Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1092 | 1093 | (Page 1094) | 1095 | 1096 | .... | 3278 | newer

  0 0


  0 0

  Baadhi ya Askari jeshi la Polisi wa kikosi usalama barabarani wakiongozwa na Msaidizi wa meneja miradi ya Tehama ndani ya Jeshi la Polisi hilo, Inspekta Bakari Mwamgugu (kushoto) wakiwafuatilia taarifa za magari ambayo madereva wake wamekwisha fanya makosa mbalimbali wakati wa zoezi la ukaguzi na ulipaji wa faini mbalimbali jijini Dar es Salaam Januari 15 2016.
  Msaidizi wa meneja miradi ya Tehama ndani ya Jeshi la Polisi Tanzania, Inspekta Bakari Mwamgugu akiweka alama ya kituo cha ukaguzi wakati mbele ya kamera maalum ya kuchukuwa taarifa za magari ambayo madereva wake wamekwisha fanya makosa mbalimbali wakati wa zoezi la ukaguzi na ulipaji wa faini mbalimbali jijini Dar es Salaam Januari 15 2016.
  Polisi wa usalama barabarani Happy Kataraia na Msaidizi wa meneja miradi ya Tehama ndani ya Jeshi la Polisi Tanzania, Insp Bakari Mwamgugu wakiweka sawa kamera ya kuchukuwa taarifa za magari ambayo madereva wake wamekwisha fanya makosa mbalimbali wakati wa zoezi la ukaguzi na ulipaji wa faini mbalimbali jijini Dar es Salaam Januari 15 2016. 
   Na Mwandishi Wetu. 
    Kikosi cha Usalama Barabarani kimefanikiwa kuwalipisha faini madereva na wamiliki wa vyombo vya moto hususani magari kwa asilimia 49 kwa kutumia mfumo kutumia mfumo mpya maalum wa taarifa za kielekroniki jijini Dar es Salaam. 
  Mfumo huo unasimamia sheria za usalama barabarani kwa njia ya kieletroniki sambamba na ukusanyaji wa tozo za makosa ya barabarani kwa njia ya kieletroniki. 
  Kwa kutumia mfumo huo jeshi la polisi limefanikiwa kuyakamata magari ambayo yana makosa mbalimbali yakiwemo ya TRA na SUMATRA. Pia mfumo unatambua na kuwabaini wale wote ambao hawajalipia faini za makosa yao ya usalama barabarani Kwa kutumia kamera maalum ya kuwabaini..
  Mkaguzi wa Polisi wa Kikosi hicho, Bakari Mwangungu alisema jana kuwa kwa kutumia mfumo huo huduma za usalama barabarani zimeendelea kuboreshwa na kufanikiwa kuwalipisha faini madereva na wamiliki wa magari waliokuwa na mtindo wa kukwepa ama kuchelewa kulipia faini hizo kwa wakati kwa mujibu wa sheria za usalama barabarani. 
  Zaidi ya makosa 12,000 yamelipiwa faini kwa kutumia mfumo huo ambapo asilimia 51 hayajalipwa na zoezi la ukaguzi linaendelea kuhakikisha wale wote wenye makosa na wanaendelea kutenda makosa ya usalama barabarani wataendelea kuchukuliwa hatua ili kuhakikisha madereva wanaendelea kuwa na nidhamu na kujirekebisha ili kuongeza umakini wawapo barabarani. 
  Alisema wananchi wanashindwa kuelewa swala la adhabu za makosa wa wanalipia nusu nusu na kwa kuwa mfumo autambui na hivyo kurudisha fedha kwa mlipaji mpaka atakapolipia kiasi kamili ndipo mfumo utamtambua na kumpatia risiti.  
  Inspector Mwangungu amewatahadharisha wananchi kutokosea namba za kumbukumbu wafanyapo malipo ili kuepuka usumbufu utakaosabishwa na kurudishwa ama kukamilisha malipo ya faini zao. 
  Ameongeza kwamba zoezi hilo ni endelevu na linasaidia kupunguza kero ya risiti kwani kwa kutumia mfumo wanazipata moja kwa moja kwenye mtandao. 
  Pia amebainisha faida za mfumo huo kuwa ni pamoja na kuongeza wigo wa wananchi wa kutumia Tigo Pesa, Airtel Money na M-pesa ambapo amewatahadharisha kutosubiri mpaka muda wa siku saba za faini kupita ili kuepusha usumbufu wa kulipia faini pamoja na faini ya uchelewashaji wa malipo. 
  Mfumo huo ulizinduliwa Disemba mwaka jana na umeonesha mafamanikio makubwa kwa kuongeza makusanyo ya malipo ya serikali pia kuwarahisishia wananchi kuepusha usumbufu wa kupewa risiti kama zamani ambapo ilibidi wakamilishe kwa kufiki vituo vya polisi.  

  0 0

  WANAFUNZI 538 wa chuo cha Mamlaka ya Mapato (TRA) wametunukiwa vyeti vyao leo katika mahafari ya nane ya chuo hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.

  Pia wahitimu hao wameaswa kuwa waadilifu katika kazi zao kwani taaluma yao ni ukusanyaji wa mapato ya sehemu zao za kazi. 

  Wameaswa hayo na Naibu waziri wa Fedha na Mipamgo, Ashatu Kijaji wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa mahafari ya nane ya chuo cha Mamlaka ya Mapato (TRA) yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere. 

  amesema kuwa wahitimu wa chuo hicho wafanye kazi kwa weredi na uaminifu kwani wasipofanya hiyo hawataweza kufanya kazi hayo vile inavyopaswa. 

  Chuo cha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kitajengwa kingine huko kibaha mkoani pwani ili kuongeza wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri kwani chuo kilichopo Mwenge kimezungukwa na viwanda. 
  Naibu waziri wa Fedha na Mipamgo, Ashatu Kijaji akizumgumza na wahitimu wa chuo cha Mamlaka ya mapato Tanzania TRA leo katika mahafari ya nane ya chuo hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere leo jijini Dar es Salaam
  Makamu Mkuu wa Chuo, Lewis Ishemoi akiwaita majina wanafunzi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) leo katika mahafari ya nane ya chuo hicho ikiwa wahitimu 538 wamehitimu mafunzo yao katika chuo hicho jijini Dar es Salaam leo.Wahitimu wakivaa kofia zao mara baada ya kutunukiwa katika mahafari yaliyofanika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
  Wahadhiri wakiwitunukiwa vyeti pamoja na zawadi mbalimbali katika mahafari ya nane ya chuo cha mamlaka ya mapato (TRA) leo jijini Dar es Salaam. kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Alphayo Kidata na Makamu Mkuu wa Chuo, Lewis Ishemoi.
  Wahitimu wa Mahafari ya nane ya chuo cha Mamlaka ya Mapato (TRA) leo jijini Dar es Salaam.
  Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

  0 0

   Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana  na Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Iddi  kabla ya mazungumzo yao Ofisini kwake jijini Dar es salaam 
  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majalaiwa akizungumza  na Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Iddi, ofisini kwake jijini Dar es salaam Januari 16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0


  SIMU.TV:  TANESCO yazoa zaidi ya shilling milioni 20 baada kufanya msako wa wezi wanaolihujumu shirika hilo la umeme; https://youtu.be/WF_42psYtAc
   SIMU.TV:  Waliovamia eneo la hifadhi la wazee eneo la Nyungwe Kigamboni wapewa siku 21 kuboa nyumba zao na kuhama maeneo hayo; https://youtu.be/fGuqPTKDC2s
   SIMU.TV:  Wakazi wa vijiji vya Chalinze wanalazimika kutumia maji ya kwenye malambo ya kunyweshea mifugo kutokana na ukosefu wa maji safi na salama;https://youtu.be/DB6GcxSZXgc
    SIMU.TV:  Klabu ya Simba yaigomea Etoile Du Sahel kulipa kwa awamu ada ya uhamisho wa mchezaji Emmanuel Okwi; https://youtu.be/SRxE_UJADmk
   SIMU.TV:  Vigogo wa mamlaka ya bandari warudishwa wizarani huku nafasi zao zikichukuliwa na watumishi wengine; https://youtu.be/crvziUux9KQ
   SIMU.TV:  Mgogoro kati ya wafanyabiashara na halmashauti ya Nzega wafikia tamati kwa kusainishana mikataba na kuwataka wafanyabiashara hao kulipa ushuru;https://youtu.be/idxZ2T0A0YE
   SIMU.TV:  Makampuni za uchimbaji madini ya Tanzanite 24 yaingia matatani kwa uharibifu wa miundombinu ya umeme;

  0 0
 • 01/16/16--08:13: TAARIFA YA MSIBA
 • FAMILIA YA MAREHEMU  HUSSEIN CHOMBA WA MWENGE DAR ES SALAAM, INASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA DADA YAO MPENDWA JAMILA HUSSEIN CHOMBA KILICHOTOKEA TAREHE 16/01/2016 SAA  8:30 KATIKA HOSPITALI YA HINDU MANDAL, DAR ES SALAAM. 
  MAZISHI YATAFANYIKA LEO  TAREHE 17/01/2016 SAA 10:00 JIONI KATIKA MAKABURI YA SINZA. HABARI ZIWAFIKIE NDUGU JAMAA NA MARAFIKI POPOTE WALIPO. 
  KWA TAARIFA ZAIDI ZA MSIBA HUU TUMIA NAMBA HII KWA MAWASILIANO. +255715297308

  0 0
 • 01/16/16--19:00: NGOMA AZIPENDAZO ANKAL
 • KINYAMA NYAMA HICHO-THE KILIMANJARO BAND WANA NJENJE

  0 0

  Kampuni ya Koyo Corporation ya nchini Japan imeonesha nia ya kuwekeza nchini katika uzalishaji wa umeme kwa kutumia gesi asilia.

  Hayo yameelezwa jana jijini Dar es Salaam katika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini kwenye kikao cha Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Noria Shoji ambaye alifika wizarani hapo na ujumbe wake ili kujadili fursa za uwekezaji nchini hususan katika ufuaji umeme kwa gesi asilia.

  Waziri Muhongo aliueleza ujumbe huo kwamba fursa za uwekezaji kwenye nishati hususan katika uzalishaji umeme kwa kutumia gesi asilia ni nyingi na hivyo Serikali inakaribisha wawekezaji wa ndani na nje.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akimsikiliza Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Koyo Corporation ya Japan, Norio Shoji wakati wa kikao cha kujadili fursa za uwekezaji nchini.

  Alisema wawekezaji wanakaribishwa kujenga mitambo ya kufua umeme kwenye maeneo mbalimbali ambapo kuna matoleo ya gesi asilia na huku akiyataja maeneo hayo kuwa ni Mtwara, Lindi, Somangafungu na Mkuranga.

  Waziri Muhongo alisema gesi asilia iliyogundulika ni ya kutosha kuzalisha umeme mwingi na hivyo wawekezaji wenye nia ya kuwekeza kwenye ufuaji wa umeme kwa kutumia gesi asilia wanakaribishwa.

  Awali, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo ya Koyo, Norio Shoji alisema lengo la ujio wake na ujumbe alioongozana nao, ni kutafuta ukweli wa mambo kuhusiana na masuala ya uwekezaji kwenye uzalishaji umeme kwa kutumia gesi asilia.
  Wajumbe wa mkutano baina ya Wizara ya Nishati na Madini na Kampuni ya Koyo Corporation ya Japan ukiongozwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati).


  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concepts, Juma Pinto  (kushoto), akimuelezea Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Richard Mwaikenda kuwa wakati gazeti la Jambo Leo lilipoanzishwa 2009, alikuwa mfanyakazi wa kwanza kujiunga na gazeti hilo akitokea Kampuni ya Business Times.
   Baadhi ya wafanyakazi wa  Gazeti la Jambo Leo na familia zao, wakigongeana glasi zenye vinywaji ikiwa ni ishara ya kutakiana heri wakati wa hafla ya kuuaga mwaka 2015 na kuukaribisha ya Mwaka Mpya 2016, katika Mgahawa wa City Sports Lounge, Dar es Salaam
   Wafanyakazi wa Jambo Leo na familia zao pamoja na wageni waalikwa wakiburudika kwa muziki uliokuwa ukiporomoshwa wakati wa hafla hiyo iliyofanyika kwenye Mgahawa wa kisasa wa City Sports Lounge, katikati ya Jiji la Dar es Salaam.


  0 0

   Meneja wa kinu cha kuchenjua dhahabu wa Mgodi wa Buzwagi Festo Shayo (wa kwanza kulia) akitoa maelezo kwa Naibu waziri ofisi ya makamu wa rais anaeshughulikia mazingira na Muungano, Luhaga Mpina namna mgodi wake unavyohifadhi maji yaliyotumika kusafishia dhahabu.

  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Luhaga Mpina, ameupongeza Uongozi na wafanyakazi wa Mgodi wa Buzwagi kwa kuzingatia sheria za mazingira Mgodini hapo.

  Pongezi hizo alizitoa wakati alipofanya ziara ya kushitukiza katika Mgodi huo kwa lengo la kujionea namna mwekezaji huyo anavyozingatia maelekezo ya wataalamu wa wizara yake juu ya utunzaji wa mazingira.

  Akiwa katika ziara hiyo Naibu Waziri huyo alitembelea bwawa maalumu kwa ajili ya kuhifadhia maji yalitumika kuchenjulia dhahabu na kujionea namna ambavyo mgodi huo unavyochukua tahadhari ya hali ya juu katika kuhakikisha maji yanayohifadhiwa ndani ya bwawa hilo hayawezi kuwa na madhara kwa Jamii, pia naibu Waziri huyo alitembelea kituo cha udhibiti taka, Uwanda wa kuvuna maji ya mvua mgodini hapo pamoja na karakana ya mgodi huo.
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira na Muungano Luaga Mpina (wa kwanza kushoto), akisikiliza maelezo ya Afisa Mazingira wa Mgodi wa Buzwagi bwana Frank Ngoroma (wa kwanza mkono wa kulia), aliyesimama katikati ni meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo.

  “Bwawa hili kama unavyoliona usanifu wake, umezingatia tahadhari zote kuhakikisha hakuna maji yoyote yanatoka nje na hasa ukizingatia maji yanayopatikana hapa ni yenye mchanganyiko wa madawa yanayotumika kuchenjua dhahabu” Alisema Meneja wa Kituo cha Uchenjuaji dhahabu bwana Festo Shayo, wakati alipokuwa akitoa maelezo juu bwawa hilo.


  0 0


  0 0

  Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Albert Msole akizungumza kwenye baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo kushoto ni Mkuu wa wilaya hiyo Mahmoud Kambona na kulia ni Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Jackson Lesikar Sipitieck.
  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Jackson Lesikar Sipitieck na Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Albert Msole wakifuatilia kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika mji mdogo wa Orkesumet
  Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wakifuatilia kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika mji mdogo wa Orkesumet.Picha na Joseph Lyimo - Globu ya Jamii, Manyara.

  0 0
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (mwenye suti ya kijivu) akiwaeleza Waandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya Uamuzi wa Serikali wa kulifuta Gazeti la MAWIO katika Daftari la Msajili wa Magazeti mara alipokutana na waandishi hao 17 Januari 2016 katika Ukumbi wa Idara ya Habari uliopo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Bw. Assah Mwambene, wa pili kulia ni Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia usajili wa Magazeti, Bw. Raphael Hokororo.  Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa ya Serikali toka kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (hayupo pichani) juu ya Uamuzi wa Serikali wa kulifuta Gazeti la MAWIO katika Daftari la Msajili wa Magazeti mara alipokutana na waandishi hao 17 Januari 2016 katika Ukumbi wa Idara ya Habari uliopo jijini Dar es Salaam.PICHA NA MICHUZI JR-MMG.  SERIKALI  YALIFUTA GAZETI LA MAWIO

  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kulifuta kutoka katika Daftari la usajili wa magazeti, gazeti lijulikanalo kama “MAWIO”. Amri ya kulifuta Gazeti hilo imetolewa kwa Tangazo la Serikali Na. 55 lililotolewa tarehe 15 Januari, 2016. Uamuzi huo umetolewa kwa mjibu wa Sheria ya Magazeti Sura ya 229, kifungu 25(1).


  Hatua hii pia inazuia gazeti la Mawio kuchapishwa katika njia nyingine yoyote ikiwa ni pamoja na mitandao (Online publication) kwa mujibu wa Sheria ya Mawasiliano ya Kieletroniki na Posta Sura ya 306.  Serikali kwa masikitiko makubwa, imechukua uamuzi huu kutokana na mwenendo wa uandishi wa gazeti hilo usioridhisha wa kuandika na kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na kuhatarisha amani, utulivu na usalama wa nchi yetu.


  Aidha, hatua hii ya kulifuta gazeti hilo imechukuliwa baada ya Msajili wa Magazeti kufanya juhudi kubwa za muda mrefu kuanzia Juni, 2013 hadi Januari,  2016  kumtaka Mhariri wa gazeti hilo kubadili aina ya uandishi wa habari na makala katika gazeti lake, bila mafanikio.


  Msajili wa magazeti kwa juhudi zake alifanya mawasiliano na mhariri wa gazeti hilo mara nane kwa lengo la kutaka afanye marekebisho ya  mtindo wa kutoa habari zake lakini mhariri wa gazeti hilo hakuzingatia ushauri mzuri aliopewa na Msajili wa Magazeti.


  Ninatoa wito kwa wamiliki, wahariri, waandishi na watangazaji wa habari kuzingatia sheria, Kanuni na taratibu za taaluma ya uandishi wa habari ambazo zikizingatiwa hakutakuwa na migogoro yoyote. Aidha Serikali inasisitiza kwamba inaheshimu uhuru wa vyombo vya habari unaozingatia maadili, weledi na Sheria za nchi na kwamba Serikali itaendelea kushirikiana navyo


  Kwa upande mwingine ninatoa pongezi kwa vyombo vyote vya habari nchini vinavyozingatia maadili, weledi na Sheria zinazosimamia taaluma ya habari na sheria nyingine za nchi.  Kwa namna ya pekee Serikali inawapongeza wamiliki na wahariri wa vyombo vya habari ambavyo vinapofanya makosa vikielekezwa hujirekebisha na kutoa ushirikiano kwa Serikali na pia kubadili mwenendo wao; hawa ni pamoja  na wahariri wa magazeti ya;

  ·        Mwananchi Tanzania

  ·        Mtanzania

  ·        The East African

  ·        Magazeti ya Daily News na Habari Leo

  ·        Uhuru na mengineyo


  Ninapenda  kusisitiza kwamba Serikali inapenda kujenga uhusiano mzuri na wa kirafiki kati yake na wadau wa sekta ya habari. Aidha ninasisitiza tena wadau wa sekta hii kuzingatia Sheria ili kujenga heshima ya tasnia ya habari na kulinda amani ya nchi yetu.

    
    
  Imetolewa na Nape M. Nnauye(Mb,)

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dar es Salaam, leo tarehe 17 Januari, 2016


  0 0

   Mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam mwaka wa tatuMwakijangile Frank  akipiga shuti kali kuelekea katika goli la wanafunzi wa mwaka wa pili wakati wa Tamasha la”Back to School Bash” lililofanyika kwenye viwanja vya Mabibo Hosteli jana  lililoandaliwa na Vodacom Tanzania,Ambapo mwaka wa pili walifungwa 2-1.
   Mshambuliaji wa timu ya mwaka wa tatu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Charles Mgao(katikati) akijaribu kuwatoka Mabeki wa timu ya  mwaka wa pili  wakati wa Tamasha la”Back to School Bash” lililofanyika kwenye viwanja vya Mabibo Hosteli jana  lililoandaliwa na Vodacom Tanzania,Ambapo mwaka wa pili walifungwa 2-1.
   Msanii wa muziki wa Kufokafoka”Hip Hop”Roma Mkatoliki, akikonga nyoyo za mashabiki wake wakati wa Tamasha la”Back to School Bash” lililofanyika hapo jana katika viwanja vya Mabibo Hosteli  jijini Dar es Salaam kwa Udhaminiwa wa Vodacom Tanzania.


  0 0

   Balozi wa Israel nchini Tanzania Bw.Yahel Vilan(kushoto) akimpongeza Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe,Nape Nnauye(kulia) kwa kuchaguliwa kuwa Waziri  pamoja na kumpatia zawadi ya kitabu na kikombe kutoka Israel alipomtembelea leo jijini Dar es Salaam.

  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye(kulia) akifurahia jambo na Balozi wa Israel nchini Tanzania Bw.Yahel Vilan alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.Katika maongezo yao wamekubaliana kuimarisha ushirikiano uliokuwepo na kuangalia sehemu zaidi za kushirikiana katika sekta za Habari na Utamaduni.


  0 0


  0 0

   Wageni waalikwa kutoka Jimbo la Segerea wakiwepo wananchi wa kawaida wakifuatilia tukio la uzinduzi wa kampeni hiyo.

   Mwanamitido  wa Kimataifa, Flaviana Matata akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya  ya Mazingira Bora kwa Elimu Bora yenye lengo la kufanikisha maendeleo ya elimu katika Jimbo la Segerea kwa kusaidia kununua madawati, kuchimba matundu ya vyoo, kuchimba visima vya maji na kujenga vyumba maalum vya watoto wa kike, chini ya uratibu wa Mfuko wa Udhamini wa Elimu wa Bonnah (BETF), jijini Dar es Salaam jana. Wengine pichani ni mwandaaji wa kampeni hiyo ambaye ni Mbunge wa Segerea, Bonnah Kaluwa na Mratibu wa Elimu Josephat Peter.

  1.       Mbunge wa Segerea Mhe Bonnah Kaluwa akiongea  wakati wa mkutano na waandishi wa habari.


  0 0
  0 0

   Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Philip Mpango (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawamo pichani)jijini Dar es Salaam, kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali dhidi ya Benki ya Stanbic Tanzania kutokana na ushiriki wake katika kuwezesha mkopo wa Serikali wa Dola za Kimarekani Milioni 600 na Kulia kwake ni Naibu Gavana  wa Benki Kuu ya Tanzania(BOT) Bw. Lila Mkila.

  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Philip Mpango (katikati)  akitoa tamko kwa waandishi wa habari (hawamo pichani) jijini Dar es Salaam, kuhusiana na kusudio la kuitoza Benki ya Stanbic faini ya shilingi bilioni 3.  Kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servicius Likwelile na Kushoto kwake ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Bw. Lila Mkila.
  Utangulizi

  1.    Mwezi Julai 2013, Benki Kuu ya Tanzania kupitia ufuatiliaji wa kawaida wa shughuli za mabenki iligundua matatizo yaliyohusiana na hasara itokanayo na mikopo na pia kuacha na kuondolewa kazini kwa viongozi waandamizi wa Stanbic Bank Tanzania Limited (Stanbic) katika muda mfupi. Kutokana na hilo, Benki Kuu iliamua kufanya ukaguzi wa kulenga (Targeted Examination) katika benki hiyo. Ukaguzi huo ni kwa mujibu wa mamlaka iliyopewa Benki Kuu chini ya Kifungu 47 cha Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2006 na Kifungu 31 cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006.


  Matokeo ya Ukaguzi wa Benki Kuu


  2.    Katika ukaguzi huo, wakaguzi wa Benki Kuu, pamoja na mambo mengine walibaini miamala ya kutia shaka iliyohusu malipo kwa kampuni ya kitanzania ya Enterprise Growth Market Advisors (EGMA). Kampuni ya EGMA ilihusika katika uwezeshaji wa upatikanaji wa Mkopo kwa Serikali ya Tanzania ambapo Standard Bank Plc (ambayo kwa sasa inajulikana kama ICBC Standard Bank) na Stanbic Bank Tanzania Limited kwa pamoja walikuwa “Mwezeshaji Mkuu” (Lead Arranger). Malipo hayo kwa kampuni ya EGMA yalikuwa yamefanyika kinyume na taratibu za kibenki na yalihusisha uongozi wa benki ya Stanbic. Jumla ya malipo yalikuwa ni kiasi cha dola za kimarekani milioni 6, na zililipwa katika akaunti ya EGMA na kutolewa kwa muda mfupi kwa njia ya fedha taslimu (cash) ambayo ni nje ya taratibu za kibenki.


  3.    Taarifa ya ukaguzi huo iliwasilishwa kwa benki ya Stanbic kwa mujibu wa taratibu, na Benki Kuu iliiagiza Bodi ya Wakurugenzi ya benki hiyo kuchukua hatua stahiki za kurekebisha kasoro zilizoonekana. Aidha, benki ya Stanbic iliagizwa kutoa taarifa kwa Kitengo cha Financial Intelligence Unit (FIU) kilichopo Wizara ya Fedha na Mipango kuhusiana na miamala hiyo yenye mashaka katika akaunti ya EGMA kama Sheria ya Kuzuia Utakatishaji wa Fedha Haramu ya mwaka 2006 (The Anti-Money Laundering Act, 2006) inavyoelekeza. Benki ya Stanbic ilitekeleza maagizo na kutoa taarifa FIU kuhusu miamala inayotiliwa shaka.


  4.    Mnamo 29 Septemba 2015, Benki Kuu ilipokea barua toka Idara ya Serikali ya Uingereza inayohusika na Upelelezi wa Makosa ya Kugushi na Rushwa (Serious Fraud Office - SFO) ikiiomba Benki Kuu ruhusa ya kutumia ripoti yake ya ukaguzi kama ushahidi katika kesi dhidi ya Standard Bank Plc ambayo ilikuwa ni mshirika wa Stanbic Bank Tanzania Limited katika kuwezesha mkopo wa dola za kimarekani milioni 600 kwa Serikali na kwamba ripoti hiyo ingekuwa wazi kwa umma. Benki Kuu iliijibu SFO kuwa kwa mujibu wa Sheria ripoti za Benki Kuu zinatolewa tu kwa benki au taasisi ya fedha inayohusika, hata hivyo, Benki Kuu haikuwa na pingamizi  kwa SFO kutumia taarifa za ripoti hiyo kwa kuzingatia chanzo cha ripoti hiyo.


  5.    Hatimaye, Standard Bank Plc ilikubali makosa na ilitozwa faini ya jumla ya dola za kimarekani milioni 32.20, ambapo kiasi cha dola za kimarekani milioni 7 zinalipwa kwa Serikali ya Tanzania (dola za kimarekani milioni 6 zilikuwa ni fidia na dola za kimarekani milioni 1 ni riba).


  6.    Kwa kuzingatia mapungufu ya kufanya miamala iliyohusisha EGMA na pia kutokuweka taratibu madhubuti za udhibiti wa ndani, na kwa kuzingatia Kifungu 67 cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, Benki Kuu imeiandikia benki ya Stanbic barua ya kusudio la kuitoza faini ya shilingi bilioni 3. Sheria inaitaka benki ya Stanbic kutoa utetezi katika kipindi cha siku ishirini (20) ambacho kitaisha tarehe 30 Januari 2016.  Endapo Benki Kuu haitaridhika na utetezi, benki ya Stanbic italazimika kulipa faini hiyo.


  Hitimisho


  7.    Benki Kuu imechukua hatua hizo kama onyo kwa benki ya Stanbic na ili iweze kuwa makini katika kuhakikisha kuwa shughuli zake zinaendeshwa kwa mujibu wa taratibu za kibenki na kuzingatia Sheria.  8.    Aidha, hatua hii ni onyo kwa mabenki na taasisi za fedha zisijihusishe na makosa ya aina hii ambayo ni kinyume cha taratibu za kibenki na ni uvunjaji wa Sheria za nchi. Hatua kali zitaendelea kuchukuliwa kwa benki au taasisi ya fedha yoyote itakayobainika kwenda kinyume na taratibu za kibenki na Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006.


  0 0

  Na Skolastika Tweneshe-MAELEZO

  Mbunge wa Jimbo la Segerea kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Mh. Bonna Kalua amesema kuwa hakuna nyumba ya mwananchi itakayobomolewa ambayo imejengwa katika umbali unaohitaji kisheria wa mita 60 kutoka mtoni.

  Mh.Kalua alitoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na wananchi wa Karakata kwenye mkutano wa hadhara.

  Aidha alitoa wito kwa wale ambao wamejenga ndani ya mita 60 na nyumba zao zimewekewa X kujiorodhesha majina yao kwa wenyeviti wa mitaa ili wamfikishiea Ofisi kwake kwa ajili ya kulifuatilia jambo hilo kwa ukaribu na hatimaye wapate haki zao.

  Mh.Bonna aliwatahadharisha wananchi kutodanganywa na watu wanaowachangisha fedha kwa kigezo cha kufungua kesi mahakamani kuwa ni uongo na hawana nia nzuri kwa wananchi kwa sababu kesi ya bomoa bomoa tayari ilishafunguliwa kwa niaba ya nchi nzima. 

  Aliwataka wananchi kuwa wavumilivu mpaka hapo shauri lilipo mahakamani litakapotolewa tamko .


older | 1 | .... | 1092 | 1093 | (Page 1094) | 1095 | 1096 | .... | 3278 | newer