Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1082 | 1083 | (Page 1084) | 1085 | 1086 | .... | 3270 | newer

  0 0
 • 01/07/16--01:30: PRESS STATEMENT

 • East African Community

  PRESS STATEMENT

  1. The Minister for Foreign Affairs, EAC, Regional and International Relations of the United Republic of Tanzania, also Chairperson of the EAC Council of Ministers, Hon. Ambassador Dr. Augustine Mahiga, convened a Consultative Meeting in Arusha on 6thJanuary 2016 to deliberate on the way forward on the situation in Burundi,

  1. The meeting was attended by the Hon. Georges Rebelo Pinto Chikoti, Minister of Foreign Affairs of the Republic of Angola, also Chairperson of the Regional Inter-Ministerial Committee of the International Conference on the Great Lakes Region (ICGLR); Hon. Dr. Crispus Kiyonga, Minister for Defence of the Republic of Uganda and representative of President Yoweri Museveni, the Facilitator of the Dialogue; Ambassador Dr. Richard Sezibera, EAC Secretary General; Mr. Kassimi Bamba, from the African Union Office in Burundi and the Great Lakes region. Others in attendance were senior officials accompanying the esteemed leaders of delegation.

  1. The consultative meeting was a follow up on the re-launch of the dialogue in Kampala by President Yoweri Musevenion 28thDecember 2015, in his capacity as Facilitator of the Burundi dialogue.

  1. The meeting noted with appreciation and expressed support for the  steps taken in particular by the EAC, the AU and the UN and the resultant Communiques and related pronouncements including by the EAC Emergency Summits of 13th May and 6th July 2015; by the AU Peace and Security Council on 17th October, 13th November and 17th December 2015;  the United Nations Security Council’s Presidential Statement of 28th October 2015 and the United NationsSecurity Council’s Resolution 2248(2015) of 12th November 2015.

  1. The meeting expressed concern on the continued political crisis in Burundi and its potential to degenerate further with far reaching humanitarian implications; and in that regard reiterated the need for the parties to embrace political dialogue as the only feasible way to end the crisis in Burundi.

  1. The meeting expressed support for the facilitation efforts under President Yoweri Museveni and noted that the dialogue scheduled for 6th January 2016 did not take place due to ongoing consultations. The meeting committed to intensify consultations with the Burundi government and the opposition with a view to continue the Burundi political dialogue as soon as possible.

  1. The meeting thanked Hon. Amb. Dr Augustine Mahiga for convening the Consultative meeting and expressed appreciation to the Government of the United Republic of Tanzania and the EAC Secretary General for the conducive environment that facilitated the deliberations.


  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akizungumza na Bi. Ester Maganga aliyekatwa kidole na watu wenye imani potofu alipomtembelea nyumbani kwake kumjulia hali na kumpa pole ya kupoteza kidole chake, katika kijiji cha Mlalo Wilayani Lushoto. Januari 5,2016.
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akitoa pole kwa Bi. Ester Maganga baada ya kukatwa kidole chake na watu wenye imani potofu katika eneo la Mlalo Wilayani Lushoto Tanga, tarehe 5 Januari, 2016.
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi (katikati mwenye miwani) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa ngazi mbalimbali wa Wilaya ya Lushoto alipomtembelea Bi. Ester Maganga (kushoto kwake) aliyefanyiwa tukio la kikatili la kukatwa kidole na watu wenye imani potofu.
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akipanda mche wa mparachichi nje ya makazi ya Bi. Ester Maganga (hayupo pichani) aliyefanyiwa ukatili wa kukatwa kidole ikiwa ni sehemu ya ukumbusho wa ujio wa Naibu Waziri.Tarehe 5, Januari, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

  Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (StarTimes League) inaendelea wikiendi hii kwa michezo 12 kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini ikiwa katika mzunguko wa kumi, huku kila timu ikisaka pointi tatu muhimu kuweza kupanda Ligi Kuu ya Vodacom msimu ujao wa 2016/2017.
  Kundi A, Jumamosi Mji Mkuu watawakaribisha Ashanti United uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, Kiluvya United dhidi ya Polisi Dar uwanja wa Mabatini – Mlandizi, Africa Lyon v Friends Rangers uwanja wa Karume jijini Dar es salaam huku Polisi Dodoma wakiwa wenyeji wa KMC FC uwanja wa Mgambo Mpwapwa.
  Kundi B, Polisi Morogoro watacheza dhidi ya Lipuli uwanja wa Jamhuri Morogoro, JKT Mlale watawakaribisha Kimondo FC uwanja wa Majimaji mjini Songea, Kurugenzi FC dhidi ya Ruvu Shooting uwanja wa Wambi Mafinga na Njombe Mji watakua wenyeji wa Burkinafaso uwanja wa Amani- Njombe.
  Kundi C, Panone FC watawakaribsha maafane wa JKT Kanembwa uwanja wa Ushirika mjini Moshi, Polisi Mara watacheza dhidi ya JKT Oljoro uwanja wa Karume mjini Musoma, Rhino Rangers dhidi ya Geita Gold uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Tabora, huku Mbao FC wakicheza dhidi ya Polisi Tabora mchezo utakaonyeshwa moja moja na kituo cha Star TV.

  0 0

  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa chama cha soka cha Zanzibar (ZFA) kufuatia kifo cha mwamuzi mstaafu wa FIFA Juma Ally Khamis kilichotokea jana kisiwani Pemba.
  Katika salamu zake, Malinzi amewapa pole familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na wadau wa mpira wa miguu na kusema TFF ipo pamoja na wafiwa katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.
  Wakati wa uhai wake marehemu Juma Ally Khamis alikuwa mwamuzi mwenye beji ya FIFA, mkufunzi wa waamuzi Tanzania, Meneja wa uwanja wa Amani – uliopo Zanzibar na mratibu wa michezo Wizara ya Habari na Utamaduni na Michezo kisiwani Zanzibar.
  Mazishi yanatarajiwa kufanyika leo Alhamis nyumbani kwake Pemba.

  0 0

   Kamera ya Globu ya Jamii, imeinasa taswira hii ya Mama na wanawe wakiwa wamepakiwa kwenye Baiskeli ya abiria ambayo ni moja ya vyombo vinavyotumika sana kwa usafirishaji hapa Mkoani Geita. Picha hii imepigwa katika barabara kuu ya Sengerema-Geita.


  0 0


  0 0

  Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Hospitali ya Muhimbili mara baada ya kumtembelea Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhadhama Polycarp Kardinali Pengo, Kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Profesa Jenad Abdallah leo jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani mara baada ya kuitembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete leo jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Profesa Jenad Abdallah, Kulia ni Katibu wa Wizara hiyo, Dk.Mpoki Ulisubisya.
  WAZIRI wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Ummy Mwalimu, akimjulia hali mmoja wa wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa moyo, katika taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam leo. Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo,  Dk.Mpoki Ulisubisya na katikati ni  Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto Dk. Godwin  Godfrey.

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
  MKURUGENZI wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ya Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Jenad Abdallah amesema kuwa afya ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo inaendelea vizuri tofauti na hali aliyokwenda nayo.  Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo alipelekwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili Januari Mosi akisumbuliwa na tatizo la moyo.  Profesa Jenad Abdallah amesema kuwa kutokana na huduma anayoipata katika taasisi hiyo, Kardinali Pengo hali yake inaimarika na si muda mrefu anaweza kuruhusiwa.

  Profesa Abdallah amesema hata kiongozi huyo akitaka kwenda nje kwa matibabu wataka kujiridhisha na huduma wanayoitoa.

  Waziri wa Afya Maendeleo Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amemtembelea Muadhama Polycap Kardinali Pengo na kujioanea hali yake na kudai kuwa kiongozi huyo amemkuta akiwa amekaa na tofauti na baadhi mitandao ya Jamii si Globu ya Jamii ya Michuzi zikidai kuwa yuko katika chumba cha uangalizi maalum (ICU).

  Amesema huduma anayoipata Kardinali Pengo atakuwa Balozi mzuri wa kuelezea huduma ya taasisi ya moya ya Jakaya Kikwete na kuwataka watu wengine kwenda kupata huduma hiyo na sio kwenda nje.

  Amesema Serikali itaendalea kuboresha huduma hiyo kwa sasa kwa viwango vya dunia Tanzania imefikia asilimia nne na kiwango cha kimataifa cha juu ni asilimia sita.

  Wakati huu Waziri huyo amekutana na menejimenti pamoja na wafanyakazi wa Hospitali ya Muhimbili kusikia changamoto zinazowakabili pamoja na mafanikio walioyapata.

  0 0

  SAM_7189
  Kada wa CCM Kenedi Mpumilwa kushoto akipokea fomu ya kuwania nafasi ya uenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha kutoka kwa katibu msaidizi wa CCM mkoa wa Arusha Omar Billal mapema leo katika makao makuu ya mkoa(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
  SAM_7190
  Kada Mpumilwa akionyesha fomu yake ya uenyekiti wa CCM mkoa kwa wanahabari mara baada ya kuipokea kutoka kwa katibu msaidizi wa CCM mkoa
  SAM_7176
  Kada Mpumilwa akisaliamiana na katibu msaidizi wa mkoa wa Arusha mara baada ya kuingia ofisini kwake kwaajili ya kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya uenyekiti wa mkoa.


  0 0


  Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza (CCM) Stanslaus Mabula.

  Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG

  Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza Stanslaus Mabula (CCM, ameahidi kushughulikia suala la ujenzi wa maegesho ya magari makubwa ya mizigo nje ya jiji la Mwanza ili kuzuia magari hayo kuingia katikati ya jiji.

  Akizungumza ofisini kwake hii leo, Mabula amebainisha kuwa upo mpango wa kujenga maegesho hayo katika maeneo yaliyo nje ya Jiji la Mwanza, hatua ambayo itasaidia magari hayo kutoingia katikati ya Jiji na hivyo kuondoa malalamiko yaliyopo kutoka kwa madereva wa magari madogo ya mizigo wanaolalamikia uingiaji wa magari makubwa ya mizigo katikati ya jiji.

  Ameyataja maeneo yanayotarajiwa kujengwa maegesho hao kuwa ni Buhongwa pamoja na Igoma na kwamba baada ya ujenzi wake kukamilika, magari yote makubwa ya mizigo hayataruhusiwa kuingia katikati ya Jiji.

  Mabula ambae alikuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza katika uongozi uliomalizika mwaka jana, amebainisha kuwa utekelezaji wa ujenzi wa maegesho hayo unatarajiwa kufanyika kwa uharaka zaidi ambapo amewahimiza wawekezaji mbalimbali kujitokeza ili kushirikiana na halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa ajili ya kufanikisha ujenzi huo.

  Suala la magari makubwa kuingia katikati ya Jiji la Mwanza huku yakiwa na mizigo, linalalamikiwa na madereva wa magari madogo ya mizigo kwa kile wanachoeleza kuwa wanaingiliwa katika shughuli ambazo wao wangezifanya na hivyo kujiingia kipato ambapo wameiomba halmashauri ya Jiji la Mwanza kutoruhusu magari hayo kuingia katikati ya Jiji.
  Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza (CCM) Stanslaus Mabula.
  Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza (CCM) Stanslaus Mabula akiongea na wanahabari ofisini kwake.

  0 0

   Waziri wa fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Fedha zilizo pelekwa katika halmashauri zote hapa nchini kiasi cha shilingi bilioni 18.77  kwenye akaunti za shule za msingi na Sekondari kwa ajili ya kutoa elimu bure kwa wanafuzi wa shule zote hapa nchini.
   Gavana wa Benki kuu ya Tanzania, Benno Ndulu akifafanua jambo kwenye mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia Katibu Mkuu wa wizara ya Fedha na Mpango, Servacius Likwelile.
   Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alphayo Kidata akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusiana na ukusanyaji wa mapato katika Malaka ya Mapato Tanzania kwa kila robo mwaka. 
  Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango jijini Dar es Salaam leo.
  Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

  KIASI cha shilingi bilioni 18.77 zimetumwa kwenye akaunti za shule za Msingi na Sekondari za halmashauri zote hapa nchini kwaajili ya wanafunzi kusoma bure.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa fedha na Mpango, Dk. Philip Mipango wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

  Pesa hizo zimegawanywa kwenye akaunti za shule za shule za Msingi na Sekondari katika halmashauri zote kiasi cha shilingi bilioni 15.7 na bilioni 3  kwenye akaunti vyombo vya usimamizi wa mitihani katika Halmashauri zote hapa nchini.

  Dk.Mpango amewatahadharisha wakuu wa Mikoa, wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri zote kutumia ipasavyo pesa hizo kwa kuwa zikitumika kwa matumizi mengine watalala nao mbele kwa kula jasho la wananchi.

  Pia Waziri wa fedha na Mipango, Dk. Mpango amewaomba waalimu wakuu wa shule zote za Msingi na Sekondari katika halmashauri zote hapa nchini waweke wazi matumizi ya fedha hizo  katika mbao za matangazo kwa kila shule ili kila mzazi aweze kujua kiasi gani kimetumika.

  0 0


  0 0


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamin Wiliam Mkapa Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamin William Mkapa Ikulu jijini Dar es Salaam
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
  Simu: 255-22-2114512, 2116898
  E-mail: press@ikulu.go.tz
  Tovuti : www.ikulu.go.tz              

  Faksi: 255-22-2113425  OFISI YA RAIS,
        IKULU,
   1 BARABARA YA BARACK OBAMA,  
  11400 DAR ES SALAAM.
  Tanzania.
   

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Januari, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu Jijini Dar es salaam.

  Akizungumza mara baada ya Mazungumzo hayo Rais Mstaafu Mkapa amesema lengo la kukutana na Rais Magufuli ni kumpongeza kwa dhamana aliyopewa na watanzania kuiongoza nchi, kuunda serikali na kumtakia heri ya Mwaka Mpya.Rais Mstaafu Mkapa pia amemhakikishia Rais Magufuli kuwa yupo tayari kutoa ushirikiano wakati wote ama kufanya kazi yoyote endapo atahitajika kufanya hivyo.

  Kwa upande wake Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba pamoja na kumtakia heri ya Mwaka Mpya, amempongeza Rais Magufuli kwa jinsi alivyoanza kazi vizuri hususani katika kusimamia ukusanyaji wa mapato, kubana matumizi na kuelekeza matumizi kwenye maeneo muhimu ambayo yanawahusu wananchi yakiwemo afya na maji.Jaji Warioba ameongeza kuwa Watanzania wote wanapaswa kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kazi kubwa anazofanya, ambazo ni kukomesha rushwa, ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka na wizi wa mali ya umma.

  "Lazima kila mmoja amuunge mkono Rais, tusije tukamuachie, pale ulipo kama ni mambo ya rushwa uanzie hapo hapo, kama ni mambo ya matumizi mabaya ya madaraka anzia hapohapo, tusije tukamuachia Rais pekee yake, yeye awe kiongozi wetu, lakini watanzania wote tushughulike na matatizo hayo" alisisitiza Jaji Warioba.

  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Dar es salaam  07 Januari, 2016

  0 0


  0 0
  0 0

  Beki wa Ivory Coast, Kolo Toure (kulia) akipambana na Mbwana Samatta wa Taifa Stars wakati wa mechi ya kuwania nafasi ya kushiriki kombe la dunia 2014.

  Mwanasoka raia wa Tanzania anayechezea TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mmbwana Ally Samatta amenyakua tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika anachezea ndani ya bara la Afrika, wakati  tuzo ya mwanasoka bora barani Afrika ikienda kwa Pierre-Emerick raia wa Gabon anayesakata kabumbumbu katika klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani.

  Tuzo hizo za kila mwaka zinazotolewa na Shirikisho la soka barani Afrika almaarufu kama CAF zimetolewa usiku kuamkia leo mjini Abuja nchini Nigeria. Kwa upande wa timu ya wanawake ya mwaka tuzo imekwenda kwa timu ya Cameroon. Timu bora kwa wanaume kwa mwaka uliopita ni kutoka Ivory Coast.
  Mbwana Ally Samatta akiwa amejifunika bendera ya Taifa kwa furaha baada ya kunyakua tuzo ya mchezaji bora wa afrika anayechezea barani Afrika.

  Kocha bora wa mwaka ni – Herve Renard, kutoka Cote d’Ivore ambayo inashinda kwa mwaka wa pili mfululizo wakati Klabu bora ya soka barani Afrika ni – TP Mezembe, kutoka DR Congo ambapo mwanasoka bora wa kike Afrika ni Gaelle Enganamouit kutoka Cameroon na Mwamuzi bora wa mwaka ni – Bakary Gassama kutoka nchini Gambia.

  Tuzo hizo zilipambwa na shamra shamra za kila aina kutoka kwa wasanii maarufu pamoja na wanenguaji walitumbuiza akiwemo mwanamuziki nguli kutoka nchini Mali, Salif Keita pamoja na mwanamuziki kutoka Nigeria Omowumi.

  0 0

  A'alaykum warahmatuLlahi wabarakatuh, 
  Ina Llillah waina ilaih rajiun.

  Ndugu zetu wa kiislam, tumepata faradh katika mji wetu wa coventry, Jana (06/01/2016)  ndugu yetu Abeid said MPATE (pichani) ametangulia mbele ya haki. Ni wajib  wetu waislam kumstiri muislam  Mwenzetu.  

  Tunaomba  michango yenu ili tuweze  kumstiri  ndugu yetu kwa chochote utakacho  jaaliwa inshAllah.

  Jina : Mohamed Saleh 
  Account number: 19891363
  Sort :  30-92-33
  Lloyd.  
  : 07939294471 (wanawake)
  :07801750508 (wanaume )

  Maziko tutawajulisha baada ya kupatikana  mwili wa marehemu, InshAllah. 
  Tafadhali ukipata ujumbe huu mtumie na mwenzio. 

  Shukran  wa JazakumLlah khayran.


  0 0

  Napenda kuchukua nafasi hii kuwakaribisha watu wote waliosoma shule ya sekondari ya wanaume ya Sengerema,kwenye mkutano wa wanafamilia hii,utakaofanyika tarehe 16/01/2016 siku ya jumamosi, kuanzia saa nane mchana katika ukumbi wa YWCA posta mpya.

  Napenda kukufahamisha mwanafamilia hii kuwa ,siku hii itakuwa ni siku mhimu ya kukutana na watu uliopotezana nao kwa siku nyingi ,ni siku itakayotoa nafasi kwa kila mtu kujua wenzako walipo na kujenga mtandao wa kimaisha.Ni fulsa nzuri ya kujua nani yuko wapi na anaweza kukuongoza katika lipi.

  Tutakuwa na mambo mbalimbali ya kuzungumzia ya kimaendeleo na kimaisha ,kulingana na bwawa(pool) la kitaaluma na uzoefu lililopo kwenye familia hii.

  Mpaka sasa kuna wastani wa watu therasini wamethibitisha ushiriki

  Kwa mawasiliano tumia email ya kikundi : sesescofamily@gmail.com  au  Sesesco-family@googlegroup.com

  Upatapo taarifa hii mjulishe na mwenzako umjuaye

  KARIBUNI SANA

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa amefarijika kuona wazee wanapata huduma za matibabu bure na kwa utaratibu mzuri katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma.

  Akizungumza na madaktari, wauguzi na watumishi wengine wa hospitali hiyo wiki hii, alivyokuwa kwenye ziara mkoani humo, Waziri Mkuu  Majaliwa amesema  utaratibu wa kutenga chumba maalum chenye madaktari wawili  mahsusi kwa ajili ya kuwahudumia wazee  unaotekelezwa hospitalini hapo  umeondoa  adha kubwa  kwa wazee kusubiri matibabu kwa muda mrefu  jambo  ambalo ni kero kwao.

  Amesema  kuwa hospitali ya Mkoa wa Ruvuma  imethibitisha kwamba    agizo la Serikali la kutaka  hospitali zote za Serikali  nchini ziwe na dirisha maalum kwa ajili ya wazee na  watibiwe bure linatekelezeka na kuzitaka hospitali zote nchini kuiga mfano huo.

   “Hospitali zote nchini  ziige  mfano wa hospitali ya  Mkoa wa Ruvuma kwa  kuwaheshimu wazee wanaokwenda kutibiwa katika hospitali hizo kwa kuanzisha dirisha maalum kwa ajili yao kama agizo la serikali linavyosema na wasitozwe malipo ya aina yoyote” alisema Waziri Mkuu.

   Aidha, ameongeza kwa kusema kuwa hata wanapokwenda kuchukuwa dawa uwekwe utaratibu wa kuwapa kipaumbele kwa kuwahudumia kwanza ili wasisubiri kwa muda mrefu. Na kusisitiza kuwa kibali maalum kinachowapa fursa wazee kutibiwa bure hospitalini hapo kindelee kutolewa na kiheshimiwe.

  Awali, alitembelea chumba maalum cha wazee  ambapo Waziri Mkuu alipata fursa ya kuzungumza na Bibi Antonia Moyo  ambaye alisema hajawahi kutozwa fedha wala kukaripiwa  wakati wote alipofika hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu kupitia dirisha la wazee.

  Waziri Mkuu Majaliwa, pia ametembelea wodi mbalimbali, chumba cha upasuaji pamoja na duka la dawa kwa wagonjwa wanaotumia huduma za Bima ya Afya.

  0 0

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia) akiwa na Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam, Profesa Mohamed Janabi alipomtembelea taasisi hiyo na kwenda kumjulia hali Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki la Dar es salaam, Muadhama Kardinali Pengo alielazwa hapo.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, ni Ummy Mwalimu (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)  jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Taasisi hiyo ya Moyo, Profesa Mohamed Janabi.

  0 0

  MENEJIMENTI na Wafanyakazi wa Malunde1 blog,kwa bashasha wanatoa salamu za pongezi kwa mwanzilishi wa Malunde1 blog,Fahari ya Shinyanga ndugu Kadama Malunde kwa kujaaliwa , leo Januari 08,2016;kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake. 

  Kadama Malunde aliyelelewa na wazazi wake kwa maadili ya kabila la Kisukuma ndiye mwanzilishi pia Mmiliki wa Malunde1 blog, alizaliwa katika kijiji cha Zobogo wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga miaka kadhaa iliyopita. 

  Wazazi wake waliamini kuwa elimu ndiyo urithi pekee utakaomfaa mtoto wao.

  Mwaka 1995 alianza safari yake ya kujipatia Elimu,kwa kuanza darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Bugisi wilaya ya Shinyanga,hadi mwaka 2001 alipohitimu Elimu hiyo ya msingi. 


  Mwaka 2002 hadi 2005,alijiunga katika shule ya sekondari Kituli iliyopo wilayani Shinyanga kwa masomo ya kidato cha Kwanza hadi Nne;ndipo alipojiunga katika shule ya sekondari Ngudu iliyopo mkoani Mwanza kwa masomo ya kidato cha Tano na Sita mwaka 2006/2008.


older | 1 | .... | 1082 | 1083 | (Page 1084) | 1085 | 1086 | .... | 3270 | newer