Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

Jovago’s Interview with the Executive Secretary of Tourism Confederation of Tanzania (TCT), Mr Richard Rugimbana

0
0
Dar es Salaam, January, 2016 - Over the last two years the hospitality industry has experienced the advancement in technology and a shift in marketing predominance, customer preference and management structure. To find out the insights, JovagoTanzania has done an interview with the Executive Secretary of Tourism Confederation of Tanzania (TCT) Mr Richard Rugimbana (pictured) that would be more helpful for 2016 master plans on the sector.


 JOVAGO: What is the outlook for the hospitality industry in terms of market predominance, the impact of technology and the shift in management structures?
R.R: Tanzania’s hospitality sector is still in its infancy but growing rapidly to serve both domestic and foreign guests. At present, the Ministry of Natural Resources and Tourism’s master plan has a goal of attracting 2 Million arrivals by 2017.  Greater emphasis will be placed on attracting tourists from other African countries in addition to established international market such as the United States and United Kingdom. At present there are a limited number of accommodation offering with global brand names though we have prestigious names such as Singita Grumeti, Hyatt, Ramada, Sopa and Serena etc. Manpower is still a challenge but we are building the capacity of young Tanzanians to take over managerial roles in the near future


JOVAGO: Are there any trends in customer preferences?

R.R: Yes many desire or looking for memorable holidays. Tanzania has a lot to offer for travelers although with the rise of internet penetration free WIFI is an essential need. However the most import thing is a quality services from the workers.


JOVAGO: Is there any difference in challenges when developing a hotel group chain as opposed to a stand-alone brand?

R.R: Yes it is clear that brand names have an advantage based on recognition although new entrants are also offering competition, especially in terms of price and quality of services. New ‘local’ hotels are also offering improved amenities to attract foreign and domestic tourists. 
 About Jovago
Jovago.com is an online hotel booking service with offices in Lagos (Nigeria), Nairobi (Kenya), Dakar (Senegal) and Dar es Salaam (Tanzania) founded by Africa Internet Group and has MTN and Millicom as its investors. Jovago.com, Africa’s No.1 booking portal, facilitates the booking process for its users to provide them with the best hotel booking experience with fast, transparent and easy-to-use services. Jovago.com has over 25,000 local hotel listings across Africa and over 200,000 hotels around the world.

BALOZI PAUL RUPIA AFANYA MISA YA KUTIMIZA MIAKA 80

0
0
Mzee Balozi Paul Rupia (kulia) akizungumza katika Misa ya shukrani iliyoongozwa na Askofu wa Dayosisi ya Dar es Salaam ya Kanisa la Kianglikana Tanzania Valentino Mokiwa (kushoto) iliyofanyika katika Kanisa la St. Alban Posta Dar es Salaam jana. Misa hiyo ya shukrani ilifanyika katika kuadhimisha sikukuu ya kuzaliwa ambapo jana alitimiza miaka 80. Katika ni Mke wake Mama Rose Paul Rupia.
Askofu Valentino Mokiwa akitoa Baraka kwa Balozi Paul Rupia, familia yake na ndugu na jamaa waliohudhuria misa ya shukrani ya kutimiza miaka 80 ya kuzaliwa katika Kanisa Kuu la Anglikana la Mtakatifu Albano Dar es Salaam.
Balozi Paul Rupia akiwashukuru ndugu na jamaa waliohudhuria ibada ya shukrani ya kutimiza miaka 80 iliyofanyika katika Kanisa kuu la Mtakatifu Albano Dar es Salaam jana.

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ZANZIBAR na Naibu Waziri wa Mabo ya Ndani Mhe Hamad Masaudi Atembelea Miradi ya Jimbo lake.

0
0
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe. Hamad Masauni akiwa katika ziara yake kutembelea mradi wa kisima cha maji kaburukikombe migimbani Zanzibar.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe Hamad Yussuf Masauni akizungumza na Wananchi wa Jimbo hilo wakati wa ziara yake katika mradi wa maji kaburi kikombe migombani Zanzibar Mradi huo unasimamiwa na Jumuiya ya TAYI  Tanzania Youth Icon kulia aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo na kwa sasa anagombea Jimbo la Kikwajuni Zanzibar Mhe Nassor Salim Jazira. 
Wananchi wa Jimbo la Kikwajuni akiangalia mradi wa kisima kipya kinachosimamiwa na TAYI kinachochimbwa katika eneo la Kaburi Kikombe Zanzibarb hicho kitakuwa kisima cha Pili kuchimbwa na TAYI kwa Wananchi wa Jimbo la Kikwajuni kikiwa na urefu wa mita 42 kinachotarajiwa kukamilika kwake kutumia shilingi milioni 20 hadi kukamilika kwake.
Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya TAYI Abdalla Ahmeid akitowa maelezo ya mradi huo wa Pili wa Uchimbaji wa Kisima cha Maji kwa ajili ya Wananchi wa Jimbo la Kikwajuni na jirani zake kikiwa katika hatu ya mwisho ya uchimbaji wake. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

TFDA yajizatiti kukabiliana na madhara yatokanayo na madhara ya chakula kisicho salama

SAMATTA ALIVYOPOKELEWA RASMI NA MASHABIKI WA SOKA JIJINI DAR

WAZIRI KITWANGA AFANYA ZIARA JIMBONI KWAKE MISUNGWI, AWATAKA WANANCHI KUCHANGIA MIRADI YA MAENDELEO

0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akipokelewa kwa shangwe na wananchi wa Kata ya Kanyelele jimboni humo kabla ya kuanza mkutano wake na wananchi hao uliofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mwakalima. Waziri Kitwanga alichangia shilingi laki tano kwa ajili ya ujenzi wa choo cha Shule ya Sekondari Kanyelele ambapo kimeharibika. Hata hivyo, aliwataka wananchi hao waweke utamaduni wa kuchangia maendeleo ya vijiji vyao.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (wapili kushoto) akimuuliza swali Diwani wa Kata ya Kanyelele, Paschal Kilangi (kulia) wakati Mbunge huyo alipokuwa akikiangalia choo cha Shule ya Sekondari Kanyelele jimboni humo kilichobomoka. Waziri Kitwanga alichangia shilingi laki tano kwa ajili ya ujenzi wa choo hicho na kuwaomba wananchi wa kata hiyo waanze kuchanga kwa kasi ili choo hicho kiweze kutengenezwa kwa haraka.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (wapili kushoto) akiwa na Diwani wa Kata ya Kanyelele, Paschal Kilangi (kushoto) pamoja na Mkuu wa Shule ya Sekondari Kanyelele, Kudehwa Gapi (wapili kulia) wakiwa wanaikagua shule hiyo ambayo choo chake kilikuwa kimebomoka kwa kudidimia chini ya ardhi. Waziri Kitwanga alichangia shilingi laki tano kwa ajili ya ujenzi wa choo hicho na kuwaomba wananchi wa kata hiyo waanze kuchanga kwa kasi ili choo hicho kiweze kutengenezwa kwa haraka.

MSIBA DMV NA TANZANIA LETICIA NYERERE HATUKONAE TENA.

0
0
Leticia Nyerere enzi ya uhai wake

Familia ya Leticia Nyerere ya Lanham, MD inasikitika kutangaza kifo cha mama Yao mpenzi kilichotokea tarehe 10 January 2016 nchini marekani. Mipango na utaratibu wa kusafirisha mwili inafanywa.
Msiba upo 9004 brightlea court, Lanham MD 20706.
Kama mila na desturi zetu tufike kuwafariji familia. Kwa maelezo zaidi wasiliana na :
Margareth mageni 240 462 9138
Emmanuel muganda 240 447 2801
Ramadhani kamguna 202 459 3838

Bwana ametoa, Bwana ametwaa na jina lake lihimidiwe.

MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA YAONGEZEKA TANZANIA

0
0
Mtaalamu wa masuala ya Afya kutoka akipima mzunguko wa damu Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasiyoambukizwa (TANCDA)jana katika hospitali ya mkoa wa Mount Meru ambapo shughuli za upimaji wa magonjwa ya moyo,kisukari na saratani yalifanyika bure kwa wananchi wote.
Wakazi wa Arusha wakiwasikiliza waelimishaji wa magonjwa yasiyoambukiza kutoka Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasiyoambukizwa (TANCDA)jana katika hospitali ya mkoa wa Mount Meru ambapo shughuli za upimaji wa magonjwa ya moyo,kisukari na saratani yalifanyika bure kwa wananchi wote.

Na Woinde Shizza,Arusha.
Kutokana na ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo magonjwa ya moyo ,kisukari na saratani ,Watanzania wameaswa kuzingatia lishe bora na mtindo bora wa maisha ili kuepuka magonjwa hayo ambayo husababishwa na mtindo mbaya wa maisha pamoja unywaji pombe,uvutaji sigara na ulaji uisiofaa.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasiyoambukizwa (TANCDA) ,Dokta Tatizo Waane alisema kuwa kumekua na ongezeko kubwa la watu wenye magonjwa hao kitaifa ambapo ugonjwa wa moyo asilimia 26% ugonjwa wa kisukari umeongezeka kwa Asilimia 9.6.

Akizungumza katika zoezi la upimaji na utoaji elimu kwa wananchi juu ya magonjwa hayo ,Dr.Waane amesema kuwa magonjwa ya moyo yameongezeka kwa asilimia 10 hivyo Watanzania hawana budi kuangalia hali yao ya lishe na kuzingatia kufanya mazoezi ili kuepuka magonjwa yasiyo ya lazima.

"Watu wengi wamekua hawatilii maanani magonjwa yasiyoambukiza lakini yana athari kubwa kiafya na kwenye uchumi wa watu kwani hutumia muda mrefu na fedha nyingi kutibu" Alisema Dokta Waane.

Mratibu wa zoezi la upimaji wa magonjwa hayo kwa mkoa wa Arusha Dokta David Shungu alisema kuwa wananchi wanapaswa kupatiwa elimu kwani magonjwa hayo yanaongoza kwa kusababisha vifo sawa na magonjwa yanayoambukiza.

Kwa upande wake Mkazi wa Arusha aliyejitokeza kupima afya yake na kupata ushauri Tunu Ndege alisema kuwa zoezi hilo litawasaidia wananchi wengi kujua afya zao na kuchukua hatua kulinda afya zao dhidi ya magonjwa ,pia ameshauri huduma hiyo ya upimaji iwafikie watu wa vijijini wanaoteseka na magonjwa bila kujua.


Alisema Mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza ya moyo,sukari na saratani yanapaswa kutiliwa mkazo kwa kutoa elimu na tiba kwa wananchi kwani magonjwa hayo hudumu kwa muda mrefu na kusababisha hasara ya kijamii na kiuchumi hata kupelekea vifo na ulemavu.

TANCDA Yatoa huduma bure ya kupima magonjwa yasiyoambukizwa jijini Arusha

0
0
Wakazi wa jijini Arusha wakiwa kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa huo ya Mount Meru kwa ajili ya kupima magonjwa yasiyoambukizwa huduma iliyokuwa inatolewa bure na shirikisho la vyama vya magonjwa yasiyoambukiza nchini (TANCDA) wakimsikiliza mfanyakazi wa TANCDA, Alphonce Kabili aliyekuwa anawapa utaratibu wa kupata huduma zao.
Wakazi wa jijini Arusha wakiwa kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa huo ya Mount Meru kwa ajili ya kupima magonjwa yasiyoambukizwa huduma iliyokuwa inatolewa bure na shirikisho la vyama vya magonjwa yasiyoambukiza nchini (TANCDA).
Manesi wakichukua maelezo ya mkazi wa jijini Arusha, Mariam Mohamed ili kumpima magonjwa yasiyoambukizwa ya ambayo huduma hiyo ilitolewa bure na shirikisho la vyama vya wagonjwa yasiyoambukiza (TANCDA).

WAZIRI MKUU AKUTANA NA BALOZI WA CUBA NCHINI- MHE. JORGW LUIS LOPEZ TORMO

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Cuba nchini, Mhe. Jorge Luis Lopez Tormo, kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwake jijini Dar es slaam Januari 11, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Cuba nchini, Mhe. Jorge Luis Lopez Tormo, ofisini kwake jijini Dar es slaam Januari 11, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

INTRODUCING New Video: Mwasiti Ft Queen Darleen - Sema Nae

Dar es salaam, Mbeya, Rukwa,Katavi, Kigoma na Mtwara yatokomeza ugonjwa wa kipindupindu

0
0
Na Skolastika Tweneshe-Maelezo

Jiji la Dar es salaam limeripotiwa kutokuwa na mgonjwa yoyote wa kipindupindu  kuanzia Desemba mwaka jana.

Akizungumza leo na waandishi wa habari  jijini Dar es salaam  Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto Mh. Dkt Hamisi  Kigwangalla amesema kuwa licha ya ugonjwa wa kipindupindu kuanzia jijini Dar es salaam na kudumu kwa miezi mine lakini kuanzia kwa sasa hajaripotiwa mgonjwa wa kipindupindu.

“Mkoa wa Dar es salaam ambako ndipo ugonjwa ulipoanzia na kudumu kwa miezi minne haujaripotiwa  kuwa mgonjwa wa kipindupindu kuanzia tarehe 22/12/2015,” alisema Kigwangalla.

Waziri aliongeza  Kigwangalla aliongeza kuwa mikoa mingine ambayo haijaripotiwa kuwa na maambukizi kwa muda wa wiki moja ni pamoja na Mbeya,Rukwa,Katavi,Kigoma,Kagera  na Lindi.

Aidha  alisema kuwa mikoa ambayo haijarioptiwa ugonjwa huo kwa zaidi ya miezi miwili iliyopita ni  Shinyanga, Kilimanjaro na Iringa  pia amesema kuwa kuna mikoa ambayo haijawahi kuripoti ugonjwa wa kipindupindu uanze nayo ni mikoa ya Njombe, Ruvuma na Mtwara.

Dkt. Kigwangalla alisema mikoa iliyotoa idadi kubwa ya wagonjwa wa kipindupindu ambayo ni Halmashauri ya Morogoro(66), Arusha (50), Singida(40), na manispaa ya Dodoma (33).

Pia amewaasa wananchi  kunywa maji yaliyo safi na salama, kuepuka kula chakula kilichoandaliwa katika mazingira yasiyo safi na salama pamoja na kunawa mikono na maji safi na sabuni kwa maji safi yanayotiririka pamoja na kutumia vyoo wakati wote na kutokujisaidia ovyo katika vyanzo vya maji ,maziwa na mabwawa.

Kwa mujibu wa wizara ya afya tangu ugonjwa wa kipindupindu uanze, jumla ya watu 13,491 wameugua kipindupindu, na kati yao watu 205 wameshafariki kutokana na  ugonjwa huo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala (kushoto) akitoa taarifa ya hali ya ugonjwa wa kipindupindu nchini katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika leo kwenye ukumbi wa wizara hiyo jijini Dares Salaam. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya la Dunia(WHO), Dkt .Rufaro Chotaro.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya(kushoto) akitoa ufafanuzi juu ya ugonjwa huo.Kulia ni Waziri wa wizara hiyo Dkt. Hamis Kigwangala. (Picha kwa hisani ya Wizara ya Afya)

WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI YASHTUSHWA NA KASI YA DAWASCO.

0
0
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maji safi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASCO) Mhakndisi Cypian Luhemeja akiongozana na Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Mbogo Mfutakamba ,wakielekea katika kikao cha Unongozi na wafanyakazi wa DAWASCO kilichofanyika makao makuu y a shirika hilo. 
 Mkurugenzi wa Rasilimali watu w Shirika la Maji safi na Maji taka Dar es Salaam,DAWASCO,Bi,Joy Chidosa akifanya utamburisho katika kikao hicho.
Baadhi ya Mameneja wa vitengo mbalimbali katika Shirika la Maji safi na Maji taka jijini Dar es Salaam DAWASCO ,wakiwa katika kikao hicho.

Pam D azindua Video yake ya Popo Lipopo Maisha Basement

0
0
Usiku wa kuamkia leo, staa wa muziki wa Bongo Fleva, Pamela Daffa 'Pam D' kwa kushirikiana na mtayarishaji na mwanamuziki hatari Bongo, Mesen Selekta walikinukisha vya kutosha ndani ya Ukumbi wa Maisha Basement uliopo Kijitonyama jijini Dar.

Usiku huo uliotawaliwa na redcarpet ya hatari ambapo mashabiki kibao walipata nafasi ya kupiga picha na Pam sambamba na kuzungumza naye mawili-matatu, ulianza kwa kwa Mesen kupanda na kundi zima la Team Selekta ambapo alipopanda Mesen aliwapagawisha vilivyo na ngoma zake zote kali kama vile Kanyaboya, Sweetlove, Team Selekta pamoja na wimbo wake mpya wa Love Me.

Shangwe zilizidi pale walipopanda madensa wa PAm D kwa sarakasi kibao na madoido ambapo Pam alitokelezea na kuanza kuvurumusha nyimbo zake zote kali kuanzia Nimempata kisha akamalizia na Popo Lipopo ambapo mashabiki walipata fursa ya kuuona kwa mara nyingine live ukumbini hapo.
PAM D (70) Mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini, Pamela Daffa akiwaburudisha mashabiki waliojitokeza kwenye uzinduzi wa video yake ya Popo Lipopo ndani ya Maisha Basement usiku wa kuamkia leo.
PAM D (75)Pam D (mwenye kipaza sauti) akichana freestyle mbele ya mashabiki wake.
PAM D (64)Madensa wa Pam D wakiendelea kufanya yao.


HOSPITALI YA TUMBI KIBAHA YANUFAIKA NA MSAADA TOKA VODACOM FOUNDATION

0
0
Madaktari na Wafanyakazi wa Shirika la Elimu Kibaha, Mkoa wa Pwani wakiwa kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa vifaa vya kuwasaidia watoto waliozaliwa kabla ya wakati wake”watoto njiti” . Vifaa hivyo vilivyotolewa na Vodacom Foundation kupitia taasisi inayojishughulisha kusaidia watoto hao ya Doris Mollel, thamani ya vifaa hivyo ni zaidi ya shilingi Milioni 6/-
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Elimu Kibaha,Robert Shilingi (wa pili kutoka kushoto) na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya watoto katika Hospitali ya Tumbi Dkt.Andrew Lwali (kushoto) wakipokea msaada wa baadhi ya vifaa vya kuwasaidia watoto waliozaliwa kabla ya wakati(Njiti) kutoka kwa Maneja wa Vodacom Foundation, Sandra Oswald (kulia) wakati wa hafla fupi ya kukabidhiana vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 6/- katika Hospitali ya Tumbi mkoani Pwani vilitolewa msaada na mfuko huo kupitia taasisi ya Doris Mollel.Anayeshuhudia watatu toka kushoto ni Mkurugenzi wa taasisi inayojishughulisha na watoto hao,Doris Mollel.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Elimu Kibaha,Robert Shilingi (kushoto)akimshuhudia Muuguzi wa watoto katika Hospitali ya Mkoa wa Pwani Tumbi,Linda Makundi akionyesha mfano kwa Maneja wa Vodacom Foundation,Sandra Oswald,Njisi mashine ya Oxgen Concentrator inavyofanya kazi ya kuwasaidia watoto waliozaliwa kabla ya wakati(Njiti) wakati wa hafla ya kukabidhiwa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 6/- vilivyotolewa na Vodacom Foundation kwa ajili ya kusaidia watoto hao.Katika picha kulia ni Mkurugenzi wa taasisi inayojishughulisha na watoto hao,Doris Mollel.
Meneja wa Vodacom Foundation, Sandra Oswald akiwa amembeba mtoto aliyezaliwa kabla ya wakati (Njiti) Emmanuel Evodius katika hospitali ya Mkoa wa Pwani Tumbi alipofika hospitalini hapo kwa ajili ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani zaidi ya Shilingi Milioni 6/- kwa ajili ya kuwasaidia watoto hao vilivyotolewa na Vodacom Foundation,wengine katika picha kushoto ni Mama wa mtoto huyo,Emireta Evodius na Mkurugenzi wa Taasisi ya inayojishughulisha na watoto hao,Doris Mollel.

Tanesco watakiwa kufanya kazi na wazalishaji wadogo

0
0
Asteria Muhozya na Rhoda James - Njombe

Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo ameanza ziara yake Mkoa wa Njombe kwa kutembelea Mradi wa Kufua Umeme kwa kutumia mabaki ya miti ya Miwati (TANWAT.)

Baada ya kukagua mradi huo, Prof Muhongo ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kufanya majadiliano na TANWAT ili waongeze uzalishaji kutoka Megawati 2.5 za umeme hadi kufikia Megawati 10.

Aidha, ameagiza TANESCO na Wakala wa Nishati Vijijini REA kufanya majadiliano na TANWAT ili kuanza kununua nguzo zinazozalishwa na kampuni hiyo yenye uwezo wa kuzalisha nguzo 120,000 kwa mwaka badala ya kununua nguzo hizo katika nchi za Kenya, Zambia, Uganda na Afrika Kusini.

"REA na TANESCO watakuja hapa kuangalia hizi nguzo na kufanya ukaguzi kama zinakidhi viwango vya TANESCO. Ikiwa zinakidhi viwango REA wawaelekeze Wakandarasi kununua nguzo za TANWAT kwa kufuata taratibu za manunuzi," ameongeza Prof. Muhongo.

Pia Prof. Muhongo amewataka TANESCO kubadilika kiutendaji na kuongeza wigo wa uzalishaji umeme kwa kuwatumia wazalishaji wakubwa, wa kati na wadogo ambao wote kwa pamoja watasaidia kuondoa tatizo la uhaba wa nishati hiyo.

Akikagua Mradi wa kufua umeme wa Uwemba, Prof Muhongo ameiagiza  TANESCO Njombe kuandaa orodha ya vyanzo vya umeme vinavyotokana  na maji vilivyo katika gridi na visivyo katika gridi na kujadiliana na wazalishaji  ili kukubaliana nao kuuziana umeme

"Uzalishaji umeme kutumia maji ndio rahisi zaidi. TANESCO angalieni orodha hiyo, wawaeleze Mikataba yao muone namna ya kuuziana umeme. Bila umeme huwezi kuzalisha ajira na bila umeme wa uhakika hatuwezi kuwa na viwanda vya kutosha," alisema.

Waziri Muhongo ameongeza kuwa ni wajibu wa Serikali kuwasaidia na kufanya kazi na wazalishaji wadogo wa umeme ili waweze kuongeza  kiwango cha uzalishaji umeme hivyo pia ameutaka Mkoa wa Njombe kufuatilia kwa pamoja na TANESCO suala hilo na kulifanyia kazi.

Vilevile, aliwataka TANESCO kukaa na wazalishaji wadogo ili kuangalia bei zao, jambo ambalo litaiwezesha Serikali kujua bei kwa lengo la kuhakikisha kwamba bei hizo hazimuumizi mwananchi.

Aidha, Profesa Muhongo aliwaagiza TANESCO kufanya ukarabati wa mashine zilizoharibika ili ziendelee kufanya kazi kwa ajili ya kuongeza uzalishaji.

Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Jackson Saitab aliahidi kuyafanyia kazi maagizo yote ya Waziri na kuongeza kuwa, nishati ni sekta muhimu hata katika uongezaji thamani ya mazao.

NAIBU WAZIRI MASAUNI AWAONYA WANAOCHAFUA SERIKALI KUHUSIANA NA OPERESHENI KAMATA WAHAMIAJI HARAMU.

0
0
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi akisalimiana na Naibu Kamishna wa uhamiaji Haji Hamza wakati alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi za Uhamiaji Zanzibar zilizopo katika eneo la Kilimanim, kulia ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Sururu.
 Naibu Waziri wa Mmambo ya Ndani ya Nnchi Hamad Masauni akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Kamishina Mkuu wa Uhamiaji Zanzibar alipofanya ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kujionea shughuli za kiutendaji katika ofisi hizo zilizoko Kilimani Zanznibar.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni akizungumza na wananchi wa Visiwani Zanzibar waliokuwa wakisubiri huduma katika ofisi za Uhamijia  alipofanya ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kujionea shughuli za kiutendaji  zilizoko Kilimani Zanzibar.
(IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO MAMBO YA NDANI YA NCHI).

WANACHI WASHAURIWA KUTUMIA KITUO CHA KURATIBU MATUKIO YA SUMU

0
0
Mratibu wa Kituo cha kuratibu matukio ya sumu nchini toka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Bw. Yohana Goshashy akiwaeleza waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam. kuhusu umuhimu wa kituo hicho hapa nchini ikiwemo kuwakinga na madhara ya sumu kwa kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya kemikali mbalimbali.kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Frank Mvungi.

(PICHA NA BENEDICT LIWENGA- MAELEZO).

Na Jovina Bujulu –Maelezo
SERIKALI imewataka wananchi kutumia kituo cha kuratibu matukio ya sumu wapatapo madhara yatokanayo na Sumu kote nchini.

Hayo yamesemwa na Mratibu wa Kituo hicho kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Bw. Yohana Goshashy wakati wa mkutano na Vyombo vya habari leo Jijini Dar es salaam.

“kwa sasa matukio mengi yanayotolewataarifa kituoni hapo ni dawa za kulevywa na dawa za kuulia wadudu waharibifu kwenye mimea(viuatilifu)” Alisema Ndudu Goshashy.

Akizungumzia majukumu ya kituo hicho Ndugu Goshashy alisema kuwa ni pamoja na kutoa taarifa za matukio ya sumu, kuzuia ajali za kemikali na kuratibu matukio ya Sumu, uchunguzi na utambuzi wa sumu mbalimbali na kufanyatafiti mbalimbali zinazohusiana na kemikali na sumu.

Aidha Ndugu Goshashy alisema kuwa kituo hicho kina wajibu wa kuzitahadharisha mamlaka husika juu ya uwepo wa viashiria vya athari za sumu ili hayua stahiki ziweze kuchukuliwa kuzui athari hizo.

“Taarida za tahadharizinaweza kusaidia kuweka mfumo wa udhibiti na usimamiaji wa kemikali na sumu kuweka alama ya utambulisho au kuiondoa bidhaa sokoni” alisema Ndugu Goshashy.

Akizungumiza utoaji waelimu kwa umma kuhusu huduma zitolewazo na kituo hicho Ndugu Goshashy alisema kwamba wanaelimisha kuputia vyombo vya habari, kutoa namba za simu na kuchapisha vipeperushi na kuisambaza.

“Tunatoa ushauri kuhusiana na dawa za kulevya, jinsi ya kuyaepuka na kushauri aina sahihi za vifumbua sumu” aliongeza Ndugu Goshashy.

Aidha ndugu Goshashy aliwashauri wananchi kuepuka madhara yanayoweza kutokea na kutoa taarifa za matukio mbalimbali kama kula, kunywa au kuvuta.
Mratibu wa Kituo cha kuratibu matukio ya sumu nchini toka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Bw. Yohana Goshashy akiwalezea waandishi wa Habari kuhusu kuanzishwa kwa kituo cha KuratibuMatukio ya sumu hapa nchini ambacho ni sehemu ya Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali.Baadhi ya waandishi wa Habariw akifuatilia mkutano wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali na Vyombo vya Habari uliofanyika leo Jijini Dar es salaam leo.

TAARIFA YA UTEUZI WA WABUNGE KWENYE KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE

Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images