Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1067 | 1068 | (Page 1069) | 1070 | 1071 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Taswira za shughuli malumu ya chakula cha mchana iliyofanyika pale Courtyard Protea hotel ya Sea View jijini Dar es salam  kwa ajili ya wazee wasiojiweza wanaosaidiwa na Asasi ya Tushikamane Pamoja Foundation siku ya Jumamosi tarehe 19 Desemba, 2015. 
  Shughuli iliandaliwa na uongozi wa  Protea na Rickshaw kwa ajili ya kusherehekea Krismas na mwaka mpya. Jumla ya wazee 60 na wajukuu wao  walikaribishwa na kusaidiwa na wafanyakazi wa Protea. Viongozi pamoja na wahudumu waliopokea wageni wao kwa kujituma na uchangamfu mkubwa. 
  Mmoja wa wazee hao akisaidiwa kuketi 
  Bibi akiongozwa kuketi
  Pasina kujali nyadhifa zao mafisa wa Courtyard Protea hotel walisaidiana na wahudumu kuhudumia wazee hao kwa furaha na upendo
  Bibi akisaidiwa kuketi mezani
  Mwenyekiti wa TPF  Mama Rose Mwapachu akikawashukuru Viongozi na wafanyakazi wa Protea na Rickshaw kwa shughuli hiyo iliyofana sana 
  "Asante sana mwanangu..." anaonekana kusema bibi huyu wakati akiandaliwa chakula. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Nesi Wangu
  Kilimanjaro Studio iliyopo Beltsville, Maryland inatoa salamu za kheri ya sikukuu ya Maulid, Christmas na mwaka mpya kwa wadau wote wa Vijimambo Blog, Kwanza Production na Nesi Wangu Blog. Sikukuu iwe ya upendo na amani na muweze kusherehekea kuuaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka 2016.
  Kama hukutimiza malengo mwaka 2015 usijali mwaka 2016 ni mwaka wa kujipanga upya na Kilimanjaro studio inakutakia kila la kheri kwa mwaka mpya 2016 uwe mwaka wa mafanikio makubwa kwako na kumwomba Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema palipokua na giza 2015 mwaka mpya apatie mwanga, palipokua na chuki 2015 mwaka mpya apaweke amani yote na tunaimani utafikia malengo na sisi kujipanga kwa mambo mapya kwa kuongeza vipindi kwenye Radio na kukuhabarisha kwenye Blogs zetu.

  SOTE KWA PAMOJA TUNASEMA KHERI YA SIKUKUU YA MAULID, CHRISTMAS NA MWAKA MPYA

  0 0

  Mwenyekiti wa NGOs ya Go For Zanzibar Antje Fleischer na Meneja Mradi Mussa Khamis Baucha , wakimkabidhi  msaada Mwakilishi wa Wazee wa Kijiji cha Welezo Zanzibar  Mzee Kombo Shein, vyakula kwa ajili ya wazee hao ili kuweza kujimuika na Wananchi katika kusherehekea Sikukuu ya Krismax  na mwaka mpya  kulia Msimamizi wa Kijiji hicho Sister Mary Gemma na Hassan Khamis hafla hiyo imefanyika katika makaazi ya wazee hao welezo jana

  Mwakilishi wa Wazee Welezo Mzee Shein, akimshukuru Mwenyekiti wa NGOs ya Go For Zanzibar Antje Fleische, kwa msaada wao na kumtaka kuwa Balozi wao huko Nje kuwawakilishi ili kuweza kupata misaada zaidi hasa gari kwa ajili ya kutembelea sehemu mbalimbali wakati wa sikukuu na kutumika kwa shughuli zao za kawaidi.
  Mzee Shein akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhiwa Vyakula kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Krismax na Mwaka Mpya 
    

  Sister Mary Gemma akitowa shukrani kwa Ngo ya  GOZA kwa msaada wao kwa kuwajali Wazee hasa kwa wakati huu wa kusherehekea Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya. 

  German help organization GOZA is celebrating Christmas 6 degrees south in Zanzibar together with the old people (Wazee) in Welezo Old Age Home.
  Since five years now the German help organization GO FOR ZANZIBAR (GOZA) NGO is supporting the Welezo Old Age Home.

  Different charity offers have been done since the cooperation with the old age home in Welezo started in 2010.

  The main offers in the last years were:

  -        Renovation of two wards and improvement of the sanitary facilities
  -        Establishing a regular medical support for the old people
  -        Support of food, medecine, clothes, wheel chairs
  -        Workshops in basic nursing for the nurse assistance

  The donation amount in the last five years covers a budget of round 22,000,000 TSH (10,000 Euro).
  A main goal for the German help organization is the knowledge transfer to the medical staff of the old age home. Therefore very experienced nurses from Germany traveled to Zanzibar and hold several workshops in basic nursing as well as mobilization of old people.
  In January 2016 the next workshops will take place. The manager nurse Renate Conrad from Tuebingen will teach in Welezo.
  Antje Fleischer, Director of GOZA NGO:“We are very thankful for the good cooperation with the nurses in Welezo as well as with the government of Zanzibar and cooperation partners like ZOP (Zanzibar Outreach Program). Without the help of the local partners it would not be possible for us to do a sustainable work here in Zanzibar.“
  Mussa Baucha, project manager of GOZA NGO:“As I am a Zanzibari I am very proud to be able to work for my own people in such a professional way together with my co-workers and board members of our organization GOZA.“
  Fact sheet:
  -          Founded in May 2010 in Tuebingen/Germany by  Antje Fleischer and Mario Mueller
  -          GOZA NGO is registered as a charitable association by German law
  -          Each donation will be forwarded directly and without full deduction to 100 percent of the projects in Zanzibar
       Projects and goals:
  -  Support for (HIV)-orphans
  -   Support for kindergartens and schools
  Amelioration of living conditions especially for elderly, destitute people
  Amelioration of medical/health care

  Further informations:
  Do not hasitate to contact us! Ahsante sana for your cooperation.
  -----------------------------------------------------------------------------------------
  GO FOR ZANZIBAR e.V. (NGO)
  Heerweg 1

  72070 Tübingen

  Germany 

  0 0

   Leo ndio siku ya kuzaliwa mwanamtindo na mbunifu maarufu wa mitindo ya mavazi wa kimataifa Asya Idarous wa  Khamsin almaarufu kama "Mama wa Mtindo" Mtanzania aliyejizolea sifa kedekede na anayeendelea kuiwakilisha Tanzania kimataifa katika fani ya mitindo ya mavazi.
  Tunamtikia kila la kheri, afyaa njema,maisha bora, maisha marefu,na furaha ya maisha.

   Keki ya Mama wa Mitindo
  Mama wa Mitindo akionesha kwa nini anaitwa hivyo.
  Globu ya Jamii inamtakia Mama wa Mitindo maisha marefu ya furaha, heri na fanaka, Tunamshukuru sana yeye na mume wake Kaka Khamsin kwa kuwa mstari wa mbele kutupa ushauri wa kikazi na wa kifamilia katika shida na raha bila kuchoka. HAPPY BIRTHDAY MAMA WA MITINDO!!!

  0 0

   Waumini wa Dini ya Kiislam wakiandamana jijini Dar es Salaam leo jioni, wakati wa kuadhimisha Sikukuu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.W.A).

  PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
  0 0


  0 0

  Nairobi is one of the most popularly requested destinations and we’re thrilled to announce our two new routes to the destination! You can now fly with fastjet from both Kilimanjaro and Dar es Salaam daily to Nairobi! 
  Tickets are now on sale and flights to Nairobi take just an hour from Kilimanjaro and 90 minutes from Dar es Salaam. It’s never been quicker to get to Kenya from Tanzania!
  The first flight departs 11th January, so 2016 has already got off to a flying start. One-way prices start from just:
  Dar es Salaam to Nairobi Tsh 283,800 (Tsh 176,000 fare, Tsh 107,800 taxes)
  Nairobi to Dar es Salaam Tsh 264,000 (Tsh 176,000 fare, Tsh 88,000 taxes)
  Kilimanjaro to Nairobi Tsh 217,800 (Tsh 110,000 fare, Tsh 107,800 taxes)
  Nairobi to Kilimanjaro Tsh 198,000 (Tsh 110,000 fare, Tsh 88,000 taxes)


  Buy your tickets today at www.fastjet.com 
  And be one of the first to fly fastjet to Kenya....

  0 0

  Hapa ni Kwa Msisi mkoani Tanga ambapo mdau katutumia taswira hii ya wadau wakielekea "KUHESABIWA" vijijini kwao sehemu mbalimbali Kaskazini mwa Tanzania, ikiwa ni utamaduni wa miaka nenda miaka rudi ya kusherehekea Krismas na Mwaka Mpya. Globu ya Jamii inawapongeza wadau hawa wote kwa kukumbuka kurudi nyumbani katika msimu huu...

  0 0

  Wakazi (Tanzania) has been nominated for the 2016 Kora Awards as "Best Hip Hop Act" alongside K.O (South Africa), Sarkodie (Ghana), Stanley Enow (Cameroon), Hamzaoui Med Amine (Tunisia) & Kiff No Beat (Cote D'voire). The Award Ceremony will take place in Windhoek, Namibia on March 20th 2016.
  Here is Wakazi's Ojuelegba Flip dubbed "Natokea Dar" which just like Wizkid's original, he gives tales of the neighborhood he is from in a realistic narrative. The bilingual emcee talks of his upbringing as well as the tales of the streets that captures an average joe's day to day life.The video was directed by Mecky 

  0 0


  Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inakanusha taarifa zilizoandikwa katika gazeti la Mwananchi la tarehe 24.12.2015 yenye kichwa cha habari “JPM kutolipa makocha Stars”.


  Serikali  kupitia Wizara inayohusika na michezo haijatoa tamko  la kutowalipa makocha wanaofundisha timu ya Taifa Stars kama ilivyoripotiwa na gazeti hilo.


  Suala la malipo ya makocha wa Taifa Stars linashughulikiwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za Serikali, pindi maamuzi yatapofikiwa, serikali itatoa maelekezo kama itaendelea kuwalipa au la.


  Serikali ya Awamu ya Tano inathamini michezo yote ikiwemo mpira na miguu , kwa hiyo itaendelea kushirikiana na Vyama vya vyote vya michezo na wadau wote wa michezo kwa ujumla katika kuhakikisha kuwa michezo inaimarika na kuwa chanzo cha ajira kwa vijana nchini.


  IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI (MAELEZO)


  24 DESEMBA, 2015


  0 0


  0 0
  0 0

   Baadhi ya Maofisa wa Jeshi la Magereza waliohudhuria katika hafla ya kuaga mwili wa Marehemu Mkaguzi wa Magereza, Morice Peter.
   Mke wa Marehemu Mkaguzi wa Magereza, Dorice Peter(kulia) akipewa msaada ndugu wa karibu wakati wa kusindikiza mwili kuelekea kwenye gari tayari kwa safari ya kuelekea Mkoani Morogoro kwenye mazishi.

   Mkaguzi wa Magereza, Seleman Sued wa Gereza Kuu Ukonga, Jijini Dar es Salaam akisoma Wasifu wa Mkaguzi wa Magereza Morice Peter aliyefariki juzi Desemba, 2015 katika Hospitali ya Dar Group, Jijini Dar es Salaam.
   Ndugu na jamaa waliojitokeza kuuaga mwili wa Marehemu Mkaguzi wa Jeshi la Magereza, Morice Peter aliyekuwa akihudumu katika Gereza Kuu Ukonga, Jijini Dar es Salaam. Mkaguzi Morice Peter amefariki juzi Desemba 22, 2015 baada ya kuugua muda mrefu katika Hospitali ya Dar Group Jijini Dar es salaam
  Maafisa wa Jeshi la Mageereza wameubeba mwili wa Marehemu  Mkaguzi wa Magereza, Morice Peter wakiuingiza nyumbani kwake kabla ya kutoa heshima za mwisho leo Desemba 24, 2015 katika Viwanja vya Gereza Kuu Ukonga Jijini Dar es Salaam.Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza)

  0 0


  0 0


  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa na Rais Mstaafu, Ali Hassn Mwinyi wakisikiliza Kasida katika Baraza la Iddi lililohutubiwa na Waziri Mkuu kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam Desemba 24, 2015. Wapili kulshoto ni Sheikh Mkuu wa Tanzania Kufti Abubakari Zubri na kushoto ni Kadhi Mkuu wa Tanzania Alhaji Mnyasi.
  Baadhi ya washiri wa Baraza la Maulid wakimsikilza Waziri Mkuu, Kassim Majliwa wakati alipohutubia Baraza hilo kwenye ukumbi wa Karimjee jijiniDar es salaam Desemba 24, 2015.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Shinyanga, Hamisi Mgeja na baadhi ya washiriki wa baraza hilo baada ya kuhutubia Baraza la Idd kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam Desemba 24, 2015.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim katika baraza la idd alilolihutubia kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam Desemba 24, 2015. ,Kushoto ni Bw. Azim Dewji na wapili kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku na kulia nii Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, Ramadhani Kailima.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0  0 0

  Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limejipanga kikamilifu katika kuhakikisha Maadhimisho ya sikukuu katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka 2015 na mwanzo wa mwaka 2016. Siku kuu zinazotarajiwa ni Mkesha wa X- Mass katika Makanisa mbalimbali hadi siku yenyewe ya X- Mass tarehe 25/12/2015 na hatimaye tarehe 01/01/2016 Sikukuu ya mwaka mpya. 

  Jeshi hilo limesema litaimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali ya biashara na mikusanyiko ya watu kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola ili kuhakikisha yeyote mwenye nia ovu ya kufanya uhalifu wa aina yeyote anadhibitiwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

  Kamati za ulinzi na usalama katika nyumba za ibada na makampuni ya ulinzi binafsi nao wametakiwa kushiriki kikamilifu ili kuhakikisha ulinzi unaimarika na ibada zinafanyika bila bughudha ya aina yeyote. 
  Wananchi wote wakazi wa Dodoma na wageni watakao kuwa Dodoma katika kipindi hiki cha siku kuu za mwisho na mwanzo wa mwaka wanatakiwa kuchukua tahadhari za kiusalama, washerehekee kwa amani na utulivu  na shamra shamra zao zisivunje sheria. 

  Wazazi wahahikikishe watoto wao hawaendi katika kumbi za starehe na bar bali wanasherehekea katika mazingira salama wakiwa chini ya uangalizi makini, ulinzi majumbani uimarishwe wasiache nyumba peke yake. Wamiliki wa kumbi za starehe wahakikishe hawajazi watu kupita kiasi, wahakikishe usalama ni wa kutosha katika kumbi zao. 
  Aidha watumiaji wote wa barabara wazingatie sheria za usalama barabarani na hasa waendesha vyombo vya moto wazingatie udereva wa kujihami na kuhakikisha kwenye makazi ya watu hawaendeshi vyombo vya moto zaidi ya spidi 50kph kama sheria za usalama barabarani kifungu cha 51 kinavyoelekeza. Kuepukana na ulevi kupita kiasi na kutoendesha magari wakiwa wamelewa ili kuepusha ajali zisizozalazima. 

  Kila mmoja ni vizuri akatambua kuwa usalama unaanza na yeye mwenyewe na maana halisi ya sikukuu hizi ni kumtukuza Mungu na kudumisha amani na pale watakapotilia shaka jambo lolote watoe taarifa Polisi ili kupatiwa msaada wa haraka. Ninawatakia sikukuu njema zenye amani na utulivu.

  0 0

  Mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ameanza kwa kishindo kutekeleza ahadi zake kwa wananchi wa jimbo hilo na huku akiahidi maendeleo kwa kasi zaidi.

  Profesa Muhongo alidhihirisha hayo juzi katika kijiji cha Murangi, Mkoani Mara katika kikao chake na baadhi ya wananchi wa jimbo hilo, watendaji wa Halmashauri ya Musoma Vijijini na madiwani huku lengo la kikao likiwa ni kujadili mipango na miradi ya uchumi na maendeleo ya jimbo hilo.

  Katika kikao hicho, iliazimiwa kuanzishwe Mfuko wa Elimu wa Jimbo ambapo Profesa Muhongo aliahidi kutoa kiasi cha Shilingi Milioni mia moja ambazo atakopeshwa na Bunge kwa ajili ya kununulia gari.

  Alisema badala ya kununulia gari, fedha hiyo ataiingiza kwenye Mfuko huo ili kuleta maendeleo kwenye jimbo hilo. “Dhamira yangu ni kuhakikisha jimbo letu linasongo mbele kiuchumi na kimaendeleo na siyo maneno bila mipango madhubuti,” alisema.
  Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akizungumza jambo wakati wa kikao chake na wananchi wa jimbo hilo pamoja na wadau wa maendeleo.

  Katika maelezo yake ya mikakati ya maendeleo kwa jimbo hilo, Profesa Muhongo alisema kufikia Mwezi Januari mwanzoni, ataanzisha Ofisi tano za Mbunge jimboni humo ili kufikisha huduma kwa wananchi kiurahisi.

  SOMA ZAIDI HAPA

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad alipowasili katika sherehe za Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis, Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad (kushoto) na Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali wakiwa katika sherehe za Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja.
  Wanafunzi wa Madrasa mbali mbali za Zanzibar wakiwa katika sherehe za Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja,ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein.


  0 0

  S1
  Mkuu wa Wilaya ya Iringa akipokea maelezo toka kwa Mshauri wa Mgambo wa Mkoa Luteni Kanali J. Kitita
  S2
  Mkuu wa Wilaya Bwana Richard Kasesela akiongea na wana Mgambo na kuwaasa kuwa waaminifu kwani wao ndio walinzi namba moja katika nchi kwani wao wako karibu sana na wananchi. pia Mkuu wa wilaya alisistiza suala la usafi kama nguzo moja wapo ya uadilifu.
  S3
  Mkuu wa wilaya akizindua mafunzo ya shabaha. alifanikiwa kulenga 10 kati ya 30 zilienda kwenye shabaha
  S4
  Mkufunzi wa mafunzo akihesabu shabaha.
  S5

  Mkuu wa wilaya akionyesha jinsi ya kutumia SMG 

older | 1 | .... | 1067 | 1068 | (Page 1069) | 1070 | 1071 | .... | 3286 | newer