Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

WANAFUNZI NA WALIMU 70 WAPATIWA MAFUNZO YA UKOCHA JIJINI ARUSHA

$
0
0
baadhi ya wanafunzi wakifanya mafunzo ya ukocha kwa vitendo yaliokuwa yakiendeshwa na kituo cha International Insparation kanda ya kaskazini kwenye viwanja vya sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
picha ya pamoja baada ya kumaliza mafunzo yao wakiwa na nyuso za furaha baada ya kutunukiwa vyeti na katibu wa baraza la michezo la taifa Henry Lihaya kwenye uwanja wa Seikh Amri kalita Abeid (picha zote na Mahmoud Ahmad Arusha)

Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria akutana kwa mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Bodi ya AU kuhusu masuala ya Rushwa

$
0
0
Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju akimkaribisha Katibu Mtendaji wa Bodi ya Ushauri kuhusu Masuala ya Rushwa ya Umoja wa Afrika (African Union Advisory Board on Corruption-AUABC), Prof. Adolphe Lawson mara baada ya kuwasili Wizarani kwa ajili ya mazungumzo kuhusu  mpango wa kuanzishwa kwa Makao Makuu ya AUABC Mkoani Arusha, Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika Wizarani tarehe 19 Aprili, 2013.
Prof. Lawson akimweleza jambo Balozi Kasyanju wakati wa mazungumzo yao.
Prof. Lawson (kushoto) akiendelea na mazungumzo na Balozi Kasyanju huku Bw. Benedict Msuya (kulia), Afisa Mambo ya Nje katika Kitengo cha Sheria akinukuu mazungumzo hayo.

taarifa ya jeshi la polisi mkoani dodoma

MAAFISA MAGEREZA WALIOPANDISHWAA VYEO LEO

$
0
0
Jenerali wa Magereza John Casmir Minja akiwa katika picha ya pamoja na baadhi  ya Maafisa wa Jeshi la Magereza waliopandishwa vyeo mbalimbali  katika ukumbi wa Bwalo Kuu la Magereza Ukonga. Zoezi la uvalishwaji vyeo leo baada ya kikao cha Tume ya Polisi na Magereza kilichofanyika jana chini ya uenyekiti wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Dkt. Emanuel J.Nchimbi (Mb)

Tanzania yapokea shilingi bilioni 314 kutoka Benki ya Dunia

$
0
0
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yapokea shilingi bilioni 314 kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya kusaidia miradi ya Umeme, Gesi, Bajeti ya Serikali pamoja na kuwajengea uwezo wa kuendesha miradi ya gesi. Mkataba huo umesainiwa leo na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt Wiliam Mgimwa Waziri wa fedha, pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier Mjini Washington DC.

Waziri wa Fedha Mhe Dkt. Wiliam Mgimwa pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier wakati wa kusaini mikataba hiyo.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria Bi. Susan Mkapa pamoja na wanasheria wa Benki ya Dunia wakifuatilia kwa makini wakati Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mgimwa pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier wakitia sahii mikataba hiyo.
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa wakibadilishana mkataba na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier. Picha na mdau Ingiahedi mduma

madereva wa kweli wapo kazini......

MAALIM SEIF AFUNGUA MSIKITI LEO HUKO MWERA

$
0
0
Viongozi wa misikiti wametakiwa kutunza nidhamu katika nyumba hizo za ibada, na kuachana na tabia ya kugombaniana uongozi, ili kuepusha migogoro isiyokuwa ya lazima. Wito huo umetolewa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Al-hajj Maalim Seif Sharif Hamad katika hafla ya ufunguzi wa “Masjid Maulana” ulioko Mwera, katika Wilaya ya Magharibi Unguja. 
Amesema misikiti ni nyumba za ibada, hivyo hakuna sababu kwa waislamu kugombania misikiti, na badala yake viongozi watakaochaguliwa wawajibike kutunza nidhamu na kuendeleza harakati za kiibada ikiwa ni pamoja na kuendeleza darsa na mijadala ya kuuendeleza Uislamu. 
 Maalim Seif amewataka waumini wa msikiti huo kushirikiana na kusaidiana katika mambo mbali mbali ya kijamii, sambamba na kuchangia harakati za misikiti kwa kuhakikisha kuwa wanasaidia kutatua kasoro zinazoweza kujitokeza. “Ipo misikiti inawaumini wengi wenye uwezo, lakini hufikia hatua ya waumini kufanya ibada kizani kutokana na kukosa fedha za kununulia umeme, au kuna mingine sehemu za vyooni hufungwa kwa muda mrefu kwa sababu hali ya usafi hairidhishi”, alitanabahisha. 
Amewahimiza viongozi wa msikiti huo kuendeleza darsa ambazo zitasaidia kuwafunza vijana maadili mema na kuweza kutekeleza ibada zao kwa uhakika. Kwa upande wake Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Ngwali, amesema waislamu wana wajibu wa kuitunza na kuihifadhi misikiti, ili iweze kuwa katika hali nzuri na usafi wakati wote. Amesisitiza haja kwa waislamu kuitumia misikiti kwa shughuli za ibada na elimu, na kuwataka viongozi kuwa mifano bora katika jamii juu ya kuendeleza maadili ya kiislamu na ibada.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na wananchi alipofika Mwera kwa ajili ya ufunguzi wa Masjid Maulana leo
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akifungua pazia kuashiria ufunguzi wa Masjid Maulana ulioko Mwera.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akikabidhi funguo za msikiti kwa Mzee wa “Masjid Maulana” ulioko Mwera, Sheikh Soud,  katika hafla ya ufunguzi wa msikiti huo. (Picha na Salmin Said, OMKR)

MWAKILISHI WA FIFA ATEMBELEA WIZARA YA HABARI,VIJANA,UTAMADUNI NA MICHEZO

$
0
0
4Ofisa Maendeleo wa Kusini mwa Afrika wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Ashford Mamelodi (kushoto) akisistiza jambo jana alipotembelea wizara ya Habari ,Vijana,Utamaduni na Michezo. 5Katibu Mkuu Wizara ya Habari ,Vijana, Utamaduni na Michezo Bw.Seth Kamuhanda wa kwanza kulia akimsikiliza mwakilishi wa Fifa wa kwanza kushoto aliyekuja nchini kutatua mgogoro uliokuwepo kwenye uchaguzi wa rais wa shirikisho la mpira nchini katikati ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw.Leodgar Tenga katika ukumbi wa Wizara ya Habari jana jijini Dar es salaam. 6Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya  Michezo Wizara ya Habari, ,Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Loenard Thadeo kushoto kwake ni Mkurugenzi Wa Habari Bw.Assah Mwambene,Mkurugenzi wa Msaidizi wa Michezo Bi.Juliana Yasoda na Afisa Habari Mkuu wa Wizara Bw.Godlease Malisa wakimsikiliza Katibu Mkuu wa wizara hiyo Bw.Seth Kamuhanda hayupo kwenye picha . 7Wawakilishi wa fifa wakiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Bw.Seth Kamuhanda aliyekaa Katikati na baadhi ya viongozi wa wizara na Shirikisho la mpira wa Miguu (TFF) wakiongozwa na Rais Leodgar Tenga  aliyeketi wa Kwanza Kushoto.

RAIS KIKWETE AKUTANA NA RAIS WA SHIRIKISHO LA WAFANYABIASHARA NA WENYE VIWANDA LA UTURUKI (TUSKON) NA UJUMBE WAKE LEO

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Rais wa Shirikisho la Wafanyabiashara na wenye viwanda la Uturuki (TUSKON) Bw. Rizanur Meral na ujumbe wake leo April 19, 2013 Ikulu jijini Dar es salaam. PICHA NA IKULU

wadau boston waamriwa kubaki ndani wakati gaidi akisakwa

$
0
0
Tumefungiwa ndani, hakuna kutoka nje! Wanasema kuwa hakuna kufungua mlango hata kama ni polisi, wanasema kuwa jamaa anataka kuua watu!  Chini ni Tangazo la gaidi wanayemtafuta! Nilikuwa nawaona hapa Cambridge lakini nilidhani ni wanafunzi wa kawaida!

Toka kwa Da'Chemi CheMponda


SERIKALI YA TANZANIA YASAINI MKATABA WA MABILIONI KUTOKA BENKI YA DUNIA

$
0
0
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yapokea shilingi bilioni 314 kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya kusaidia miradi ya Umeme, Gesi, Bajeti ya Serikali pamoja na kuwajengea uwezo wa kuendesha miradi ya gesi. Mkataba huo umesainiwa leo na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt Wiliam Mgimwa Waziri wa fedha, pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier Mjini Washington DC.
Waziri wa Fedha Mhe Dkt. Wiliam Mgimwa pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier wakijadiliana jambo kabla ya kusaini mikataba hiyo.
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa wakibadilishana mkataba na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier.

KATIBU MKUU KIONGOZI AKUTANA NA BALOZI WA UINGEREZA NCHINI

$
0
0
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika mazungumzo na balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe Diana Melrose aliyemtembelea leo April 19, 2013 ofisini kwake Ikulu jijini Dar es salaam. mazungumzo hayo yalihusu maswala mbalimbali ya ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akisalimiana na Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Uingereza (DFID) nchini Bw. Elliot Marshall aliyeongozana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe Diana Melrose (katikati) aliyemtembelea leo April 19, 2013 ofisini kwake Ikulu jijini Dar es salaam. mazungumzo hayo yalihusu maswala mbalimbali ya ushirikiano baina ya nchi hizo mbili. PICHA NA IKULU

POLISI MKOA WA DODOMA WANAWASHIKILIA WATU SITA KWA VITENDO VYA USHIRIKINA

$
0
0
Jesli la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu sita ambao wanajihusisha na vitendo vya kishirikina kwa kujifanya wanaagua na kufichua watu wachawi katika vijiji mbalimbali. Wanaenda mbali zaidi na kudai wanafichua watu wachawi wanaozuia mvua isinyeshe katika maeneo mbalimbali hapa Dodoma. Watuhumiwa hao hujulikana hapa Dodoma kwa jina maarufu LAMBALAMBA. Watuhumiwa walikamatwa tarehe katika kijiji cha MBALAWALA.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma David Misime akielezea ukamatwaji huo na kuonesha tunguli walizokuwa wanatumia




Article 4

Kinana azungumza na wakulima wa miwa Turian-Mtibwa.!


mazishi ya Bi Kidude

Banana na Maunda

$
0
0
Banana Zahir Ally Zorro na dada yake Mauda wakitumbuiza usiku huu katika uzinduzi wa umoja wa wafanyabiashara ya wenye viwanda wa Tanzania na Uturuki katika hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency jijini Dar es salaam usiku huu ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete

SAFARI LAGER YASHEREHEKEA USHINDI WAKE NA WAHESHIMIWA WABUNGE MJINI DODOMA

$
0
0

 Mgeni Rasmi kwenye hafla ya Kupongeza Ushindi wa Bia Bora Barani Afrika ulioupata Bia ya Safari Lager,Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Anne Makinga (katikati) akiwa amenyanua juu moja ya vikombe vya ushindi huo ikiwa ni ishara ya kuzindua ziara Bia hiyo katika mikoa mbali mbali hapa nchini ili kuwaonyesha Watanzania ushindi huo.
Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinga akitoa hotuba yake fupi kwa waheshimiwa Wabunge na Wageni waalikwa waliokuwepo kwenye hafla hiyo iliyofanyika usiku huu kwenye viwanja vya Bunge,Mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Miradi Maalum wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Phocas Laswai akitoa hotuba yake mbele ya Mgeni Rasmi,Viongozi mbali mbali pamoja na wageni waalikwa waliohudhulia hafla hiyo iliyofanyika usiku huu kwenye Viwanja vya Bunge,Mjini Dodoma.
Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo akiutambulisha Ujumbe wa TBL ulioambatana nae kwenye ziara hiyo.
Mpishi Mkuu wa Bia za TBL,Gaudence Mkolwe (kulia) akitoa ufafanuzi juu ya utaalam uliotumika kutengeneza Bia hiyo hadi kupelekea kuibuka na ushindi huo mkubwa Barani Afrika huku akisikilizwa kwa Makini na Mgeni Rasmi pakoja na Waheshiwa Mawaziri na Wabunge waliokuwepo kwenye hafla hiyo ya kupongeza ushiwa huo wa Bia Bora Afrika ulioupata Bia ya Safari Lager.
Tukio la Picha ya Pamoja.

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Ngoma ya Bi Kidude ya 'Ya laiti' ikifanywa na Linah na Mwana FA

hii ni hatari sana

$
0
0
Hivi karibuni,kamera ya Globu ya Jamii ilimnasa mtu huyu anaedaiwa kuwa ni omba omba akiwa amekaa katikati ya Barabara ya Bagamoyo katika eneo la Victoria jijini Dar es Salaam,akijaribu kuomba wenye magari wanaotumia njia hiyo.hali hii ni ya hatari sana kwake,hasa ukizingatia kuwa barabara hiyo iko na njia tatu.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images