Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1077 | 1078 | (Page 1079) | 1080 | 1081 | .... | 3286 | newer

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa   anatarajia kuanza ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Ruvuma, ambapo atawasili mkoani  hapo  leo saa tisa alasiri.

  Baada ya Waziri Mkuu kuwasili Uwanja wa Ndege wa Songea, atapokelewa na viongozi wa Chama na Serikali, pia atakwenda Ikulu kupokea taarifa ya maendeleo ya mkoa wa Ruvuma.

  Aidha, siku ya jumatatu  atakuwa na shughuli za kufungua  tawi la Benki ya Posta mjini Songea, kukagua  maghala ya Wakala wa Taifa wa  Hifadhi ya chakula  (NFRA) kanda ya Songea na kukagua  makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea.

  Siku inafuata atatembelea na kukagua Hospitali ya Rufaa ya mkoa, na baadaye kuzungumza na watumishi wa hospitali  hiyo.

  Siku ya nne ya ziara yaani jumatano, Waziri Mkuu atafanya majumuisho ya ziara mkoani humo, kabla ya kuagana na viongozi wa Chama na Serikali na kurejea Dar es Salaam.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S. L. P 3021,
  11410 DAR ES SALAAM

  JUMAPILI, JANUARI 3, 2016.

  0 0
 • 01/02/16--22:36: UCHAMBUZI WA MAGAZETI YA LEO • AZAM TV: Arsenal yapaa, Man united yashinda, Azam na Simba vitani Zanzibar, Liverpool chali, Chacharito ang’ara, Niyonzima atoa ya moyoni. Tazama uchambuzi wa magazeti ya leo. https://youtu.be/7l4a3gY8ngM  

  TBC: Kingunge ampa siku 100 Magufuli, Wananchi wavamia shamba la Sumaye, Basi lenye abiria 42 latumbukia mtoni, Mwigulu acharuka; Pata dondoo za magazeti ya leo. https://youtu.be/0gFnivfZUfc  

  STAR TV: Mchungaji Rwakatare aivimbia serikali, Wingu zito lazidi kutanda Zanzibar, Panga la Magufuli lawanyemelea Mabalozi. Furahia uchambuzi wa magazeti. https://youtu.be/CviaHbXdM_o

  CH10: Lowassa amemponza, Ubadhilifu wa kutisha mnadani, Mawaziri wakuu wamjadili Magufuli, Bomoa bomoa yahamia kwa Vigogo. Tazama habari zilizopewa uzito wa juu magazetini. https://youtu.be/ADpPuEdXzeA

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akizoa taka katika zoezi la Usafi wa mazingira uliofanyika leo eneo la Soko la Mbogamboga Mombasa Mjini Zanzibar ikiwa ni Uzinduzi wa Sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akibeba taka katika zoezi la Usafi wa mazingira uliofanyika leo eneo la Soko la Mbogamboga Mombasa Mjini Zanzibar ikiwa ni Uzinduzi wa Sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  Baahi ya Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ wakitandaza kifusi kwa kukiweka sawa katika zoezi la Usafi wa mazingira uliofanyika leo eneo la Soko la Mbogamboga Mombasa Mjini Zanzibar ikiwa ni Uzinduzi wa Sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.


  0 0

  Wananchi mkoani Kigoma waiomba serikali kupitia upya mradi wa uzalishaji umeme kupitia maporomoko ya mto Malagarasi.https://youtu.be/cgA6PXGShWg

  Serikali ya imeitaka kampuni inayotandaza nyaya za umeme kwenye mradi mkubwa wa gridi ya taifa ya GD STRUCTURES LTD kukamilisha kazi zake kulingana na mkataba. https://youtu.be/arrqGSNxMEk
    
  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Magharibi visiwani Zanzibar asema licha ya changamoto zilizojitokeza ndani ya chama hicho bado kimekuwa kimbilio la wanyonge. https://youtu.be/s6fF5R33xsA
    
  Halmashauri ya wilaya ya Uyui mkoani Tabora yavunja mkataba na kampuni ya SARAM kutoka jijini Dar es salaam iliyokuwa inajenga jengo la wagonjwa wan je baada ya kukiuka masharti ya mkataba. https://youtu.be/WcRP_SDT8Ic

  Naibu waziri wa afya Dr. Kigwangala aiagiza hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete kukusanya mapato yake kwa mfumo wa kieletroniki ili kuepuka upotevu wa mapato. https://youtu.be/K0F8XWU5UOk

  Baadhi ya wananchi wilayani Korogwe mkoani Tanga wahoji kutokamilika kwa mradi wa maji licha ya kuigharimu serikali kiasi cha shilingi milioni 621.https://youtu.be/plJ9kBA2WfA

  0 0

  Programu ya kitaifa ya kupanda na kutunza mazingira inaanza mwezi huu, Waziri wa Maliasili na Utalii,Profesa Jumanne Maghembe, ametangaza Jijini Dar es Salaam jana. 
   Akizungumza katika kikao cha pamoja na Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Mungano, Bw. January Makamba, Waziri Maghembe alieleza kuwa Tanzania imetenga maeneo makubwa ya hifadhi ya misitu na mazingira ili kuhifadhi na kuongeza kuwango cha maji nchini. 
   Profesa Maghembe ambaye katika serikali iliyopita alikuwa waziri wa maji, alieleza umuhimu wa miti na misitu katika kuhifadhi maji na umuhimu wa maji kwa viumbe hai. 
  Maji katika uasilia wake huvifikishia viumbe hai vyote madini na ili kupata afya na ustawi kwa njia kupitia viiini au seli. Kwa hiyo, alisema waziri, “maeneo makubwa haya ya hifadhi ya misitu na mazingira yametengwa ili yasaidie kupata hewa nzuri kwa afya yetu, maji, mvua, kuzuia joto kupanda na kupambana na mabiliko ya nchi kugeuka jangwa.” 
   Amesema kumekuwa ukataji mkubwa wa miti na uharibifu wa mazingira nchini na kueleza kwamba programu hii inalenga kuwa na mazingira bora (ecosystem), upandaji miti na utunzaji wake. 
  Waziri amesema kiako cha cha mawaziri husika cha kuweka mkakati wa ya kutekeleza kampeni hiyo ya upandaji miti na utunzazi mazingira cha siku mbili kitaanza tarehe 16 January na wataalam wa wizara mbili husika tayari wameagiza kuandaa kwa pamoja mkakati utakaotumika kutekeleza programu hiyo. Mkutano wa pamoja utazingatia masuala yote ya upatikanaji wa rasirimali zitokanazo na faida ya misitu na mazingira. 
   Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano,Bw. January Makamba alisema suala la mazingira linagusa shughuli za wizara zote na taasisi nyingi na sekta binafsi na kueleza kuwa kuna kila sababu ya vyombo mbali mbali kushirikiana. 
  Amesema programu hii ya kitaifa ni ya aina yake nchini na katika utaratibu huu TAMISEMI itawashirikisha wananchi ili kila mwananchi ajivumie kupanda miti katika eneo lake. 
   Waziri Makamba amesema kuwa matarajio ya wazira hizi ni kwamba kwa kutumia progamu hii baada ya miaka mitano matokeo yake juu ya uhifadhi wa mazingira na misitu yawe yanaonekana yenyewe pasipo kusemewa na kutetewa na mtu yeyote. 
   “Tukitekeleza programu hii kwa uangalifu na kufanikiwa matunda yake yatavutia watu wote wa ndani na nje ya nchi kwa faiada ya taifa letu,” alisema Waziri Makamba.
  Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Mungano, Bw. January Makamba (kulia) akifafanua jambo wakati alipokutana na Waziri wa Maliasili na Utalii,Profesa Jumanne Maghembe (wa tatu kushoto) makao makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii jinini Dar es Salaam. (Pili kushoto) ni aliyekuwa  Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt.Adelhelm Meru, na kulia ni Naibu Katibu Mkuu,Bw. Selestine Gesimba

  0 0


  AZAM TV: Arsenal yapaa, Man united yashinda, Azam na Simba vitani Zanzibar, Liverpool chali, Chacharito ang’ara, Niyonzima atoa ya moyoni. Tazama uchambuzi wa magazeti ya leo. https://youtu.be/7l4a3gY8ngM  

  TBC: Kingunge ampa siku 100 Magufuli, Wananchi wavamia shamba la Sumaye, Basi lenye abiria 42 latumbukia mtoni, Mwigulu acharuka; Pata dondoo za magazeti ya leo. https://youtu.be/0gFnivfZUfc  

  STAR TV: Mchungaji Rwakatare aivimbia serikali, Wingu zito lazidi kutanda Zanzibar, Panga la Magufuli lawanyemelea Mabalozi. Furahia uchambuzi wa magazeti. https://youtu.be/CviaHbXdM_o

  CH10: Lowassa amemponza, Ubadhilifu wa kutisha mnadani, Mawaziri wakuu wamjadili Magufuli, Bomoa bomoa yahamia kwa Vigogo. Tazama habari zilizopewa uzito wa juu magazetini. https://youtu.be/ADpPuEdXzeA


  0 0

  Timu ya wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini,Wizara ya kilimo, mifugo na Uvuvi ,Wizara ya maji, na Umwagiliaji , Shirika l Umeme Tanzania (Tanesco) pamoja na Watalamu wa bonde la Mto Rufiji wametembelea vyanzo vya maji vinavyotiririsha maji katika mito inayomwaga maji kwenye mabwawa ya kuzalisha umeme wa maji ikiwemo Mtera, Kihansi na Kidatu ili kuunganisha nguvu ya pamoja na kurejesha vyanzo hivyo katika hali yake ya awali kutokana na kuathiriwa na shughuli za kibinadamu na hivyo kusababisha kukauka na upungufu wa maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme wa maji ilivyokuwa katika miaka ya nyuma.
  Muonekano wa Bwawa la Kihansi kwa sasa ambalo pia limepunguza uzalishaji wa umeme wa maji kutokana na kupungua kwa kina cha maji.

  Timu ya wataalamu  kutoka Wizara ya Nishati na Madini,Wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi ,Wizara ya maji, na umwagiliaji , Shirika l Umeme Tanzania (Tanesco )pamoja na Watalamu wa bonde la mto Rufiji waliotembelea  vyanzo vya maji vinavyotiririsha  maji katika Mabwawa ya kuzalisha umeme.
  Moja ya sehemu ya mashine ama mtambo inayotumika kuzalisha umeme wa maji katika vituo vya Kihansi, Kitadu na Mtera.

  Mashine inayotumika kuondoa  taka  kama vile magogo na nyingine zanamna hiyo katika mabwawa ya kuzalisha umeme wa maji.

  Baadhi ya wajumbe wa Timu ya kutoka Wizara ya Nishati na Madini,Wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi ,Wizara ya maji, na umwagiliaji , Shirika l Umeme Tanzania (Tanesco )pamoja na Watalamu wa bonde la mto Rufiji wakipata maelezo ya namna ambavyo umeme wa maji huzalishwa katika kituo cha Kihansi .


  0 0

  WAZIRI MKUU Mhe Kassim Majaliwa   anatarajia kuanza ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Ruvuma, ambapo atawasili mkoani  hapo  leo saa tisa alasiri.

  Baada ya Waziri Mkuu kuwasili Uwanja wa Ndege wa Songea, atapokelewa na viongozi wa Chama na Serikali, pia atakwenda Ikulu kupokea taarifa ya maendeleo ya mkoa wa Ruvuma.

  Aidha, siku ya Jumatatu  atakuwa na shughuli za kufungua  tawi la Benki ya Posta mjini Songea, kukagua  maghala ya Wakala wa Taifa wa  Hifadhi ya chakula  (NFRA) kanda ya Songea na kukagua  makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea.

  Siku inayofuata atatembelea na kukagua Hospitali ya Rufaa ya mkoa, na baadaye kuzungumza na watumishi wa hospitali  hiyo.

  Siku ya nne ya ziara yaani jumatano, Waziri Mkuu atafanya majumuisho ya ziara mkoani humo, kabla ya kuagana na viongozi wa Chama na Serikali na kurejea Dar es Salaam. 

  0 0

  Kazi za usafi wa mazingira kwenye maeneo tofauti Nchini katika kuanza rasmi kwa maadhimisho ya sherehe za kutimia miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar zimeonekana kuitikiwa vyema na Wananchi walio wengi pamoja na vikosi vya ulinzi hapa Nchini. 
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alijumuika na Wananchi hao kwa kazi za usafishaji wa Mtaro wa maji machafu unaokusanya maji kutokea mitaa ya Muembe Njugu, Kwahani, Kariakoo, Kilimani na Kumalizikia Pwani ya Kilimani. 
  Akimuelezea Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhandisi wa Baraza la Manispaa Zanzibar Nd. Mzee Khamis alisema Baraza la Manispaa limeanzisha mradi maalum wa usafi wa mazingira katika Manispaa ya Zanzibar kwa kuwashirikisha moja kwa Wananchi kwenye Mitaa yao. Mhandisi Mzee alisema hatua hiyo itatoa fursa pana kwa kila mwananchi kuona kwamba suala la usafi wa mazingira ambalo linapaswa kuwa la kudumu linaigusa Jamii moja kwa moja badala ya kufikiria kuwa jukumu hilo ni la Baraza la Manispaa pekee. 
  Akizungumza na washiriki wa zoezi hilo la usafi wa mazingira kwa ajili ya kuanza kwa shamra shamra za maadhimisho ya sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia Miaka 52 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliwapongeza Wananchi pamoja na Vikosi vya ulinzi kwa ushiriki wao wa usafi wa mazingira. 
  Katika kazi hiyo ya usafi wa mazingira kuanza rasmi kwa maadhimisho ya sherehe za kutimia Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikabidhi zawadi ya vifaa tofauti vya usafi wa mazingira kwa Kikundi cha usafi wa Mazingira cha Kilimani City. 
  Vifaa hivyo vyenye Thamani ya Shilingi Laki Saba vimetolewa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia Idara yake ya Mazingira ikiwa ni muendelezo wa utaratibu iliyojipangia wa kutoa zawadi za vifaa kila mwaka kwa Vikundi vilivyoonyesha juhudi katika kushiriki kwenye usafi wa mazingira maeneo mbali mbali Nchini.
   Watendaji wa Baraza la Manispaa Zanzibar wakijumuika pamoja na Wananchi na Vikosi vya Ulinzi kwenye usafishaji wa mazingira hapo Mtaa wa Kwahani Uwanja wa Farasi Mjini Zanzibar.
   Balozi Seif akimkabidhi vifaa vya usafi wa mazingira Mwenyekiti wa Kikundi cha Usafi wa Mazingira cha Kilimani { Kilimani City } Nd. Khamis Shaali Chum  { mwenye T. Shirt Nyeupe  }vilivyotolewa zawadi na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia Idara ya Mazingira.Kushoto ya Mwenyekiti huyo wa Kilimani City ni Mkurugenzi Maingira Nd. Juma Bakari Alawi na wa kwanza kutoka Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Mazingira Zanzibar Nd. Juma Mjaja.

   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akishiriki na Wananchi, Vikundi ya vya usafi wa mazingira pamoja na Vikosi vya Ulinzi kwenye usafi wa mazingira hapo Kwahani Uwanja wa Farasi ikiwa ni kuanza rasmi kwa maadhimisho ya sherehe za kutimia Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.
  Baadhi ya wapiganaji wa Vikosi vya ulinzi wakishiriki zoezi la usafi wa mazingira katika Mtaa wa Kwahani Uwanja wa Farasi kuanza kwa shamra shamra za maadhimisho ya sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia Miaka 52. Picha na – OMPR – ZNZ.

  0 0


   Baahi ya Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ wakitandaza kifusi kwa kukiweka sawa katika zoezi la Usafi wa mazingira uliofanyika leo eneo la Soko la Mbogamboga Mombasa Mjini Zanzibar ikiwa ni Uzinduzi wa Sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumzaa na wananchi baada ya kumalizika kwa  zoezi la Usafi wa mazingira uliofanyika leo eneo la Soko la Mbogamboga Mombasa Mjini Zanzibar ikiwa ni Uzinduzi wa Sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akizoa taka katika zoezi la Usafi wa mazingira uliofanyika leo eneo la Soko la Mbogamboga Mombasa Mjini Zanzibar ikiwa ni Uzinduzi wa Sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiteta  akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Magharibi B.Unguja Ayoub Maohammed Mahmoud wakati zoezi la Usafi wa mazingira uliofanyika leo eneo la Soko la Mbogamboga Mombasa Mjini Zanzibar ikiwa ni Uzinduzi wa Sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akibeba taka katika zoezi la Usafi wa mazingira uliofanyika leo eneo la Soko la Mbogamboga Mombasa Mjini Zanzibar ikiwa ni Uzinduzi wa Sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Picha na IKULU, ZnZ

  0 0


  0 0

  Kundi la Mziki la Navy Kenzo Linaloundwa na Aika na Nahreel wametutoa kimasomaso Watanzania Baada ya Video yao ya Wimbo wa Game Walioshirikiana na Vanessa Mdee Kushika Namba Nne katika Chat ya Video 50 Bora za MTV Base Africa Zilizofanya Vizuri mwaka 2015..
  Diamond Platnumz na Wimbo wake wa Nana umeshika namba 5 Katika Chat hizo, Wimbo huo wa Nana Pia Umetengenezwa na Producer Nahreel Kitu kinachomfanya Aendelee kuwa Producer Bora zaidi Kuwahi kutokea Tanzania na East Africa kwa Ujumla, Mwimbaji Wizkid wa Naigeria Ameshika Namba 6.

  Pongezi ziende kwao @nahreel,@aikanavykenzo wanaounda Kundi la Navykenzo. Mwaka Huu Tegemea Mambo Makubwa Kutoka Kwao na The Industry Kwa Ujumla.

  Management/Bookings:
  Paschal M.G
  +255 769 352 825
  +255 782 481 971
  Email: bookings@navykenzo.com
  Website: www.navykenzo.com

  For more information
  Twitter: https://twitter.com/navykenzo
  Instagram: https://instagram.com/navykenzoofficial
  Snapchat: navykenzo
  Be sure to subscribe to our Vevo: https://www.youtube.com/user/NavyKenzoVEVO/videos

  0 0

  Zaidi ya wanafunzi 5,100 wa shule za msingi Wilayani Mufindi Mkoani Iringa, wanatarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza baada ya kufaulu mtihani wa darasa la 07 ulifanyika mapema mwaka jana, huku ufaulu huo ukipanda na kufikia asilimia 80.39 ukilinganisha na asilimia 68.21 ya mwaka 2014.
   Taarifa ya kitengo cha habari na mawasiliano cha halmashauri ya wilaya ya mufindi kwa nyombo vya habari, imetanabaisha kuwa, wanafunzi waliokuwa wamesajiliwa   kufanya mtihani walikuwa 7,220 na miongoni mwao waliofaulu na kuchaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari ni 5,198.
  Taarifa hiyo imeainisha mgawavyo wa wanafunzi hao kwa kuzingatia jinsi, ambapo kati ya waliofaulu, wasichana wameongoza kwa takwimu za ufaulu huo wakiwa elfu 2,831 wakifuatiwa na wavulana 2,367. Aidha, wanafunzi wote waliofaulu wamepangiwa shule ili kuendelea na elimu ya sekondari itakayokuwa ikitolewa bure hapa nchini.
  Wilaya ya Mufindi yenye jumla ya shule za msingi 178 imeshika nafasi ya pili Mkoani Iringa kwa kufaulisha wanafunzi wengi kwaasilimia 80.39 ikitanguliwa na Manispaa ya Iringa iliyofaulisha kwaasilimia 80.55 ikiwa na jumla ya shule za msingi 50.

  0 0


  UD1
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya kukusanya Zaka na Sadaka Zanzibar (JUZASA) Shekh. Said Masoud (Gwiji) akitoa maelezo ya Jumuiya na kumkaribisha mgeni rasmi (kushoto) Katibu Mtendaji Kamisheni ya Wakfu na Mali ya amana Zanzibar Shekh. Abdalla Talib kufungua Mkutano wa Jumuiya hiyo uliofanyika katika ukumbi Sha-Ntimba Mombasa Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanziba
  UD2
  Baadhi ya wanachama wa Jumuiya na wageni walikwa wakisikiliza nasaha za Mwenyekiti wa Jumuiya ya kukusanya Zaka na Sadaka Zanzibar (JUZASA) Shekh. Said Masoud (Gwiji) hayupo pichani wakati wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo.
  UD3
  Mjumbe wa Bodi ya Jumuiya hiyo Dkt. Muh’d Hafidh akitoa neno la shukrani mara baada ya kumaliza kwa Mkutano. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.  
  ………………………………………….
  Na Maelezo Zanzibar.

  Taasisi za kiislamu nchini zimeshauriwa kushawishi kuwepo kwa mfumo wa pamoja wa ukusanyaji wa Zaka na Sadaka ili ziweze kuleta tija katika kundi kubwa la jamii ya Kislam.

  Katibu mtendaji wa kamisheni ya mufti namali ya amana Zanzibar sheikh abdalla talib amesema Lengo la mfumo huo uliwekwa kwa mujibu wa sheria za kiislamu ni kusadia na kupunguza umasikini katika jamii lakini kwa sasa wengi wanaotaoa sadka hizo hazifikii lengo hilo kwa vile kumekosekana mfumo bora  unaowafikia watu wengi na kuleta mabadiliko makubwa.

  Akifungua mkutano wa jumuiya ya zaka na sadaka Zanzibar ZASA ametolea mfano wan chi ya denmar amabyo ina waislamu kwa asilimi 3 tu imekuw ana utaratibu mzuri wa ukusanyaji wa sadka na zaka  hali iliyofanikisha kupatikana  misaada mingi iliyosaidia  katika nchi hiyo na hata nchi nyengine.

  Amefahamisha kuwa  kwa kuwa  Zanzibar asilimia kubwa ya wanananchi wake ni waislamu ina nafasi ya kufikia malengo hayo kama pia itatoa elimu kwa wananchi hasa wenye uwezo  ili kufahamu  umuhimu wa Ibada hiyo pamoja na njia bora za kutoa zaka na sadaka katika jamii.
  Nae mwenyekii wa jumuiy hiyo sheikh said masoud  amesema kwa sasa umekuwa na mwamko mdogo hasa kwa wafanyabiashara kutoa zaka na sadaka  kulingana na taratibu zinazotakiwa  kidini.

  Nae katibu wa jumuiya hiyo ya jusaza omar abubakar Mohamed amesema jumuiya hiyo  imeshatoa zaka kwa watu 46 zikiwemo za fedha taslim, charahani, friza na wengine kujengewa nyumba.  

  0 0

  e92a2ca8-1b8e-49f8-a0bc-fa4646427e30

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary   (kushoto kwake )  wakielekea kwenye Chumba cha mapumziko baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Songea na kupokelewa na wanachi na viongozi wa mkoa huo Januari 3, 2016.  Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma , Thabiti Mwambungu na kushoto ni Mbunge wa Songea Leonidas Gama. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0


  WANANCHI wa mikoa mbalimbali wamejitokeza kuiomba kkampuni ya Msama Promotions ianzie Tamasha la Pasaka mikoa kwao mwaka huu huku wakazi wa dare s salaam wakisisitiza libaki mkoani humo.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama ameliambia Gazeti hili kuwa, tayari amepokea maombi toka kwa wananchi na mashabiki wa mikoa ya Morogoro, Mwanza, Mbeya, Dodoma na Dar es Salaam wakitaka tamasha hilo lianzie kwao mwaka huu.

  “Kamati yangu  inafuata taratibu za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambazo ni pamoja na kupata kibali cha kufanikisha kufanyika kwa Tamasha hilo linaloshirikisha waimbaji mbalimbali wa muziki wa Injili  wa ndani na nje ya Tanzania,” amesema Msama.

  Salum Ismail Hamad ambaye ni mdau mkubwa wa Tamasha la Pasaka amesema anawaomba waandaaaji wa Tamasha hilo kutoliondoa jijini Dar es Salaam kwa sababu ni mkoa unaohusisha idadi kubwa ya mashabiki wa muziki wa Injili.

  Rukia Joseph wa Kimara Dar es Salaam, alisema yeye anawapigia magoti waandaaji  kutoliondoa tamasha hilo jijini  Dar es Salaam hasaa kwa waimbaji wa nje ya Tanzania kama Solly Mahlangu na wengineo toka nje ya nchi.


  Michael Deogratius alisema  ni ngependa Tamasha la Pasaka lihamie mikoani  kwa sababu ya ukubwa na umuhimu wa tamasha hilo ambalo linatimiza miaka 16 tangu kuasisiwa kwake.Msama alisema bado wanasubiri taratibu za kufanikisha tamasha hilo  kutoka Basata, hivyo nawaomba wakazi wa mikoani kuvuta subira wakati wakijiandaa.

  0 0
  0 0

  Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewataka watendaji wa Shirika la Reli nchini (TRL) na Kampuni Hodhi ya Mali za Reli (RAHCO) kuhakikisha sehemu ya reli iliyosombwa na mafuriko wilayani Kilosa mkoani Morogoro inaunganishwa ndani ya siku tatu na huduma za treni kurejea. 
  Prof. Mbarawa amesema hayo baada ya kukagua sehemu ya reli hiyo kutoka Kilosa hadi Magulu- Kidete kuona athari zilizosababishwa na mafuriko yaliotokana na mvua zilizonyesha katika mikoa ya Iringa na Dodoma. 
  “ Fanyeni kazi usiku na mchana ili ikifika alhamisi mawasiliano ya reli kati ya mkoa wa Morogoro na Dodoma yawe yamerejea na abiria waendelee kupata huduma ya treni ,” amesema Waziri Prof. Mbarawa. 
  Amewahakikishia wananchi wa vijiji vya Munisagara, Mkadage, Mzaganza, Magulu na Kidete ambao usafiri wao pekee wa uhakiki ni wa kutumia reli watoe ushirikiano kwa serikali ili ukarabati na ujenzi wa reli hiyo ukamilike kwa haraka. 
  Amewataka wananchi waishio pembezoni mwa reli katika wilaya ya Kilosa kupanda miti ili kuzuia mmomonyoko wa udongo unaosababisha mafuriko kwa urahisi wakati wa mvua na kubomoa reli kila wakati.
  “Pandeni miti, lindeni miundombinu ya reli na acheni vitendo vya uharibifu wa mazingira ili ujenzi wa mwaka huu uwe wa kudumu na reli isiathiriwe kirahisi na kuwasababishia kero wananchi,” amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa. 
  Naye Diwani wa kata ya Kidete Bw. Mohamed Seleman Mbunda amemhakikishia Waziri Mbarawa kuwa wananchi wake watashirikiana na serikali kulinda mazingira ili kudhibiti mafuriko yanayoharibu miundombinu ya reli kila wakati wilayani humo. 
  Mafuriko wilayani Kilosa ni matokeo ya mvua zinazonyesha katika mikoa ya Iringa na Dodoma ambayo husababisha maji ya mto mkondoa kuacha mkondo wake na kubomoa tuta la reli katika eneo la Msagali hadi Kilosa kila wakati. Mvua za hivi karibuni zilizonyesha mkoani Iringa na Dodoma zimesomba reli katika eneo la Magulu-Kidete kilomita 315 kutoka Dar es Salaam na kukata mawasiliano ya reli kwa siku tatu sasa. 
  Katika hatua nyingine Waziri Prof. Mbarawa amewataka watendaji wa TRL na RAHCO kutafuta suluhisho la kudumu katika madaraja 32 yaliyo katika mtandao wa reli ya kati ili yasiathiriwe na mvua wakati wote.
   Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Profesa, Makame Mbarawa wa kwanza (kushoto), akitoa maelekezo kwa viongozi wa shirika la reli Tanzania TRL na kampuni hodhi  ya mali za reli RAHCO kuhusiana na ujenzi wa reli

   Sehemu ya tuta la reli lililosombwa na maji katika kijiji cha magulu kama inavyoonekana kwa upande wa chini.

   Sehemu ya tuta la reli lililosombwa na maji katika kijiji cha Magulu

   Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Profesa, Makame Mbarawa akipanda kiberenge tayari kwa ukaguzi wa sehemu ya reli iliyosombwa na maji wilayani Kilosa.
  Athari ya maji kijijini Magulu

  0 0

  Mmiliki wa kiwanda cha uongezaji thamani madini ya jasi kilichopo mkoani Singida, Emmanuel Shilla akimuonesha Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (wa kwanza kushoto) moja ya bidhaa za urembo wa ndani ya nyumba unaotengenezwa kutokana na madini ya jasi yanayopatikana mkoani Singida.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (wa kwanza kushoto) akitazama jinsi madini ya jasi yanavyotumika kutengeneza vitu mbalimbali ikiwemo urembo wa ndani ya nyumba mara baada ya kutembelea kiwanda cha uongezaji thamani madini ya jasi cha Singida Cornice.Aliyevaa shati jeupe ni mmiliki wa kiwanda, Emmanuel Shilla.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akiangalia jinsi mtambo wa bayogesi ulivyomwezesha mmiliki wa mtambo huo, Habiba Sengasu (kulia) kupata faida mbalimbali ikiwemo nishati ya kupikia. Naibu Waziri aliutembelea mtambo huo akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya Nishati na Madini mkoani Singida.

  Na Teresia Mhagama, Singida 
  SERIKALI imesema kuwa itanyang’anya vitalu vya madini visivyoendelezwa na kuwapatia wachimbaji wadogo nchini ili waviendeleze. 

  Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani wakati akizungumza na Mkuu wa wilaya ya Manyoni Fatma Toufiq kabla ya kukagua miradi ya uchimbaji madini pamoja miradi ya umeme wilayani humo.

  “Tutachukua maeneo yasiyoendelezwa na kuwagawia wachimbaji wadogo kama sheria ya madini ya mwaka 2010 inavyoelekeza hivyo Kamismhna Msaidizi wa Madini Kanda hii ya kati hakikisha hilo linatekelezwa,’’ alisema Dkt. Kalemani.

  Naibu Waziri alitoa agizo hilo baada ya Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Fatma Toufiq kumueleza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wachimbaji wadogo katika wilaya hiyo ikiwemo utumiaji wa zana duni za uchimbaji madini pamoja na ukosefu wa maeneo ya uchimbaji madini kutokana na watu wengi kuhodhi maeneo hayo kwa muda mrefu bila kuyafanyia kazi.

  Aidha, Mkuu wa wilaya alimueleza Naibu Waziri kuwa licha ya changamoto za wachimbaji wadogo, wilaya hiyo pia inakabiliwa na changamoto ya umeme kukatika mara kwa mara jambo ambalo linaathiri shughuli za kiuchumi za wananchi katika wilaya hiyo.

  Akifafanua suala hilo Naibu Waziri alimueleza kuwa umeme katika wilaya hiyo na mikoa ya Iringa, Singida, Dodoma na Kanda ya Ziwa utatengemaa mara baada ya ujenzi wa njia kuu ya umeme wa msongo wa kilovolti 400 kutoka Iringa hadi Shinyanga kukamilika mwezi Juni mwaka huu kwani mitambo hiyo itasafirisha umeme kwa kiwango kikubwa tofauti na miundombinu ya sasa ambayo inasafirisha umeme kwa msongo kilovolti 220.

  Hata hivyo Naibu Waziri aliwataka watendaji wa Tanesco katika wilaya hiyo kuhakikisha kwamba umeme haukatiki kwa sababu ya uzembe wa kibinadamu kufanya au kutokufanya kitu fulani bali utokane na majanga ya kiasili ambayo hayazuiliki.

  “ Watendaji wa Tanesco nileteeni taarifa kwa nini umeme unakatika mara kwa mara katika wilaya hii na kama ni uzembe wa mtu basi naye akatike hapohapo,” alisisitiza Dkt. Kalemani.

  Wakati huohuo Naibu Waziri ameitaka kampuni ya spencon iliyopewa tenda ya kusambaza umeme katika vijiji 90 mkoani Singida kukamilisha kazi hiyo ifikapo mwezi Mei mwaka huu.

  Naibu Waziri alitoa agizo hilo baada ya kampuni hiyo kusuasua katika kusambaza umeme vijiini kwani kazi ya kusambaza umeme katika vijiji hivyo ilipaswa kukamilika mwezi wa 11 mwaka jana lakini hadi sasa wamesambaza umeme katika vijiji 17 tu.

  “Mradi huu unahusisha kilomita 188 lakini mpaka sasa nguzo zimefikia kilomita 48 tu, asipokamilisha kazi hii kwa muda huu tuliompa tutataifisha mali zake, na watendaji wa Tanesco mniletee taarifa ya kina sababu za mradi huu kuchelewa na hatua mlizochukua,” alisema Dkt. Kalemani.

  0 0


  Promota Juma Msangi kushoto akiwa na Rais wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassin Abdallah ‘Ustadhi’ pamoja na Meneja msaidizi wa bondia  Fransic Cheka  wakitambulisha mpambano wa bondia Cheka mbele ya waandishi wa habari mpambano utakaofanyika Feb 27 katika uwanja wa Leaders Club .
   
   Promota Juma Msangi kushoto akiwa na Rais wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassin Abdallah ‘Ustaadhi’ pamoja na Meneja msaidizi wa bondia  Fransic Cheka  wakitambulisha mpambano wa bondia huyo mbele ya waandishi wa habari mpambano huo utakaofanyika Feb 27 katika uwanja wa Leaders Club Picha naSUPER D BOXING NEWS

older | 1 | .... | 1077 | 1078 | (Page 1079) | 1080 | 1081 | .... | 3286 | newer