Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1081 | 1082 | (Page 1083) | 1084 | 1085 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Na Raymond Mushumbusi MAELEZO

  Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) imesema imeongeza muda kwa usajili  wa vyombo vya usafiri vya Pikipiki za magurudumu mawili na matatu mpaka  Februari Mosi mwaka 2016.

  Hayo yamesemwa leo na Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Alphayo Kidata alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari katika kikao chake cha kutoa taarifa kwa umma juu ya ukusanyaji wa kodi, Kaimu Kamishna Mkuu amesema wameamua kuongeza muda wa zoezi la usajili wa pikipiki ili kuiwapa nafasi wale ambao bado hawajasajili. “ Natoa wito kwa wamiliki wa vyombo vya pikipiki kusajili vyombo vyao mapema ili wasipatwe na adha itakayojitokeza baada ya muda uliotolewa kumalizika ” Alisema Kaimu Kamishna Kidata.

  Ameongeza kuwa zoezi hilo lilikumbwa na changamoto kadhaa zilizowalazimu kuongeza muda mara mbili, ambazo ni umbali wa vituo vya usajili na makazi ya wamiliki wa pikipiki hasa mikoani,pamoja na upotevu wa nyaraka za kununulia pikipiki.

  Aidha Kaimu Kamishna Alphayo Kidata ameomba wananchi kufungua ukurasa mpya wa ushirikiano na  Mamlaka  ili kutimiza azimio la Serikali ya Awamu ya Tano ya kulijenga taifa kwa kufanya kazi na hasa kulipa kodi stahiki zinazoleta mapato yanayowezesha maendeleo katika taifa letu.

  Zoezi la usajili wa pikipiki lilianzishwa kwa lengo la kurahisisha ukusanyaji wa mapato kutoka katika vyombo hivyo, zoezi hili lilipangwa kukamilika tangu Desemba 31 2015 lakini ikaonekana wengi hawakusajili pikipiki zao hivyo basi Mamlaka imetoa mwezi mmoja mpaka Februari Mosi 2016 kwa wenye Pikipiki  kusajili.

  0 0

   Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil ambaye sasa ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, akimkabidhi Katibu Mkuu mpya, Meja Jenerali Projest Rwegasira, moja ya Nyaraka za Ofisi za Wizara hiyo kama ishara ya kumkabidhi ofisi.

  Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakiwa katika mkutano wa kumuaga aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, ambaye sasa ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, na kuwakaribisha Katibu Mkuu mpya, Meja Jenerali Projest Rwegasira na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Hassan Simba Yahaya.  Hafla hii ilifanyika katika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

   Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil ambaye sasa ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, akiwaaga watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika katika Makao Makuu ya Wizara hiyo. Katikati ni Katibu Mkuu mpya wa Wzara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira na kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Hassan Simba Yahaya.


  0 0

  Gazeti la 'The Citizen' la Januari 5, 2016 lilichapisha habari katika ukurasa wake wa 12 yenye kichwa cha habari: ‘Umma kununua asilimia 49 ya hisa za Tanesco’.

  Taarifa hiyo siyo sahihi.


  0 0

  Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Profesa Makame Mbarawa akitoa maelezezo ya utendaji kwa Naibu Mkurugenzi wa TAZARA Bw. Betram Kiswaga alipotembelea Ofisi za Shirika hilo leo jijini Dar es salaam. 
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Profesa Makame Mbarawa akiongea na Viongozi pamoja na Wafanyakazi wa TAZARA alipotembelea ili kutoa muongozo wa utendaji kazi katika Shirika hilo. 
  Wafanyakazi wa Shirika la TAZARA Wakimsikiliza Waziri Profesa Mbarawa (Hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao.

  WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame mbarawa amewataka watendaji na wafanyakazi wote wa shirika la reli la Tanzania na Zambia (TAZARA), kufanya kazi kwa umoja,uwazi na uadilifu ili kufikia malengo yaliokusudiwa na kuhuisha ustawi wa shirika hilo.

  Akitoa mwelekeo wa utendaji wa shirika hilo kwa watendaji na watumishi wa TAZARA Prof. Mbarawa amesema Serikali ya awamu ya tano inaitaka TAZARA kufanya kazi kibiashara kwa kuhudumia wasafiri na wasafirishaji kikamilifu ili kuinua uchumi wa shirika hilo na kuliondolea unyonge na migogoro ya mara kwa mara.

  “Acheni kufanyakazi kwa upendeleo na usiri kwani huo ndio mwanzo wa hujuma na ubadhirifu hali inayochochea malalamiko na kudumaza TAZARA”, amesema Prof. Mbarawa. 

  Amezungumzia umuhimu wa kila mfanyakazi kufanya kazi kwa uadilifu na malengo ili kuleta matokeo chanya kwa manufaa ya TAZARA na nchi wanachama. 

  Kuhusu ubadhirifu unaotokea TAZARA Prof. Mbarawa uchunguzi wa TAKUKURU umeshaanza na kusisitiza kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wahalifu wote bila kujali wanatoka upande gani wa TAZARA. 

  Naibu Mkurugenzi wa TAZARA Bw, Betram Kiswaga amemweleza Waziri kuwa TAZARA inakabiliwa na changamoto za kimtaji,kiufundi na upungufu wa injini na mabehewa hivyo ameiomba serikali kuiwezesha ili imudu kujiendesha. 

  Amemhakikishia Waziri kuwa tayari shirika hilo limeanza kupata wasafirishaji wa uhakika hivyo kuimarika kimtaji kutavutia wasafirishaji wengi zaidi. 

  Reli ya TAZARA inayounganisha nchi za Tanzania na Zambia iliyojengwa na wachina miaka ya sabini na ina mtandao wa KM 1860 kutoka Dar es Salaam hadi Kapirimposhi lengo likiwa ni kuimarisha biashara na uchukuzi kati ya nchi hizo na kukuza uchumi. 

  Imetayarishwa na Kitengo cha Habari, Mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

  0 0

  Meneja wa Kampuni ya Mitandao ya Mawasiliano ya Simu za Mkononi ya Airtel Tawi la Zanzibar bwana Muhidin Mikidadi wa kwanza kutoka kulia akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  kuliani kwake Ofisini Vuga Mjini Zanzibar.Bwana Muhidini alifika Ofisini kwa Balozi Seif kukabidhi mchango wa Shilingi Milioni Moja kwa ajili ya kusaidia Sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia miaka 52.Wa kwanza kutoka kushoto ni Katibu wa Makamu wa Pili Nd. Abdullah Ali Abdullah {Kitole } na Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Ahmad Kassim.
   Meneja wa Kampuni ya Mitandao ya Mawasiliano ya Simu za Mkononi ya Airtel Tawi la Zanzibar bwana Muhidin Mikidadi akimkabidhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Mchango wa shilingi Milioni 1,000,000/- kusaidia sherehe za Mapinduzi kutimia miaka 52.
   Balozi Seif Ali Iddi akimshukuru Meneja huyo wa Airtel Tawi la Zanzibar kwa mchango mkubwa utakaosaidia huduma za sherehe Mapinduzi katika mambo mbali mbali.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akibadilishana mawazo na Meneja wa Tawi la Kampuni ya Mitandao ya simu za Mkononi Zanzibar Bwana Muhidin Mikidadi.Picha na – OMPR – ZNZ.


  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe (MB) ameitaka Bodi ya Utalii Tanzania- TTB kuendelea kutumia vyombo vya habari vya Kimataifa kama vile CNN, BBC n.k kuitangaza Tanzania kama eneo la Utalii duniani sambasamba na kuweka makala na matangazo ya utalii wetu katika majarida ya Kimataifa yanayoandika habari za Utalii na usafiri (Travel Magazine) ambayo ndiyo husomwa na watalii wengi duniani.

   “Kama kweli tunataka kupata watalii wengi zaidi pamoja na mambo mengine ni lazima tutumie vyombo vikubwa vya Kimataifa vinavyofikia watu wengi zaidi duniani” alisema na kuongeza kuwa pamoja na njia nyingine zinazotumiwa katika kuitangaza Tanzania kimataifa, mbinu hii ya kutumia vyombo vya habari yaweza kuwa na ufanisi mkubwa zaidi .


  Waziri Maghembe ameyasema hayo leo alipotembelea Bodi ya Utalii Tanzania na kukutana na Menejimenti  ya TTB kwa lengo la kujitambulisha na kubadilishana mawazo kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Bodi katika utangazaji utalii ndani na nje ya nchi.


  Akizungumzia kuhusu madeni makubwa yanayoikabili TTB,  Mh. Profesa Jumanne Maghembe ameahidi kuwa Wizara yake itachukua madeni yanayoikabili TTB na hasa yaliliyotokana na maelekezo ya Wizara ya kama yale yaliyotokana na kuitaka Bodi iingie mikataba ya kuweka matangazo katika ligi kuu ya Uingereza na klabu za mpira wa mguu na Sunderland Football Association pia ya nchini Uingereza. 

  Amesema Wizara ni lazima ilipe madeni hayo ili kulinda taswira ya Bodi ya Utalii kwa wadau na kuiondolea Bodi mzigo wa kuhangaikia madeni hayo badala yake ijikite zaidi katika kutangaza utalii.Kuhusu ukuzaji na uendelezaji wa utalii nchini Profesa Maghembe amebainisha kuwa pamoja na uwepo wa mashirika mbalimbali ya ndege yanayokuja hapa nchini lakini kuna haja kubwa Tanzania kuwa na shirika lake imara la ndege ambalo litasaidia sana kukuza utalii nchini kama ilivyo kwa nchi nyingine kama Kenya na Afrka ya Kusini. 

  Aidha amesema kuna haja pia ya kuboresha na kuendeleza zaidi  vivutio vyetu vya utalii na mazao mengine ya utalii kama vile Utalii wa fukwe na  Utalii wa utamaduni sambasamba na kukamilisha zoezi la uwekaji madaraja hoteli zetu na kutoa elimu kwa wenye hoteli kuboresha zaidi hoteli zao na hudiuma watoazo.


  Katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na viongozi wengine kutoka Wizarani akiwemo Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Bw. Ramo Makani, Naibu katibu Mkuu Bi Angelina Madata na Mkurugenzi wa Idara ya Utalii Bw. Zahoro, Waziri Maghembe amesema anataka kuona idadi ya watalii ikiongezeka kutoka 1,100,000 ya sasa na kufikia Milioni 3,000,000  mwaka 2018.


  Mapema kabla ya kumkaribisha waziri kuzungumza na Menejimenti, Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Bi Devota Mdachi alimwelezea Mh. Waziri mafanikio kadhaa ambayo Bodi imeyapata ikiwa ni pamoja na kuanzisha onesho la Utalii la Kimataifa la Swahili Swahili International Tourism Expo (S!TE) linalofanyika kila mwaka jijini Dar es salaam, kuanzishwa kwa tovuti maalumu (Portal) ya kuitangaza Tanzania na kulipia huduma nyingine za utalii moja kwa moja , uwekaji wa matangazo sehemu mbalimbali duniani.  

  Bi Devota alimfahamisha pia Mh. Waziri kuwa TTB imechaguliwa kuwa miongoni mwa Bodi za Utalii tatu bora barani Afrika ambazo zinashindanishwa kumpata mshindi wa kwanza na wa pili. “Mh. Waziri, pamoja na matatizo mengi yanayoikabili TTB lakini tunafurahi kukujulisha kuwa TTB ni miongoni mwa bodi za utalii tatu zilizoingia katika hatua ya mwisho ya kutafuta mshindi wa Bodi ya Utalii borani Afrika tukishindana na Bodi za utalii za Afrika ya Kusini na Namibia katika shindano linaoendeshwa na taasisi ya Travvy ya Marekani” alidokeza Bi Mdachi.


  Kaimu Mkurugenzi  huyo alidokeza pia kuhusu changamoto kadhaa zinazoikabili Bodi kubwa zaidi ikiwa ni madeni makubwa ya nje na ndani, na bajeti ndogo ya utangazaji. 

   Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Profesa Jumanne Maghembe akizungumza na Menejimenti ya Bodi ya Utalii leo jijini Dar es salaam.

   Kamimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bi Devota Mdachi akitoa taarifa ya masuala mbalimbali yahusuyo Bodi yake mbele ya Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Profesa Jumanne Maghembe wakati wa mkutano na Menejimenti ya TTB leo. Kulia kwa Bi Devota ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bibi Agelina Madata.

  Wajumbe wa Menejimenti ya TTB wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Bw. Ramo Makani  (wa pili kulia katika meza kuu) leo  jijini Dar es salaam.

  0 0


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. George Nyatega.

  Na Mwandishi Wetu.
  OFISI ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) imeanza kukagua taasisi za umma kuhusu utekelezaji wa matakwa ya sheria inayowataka kuwatambua waajiriwa walionufaika na mikopo ya elimu ya juu na kuwasilisha makato kwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).
  Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. George Nyatega, sheria iliyoanzisha HESLB inazitaka taasisi zzote za umma kuijulisha Bodi kwa maandishi kuhusu waajiriwa wapya katika taasisi hizo ndani ya siku 28 na Bodi kuthibitisha kama waajiriwa hao ni wanufaika wa mikopo au hapana.

  “Baada ya kuajiriwa mtu huyo ambaye amepata elimu yake ya chuo kikuu au taasisi yoyote ya elimu ya juu nadni au nje ya nchi kuanzia mwaka 1994 hadi sasa, mwajiri anapaswa kuitaarifu Bodi kwa maandishi ndani ya kipindi cha siku 28 tangu ajira hiyo,” inasomeka sehemu ya taarifa ya hiyo iliyochapishwa na vyombo mbalimbali vya habari jana ikiwemo tovuti ya HESLB.
  Taarifa hiyo, ambayo pia inapatikana katika tovuti ya HESLB, inaongeza kuwa baada ya Bodi kupokea taarifa kutoka kwa waajiri hao na kuthibitisha kuwa waajiriwa ni wanufaika wa mikopo, mwajiri atapaswa kuijulisha Bodi na kuanza kukata sehemu ya mshahara wa mwajiriwa ndani ya siku 30 na kuwasilisha makato hayo kwa Bodi ndani ya siku 15 kabla ya kila mwisho wa mwezi.
  Kwa msingi huo, HESLB kupitia tangazo hilo, HESLB imewajulisha waajiri kuwa CAG amejumuisha matakwa hayop ya kisheria katika kazi zake za ukaguzi katika taasisi za umma kwa lengo la kuongeza kasi ya ukusanyaji mikopo iliyoiva.
  “Ni imani ya HESLB kuwa waajiri katika utumishi wa umma watatoa ushirikiano kwa ofisi ya CAG ili kuondokana na matatizo ya kisheria,” amesema Bw. Nyatega katika taarifa yake.
  HESLB ilianzishwa mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai 2005 ili, pamoja na mambo mengine, kutoa mikopo ya elimu ya juu kwa Tanzania wahitaji na kukusanya mikopo iliyoiva kutoka kwa wanufaika wa mikopo hiyo tangu mwaka 1994.

  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitembelea na kukagua chanzo na mtambo wa kuchujia maji unaofadhiliwa na kampuni ya Uchimbaji ya Geita Gold Mining (GGM) kabla ya kuzindua mtambo huo katika kijiji cha Nyankanga Mkoani Geita. kushoto Mkurugenzi Mkuu wa GGM Terry Melpeter, kulia Mwenyekiti wa CCM Mkoa Geita King Msukuma.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kalangalala Mkoani Geita baada ya kuzindua na kupokea Magreda yatakayoanza ujenzi wa Barabara ya Geseko itakayoharimu jumla ya Tshs 1.2 Bl hadi kukamilika. Wa pili kulia Mkuu wa Mkoa Geita Mhe. Fatma Mwassa.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Geita Gold Mining Terry Melpeter kwenye Uwanja wa Ndege wa GGM Geita baada ya kukamilisha ziara ya siku mbili ya kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo ya wananchi Mkoani humo leo.

   (Picha na OMR).

  0 0


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere baada ya kuwasili akitoka Songea leo Jumatano Januari 6, 2016. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es slaam Meck Sadiki.

  ------------------------
  WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali haijaridhia viwango vipya vya nauli ya mabasi yaendayo kasi vilivyopendekezwa na waendeshaji wa huduma ya mabasi yaendayo kasi Dar es salaam (UDART).  Akizungumza leo na waandishi wa habari, mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea mkoani Ruvuma kwa ziara ya siku 3, Waziri Mkuu amesema Serikali haijaridhia viwango vipya vya nauli ya mabasi yaendayo kasi. Ambapo nauli ya kutoka Mbezi hadi Kimara shilingi 700, Mbezi hadi Kariakoo shilingi 1200, na nauli ya kutoka Mbezi hadi Mwenge shilingi 1400 na wanafunzi watatozwa nusu ya viwango hivyo vya nauli. 

  Waziri Mkuu amesema gharama hizi ni kubwa mno kwa wananchi na watumishi kwani amesisitiza kuwa mradi ulilenga kumrahisishia mtumishi wa Serikali anayeishi nje ya jiji.
  “Serikali iliwekeza katika mradi huu ili kusaidia watumishi na wananchi ambao hawana vipato vikubwa” alisema Waziri Mkuu. 
  Aidha, ameagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa George Simbachawene na Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi, na Mawasiliano pamoja na wadau wakutane kupanga upya viwango hivyo na kama watashindwa basi Serikali itaendesha mradi huo. 
  Tarehe 25, Novemba 2015, Waziri Mkuu alimuagiza aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya TAMISEMI na waendeshaji wa mradi wa mabasi yaendayo kasi Dar es salaam (UDART) kupitia misuada yote na kurekebisha miundombinu ili mradi huo wa mabasi uanze kufanya kazi ifikapo tarehe 10, Januari 2016, imebainika kwamba UDART hawakuandaa mpango wa biashara wala kuanisha gharama za uendeshaji.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais Mstaafu wa Awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam.


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  Ikulu jijini Dar es Salaam leo Januari 6, 2016.


  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
  Simu: 255-22-2114512, 2116898
  E-mail: press@ikulu.go.tz
  Tovuti : www.ikulu.go.tz              

  Faksi: 255-22-2113425


  OFISI YA RAIS,
        IKULU,
   1 BARABARA YA BARACK OBAMA,  
  11400 DAR ES SALAAM.
  Tanzania.
   

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu Jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 6, 2016.

  Katika Mazungumzo hayo Rais Mstaafu Kikwete amemtakia Rais Magufuli heri ya Mwaka mpya na kumpongeza kwa uongozi mzuri.

  Rais Kikwete pia amesema anaunga mkono juhudi mbalimbali zinazofanywa na Rais Magufuli ikiwemo ukusanyaji wa mapato ya serikali.

  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  06 Januari, 2016. 

  0 0


  0 0


                                                        Dr. Fanuel ISAAC MARO 
                                                2 December 1933 - 7 January 2012

  WE THOUGHT OF YOU TODAY
  We thought of you today
  But that is nothing new
  We thought of you yesterday
  And will tomorrow too
  We think of you in silence
  And make no outward show
  For what it meant to lose you
  Only those who love you know
  Remembering you is easy
  We do it every day
  Its the heartache of losing you
  That will never go away.
                                                        
  REST IN PEACE
  Deeply remembered by your Wife, Sons & Daughters, 
  In Laws, Grandchildren, Relatives & Friends.

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Mkurugenzi wa Ofisi ya Baraza la Mji Mkoani Pemba Issa Juma Othman (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya
  Mkoani Hemedi Rashid wakati alipotembelea leo miradi ya ujenzi wa Vidaraja (Steps)Kikwajuni Skuli ya Ng’ombeni vilivyojengwa na Kampuni ya ZECCON CO.LTD ya Zanzibar  ikiwa katika shamra shamra za miaka 52 
  ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Ofisi ya Baraza la Mji Mkoani Pemba Mkoa wa Kusini Pemba Issa Juma Othman wakati alipotembelea maendeleo ya ujenzi wa mitaro ya maji ya mvua kutoka Mikarafuuni hadi Mpika Tango leo iliyojengwa na Kampuni ya ZECCON CO.LTD ya Zanzibar ikiwa katika shamra shamra za miaka 52 ya
  Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mkandarasi  wa Kampuni ya NOWE INVESTMENT CO.LTD Elimeka Shumu (kushoto) inayofanyia
  matengenezo  Ofisi ya Baraza la Mji wa Chake chake   wakati alipotembelea maendeleo ya ujenzi huo leo  Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba ikiwa katika shamra shamra za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar(kulia) Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohamed Aboud Mohammed

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akitoa ushauri  kwa Mkandarasi  wa  Kampuni ya NOWE INVESTMENT CO.LTD inayojenga Machinjio ya Ngo’mbe Elimeka
  Shumu(wa tatu kulia) wakati alipotembelea machinjio hayo leo Wesha Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba ikiwa katika shamra shamra za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar(kulia) Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohamed Aboud Mohammed,[Picha na Ikulu.].


  0 0

  Na  Bashir  Yakub
  Kawaida  serikali  hutwaa  maeneo. Huhamisha  wahusika  wamiliki  na  kuchukua  eneo  kwa  malengo  maalum  yaliyokusudiwa. Yaweza  kuchukuliwa  nyumba yako, kiwanja,au  hata  shamba. Mara  kadhaa  serikali  hufanya  hivi  panapo  mahitaji  maalum  ya shughuli  za  umma  kama  ujenzi  wa  miundombinu  kama  barabara  reli, huduma za  umeme  na  maji,  ujenzi  wa  shule vyuo, vituo  vya  afya  na  miradi  mingineyo  kwa  manufaa  ya umma.


  1.FIDIA  YA  ARDHI NI NINI...

  Fidia  ya  ardhi  ni  stahili  ambayo mwenye  ardhi  mmiliki  anatakiwa  kupata  pale  ambapo  ardhi  yake  inatwaliwa/inachukuliwa  na  serikali  kwa  matumizi  maalum  ya  serikali/umma.


  2.  JE UNAWEZA  KUIKATALIA  SERIKALI   ARDHI  YAKO  ISICHUKULIWE ? 

  Serikali  inapotaka  kumhamisha  mwananchi na  kuchukua ardhi  yake kupisha mradi wa umma  kisheria  mwananchi   hana  uwezo  wa  kukataa. Hii  ni  kwasababu  ardhi  yote  ni  mali  ya  umma  ambayo  mdhamini  wake  mkuu  ni  serikali kupitia  mamlaka  ya  rais. 
  Hivyo  tunaweza  kusema  kuwa  ardhi  ni  mali  ya umma inayodhaminiwa na Serikali/Rais.

  Kwa  hiyo  mwananchi  hawezi  kuikatalia  serikali kuchukua  mali   hiyo  isipokuwa  kisheria  ni  kuwa  anayehamishwa  apewe  fidia.  

  Hata  ukiamua  kwenda  mahakamani  kupinga  kutwaliwa  ardhi  hautapinga  kuwa  serikali  isichukue  ardhi yako  kabisa, isipokuwa  utapinga  kuhusu  fidia,  labda  fidia  ndogo  au  utaratibu  mbovu  uliotumika  kukadiria  fidia, riba n.k.


  Labda  kuwe  na  uonevu  au  hila  katika  kutaka  kutwaliwa  ardhi  yako  au namna  nyingineyo  ya  nia  ovu  ndipo  unaweza  kupinga  ardhi  yako  kutwaliwa.  Lakini  haitawezekana  kupinga  hatua  hiyo  ikiwa  kuna  malengo  maalum  ya  kutwaa  ardhi  kwa  ajili  ya  shughuli  za  umma.  Kusoma zaidi BOFYA HAPA


  0 0

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard  Kalemani (wa pili kulia) akimsikiliza mmoja wa wananchi wanaozunguka mgodi wa dhahabu wa Busolwa mkoani Geita wakati alipofanya ziara katika mgodi huo ili kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanyika katika mgodi huo.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard  Kalemani (wa tatu kulia) akiangalia baadhi ya mitambo inayotumika katika shughuli za uzalishaji dhahabu katika  mgodi wa Busolwa mkoani Geita wakati alipofanya ziara katika mgodi huo . Wa kwanza kulia ni mmiliki wa mgodi huo, Baraka Ezekiel.
   Baadhi ya mitambo inayotumika katika shughuli za uzalishaji dhahabu katika  mgodi wa Busolwa mkoani Geita unaomilikiwa na  Baraka Ezekiel. 
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard  Kalemani (katikati) akiwa na watendaji mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umem e nchini (TANESCO), Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), Wakala wa Nishati Vijijini (REA)na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) wakati wa kikao chake na wakandarasi wanaosambaza umeme vijijini (hawapo pichani) kilichofanyika mkoani Geita .
  0 0
  SIMU.TV: Vigogo wajisalimisha kwa rais Magufuli. Dkt.Shein atoa ya moyoni. TRA yaweka rekodi mpya ukusanyaji mapato;https://youtu.be/11zJt_tkfDw
   SIMU.TV: Serikali yatangaza kiama kwa raia wa kigeni. Jipu latumbuliwa Ushirika Songea. Nauli za DART zapigwa chini;https://youtu.be/vlUG69xi5EY
  SIMU.TV: Nyumba 678 kuhakikiwa upya bonde la Mkwajuni. CHADEMA wakutana Moshi. Moto wazuka makao makuu ya polisi;https://youtu.be/7BwHfzOjfQY 
   SIMU.TV: Yanga,Mtibwa zaogopana mechi ya leo. Mkude, Majwega waruka mtego. Pluijm aishtukia Yanga;https://youtu.be/V5MJOicmYZE  
   SIMU.TV: Fatma Karume ashauri rais Shein akae pembeni.  Mahakama yanusuru nyumba ya mchungaji Lwakatare kubomolewa. TAKUKURU kuwapandisha kizimbani maafisa ardhi kinondoni; https://youtu.be/fITJEUbDhHc

  0 0

  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akimweleza jambo Balozi wa Norway Nchini Hanne-Marie Kaarstad (kushoto) ofisini kwake mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho.
  Balozi wa Norway Nchini Hanne-Marie Kaarstad, akisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kabla ya kuanza kwa kikao hicho.
  Balozi wa Norway Nchini Hanne-Marie Kaarstad, akielezea uzoefu wa Norway kwenye sekta ya gesi na mafuta katika kikao chake na Waziriri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo. Kikao hicho pia kilihusisha watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini pamoja na taasisi zake.
  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (mbele katikati) akiongoza kikao kilichohusisha Balozi wa Norway Nchini Hanne-Marie Kaarstad aliyeambatana na ujumbe wake, watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini pamoja na taasisi zake.
  Naibu Katibu Mkuu- Nishati, Dk. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) na Naibu Katibu Mkuu- Madini Prof. James Mdoe. (kushoto) wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Balozi wa Norway Nchini Hanne-Marie Kaarstad (hayupo pichani).

  ……………………………………………………………………………………..

  Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospter Muhongo, ameiomba nchi ya Norway kuisaidia Tanzania kupitia mafunzo hususan katika utafutaji na uchimbaji wa gesi na mafuta ili kuongeza wataalam wa gesi na mafuta nchini.

  Profesa Muhongo aliyasema hayo katika kikao chake na balozi wa Norway Nchini Hanne-Marie Kaarstad aliyeambatana na ujumbe wake uliomtembelea ofisini kwake jijini Dar es salaam.

  Kikao hicho pia kilishirikisha watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini ambao ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu- Nishati, Dk. Mhandisi Juliana Pallangyo, Naibu Katibu Mkuu- Madini Prof. James Mdoe.

  Aidha, kikao hicho kilishirikisha watendaji kutoka katika taasisi zilizopo chini ya Wizara ambazo ni pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA)

  Profesa Muhongo alisema kuwa sekta mpya ya utafiti na uchimbaji wa gesi na mafuta inahitaji wataalam zaidi na kuongeza kuwa serikali imekuwa ikiwapeleka wataalam wake kwenda kusomea masuala ya gesi na mafuta katika vyuo vilivyoko nje ya nchi kama Scotland na Uingereza.

  Alisema kuwa serikali imeanzisha kozi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Dodoma pamoja na Chuo cha Madini Dodoma.

  “ Bado tuna uhitaji mkubwa wa wahadhiri wenye Shahada za Uzamifu (PhD) kwa ajili ya kufundisha katika vyuo vyetu, na kuzalisha wataalam watakaofanya kazi katika makampuni yanayojishughulisha na utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi nchini.

  Akielezea kuhusu hali ya umeme nchini Profesa Muhongo alisema kuwa hali ya umeme nchini ni nzuri kutokana na serikali kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa wananchi wanapata umeme wa uhakika.

  Alisema kuwa Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini imekuwa ikisambaza nishati ya umeme vijijini pamoja na kutoa ruzuku kwa wazalishaji umeme mdogo kwa njia ya maji (min-hydro) na kuitaka Norway kuisaidia REA ili iweze kufanikisha miradi yake.

  Akielezea changamoto katika uzalishaji wa umeme nchini Profesa Muhongo alisema ipo mitambo ya kuzalisha umeme kwa njia ya maji yenye kuhitaji matengenezo na kuiomba serikali ya Norway kusaidia matengenezo ya mitambo hiyo.

  Aliongeza changamoto nyingine ni vyanzo vya maji kutosimamiwa ipasavyo katika mabwawa ya maji ya kuzalishia umeme na kusisitiza kuwa tayari serikali imeanza kufanyia kazi changamoto hiyo.

  Naye Balozi wa Norway Nchini Hanne-Marie Kaarstad alisema kuwa serikali ya Norway imekuwa na ushirikiano mzuri na serikali ya Tanzania katika sekta ya nishati na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo.

  0 0

  WADAU na wapenzi wa muziki wa injili nchini, wametoa wito kwa waratibu wa tamasha la Muziki wa Injili la wakati wa  Pasaka, Kampuni ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam, kuongeza wigo wa kufanyika katika nchi zote za Afrika Mashariki.

  Kwa mujibu wa mmoja wa mashabiki wa Tamasha hilo linalobeba malengo ya kuutukuza ufalme wa Mungu na mengineyo ikiwemo kupata fedha za kusaidia makundi maalumu katika jamii, Anna Shibamla wa Yombo- Machimbo, jijini Dar es Salaam, umefika wakati sasa tukio hilo likawa la nchi za Afrika Mashariki.

  “Unajua Tamasha la Pasaka tayari lina sura ya kimataifa kwa sababu limekuwa likiwaleta pamoja waimbaji kutoka nchi mbalimbali, lakini kwa mawazo yangu umefika wakati sasa likawa linafanyika katika nchi za Afrika Mashariki ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi,” alisema Anna.

  Anna aliyejitambulisha kama mmoja wa wadau wakubwa wa muziki wa injili na matamasha la Msama Promotions, alisema kwamba kama wazo hilo litafanyiwa kazi, kutalifanya tamasha lenyewe kuwa kubwa zaidi na kubeba maana zaidi kwani linaweza kuwa kielelezo cha umoja na nchi za Afrika Mashariki.

  “Kwa mtazamo wangu, ni jambo linalowezekana kama waratibu watakuwa wamejipanga kwa mfano Tamasha la Pasaka likafanyika hapa jijini Dar es Salaam, kisha likaenda kutikisa Nairobi (Kenya); Kigali (Rwanda); Kampala (Uganda) na kule mjini Bujumbura (Burundi),” aliongeza.

  Anna alisema kwa uzoefu wa zaidi ya miaka 16 wa Msama Promotions katika kuandaa tamasha hilo kwa ufanisi, anaamini anaweza kulifanya tukio jhilo kuwa la Afrika Mashariki na likawa na mvuto wa aina yake huku likibeba uzito zaidi katika kutangaza ujumbe wa Neno la Mungu, amani na upendo kuanzia kwa watu hadi kwa nchi za ukanda huo.

  Wazo hilo limeungwa mkono na Jasmin Jeremiah wa Ilonga Kilosa, Mkoani Morogoro kwa kusema hiyo itachangia kwa kiasi kikubwa waimbaji wa nchi moja kufahamika katika ncho zote za ukanda wa Afrika Mashariki, hivyo kuongeza wigo wa kupata soko la huduma yao ya uimbaji.

  “Kama Tamasha la Pasaka litakuwa likifanyika katika nchi zaidi ya moja kwa mwaka, itawapa nafasi waimbaji kwa mfano wa Tanzania kujulikana katika nchi hizo kwa mfano Kenya, Rwanda na Burundi, hivyo sio tu kutaimarisha uhusiano kati ya nchi na nchi, pia itakuwa hivyo kwa waimbaji,” alisema Jasmine akiungwa mkono na Neema Gerald.

  Neema alisema kitendo cha waimbaji wa nje kama Rebecca Malope wa Afrika Kusini ana Anastazia Mukabwa wa Kenya wakaenda kutumbuiza katika Tamasha la Pasaka nchini Rwanda au Burundi, kutaleta mvuto zaidi wa tukio hilo na kusema  anaunga mkono suala hilo kwa asilimia 100.

  Wazo hilo la wadau ni kutokana na tamasha hilo lililoasisiwa tangu mwaka 2000, limekuwa likifanyika nchini kwa kuanzia jijini Dar es Salaam na katika mikoa kadhaa, hivyo maoni ya wadau ni tukio hilo kwenda mbali zaidi ya hapo kwamba liwe linafanyika katika nchi zaidi ya moja katika ukanda wa Afrika Mashariki.


  Alipotafutwa kuhusu maoni hayo ya wadau, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizii ya Tamasha hilo, Alex Msama, alisema ni wazo zuri kwani huduma na malengo yake vitazidi kupanuka na kubeba sura ya kimataifa zaidi ikiwemo kuwa kielelezo cha umoja na mshikamano wa nchi za Afrika Mashariki na kuongeza wataketi kutafakari suala hilo.

  0 0
  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

   OFISI YA RAIS

  Anuani ya Simu: “TAMISEMI”

  Simu Na: (026) 2322848, 2321607

   2322853, 2322420

  Nukushi: (026) 2322116, 2322146

  2321013 

  Barua pepe: ps@poralg.go.tz  Tawala za Mikoa na

  Serikali za Mitaa,

  S.L.P. 1923,

  DODOMA.
  TAARIFA KWA UMMA.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Simbachawene (Mb) amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kumsimamisha kazi mara moja Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa ya Ilala Bw. Dennis. N. Mrema kuanzia leo tarehe 07 Januari, 2016 kwa kosa la kusababisha upotevu wa Mapato ya Serikali kutokana na urasimu wa kukusudia, mazingira ya rushwa na uzembe katika utoaji wa leseni za Biashara.

  Kutokana na hali hiyo Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI ameelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kumuondoa kwenye nafasi yake Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa ya Ilala na nafasi yake kukaimiwa na mtu mwingine ili kupisha uchunguzi zaidi juu ya tuhuma zilizotolewa dhidi yake.

  Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI amefikia uamuzi huu baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa Wafanyabiashara ambao wamemlalamikia Mtendaji huyu kwa ukiukwaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu za utoaji wa Leseni za Biashara, Urasimu na Mazingira ya rushwa.

  Katika uchunguzi wa awali uliofanyika kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Ilala mambo yafuatayo yamegundulika:

  (i)                  Ukiukwaji wa Makusudi wa Sheria,  Kanuni  na Taratibu  za utoaji wa Leseni za Biashara.
  (ii)               Kutoa Leseni za Biashara zaidi ya 843 bila kuwa na Vyeti vya uthibitisho wa Walipa kodi ‘Tax Clearance Certificates” hivyo kuikosesha Serikali Kodi ya Mapato.
  (iii)           Kukaa na fomu za Wafanyabiashara 336 kwa muda mrefu bila sababu za msingi.
  (iv)              Kukiuka Mwongozo wa Mkataba wa Huduma kwa wateja ambao unamtaka Afisa Biashara kutoa Leseni za Biashara ndani ya siku 2 hadi 3 baada ya muombaji kuwasilisha maombi yake ya kupatiwa Leseni ya Biashara.

  Aidha, Mheshimiwa Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais-TAMISEMI amewaagiza Maafisa Biashara wote nchini watoe huduma za Leseni kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu , kuacha urasimu na kujiepusha na vitendo vya rushwa.

  Imetolewa na:
     Kitengo cha Mawasiliano  Serikalini
     Ofisi ya Rais-TAMISEMI,     07 Januari, 2016.

older | 1 | .... | 1081 | 1082 | (Page 1083) | 1084 | 1085 | .... | 3272 | newer