Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1068 | 1069 | (Page 1070) | 1071 | 1072 | .... | 3270 | newer

  0 0

  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA, KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED ZAHORO MSANGI - SACP, ANAWATAKIA WAANDISHI WOTE WA HABARI "HERI YA KRISMAS NA MWAKA MPYA, 2016"

  KAULI MBIU: "ULINZI UNAANZA NA MIMI, WEWE NA SISI SOTE"
  KUMBUKA: WHEN YOU SEE SOMETHING, SAY SOMETHING.
  TUSHEREHEKEE KWA AMANI NA UTULIVU SIKUKUU YA KRISMAS NA MWAKA MPYA, 2016.

  AHSANTENI!!!!

  0 0
 • 12/25/15--00:46: MAPITIO YA MAGAZETI LEO

 • 0 0

  SIMU.TV:  Wafanyabiashara Katavi walalamikia uamuzi wa kuzuiwa kupakia na kusafirisha mazao kutoka kwenye ghala la chakula;  https://youtu.be/PpQjIfK7ZP4  
  SIMU.TV:  Madereva Makambako wailalamikia halmashauri kwa ubovu wa stendi ya mkoa licha ya ushuru unaolipwa na wafanyabiashara; https://youtu.be/OYrqlIv5kGY    
  SIMU.TV:  Wakazi wa mkoa wa Lindi hatarini kupata upofu kutokana na kuenea kwa ugonjwa wa vikope ambao umeenea sana wilayani  Ulanga;https://youtu.be/CWG8iJ5-EME  
   SIMU.TV:  Kaya 12 mkoani Mbeya zakosa makazi baada ya mvua kubwa kubomoa nyumba za wananchi na kuharibu takribani heka 14 za mazao;https://youtu.be/ft7zt7tYPk0 
   SIMU.TV:  Bodi ya mchezo wa bahati na sibu yazitaka kampuni zinazoendesha mchezo huo kuanza kulipa kodi za mapato;  https://youtu.be/KMfYm-SJb64
   SIMU.TV:  Tamaa ya fedha yawaponza mke, mtunza bustani na rafiki wa kike wa aliyekuwa afisa wa TANAPA mkoani Arusha; https://youtu.be/JQXxFSvUT1E 
   SIMU.TV:  Tiger Woods atamba kurudisha makali yake katika mchezo wa golf katika michuano ijayo licha ya tatizo la kiafya alilonalo; https://youtu.be/QL2OPH9D3zE
   SIMU.TV:  Polisi waitahadharisha jamii kusherekea sikukuu bila ya kujihusisha na vitendo vya uvunjifu wa sheria za nchi; https://youtu.be/k0V4uIXESns  


  0 0

  Askofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT( Dayosisi ya Iringa Dr OwdenBurg Mdegella akimpa baraka ya Christmas mtoto Monica Kasesela huku babake mkuu wa wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela na binti yake Cathelin Kasesela wakishuhudia baada ya kumalizika kwa ibada ya pili katika usharika wa kanisa kuu
  Askofu Dr Mdegela akitoa baraka 
  Mwalimu wa kwaya ya vijana katika kanisa kuu Bw Lupyana Samweli akipokea baraka za Christmas kutoka kwa askofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa Dr OwdenBurg Mdegela leo mara baada ya ibada.
  Askofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa Dr OwdenBurg Mdegela akimpa baraka za Chritmas mlemavu ambae ni mwimbaji maarufu wa kwaya ya vijana kanisa kuu Gift Mwanuka 

  WAKATI waumini wa Dini ya kikristo hapa nchini leo wakiungana na wakristo wenzao kote ulimwenguni kusherekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo , Askofu wa Kanisa la Kilutheri (KKT) dayosisi ya Iringa Dkt. Owdenburg Mdegella amesifu amani iliyotawala nchini kutoka uchaguzi mkuu hadi sasa na kuwaomba watanzania kumwombea Rais Dr John Mapuguli kwa kuleta mabadiliko ya kweli ambayo hata wapinzani walikuwa wakiyataka.

  "Salamu zangu na maelezo yangu ni mafupi kila mmoja anafahamu Burundi na Kenya walifanya uchaguzi na hadi leo hii bado wanauana na maisha yanakuwa magumu......ninyi mnafahamu awamu ya kwanza kuja ya pili tumevuka salama ,awamu ya pili kuingia ya tatu pia salama na awamu ya nne kuingia ya tano ndio tumevuka salama salimini zaidi kuliko awamu nyingine zote.....kwa nilitaka kuasema hata wale waliotumia mabomu na kutumia gharama kubwa wakati wa uchaguzi nafikiri walikuwa wamekosa mazoezi kwa muda mrefu ya kutumia mabomu hayo bila sababu Watanzania ni wapenda amani"

  0 0

  Watu zaidi ya 10 wahofiwa kufariki Dunia eneo la Soni, Lushoto Mkoani Tanga kufuatia ajali ya Fuso iliyotokea kwenye Maulidi kuanguka nakubiringika bondeni. Chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana mpaka sasa.
   sehemu ya umati wa watu waliofika kushuhudia tukio la ajali hiyo iliyotokea Soni,Lushoto mkoani Tanga
   Baadhi ya mashuhuda wakitazama Lori hilo lililopelekea vifo vya watu zaidi ya kumi baada ya kupinduka na kubiringika bondeni,huko Soni,Lushoto mkoani Tanga

  0 0


  0 0

   Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwan J. Kikwete.

  Ndugu zangu waandishi wa habari, nimeamua kuwaita ili kuzungumza nanyi kuhusu baadhi ya mambo yaliyokuwa yanasemwa katika vyombo vya habari kuhusu mimi.

  Awali ya yote napenda kusema kuwa habari hizo ni UONGO mtupu, ni mambo yanayozushwa na waandishi wa habari hizo kwa nia ya kuchafua jina langu kwa sababu wanazozijua wanaoandika. UKWELI ni kwamba haya ni mambo yenye kufanywa kwa nia na dhamira mbaya dhidi yangu na hata familia yangu.

  Hivi karibuni, kwa mfano, lipo gazeti moja liliandika na kutoa picha yangu na mtu mmoja waliyedai ni Mhe. Paul Makonda eti akinifunga kamba za viatu. Katika maelezo yake mwandishi akadai kuwa Mhe. Makonda alipata uteuzi kuwa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni kwa sababu hiyo. Huu ni uongo usiokuwa na hata chembe ya ukweli. 

  Napenda watanzania wajue kuwa hakuna wakati wowote Baba yangu alipokuwa Rais wa nchi yetu alinihusisha kwa namna yeyote ile katika uteuzi wa mtu yeyote katika Serikali. Hivyo basi kujaribu kunihusisha na uteuzi wa Mhe. Paul Makonda kuwa Mkuu wa Wilaya wa Kinondoni ni jambo lisilokuwa na ukweli wowote. 

  0 0

    Maofisa wa Jeshi la polisi kitengo cha Usalama barabarani pamoja na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu(wapili toka kushoto)wakimshuhudia dereva Frank Masawe wa basi lenye Namba za usajili T 798 DCT linalofanya safari za mikoa ya Dar es Salaam na Mtwara akisoma karatasi yenye majibu baada ya kupimwa kilevi,wakati wa zoezi lilioendeshwa na Jeshi la polisi kitengo hicho kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania kupitia kampeni ya”Wait to send”inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto ikiwa ni mwendelezo wa kampeni hiyo iliyofanyika jana katika Vituo vya mabasi ya kwenda mikoani cha Ubungo na Mbagala jijini.
   Askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Dar es Salaam, SGT. John Jonas(kushoto)akimpima kiwango cha pombe mwilini dereva wa basi lenye namba za usajili T 798 DCT la Dar es Salaa na Mtwara ,Frank Masawe ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send” inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto ikiwa ni mwendelezo wa kampeni hiyo iliyofanyika jana katika Vituo vya mabasi ya kwenda mikoani cha Ubungo na Mbagala jijini,katikati katika picha ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu ambao ni wadhamini wakuu wa kampeni hiyo.
   Baadhi ya Madereva wa Mabasi yanayoenda mikoani na wadalala wa jijini Dar es Salaam,wakimsikiliza Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kulia)akitoa elimu kuhusiana na pete ya kidoleni yenye ujumbe maalumu wa “Wait to send” wakati wa zoezi la kukagua magari na kutoa elimu kwa madereva hao kuhusiana na kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto ikiwa ni mwendelezo wa kampeni hiyo iliyofanyika jana katika Vituo vya mabasi ya kwenda mikoani cha Ubungo na Mbagala jijini.
   Mkuu wa kitengo cha elimu kwa Umma kitengo cha Usalama barabarani makao makuu ya Polisi ASP,Abel Swai(katikati) akifafanua jambo kwa Madereva wa mabasi ya endayo mikoani na daladala za jijini Dar es Salaam pamoja na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, matina Nkurlu(kulia) wakati wa zoezi lililofanyika Stendi kuu ya Ubungo na Mbagala ya kutoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send”inayoendeshwa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama Barabarani.
  Baadhi ya abiria wa Mabasi yaendayo mikoani wakimsikiliza Mkuu wa kitengo cha elimu kwa Umma kitengo cha Usalama barabarani makao makuu ya Polisi ASP,Abel Swai,wakati alipokuwa anawaelimisha abiria hao ndani ya basi linalofanya safari zake mikoa ya Dar es Salaam na Mtwara ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send”inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto.Kampeni hiyo inaendeshwa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kitengo hicho ilifanyika jana katika Stendi kuu ya Ubungo na Mbagala jijini.

  0 0

  Mraghbishi Noorkiyengop Mbaima toka kijiji cha Enguserosambu akisimama mbele ya mifugo iliyokutwa msituni katika eneo lililoruhusiwa la msitu wa jamii wa Enguserosambu

  Ilikuwa ni siku ya shangwe na furaha kwa wananchi wa kata ya Enguserosambu wilayani Ngorongoro. Hii ni baada ya serikali kukubali ombi lao la kusimamia rasilimali ya msitu wa Loliondo namba 2 unaopakana na vijiji vinne vinavyokadiriwa kuwa na idadi ya wakazi wapatao 20,000 wanaotegemea mahitaji yao toka katika huo msitu.

  Huu ni msitu pekee ambao wananchi kwa kushirikiana na Mkuu wao wa wilaya, na mashirika rafiki, wamefanikiwa kuishawishi serikali kuukabidhi msitu huo kwao. Katika mchakato huo uliochukua miaka kadhaa wanawake toka katika vijiji vya Enguserosambu, Ng’arua, Orkiu na Naan wamekuwa mstari wa mbele katika kufanikisha azma hiyo ya kubakiza msitu wao wa enzi mikononi mwao. Akielezea furaha yake aliposikia msitu wa Loliondo namba 2 umekabidhiwa kwa wananchi, mraghbishi mwanamke Noorkiyengop Mbaima alisema 

  “Mimi mwenyewe nimefurahia, kwa sababu sisi akina mama tunategemea sana msitu huu kwa mahitaji yetu. Huu msitu kama ungeondoka katika mikono ya jamii basi tungeathirika sana sisi kina mama.” Umuhimu wa msitu huu kwa kina mama ndio uliowapelekea wao kutunga na kuimba nyimbo za hamasa na kutumbuiza, kushiriki kwa wingi katika vikao mbalimbali vya maamuzi wakati wote wa mchakato huo. 

  Kwa kuwa msitu huu ndio tegemeo lao katika kuendesha maisha ya kila siku. Hakuna chochote ambacho kiliamriwa bila ya wao kuchangia na kushirikishwa kuanzia utungaji wa sheria ndogongogo za usimamizi wa msitu hadi kukabidhiwa rasmi msitu huo. “Nikichukulia mfano katika mikutano yote ya vijiji. Kiukweli wanawake wamekuwa wanajitokeza kwa wingi, kuliko makundi mengine yoyote. Hata ile siku ya uzinduzi wa msitu walikuwa wengi zaidi,” anaelezea Jackson Nangiria 

  Ushiriki huu wa wanawake unatokana na ukweli kwamba wana uhusiano wa karibu na msitu huo wa enzi wa Enguserosambu.Si kwa ajili yao tu pamoja na watoto wao pia. Ni watoto hawa wa kike wenye majukumu ya kujenga nyumba kwa kutumia miti inayotoka ndani ya msitu huu, ndio wanaotembea na punda wakiwabebesha maguduria ya maji kwa umbali mrefu wakitafuta maji ambayo chanzo chake kipo kwenye msitu huu. Wanapopata watoto wanahitaji dawa za kuwaogeshea na dawa za uzazi ambazo zinatoka kwenye msitu huu. 

  0 0

  Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya The Ngoma Africa Band aka FFU-ughaibuni inayoongozwa na Kamanda  Ras Makunja yenye maskani nchini ujerumani inawatakieni kila la heri katika siku kuu ya Maulid el Nabii Muhammad(S.W.A) pia Heri ya siku kuu ya Krismasi kwa wadau wote iwena amani,upendo,furaha na mshikamano bila kusahau kupata muziki at www.ngoma-africa.com au www.reverbnation.com/ngomaafricaband

  0 0

  Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwasili kushiriki Ibada ya Krismas misa ya kwanza katika Kanisa la Mtakatifu Peter jijini Dar es salaam leo Desemba 25, 2015.
  Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli, mkewe Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakishiriki Ibada ya Krismas katika Kanisa la Mtakatifu Peter jijini Dar es salaam leo Desemba 25, 2015
  Sehemu ya waumini katika Ibada ya Krismas misa ya kwanza katika Kanisa la Mtakatifu Peter jijini Dar es salaam leo Desemba 25, 2015.
  Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli, mkewe Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakishiriki Ibada ya Krismas katika Kanisa la Mtakatifu Peter jijini Dar es salaam leo Desemba 25, 2015.


  0 0

  STAR TV: Kasi ya Rais Magufuli yawavutia maasikofu, Balozi Mahiga aanza kusaka suluhu Burund,kwa uchambuzi Zaidi tazama hapa;https://youtu.be/gwlQ8B9cJcY
   STAR TV: Kocha Kerry ahofii kutumuliwa simba, Mbwana Samata kutimkia Ubelgiji,kwa habari Zaidi tazama uchambuzi wa magazeti hapa;https://youtu.be/4ynD8I2e8wQ
   TBC: Maaskofu wampa rungu Magufuli, Kasi ya Rais Magufuli yawavutia maaskofu, Kocha Kerry ahofii kufukuzwa Simba. Fuatilia dondoo za magazeti hapa; https://youtu.be/ep5PBTGeWKQ
   AZAM TV: Hapatoshi Kerry dhidi ya Julio uwanjani leo, Guardiola yupo tayari kutua Old Trafford, Wenger amtengea dau Chicharito. Fuatilia Magazeti ya michezo hapa; https://youtu.be/Toht3vyivWc

  0 0

   Mwanamuziki wakizazi kipya kipenzi cha wengi afaamikae kwa Jina la Mr.Blue apagawisha mashabiki wa muziki wa kizazi kipya Jijini Mbeya katika Shoo ya Xmass iliyo andaliwa na Radio Dream Fm 91.3 Mbeya na kusapotiwa na Cocacola, Paradise In Hotel, Wasanii wa Muziki kutoka Mbeya na Michuzi Media Group, Shoo Nzima ilifanyika katika ukumbi wa wazi Paradise In Soweto                                                                     Jijini Mbeya.
   Kutoka Shoto ni Meneja wa Radio Dream Fm Mzee wa Masauti Tom Chilala akiwa Sanjari na Mwanamuziki wa muziki wa Kizazi kipya Mwana Dada Petronia katika Picha. 
  Mwana Daa Petronia akitumbuiza baadhi ya Nyimbo zake katika Shoo ya Xmass iliyo andaliwa na  Radio Dream Fm mbeya.
                                    PICHA ZOTE NA MR.PENGO MBEYA.
                                             PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0


  Na Editha Karlo wa 
  Blog ya jamii, Kigoma
  WAZIRI Mkuu Kassimu M Majaliw  (pichani) kesho ataanza ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Kigoma,
  Akizungumza na waandishi wa habari juu ya ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya alisema kuwa Waziri Mkuu atawasili Mkoani hapa kesho majira ya saa tatu asubuhi.
  Alisema kuwa atapokelewa na viongozi mbalimbali wa serikali ya Mkoa na kisha atasomewa taarifa ya Mkoa.
  Baada ya hapo ataelekea katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyopo Wilayani Kasulu pamoja na kambi ya wakimbizi ya Nduta iliyopo Wilayani Kibondo
  Na siku ya jumatatu atafungua mwalo wa kibirizi na kufanya majumuisho ya ziara yake katika ukumbi wa NSSF na kisha kurejea Dar es salaam.

  0 0


  Afisa Muuguzi Msaidizi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam Mwanne Satara akimsaidia kumuelekeza Lulu Mohamed namna ya kumfunika nguo Mtoto aliyezaliwa usiku wa kuamkia Krismas Dar es Salaam ambapo akinamama 12 walipata watoto na Mmoja wa akinamama hao alipata mapacha 2 na kufanya watoto wa kiume kufikia 6 na wakike 7, kati yao akinamama waliofanyiwa upasuaji ni akinamama 10 na kati ya hao watoto njiti 2 na Hospitali ya Temeke akina mama waliojifungua hospitalini hapo kufikia idadi ya watoto 12, wakiume 4 na wakike 8 .
  (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA).
  Afisa Muuguzi wa Zamu wa Hospita ya Mkoa Amana Florensia Ndumbaro akizungumza na waandishi wa Habari (pichani hawapo), Hospitali tumepokea idadi ya watoto waliozaliwa mkesha wa Krismas ni 33 kati yao 15 ni wakike na 18 ni wakiume na wote wapo katika hali nzuri na wananyonya vizuri pia mama zao wanaendelea vizuri.

  0 0

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye aliyekuwa mgeni rasmi akimuwakilisha Makamu wa Rais Mh. Mama Samia Suluhu Hassan akizindua rasmi albam mbili za kwaya ya Wakorintho wa Pili kwenye tamasha la Krismas lililofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee leo, ambapo mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika ya Kusini Rebecca Malope amefanya onesho kubwa lililovuta hisia za mashabiki wengi waliohudhuria katika tamasha hili akishirikiana na waimbaji mbalimbali wa hapa nyu mbani na nchi jirani ya Kenya.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Nape Nnauye amewaomba watanzania kuzidi kumuombea Rais Dk . John Pombe Magufuli kwa kazi ya kutumbua majipu ambayo amekwishaianza kwani kazi hiyo ni ngumu na ina vikwazo vingi, lakini pia amewataka watanzania na waumini wa madhehebu mbalimbali kuwaombea wasaidizi wake ili waweze kuwa bega kwa bega na Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli ili kutekeleza kazi hii kwa ufanisi na kisha watanzania wafaidi matunda na rasilimali zao wenyewe.

  Waimbaji kutoka Kenya walikuwa ni Faustine Munishi na Sara K na Solomon Mukubwa kutoka jiji la Nairobi huku waimbaji wa hapa nyumbani wakiwa ni Rose Muhandom Upendo Nkone, Christine Shusho, Edson Mwasabwite, Joshua Mlelwa na wengine wengi, Tamasha hilo pia lilikuwa na lengo la kumshukuru mungu kwa nchi yetu ya Tanzania kufanya uchaguzi kwa amani, Kulia ni Akex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion ambayo ndiyo imeandaa tamasha hilo.(PICHA NA JOHN BUKUKU- FULLSHANGWEBLOG-DAR ES SALAAM)
  Akex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion ambayo ndiyo imeandaa tamasha hilo. akimkaribisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye ili kuzungumza na wananchi katika tamasha hilo kushoto ni Mbunge Martha Mlata na MC Mwakipesile mshereheshaji wa Tamasha hilo.

  0 0
 • 12/25/15--22:51: IN LOVING MEMORY
 • Its been 19 years since our beautiful queen left us on 26 Dec 1996. 
  We miss you but you are in a better place. 
  Your daughters Dr Happiness Wimile  and Neema Mbeyela, grandchildren Hellen, Harris and Hope Wimile along with friends and family  pray that Almighty God grant eternal rest to Wampela Rehema Mbeyela. 
  Amen

  0 0

  IMG_7348Diamond Platnumz akisema na mashabiki wake waliofurika Dar Live usiku wa kuamkia leoIMG_7989Diamond akicheza na mashabiki wake waliofurika Dar Live.
  IMG_7359Akicheza na wacheza shoo wake wa kike.


  0 0

  Jeshi la polisi mkoani Tabora limetoa agizo kuwachukuliwa hatua polisi wanaojihusisha na uharifu na wanaotoa siri za jeshi hilo: https://youtu.be/ke0jqZIOm3o

  Waumi ni wa pentekoste mkoani  Singida wamefanya ibada maalumu ya kumuombea Rais Magufuli ili aendelee kutumbua majipu: https://youtu.be/1dRmKUcqGHg

  Waumini wa dini ya kiislamu wajitoa kusaidia wasiojiweza katika kuadhimisha sikukuu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) https://youtu.be/-sI1j96PQ4E

  Viongozi wa kamati ya Shehia visiwani Unguja wamewaomba wananchi hususani  vijana kuepukana na maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi :https://youtu.be/CkyBCyBhXRQ

  Wakazi wa mkoa wa Iringa wagundua dawa ya kuzuia mvua za mawe pamoja na mvua za upepo ili kuondokana na maafa yatokanayo na mvua hizo:https://youtu.be/NILch8FjIRE

  Watanzania watakiwa kumshukuru Mungu kwa kumaliza uchaguzi salama na kupata viongozi wanaofanya kazi kwa bidii: https://youtu.be/BNCl6PYAPcY

  Baadhi ya viongozi wa dini ya kikristo wameliombea taifa kuishi kwa umoja na mshikamano na kuwasaidia wasiojiweza: https://youtu.be/UbWQVx3h9H8

  Mchungaji wa kanisa la mlima wa moto amewataka watanzania kumuombea afya njema Rais Magufuli ili taifa liweze kusonga mbele: https://youtu.be/S_JIdytcdLQ

  0 0

  Ndugu na jamaa wanatarifiwa kwamba Bw. Hemed Mzee Ibrahim "Njemba" (pichani)  ametoweka nyumbani kwake Magomeni Makuti mtaa wa Mchinga namba 22 jijini Dar es salam toka siku ya Alhamisi tarehe 24/12/2015. 
  Alionekana mara ya mwisho kwenye msikiti wa Magomeni Makuti muda wa alasiri alipokwenda kuswali, akiwa kavaa balaghashia (kama hiyo pichani), shati la light purple, suruali ya bluu na kandambili za bluu. Baada ya hapo hakurudi nyumbani kwake na hadi sasa hajulikani alipo. Mzee Njemba hupendelea kutembelea Magomeni Makuti.
  Wanafamilia wanaomba mwananchi atayebahatika kumuona atoe tarifa kwa mkwewe Yusuf  anayepatikana katika namba 0784 606 262.

  Wanatanguliza Shukurani za dhati kwa wote na kumuombea salama mzee wao.
older | 1 | .... | 1068 | 1069 | (Page 1070) | 1071 | 1072 | .... | 3270 | newer