Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1066 | 1067 | (Page 1068) | 1069 | 1070 | .... | 3286 | newer

  0 0

  un2

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na hatua zilizofikia katika kutatiua mgogoro baina ya Timu ya Stand Unite ya mjini Shinyanga na kamati ya uendeshaji ya timu hiyo iliyopo chini ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa leo jijini Dar es Salaam.Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,WHUSM.
  un1
  Baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji ya timu ya Stand United ya mjini Shinyanga wakifuatilia maelezo ya Waziri wa Habaroi, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (hayupo pichani) wakati wa kikao baina yao na Waziri huyo leo jijin Dar es Salaam.
  un3
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (kushoto)akifuatilia maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa timu ya Stand United Bw. Aman Vicent (katikati)wakati wa kikao baina ya wajumbe wa Kamati tendaji ya Club hiyo na Mhe. Waziri ili kujadili mgogoro unaoikabili timu hiyo leo jijini Dar es Salaam.
  ………………………………………………………………………………………….
  Na: Frank Shija, WHUSM.

  Serikali imeagiza kumalizika kwa mgogoro uliopo baina ya Timu ya mpira wa miguu ya Stand United na Kamati ya uendeshaji wa timu hiyo iliyopo chini ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

  Agizo hilo limetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye mara baada ya kumaliza kikao na uongozi wa Stand United.

  Nape amesema kuwa imefika wakati vilabu vikapewa uhuru wa kujiendesha kwa kutumia katiba zao badala ya kingiliwa na chombo kingine chenye  maslahi binafsi.

  “Wizara itasaidia kuona mgogoro huu unaisha kwa Stand United kupewa uhuru wa kujiendesha yenyewe na uongozi uliokuwapo kupewa mamlaka yake ya kusimamia na kuendesha shughuli za Timu yao kwa mujibu wa Katiba”

  Aidha aliongeza kuwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kusimamia uendeshaji wa mchezo wa mpira wa miguu kwa kuzingatia sheria ,kanuni na taratibu za mchezo huo ili kuepuka migogoro isiyokuwa na tija.Kwa upande wake Mwenyekiti wa Timu ya Stand United Bw. Aman Vicent ameishukuru Serikali kupitia Wizara yenye dhamana na masuala ya michezo kwa kuona umuhi wa kushughulikia na kumaliza mgogoro wao.

  Aman amesema kuwa kutokana na makubaliano waliyofikia katika kikao hicho imani yao ni kuwa suala hili litamalizika mapema kwa kuwa Waziri mwenye dhamana ameonyesha nia na utayari wa kuhakikisha suala hili linaisha kwa wakati ili Timu iweze kusonga mbele katika kujiletea maendeleo.

  Kikao baina ya Waziri na uongozi wa Timu hiyo kimefanyika ikiwa ni matokeo ya juhudi za uongozi wa Timu ya Stand Uinted kuinusuru timu yao baada ya kujikuta katika mgogoro usiokuwa na tija zaidi ya maslahi binafsi kutoka na udhamini walionao.

  0 0


  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akimsalimia Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile wakati alipowasili Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya ziara ya kikazi. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo. Katika ziara hiyo, Waziri Kitwanga aliitaka Idara hiyo ya Uhamiaji kuanz rasmi kwa operesheni ya kuwakamata Wahamiaji Haramu nchini. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (aliyevaa tai) akiwasalimia wananchi  wanaosubiri kupata huduma ya Hati za Kusafiria katika Ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam. Waziri Kitwanga alifanya ziara ya kikazi katika ofisi hizo kwa lengo la kujifunza kazi mbalimbali zinazofanywa na Uhamiaji. Katika hotuba yake, licha ya maelekezo mengine aliyoyatoa kwa viongozi wakuu, pia aliitaka Idara hiyo ya Uhamiaji kuanza rasmi kwa operesheni ya kuwakamata Wahamiaji Haramu nchini. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  Afisa Uhamiaji anayeshughulika na uchapaji wa Hati za Kusafiria, Amir Hassan (kushoto), akitoa maelezo ya jinsi wanavyozichapisha Hati za Kusafiria, kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) ambaye alifanya ziara ya kikazi katika ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile (kushoto) akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, wakati Waziri huyo alipokuwa anafanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Uhamiaji. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akiwaeleza jambo Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya idara hiyo, Kurasini, jijini Dar es Salaam leo. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani
  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (wasita kulia), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil (watano kushoto), Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo (wanne kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Wakuu wa Idara ya Uhamiaji wakati Waziri huyo alipotembelea Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam. Wasita kushoto ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0


  Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
  WAZIRI wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk.Diwani Msemo ili kupisha uchunguzi pamoja na mambo mengine ili kubaini  mgongano wa kimaslahi ulioathiri utendaji wa taasisi  hiyo chini ya kaimu mkurugenzi huyo.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto mwenye Wizara hiyo, Ummy Mwalimu imesema kuwa kutokana na ziara alizofanya Rais Dk. John Pombe Magufuli inaonyesha kukosekana kwa dawa katika hospitali za Serikali huku vituo vya afya vya  binafsi vikiwa na dawa.

  Taarifa ya Waziri huyo imesema kuwa upungufu wa dawa umeendelea kujitokeza kwa karibu zaidi na baadhi ya wagonjwa walieleza kwa uchungu jinsi wanavyopata dawa kwa tabu hatazile wanazotakiwa wapate kwa bei ya ruzuku au zilezinazotakiwa kutolewa bure na serikali.

  Kwa msingi wa uwazi na uwajibikaji ameagiza watendaji wote wa sekta afya hususani wakuu wa vituo vya kutolea huduma za afya, Wafamasia, Wauguzi na Waganga Wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za afya kukiri kwa maandishi kwa ngazi zao za uwajibikaji endapo wanamiliki Hospitali, Zahanati, Kiliniki, Maduka ya Dawa ndani ya siku 21 kuanzia leo Desemba 23 mwa huu ambapo  agizo hilo limeotolewa.

  Aidha taarifa hiyo imedai kuwa kufanya hivyo kutaziba mianya ya upotevu wa dawa na vifaa tiba katika vituo vya umma.

  Bodi ya Taasisi ya Ocean Road imeagizwa kutafuta mtu atakayekaimu nafasi iliyoachwa wazi na Dk.Msemo anayefanyiwa uchunguzi.

  0 0


  maj2

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa wanaongeza udhibiti na usimamizi wa migogoro ya  ardhi kwenye maeneo yao husika.
   Ametoa agizo hilo leo mchana (Jumatano, Desemba 23, 2015) wakati akizungumza na viongozi wa mkoa wa Lindi kwenye Ikulu ndogo mara baada ya kuwasili akitokea jimboni kwake Ruangwa.

  “Ardhi ni mali ya Serikali lakini maeneo yanayotwaliwa kwa sababu mbalimbali za maendeleo yasiwe chanzo cha migogoro na wananchi tunaowaongoza,” alisema.

  Akitoa mfano, Waziri Mkuu alisema anatambua kuna mgogoro wa eneo la mgodi katika wilaya ya Ruangwa baina ya wananchi na wawekezaji wa kampuni ya Uranex. Na hii ni kwa sababu wao ndiyo waliamua kufanya tathmini (evaluation) ya eneo hilo. Yale ni makosa kwa sababu aliyepaswa kufanya tathmini ni Halmashauri na siyo mwekezaji,” alisema.

  Alisema wawekezaji wanaruhusiwa kisheria kufanya tathmini lakini sheria waliyoitumia ni sheria namba 8 peke yake. “Kama Halmashauri ingefanya kazi hiyo ni lazima wangetumia sheria ya ardhi ya vijiji pamoja na sheria ya madini na wananchi wangepata thamani halisi ya ardhi yao,” alisema.

  “Ninaagiza Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa ikahakiki lile eneo na kubaini kama ni la kilimo au la madini na kama ni la kilimo, wananchi wamelima mazao gani na kwa muda gani kisha wafanye tathmini upya. Yuko valuer wa Halmashauri mwenye dhamana hiyo na siyo wao,” alisema.


  “Nasisitiza tena ni vema Wakurugenzi wote, Wakuu wa Wilaya chini ya uongozi wa Wakuu wa Mikoa mjiridhishe kuwa hakuna migogoro kwenye maeneo yenu. Kama ipo, imalizeni kwa kukaa mezani na kuzungumza na pande husika, inawezekana kabisa,” alisisitiza.

  0 0

  pu3
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi  Bw.Bakari Amir pampu  mbili za kusukuma maji na mipira yake, Mwenyekiti wa kikundi cha kufyatua matofali ya kuchoma cha Jitumecha kilichopo eneo la Gogovivu wilayani Ruangwa  Desemba 23, 2015.  Pampu hizo zitawapunguzia wnakikundi mzigo wa kubeba maji toka mtoni. 
  pu4
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi funguo na kadi ya pikipiki Mwenyekiti wa kikundi cha Bodaboda Mkowe cha kijiji cha Nandagara, Yahya Chitanda ambayo ameikipatia kikundi hicho  Desemba 23, 2015 ili kiweze kukuza mtaji wake. 
  pu1
   Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na  maofisa wa jeshi la Polisi wakati alipotembelea kituo kikuu cha polisi zcha wilaya ya Ruangwa kusalimana na Askari Desemaba 23, 2015. Wapili kushoto ni mkewe Mary na watatu kushoto ni Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Lindi, Renata  Mzinga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Said Meck Sadick akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani ofisini kwake leo alipokutana nao kuelezea utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa kwa DAWASCO kuhusu usambazaji wa maji safi na salama ili kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa  DAWASCO Mhandisi Cyprian Luhemeja akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani Dar es salaam  leo alipokutana nao kuelezea utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na  Serikali kuhusu usambazaji wa maji safi na salama ili kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.Picha zote na Ally Daud-Maelezo.


  NA ALLY DAUD-MAELEZO

  Shirika la Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASCO) limeongeza uzalishaji na usambazaji wa Maji safi na Salama kwa wakazi wa jiji hilo hadi kufikia mita za ujazo 280,000 kwa siku ili kubabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu  uliolikumba jiji hilo hivi karibuni. 

  Hatua hiyo inatokana na utekelezaji wa maagizo ya Serikali yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadiki kuitaka DAWASCO kusambaza maji safi na salama kwa wakazi wa jiji hilo ili kupambana na Ugonjwa wa Kipindupindu.

  Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkuu wa mkoa huo Bw. Sadick amesema kuwa kufuatia maagizo aliyoyatoa kwa shirika hilo ikiwemo kusambaza maji safi na salama kwa wananchi pamoja na kutengeneza mifereji ya kupitsha maji taka ili yasiingiliane na mikondo ya maji safi, DAWASCO wametekeleza kwa kiasi kikubwa maagizo hayo.

  “Dawasco imehakikisha inazalisha maji safi na salama kati ya mita za ujazo 270,000 na 280,000 kila siku kwa muda wote tangu mlipuko ulipotokea na imehakikisha inasafisha na kusambaza kwa wananchi yakiwa katika viwango vya ubora unaokubalika kwa ajili ya matumizi kwa binadamu” amesema Bw. Sadick.

  Ameongeza kuwa Dawasco imejenga vizimba vya maji  safi na salama kwenye maeneo mbalimbali ambayo hayajakumbwa na yaliyokumbwa na athari za mlipuko wa ugonjwa huo kwa jumla ya vizimba 48 ambavyo maeneo ya Kinondoni vizimba 5, Magomeni vizimba 38 na Ilala vizimba 5.

  Aidha, amesema kuwa DAWASCO kwa kushirikiana na Ofisi ya Bonde Wami Ruvu imeanza kazi ya kusajili na kuwatambua watu binafsi wenye visima virefu vilivyopo kisheria ambao wanauza maji kwa wananchi ili kuvitambua na kudhibiti ubora wa maji na bei yake ambapo zoezi hili litaendelea hadi Machi 2016.

  “Dawasco imefanya jitihada za kuweka dawa ya kuua wadudu aina ya chrolination kwenye maboza  wakati wa  usajili kabla ya kuruhusiwa kufanya biashara ya kuuza maji kwa wananchi na kuongeza sehemu za kuchota maji kwa kuwapelekea wananchi huduma hiyo wakitumia magari yenye matanki yaliyokuwepo kutoka 12 mpaka kufika 49 kwa sasa” aliongeza Bw.Sadick.Katika hatua nyingine Bw. Sadick alitoa rai kwa wakazi wa jiji hilo kuendelea na tabia ya kufanya usafi mara kwa mara ili kutokomezakabisa ugonjwa wa kipindupindu kwani kuanzia juzi hakuna wagonjwa waliopokelewa katika vituo vyote.

  Kwa upande wa Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO Mhandisi Cyprian Luhemeja alisema kuwa wako katika hatua za mwisho kukamilisha ujenzi wa mifereji ya kupitisha maji machafu ili isiingiliane na maji safi kwa wiki mbili zijazo.

  “kufikia Februari mwakani tutaweza kutoa maji safi na salama ya kutosha kwa wananchi  wote wa Dar es salaam bila ya matatizo yoyote” alisisitiza Mhandisi Cyprian.   


  0 0

   Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma Bi. Ziada Nkinda (Aliyebeba Mtoto) akikabidhi zawadi za siku kuu ya Noeli (Christmas) zilizotolewa na Mhe. Rais John Pombe Magufuli kwa watoto wanaoishi kwenye kituo cha kuhudumia watoto cha kijiji cha matumaini Mkoani Dodoma.
  Meneja wa kituo cha kuhudumia watoto cha kijiji cha matumaini kilichopo Dodoma  Padiri Vicent, kwa niaba ya watoto wa kituo hiko, akimshukuru Bi. ziada Nkinda kwa kukabidhi zawadi zilizotolewa na Mhe. Rais John Pombe Magufuli zikijumuisha mchele kilo 121, Mbuzi wawili na mafuta ya kupikia lita 40 vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya laki sita.
  (PICHA NA OFISI YA MKUU WA MKOA DODOMA)

  0 0


  0 0


  Mkurugenzi Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Ofisi ya Mazingira, Bwana Julius Ningu (kulia) akiwapongeza Vijana wa Shule ya International School of Tanganyika (IST) mbele ya Waandishi wa Habari leo 23 Desemba, 2015 katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) kwa ubunifu wa kutengeneza mifuko kwa ajili ya utunza mazingira dhidi ya utupaji taka ovyo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko Limited, Bwana Constantine Majavika, anaemfuatia ni Alyanz Nasser na mwenzie Shilen Dauda (wa pili kulia).
  Mkurugenzi wa Masoko Limited, Bwana Constantine Majavika (kushoto) akifafanua kuhusu ubunifu uliofanywa na vijana wa Shule ya International School of Tanganyika (IST) mbele ya Waandishi wa
  Habari leo 23 Desemba, 2015 katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) wa kutengeneza mifuko kwa ajili ya utunza mazingira dhidi ya utupaji taka ovyo. Kushoto ni Shilen Dauda na katikati ni Alyanz Nasser. 


  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  As a powerful global voice for Girls Education, Zuriel has presented her second annual DUSUSU Award to Her Excellency First Lady of Kenya, in a colorful ceremony at the State House, in Nairobi.

  Earlier in the year, she presented her Gender Minister Award to Hon Nana Oye Lithur of Ghana. Last year in 2014, the Gender Minister Award went to Hon Mireille Martins of Mauritius, while the First Lady Award went to Her Excellency Salma Kikwete of Tanzania.  The Award recognizes Gender Ministers advancing women's issues in Africa, and First Ladies making a strong case for Girls Education in their countries.

  The search for 2016 Awardees has begun.

  THE ZURIEL PHEANOM

  Some seek power, to become influential. Others by virtue of a "steel small voice" become influential at such a young age, and thus, powerful. Zuriel has become a powerful voice on the global civil society scene. In December 2013, she was named at age 11 in New Africa Magazine's annual 100 Most Influential African's List, along side 3 serving African Presidents.

  ELLE Magazine named her in March 2015 in their annual ranking of "33 Women Who Changed The World", and she has been featured on CNN, BBC, CNBC Power Lunch, Bloomberg TV and Forbes Magazine at age 10. New York's Business Insider named her the Most Powerful 11 Year Old In The World in April 2014.

  Zuriel has focused on doing 2 simple things - making the case for girls education in Africa, and making compelling films that show a positive Africa.

  She is on her way to Namibia, to spend some time with the children of the "San Tribe", better known to the rest of the world as the Bushmen of the Kalahari Desert.

  0 0


  0 0
  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhani Dau akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni wakati waziri huyo  alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo, ambapo ujenzi wake utakamilika mwishoni mwa mwezi Januari mwakani.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhani Dau (katikati) wakati alipofanya ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Mradi ujenzi wa Daraja hilo. Mhandisi Kareem Mataka. 
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhani Dau (wa pili kulia), akitoa maelezo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (kulia), alipofanya ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo, ambalo ujenzi wake utakamilika Januari Mwakani. 
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau wakati alipofanya ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo ambalo ujenzi wake utakamilika Januari Mwakani. Kwa habari kamili BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) na Ofisa Ufundi (IT) wa kampuni hiyo, Rehema Maswanya (kulia) kwa pamoja wakifungua pazia kuashiria uzinduzi wa teknolojia ya 4G LTE iliyozinduliwa leo jijini Dar es Salaam. 
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya uzinduzi wa teknolojia ya 4G LTE inayotolewa na kampuni hiyo. Kushoto ni Ofisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya TTCL, Peter Ngota akiwa katika mkutano huo. 
  Ofisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya TTCL, Peter Ngota (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hafla ya TTCL kuzinduwa teknolojia ya 4G LTE iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura. 

  KAMPUNI ya Simu nchini Tanzania (TTCL) leo imezinduwa mtandao unaotumia teknolojia ya 4G LTE unaoanza kutoa huduma jijini Dar es Salaam. Mtandao huo wenye teknolojia mpya na ya kisasa wenye kasi kubwa utatoa huduma katika maeneo 11 ambayo ni pamoja na Uwanja wa Ndege wa Mwalimu J.K. Nyerere, Pugu Road, Posta Mpya, Upanga, Kinondoni, Ubungo, Oysterbay, Mwenge, Mbezi Tangibovu, Mbezi Exchange, Kunduchi Salasala, na Wazi Tegeta.

  Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati akizinduwa rasmi teknolojia hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura alisema licha ya kuzinduwa huduma hiyo katika maeneo 11 kwa sasa mafundi wa kampuni hiyo wapo kazini wakiendelea na awamu ya pili ya kufunga mitambo ili huduma hiyo itolewe pia katika maeneo mengine 14 ya jiji la Dar es Salaam.


  Aliyataja maeneo mengine ambayo mitambo inaendelea kufungwa kwa sasa kuwa ni pamoja na Kigamboni, Masaki, Temeke, Kimara, Jangwani, Kariakoo, Chuo Kikuu, Kurasini, Mbezi Chini Gongo la Mboto, Tabata, Kibamba, Kongowe na Bunju.

  "...Awamu ya pili ya mradi huu itakuwa imekamilisha maeneo yaliyobaki ya mkoa wa Dar es Salaam na pia kupeleka mawasiliano hayo katika mikoa mingine ikiwa ni pamoja na Arusha, Mwanza, Mbeya, Dodoma na kwingineko," alisema Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kazaura.

  Alisema uzinduzi wa teknolojia ya 4G LTE unakuwa umekamilisha nia ya siku nyingi ya kampuni ya TTCL ya kuwahudumia wateja katika nyanja zote za mawasiliano (Fixed-mobile convergence) kwa kutumia teknolojia ya simu za mezani na simu za mkononi.

  Akifafanua zaidi Dk. Kazaura alisema uzinduzi wa teknolojia ya 4G LTE utakuwa na mchango mkubwa katika kukuza na kuongeza kasi ya shughuli za maendeleo ya kijamii na kiuchumi, kuchangia katika kukuza teknolojia ya habari na mawasiliano na pia kuongeza uzalishaji kwenye sekta mbalimbali za maendeleo.

  Aidha aliongeza kuwa TTCL inaamini mtandao wa 4G LTE utafungua fursa pekee katika kukuza sekta ya elimu nchini kwa njia ya mtandao (E education). Na pia ubora wa huduma hiyo ya intaneti utatoa fursa kwa wanafunzi, wakufunzi, wataalam, wanazuoni na walimu kutumia teknolojia katika kujifunza mambo mbalimbali ya kitaaluma na nje ya taaluma.

  Kwa upande wake Ofisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya TTCL, Peter Ngota akifafanua zaidi kwa wanahabari alisema mtandao wa 4G LTE utaongeza fursa katika sekta ya afya ambapo hospitali, vituo vya afya, vyuo vya afya na wadau mbalimbali wataweza kutumia mtandao huo katika kuongeza ufanisi wa kutoa huduma bora za afya kwa wananchi tena kwa haraka zaidi.


  Alisema mtandao huo pia utazinufaisha sekta nyingine za kiuchumi kama vile sekta ya biashara, viwanda, kilimo na nyinginezo. "...Wafanyabiashara na wazalishaji wa bidhaa wanahitaji mawasiliano ya uhakika katika shughuli zao. Mtandao huu wa 4G LTE utakuwa mkombozi wao na utaleta mageuzi katika kuongeza uzalishaji, kupanua wigo wa masoko ya bidhaa kwa wakulima, masoko kwa wajasiliamali, masoko kwa makampuni ndani na nje ya mipaka ya Tanzania," alisema Peter Ngota.


  Hata hivyo, Ngota aliongeza kuwa uzinduzi huo unaenda sambamba na uboreshaji vifurushi rafiki vya intaneti kwa wananchi hivyo kuwaomba wananchi kuiunga mkono kampuni ya kizalendo ya TTCL katika kuboresha huduma za mawasiliano nchini.

  0 0

  pombe
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
  ………………………………………………
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemalizia kujaza nafasi za uteuzi wa Mawaziri na Naibu Waziri alizobakiza wakati akitangaza baraza la Mawaziri la kwanza katika awamu ya tano ya utawala wake.
  Uteuzi huo ni kama ifuatavyo;
  1. Profesa Jumanne Maghembe – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.
  2. Dkt. Philip Mpango – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango (Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge).
  3. Mhandisi Gerson Lwenge – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji.
  4. Dkt. Joyce Ndalichako – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi. (Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge)
  5. Mheshimiwa Hamad Masauni – Ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
  6. Prof. Makame Mbarawa – Amehamishwa kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kwenda Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano
  Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewatakia heri watanzania wote katika Sikukuu za Maulid, Christmas na Mwaka Mpya na kuwataka washerehekee kwa amani na utulivu. 
  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

  23 Desemba, 2015

  0 0  0 0

   Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Katibu Msaidizi Mkoa wa Magharibi Kichama Zanzibar Suleiman Mzee (CHARAS) alipowasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Karume Zanzibar leo Disemba 24,2015 kwa ajili ya kuhudhuria  Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W).
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Makamu wa Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipowasili nyumbani kwake Migombani Zanzibar leo Disemba 24,2015 kwa ajili ya kuhudhuria Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) yanayofanyika kila mwaka.
  Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal katikati, akisalimiana na kumfahamisha wake zake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kushoto alipowasili nyumbani kwake Migombani Zanzibar leo Disemba 24,2015 kwa ajili ya kuhudhuria  Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) yanayofanyika kila mwaka. Picha na OMR

  0 0

  SIMU.TV:  Wananchi wameaswa kuwa waadilifu kipindi hiki cha sikukuu na kudumisha sala kila siku badala ya kusali siku za sikukuu pekee; https://youtu.be/yb5nfF5p1Lw
   SIMU.TV:  Wadau wa soka wasema kufungiwa kwa viongozi wa FIFA Blatter na Plattini hakutaathiri misaada ya michezo kwa nchi za Afrika; https://youtu.be/YxTar3tzgBM
   SIMU.TV:  Rais Magufuli ametoa misaada ya vyakula katika vituo vya watoto yatima na watoto wenye ulemavu mkoani Kagera; https://youtu.be/MFtmYmoPWgs
   SIMU.TV:  Uwepo wa changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa mashabiki na imani potofu miongoni mwa wazazi vyaeleza kusababisha kudorora kwa kandanda upande wa wanawake; https://youtu.be/glJKgy2riiY
   SIMU.TV:  Wakulima wa kujitegemea wa tumbaku waitaka serikali kuingilia kati uamuzi wa bodi ya tumbaku kuwafuta wakulima binafsi katika bodi na kuwataka wakulima hao kufanya ushirika;https://youtu.be/H4HdmVVmsKw
   SIMU.TV:  Katibu wa hospitali Zanzibar alaani wizi wa vitendeakazi katika vituo vya tiba na kueleza kuwa vitendo hivyo vinarudisha nyuma maendelea ya huduma katika hospitali; https://youtu.be/CYIFhWdCpuA
   SIMU.TV:  Chama cha wafugaji kanda ya ziwa kimeitaka serikali kuwaingiza wafugaji kwenye bajeti ili kukuza uchumi wa taifa;  https://youtu.be/-Se09D-zoSE  
   SIMU.TV:  Wazazi wametakiwa kutatua tofauti zao ili kupunguza ongezeko la watoto wa mitaani; https://youtu.be/7cib6LRMQ9o
   SIMU.TV:  Hali ya usafiri yazidi kuwa tete katika kituo cha usafirishaji Ubungo hali inayosababisha abiria kupata usumbufu; https://youtu.be/O4Q7IoqGpbA

  0 0

   Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika ya Kusini,Rebecca Malope akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa JNIA jioni hii tayari kwa ajili ya kutumbuiza kaika tamasha la Krismass litakalofanyika ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam kesho likishirikisha waimbaji mbalimbali wakiwemo wa nchini Tanzania kama vile Rose Muhando, Upendo Nkone, Joshua Mlelwa na wengine wengi , kushoto katika picha anayefurahia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion iliyoandaa na kumleta mwimbaji huyo  Bw. Alex Msama.
    Rebecca Malope akiwasalimia baadhi ya mashabiki wake (hawapo pichani) waliokuja kumlaki mara baada ya kuwasilia uwanja wa ndege wa JNIA jioni hii tayari kwa ajili ya kutumbuiza tamasha la Krismass litakalofanyika ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam kesho
   Marope akikaribishwa kwa upendo na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Msama Promotions.
   Rebecca Malope Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika ya Kusini akizungumza na mratibu wa tamasha hilo Bw. Hadson Kamoga mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa JNIA jijini Dar es salaam.
  Rebecca Malope Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika ya Kusini akisisitiza jambo huku akitabasamu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa JNIA.
   Rebecca Malope Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika ya Kusini akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili nchini kwenye uwanja wa ndege wa JNIA jijini Dar es salaam, waliosimama nyuma Bw. Alex Msama na mmoja wa waratibu wa tamasha hilo Hadson Kamoga.


older | 1 | .... | 1066 | 1067 | (Page 1068) | 1069 | 1070 | .... | 3286 | newer