
 SIMU.TV:  Upungufu wa makocha wawa changamoto kubwa kwa shirikisho la soka nchini katika kukuza vipaji vichanga; https://youtu.be/WxhBh9wjZtQ
 SIMU.TV:  Uwepo wa mabango ya waganga wa jadi wakinadi sifa zao za kutuibu maswala y ngubvu ya kiume inaonesha ukubwa wa tatizo hilo katika jamii;https://youtu.be/mCwix2CL0RM
 SIMU.TV:  Fahamu mambo mbalimbali yanayohusishwa na urukaji wa hatua za ukuwaji kwa binadamu; https://youtu.be/C11WGbVI3lU
 SIMU.TV:  Fahamu umuhimu wa kufanya mazoezi kwa mwili wa binadamu na njia sahihi za kuboresha afya yako; https://youtu.be/A8LYMSCSdXU

DC AWATAKA MADIWANI WASHIRIKIANE KUMALIZA MIGOGORO WILAYANI SIMANJIRO

$
0
0
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Lucas Mweri akizungumza juzi kwenye baraza la madiwani wa wilaya hiyo (katikati) ni Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Jackson Sipitieck na Makamu Mwenyekiti Albert Msole.  
Diwani wa Kata ya Ruvu Remit Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Alamayani Ranga akisoma taarifa kwenye baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo juzi juu ya uboreshaji wa huduma za jamii

Na Woinde Shizza, Arusha
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona amewataka madiwani wa kata 18 za wilaya hiyo kushirikiana na maofisa watendaji wa vijiji vyao kuhakikisha migogoro inakwisha.
Kambona aliyasema hayo juzi wakati akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo na kuagiza mipaka ya vijiji na vitongoji vya miji midogo ya Orkesumet na Mirerani izingatiwe kwa kupimwa.
Alisema kila diwani akishirikiana na maofisa watendaji wa vijiji wataweza kumaliza migogoro hiyo na maeneo ya kilimo na mifugo yabainishwe na kuhakikisha suala la mifugo kuzagaa likomeshwe ikiwemo punda na ng’ombe.
“Mifugo inazagaa ovyo na kuharibu mazao, lidhibitini hilo kwa kutumia kanuni ndogo zetu, kwani mifugo inaachiwa sana na ukitembelea sehemu nyingine unakuta punda wanaingia hadi kwenye madarasa ya shule,” alisema Kambona.
Pia, Kambona amemuagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Lucas Mweri kuwapangia wakuu wa idara, vitengo na watumishi wengine wawe walezi wa kata mbalimbali ili wawe wanazitembelea na kutoa ushauri.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro Jackson Sipitieck alisema hivi sasa madiwani na watumishi kwa pamoja wanatakiwa kujipanga kikamilifu ili kuhakikisha wananchi wa kata za eneo hilo wanapatiwa maendeleo.
“Tujipange kikamilifu kwa pamoja na kuhakikisha kuwa wananchi wetu wanapata huduma stahiki, kwani sisi tulichaguliwa kwa ajili ya kutumikia jamii ya Simanjiro ili wapate maendeleo kwenye sekta mbalimbali,” alisema Sipitieck. 

WAZIRI MKUU MAJALIWA AMWAKILISHA MAGUFULI MKUTANO WA SADC

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Katibu Mtendaji wa SADC,Dkt, Srergomena Tax mjini Gaborone ambako Mheshimiwa Majaliwa anamwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano wa SADC Januari 17, 2016. Katikati ni Balozi wa Tanzania Nchini Afrika ya Kusini na Botswana 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wa Botswana, Bw. Tshenolo Mabeo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sir Seretse Khama  uliopo  Gaborone Januari 17, 2016. Majaliwa amemwakilisha Rais John Magufuli katika Mkutano wa SADC. 

BONDIA FRANCIS CHEKA AJICHIMBIA NCHINI ZAMBIA KUTAFUTA MBINU ZA KUMCHAPA MUINGEREZA

$
0
0
Bondia wa Kimataifa, Francis Cheka anaendelea kujinoa vizuri nchini Zambia, kujiandaa Mpambano wake dhidi ya mpinzani wake kutoka nchini Uingereza, GEARD Ajetovic katika pambano lao la marudiano, linalotarajiwa kufanyika Februari 27, 2016 kwenye Viwanja vya Leaders Club, Jijini Dar es salaam.

Cheka ambaye alipoteza mchezo wa awali kule jijini Manchester nchini Uingereza, sasa amejipanga vyema kumkabili mpinzani wake katika ardhi ya Tanzania.

Cheka anaendelea kujifua chini ya Kocha mpya kutoka nchini South Africa akishirikiana na Kocha kutoka Zambia.

TAMKO LA SERIKALI KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI


introducing hit single "Pole Pole" by Sweet Flavour

$
0
0
Mpaka hivi sasa kumekua na so many short video clips za watu mbali mbali zilizo sambaa sana sana mitandaoni wakiji record huku wakiimba nakutumiana wimbo wa Pole Pole ulioimbwa na vijana wapya katika tasnia hii ya Music. Vijana hawa wenye sauti yakubembeleza wanaoitwa Sweet Flavour wamekua nitishio sana kwa wengi kutokana na vile wimbo wao ulivyoweza kusambaa kama umeme mitandaoni.
Kwa muda mchache tu baada ya wimbo huu kudakwa na moja kati ya watu waliotembelea studio za Kaburu Records nakuutuma kwa mwenzake na mwenzake pia kwa mwenzake wimbo huu umekua ukisambaa kwa kasi sana nakuinua maswali mengi kwa wapenzi wa Music.

Wengi wamekua wakitaka kuwajua zaidi vijana hawa wenye sauti zakuwavutia na kuwaburudisha wengi haswaa wakina dada mpaka kuwapelekea kuushika wimbo huu kwa kipindi kifupi tu na hapa ndipo utakapo pata nafasi yakuwajua Sweet Flavour.
Sweet Flavour ni kundi la vijina wawili toka Kaburu Entertainment wakiwa kama label na kusimamiwa kazi zao zote hapo chini ya Kaburu Entertainment. Vijana hawa T More na Singano huu ni wimbo wao wa kwanza kabisa na umeonyesha neema kubwa baada yamashabika kuupokea vyema. Wimbo umefanyika Kaburu Music Studio chini ya Producer Father Beat a.k.a Kona nakusimamiwa na CBH a.k.a Sampa Music King.
Zaidi na zaidi wimbo huu wenye melody yakuto toka kichwani pindi ukiusikia, vijana hawa wameweka kilio chao chote ndani ya mapenzi nakulalamika juu ya mapenzi yanayowatesa wengi huku bado wakijishusha kinyonge! Wamejaribu kuwakilisha kila chozi la mnyonge wamapenzi nakumfanya kila mtu aguswe nakuhisi wimbo huu ni sahihi kumtumia mpenzi wake.
Sio maneno tu! Sikiliza wibo huu hapa alafu utajua nikipi kimeupa nafasi yamkupenya na kupendwa na watu wengi.
For Booking, shows and Interviews check with kaburu Entertainment +255717969666
Follow them on Instagram: @sweet_flavourtz or @kaburu_ent or @cbhhalawa

Thanks

Warning for heavy rains/Tahadhari ya mvua kubwa 18/01/2016 - 20/01/2016.

TEASER JOTO LA ASUBUHI JUMANNE JANUARY 19, 2016

Ngoma azipendazo ankal

Ommy Dimpoz alivyorushwa kichura na Wanajeshi pale Lugalo.

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images