Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110104 articles
Browse latest View live

Washiriki wa Kitanzania wa Programu ya Wajasiriamali Wanawake wa Kiafrika inayoendeshwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Waanzisha Tawi Tanzania

$
0
0
 African Women Entreprenuership Programme (AWEP) Tanzania Chapter imezinduliwa rasmi Ijumaa jioni katika hoteli ya Double Tree,mgeni rasmi akiwa ni Waziri wa Viwanda na Biashara ,Abdallah Kigoda ,pamoja na Balozi wa Marekani nchini  Alfonso Lenhardt
 Hii ni Ngao iliyobidhiwa rasmi na Sylvia Banda  ambaye ni balozi na mwenyekiti wa AWEP Zambia ,kudhihirisha kuwa AWEP Tanzania imezinduliwa rasmi kwa kuikabidhi kwa Mgeni rasmi wa Waziri wa Viwanda na Biashara ,Abdallah Kigoda na Balozi wa Marekani nchini ,Alfonso Lenhardt
 Madam Sylvia Banza, Balozi wa AWEP Zambia akiikabidhi ngao hii , ambayo nae alikabidhiwa na Mama Bill Clinton alipoizindua AWEP Zambia mwaka juzi
                                         Mwenyekiti wa AWEP Tanzania, Bi Flotea Masawe.
              Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt,  ambao ni wafadhili  wa AWEP  katika mkakati wake wa kuwakwamua wanawake  wajasiriamali wa Afrika
                    Waziri Abdallah Kigoda akiwasili katika hafla ilofanyika jioni hii, na kuhudhuriwa na wanachama kutoka sehemu mbalimbali nchini, ambao baadhi walikuwa katika mafunzo ya kujifunza ujasiri amali ambao unalengo la kuwafanya wawekezaji
Mama Lowasa pamoja na Balozi Maajar walihudhuria uzinduzi huu wa AWEP Tanzania
Baadhi ya wanachama wa AWEP Tanzania Chapter katika picha ya pamoja na mgeni rasmi sambamba na Balozi Alfonso
burudani ilikuwa toka kwa Makumbusho Traditional Dancers
Picha na Shamim Zeze


Wajasiriamali wanawake wa Kitanzania waliowahi kushiriki katika Programu ya Wajasiriamali Wanawake wa Kiafrika inayoendeshwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani wameanzisha tawi la Tanzania la Chama cha Wajasiriamali Wanawake wa Afrika (AWEP). Tawi hilo limezinduliwa leo katika hoteli ya Doubletree, Hilton jijini Dar es Salaam katika hafla iliyohudhuriwa na Balozi wa Marekani Alfonso E. Lenhardt na Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda.

Katika hotuba yake wakati wa hafla hii, Balozi Lenhardt alisema, "Kuzinduliwa kwa tawi la Tanzania la AWEP kunaanzisha rasilimali muhimu kwa wajasiriamali wanawake nchini kote. Hivi sasa wanawake wajasiriamali nchini Tanzania watakuwa na chombo watakachoweza kukitumia kubadilishana mawazo na uzoefu wao kuhusu mbinu bora za kuanzisha na kuendesha biashara. Balozi Lenhardt alisisitiza kuwa " Tawi la Tanzania la AWEP ni kielelezo cha dhamira na jitihada za wanawake wa Tanzania za kuwajengea uwezo wanawake wenzao nchini. Tawi hili litakuwa ni mtandao mwingine wa kukuza sekta binafsi nchini na kuwasaidia wajasiriamali wanawake kutimiza ndoto zao."


AWEP ilianzishwa mwaka 2012 na  washiriki wa Programu ya kila mwaka ya Wajasiriamali Wanawake wa Kiafrika inayoendeshwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kama hatua ya kwanza ya mkakati wa kujenga mtandao wa wajasiriamali wanawake kutoka nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara waliodhamiria kubadilisha jamii zao kwa kumiliki na kuendesha biashara ndogo ndogo na za kati na kuwa sauti ya kuchagiza mabadiliko ya kijamii katika jamii hizo.


Msemaji wa Ubalozi wa Marekani Bi. Dana Banks alisema, " Hadi mwishoni mwa mwaka huu ambapo awamu ya tatu ya ziara za mafunzo nchini Marekani itakapokuwa imekamilika, jumla ya wanawake wajasiriamali 122 wanaojihusisha na biashara ndogo na za kati katika kilimo, usindikaji vyakula, mavazi, ubunifu, mapambo ya nyumbani na sekta nyinginezo watakuwa wamehudhuria program ya AWEP."


AWEP ni programu ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani inayolenga kuinua usawa wa kijinsia kwa kuongeza ushiriki wa wanawake wa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara katika shughuli za kijamii na kiuchumi. Aidha, programu hii inalenga kujenga mtandao wa wajasiriamali wanawake  katika nchi hizo waliodhamiria kuchangia kuleta mabadiliko ya kijamii, ukuaji uchumi na kupanua ukubwa na wigo wa biashara kikanda na kimataifa, hususan kuongeza biashara na Marekani kupitia mpago wa AGOA.


Mwenyekiti wa tawi la Tanzania la AWEP Bi. Flotea Massawe alisema "tawi hili litajenga mwamko wa wanawake wa Kitanzania na kuwawezesha kubadilishana uzoefu wao. Aidha, litawapatia nyenzo na fursa za kuwa viongozi katika jamii zao kwa kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika jamii zao na kuwawezesha kuwa sauti ya mabadiliko."




Eveline Kabwelile kuachia albam yake ya kwanza ya injili iliyobeba jina la YESU KOMANDO

$
0
0
Msanii chipukizi wa Injili hapa nchini Eveline Kabwelile anategemea kuachia albamu yake ya kwanza aliyoibatiza jina la YESU KOMANDO yenye jumla ya nyimbo tisa aliyoirekodi katika studio ya Iki Production chini ya Producer Iki

1. Yesu komando
2. Ananitosha bwana
3. Mungu hawezi kukusahau
4. Nakupenda mokozi
5. Mshukuru Mungu
6. Ni wewe mwenyewe
7. Usinipite Mokozi
8. Mokozi asifiwe
9. Ni nani

Albamu hiyo inategemewa kuzinduliwa tarehe 12 may 2013 katika Kanisa la Hollyness pentecote kwa Mchungaji Ndalima Ubungo kuanzia saa nane mchana mpaka saa kumi na mbili jioni.

Akizungumzia sababu hasa iliyomfanya kuingia kwenye uimbaji wa Nyimbo za injili Eveline amesema kwa upande wake anasukumwa sana na wito wa Mungu kwani nilianza kupenda kuimba toka nikiwa mdogo na iko kwenye damu, yake

“Nilianza kuimba toka nikiwa mdogo sikumbuki ni mwaka gani, albamu hii nimeanza akuiandaa 2010 na 2011 ndio nikaanza kurekodi audio za nyimbo zangu na nilianza kurekodi video za nyimbo zangu mwaka 2012 katika studio Brayanz work chini Byayan Hasani na nyimbo zote zimeshakamilika audio na video tayari kwa uzinduzi”

Albamu ya audio na video ya albamu Yesu Komando itaanza kuuzwa siku ya uzinduzi

UJUMBE WA MAKAMISHNA WA TUME YA UTUMISHI YA BUNGE ZIARANI AUSTRALIA

$
0
0
  Ujumbe wa Makamishna wa Tume ya Utumishi ya Bunge ukiwa katika picha ya Pamoja na watumishi wa Bunge la Australia.
 Kamishna wa Bunge la Tanzania Dkt Maua  Daftari akikabidhi zawadi ya picha ya Jengo la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Katibu wa Bunge la Maseneta la Australia Dr.Rosemary Laing Mara walipofika Ofisini kwake kumsalimu. Wengine katika Picha ni Mhe. Hamad Rashid Mohamed na Mhe. Abdukarim Shah ambo wote ni Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge.Ujumbe wa makamishna wa Bunge la Tanzania upo Nchini, Australia kwa ziara ya Mafunzo
Kamishna wa Bunge la Tanzania Dkt Maua Daftari akikabidhi zawadi ya picha ya Jengo la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Katibu wa Bunge la wawakilishi la Australia Ndg. Bernard Wright  Mara walipofika Ofisini kwake kumsalimu. Wengine katika Picha ni Mhe. Hamad Rashid Mohamed na Mhe. Abdukarim Shah ambo wote ni Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge. Ujumbe wa makamishna wa Bunge la Tanzania upo Nchini, Australia kwa ziara ya Mafunzo

Jarida la Mzuka la mwezi April limeingia mtaani

$
0
0
Jarida la Mzuka la mwezi April linaloandaliwa na Bongo5 Media Group limetoka huku likiwa na cover story ya kundi jipya la akinadada warembo wa Shosteez.

Katika cover hiyo Shosteez wamefunguka mengi kuanzia jinsi walivyokutana na Lamar, historia ya familia zao na jinsi ambavyo wote wamekua bila kuwa na baba zao, maisha ya ustaa na jinsi wanavyosumbuliwa na wanaume, uhusiano, muziki na mambo mengi kibao.

Pia kuna story kibao kama wanamumuziki wa kike Tanzania wenye mvuto zaidi, mastaa 10 wa kiume Tanzania wanaopiga pamba kali zaidi, madj 10 wa kike Afrika wenye mvuto zaidi, nani aliyeanzisha jina Bongo Flava na historia yake, makosa yanayofanyika kwenye filamu za kibongo na wasichana 8 wapya watakaoupeleka muziki wa Tanzania kimataifa.

Zingine ni pamoja na One on One na Rose Ndauka, Nani zaidi kati ya Sam Misago na B Bozen? (wananchi wameongea). Uchambuzi wa wimbo wa Ney wa Mitego na Diamond – Muziki Gani, Makala kumhusu Navio wa Uganda, bila kusahau Kona ya Mjasiriamali ambapo Patrick Ngowi (mtanzania aliyetajwa na jarida la Forbes miongoni mwa wajasiriliamali bora 30 waliochini ya miaka 30 - 2013) pamoja na picha kali za matukio mbalimbali ya burudani.

Kopi ni shilingi 3,000. Ili kupata nakala yako wasiliana na fred@bongo5.com ama simu 0765537130.

Thanks.
Fredrick Bundala aka Skywalker.
Head of Content, bongo5.com

WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA MKWAWA WAPEWA MAFUNZO YA KUZIMA MOTO

$
0
0
Askari wa Kikosi cha Zimamoto mkoani Iringa akionyesha namna ya kuzima moto kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Mkwawa,wakati wa mafunzo ya tahadhari ya moto na jinsi ya kujikinga na moto pamoja na mbinu za uzimajimoto,yaliyofanyika Chuoni hapo.
Mmoja wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Mkwawa akifanya mazoezi ya uzimaji moto wakati wakufunga mafunzo hayo.Picha na Francis Godwin.

Posterous Will Turn Off On April 30, 2013 After Being Bought By Twitter

$
0
0

Dear SJ POST Visitors,
 
My blog's host (Posterous) launched in 2008. I started using Posterous as a simple blogging platform since 2010 to share with you by republishing mosaic of news and information and some inspiring and valuable pieces that I came across when surfing the net and from other reliable sources. I hope you liked them and you found them useful.
 
Last year on March 12, 2012, Posterous was bought by Twitter.
 
This year on April 30, 2013, Posterous will turn off posterous.com and its mobile apps in order to focus 100% of their efforts on Twitter. This means that as of April 30, 2013, Posterous Spaces including my blog www.sjpost.posterous.com will no longer be available either to view or to edit.
Right now I am working hard to make sure the SJ POST blog will continue beyond 30th April 2013.
I will miss Posterous, but as the old saying goes:

Yesterday is but a dream
And tomorrow is only a vision;
And today well-lived, makes
Yesterday a dream of happiness
And every tomorrow a vision of hope.

Sanskrit Proverb
Therefore, the new SJ POST blog is now moving to WordPress and can be accessed here www.sjposters.wordpress.com

Bendi ya Ras Inno yakamilika, kuzinduliwa mwezi ujao

$
0
0
Na Mwandishi Wetu

HATIMAYE bendi ya nguli wa muziki wa reggae nchini, Ras Inno Nganyagwa imekamilika na anatarajia kuizindua rasmi mwezi ujao jijini Dar es Salaam.

Ras Inno ambaye ni mshindi wa tuzo nne za mwanamuziki bora wa reggae Tanzania, amesema bendi yake hiyo ina wanamuziki 11 na itazinduliwa katika hafla maalumu katika ukumbi utakaotangazwa hapo baadaye.

Amasema nia ya kuanzisha bendi hiyo ni kuwa na ufanisi bora zaidi wa kufanya kazi zake za muziki, kwani bendi ya kudumu na wanamuziki wa kudumu hujenga ‘patern’ ambayo ni sawa na wachezaji waliozoeana uwanjani.

“Hiyo hulinda ladha ya nyimbo husika kutobadilika kila show, pia uhakika wa kufanya kazi njema nje ya nchi. Lakini pia kuwa na bendi huhakikisha upatikanaji wa tija ya kudumu, tofauti na ukiwa ‘solo’ tu bila jina la bendi kazi huja kwa misimu kutokana na mazoea ya hapa kwetu Bongo,” amesema.

Amesema bandi hiyo ni mojawapo ya miradi iliyo chini ya usimamizi wa taasisi yake mahsusi ya kuupromoti muziki wa reggae, kwa ushirikiano na wadau wengine miongoni wa mitindo mingine kwa kuzingatia weledi.

“Taasisi inaitwa Reggae Production House ambayo itahakikisha uzalishwaji wa vipaji vipya vya vijana wanaotaka kuingia kwenye reggae, kwa kufuata njia sahihi itakayowajenga kuwa wanamuziki bora wa reggae nchini watakaoweza kufanya kazi kimataifa.

“Dhima nzima ni kuufufua muziki wa reggae hapa nchini si kwa kuwa umekufa, la hasha, ila kuna mazingira yanayoufanya muziki huu uonekane kama haupo, lakini mahitaji yapo na mashabiki wana hamu kubwa nao.”

Aidha ameongeza kusema kwamba, ukimya wake wa muda mrefu una sababu kadhaa zikiwemo za kibinafsi kimaisha, lakini muda aliokuwa nje ya ulingo, ameyasoma vyema mazingira yanayoukabili mtindo wa reggae hivyo naamini ana dozi ya kuutibu.

“Ninayodhamiria kuyafanya kupitia taasisi yangu na vitengo vyake ikiwemo bendi, havijapata kuonekana kabla kwenye tasnia ya reggae hapa nchini. Hivyo basi naamini mwanzo huu wa mapinduzi, utaungwa mkono na wadau wote wenye mapenzi mema.”

UMOJA WA WATANZANIA UJERUMANI KUSHEREHEKEA MIAKA 50 YA MUUNGANO WA TANZANIA NCHINI UJERUMANI

$
0
0
Mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania nchini Ujerumani Bw. Mfundo Peter Mfundoanayofuraha kubwa kuwakaribisha watanzania na wale wasio watanzania kutoka pembe mbali mbali za Dunia katika maadhimisho ya Sherehe Ya Muungano wa Tanzania Bara na Visiwani, zitakazofanyika mjini Koloni hapa ujerumani.siku ya juma mosi Tarehe 27.04.13 kuanzia saa :08:00 Za mchana hadi usiku wa manane.

Katika sherehe hio ambayo imedhaminiwa na Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU) kushirikiana na culture center ya sarakasi. Die Zirkus Fabrik, kutakuwa na maonyesho ya bidhaa za Tanzania, na atakayependa anaweza pia kununua bidhaa hizo. Ngoma za asili kutoka Tanzania, Bongo Flava Live kutoka kwa Msanii SHAH SMOOTH aliye na makazi yake DUBLIN,. Sarakasi na mwisho watanzania watapata Fursa ya KUDUARIKA na midundo kutoka Tanzania kupitiaDJ SUDI MNETE wa Deutschwelle.

Akihojiwa na vyanzo vyetu vya habari mwenyekiti Bw Mfundo Alisema, Madhumuni ya sherehe hiyo sio tu kusherehekea siku kuu ya muungano pekee, bali ni kutimiza moja ya azimio la U T U la kuwakutanisha Watanzania wanaoishi nchini humo na kutangaza utamaduni wetu wa Tanzania kwa wenyeji wetu haba Ulaya.

Aliendelea kufafanua kwamba moja ya Agenda ya UTU ni kuhakikisha Watanzania wanaoishi nchini Ujerumani wanakuwa pamoja kwa hali zote, wanashirikiana kwa karibu na kusaidiana. Aidha pia kuhakikisha wasanii wanaoisha hapa ujerumani wanatangaza kazi zao hadharani na wanazitumia kazi hizo kujipatia manufaa zaidi.

Hivyo katika sherehe hii (UTU) imealika wasanii mbali mbali kuja kuonyesha kazi zao. Mwenyekiti alimaliza kwa kuwashukuru wasanii na watanzania ambao tayari wameshajiandikisha kushiriki katika sherehe hiyo kubwa Mjini Koloni.

KARIBUNI SANA KOLONI

Balozi Seif Iddi afungua Semina ya siku moja ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiifungua Semina ya siku moja ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kuhusu uimarishaji wa Jeshi la Polisi Tanzania iliyofanyika katika ukumbi wa Juu wa Baraza la Wawakilishi Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakili wakisikiliza Hotuba ya mgeni rasmi Balozi Seif katika semina ya Wajumbe hao kuhusu maboresho ya Jeshi la Polisi Tanzania iliyofanyika katika Ukumbi wa juu wa Baraza hilo uliopo Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Maafisa wa ngazi ya juu wa Jeshi la polisi Tanzania walioshiriki semina ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakifuatilia Hotuba ya ufunguzi wa semina hiyo uliofanywa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwenye ukumbi wa Baraza hilo uliopo Mbweni.Picha na Hassan Issa wa - OMPR – ZNZ.

Wanafunzi wa shule mbali mbali jijini Dar wapewa mafunzo ya mchezo wa Rugby

$
0
0
Kocha kutoka Marekani Jonathan Markowitz akiwafundisha mchezo wa Rugby wanafunzi wa kutoka shule za msingi mbalimbali za Dar es Salaam katika tamasha la michezo lilofanyika viwanja vya shule ya kimataifa ya Tanganyika Aprili, 20, 2013. Tamasha hilo lilidhaminiwa na kampuni ya ulinzi ya G4S.
Kocha kutoka Uingereza Ben Illingworth akiwafundisha mchezo wa Rugby wanafunzi wa kutoka shule za msingi mbalimbali za Dar es Salaam katika tamasha la michezo lilofanyika viwanja vya shule ya kimataifa ya Tanganyika Aprili, 20, 2013. Tamasha hilo lilidhaminiwa na kampuni ya ulinzi ya G4S.
Wanafunzi wa kutoka shule za msingi mbalimbali za Dar es Salaam wakiwa katika tamasha la michezo ya Rugby kuendeleza mchezo huu Tanzania na lilohusishwa na Bhubesi Pride kutoka Uingereza, lilofanyika viwanja vya shule ya kimataifa ya Tanganyika Aprili, 20, 2013. Tamasha hilo lilidhaminiwa na kampuni ya ulinzi ya G4S.

Mnadani kwenye nyama choma,Msalato Mkoani Dodoma

$
0
0
 Kila ifikapo siku ya jumamosi kama ya leo,Wakazi wa Mkoani Dodoma na wengine watokao sehemu mbalimbali hupenda kutembelea eneo hili la Msalato maarufu kama Mnadani kwa ajili ya kujipatia maakuli ya chama choma.Pichani ni mmoja wa vijana wanaohusika na uchomaji nyaka katika eneo hilo akiendelea na shughuli yake.
 Kila muuza Nyama huvutia wateja kwa namna yake,na huyu akionekana kunyanyua moja ya pende la nyama hizo kama anavyoonekana.
 Nyama ya Mbuzi ikiwa imepangwa tayari tayari.
 mzigo upo jikoni.

Msama Promotions kuizindua Haleluya Collection Septemba

$
0
0
KAMPUNI ya Msama Promotions inatarajia kufanya uzinduzi mkubwa wa albamu ya sita ya Haleluya, ambayo inawahusisha wanamuziki wa Injili wa nchi za Afrika Mashariki.  
Uzinduzi wa albamu hiyo unatarajiwa kufanyika Septemba mosi mwaka huu, ambapo kutakuwa na wanamuziki mbalimbali wa muziki wa Injili kutoka ndani na nje ya nchi ambao watausindikiza uzinduzi huo.

Akizungumza  mapema leo jijini Dar, Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama amebainisha kuwa maandalizi ya albamu hiyo yanakwenda vizuri na wanauhakika wa kufanya mambo mazuri zaidi. “Tumeshaanza maandalizi ya Haleluya Collections, tumejipanga kutoa albamu bora iliyoshiba, itakuwa ni albamu kali ya muziki wa Injili nchini na Afrika kwa ujumla,”alisema Msama.

Alieleza kuwa uzinduzi huo utafanyika pia kwenye mikoa zaidi ya saba, ambapo utaratibu wa kuteua mikioa hiyo bado unaendelea. Alisema uzinduzi huo utakuwa ni wa CD na DVD na albamu hiyo itakuwa imebeba nyimbo zaidi ya tano.

mwenyekiti wa chadema kata ya Kiroka morogoro vijijini ajiunga na ccm.

HUDUMA ZA NSSF ZAVUTIA WENGI KATIKA MAONESHO YA HUDUMA ZA HOSPITALI YA MUHIMBILI

$
0
0
 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mh.UmmyMwalimu akimkabidhi cheti Ofisa Uhusiano Hudumwa kwa wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Maife Kapinga wakati wa hafla ya kufunga Maonesho ya Huduma za Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dk. Merina Njelekela akisoma hotuba yake wakati wa kufunga maonesho ya Huduma za Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mh.Ummy Mwalimu akisoma hotuba yake wakati wa hafla ya kufunga Maonesho ya Huduma za Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.
Watu mbalimbali wakipata maelezo ya huduma za NSSF ikiwemo Fao la matibabu.
 Baadhi wa wadau waliojitokeza katika maonesho hayo.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mh.UmmyMwalimu akiweka sahihi katika kitabu cha wageni wakati alipotembeklea banda la NSSF. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dk. Merina Njelekela.

kiota cha maraha cha dar live kinavyoonekana kwa nje usiku


Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia afanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom juu ya sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini

$
0
0
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof: Makame Mbarawa akimkaribisha ofisini kwake jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw.Rene Meza ambapo baadae viongozi hao walifanya mazungumzo juu ya masuala mbalimbali katika sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini na mipango ya Vodacom ya kushirikiana na serikali kuboresha zaidi sekta hiyo.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof: Makame Mbarawa akisalimiana na Ofisa Mkuu wa Masuala ya Sheria wa Vodacom Tanzania Bw.Walarick Nittu wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania(katikati)akiwa na ujumbe wake walipomtembelea Waziri Prof:Mbarawa na kuwa na mazungumzo juu ya masuala mbalimbali katika sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini na mipango ya Vodacom ya kushirikiana na serikali kuboresha zaidi sekta hiyo.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof: Makame Mbarawa akisalimiana na Ofisa Mkuu wa Mitandao wa Vodacom Tanzania Bw.Alec Mulugo wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania(kulia)akiwa na ujumbe wake walipomtembelea Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Prof: Mbarawa na kuwa na mazungumzo juu ya masuala mbalimbali katika sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini na mipango ya Vodacom ya kushirikiana na serikali kuboresha zaidi sekta hiyo.

Taswira za kigamboni kutoka angani leo

$
0
0
 Jirani na feri
 Mkeka wa nguvu pia upo
 Kijani imetawala
Ujenzi wa daraja la Kigamboni ukiendelea kwa kasi

soko la samaki na neshno

$
0
0
 Soko la samaki la feri linavyoonekana asubuhi hii
Uwanja wa TAifa na vitongoji vyake leo

mdau saumu alamba nondozzzz

$
0
0
Mdau  Saumu Adadi Rajabu  akifurahi na baba yake Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Mhe Adadi Rajabu na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mhe Peter Kallaghe baada ya kulamba nondozzz yake  ya Saumu Adadi Rajabu who graduated on Monday 15th of April, 2013 at Coventry University with Masters in Advertising and Marketing. katika chuo kikuu cha Coventryiversity with Saumu Adadi Rajabu who graduated on Monday 15th of April, 2013 at Coventry University with Masters in Advertising and Marketing.Marketing.
Mdau Saumu akipozi na baba kwa furaha

OFFICIAL LAUNCH OF OF ABITAT IN DAR ES SALAAM

$
0
0
The official launch of the Alliance of businessmen and Industrialists of Tanzania and Turkiye (ABITAT) at the Kilimanjaro Hyatt Regency hotel in Dar es salaam officiated by Tanzania's President Jakaya Mrisho Kikwete April 19, 2013
Viewing all 110104 articles
Browse latest View live




Latest Images