Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

Magavilla's Take - Magufuli's first two months...

$
0
0
 President Dr. John Pombe Joseph Magufuli's first two months have been nothing less than eventful; so eventful that we may be missing the point. So as I make a return to this platform I chose to reflect on what is at stake and what these two months could mean as a result.
First off, the next five years can be anything else but business as usual. With 58% of the Presidential votes, 2015 was the lowest victory margin secured by CCM in our 20 year old multiparty democracy!
Also worth noting is that Dr Magufuli is by many measures an 'unexpected' President. Just as much as most people didn't expect him to be President, there are many more who didn't and still don't know what to expect from him as President.
His initial blows were just as targeted as they were hard hitting: working without a cabinet for a record 1month, exposing tax evaders, unseating one suspected culprit after the other, speaking his heart's truth while making the establishment types cringe; sending a clear message of a no nonsense work ethic. This coupled with budget.
Yet it is quickly becoming evident with detractors throwing some blows of their own on such matters as the 'real' size of his government, some 'suspect' appointments in his newly formed cabinet and the dramatization of his signature unannounced visits, that he is not completely removed from scrutiny and judgment.
Yet, one cannot help but commend, with admiration, the sheer gravity of the impact of his first two months. It's always suspect when global media draws attention to anything positive out of Africa. 
But this in itself is telling as most global media outlets that gave a nod of approval to the 'Magufuli Fever' were simply in a state of shock that 'there was an African leader with common sense and willing to use it'; I wouldn't really call this positive news on Africa.

READ MORE HERE

DRFA YAJIVUNIA TUZO YA SAMATTA KUWA MCHEZAJI BORA AFRIKA

$
0
0
Chama cha soka mkoa wa Dar es salaam DRFA,kimeeleza kufurahishwa kwake na ushindi wa tuzo ya mchezaji bora barani afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani,aliyoipata mtanzania Mbwana Samatta,baada ya kuwabwaga wenzake wawili kwenye kinyang’anyiro hicho,akiwemo mchezaji mwenzake wa TP Mazembe,Kipa Robert Kidiaba pamoja na Mualgeria,Baghdad Boundjah anayeichezea klabu ya Etoile Du Sahel.

Mwenyekiti wa DRFA,Almas Kasongo,amesema kamati yake ya utendaji ilianza kuwa na matumaini makubwa ya Samatta kushinda tuzo hiyo,baada ya kuibuka kuwa mfungaji bora katika michuano ya klabu bingwa Afrika na kuisaidia timu yake ya TP Mazembe kutwaa taji hilo kubwa barani Afrika kwa upande wa vilabu.

Kasongo amesema,tuzo aliyoipata Samatta imechangiwa pia kwa kiasi fulani na usimamizi mzuri wa chama chake cha mkoa kwa vilabu alivyowahi kucheza kabla ya kujiunga na Mazembe,ikiwemo African Lyon na Simba SC,ambavyo vyote maskani yake ni jijini Dar es salaam.

Amesema Samatta ameandika historia ya aina yake kwa kuipeleka Tanzania katika ramani ya soka barani afrika,kwa kuwa tuzo hiyo haijawahi kuletwa na mchezaji yeyote yule kuwahi kutokea hapa nchini.

Kasongo ameongeza kuwa DRFA,itaendelea kuunga mkono juhudi za wachezaji wote wanaojituma kusaka mafanikio ndani na nje ya chini,ikiwa ni pamoja na kuunga mkono juhudi za vyama vingine vya soka vya mikoa katika harakati za kusimamia na kuharakisha maendelea ya mpira wa miguu kwa faida ya taifa zima.

WAZIRI NAPE NNAUYE AKUTANA NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI LEO JIJINI DAR

$
0
0
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Mh.Nnape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na na baadhi ya Wakuu wa Idara ya Habari Maelezo na Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari  mapema leo,alipokutana nao na kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabiri tasnia hiyo,mkutano huo umefanyika kwenye moja ya ukumbi ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar.
  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Mh.Nnape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na na baadhi ya Wakuu wa Idara ya Habari Maelezo na Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari 

 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Mh.Nnape Nnauye akizungumza na Wahariri wa vyombo vya habari (hawapo pichani),mapema leo jijini Dar,kwenye mkutano uliohusu kujadili mambo mbalimbali zikiwemo changamoto zinazoikabiri tasnia ya habari hapa nchini.Pichani kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda na kushoto ni  Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa . 
 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa akiwakaribisha Wahariri wa vyombo vya habari (hawapo pichani),mapema leo jijini Dar,kwenye mkutano ulioitishwa na Waziri Nape kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali yanayoikabiri tasnia ya habari hapa nchini.Pichani kati ni Waziri Mh.Nape pamoja na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda akitoa muongozo kwa Wahariri wa Vyombo vya habari (hawapo nchini) kuhusina na mkutano wao ulioitishwa na Waziri Nape kujadili mambo mbalimbali na changamoto zinazoikabiri tasnia hiyo kwa ujumla.
 Baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano huo wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa ukumbini humo.
 Mmoja wa Wahariri Kurwa Kaledia kutoka New Habari Hause akiomba ufafanuzi wa jambo kwa Mh Waziri Nape huku baadhi ya wahariri wakifuatilia kwa makini.

PICHA NA MICHUZI JR -MMG

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

TASWIRA ZA VIJANA WAKIVUA SAMAKI KATIKA MFEREJI WA MAJI YOMBO BUZA

$
0
0
Katika pita pita za Mtaa kwa Mtaa, nilibahatika kufika eneo la Yombo Buza Wilayani Temeke jijini Dar. nikiwa eneo la Buza Mwisho nilikutana na kundi la watu likiwa limejikusanya kando kando ya mfereji wa maji unatenganisa kati ya Buza na Mwanagati. nilijisogeza mpaka lilipo kundi hilo ili kufahamu zaidi ni jambo gani lililopo pale, Nilipofika nilikuta kuna kundi kubwa la Watoto wakiwa ndani ya Mfereji huo, nilipouliza kulikoni?? niliambia na baadhi ya watu niliowakuta pale kuwa watoto hao wanavua Samaki ambao walijitokeza kwa wingi wakati wa zoezi la kuyaondoa maji hayo ili mfereji huo ufanyiwe usafi. Nilishangazwa kidogo na hali ile, kwani ilikuwa ni ngeni machoni mwangu, na hapo ndipo nikajiuliza kuwa uvuvi huu ni halali au ni haramu?? lakini ukiachana na hilo, je,usalama wa afya ya vijana hawa uko wapi?? kuna kupona kweli kwa magonjwa ya mlipuko?? bado sikupata majibu na baadae nikaishia zangu kuendelea na majukumu mengine ya ujenzi wa Taifa.
 Hapa zoezi la Uvuvi likiendelea huku baadhi ya watoto hao, wakiwa wamefanikiwa kupata vitoweo vyao.
 Mwanzo nilidhani ni Watoto tu waliokuwa wakijishughulisha na Uvuvi, huo nilipohamia upande wa pili nilikutana na wengine lakini hawa sasa ni vijana wakubwa.

Wakazi wa Magomeni mjini Morogoro kuhamishwa kutoka mabondeni

$
0
0
Halmashauri ya wilaya wilaya ya kilosa mkoani Morogoro imepanga kuwahamisha wakazi wote wanaoishi katika kata ya Magomeni wilayani humo kutokana na kata hiyo kuwa bondeni hali ambayo inapelekea kuwa inakumbwa na mafuriko kila mwaka. 
Kufuatia mvua zilizonyesha wilayani humo na kusababisha mafuriko mnamo tarehe 4 na 5, Januari, 2016 katika kata hiyo yenye vitongoji 8, kati ya hivyo vitongoji 5 viliathirika na mafuriko sawa na asilimia 62.5 ya vitongoji vilivyoathirika na mafuriko hayo. 
 Akitoa taarifa ya athari ya maafa hayo kwa Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen. Mbazi Msuya aliyetembelea maeneo yaliyoathirika na maafa katika wilaya hiyo tarehe 9 Januari, 2016, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, Idd Mshili alisema, katika kata hiyo Jumla ya nyumba 248 zimebomoka, nyumba 834 ziliingiliwa na maji na kaya 1,494 zenye watu 6,243 wameathirika na mafuriko. 

“Tumeamua kuwa na suluhisho la kudumu la mafuriko katika kata hii iliyopo mabondeni , kwa kuwapeleka eneo salama. Tumeshaainisha eneo hilo kule Masugu lenye ukubwa wa ekari elfu 7, ambapo tutawagawia bure viwanja wakazi watakao hamia eneo hilo ambalo kimsingi tumelenga pia kuwaweka karibu na mashamba yao ili waweze kuendelea na shughuli za kilimo ambazo wakazi wengi wa hapa wanajishughulisha” alisema.

Mshili Mshili alifafanua kuwa Halmashauri katika mipango yake ya muda mrefu inakusudia kupima viwanja kwenye eneo la Halmashauri ambalo awali lilitolewa kwa ajili ya kupima mashamba ili wananchi ambao wameathirika na amabao hawako kwenye orodha ya waliopewa awali waweze kupewa na kuhamia kwenye viwanja vitakavyopimwa. 

Akiongea baada ya kutembelea maeneo yaliyoathirika na maafa katika wilaya hiyo Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen. Mbazi Msuya aliwashauri wawashirikishe wadau na wananchi katika kuchukua hatua za muda mfupi za kukabili maafa hayo kwa kuchimba mitaro ya maji katika kata ya Magomeni.

“Halmashauri mkifanikiwa kuchimba mitaro Ofisi ya Waziri Mkuu itawapatia mifuko ya Saruji ya kujengea mitaro hiyo ili kuweza kusafirisha maji hadi mto mkondoa badala ya kuingia katika makazi ya watu ambao wanaishi hapa kabla hamjawaamisha” alisisitiza Msuya.
 Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen. Mbazi Msuya (wa kwanza kushoto) akijadiliana na viongozi wa Kata ya Magomeni, wilayani Kilosa   mkoani Morogoro, na  watendaji wakuu wa wilaya hiyo mipango ya kukabili na kupunguza  athari za maafa katika kata hiyo leo tarehe 9 Januari, 2016.
 Sehemu ya barabara iliyoathiriwa na mafuriko yaliyotokea tarehe 4 na 5 Januari mwaka huu katika Kata ya Magomeni, wilayani Kilosa   mkoani Morogoro. Jumla ya kaya 1, 494 zimeathirika na mafuriko hayo.
 Moja ya nyumba iliyoathiriwa na mafuriko yaliyotokea tarehe 4 na 5 Januari mwaka huu katika Kata ya Magomeni, wilayani Kilosa   mkoani Morogoro. Jumla ya nyumba 248 zimeathirika na mafuriko hayo katika kata hiyo.
Mkazi wa Kata ya Magomeni, wilayani Kilosa   mkoani Morogoro, Bi. Prisca Michel akianika madaftari yaliyoharibiwa na maji  baada ya kuingia katika Duka lake la kuuza vifaa vya shule kutokana na mafuriko yaliyotokea tarehe 4 na 5 Januari mwaka huu. katika wilaya hiyo jumla ya nyumba 1980 zimeingiliwa na maji. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI NAPE ATOLEA UFAFANUZI SUALA LA MALIPO YA KOCHA WA TIMU YA TAIFA

Nyumbani na Diaspora with Jeann Milken

$
0
0
Kwenye ' Nyumbani Na Diaspora' kilichorushwa jana usiku TBC1, Maggid Mjengwa amezungumza na mwanadiaspora Jean Miliken aliyerudi nyumbani na kuamua kufanya kazi Iringa. Jean Milliken ni mzaliwa wa Mtama, Lindi, ni mzazi, mwalimu na aliyepitia shule maalum ya kijeshi kule Tabora. Ana mengi ya kusema kuhusu safari yake ya kimaisha.

KIJIJI CHA NANJILINJI A CHATOA RUZUKU KWA WA MAMA WAJAWAZITO

$
0
0
Na Ahmad Mmow, Kilwa-LINDI.
Uhifadhi wa msitu katika kijiji cha Nanjirinji A, wilayani Kilwa mkoani Lindi, umeendelea kuwanufaisha wananchi wakazi wa kijiji hicho baada ya kuanza kuwapatia ruzuku akina mama wajawazito wanaoishi katika kijiji hicho.
Kilwa
Hayo yameelezwa na mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho, Jafari Nyambate, mwanzoni mwa wiki hii alipozungumza na Lindiyetu.com mjini Kilwa masoko. 
Nyambate alisema baada ya kutekeleza miradi mbalimbali ya jamii kwa kutumia fedha zilizotokana na mauzo ya mazao ya msitu waliohifadhi, unaofahamika kwa jina la Mbumbila, Kijiji kimeanza kuwapa ruzuku ya shilingi 30,000 akina mama wajawazito wakazi wa kijiji hicho, ikiwa ni mchango wa maandalizi ya gharama za matibabu wakati wakujifungua.
"Fedha hizo zinatolewa kwa mama ambaye mimba yake imefikisha umri wa miezi tisa, muda ambao anatarajia kujifungua ili aweze kufanya maandalizi ikiwamo kununua vifaa vitakavyotumika wakati huo,"alisema Nyambate.

Alibainisha kuwa huo nimwendelezo wa huduma mbalimbali za jamii zilizotekelezwa kutokana na mapato ya msitu huo. Ambapo baada ya kufanikiwa mpango huo,wanajipanga kuanza kutoa ruzuku kwa wazee wasiojiweza.
Mwenyekiti huyo aliitaja baadhi ya miradi iliyotekelezwa kutokana na mapato ya msitu huo kuwa ni vyumba vi 3 vya madarasa ya shule ya msingi, visima vifupi 7 vya maji, soko, vyoo vya kudumu vya shule ya msingi vyenye matundu 6.
Aliitaja miradi mingine kuwa ni pamoja na nyumba moja ya mwalimu, madawati 26, bomba la maji la shule na viti 100 vinavyotumika wakati wa mikutano mikuu ya kijiji.
Hata hivyo pamoja na mafanikio hayo, mwenyekiti huyo alisema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali. Ikiwamo uvamizi unaofanywa na wakulima, hasa wa zao la ufuta ambao wanalazimisha kuendesha shughuli za kilimo ndani ya msitu waliouhifadhi.
"Lakini pia wapo wanaopasua mbao kwa njia haramu, nao wanatusumbua sana ila tunakabiliana nao kwa kufanya doria za mara kwa mara, hasa baada ya kamati ya maliasili kuwezeshwa pikipiki tatu zinazotumika kwa doria," aliongeza kusema.
Uvunaji katika msitu huo wenye hekta 61724, ulianza rasmi mwaka 2012.

UFUNGUZI WA JENGO LA WAGONJWA WA NJE HOSPITALI YA KIVUNGE KASKAZINI UNGUJA

$
0
0
kutimia miaka 52
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwyinyihaji Makame kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akikata utepe  kufungua Jengo la Wagonjwa wa Nje Hospitali ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja lililojengwa na Shirika lisilokuwa la kiserikali kutoka Uingereza (HIPZ) ikiwa ni katika shamra shamra za Mapinduzi matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52 (wa pili kushoto) Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo Jecha
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwyinyihaji Makame (kushoto) pamoja na Viongozi wa Wizara ya Afya wakiangalia Uodhoreshaji majina kwa wagonjwa wanaofika Hospitali kwa njia ya Mtandao baada ya kufungua Jengo la Wagonjwa wa Nje Hospitali ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja leo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, sherehe hizi ni katika shamra shamra za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia miaka 52,(wa pili kushoto) Dr,Alexander Vogt wa kujitolea wa Shirika la HIPZ kutoka Uingereza
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwyinyihaji Makame Mwadini (kushoto) akimsalimia Mtoto aliyefika kupima Nazna Ali Silima,miezi 5 uzito kilo 7.3 katika Hospitali ya Kivunge wagojwa wa nje,baada ya kifungua Hospitali hiyo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,jengo hilo limejengwa kwa ufadhili wa Shirika lisilo la kiserikali (HIPZ) kutoka Uingereza,(katikati) Dkt.Tamim Hamad Said Daktari Dhamana Hospitali ya Kivunge na Muuguzi Filonema Raumond Woga.


MAANDALIZI YA JUBILEE YA MIAKA 50 YA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA RUGAMBWA YA BUKOBA

$
0
0

Jumuiya ya wana-Rugambwa (Rugambwa Girls Foundation) wanayo furaha kukualika kwenye mkutano wa pamoja utakaofanyika tarehe 23 Januari, 2016 kuanzia saa 7 mchana, Leaders Club jijini Dar es salaam.


Ukiwa kama mdau wa Rugambwa Sekondari: mwanafunzi, mwalimu, mtumishi wa aina yoyote aliyewahi kupita Rugambwa Sekondari pamoja wanafunzi wote waliosoma shule rafiki za Rugambwa (Ihungo, Kahororo, Bukoba Sekondari, Nyakato, Ntungamo Seminari, n.k. tunakualika kushiriki.

Lengo ni kukutana kubadilishana mawazo na kupeana mikakati jinsi ya kupata fedha kwa ajili ya kufanikisha jubilee ya miaka 50 ya Rugambwa Sekondari itakayofanyika, Machi 2016 pamoja na ukarabati na uboreshaji wa shule hiyo.
Atakayesikia au kusoma tangazo hili amfahamishe na mwingine.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na:
Rugambwa Girls Foundation

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA MHE. MWIJAGE ATEMBELEA TBL

$
0
0

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijage(kulia) akipata maelezo kwa mwendesha mitambo wa kampuni ya TBL, Mecky Mlay alipotembelea mitambo ya uzalishaji wa bia kwenye kiwanda hicho. Kulia (kwake) ni Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Roberto Jarrin na Meneja wa Kiwanda cha Dar es Salaam, Calvin Martin.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijage(kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kiwanda cha Dar es Salaam, Calvin Martin

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijageakifuahia jambo aliowasili kwenye mitambo ya uzalishaji wa bidhaa za TBL.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijage(kushoto) akipata maelezo kwa mmoja wa wafanyakazi wa TBL alipotembelea mitambo ya uzalishaji wa bia kwenye kiwanda hicho. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Roberto Jarrin na Meneja wa Kiwanda cha Dar es Salaam, Calvin Martin. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Waziri Nape atolea ufafanuzi kuhusu mapokezi ya Samatta.

Article 2

$
0
0
Watu wengi wamekuwa wakilalamika ifikapo Jumamosi wanakuwa wamechoka  kwa usiku wa jana yake yaani ijumaa, na wengine hushindwa kufanya shughuli zao muhimu kwa ufanisi siku ya Jumatatu sababu ya uchovu wa wikiendi,  je ni siku ipi nzuri kwa starehe?. JovagoTanzania inakupa njia sahihi za kufurahia wikiendi yako kuanzia Ijumaa mpaka Jumapili.

1.       Ijumaa

Hii ni siku ndani ya siku za kazi, baadhi ya watu humaliza kazi zao kuanzia saa sita mchana na ofisi nyingine hadi jioni.  Je ni muhimu kutoka siku hii?  Jibu ni inategemea na umuhimu wa siku ya kesho yake (Jumamosi) au jinsi ya mtoko uliouandaa.  Ukiangalia kwa undani zaidi hii siku nzuri sana kwa kupunguzia uchovu wote wa wikinzima kazini, unaweza kutoka na wafanyakazi wenzako sehemu mbali mbali za starehe,  lakini pia  ni siku nzuri ya kuikaribisha vyema siku ya pili yake ambayo ni Jumamosi, hivyo unashauriwa kama unakunywa kunywa kidogo sana, jaribu kufanya starehe ambayo haitakuchosha mwili wako mpaka ukashindwa kuamka siku nzima ya Jumamosi au ukashindwa kurudi nyumbani kabisa.


2.       Jumamosi

Jumamosi ni siku nzuri ya kutoka kwa mapumziko lakini pia kuna baadhi ya watu huenda kazini na kurudi mchana, jaribu kuitumia siku hii ipasavyo kwani ni siku nzuri kwa kupunguzia uchovu wote wa jana (Ijumaa)  na wa wiki nzima.  Wengi hupendelea kwenda ufukweni mida ya mchana na jioni, na usiku kwenda sehemu za muziki tulivu, sinema, mpira au kwenda mbali na mji kama Bagamoyo.  Lakini pia kama siku ya Jumapili ni muhimu kwako jali muda wako ifikapo usiku na aina ya starehe utakayoifanya.


3.       Jumapili.


Siku ya Jumapili itumike kwa umakini kwani huikaribisha siku ya kazi ambayo ni Jumatatu. Unaweza kuwa ulienda mbali na mji siku ya jumamosi, basi jaribu kurudi mapema nyumbani. Pia ni siku nzuri kwa sinema, mpira na kupiga stori nyumbani au kutembelea ndugu na marafiki. Hakikisha siku hii haikuharibii siku ya kazi ambayo ni Jumatatu, bali ikupe uhuru wa kurudisha nguvu zako kazini.

SIMU TV: HABARI K UTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

KITUO CHA MAZOEZI CHA MANGO KINONDONI CHAADHIMISHA MIAKA 15 TANGU KUANZISHWA

$
0
0
Jumanne tarehe 12 Januari 2016 Kituo cha Mazoezi cha Mango kilichopo Kinondoni kitaadhmisha miaka 15 tangu kuanzishwa.
Uongozi wa kituo umeandaa Bonanza la kukata na shoka ambapo wanamazoezi wote chini ya waalimu wao mahiri akiwemo Chambuso,Simba, Sukamba na Mr.Nice watashiriki katika mazoezi mbalimbali ya viungo kuanzia saa kumi na mbili asubuhi na kisha kufuatiwa na michezo mbali mbali ikiwemo ngumi, kuvuta kamba, kukimbia na gunia,kunyanyua vitu vizito na kutunisha misuli na baadaye viburudisho na muziki.
Karibuni sana wapenzi wote wa michezo mujumuike nasi.

SIMU TV: UCHAMBUZI WA MAGAZETI YA LEO

$
0
0

CH10: Ma RC na DC wapya wachunjwa, Msururu wa viongozi kuelekea Ikulu, Vigogo watakatisha bomoa bomoa Dar, Utata wagubika kutoroka kwa mtuhumiwa wa meno ya tembo, Mawaziri wavuruga uchaguzi. Tazama yaliyoruhusiwa na wahariri magazetini leo.https://youtu.be/AWMMGce_w-w  

TBC ;Umeya wa Ilala na Kinondoni Moto, Msimamizi mkuu bomoabomoa atekwa na kuteswa; Kwa habari zaidi tazama uchambuzi wa magazeti ya leo; https://youtu.be/YwQBKRFiRg8

WIZARA YA MAJI YASHTUSHWA NA KASI YA DAWASCO

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Mbogo Futakamba akitoa zawadi kwa mfanyakazi bora wa mwaka 2015 toka DAWASCO wakati alipotembelea Shirika hilo mapema wiki hii. Pamoja na mambo mengine alielekeza shirika juu ya utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Serikali ya kuunganisha Wateja Milioni Moja ifikapo June 2016. Picha na Everlasting Lyaro- DAWASCO.

WIZARA ya maji na umwagiliaji, imesema inaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mipango ya usambazaji wa huduma za maji, inayofanywa na shirika la majisafi na majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO) na kutoa rai kwa watumishi wa shirika hilo kushirikiana ili kufikia malengo ya utoaji wa huduma kwa wananchi.

Hayo yalisemwa jana na katibu mkuu wa wizara hiyo mhandisi Mbogo Futakamba, alipokuwa akiwahutubia wafanyakazi wa DAWASCO, katika makao makuu ya shirika hilo jijini Dar es Salaam.

Mhandisi Futakamba, alisema kasi ya utoaji wa huduma bora za maji kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam, imepunguza malalamiko mengi ya wananchi, na kwamba serikali imeanza kupata matumaini makubwa na kujenga imani kwa shirika hilo kwa kufanikisha malengo makuu ya usambazaji wa huduma hiyo kwa wananchi.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

EWURA YASEMA NCHI INA AKIBA YA KUTOSHA YA MAFUTA

$
0
0
Mkurungenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji (EWURA), Felix Ngamlagosi akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam jana juu ya takwimu dhahiri kuwa nchi ina akiba ya kutosha ya mafuta na wataendelea kupokea shehena za mafuta kama kawaida na kwa kiasi kitakachoendelea kutosheleza mahitaji ya nchi.
Wandishi wa habari wakimsikiliza Mkurungenzi wa Mkuu wa Mamlaka wa Udhibiti wa Huduma Nishati na Maji (EWURA), Felix Ngamlagosi. Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii

SHUJAA WETU MBWANA SAMATTA ALIVYOPOKELEWA NA WADAU WA SOKA MAENEO MBALIMBALI JIJINI DAR

$
0
0
Msafara wa magari uliokuwa umembeba Mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika wa Wachezaji wa Ndani 2015, Mbwana Samata,ulionaswa na Camera ya Globu ya jamii maeneo ya Morocco jana jioni ukitokea hoteli ya Kempinsk baada ya kuzungumza na vyombo vya habari,Msafara huo akiwemo Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye ulipita maeneo kadhaa ya jiji la Dar na kukomea katika kiota cha Escape One Mikocheni jijini Dar,ambako alikutana na kupongezwa na Wadau mbalimbali wa tasnia ya Michezo.Mwanasoka huyo aliwasili juzi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam akitokea Abuja, Nigeria katika hafla ya utoaji tuzo kwa mwanamichezo bora.
PICHA NA MICHUZI JR-MMG.
Baadhi ya Waendesha Boda boda nao hawakuwa na hiyana kuunga mkono mafanikio ya Mbwana Samatta,ambayo yameiletea heshima kubwa nchi yetu.
Msafara wa Mbwana Samatta ukikatiza maeneo ya Morocco
Baadae akawasili viwanja vya Escape One akiwa ameambatana na Waziri Nape Nnauye tayari kwa kukamilisha ratiba nyingine,pia alipata selfie na washabiki wa soka kama uonavyo pichani
Baadae akawasili viwanja vya Escape One akiwa ameambatana na Waziri Nape Nnauye tayari kwa kukamilisha ratiba nyingine,pia alipata selfie na washabiki wa soka kama uonavyo pichani
Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kazini,huku Nyota wetu Mbwana Samatta akiwa amepozi na tuzo yake ya mchezaji bora wa Afrika.
Samatta akipata picha ya pamoja na Waziri Mh.Nape Nnauye.
Wadau wa Soka wakijadiiana jambo,wakati huo Samatta anafanya mahojiano ya hapa na pale na baadhi ya vyombo vya habari
Kutoka kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Mazingira na Muungano) Mh. January Makamba sambamba na Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauyewakijumuika pamoja kwenye hafla fupi ya kumpongeza Mbwana Samatta ndani ya kiota cha maraha-Escape One Mikocheni jijini Dar
Kutoka kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Mazingira na Muungano) Mh. January Makamba sambamba na Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh.Nape na wadau wengine wa soka wakijumuika kwa pamoja kumpongeza Samatta. PICHA NA MICHUZI JR-MMG.

SIMU TV: BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU YATUPIWA LAWAMA

Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images