Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1083 | 1084 | (Page 1085) | 1086 | 1087 | .... | 3282 | newer

  0 0

  Kamera yetu ikiangazia Taswira mbalimbali za Jiji la Mbeya hii leo..., Pichani hapo juu ni kipita Shoto kikuu cha Mkoa wa Mbeya kilichopo katikati ya Jiji  njiapanda ya kuelekea Sokomatola, Uyole, Uhindini na Uzunguni..
  Utulivu mwanana Barabara ya Uhindini..
  Pilika pilika za hapa na pele katika Stendi ya Daladala Kabwe Jijini Mbeya...
  PICHA NA MR.PENGO MBEYA.

  0 0


  0 0

  SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS), limeamuru shehena ya mafuta ya petroli iliyoagizwa kutoka Falme za Kiarabu irejeshwe ilikotoka kutokana na kubaini hayana ubora unaotakiwa kwa matumizi ya magari na mitambo.


  Akitoa taarifa hiyo Dar es Salam jana, Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Joseph Masikitiko alisema, vipimo vya maabara vya sampuli ya mafuta hayo vimeonesha kuwa hayafai kwa matumizi. Alisema hayo ni matokeo ya ukaguzi wa hivi karibuni wa shehena hiyo yenye ujazo wa tani za metriki 38,521.018 katika meli ya MT. Ridgebury John B, yaliyokuwa yasambazwe na kuuzwa nchini.

  Alisema, "Vipimo vinaonesha kuwa baadhi ya matakwa ya viwango vya mafuta ya petroli hayajafikiwa, hivyo kuamuru yarejeshwe yalikotoka. Kiwango cha ubora cha mafuta ya petroli ni TZS 672:2012/ EAS 158:2012 ambacho hakikufikiwa".

  Matakwa ya kiwango ambacho mafuta hayo hayakukidhi ni pamoja na kuwa na kemikali zilizo na oksijeni ndani yake ambazo husababisha madhara kwenye injini za magari na mitambo.Alisema, "Kiwango cha petroli hakiruhusu uwepo wa kemikali hizo kwenye mafuta hayo kwa sababu zinaua injini, kuhatarisha afya za watu na kuharibu mazingira kutokana na kusababisha moshi mchafu mwingi".

  Alifafanua kuwa mafuta hayo yameonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kuvuta maji au mvuke na kuwa sehemu ya petroli, kiasi cha kuifanya iwe na maji mengi ambayo ni hatari kwa injini za magari na mitambo.

  Pia, alieleza uhafifu mwingine katika mafuta hayo kuwa ni kupungua kwa nguvu ya kuendesha injini au mitambo hivyo kusababisha uharibifu na hasara. Aliongeza kuwa, mvuke unapokuwa mwingi kwenye petroli husababisha mtiririko wa mafuta kwenda kwenye injini kutokuwa mzuri, huku kemikali aina ya benzene iliyoonekana kuzidi katika petroli hiyo ikiwa ni chanzo cha kansa kwa wanaotoa huduma ya uuzaji wa mafuta hayo.

  Sambamba na hayo, Masikitiko aliongeza kuwa walibaini kuwa uhafifu katika mafuta hayo unaongeza wingi wa ujazo wa nishati hiyo pasipokuwa na uhalisia na kisha kutoa nguvu isiyolingana na wingi wake. Alisema, madhara yake ni mnunuzi kulipia wingi wa mafuta usio na thamani halisi.Aliwahakikishia watumiaji wa mafuta kuwa, shirika hilo litahakikisha linafanya ukaguzi katika meli zote zenye mafuta yanayokusudiwa kusambazwa nchini ili kuzuia yasiyo na ubora yasiingizwe sokoni.

  Katika hatua nyingine, Tbs ilisema kuwa iliagiza vilainishi vya mitambo na magari vya kampuni ya HASS Petroleum (T) Limited vyenye ujazo wa lita 16,080 kutoka Falme za Kiarabu virejeshwe vilikotoka pia kwa sababu ya kukosa ubora unaofaa kwa matumizi na kwamba mwagizaji alitekeleza agizo hilo tangu Desemba 31 mwaka jana.

  Ewura yazungumza Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) imekiri kufahamu kuhusu suala hilo na kueleza wananchi kuwa licha ya mafuta hayo kutakiwa kurejeshwa yalipotoka, bado nchi ina akiba ya petroli inayoweza kutumika hadi shehena nyingine iletwe."Wananchi wasiwe na wasiwasi," alisema Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa Ewura, Titus Kaguo. Alisema kwa siku nchi inatumia lita za petroli 2,700,000, na kwamba kila metriki tani moja ya petroli huwa na lita 700,000.

  "Kwa maana hiyo, lita 33,000,000 za petroli zilizokuja na kukataliwa endapo zingeshushwa na kutumika nchini zingeweza kutosheleza mahitaji kwa zaidi ya siku saba," alisema Kaguo . Hata hivyo, aliongeza kuwa si mafuta yote yanayoingia na meli bandarini hushushwa kwa ajili ya matumizi ya nchi, bali mengine huwa safarini kwenda nchi nyingine.


  0 0

  Mkuu wa Huduma za Rejareja wa First National Bank Tanzania, Francois Botha akimkabidhi Peter Kimune, mkazi wa Dar es salaam hundi ya shilingi milioni tano baada ya kuibuka mshindi wa kampeni ya benki hiyo kuhamaisisha uwekaji akiba ambayo imefikia tamati. Makabidhiano haya yamefanyika leo jijini Dar es Salaam. 
  Mkuu wa Masoko wa First National Bank, Blandina Mwachanga (kulia) akiongea na waandishi wa habari baada ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni tano kwa Peter Kimune (katikati) mshindi wa kampeni ya uhamasishaji kuweka akiba iliyokuwa ikiendeshwa na benki hiyo kwa muda wa miezi mitatu. Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha huduma za reja reja wa benki hiyo Francois Botha. 
  (Picha Mpiga Picha Yetu) 

  KAMPENI ya kuhamasisha Watanzania kujiwekea akiba zaidi iliyokuwa ikiendeshwa na First National Bank Tanzania kwa miezi miatu imefika mwisho huku mshindi wa tatu na wa mwisho akikabidhiwa zawadi ya shilingi milioni tano.

   Akizungumza kwenye hafla ya kuhitimisha kampeni hiyo na kumkabidhi zawadi Peter Kimune, mkazi wa Dar es salaam aliyeibuka mshindi wa mwezi Disemba 2015, Mkuu wa kitengo cha rejareja cha benki hiyo, Francois Botha alisema “imekuwa kampeni ya yenye mafanikio makubwa na ni furaha kuona wateja wengi wakijitokeza kushiriki.” “Kampeni hii haikuwa tu shindano bali pia imetoa somo na kuhamasisha Watanzania wengi kujitokeza kwenye kuweka akiba. FNB inaamini kwamba kupitia kampeni hii imeweza kuhamasisha Watanzania kuweka akiba kwa ajili ya mustakabali salama wa kifedha hapo badae. 

  Akiba inaleta uwezo wa kuwekeza siku zijazo na husaidia wakati wa dharula au pale unapotaka kutimiza mipango yako,” alisema Botha. Kampeni hiyo ya uwekaji akiba ilizinduliwa Oktoba, 2015 na kwa miezi mitatu imeweza kutoa nafasi kwa wateja wapya na wa zamani kuingia moja kwa moja kwenye droo kutokana na kila shilingi elfu hamsini waliyoweka kwenye akaunti zao.

   Akizungumza baada ya kukabidhiwa hundi ya shilingi milioni tano, mshindi huyo aliishukuru benki hiyo kwa kuanzisha mpango huo na kuongeza kuwa uwekaji akiba ni muhimu katika uhifadhi wa fedha binafsi na pia husaidia katika kujenga jamii imara yenye uhakika wa kuishi maisha bora.

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza (CCM) Stanslaus Mabula.

  Na:George Binagi.
  MBUNGE wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza Stanslaus Mabula (CCM, ameahidi kushughulikia suala la ujenzi wa maegesho ya magari makubwa ya mizigo nje ya jiji la Mwanza ili kuzuia magari hayo kuingia katikati ya jiji.

  Akizungumza ofisini kwake hii leo, Mabula amebainisha kuwa upo mpango wa kujenga maegesho hayo katika maeneo yaliyo nje ya Jiji la Mwanza, hatua ambayo itasaidia magari hayo kutoingia katikati ya Jiji na hivyo kuondoa malalamiko yaliyopo kutoka kwa madereva wa magari madogo ya mizigo wanaolalamikia uingiaji wa magari makubwa ya mizigo katikati ya jiji.

  Ameyataja maeneo yanayotarajiwa kujengwa maegesho hao kuwa ni Buhongwa pamoja na Igoma na kwamba baada ya ujenzi wake kukamilika, magari yote makubwa ya mizigo hayataruhusiwa kuingia katikati ya Jiji.

  Mabula ambae alikuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza katika uongozi uliomalizika mwaka jana, amebainisha kuwa utekelezaji wa ujenzi wa maegesho hayo unatarajiwa kufanyika kwa uharaka zaidi ambapo amewahimiza wawekezaji mbalimbali kujitokeza ili kushirikiana na halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa ajili ya kufanikisha ujenzi huo.

  Suala la magari makubwa kuingia katikati ya Jiji la Mwanza huku yakiwa na mizigo, linalalamikiwa na madereva wa magari madogo ya mizigo kwa kile wanachoeleza kuwa wanaingiliwa katika shughuli ambazo wao wangezifanya na hivyo kujiingia kipato ambapo wameiomba halmashauri ya Jiji la Mwanza kutoruhusu magari hayo kuingia katikati ya Jiji.
  Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza (CCM) Stanslaus Mabula.
  Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza (CCM) Stanslaus Mabula akiongea na wanahabari ofisini kwake.

  0 0

  Walimu (Msingi) wakishiriki mafunzo ya Kujenga Uwezo katika ufundishaji na ujifunzaji katika Mkoa wa Ruvuma. Mafunzo hayo yanawezeshwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA) kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

  MAMLAKA ya Elimu Tanzania kwa kushirikiana na  Wizara ya Elimu, Sayansi, na Teknolojia, na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imewezesha awamu ya pili ya Programu ya kujenga uwezo wa walimu na wanafunzi, kwa walimu mahiri (Msingi) wa masomo ya Hisabati, Kiswahili na Kiingereza  katika mikoa mitatu nchini; Songea, Katavi, na Singida.


  Lengo la mafunzo haya ni kuwawezesha walimu kuwatambua wanafunzi wenye uwezo mdogo kimasomo na kuwapatia mafunzo rekebishi; na kuwajengea uwezo ili wote wawe na uelewa unaolingana.


  Programu ya kujenga uwezo wa walimu na wanafunzi katika ufundishaji na ujifunzaji (Student Teaches Enrichment Program)  ni moja kati ya mikakati  9 iliyoibuliwa wakati wa maabara ya BRN katika sekta ya elimu ambao unatekelezwa kupitia mafunzo kwa walimu, na kufadhiliwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania.


  Awamu ya kwanza ya mafunzo haya ilihusisha  Halmashauri 40 ambapo jumla ya walimu 19,300 walipatiwa mafunzo kwa mwaka 2014/15. Hii ni awamu ya pili ya mafunzo haya ikihusisha halmashuri 60 ambapo jumla ya walimu mahiri 900 wanawezeshwa katika vituo 8 vilivyoteuliwa kuwa mwenyeji wa mafunzo haya, yanayolenga kuwafikia walimu 18,501 katika mwaka huu wa fedha 2015/2016.


  Mafunzo wezeshi kwa walimu wa sekondari wa masomo ya Kiingereza, Hisabati, Kiswahili, na Biology nayo yanaendelea kwa ufadhili wa Mamlaka ya Elimu Tanzania.

  0 0
 • 01/08/16--02:47: HONGERA KWA TUZO SAMATTA.
 • RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), Jamal Malinzi amempongeza mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya TP Mazembe ya Congo DR (Pichani) kwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani.
  Samatta ameshinda tuzo ya mchezaji bora kwa wachezaji wanaocheza Afrika baada ya kwashinda Robert Kidiaba (Congo DR) alieshika nafasi ya pili na Bounedjah Baghdad (Algeria) aliyeshika nafasi ya tatu.
  Kwa kushinda tuzo hiyo, Samatta amekua mchezaji wa kwanza kwa ukanda wa Afrika Mashariki kushinda tuzo kubwa barani Afrika.
  Pamoja na kushinda tuzo hiyo, Samatta pia amejumuishwa katika kikosi bora cha wachezaji wa Afrika kwa mwaka 2015 sambamba na Robert Kidiaba (Congo DR), Sergie Aurier (Ivory Coast), Aymen Abdenmor (Tunisia), Mohamed Meftah (Algeria), Sadio Mane (Senegal), Yaya Toure (Ivory Coast), Yacine Ibrahim (Algeria), Andrew Ayew (Ghana), Mbwana Samatta (Tanzania), Pierre-Emercik Aubameyang (Gabon) na Baghdad Bounedjah (Algeria).
  Mshambuliaji Mbwana Samatta alieyambatana na Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine wanatarajia kuwasili nchini leo saa 8 usiku kwa shirika la ndege la Ethiopia.

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amewataka watendaji na wafanyakazi wote wa Wakala wa ufundi na umeme (TEMESA), kufanya kazi kwa umoja, uwazi na uadilifu ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na kuhuisha ustawi wa wakala huo.


  Akitoa mwelekeo wa utendaji wa wakala huo wakati akizungumza na watendaji wa TEMESA Mhe.Prof. Mbarawa amesema Serikali ya awamu ya tano inaitaka TEMESA kufanya kazi kwa weledi ili kuongeza mapato na kuhudumia wateja wao  kikamilifu ili kuinua uchumi wa wakala huo na kuondoa malalamiko kwa wadau na watumishi.


  ‘Acheni kufanya kazi kwa upendeleo na usiri kwani huo ndio mwanzo wa hujuma na ubadhirifu hali inayochochea malalamiko na kudumaza huduma za TEMESA’, amesema Prof. Mbarawa.


  Prof. Mbarawa ameitaka TEMESA kuhakikisha inatengeneza magari ya wadau wote kwa wakati na kutoa huduma za vivuko kwa ufanisi na kujiepusha na vitendo vya rushwa ili kukuza mapato na kuboresha huduma za ufundi na umeme.


  Kwa upande wake Katibu mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano sehemu ya ujenzi eng. Joseph Nyamhanga  ameitaka TEMESA kuongeza bidii Katika kukusanya madeni yake ili ipate uwezo wa kibiashara na hivyo kumudu ushindani wa kibiashara.


  Naye Mtendaji mkuu wa TEMESA Eng. Marceline Magesa amemhakikishia Waziri  Mbarawa kuwa TEMESA inaendelea na mkakati wa kujenga vivuko vipya viwili ili kuongeza huduma hiyo katika eneo la Magogoni jijini Dar es salaam na Pangani mkoani Tanga.


  Aidha amemhakikishia Waziri kuwa ukarabati wa vivuko unazingatiwa na uboreshaji wa karakana unaendelea ili kuvutia wadau wengi kutengeneza magari yao katika karakana hizo.


  Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA ulianzishwa mwaka 2006 kwa lengo la kusimamia huduma za ufundi, umeme na usimamizi wa vivuko ambapo hadi sasa takriban vivuko 28 vinasimamiwa na wakala huo nchini kote.

  Imetayarishwa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano.

  0 0


  “The changing Accounting and Economic Landscape:  Opportunities and Challenges for the East African Community”.

  The 1st East Africa Congress of Accountants (EACOA) will be held at  AICC Arusha – Tanzania from 2th to 4thMarch 2016.


  The objective of the conference is to create a forum for professional accountants in the region to interact, seek opportunities and to discuss issues impacting the accounting profession in the region.


  The conference is jointly organised by the Accounting Bodies in the Region: OPC Burundi; Institute of Certified Accountants Kenya (ICPAK); Institute of Certified Accountants of Rwanda (ICPAR); National Board of Accountants and Auditors –Tanzania (NBAA); Institute of Certified Accountants of Uganda (ICPAU).NBAA is the host of the conference.


  Members of the accountancy profession, academicians and all interested persons are invited to attend this important professional conference.


  Registration and Conference Fee

  Early registration start on 7th December,  2015 to 29th January 2016 conference fee is Tsh. 860,000 or USD 400.  Late registration is from 1st– 29th February 2016 conference fee  Tsh. 950,000 or USD 450.  The fee include 1 day trip to Ngoro Ngoro Crater


  Register online through eacoa.nbaa-tz.orgor download the form through www.nbaa-tz.orgscan and send toeacoaregistration@nbaa-tz.org  0 0
 • 01/08/16--04:00: Article 0
 • PUBLIC NOTICE

  (NBAA)

  THE NATIONAL BOARD OF ACCOUNTANTS AND AUDITORS

  TANZANIA

  INTRODUCTION OF DIPLOMA IN INTERNATIONAL PUBLIC SESCTOR ACCOUNTING STANDARDS FROM 1ST FEBRUARY 2016.


  Introduction

  Due to growing demand in public sector entities to prepare and present high quality transparent financial statements, the National Board of Accountants and Auditors has introduced Diploma in International Public Sector Accounting Standards to be known as “Diploma in IPSAs” which will start on 1stof February, 2016


  The introduction of Diploma in IPSAS is in accordance with the mandate granted to the Board under Section 4 of the Accountants and Auditors (Registration) Act [Cap. 286 Revised in 2002], where the Board has been mandated to conduct examinations and grant diplomas, certificates and other awards  in accountancy, auditing and allied subjects.


  Course Objective

  The Course principal objective is to provide an in-depth understanding of the practical application of the International Public Sector Accounting Standards. At the end of the course, the Board shall award Diploma in IPSAS for those who will be successful.

   Targeted learners

  Diploma in IPSAS will benefit anyone who requires an understanding and application of international accounting standards in the public sector. In particular, it is suitable for:


  ·         Accountants and finance staff at all levels who are involved in the preparation of  financial statements

  ·         Trainers wishing to acquire advanced knowledge of the standards

  ·         IPSAS’s  implementation and sustainability teams

  ·         Both internal and external auditors and consultants dealing with financial reporting

  ·         Officers responsible for public sector financial reporting and auditing

  Entry Qualifications: Holders of Certified Public Accountant (CPA) Certificate or its equivalent or Holders of Postgraduate Studies in Accounting, Finance, Tax or related subject.

  Venue:will be at NBAA Campus

  Training hours per week: The time for classes will be from 5.00 PM to 7.00 PM

  Duration of the Course:Duration of the course will be six months and examinations will be held in two sessions in a year that is February and August. Two hour classes will be held for three days per week on Monday, Wednesday and Friday. To begin with, classes and examinations centre will be in Dar Es Salaam only.


  Fees and Registration:Application for admission in the February 2016 intake has commenced since 16thNovember, 2015 and deadline will be on 15th January, 2016.


  Registration form can be downloaded from NBAA website (www.nbaa-tz.org) or collected at Mhasibu House Room No. 208.


  Total cost for the programme is Tshs.1,500,000/- which includes registration, tuition  and examination fees.


  For more Information contact:

  EXECUTIVE DIRECTOR

  NBAA MHASIBU HOUSE

  BIBI TITI MOHAMED STREET

  P.O. BOX 5128,

  DAR ES SALAAM

  TEL: 255 22 2211890 -9

  FAX: 2151746 E-mail: info@nbaa-tz.org  WEBSITE: www.nbaa-tz.org.


  0 0

  WATCH TRAILER OF STAR-STUDDED 'BEYOND BLOOD' MOVIE OUT IN CINEMAS NATIONWIDE ON JANUARY 15, 2016

  "The choice you make when you have no choice is the most important"

   We present to you Beyond Blood, a movie directed by a true Nollywood veteran, Greg Odutayo. It is a captivating story of self-discovery, where a woman, after a series of uncontrollable events, decides to run away from her fears and consequently reaches her breaking point and gets caught in a cycle of unpleasant circumstances. Movie pundits have described it as a perfect movie for the family and it premieres in cinemas all across Nigeria on the 15th of January, 2016.
  Beyond Blood produced by Debbie Odutayo and the CEO of HF Media, Bidemi Fahm with soundtracks by fast-rising budding talent, bigLITTLE stars some of the finest actors and actresses in NollywoodKehinde Bankole, Joseph Benjamin, Deyemi Okanlawon, Carol King, Bimbo Manuel, Wole Ojo, Okey Uzoeshi, Shan George, Francis Onwochei, Uzor Osimkpa, Ifeanyi Kalu, Ijeoma Grace Agu with MFA London acting graduate Marion Bott making her Nollywood debut.
  Here's a sneak peek into the movie set to hit the cinemas in January 15, 2016: https://www.youtube.com/watch?v=m4FXD9B-cSA
  To stay up to date on all happenings around the release of Beyond Blood, follow @BeyondBloodFilm on TwitterInstagram & Facebook.

  Twitterhttps://twitter.com/beyondbloodfilm
  Instagramhttps://www.instagram.com/beyondbloodfilm/
  Facebookhttps://www.facebook.com/BeyondBloodFilm/
  Websitehttp://beyondbloodthemovie.com/

  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuendelea na matengenezo ya bara bara pamoja na ujenzi wa nyengine mpya umelenga kuimarisha sekya ya usafiri wan chi kavu. 
  Alisema kuundwa kwa mfuko wa bara bara ni hatua iliyokusudiwa kusimamia vyema Bara bara zinazojengwa katika maeneo mbali mbali Nchini chini ya Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano ili zitoe huduma bora ya mawasiliano. 
  Balozi Seif Ali Iddi alieleza hayo wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Bara bara ya Kilomita 35 itakayoanzia katika Kijiji cha Ole, Vitongoji,Mfikiwa na kumalizikia katika Kijiji cha Kengeja. Alisema maendeleo makubwa katika sekta ya mawasiliano yamepatikana hasa katika ujenzi wa bara bara Tano katika Mkoa wa Kaskazini Pemba zilizopata ufadhili wa Mfuko wa Milenia wa Marekani { MCC } na Bra bara Tano za Vijijini ndani ya Mkoa wa Kusini Pemba zilizofadhiliwa na Shirika la Maendeleo Norway { Norad }. 
  Aliwaomba Wananchi wote Nchini kuwa walinzi wa miundombinu inayojengwa na kuimarishwa na Serikali Kuu ili ichangie kwa kiasi kikubwa kupunguza umaskini kwa vile utatoa fursa kwa Wananchi hao kuitumia miundo mbinu hiyo kwa faida yao. 
  Balozi Seif alionyesha masikitiko yake kutokana na tabia kwa baadhi ya watu kuharibu kwa makusudi miundombinu ya Bara bara, majengo ya Skuli, Hospitali, huduma za Umeme pamoja na Maji. 
  Alionya kwamba katika kuilinda miundombinu hiyo inayompasa kila mwananchi awe mlinzi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haitomstahamilia Mtu au kikundi chochote kitakachojaribu kurejesha nyuma maendeleo ya Taifa kwa kuharifu rasilmali hizo. 
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwanasihi Wananchi kujiepusha na tabia ya kujenga katika maeneo ya hifadhi ya Bara bara ambayo Serikali wakati wowote huamua kuyatumia kwa upanuzi wa Bara bara kulingana na mahitaji ya usafiri wa kisasa sambamba na mabadiliko ya harakati za Kitaifa. Alisema wapo watu wenye fikra na hamu ya kupenda kujenga kando kando ya bara bara ndani ya Mita 15 maeneo ambayo Serikali Kuu haitakuwa na haki wala wajibu wa kulipa fidia kwa watu hao waliokiuka sheria na taratibu za bara bara. 
  Aliwaonya watendaji wa Serikali kuwa makini katika kukabiliana na watu wanaoamua kujenga majengo ya kudumu katika maeneo yasiyostahiki wala kuruhusiwa. 
  Alisema mfumo wa watendaji hao kusubiri watu wafanye makosa ndipo wachukuwe hatua dhidi ya wahusika hao ikiwemo kuwavunjia majengo yao waelewe kwamba wanakaribisha hasara inayoweza kuepukwa mapema kwa pande zote husika. 
  Mapema akitoa Taarifa ya kitaalamu ya ujenzi wa Bara bara hiyo ya Ole Kengeja Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Dr. Juma Malik Akil alisema ujenzi huo unatarajiwa kuchukuwa kipindi cha miezi sita ambapo kwa sasa tayari wahandisi wamefikisha kilomita Tano. 
  Dr. Malik alisema hatua ya kilomita 11 zilizoanzia Ole zifafikia katika Kijiji cha Mfikiwa chini ya makandarasi wa Idara ya Utunzaji na utengenezaji wa Bara bara Zanzibar { UUB }. 
  Alisema Bara bara hiyo inayojengwa kwa kiwango cha lami ikiwa na Madaraja 13 na uwezo wa kuhimili magari zaidi ya Tani Kumi inafadhiliwa na mfuko wa Kimataifa Mafuta { OPEC }. 
  Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar alifahamisha kwamba ukanda wa Mashariki ya Kisiwa cha Pemba unatarajiwa kukomboka kutokana na ujenzi wa bara bara hiyo itakayorahisisha usafiri. 
  Aliushukuru mfuko wa Kimataifa wa Mafuta { Opec } kwa kugharamia ujenzi wa bara bara hiyo unaokadiriwa kufikia Dola za Kimarekani Milioni Kumi na Mbili kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 
  Naye Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mh. Mwanajuma Majid alisema Wananchi wa Kisiwa cha Pemba nama wajibu wa kuishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa jitihada zake zinaziendelea kukwamua kero zinazowakabili Wananchi ikiwemo miundombinu ya bara bara, umeme, huduma za Maji pamoja na afya. Mh. Mwanajuma aliitanabahisha jamii kwamba wakati umefika kwao kujishughulisha na kazi za maendeleo badala ya ile Tabia ya baadhi ya watu kukaa vijiweni wakaendelea kudanganyana.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikata utepe kuashiria akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Bara bara ya Kilomita 35 itakayoanzia katika Kijiji cha Ole kupitia Vitongoji,Mfikiwa na kumalizikia katika Kijiji cha Kengeja Mkoa wa Kusini Pemba.  Wa kwanza kutoka Kushoto ni Afrisa Mdhamini Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Pemba Nd.Hamad Ahmed Baucha na nyuma yake ni Naibu Katibu
  Mkuu wa Wizara hiyo Nd.Tahir Abdullah.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Moh’d Aboud Moh’d wa kwanza kutoka kulia akibadilishana mawazo na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Ali Juma
  Shamuhuni kwenye sherehe ya uwekaji wa jiwe la msingi la Bara bara ya Ole hadi Kengeja. Kulia ya Waziri Shamuhuni ni Mkuu wa Wizaya ya Chake chake Bibi Hanuna Ibrahim Masoud na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Mzee Mberwa Hamad Mberwa.
  Kijana Halima Juma akifanya manjonjo yake wakati akisoma utenzi maalum katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bara bara ya Ole hadi Kengeja ambapo Mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
   Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wananchi pamoja na Watendaji wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Bara bara ya Ole hadi Kengeja.
  Baadhi ya Wafanyakazi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano pamoja na Wananchi waliohudhuria uwekaji wa jiwe la msingi la Bara bara ya Ole hadi Kengeja ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya sherehe za Kutimia miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964. 
  Picha na OMPR, Zanzibar

  0 0

  Mbunge wa Viti Maalumu, Mkoa wa Songwe, Juliana Shonza amewataka wanawake wa Wilaya ya Mbozi na mkoa kwa ujumla kumtumia ipasavyo kuwasilisha kero zao ili akawapiganie bungeni kwani ndio kazi alioomba.

  Shonza alitoa rai hiyo jana wakati akitoa shukrani zake kwa wajumbe wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM (UWT) Wilaya ya Mbozi, mkoani hapa kumuamini na kumpatia kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana kupitia chama hicho.

  Alisema kama walivyomuamini kwa kumpatia kura nyingi zilizomuwezesha kupata ubunge, ndivyo wanavyotakiwa kumtumia katika kipindi chote cha uongozi wake huku akiomba ushirikiano wa dhati kutoka kwao (wananchi) kwenye utekelezaji wa majukumu ya kijamii ikiwamo miradi mbalimbali anayotarajia kuifanya.

  Shonza alisema anafahamu changamoto zinazowakabili wananchi wa Mbozi,ikiwamo umeme hususani vijijini, pembejeo za kilimo, maji na mawasiliano hivyo wampe ushirikiano na anakwenda bungeni kupigania mambo hao muhimu kwani mawaziri wengi ‘anawamudu’.

  Aliwataka wananchi hao kujiunga kwenye vikundi iwe rahisi kusaidiwa kwa kupatiwa mikopo na misaada mingine ambayo itawasidia kukuza vipato vyao, kwani huu ni muda wa kuwezeshana hususani wanawake ambao ndio nguvu kuu ya familia.

  Alisema ‘Hivi sasa huwezi kupata mkopo mtu binafsi ni lazima ujiunge kwenye kikundi, hivyo basi leo kwa kuanzia natoa Sh600,000 kwa ajili ya kusajili vikundi vyenu, kwa vile ambavyo vipo tayari lakini hamjavisajili. Ila huu ni mwanzo tutafanya mambo mengi na mazuri zaidi’.

  Mwenyekiti wa UWT, Wilaya ya Mbozi, Issabela Mbaya alisema umoja huo utamtumia Shonza kuleta umoja na maendeleo kwa wanawake wa wilaya hiyo.
  Mbunge Viti Maalum, Mkoa wa Songwe, Juliana Shonza, akizungumza na Wajumbe wa Jumuiya ya wanawake wa CCM, (UWT) wilaya ya Mbozi, jana mchana mjini Vwawa, wilayani Mbozi, Shonza alikutana na wajumbe hao kwa lengo la kutoa shukrani zake kumuamini na kumpatia ubunge katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana.
  Mbunge Viti Maalum, Mkoa wa Songwe, Juliana Shonza,(mwenye nguo nyekundu) akicheza na Wajumbe wa Jumuiya ya wanawake wa CCM, (UWT) wilaya ya Mbozi, jana mchana mjini Vwawa, wilayani Mbozi, Shonza alikutana na wajumbe hao kwa lengo la kutoa shukrani zake kumuamini na kumpatia ubunge katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana

  0 0

  Waziri mkuu wa zamani na aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA na kuungwa mkono na UKAWA, Edward Lowassa amempongeza mwanasoka wa Kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta kwa kuchaguliwa kuwa mwanasoka bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani.

  Samatta alichaguliwa jana usiku huko Nigeria kuwa mwanasoka bora wa mwaka kwa wachezaji wanaocheza soka barani humu.

  Katika pongezi zake, Lowassa ambaye ni mshabiki wa soka asiyependa kuweka wazi anapenda Simba au Yanga, amesema ushindi wa Samatta ni changamoto kubwa kwa wana soka wa tanzania lakini zaidi kwa Serikali kuwekeza kwenye eneo hilo.

  "Huyu kijana kufikia hapo ni kujituma kwake, lakini zaidi ni malezi aliyoyapata katika timu yake ya TP Mazembe...ni lazima tuwe na utaratibu wa kujenga shule za kukuza vipaji vya soka (academy), tutawapata kina Samatta wengi" alisema Lowassa.

  Ameongeza kuwa serikali isione shida kuchukua ilani ya CHADEMA iliyoridhiwa na UKAWA ambayo inataka kufutwa kodi kwa vifaa vyote vya michezo.

  "Wasione haya kuchukua ilani yetu. sisi tulitangaza kuwa tutafuta ushuru kwa vifaa vyote vya michezo pamoja na kuanzisha Academy ilikuinua vipaji, tunaamini kwa kufanya hivyo watapatikana kina Samatta wengi tu na si katika soka, bali hata michezo mingine kama riadha na ngumi" alisisitiza na kuongeza.

  "Kumpongeza tu pekee yake hakutasaidia hawa wengine, ni lazima kuwe na mikakati ya kuwaendeleza vijana wetu hawa. Huwa sipendi kuona wachezaji kutoka nje ndiyo wanaotamba katika timu zetu kubwa, wakati kuna vipaji vingi sana...Kama tukiviendeleza itakuwa kama Brazil au Nigeria..wa nje ndiyo waje kuchukua wachezaji hapa" ameshauri.

  0 0

  Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Mtandao wa Thehabari.com, Joachim Mushi akitoa neno la shukrani kwa Kampuni ya Tigo kwa kuwakutanisha baadhi ya wamiliki na waendeshaji wa mitandao ya kijamii (bloggers & website owner) katika hafla hiyo maalumu ya chakula cha jioni iliyofanyika 'Double Tree hotel' jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Mtandao wa Thehabari.com, Joachim Mushi akitoa neno la shukrani kwa Kampuni ya Tigo kwa kuwakutanisha baadhi ya wamiliki na waendeshaji wa mitandao ya kijamii (bloggers & website owner) katika hafla hiyo maalumu ya chakula cha jioni iliyofanyika 'Double Tree hotel' jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wageni waalikwa ambao ni wamiliki wa mitandao ya kijamii (bloggers & website owner) wakiwa katika hafla maalumu ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na kampuni ya Simu ya Tigo kusherehekea mteja wa milioni moja katika 'Facebook' ya kampuni hiyo. Tigo ilitoa zawadi mbalimbali kwa wateja wanaofuatilia ukurasa wao (Facebook page). Baadhi ya wageni waalikwa ambao ni wamiliki wa mitandao ya kijamii (bloggers & website owner) wakiwa katika hafla maalumu ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na kampuni ya Simu ya Tigo kusherehekea mteja wa milioni moja katika 'Facebook' ya kampuni hiyo. Tigo ilitoa zawadi mbalimbali kwa wateja wanaofuatilia ukurasa wao (Facebook page).Msanii maarufu wa dance nchini, Christian Bella akiwaburudisha wageni waalikwa katika hafla maalumu ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na kampuni ya Simu ya Tigo kusherehekea mteja wa milioni moja katika ukurasa wa 'Facebook' wa kampuni hiyo. Msanii maarufu wa dansi nchini, Christian Bella akiwaburudisha wageni waalikwa katika hafla maalumu ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na kampuni ya Simu ya Tigo kusherehekea mteja wa milioni moja katika ukurasa wa 'Facebook' wa kampuni hiyo.


  0 0

  Na Chalila Kibuda 
  wa Globu ya Jamii.

   Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amepongeza weledi wa huduma  za madaktari na huduma zinazotolewa katika Tasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.

  Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ametoa pongezi hizo  jana  Ijumaa Januari 8, 2016 wakati akizungumza  na waandishi wa habari hospitalini hapo ambako alikuwa amelazwa kwa uchunguzi wa afya yake na matibabu. 
  Alisema kwamba awali yeye alikuwa anaogopa kutibiwa hapo kutokana na taarifa potofu zilizokuwa zinazotolewa kwenye vyombo vya habari juu ya  operesheni tata zilizowahi kufanyika katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, na kwamba  sasa ameridhika kuwa ni vinginevyo kwani Kitengo cha magonjwa ya moyo cha hospitali hiyo kimemdhihirishia kwamba kina uwezo mkubwa wa matibabu ya moyo kama ilivyo hospitali zingine popote pale duniani.
  Askofu Mkuu huyo wa Jimbo kuu la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo alilazwa katika taasisi hiyo ya moyo tangu Januari Mosi mwaka huu. Hali yake imeendelea kuimarika kila siku baada ya kufanyiwa uchunguzi na kupatiwa matibabu hapo.
  Kwa upande wake  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee, Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa Serikali imeokoa kiasi cha shilingi bilioni nne ambazo zilikua zipotee kwa ajili ya kupeleka wagonjwa wa moyo kutibiwa  nje ya nchi.
  Aidha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Mrisho Kikwete iliyopo katika hospitali ya Taifa ya Mhimbili, Profesa Mohamed Janabi amesma kuwa Askofu Pengo ataruhusiwa mwisho wa juma hili kwa kuwa afya yake imeimarika.
   Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akiingia katika ukumbi wa mikutano katika kitengo cha Moyo cha Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete kilichopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.
   Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee Mhe Ummy Mwalimu akimkaribisha Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ili aweze kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

  Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam  na kupongeza jopo la Madaktari waliomhudumia 
   Kulia ni aliyekuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwashamu Askofu Titus Mdoe na Askofu Mkuu wa Jimbo la Songea, Damian Dallu wakiwa katika mkutano wa Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo na waandishi wa habari katika ukumbi wa Mkutano wa Kitengo cha Moyo cha Jakaya Mrisho Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
   Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo  akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee,  Mhe. Ummy Mwalimu na kulia ni Askofu Mkuu wa Jimbo la Songea, Damian Dallu.
   Katika mkutano huo  Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo  alitoa zawadi za kadi za pongezi kwa baadhi ya madaktari mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari 
    Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee, Mhe. Ummy Mwalimu akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Mrisho Kikwete iliyopo katika hospitali ya Taifa ya Mhimbili, Profesa Mohamed Janabi. 
  Katibu Mkuu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee,  Dkt. Mpoki Ulisobisya akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusiana na swali lililoulizwa na mwandhishi wa habari kuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee haitoi ruhusa ya mtu yoyote kwenda kutibiwa nje ya nchi na ruhusa hiyo hutolewa na Madaktari wenyewe ambao walikua wanamtibia mgonjwa.

  0 0


  SIMU.TV:  Wasiopeleka watoto shule kutozwa faini mil.5. Wawili wafariki, mmoja apooza kwa mshtuko wa bomoa bomoa; https://youtu.be/zu3MScrBOVA 
   SIMU.TV:  Magufuli awafunga mdomo UKAWA. Mwanya safari za kwenda matibabu India wafungwa. Kikwete rais bora 2015; https://youtu.be/6O_n75Metqo  
   SIMU.TV:  Magufuli ampa tano Samatta. Yanga haishikiki Mapinduzi Cup. Wafaransa wamfuata Samatta Dar, avuliwa uraia; https://youtu.be/amljZ_oWI8w 
  0 0


  0 0


  Mwanaharakati wa mabalozi wa usalama barabarani naASASI YA WAZALENDO NA MAENDELEO TANZANIA Bw. Ally Nurdini Six anasikitika kutangaza kifo cha Baba yake mzazi marehemu mzee Hassan Nurdin (R.I.P) aliyefariki  majira ya saa 9.00 alasiri siku ya Ijumaa tarehe 08 Januari,  2016 mjini Moshi.


  Habari ziwafikie ndugu, jamaa, marafiki na majirani popote pale walipo.


  Marehem Mzee Hassan Nurdin alikuwa ameugua kwa muda wa miezi sita, ambapo mtoto wake mkubwa Bw. Ally Nurdin Six alichukua likizo kuungana na familia mjini Moshi kwa ajili ya kumuuguza mzazi wake. Lakini Mwenyezi Mungu akamchukua kiumbe wake.


  Mazishi yantarajiwa kuwa Saa 7 mchana siku ya Jumapili tarehen 10 Januari 2016 katika makaburi ya Njoro, Moshi Mjini, baada ya Marehemu kuswaliwa katika Msikiti kwa Mtei ambao uko jirani na CCM kata ya Mji Mpya Mchomba Centre.


  Mwenyezi Mungu ampumzishe amlaze 

  mahala pema peponi marehemu

  AMINA.

  Inna Lillahi wa inna Raji'un'


  Kwa maelezo zaidi na  Rambi rambi wasiliana na:

  Ally Six Nurdin

  au Chief Daudi Mrindoko  0 0

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limewashukuru watanzania wote, wapenzi, na wadau wa mpira wa miguu Tanzania waliojitokeza usiku saa 8 uwanja wa ndege wa Kimataifa  Julius Nyerere jijini Dar es salam kumpokea mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani Mbwana Samatta.
  Samatta alipokelewa na viongozi wa serikali, TFF, familia yake wakiwemo baba na mama yake mzazi na watanzania wengi walijitokeza kumlaki mchezaji huyo.
  Mara baada ya mapokezi ya uwanja wa ndege, TFF ilimpeleka moja kwa moja kupumzika katika hoteli ya Serena iliyopo eneo la Posta jijini Dar es salaam, ambapo imemlipia gharama ya kukaa kwa siku mbili.
  Akiwa hoteli ya Serena, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Michezo, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mama Juliana Yassoda alitoa salamu za pongezi kwa niaba ya Serikali, kisha mchezaji alipata nafasi ya kuongea na waandishi wa habari.
  Kwa kuwa Jumanne, Januari 12 ni Sikukuu ya Mapinduzi, na Janauri 13 ni fainali ya kombe la Mapinduzi Visiwani Zanzibar, siku ya Alhamisi Januari 14 TFF imeandaa dua maalumu ya kumpongeza Samatta itakayoongozwa na viongozi wa dini mbalimbali katika uwanja wa Karume kuanzia saa 11 jioni.
  Hata hivyo ratiba zingine za kumpongeza Mbwana Samatta zinazoweza kuandaliwa na wadau wengine zinaweza kuendelea ilimradi TFF ijulishwe mapema kwa ajili ya kuratibu uwepo wa mchezaji mwenyewe.

older | 1 | .... | 1083 | 1084 | (Page 1085) | 1086 | 1087 | .... | 3282 | newer