Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1076 | 1077 | (Page 1078) | 1079 | 1080 | .... | 3286 | newer

  0 0


  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence S.Milanzi akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na Naibu wakatibu wakuu iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Jaji Meja Jenerali Projest A.Rwegasira akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na  Naibu wakatibu wakuu  iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria,Amon Mpanju akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na  Naibu wakatibu wakuu  iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,Profesa James Epiphan Mdoe akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na  Naibu wakatibu wakuu  iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango,Amina H.Shaban akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na  Naibu wakatibu wakuu  iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eng. Juliana Leonard Kajala Pallangyo, akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na  Naibu wakatibu wakuu  iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Na Sultani Kipingo Alianza na Dkt. Abdallah Possi, wakafuata Profesa James Epiphan Mdoe na Mhe. Amon Anastaz Mpanju na kusababisha mshangao wa furaha miongoni mwa wananchi wenye ulemavu kwa kile wanachokitaja kama kukumbukwa katika uongozi wa Serikali ya awamu ya Tano ya Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. 
  Rais alipomteua Dkt. Abdallah Possi kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, kazi, Ajira, Bunge, Vijana na walemavu wengi walifurahi kuona Mtanzania wa kwanza mwenye ualbino anaingia katika Baraza la Mawaziri 
  Furaha hiyo ilizidi alipowatea Mhe. Amon Anastaz Mpanju mlemavu wa kuona kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria na Profesa James James Epiphan Mdoe kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, ambaye ni mlemavu wa miguu.
   Mhe Mpanju, ambaye kitaaluma ni mwanasheria na ambaye pia alikuwa mmoja wa wajumbe wa Bunge la Katiba, alishangaza kila mtu wakati alipokula kiapo mbele ya Rais bila kusoma mahali kama ilivyo desturi. 
  “Huyu bwana pamoja na ulemavu wake hakika ni mtu wa kazi” alisikika mmoja wa wageni waliohudhuria hafla ya kuapishwa Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu wakuu Ikulu siku ya Mwaka mpya. 
  Akiwa amesindikizwa na mke wake, Mhe. Mpanju alipokea Biblia Takatifu na kuinyanyua juu na kuanza kula kiapo, ingawa mkewe alikuwa ameshika karatasi ya maandiko ya vitoneambayo ilikuwa aitumie. Hata Rais alitabasamu kwa hilo. 
  Huko mitaani, ambako tukio hilo la kuapishwa Makatibu wakuu lilikuwa likirushwa ‘live’ na vituo kadhaa vya TV na Redio na mitandao, wengi walishikwa na butwaa, huku wakimsifia Rais Magufuli kwa kuwakumbuka watu wenye ulemavu. 
  Waliendelea kufurahi walipomuona Profesa James James Epiphan Mdoe, ambaye ni msomi aliyebobea katika Kemia,  akisogea mbele kwa mikongojo miwili na kula kiapo cha kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini. 
  “Tingatinga (Rais Magufuli) ametukuna kweli kwa uteuzi wa viongozi hawa”, mwananchi aliyejitambulisha kwa jina la Gaddy aliiambia Globu ya Jamii kwa njia ya simu kutokea mjini Iringa. Gaddy, ambaye yeye ni mlemavu wa miguu, amesema kitendo cha kuteua wananchi wenye ulemavu kushika madarka ya juu serikalini kimewapa furaha na faraja kubwa kiasi hata yeye anajisikia ana cheo tayari. 
  Mwananchi mwingine wa mjini Lindi aliyesema anaitwa Mohamed Mpanyachi alipiga simu na kusema kwamba anategemea Rais Magufuli ataendelea kuwapa nafasi walemavu katika ngazi mbalimbali kwani kama walivyo hao watatu, wananchi wenye ulemavu ambao ni wasomi na wenye uwezo wa kuongoza wamejaa kila pembe nchini.
   Dkt. Abdallah Possi, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, kazi, Ajira, Bunge, Vijana na walemavu - siku alipoapishwa rasmi Ikulu jijini Dar es salaam Desemba 13, 2015
   Profesa James James Epiphan Mdoe akila kiapo kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini mbele ya Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo January 1, 2016
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Mhe. Amon Anastaz Mpanju akiongozwa na msaidizi wake kujiunga na viongozi wenzie ili kutia saini Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma  mbele ya Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo January 1, 2016

  0 0

   Mama wa mitindo Asya Idarous Khamsini akihesabu sekunde zilizoslia kuelekea mwaka mpya kwenye sherehe ya mkesha wa mwaka mpya 2016 iliyofanyika Lanham, Maryland siku ya Alhamisi Desemba 31, 2015 iliyoandaliwa na Jumuiya ya Watanzania DMV na kuwakutanisha wana DMV na familia zao wakiwemo marafiki kutoka majimbo mengine huku wengine wakiokea Tanzania. PICHA NA KILIMANJARO STUDIO
  Wafuangaji champagne wakiwa tayari kama kikosi cha mizinga wakisubilia sekunde zilizobaki kuingia mwaka 2016 kuachia mizinga yao ikiwa ni sehemu yakusherehekea mwaka mpya wa 2016.
   Mama wa mitindo Asya Idarous Khamsini akifuahia kuuona mwaka mpaya, wapili toka kulia ni Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwn. Iddi Sandaly pamoja na Asha Hariz (kulia) wakifurahia kuuona mwaka 2016.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0
 • 01/02/16--00:24: UCHAMBUZI WA MAGAZETI LEO.

 • 0 0

  Heri ya mwaka mpya. Nina furaha kuwafahamisha kuwa kitabu kipya, "Dokta John Pombe Magufuli: Safari ya Urais, Mafaniko na Changamoto katika Urais wake" sasa kinapatikana. Kitabu hiki ni mfululizo wa vitabu kadhaa ninavyotarajia kuvichapisha mwaka huu 2016. 

  Wakati kitabu hiki kikiingia sokoni, kitabu kingine kuhusu taaluluma ya Usalama wa Taifa kipo katika hatua za mwisho, na matarajio ni kukiingiza sokoni mwishoni mwa mwezi huu.

  Kitabu hiki cha Dokta Magufuli kina sura sita. Katika utangulizi, kitabu kinazungumzia mazingira ya uchaguzi mkuu uliopita, msisitizo ukiwa kwenye hali ya nchi ilivyokuwa kabla ya uchaguzi huo.

  Kadhalika, utangulizi huo unaelezea mabadiliko ya ghalfa ya kisiasa, hususan ndani ya CCM, yaliyojitokeza kufuatia jina la mwanasiasa aliyekuwa maarufu kuliko wote wakati huo, Edward Lowassa, kukatwa na chama hicho tawala wakati wa mchakato wa kupata mgombea wake wa kiti cha urais.

  Sura ya kwanza inamtambulisha Dokta Magufuli, kwa kuangalia historia fupi ya maisha yake. Sura ya pili inaeleza mchakato aliopitia Dkt Magufuli hadi kuibuka mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM. Sura hii inachambua kwa undani ushindani miongoni mwa makada zaidi ya 40 waliochukua fomu kuwania urais kupitia chama hicho.

  Sura ya tatu inaelezea fursa alizokuwa Dokta Magufuli na CCM kwa ujumla katika kipindi cha kampeni na uchaguzi mzima kwa ujumla. Sura hii inachambua uimara wa mwanasiasa huyo sambamba na turufu za kawaida za CCM katika kila uchaguzi. Kwa uapnde mwingine sura hiyo yaangalia pia mapungufu yaliyopelekea urahisi kwa Dokta Magufuli kumshinda mpinzani wake mkuu Lowassa, sambamba na mapungufu ya UKAWA yaliyoiwezesha CCM kushinda.

  Sura ya nne inajadili changamoto na vikwazo kwa Dokta Magufuli na CCM kwa ujumla wakati wa kampeni. Kadhalika, sura hii inazungumzia jinsi Lowassa na UKAWA walivyoshindwa kutumia changamoto hizo za wapinzani wao.

  Sura ya tano inajadili urais wa Dokta Magufuli tangu aingie Ikulu, wakati sura ya mwisho inajadili changamoto zinazoukabili urais wake na kutoa mapendekezo.

  Nimejitahidi kadri nilivyoweza kuandika kitabu hicho kama mtu niliyeufuatilia uchaguzi huo kwa karibu. Natambua kuna wanaoweza kuwa na hofu kuwa 'niliisapoti CCM na Dokta Magufuli wakati wa kampeni, na kutoiunga mkono UKAWA na Lowassa.' Naomba kuwatoa hofu kwani kitabu hiki ni si cha kiitikadi bali kwa ajili ya Watanzania wote bila kujali tofauti zao za kiitikadi.

  UTAKIPATAJE?

  Bei ya kitabu sasa ni Shilingi 4,000 tu. Ili kukipata, nunua kwa M-PESA namba 0744-313-200 jina JOHN ZABLON MPEFO au TIGO-PESA namba 0652-112-071 jina CHRISTINE JOHN MANONGI

  KARIBUNI SANA

  0 0

  Miss Tanzania USA Aeesha Kamara akipata picha ya upendeleo alipofika kwenye mkesha wa mwka mpya ulioandaliwa na Jumuiya ya Watanzania DMV siku ya Alhamisi Desemba 31, 2016 Lanham, Maryalnd nchini Marekani. PICHA NA KILIMANJARO STUDIO
  Asha Hariz Kushoto) pamoja na mama wa mitindo Asya Idarous Khamsini wakipata picha ya pamoja na Miss Tanzania USA Pageant alipohudhuria mkesha wa mwaka mpya DMV.
  Aeesha Kamara katika picha ya pamoja na msanii Patience Ibembo wa Congo mwenye makzi yake Marekani kwa sasa ambaye zamani alikuamcheza show wa Koffi Olomide.

  0 0

  Katika kuboresha na kufanya maisha ya Watanzania kuwa murua, Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii”Vodacom Foundation”, imekabidhi msaada wa vitu mbalimbali na vyakula wenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 29 kwa kituo cha walemavu mbalimbali wakiwemo wenye ulemavu wa ngozi, Albino, kilichopo katika Manispaa ya Shinyanga. 
   Akikabidhi msaada huo kwa uongozi wa kituo hicho, Kaimu Mkuu wa Vodacom kanda ya Tanganyika, Sabas Ademba amesema kampuni hiyo imeamua kusherehea sikukuu ya mwaka mpya 2016 kwa kuijali jamii ya watu wenye mahitaji muhimu hapa nchini.
  Zoezi la msaada huo unaotolewa kupitia kampeni maalum ijulikanayo kama Pamoja na Vodacom inayotoa misaada mbalimbali wakati wa msimu wa sikukuu itafanyika nchi nzima huku kituo hicho kimenufaika na jozi za viatu, soksi, fulana, masweta, sare za shule, Kofia pana kwa ajili ya kujizuia na jua, shuka na vyandarua,Vingine ni madaftari, kalamu seti za hesabu, sabuni, dawa za meno, vifaa vya usafi kama mafagio na dawa za vyooni huku upande wa chakula ni pamoja na mchele, Unga, maharagwe, mafuta ya kupikia na Chumvi.. 
   Katika hatua nyingine wahudumu wa afya wa zahanati iliyopo katika kituo hicho wamesema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa dawa zinazohitajika kwa matibabu ya watoto hao wenye ulemavu wa ngozi.Wakizungumza na waandishi wa habari wahudumu hao wa afya wamesema watoto hao wanakabiliwa na magonjwa ya aina mbalimbali ikiwemo kukumbwa mara kwa mara na magonjwa ya Ngozi, Kuhara, U.T.I na Minyoo. 
   Grace Lali anasema kufuatia kuwepo kwa magonjwa hayo zahanati hiyo imekuwa ikikabiliwa na ukata wa dawa za kuwahudumia hali ambayo imewafanya kulifikisha suala hilo kwa mganga mkuu wa manispaa ya Shinyanga ili hatua zaidi zichukuliwe,
  Aliipongeza Vodacom Foundation kwa kuwajali watoto hao na anatoa wito kwa makampuni mengine kuiga mfano wa mfuko huo hivyo anawaomba watu binafsi, asasi za serikali na zisizo za serikali, mashirika na makampuni kujitokeza kuwasaidia madawa ili watoto hao waweze kukua katika afya njema. 
   Naye Felister John, muuguzi katika kituo hicho amesema watoto hao wanakabiliwa na uhaba vitamini A, kutokana na kula chakula cha aina moja tu, ya wanga, ambavyo ni ugali, ubwabwa na maharage. 
   "Watoto hawa wanahitaji matunda, vyakula bora kama nyama, maziwa ambavyo ni adimu sasa kukosekana na kwa vitu hivyo kunawafanya kuwa wadumavu" Alisema Felister John. 
   Mkuu wa kituo hicho Peter Ajali, anasema misaada wanayoipata ikiwemo iliyotolewa na Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Pamoja na Vodacom unasaidia kupunguza makali ya uhitaji wa watoto hao.
  Kwa mujibu wa mkuu huyo wa kituo cha Buhangija chenye watoto takribani 400, kinaendeshwa kwa kutegemea misaada kutoka kwa wahisani kwa kuwa serikali inawahudumia watoto 40 tu kwa kufuata takwimu za zamani. Mwisho.
   Baadhi ya watoto wenye ualbino wanaolelewa katika kituo maalum kilichopo katika Manispaa ya Shinyanga mjini wakiwa katika hafla fupi ya kukabidhiwa msaada wa vifaa mbalimbali vya michezo na vyakula wenye thamani ya zaidi ya  Shilingi milioni 29 uliotolewa na Vodacom Foundation kwa ajili ya sikuu ya mwaka mpya na kukabidhiwa na Kaimu Mkuu wa Vodacom Tanzania wa kanda ya Tanganyika,Sabas Ademba(hayupo pichani)
   Kaimu Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya Tanganyika,Sabas Ademba akiongea na watoto wenye ulemavu wa Ngozi”Albino”wanaolelewa katika kituo maalum kilichopo katika Manispaa ya Shinyanga mjini wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa msaada wa vifaa mbalimbali vya michezo na vyakula wenye thamani ya zaidi ya  Shilingi milioni 29 uliotolewa na Vodacom Foundation,kupitia program yake ya Pamoja na Vodacom kwa ajili ya sikuu ya mwaka mpya.

  Mkuu wa kituo maalum cha kulelea watoto wenye ulemavu wa ngozi cha Manispaa ya Shinganga, Peter Ajali(kushoto)akikabidhiwa moja ya msaada wa vifaa  mbalimbali vya michezo na vyakula vyenye thamani ya zaidi ya  Shilingi milioni 29  na Kaimu Mkuu wa Vodacom Tanzania wa kanda ya Tanganyika,Sabas Ademba(kulia)uliotolewa na Vodacom Foundation kwa ajili ya sikuu ya mwaka mpya.


  0 0


  0 0

  LIGI Daraja la kwanza inaendelea kesho kwa michezo miwili huku timu ya Friends Rangers (pichani) ya Dar es salaam ikishuka kwenye Uwanja wa mabatini Mlandizi kuvaana na timu ya KMC.

  Ofisa Habari wa klabu ya Friends Rangers, Asha Kigundula, alisema kuwa wanatambua ugumu wa mechi hiyo lakini lengo lao ni kushinda na kupata pointi tatu.
  Kigundula alisema anatambua kama wapinzani wao wamejipanga kushinda, lakini nao wapo kwa lengo la kufanya vizuri na kuondoka na pointi tatu.
  Alisema wao hawajataka tamaa wana amini bado wana nafasi ya kupigania kupanda daraja na kucheza ligi kuu msimu ujao.
  "Mechi ngumu sana lakini tumejipanga kushinda mchezo wetu huu, tunatambua uzuri wa KMC lakini nasi tuko vizuri kama tulivyowatoa kwenye michuano ya FA Cup.
  Alisema kuwa wapo katika nafasi nzuri ya kupigana na kufanikiwa kuvuka vizingiti wanavyowekewa na baadhi ya wadau wengi.
  Wakati huo huo mechi nyingine ya ligi hiyo itakuwa kati ya Africa Lyon dhidi ya Kiluvya United mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa Karume.

  0 0


  0 0

  Othman Khamis Ame Ofisi ya 
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar 
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba Maadhimisho ya Sherehe za kutimia Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 yatafanyika kama kawaida na kupangwa kuanza rasmi kesho jumapili ya Tarehe 3 Januri 2016. 
  Alisema Serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha kwamba katika muda wote wa maandamisho hayo kunakuwa na hali ya utulivu na usalama mkubwa katika maeneo yote ya Visiwa vya vya Unguja na Pemba. 
  Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Maadhimisho ya Kitaifa Zanzibar alisema hayo wakati akitoa Taarifa rasmi ya ratiba ya maadhimisho ya sherehe za Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar mbele ya Wana Habari hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. 
  Alisema suala la upande wa Upinzani kuzisusia sherehe za Mapinduzi kwa kisingizio cha Rais aliyepo madarakani si halali ni muendelezo wa kuwapotosha Wananchi walio wengi nchini. 
  Balozi Seif alifafanua kuwa Rais wa sasa Dr. Ali Mohammed Shein ataendelea kuwa rais hadi yule atakayechaguliwa rasmi na kihalali na Wananchi ale kiapo kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kama ilivyokwishatolewa ufafanuzi na wanasheria walio wengi. 
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alieleza kwamba Miradi yote ya Maendeleo ipatayo 24 ambapo 16 ikiwa imekamilika na Minane inatarajiwa kuwekwa mawe ya msingi imehusishwa katika maadhimisho hayo itakayoanza Jumatatu ijayo. 
  Alisema madhimisho hayo yataanza rasmi kesho Jumapili ikiwa ni siku maalum kwa kazi za usafishaji wa masingira katika maeneo mbali mbali Unguja na Pemba ukilenga zaidi katika sehemu za kutolea huduma za kijamii kama Hospitali, Vituo vya Afya pamoja na masoko. 
  Mwenyekiti huyo wa Halmashauri ya Maadhimisho ya Kitaifa Zanzibar alifahamisha kwamba ingawa zoezi hilo hufanyika kila zinapoanza sherehe za Mapinduzi lakini mwaka huu juhudi malum zinapaswa kuchukuliwa ili kuhakikisha maeneo yote yanakuwa katika hali ya usafi muda wote. Akigusia suala la hatma ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar ambalo limekuwa agenda kubwa kwa baadhi ya watu wakiwemo hata wanasiasa nchini wakiendelea kupotosha Wananchi Balozi Seif alisema Taarifa rasmi ya vikao vinavyowakutanisha Viongozi wa juu kulijadili suala hilo itatolewa rasmi mara baada ya kukamilika kwa mazungumzo hayo. 
  Hata hivyo Balozi Seif alitanabahisha kwamba Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar { ZEC } kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ndio yenye mamlaka ya kuendesha na kusimamia uchaguzi Mkuu wa Zanzibar. 
  Alisema kwa vile tume hiyo kupitia Mwenyekiti wake haikuridhika na mazingira yaliyojichomoza wakati wa zoezi la kupiga kura na kulazimika kufuta Uchaguzi pamoja na matokeo yake yote Taasisi hiyo hiyo ndio yenye uwezo wa kuitisha uchaguzi mwengine kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar. Akijibu baadhi ya maswali ya Waandishi wa Habari Balozi Seif alisema katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 iko wazi na kutoa mamlaka kwa tume ya uchaguzi ya Zanzibar kupanga uchaguzi mwengine kufuatia kufutwa kwa ule wa mwezi oktoba mwaka 2015. 

  Wanahabari wa Vyombo mbali mbali wakimsikiliza kwa makini Balozi Seif akitoa Taarifa rasmi ya maadhimisho ya Sherehe za  Mapinduzi ya Zanzibar kutimia Miaka 52.
  Balozi Seif ambae pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Maadhimisho ya Kitaifa Zanzibar akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa Habari wakati akijibu baadhi ya maswali aliyoulizwa.

  0 0

  Kundi la Mziki la Navy Kenzo Linaloundwa na Aika na Nahreel wametutoa kimasomaso Watanzania Baada ya Video yao ya Wimbo wa Game Walioshirikiana na Vanessa Mdee Kushika Namba Nne katika Chat ya Video 50 Bora za MTV Base Africa Zilizofanya Vizuri mwaka 2015..

  Diamond Platnumz na Wimbo wake wa Nana umeshika namba 5 Katika Chat hizo, Wimbo huo wa Nana Pia Umetengenezwa na Producer Nahreel Kitu kinachomfanya Aendelee kuwa Producer Bora zaidi Kuwahi kutokea Tanzania na East Africa kwa Ujumla.
  Mwimbaji Wizkid wa Naigeria Ameshika Namba 6.

  Pongezi ziende kwao @nahreel,@aikanavykenzo wanaounda Kundi la Navykenzo
  Pia Pongeze Kwa Diamond Platnumz kwa Kuwa Namba 5 Katika Chat Hiyo...

  Mwaka Huu Tegemea Mambo Makubwa Kutoka Kwao na The Industry Kwa Ujumla...

  0 0
 • 01/02/16--11:26: INTRODUCING CBH'S "SEREBUKA"

 • 0 0

  Picha na Maelezo na Festo Sanga 
  Ile kauli ya HAPA KAZI TU imeendelea kutumika vizuri kwa mawaziri wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kufuatia tukio la mawaziri watatu kufika eneo la Machinjio ya Vingunguti kwa ajili ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wanaotumia eneo hilo kwa shughuli za kuchinja mifugo. Awali,Mhe Mwigulu Nchemba alifanya ziara ya kushitukiza usiku wa tar 01/01/2016 katika machinjio hayo na kukutana na madudu ya kutafunwa kwa fedha za ushuru unaokusanywa kwenye mifugo, lakini pia hali ya mazingira ya kutoridhisha ya Machinjio hayo. 
  Hii leo mapema majira ya saa 3 asubuhi, Mhe. Mwigulu Nchemba amerejea tena kwenye machinjio hayo akiwa ameongozana na mawaziri wawili - Mhe George Simbachawene(TAMISEMI) na Mhe Dkt. Hamisi Kigwangallah(AFYA) ambao wote wanagushwa na machinjio hayo. 
  Mara baada ya kusikiliza kero na maoni ya pande zote mbili,Mawaziri hao waliamua kuchua hatua zifuatazo kwa wahusika. 
  Mhe. Mwigulu Nchemba ameagiza Mkuu wa mnada na watumishi waliokuwa zamu tarehe 24/12/2015 na tar 01/01/2016 watafute kazi nyingine kuanzia sasa, na vilevile wahakikishe Jumatatu wanafika ofisi ya Katibu Mkuu wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi. 
  Pili, Mhe. Mwigulu Nchemba ameagiza kuanzia sasa amesitisha ukusanyaji wa ushuru kwenye eneo la mnada wa Pugu,badala yake makusanyo yote yatafanyika eneo la machinjio la Vingunguti kwa kutumia mashine za kielektroniki za EFD. 
  Tatu, Mhe. Mwigulu Nchemba ameagiza wananchi kuanzia leo waanze kutumia eneo lililokuwa limetengwa kwa ajili ya kutunzia nyama. Eneo hilo awali lilisitishwa bila sababu maalum na umeme ukakatwa. Mhe. Mwigulu Nchemba ameagiza umeme urudishwe hii leo na wananchi waanze kutumia eneo hilo. 
  Wakati huohuo,Waziri wa TAMISEMI Mhe Simbachawene ameagiza watumishi wote wa machinjio hayo kujitathimini na kufika Jumanne waripoti ofisini kwake wakiwa na Mkurugenzi wa Manispa ya Ilala kwa ajili ya hatua Zaidi. 
  Mhe. Simbachawene ameenda mbali zaidi kwa kumuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kuhakikisha fedha zinazokusanywa kwenye machinjio hayo zinatumika haraka kujenga miundombinu ya eneo hilo ilikuendana sambamba na wingi wa watu wanaotumia machinjio hayo. Kwa upande wa Afya, Naibu waziri wa Afya Dkt. Kingwangallah ameagiza daktari wa machinjio hayo Ndg. Juma aache kutoa huduma eneo hilo hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo. 
  Pia upimaji wa afya kwa wanaotumia machinjio hayo uwe wa bure na uongozi wa machinjio utenge ofisi maalum ya kupima watu hao.
  .
  Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi(Wadau) wa machinjio ya Vingunguti kuhusu hatua za kinidhamu alizozichukua kwa Mkuu wa mnada wa pugu inakotoka mifugo kabla ya kufika Machinjio ya Vingunguti kwa upotevu wa mamilioni ya shilingi ya kodi za serikali.
  Mawaziri wakiagana na wananchi mara baada ya mkutano wa kutatua kero zao za Machinjio kumalizika.
  Furaha ya Wananchi mara baada ya kutatuliwa kero zao kwa hatua za awali, wanasukuma gari la Mhe. Mwigulu Nchemba kama ishara ya kukubali hatua alizochukua. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


  0 0

  Hapa ndipo kileleni na Mwonekano wa Irente 
   Hii ni Miamba mikubwa iliyopo Irente na moja ya kivutio kikubwa katika eneo hili kwa upande kwa Kushoto.
  Eneo hili wakazi wa Irente wanaliita Pango ambapo watu wengi wanapenda kupigia picha
  Hii ni njia ya kuelekea Pangoni 

  Mmoja wa walinzi akiandika akiwakatia risiti wageni mbalimbali waliotembelea eneo hilo.
   Mmoja wa wandishi wa Blogs za Mikoa Fredy Tony Njeje akiwa amefika kujionea eneo hilo.
  Watu wengi wamekuwa na utaratibu wa kukalili kuwa wanapoambiwa kwenda kufanya utalii basi mawazo yanahamia katika hifadhi za taifa au Fukwe za Bahari, wakati kuna utalii wa kupanda milima,utalii wa uwindaji utalii wa picha, utalii wa kiutamaduni,Utalii wa Ikolojia,utalii wa fukwe,Michezo ya kwenye maji, utalii wa mali kale,utalii wa mikutano,utalii wa matibabu,utalii wa mashambani na utalii wa jiji
  Irente View Point inapatikana katika kijiji cha Irente kilichopo wilayani lushoto mkoani Tanga, eneo hili liligunduliwa na wazee wa kale ambao walikuwa wakifika hapo kwa ajili ya kuomba na kufanya matambiko na wengine walikuwa wakifika katika eneo hilo kwaajili ya kufanya ibada hasa wakati wa sikukuu za Christmas.
  Eneo hili lina urefu wa Mita 1500 kutoka usawa wa Bahari , ukiwa juu unaweza kuona maeneo mbalimbali vizuri bila usumbufu wowote, pia watalii wengi wamekuwa wakifika eneo hilo kutokana na hali ya hewa kuwa nzuri, kuona Mandhari nzuri hasa wakati wa asubuhi na jioni.

  Jinsi ya kufikia ikiwa unatokea upande wowote, fika hadi Mombo, panda daladala Tsh 3,000 mpaka Lushoto mjini baada ya hapo unaweza panda Boda boda Tsh 3,000 au ukachukua Tax Tsh 10,000 , kiingilio ni Tsh 2,000. 

  (Imeandaliwa na Fredy A. Njeje 0765056399)  0 0  Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania TRL umetangaza kusitisha kwa muda kuanzia jana Januari 01, 2016, huduma zake baada ya eneo la reli ya kati ya Kilosa mkoani  Morogoro na Gulwe mkoani Dodoma tuta la reli kukumbwa na Mafuriko. 
  Kwa mujibu wa taarifa za kifundi eneo lililoathiriwa na mafuriko ni kubwa hivyo Wahandisi na Mafundi  wa TRL wako eneo la mafuriko  kutathmini ukubwa wa kazi yenyewe. 
  Kutokana na  uamuzi huo treni ya abiria kutoka bara ilibidi safari yake ikatizwe ilipofika Dodoma na tayari utaratibu unaandaliwa wa kupata mabasi 17 kuwasafirisaha hadi Dar es Salaam abiria 1,119 . wa treni hiyo. 
  Hali kadhalika kwa vile tarahe ya kuanza tena huduma bado haijaujulikana,  safari zote kuanzia  jana Januari 01,  2016,  kwenda bara zimefutwa na abiria husika wametakiwa kufika katika vituo vya reli walikokata tiketi ili warejeshewe fedha zao na kupata fursa ya kutafuta usafiri mbadala. 
  Aidha imesisitizwa kuwa Uongozi kwa wakati muafaka itatoa taarifa kamili  kuhusu lini huduma za TRL kwenda bara  zitaanza tena.

  Wito unatolewa kwa kila mwananchi atakayepata taarifa hii muhimu amwaarifu mwenzake.


  Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa niaba ya 
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Elias Mshana.
   Dar es Salaam,
  Januari 02, 2016


  0 0

   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akizungumza na Makatibu Wakuu pamoja na Manaibu Katibu Wakuu wakati akifungua Semina Elekezi kwa Makatibu hao Ikulu jijini Dar es Salaam leo January 2, 2015
   Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wakisikiliza kwa makini Hotuba ya Ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika Semina elekezi ya siku moja Ikulu Jijini Dar es Salaam.
   Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wakisikiliza kwa makini Hotuba ya Ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika Semina elekezi ya siku moja Ikulu Jijini Dar es Salaam.
   Watoa mada katika semina elekezi hiyo wakiwa ni pamoja na (toka kulia) Makatibu Wakuu Kiongozi wastaafu Balozi Dkt. Marten Lumbanga,  Balozi Charles Sanga, Katibu Mkuu Mstaafu Ofisi ya Rais - Utumishi - Mhe. George D. Yambesi, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad na wengineo
   Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wakisikiliza kwa makini Hotuba ya Ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika Semina elekezi ya siku moja Ikulu Jijini Dar es Salaam.
   Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wakisikiliza kwa makini Hotuba ya Ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika Semina elekezi ya siku moja Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wakisikiliza kwa makini Hotuba ya Ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika Semina elekezi ya siku moja Ikulu Jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

  0 0

   Mdau mwandamizi wa Globu ya Jamii ambaye ni Meneja wa Benki Bw. Jesse Harris Mlule akimvisha pete Faith Alex Ndamalya walipomeremeta leo Januari 2, 2016 katika kanisa la Mtakatifu Albano jijini Dar es salaam kabla ya kuelekea Ukumbi wa Tanzania Law School kwa mnuso wa nguvu ila si kabla ya kupitia Ledger's Plaza Bahari Beach Hotel kwa mapumziko mafupi.
   Mdau Faith Alex Ndamalya akimvisha pete mumewe Jesse
   Jesse akiweka saini katika hati ya Ndoa
   Faith akiweka saini kwenye hati ya ndoa
  Maharusi wakiwa na Wachungaji wa Kanisa la Mtakatifu Albano mara baada ya kumeremeta leo. Kwa mapicha zaidi BOFYA HAPA
  Bwana harusi na wafanyakazi wenzi wa Benki wakiwa na Hamisi (kushoto) na Manywele (kulia) ambao ni waratibu na watendaji wa Picha za Mnato na Video wa harusi hii ya kukata na shoka Kutoka Michuzi Media Group.

  0 0

  Na Teresia Mhagama, Dodoma 
  Kampuni ya Joti structures inayojenga miundombinu ya usafirishaji umeme wa msongo wa kilovolti 400 kutoka Dodoma hadi Singida imetakiwa kukamilisha ujenzi wa miundombinu hiyo ifikapo mwezi Aprili mwaka huu kama mkataba unavyoelekeza. 
  Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani wakati alipofanya ziara ya kikazi mkoani Dodoma ili kukagua miundombinu ya usafirishaji umeme, miradi ya umeme vijijini pamoja na shughuli za uchimbaji wa madini. 
  Alitoa agizo hilo baada ya Meneja anayesimamia Mradi huo kutoka Shirika la Umeme nchini (TANESCO), Mhandisi Oscar Kanyama kumueleza kuwa mkandarasi huyo amekamilisha ujenzi wa nguzo (transmission tower) kwa asilimia 30 tu toka alipokabidhiwa kazi hiyo mwaka 2013. “Mkandarasi alianza kazi Novemba 2013 na anatakiwa akamilishe tarehe 20 Aprili 2016 na hadi kufikia Desemba mwaka 2015 ilibidi awe ameshaanza kuvuta nyaya kutoka Dodoma hadi Singida lakini mpaka sasa hajaanza,” alisema Mhandisi Kanyama. 
  Naibu Waziri aliongeza kuwa mkandarasi huyo asipokamilisha kazi ndani ya muda uliopangwa atalazimika kulipa gharama ambazo serikali itakuwa imeingia kutokana na mkandarasi huyo kuchelewesha mradi husika na kupelekwa mahakamani. 
  “Serikali imeshalipa asilimia 60 ya gharama zinazotakiwa ili kukamilisha mradi huu lakini huyu mkandarasi amekamilisha kazi kwa asilimia 30 tu, hii haikubaliki, hatutamvumilia mtu yeyote anayekwamisha juhudi za usambazaji umeme nchini, awe mkandarasi au wasimamizi kutoka serikalini wanaosimamia miradi hii,” alisema Dkt. Kalemani. 
  Kwa upande wake, Meneja Mkazi wa kampuni ya Joti Structures, D.N. Charjee alimueleza Naibu Waziri kuwa watakamilisha kazi husika ndani ya muda uliopangwa kama ilivyo ndani ya mkataba na kwamba asilimia 15 iliyobaki ya vifaa vinavyohitajika ili kukamilisha kazi hiyo vitafika tarehe 12 Januari 2015. 
  Wakati huohuo Naibu waziri amepiga marufuku shughuli za uchimbaji wa madini ya ujenzi ndani ya mita 30 kutoka katika korongo la Ihumwa mkoani Dodoma kwa kuwa zimekuwa zikiathiri uwepo wa maji katika kata ya Ihumwa na sehemu nyingine zinazotegemea maji hayo kwa shughuli mbalimbali. Baada ya kuona athari za uharibifu wa mazingira katika korongo hilo, Naibu Waziri alimwagiza Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kati, Sostenes Massola kuhakikisha kwamba agizo hilo linafanyiwa kazi kwani wananchi wengi katika kata hiyo wanaopata kipato kutokana na kilimo cha umwagiliaji wanaathirika.
   “Sheria ya mazingira hairuhusu kuharibu vyanzo vya maji, kama kuna uchimbaji wa madini ya ujenzi , Kamishna Msaidizi lazima uhakikishe kwamba haufanyiki ndani ya mita 30 kutoka kwenye mito na wachimbaji lazima wawe na vibali,” alisema Dkt. Kalemani.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma kabla ya kuanza ziara ya kukagua miundombinu ya usafirishaji umeme, miradi ya umeme vijijini pamoja na  shughuli za uchimbaji wa madini mkoani humo. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa.

   Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (wa kwanza kulia) akizungumza na Meneja Mradi Ujenzi wa vituo vya kupoozea umeme katika mradi wa Miundombinu ya Usafirishaji Umeme wa Kilovolti 400 kutoka Iringa hadi Shinyanga, Mhandisi James Mtei (katikati) mara baada kukagua ujenzi wa  kituo cha kupoozea umeme  kilichopo eneo la Zuzu mkoani Dodoma.

  Sehemu ya mitambo katika kituo cha kupoozea umeme kilichopo eneo la Zuzu mkoani Dodoma. Ujenzi wa kituo hicho ni sehemu ya utekelezaji mradi wa ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji umeme wa kilovolti 400 kutoka Iringa hadi Shinyanga unaotarajiwa kukamilika mwezi Aprili mwaka huu. Kituo kinajengwa na kampuni ya GSE&C na Hyosung kutoka Korea.


  0 0

  Baadhi ya wajumbe wa Timu ya kutoka Wizara ya Nishati na Madini,Wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi ,Wizara ya maji, na umwagiliaji , Shirika l Umeme Tanzania (Tanesco )pamoja na Watalamu wa bonde la mto Rufiji wakipata maelezo ya namna ambavyo umeme wa maji huzalishwa katika kituo cha Kihansi .

  Timu ya wataalam  kutoka Wizara ya Nishati na Madini,Wizara ya kilimo, mifugo na Uvuvi ,Wizara ya maji, na Umwagiliaji , Shirika l Umeme Tanzania (Tanesco ) pamoja na Watalamu wa bonde la mto Rufiji waliotembelea  vyanzo vya maji vinavyotiririsha  maji katika mito inayomwaga maji  mabwawa ya kuzalisha umeme wa maji ikiwemo  Mtera, Kihansi na Kidatu ili kuunganisha nguvu ya pamoja na kurejesha vyanzo hivyo katika hali yake ya awali kutokana na kuathiriwa na shughuli za kibinadamu na hivyo kusababisha kukauka na upungufu wa maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme wa maji ilivyokuwa katika miaka ya nyuma.
   Muonekano wa Bwawa la Kihansi kwa sasa ambalo pia limepunguza uzalishaji wa umeme wa maji kutokana na kupungua kwa kina cha maji.
   Timu ya wataalamu  kutoka Wizara ya Nishati na Madini,Wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi ,Wizara ya maji, na umwagiliaji , Shirika l Umeme Tanzania (Tanesco )pamoja na Watalamu wa bonde la mto Rufiji waliotembelea  vyanzo vya maji vinavyotiririsha  maji katika Mabwawa ya kuzalisha umeme .
   Eneo lenye  chanzo cha cha maji pamoja na mto  mbalo hutumiwa kwa shughuli za kibinadamu na kusababisha upotevu wa maji yanayoingia katika mto unaomwaga maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme wa maji
   Moja ya sehemu ya mashine ama mtambo inayotumika kuzalisha umeme wa maji katika vituo vya Kihansi, Kitadu na Mtera.
   Mashine inayotumika kuondoa  taka  kama vile magogo na nyingine zanamna hiyo katika mabwawa ya kuzalisha umeme wa maji.


older | 1 | .... | 1076 | 1077 | (Page 1078) | 1079 | 1080 | .... | 3286 | newer