Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live

SWAHILI TV -WEEKEND SPECIAL


Ufafanuzi kuhusu hali ya mfuko wa PSPF

KUTOKA BUNGENI DODOMA LEO

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo pinda akijibu Maswali Bungeni mjini Dodoma Aprili 18,2013.
Askari wa Bungeni (kulia) wakimwamuru Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lisu kutoka nje ya ukumbi wa Bunge baada ya Naibu Spika Job Ndugai kumtaka afanyane hivyo na kukaidi. Wengine pichani ni wabunge wa Chadema wakizuia asitoke Aprili 17, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Waziriwa Kilimo , Chakula na Ushirika, Eng. Christopher Chiza kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Aprili 18 ,2013.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Ambassador of Republic of Korea pays a courtesy visit to Hon. Membe

$
0
0
Hon. Bernard K. Membe (MP), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation, welcomes H.E. Ambassador Chung Il (left), Ambassador of the Republic of Korea in Tanzania, who had paid a courtesy visit to his office earlier today in Dar es Salaam.
Hon. Membe welcomes Mr. Seongtak Oh, Deputy Chief of the Republic of Korea Mission in Tanzania.
Hon. Membe express something during his talk with Ambassador Chung Il of the Republic of Korea Mission in Tanzania. For years, the two countries have been enjoying friendly diplomatic ties that have extended well beyond political and economic connections, that include education sector which has benefited Tanzanian students through The Korean Government Scholarship Sponsorship.photos by Tagie Daisy Mwakawago of the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation.

tunakerwa na yanayotokea bungeni-Nape.

$
0
0

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara wa CCM kwenye uwanja a shule ya Msingi Gairo B, mjini Gairo mkoani Morogoro leo hii.

==========  ========  ========

NA BASHIR NKOROMO, GAIRO.

 CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeeleza kukerwa kwake na matukio ya kejeli matusi na uvunjifu wa amani yanayoanza kushamiri bungeni  na kusema kuwa matukio hayo ni dhihaka ya hali ya juu inayofanywa na wabunge dhidi ya wananchi waliowachagua.

 Hayo yalisemwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa shule ya Msingi, Gairo mkoani hapa, Aprili 18, 2013, ambao mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

 ” Mambo haya yanayofanywa na wabunge  kama ilivyotokea jana (juzi), ni dhihaka inayofanywa na wabunge kwa wanancjhi waliowachagua. Baadhi ya wabunge wanafanya vituko hivi huku wakiwa wanatambua wazi kwamba heshima waliyopewa ni kwenda bungeni kujadili matatizo ya wananchi ambayo ni mengi kama migogoro ya ardhi. Hili tukio la jana ni  aibu ya mwaka”, alisema Nape.

 Alisema, muda wanaokuwepo bungeni, wabunge wanapaswa kuutumia wote kwa hekima busara na uwezo wao wote kujadili namna ya kuwezesha Watanzania kufikia maisha bora na siyo kuutumia muda huo kujadili tofauti zao za kisiasa au namna ya kutekeleza malengo yao binafsi ya vyama vyao.

 ”Hatua hii ya wabunge wa Chadema kuamua kuzusha tafrani na kuvunja kanuni za bunge kwa makusudi ni ya hatari sana, hivyo wananchi wanapswa kujifunza kwamba hawa siyo watu wa kuwapa madaraka. Tazama hivi sasa bungeni wapo wachache sasa wananchi wakihadaika wakawachagua na kuwa wengi bungeni patakuwaje? Hili ni fundisho tosha”. alisema Nape.

 Alisema, hatua ya Wabunge na viongozi wa Chadema kulijadili suala la Mkurugenzi wa Usalama wa Chama hicho, Wilfred Lwakatare kuhusiana na ugaidi huku wakijua kwamba ni suala ambalo lipo mahakamani, ni la kujaribu kuingilia uhuru wa mahakama kwa makusudi ili ifikie mahala mahakama itupilia mbali kesi hiyo kwa kigezo cha kuinngiliwa uhuru wake.

 ”Haya ni matumzi mabaya ya bunge ambayo yanasukumwa na viongozi wao ikiwemo kuingilia uhuru wa mahakama, ili hatimaye ionekane uhuru wa mahakama umengiliwa kuhusiana na kesi hiyo na hatimaye itupiliwe mbali. Kila mwenye akili anajua kwamba  huu ni mkakati malum wa Chadema”, alisema Nape.

 Mbali na kukizungumzia bungeni suala ya Lwakatare, Chadema wamekuwa wakilisema pia mitaani, akitoa mfano hatua ya hivi karibu ya Mbunge wa Singida, Tuntu Lissu kufanya mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia suala hilo na kwamba mbali na kutafuta kesi hiyo itupwe pia ni juhudi za Chadema kujaribu kusukuma maamuzi ya mahakama. Bofya hapa kwa habari kamili.

ujio mpya wa mwana-dada Nakaaya na singo yake ya utu uzima dawa mx.

$
0
0


Baada ya kimya kingi katika fani ya muziki, nimeamua kuirudia fani yangu na kutoka na miondoko ya kiafrica. Kibao cha kwanza nilichoamua kuanza nacho kinaitwa "Utu uzima dawa" ft Dunga kilichoandikwa na mimi pamoja na Richie Mavoko. Na ku produciwa na Lamar wa fishcrab.

AS OLD AS MY TONGUE: the myth and life of Bi Kidude

$
0
0
In memory of Bi Kidude, we bring you the original version of ScreenStation's first independent feature length documentary. Shooting began in February 2003 and in 2013 we went back to update the story. Sadly, as many of you will now know, Bi Kidude passed away on April 17th 2013. Do email info@screenstation.net or join us at facebook.com/screenstation for all the latest news as we prepare the new film for release in tribute to her.

For pictures of her Burial CLICK HERE

Article 5


MAZISHI YA BOB SEMBEKE MJINI MOSHI

$
0
0

Jeneza la marehemu Bob Sambeke likiwa nje tayari kwa ajili ya kuuaga mwili
Juu na chini ni Mtoto wa marehemu Jamal akifungua jeneza la marehemu baba yake Bob
Waombolezaji wakitoa heshima za mwisho
Watoto wa marehemu Sia na Getrude 

Baadhi ya waombolezaji waliofika msibani hapo
Watu wakibadilishana mawazo kwa huzuni
Mwili wa marehemu ukiwa kwenye gari tayari kwa safari kuelekea Moshi kuzika
Gari liliokuwa limebeba mwili wa marehemu Bob
Baadhi ya waombolezaji na magari eneo la tukio nyumbani kwa marehemu Njiro, Arusha

Umati mkubwa wa watu ulifurika nyumbani kwa marehemu “Babu Sambeke” eneo la njiro jijini Arusha kuuaga mwili wake unaotarajiwa kuzikwa nyumbani kwake eneo la Karanga mjini Moshi .

Taratibu za kuaga mwili wa marehemu zilianza majira ya saa 5 asubuhi huku wafanyabiashara wa madini pamoja wafanyabiashara wengine kutoka Arusha na Moshi wakionekana kutawala msiba huo.

Magari ya kifahari nayo yalitawala na kusababisha msongamano mkubwa kwenye barabara ya Njiro.

Shughuli hizo zilikamilika majira ya saa 8:45 mchana huku mwili huo ukipakiwa katika gari maalum la kifahari tayari kusafirishwa kuelekea nyumbani kwake Moshi kwa ajili ya maziko.

Katika zoezi hilo la kuuaga mwili wa marehemu, Padri Florentine Mallya ambaye ni mdogo wa marehemu aliongoza misa ya kumuombea marehemu .

Ndani ya jeneza marehemu alivishwa nguo zake za urubani.

Tofauti na ilivyozoeleka katika misiba mingine hapa nchini, katika msiba huu watu mbalimbali walipata fursa ya kupata chakula na vinywaji mbalimbali kwa kujihudumia wenyewe, vikiwemo vinywaji aina ya Bavaria ambapo watu waliohudhuria zoezi hilo walionekana wakijihudumia zaidi kinywaji hicho.

Marehemu ameacha watoto watatu ambao ni Sia, Jamal na Getruda.

RAIS KIKWETE ASHIRIKI MAZISHI YA MDOGO WAKE DKT. BILAL HUKO ZANZIBAR

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk. Jakaya Mrisho Kikwete,akitia udongo katika kaburi la Marehemu Haji Gharib Bilali, Mdogo wake Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Mohammed Gharib Bilal, wakati wa maziko yaliyofanyika leo jioni huko Mwera,Wilaya ya Magharibi Unguja.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal,akitia udongo katika kaburi la Mdogo wake Marehemu Haji Gharib Bilali, wakati wa maziko yaliyofanyika leo jioni huko Mwera,Wilaya ya Magharibi Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,,akitia udongo katika kaburi la Marehemu Haji Gharib Bilali, Mdogo wake Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Mohammed Gharib Bilal, wakati wa maziko yaliyofanyika leo jioni huko Mwera,Wilaya ya Magharibi Unguja.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk. Jakaya Mrisho Kikwete,akitia udongo katika kaburi la Marehemu Haji Gharib Bilali, Mdogo wake Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Mohammed Gharib Bilal, wakati wa maziko yaliyofanyika leo jioni huko Mwera,Wilaya ya Magharibi Unguja,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

Wachezaji wa Kiafrika wazidi kupata soko Barani Ulaya hivyo Watanzania wasichezee fursa ya soka la kimataifa

$
0
0
Zaidi ya mawakala 15 tayari wamewasiliana na Kampuni ya Tanzania Mwandi kuwahitaji wachezaji mbalimbali kwaajili ya kuwapeleka kwenye klabu za barani Ulaya, Asia na Afrika ili kucheza soka la kulipwa.

Mwitikio huo umeongezeka kutokana na vijana wa kiafrika kuwa na soko kubwa katika ulimwengu wa sasa wa mpira wa miguu kwa nchi mbalimbali kama Sweden, Uholanzi, Denmark, Ureno na nchi nyinginezo.

Arne Anderson kutoka AA Football Service ya Sweden amesema kuwa binafsi yuko tayari kuchukua wachezaji wawili kwaajili ya kuwatafutia clubs nchini humo kwani tayari mafanikio ya wachezaji watano wa kiafrika aliowapeleka yamempa maombi ya timu nyingi za Sweden.

“Niko tayari kuchukua wachezaji wawili endapo tutakubaliana kuhusu maslahi yangu pindi wachezaji hao wakianza kucheza hapa”, Arne amesema.

Kutokana na mafanikio hayo na maombi ya mawakala lukuki Kampuni ya Tanzania Mwandi inazidi kuwasisitizia wachezaji wa Kitanzania kujaza fomu zinazopatikana kupitia blog.tanzaniamwandi.co.tz ili kufanya majaribio ya kucheza soka nchini Sweden, Norway, Denmark, Uholanzi, Ureno, Uswiss, Ufaransa na Ubelgiji, barani Asia (Kuwait, China, Qatar nk) na klabu nyingine barani Afrika.

Mpaka sasa jumla ya wachezaji wa kitanzania 15 wamekwishajaza fomu za haraka kwenye tovuti ya Tanzania Mwandi huku kampuni ikiwa imepokea pia maombi ya wachezaji 25 kutoka nje ya nchi.

“Maombi yanazidi kuja ingawa tunawahimiza Watanzania wasikimbie kiingilio cha shilingi 300, 000 wakumbuke kuwa wanafanya majaribio wakiwa nyumbani na watakapopata timu Kampuni ya Tanzania Mwandi haitachukua chochote kwenye mikataba yao, ni wao na mawakala ndio watakokubaliana juu ya watakachokipata kutoka kwa klabu husika”, alisema Teonas Aswile, Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzania Mwandi, waandaaji wa African Youth Football Tournament.

Aswile amezialika klabu mbalimbali za ligi kuu ya soka Tanzania Bara na Visiwani kutazama wachezaji watakaofika katika michuano hiyo kwani wapo baadhi ya wachezaji kutoka nje ya nchi ambao watafika na wangependa kucheza soka la Tanzania.

“Kati ya wachezaji 25 wa nje ya nchi wengine wameomba tuwatafutie timu hapa nchini hivyo klabu zikija zinaweza kuwapata wachezaji hao wakiwa huru kwasababu watakuja kwa gharama zao kufanya majaribio nchini. Pia klabu hizo zitumie fursa hii kuuza wachezaji wake.”

Michuano ya African Youth Football Tournament inatarajia kufanyika Juni 10 hadi 14 mwaka huu katika uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam na kushirikisha vijana kati ya miaka 18 hadi 21 kutoka Tanzania na bara zima la Afrika. Taarifa zaidi kuhusu michuano hiyo zinapatikana kupitia; blog.tanzaniamwandi.co.tz

Imetolewa na Idara ya Habari
Kampuni ya Tanzania Mwandi

Safari Lager kusherehekea ubingwa wa bia bora afrika na wabunge mjini Dodoma

$
0
0

 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Robin Goetzsche (wa tatu kushoto) akikabidhi Kombe la Ushindi wa Bia Bora Barani Afrika ulioupata Bia ya Safari Lager kwa Ujumbe wa Kampuni hiyo unaelekea Bungeni Mjini Dodoma kwa kupata baraka za waheshimiwa Wabunge na kuzindua rasmi wa ziara ya kupeleka kombe hilo katika mikoa mbalimbali hapa nchini.Pichani toka Kushoto ni Mkurugenzi wa Miradi Maalum wa Kampuni ya Bia Tanzania,Phocas Laswai (kushoto),Mpishi Mkuu wa Bia za TBL,Gaudence Mkolwe (pili kushoto),Mkurugenzi wa Masoko,Kushillla Thomas,Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (pili kulia) pamoja na Meneja Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo.
Ujumbe wa kampuni ya Bia Tanzania uliokabidhiwa kombe hilo kwaajili ya kupeleka Bungeni Mjini Dodoma,Ukiongozwa na Mkurugenzi wa Miradi Maalum wa Kampuni ya Bia Tanzania,Phocas Laswai (kushoto),Mpishi Mkuu wa Bia za TBL,Gaudence Mkolwe (pili kushoto),Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (pili kulia) pamoja na Meneja Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo.

Habari za Tanzania kwa kina toka TBC

News UPDATES: Boston Bombing Suspects, One has been shot dead and another is on the loose

$
0
0


The dead suspect has been identified as Tamerlan Tsarnaev, 26, and the one still being sought is Dzhokhar Tsarnaev, age 19.

Balozi kamala atembelea Mahakama ya Kimataifa ya Yugoslavia,pia akutana na Katibu Mkuu wa Mahakama ya Kudumu ya Usuluhishi

$
0
0
Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya,Dr. Diodorus Kamala akisalimiana na Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Yugoslavia Mhe. Serge Brammertz wakati alipomtembelea ofisini kwake.
Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Kamala (Mwenye miwani) akiwa na Katibu Mkuu wa Mahakama ya Kudumu ya Usuluhishi Mhe. Hugo Siblesz

Wakulima wa miwa waishitaki serikali kwa ccm,ccm yapanga kuonana nao jumatatu mjini morogoro.

$
0
0

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Wakulima wa Miwa sambamba na Uongozi wa Kiwanda cha Sukari Mtibwa,kwenye mkutano wao uliofanyika kwenye ukumbi wa hotel ya Honolulu,Turiani wilayani Mvomero,Morogoro.Mkutano huo umefanyika huku ukiwashirikisha wakulima,uongozi wa Kiwanda na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero,kufuatia Wananchi wa Wilaya ya Mvomero  mkoani Morogoro kukishitaki Kiwanda cha Sukari Mtibwa kuwa kimekuwa kikifanya dhuluma kubwa dhidi ya wakulima wa miwa huku wakimuomba Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), kufanya kila analoweza kuhakikisha mgogoro uliopo kati ya pande hizo mbili unapatiwa ufumbuzi. Aidha chama cha CCM kimetoa maelekezo ya kukukutana na Wakulima hao pamoja na uongozi wa Kiwanda cha Mtibwa siku ya jumatatu,kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo.
Baadhi ya Wakulima wa Kiwanda cha sukari Mtibwa na Uongozi wa Kiwanda hicho wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wao na Uongozi wa juu wa CCM,mapema leo uliofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Honolulu,Turiani Wilayani Mvomero .
Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza mbele ya wakulima wa miwa na uongozi wa Kiwanda cha sukari Mtibwa kuhusiana na Mgogoro wao mkubwa uliodumu takribani kwa miaka 10 sasa,aidha Uongozi wa CCM umesikiliza pande zote mbili (Wakulima wa miwa & Uongozi wa Kiwanda cha Mtibwa) na kuamua kukukutana na Wakulima hao pamoja na uongozi wa Kiwanda cha Mtibwa siku ya jumatatu,kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo.
Mmoja wa Wakulima wa Miwa kutoka kiwanda cha sukari Mtibwa,Mzee Pascal akizungumzia tuhuma na dhuluma mbalimbali wanazofanyiwa na uongozi wa Kiwanda hicho,Aidha Mzee Pascal alisema kuwa wakulima wa miwa wamekuwa na mgogoro na kiwanda hicho uliodumu kwa miaka 10 sasa,lakini kwa bahati mbaya hakuna majibu ya suluhu hali inayofanya wananchi wajiulize maswali bila majibu. Mzee Pascal aliyataja baadhi ya matatizo makubwa yanayofanywa na kiwanda cha Mtibwa kuwa ni kucheleweshwa kwa malipo ya miwa, kiwango kidogo cha malipo pindi wanapopeleka mazao yao kuuza kiwandani, madeni sugu kwa wastaafu wa kiwanda lakini kubwa zaidi wanadai kuna dhuluma ambayo imekuwa ikifanywa na uongozi wa kiwanda hicho.  
Mmoja wa Wastaafu wa Kiwanda cha sukari Mtibwa,akikishitaki kiwanda hicho mbele ya Uongozi Mkuu wa CCM,kuhusiana na malimbikizo ya mafao ya PPF,ambayo yamekuwa yakileta mgogoro mkubwa kati yao kutokana na kutolipwa kwa wastaafu hao.
Mwenyekiti wa halmashauri Wilaya ya Mvomero ,Bwa.Jonas Van Zeiland akizungumza mbele ya Uongozi wa CCM,chini ya uongozi wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana uliofika Turiani,Wilayani Mvomero  uliofika kusikiliza na kutafuta ufumbuzi wa Changamoto/Mgogoro uliopo kati ya Mwekezaji wa Kiwanda cha Sukari Mtibwa na wakulima wa Miwa.
Meneja wa kanda ya Mvomero-PPF,Bwa.John Mwalisu akitoa ufafanuzi mbele ya wakulima wa Miwa-Mtibwa,kuhusiana na malimbikizo yao ya mafao ya Kustaafu kutoka kwa Mwekezaji wa kiwanda cha sukari cha Mtibwa, kwamba Kiwanda hicho kimekuwa kikishindwa kuwalipa wastaafu mafao yao na hata wakienda mahakamani wanashangaa wanashindwa kesi na mwekezaji kuibuka mshindi hata katika kesi zao za msingi za madai.

Mratibu kutoka Uongozi wa Kiwanda cha Sukari Mtibwa,Bwa.Hamad yahaya akijibu tuhuma  na dhuluma mbalimbali zilizoelekezwa kwa mwekezaji wa Kiwanda hicho pamoja na uongozi mzima kutoka kwa Wakulima wa MiwaKufuatia tuhuma hizo wakulima wa miwa na wawakilishi wao walimwambia Kinana aliyeambatana na viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama cha CCM akiwemo Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, walisema mgogoro umedumu kwa miaka 10 lakini kwa bahati mbaya hakuna majibu ya suluhu hali inayofanya wananchi wajiulize maswali bila majibu.Aidha uongozi wa Kiwanda cha Sukari Mtibwa umeweka wazi kuwa kinatambua baadhi ya changamoto zilizopo baina yao na wakulima na kwamba sasa ni wakati wa kutafuta ufumbuzi wake na kuanza ukurasa mpya lakini pia wakaomba CCM kuiomba Serikali kuangalia wawekezaji wa ndani kwani kuna sukari inayotoka nje na kufanya wakose fedha.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa,Nassor Seif mara baada ya mkutano na Wakulima wa Miwa,Uongozi wa Kiwanda hicho pamoja na Uongozi wa juu wa CCM kukutana kwa pamoja na kusikiliza matatizo yaliyomo,uliofanyika mapema leo mchana kwenye ukumbi wa hotel ya Honolulu,Tuliani wilayani Mvomero,Morogoro.Mkutano huo umefanyika kufuatia Wananchi wa Wilaya ya Mvomero  mkoani Morogoro kukishitaki Kiwanda cha Sukari Mtibwa kuwa kimekuwa kikifanya dhuluma kubwa zidi ya wakulima wa miwa huku wakimuomba Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), kufanya kila analoweza kuhakikisha mgogoro uliopo kati ya pande hizo mbili unapatiwa ufumbuzi. 

Mkutano wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akiongoza kikao cha Uongozi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,katika utekelezaji wa kazi za taasisi hizo,katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi,(kulia) Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi pia Katibu Mkuu Kiongozi Dk.Abduhamid Yahya Mzee.
Wakuu wa Wilaya za Unguja na Pemba,pamoja na Maafisa wengine wakiwa katika mkutano uongozi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,chini ya Mwenyekiti Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) katika utekelezaji wa kazi za taasisi hizo,katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Mwinyihaji Makame,(kulia) na Wakuu wa Mikoa ya Zanzibar na wilaya wakiwa katika mkutano uongozi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Mwenyekiti akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) katika utekelezaji wa kazi za taasisi hizo,katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi.

UJUMBE WA MAKAMISHNA WA TUME YA UTUMISHI YA BUNGE ZIARANI AUSTALIA

$
0
0
Kamishna wa Bunge la Tanzania Mhe Mau Daftari akikabidhi zawadi ya picha ya Jengo la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Katibu wa Bunge la wawakilishi la Australia Ndg. Bernard Wright Mara walipofika Ofisini kwake kumsalimu. Wengine katika Picha ni Mhe. Hamad Rashid Mohamed na Mhe. Abdukarim Shah ambo wote ni Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge. Ujumbe wa makamishna wa Bunge la Tanzania upo Nchini, Australia kwa ziara ya Mafunzo.
Kamishna wa Bunge la Tanzania Mhe Mau Daftari akikabidhi zawadi ya picha ya Jengo la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Katibu wa Bunge la Maseneta la Australia Dr.Rosemary Laing Mara walipofika Ofisini kwake kumsalimu. Wengine katika Picha ni Mhe. Hamad Rashid Mohamed na Mhe. Abdukarim Shah ambo wote ni Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge.Ujumbe wa makamishna wa Bunge la Tanzania upo Nchini, Australia kwa ziara ya Mafunzo.
Ujumbe wa Makamishna wa Tume ya Utumishi ya Bunge ukiwa katika picha ya Pamoja na watumishi wa Bunge la Autralia. PICHA ZOTE NA OFISI YA BUNGE

BOMBA FM RADIO YATOA NAFASI MOJA YA KAZI KWA MTANGAZAJI

$
0
0
Kituo cha Bomba Fm Mbeya kimetangza ajira moja katika kituo hicho, ambapo mmoja kati ya watu watakao kuwa wakiwania nafasi hiyo ya ajira watashindana moja kwa moja kupitia vipindi viwili.

Akitangaza nafasi hiyo wakati wa kipindi cha Kali za Bomba kinachorushwa hewani Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 7 ya mchana hadi saa 10 ya jioni, Meneja Mkuu wa Kituo hicho FREDY HELBERT amesema licha ya ajira hiyo kutolewa kupitia mashindano bado vigezo na taratibu za kazi zitazingatiwa.

Mshindi wa mashindano atapatikana kwa ushirikiano mkubwa kati yake na wasilikilizaji ambao ndio watakuwa majaji wakuu……

VIGEZO vya mshiriki:-
1. Awe na umri wa kuanzia miaka 18.
2. Awe raia wa Tanzania.
3. Awe na elimu ya kuanzia Kidato cha nne.
4. Awe hana mkataba wowote na kampuni yoyote ile.
5. Awe hajawahi kufungwa jela au kushitakiwa na kosa lolote.
6. Awe na akili timamu.

Fomu ya ushiriki ni shilingi 10,000/= tu ya Kitanzania.

Kwa Waliopo nje ya Mbeya maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia simu ya mkononi.+255764 240 440

WATU MILIONI 14 WANUFAIKA NA HUDUMA YA MATIBABU YA MABUSHA NA MATENDE TANZANA: DK. MWELE

$
0
0
Dk. Mwele Malekela ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa NIMR akifungua Mjadala juu ya Utafiti wa udhibiti wa ugonjwa wa mabusha na matende kwa nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Baadhi ya washiriki ambao ni watafiti wakifuatilia mada za mjadala huo.

BOFYA HAPA KWA HABARI NA PICHA ZAIDI
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live




Latest Images