Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110137 articles
Browse latest View live

RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA PILI MZEE ALI HASSAN MWINYI AFAFANUA KAULI YAKE KUHUSU KUCHINJA


DEATH ANNOUNCEMENT

$
0
0
 
The late William Vedastus Mugurusi

Majadiliano kuhusu uchumi wa Tanzania na Gesi na Benki ya dunia na IMF

$
0
0
 Kutoka kushoto Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. A. Mgimwa, Mkurugenzi Mkuu wa Africa Group (IMF) Bw. Momodou Bamba Saho pamoja na Naibu Katibu Mkuu Dr. S. Likwelile wakifurahia jambo baada ya kikao cha kujadili masuala ya hali ya uchumi wa Tanzania pamoja na gesi.
 Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. A. Mgimwa akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Africa Group (IMF) Bw. Momodou Bamba Saho mara baada ya kumaliza majadiliano.
 Ujumbe kutoka Tanzania katika kikao cha pamoja na Mwakilishi Mkazi wa World Bank Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier katika majadiliano kabla ya kukutana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Bw…..
Kutoka kushoto ni Mshauri wa Mkurugenzi wa Afica Group One Bw. Wilson Toninga Banda, Mkurugenzi Mkuu wa Africa Group One Bw. Denny H. Kalyalya pamoja na Mkurugenzi Mwandamizi  wa Africa Group One  Bw. Peter Larose wakiwa katika majadiliano na ujumbe wa Tanzania  ukiongozwa na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt A. Mgimwa.

SERENGETI FREIGHT FORWARDERS LTD WAZEE WA KAZI

$
0
0

GOOD NEWS FOR KENYA
AIR CARGO TO NAIROBI 
£2.80 per KILO! INCLUSIVE CLEARANCE
ONCE YOU PAY HERE IN UK YOU DONT PAY ANYTHING IN KENYA
UKIISHA LIPA UK UNAKWENDA TU KENDA HOUSE
TOM MBOYA STREET NAIROBI
FLIGHTS EVERY WEEK
AIR CARO TO DAR £1.80 PER KILO EXCLUSIVE CLEARANCE
WE COLLECT FROM ANY ADDRESS IN UK FROM £40 
MINIMUM WEIGHT IS 35KG
KAMA UNATAKA KUTUMA DOCUMENTS KWA DHL 
TUNAKUJA  KUCHUKUA NYUMBANI KWAKO ANYWHERE IN UK BURE NA KUTUMA NI £30 KWENDA TZ

  CONTAINER PRICE CUT!
40'HC TO DAR/MOMBASA NOW £1,950
20' CONTAINER TO DAR/MOMBASA £1,350
THIS IS MORE THAN £300 DISCOUNT!
THIS IS FOR MAERSK LINE, CMA-CGM, WEC LINE NA SAFMARINE

TUNAHITAJI MTU MWENYE UZOEFU WA KUFANYA CUSTOMS ENTRY FOR EXPORT
MSHAHARA NI £11.50 KWA SAA

Mkurugenzi wa Asia na Australasia akutana kwa mazungumzo na Balozi wa China hapa nchini

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki akiongea na Mhe. Lv Youqing, Balozi wa China hapa nchini masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na China ikiwa ni pamoja na matarajio ya nchi hizi mbili baada ya ziara ya Rais wa China, Xi Jinping aliyoifanya hapa nchini mwezi Machi, 2013.
Balozi wa China hapa nchini Lv Youqing akifafanua jambo kwa Balozi Kairuki wakati wa mazungumzo yao.
Balozi Kairuki na Balozi Lv Youqing wakiendelea na mazungumzo huku wajumbe waliofuatana nao wakisikiliza. Kulia ni Bw. Medard Ngaiza, Afisa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Asia na Australasia. Wengine ni Bi. Fang Wang, Afisa katika Ubalozi wa China na Bw. Lin Zhiyong (kushoto kwa Bi. Fang), Afisa Mkuu wa Ofisi ya Biashara na Uchumi ya Serikali ya China hapa nchini.

simanzi yatawala msiba wa bi. kidude Zanzibar leo

$
0
0
 MRAJIS wa Baraza la Sanaa Zanzibar (BASAZA), Khadija Batash akizungumza na Waandishi wa Habari muda mfupi baada kutolewa kwa taarifa za kifo cha Msanii mkongwe Nchini, Fatma Bint Baraka ‘Bi Kidude’ nyumbani kwa msanii huyo Rahaleo mjini Zanzibar.
 MTENDAJI wa Busara Promotions, Stela Steven akizungumza na Waandishi wa Habari muda mfupi baada kutolewa kwa taarifa za kifo cha Msanii mkongwe Nchini, Fatma Bint Baraka ‘Bi Kidude’ nyumbani kwa msanii huyo Rahaleo mjini Zanzibar.
 WAANDISHI wa  Habari kutoka vyombo mbali mbali wakiwa kazini katika makaazi ya Msanii Bi Kidude muda mfupi baada ya kufariki kwa msanii huyo.
 WATENDAJI wa Busara Promotins wakijadiliana jambo nje ya nyumba ya msanii Bi Kidude muda mfupi baada ya kufariki.
 MJUKUU wa marehemu Bi Kidude, Bwana Baraka,  akitoa taarifa za mazishi kwa waandishi wa habari nyumbani kwa marehemu Rahaleo mjini Zanzibar.
 WAFIWA wakiwa nyumbani kwa marehemu.
 MKURUGENZI wa Kikundi cha Taarab cha TAUSI, Mariam Hamdani akizungumza na Waandishi wa Habari nyumbani kwa marehemu Bi Kidude.
 Sihaba Ismail mmoja wa watu waliofundishwa kazi za kufunda wari na dawa asilia na Bi Kidude akielezea anavyomfahamu marehemu.
MSANII wa Taarabu asilia, Makame Faki akielezea jinsi Bi Kidude alivyokua akiimudu sanaaa ya taarabu na unyago.
Picha zote na Haroub Hussein wa Globu ya Jamii, Unguja

As Old As My Tongue - a tribute to Bi Kidude

$
0
0
Bi Kidude was a living legend on her home island of Zanzibar, and has beguiled audiences around the world on her wide and varied travels. A ... all » favourite of sultans, presidents, and sailors, her story is remarkable, challenging our perception of age (she's ninety three, going on sixteen), and of women in a Muslim society. 
To see her up close in her humble home then out on the town, smoking and flirting is a unique experience. As Old As My Tongue has been filmed over the last three years in Zanzibar and on tour with Bi Kidude. More than a biography, it is an insight into the politics and personalities of Zanzibar's spicy contemporary society. 
The soundtrack features a specially commissioned soundscape by co-producer Rita Ray and featuring a hundred years of classical Indian Ocean vibes. (Find the film at www.screenstation.net or check out http://www.busaramusic.com/)

Globu ya jamii yamlilia Bi Kidude

$
0
0
 Globu ya Jamii imepokea kwa mshituko mkubwa na simanzi taarifa kuwa Bi Kidude katutoka. Tunatoa salaam za rambirambi kwa watu wote wa Zanzibar pamoja na wa Bara waliomuenzi msanii huyu ambaye pamoja na umri wake mkubwa aliendelea kutuliwaza kwa usanii wake jukwaani pamoja na matani na ucheshi usio kikomo nje ya jukwaa. Kuna wachache wa aina yake Wallahi..
Akiwa ni mmoja wa wasanii nguli Bara na Visiwani, Bi Kidude alikuwa karibu sana na Globu ya Jamii kiasi ya kwamba pamoja na umri wake mkubwa, mara kadhaa alikuwa anatutia moyo wa kuendeleza libeneke kwa namna ambayo haitoweza kusahaulika. 
Alikuwa mtu wa karibu sana na Ankal, ambaye hata katika hali yake ya kudhoofu kutokana na umri na maradhi hakukosa kumtambua na kumtania. Ankal ni mmoja wa wanaLibeneke wachache ambao Bi Kidude aliwakubalia kupozi kupigwa picha nao.
Ni kweli kwamba kila mtu ataonja mauti, lakini si uwongo kwamba kuondokewa na kipenzi chetu Bi Kidude ni pigo kubwa kwa Globu ya Jamii kama ilivyo kwa jamii yote ya tasnia ya sanaa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
MOLA AIWEKA MAHALA PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU BI KIDUDE
AMEN 
Picha ambayo Bi Kidude alimruhusu Ankal kumpiga
kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Mambo ya pamba moto Redd's Miss Kibaha

$
0
0
 Baadhi ya Warembo wa Redd's Miss Kibaha 2013 wakiwa kwenye picha ya pamoja muda mfipi kabla ya kuanza kwa mazoezi katika kambi yao ilipo kwenye hoteli ya Grand Villa,Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

News UPDATES: Massive Explosion At Texas Fertilizer Plant

ROADSHOW PILI YA KUTANGAZA UTALII WA TANZANIA YAENDELEA KATIKA JIJI LA SHANGHAI CHINA

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Utalii Ibrahimu Mussa (kulia) akihojiwa na mwanahabari jijini Shanghai wakati wa roadshow iliyofanyika jijini hapo kutangaza utalii wa Tanzania. Katikakti ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Nuru Millao.
Maafisa kutoka Tanzania (kutoka kushoto) Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Dk. Aloyce Nzuki; Meneja Sheria wa Mamlaka ya Ngorongoro Egidius Mweyunge; Meneja Huduma za Utalii wa TANAPA Johnsone Manase na Mkurugenzi wa Idara ya Utalii Ibrahimu Mussa wakiwa katika roadshow hiyo jijini Shanghai.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Nuru Millao akifungua roadshow jijini Shanghai.
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Dk. Aloyce Nzuki akiwasilisha mada kuhusu Utalii wa Tanzania kwa wakazi wa Shanghai China.
Baada ya uwasilishaji wa mada Watanzania hawa walijumuika kuimba pamoja wimbo wa TANZANIA YETU NCHI YENYE FURAHA mbele ya halaiki ya wakazi wa Shanghai China.
Mkurugenzi wa Idara ya Utalii Ibrahimu Mussa akiongea katika roadshow hiyo.
Meneja Huduma za Sheria Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Egidius Mweyunge akielezea fursa za uwekezaji zilizopo katika mamlaka hiyo.
Meneja Huduma za Utalii wa TANAPA Johnsone Manase akielezea fursa za uwekezaji zilizopo katika Hifadhi za Taifa.
Sehemu ya wakazi wa Shanghai wakifuatilia mada katika roadshow hiyo.

BASATA YAMLILIA BI KIDUDE

$
0
0

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa msanii nguli wa tasnia ya muziki wa taarab nchini Bi Kidude.
Baraza limestushwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa ya kifo hiki cha Bi Kidude ambaye mchango wake katika muziki wa taraab ni mkubwa mno na  unahitajika sana, pengo aliloliacha ni kubwa kwani ubunifu wake bado unahitajika katika tasnia hii.
Baraza linatoa pole kwa familia ya marehemu na wasanii wote nchini, aidha tunawatakia moyo wa subira katika wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na mpendwa wetu.
Mwenyezi Mungu aipumzishe mahala pema peponi roho ya marehemu. Baraza liko pamoja na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Imetolewa na

Godfrey Mngereza

Kaimu Katibu Mtendaji

Baraza la Sanaa la taifa.



NGUMI KUPIGWA CHALINZE

$
0
0

Mabondia Mwaite Juma Cosmas Kibuga na Shabani Kaoneka ni baadhi ya mabondia wa Dar es salaam watakaokwenda Chalinze mkoa wa Pwani kuhamasisha ngumi za kulipwa wilayani humo kwa kuzipiga na mabondia wakali wa huko.
Kampuni inayoandaa mapambano kwa ajili ya kunyanyua vipaji vya mabondia machipukizi ya Bigright Promotion, imaeandaa pambano hilo ili kutanua wigo wa michezo nchini kwa kuanzia kutembelea wilaya zinazohamasika kimchezo ikiwemo chalinze.
Tumeamua kufanya chalinze kwa sababu tunataka chalinze iwe ndio mfano kwa kuandaa pambano hili ambalo litawakutanisha chipukizi wakali wa dar na wakali wa chalinze,pia kutakuwepo na mapambano mengine yenye ushindani wa hali ya juu na vituko kama vile la Pius Puto atakaezipiga na iddi mkatatiketi -hawa ni mbabe wa sokoni na mbabe wa stendi watazipiga kumaliza ubishi wao uliotanda kwa muda mrefu. ukiondoa pambano hilo Minyusi abdala atazipiga na shaban kaoneka, Baraka nuhu"chalinze hamjambo" atazipiga na goodluck suleiman, alex kdo atazipiga na herman shekivuli, iddi mwera atazipiga na ramadhan misugwa na mapambano mengineyo mengi likiwemo la ustadh mwenye msimamo mkali ustadh Kurasheni aliyeahidi kuchinja kama anachinja kondoo ulingoni atakaezipiga na makali wa bodaboda mzee kachacha.mgeni rasmi wa pambano hilo atakuwa ni diwani wa  Chalinze bwilingu bw naser Karama ambaye muda wote amekuwa mstari wa mbele kuhamasisha vijana kushiriki michezo na ametoa basi kubwa kwa ajili ya mashabikitoka daresslaam kwenda kushangilia na kurudi.
wakati huohuo diwani Karama anategemea kujenga ukumbi mkubwa wangumi hapo chalinze, hivyo ngumi zote za kimataifa zitakuwa zikipigwa hapo
 

Tanzania launches One Health initiative to curb communicable diseases

$
0
0
 Tanzania’s Vice President Dr Mohammed Gharib Bilal (left) unveils a pull up banner to symbolize the launch of One Health in Tanzania initiative which will pull together health institutions to work together towards identifying, preventing and eradicating communicable diseases in Tanzania. Right is One Health Central and Eastern Africa (OHCEA) Country Focal Person Prof Japhet Kilewo. The launch was done in Arusha on Tuesday. Note: One Health in  Tanzania is (Afya Moja Tanzania) 
========  =======    ========    =======

Health institutions in Tanzania has pulled together to form a one health network which would harmonize activities done by these institutions which aims at minimising duplication of efforts to fight communicable diseases.

The network launched on Tuesday by Tanzania’s Vice President Dr Mohammed Gharib Bilal in Arusha, will see three institutions - the National Institute for Medical Research (NIMR), Southern African Centre for Infectious Diseases Surveillance (SACIDS) and One Health Central and Eastern Africa (OHCEA)- working together to identify, prevent and eradicate communicable diseases in Tanzania.

Speaking during the opening of the 27th Annual Joint Scientific Conference of the National Institute for Medical Research (NIMR) and the 2nd One Health Conference in Africa which is jointly organized by NIMR, SACIDS and OHCEA, Dr Bilal said the Government will continue to support all national, regional and international commitments for surveillance, risk management and control of communicable diseases.

He said that the fact that NIMR has joined forces with the SACIDS and OHCEA to hold the largest gathering that has brought human health and animal health experts under one roof to discuss measures on how to control the pandemic is a good start of partnership which will transform Tanzania’s health sector landscape.

The conference goes with the theme, “Changing Landscape in Health Research in Africa.” According to Dr Bilal, the theme is timely, considering that the government is preparing to implement its 4th National Health Research Priorities. “Tanzania, like many other Sub-Saharan Africa countries is challenged by a number of emerging and re-emerging communicable diseases,” he said and added, “I am glad to learn that one of the sub-themes of this conference is addressing “One Health in Africa.”

Elaborating on the One Health in Tanzania initiative, OHCEA Country Focal Person Prof Japhet Kilewo said the network will see several one health networks in Tanzania which share the common mission of driving transformational change for improvement and wellbeing of humans, animals and the ecosystem through multidisciplinary research, training and community service, working together.

“These bodies have recently met and charted out a way forward including the formation of a ONE HEALTH FORUM that would harmonize the activities of these networks so that duplication of efforts is minimized.

“Experience with the AIDS epidemic indicates that we have lost many opportunities which would have enabled us to investigate and limit the spill over of agents of disease from animals to humans. We should therefore not allow other epidemics to take us by surprise like HIV/AIDS,” he said.
Prof Kilewo mentioned that in order to do that healthcare institutions must be prepared to identify potential human disease agents which reside in animals (both wild and domestic).  They must also prepare to prevent these disease agents from spilling over to humans but when they cause overt disease in humans we must be prepared to control and/or treat it.

Elaborating National Health Priorities (2013-2020) initiative, the Director General of NIMR, Dr Mwele Malecela said that the priorities which are set every five years allow them to re-examine what the key areas for research should be.“This is done in collaboration with several stakeholders and most prominently Tanzaia Health Research forum, Dr Mwele said and added that this is the fourth set of priorities set in since 1999.”
About SACIDS Regional Strategic Plan focusing this year to 2020, the SACIDS Executive Director, Prof Mark Rweyemamu said they set about developing the capabilities of young African scientists and catalyzing institutional change of mindset.Prof Rweyemamu said, in this initiative they have introduced the concept of a community of practice for research themes.
In the current five years, he said they have focused on five specific diseases themes, namely Ebola, Rift Valley Fever, Tuberculosis, Plague and Foot-and-Mouth disease.
“We have targeted the poor communities, especially in the areas of contact between people livestock and wildlife,” Prof Rweyemamu said.

Kinana awahimiza wakazi wa Gairo kuwa na moyo wa kufanya kazi kwa kujitegemea.

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdurahman Kinana akizungumza na wakazi wa kata ya Chakwale,wilaya ya Gairo mapema leo mchana,alipokuwa akizindua shina jipya la wakereketwa wa chama hicho.katika uzinduzi huo Kinana aliwaasa  na kuwahimiza wakazi wa eneo hilo kuwa na moyo wa kufanya kazi kwa kijitegemea badala ya kusubiri serikali iwafanyie kila kitu ikiwemo na suala la kuwapa ajira.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdurahman Kinana akiwapa kifuta jasho baadhi ya wazee-waasisi wa chama cha CCM,kabla ya kufanyika kwa uzinduzi wa shina jipya la kata yao ya Chakwale,Wilaya ya Gairo mapema leo mchana.Ndugu Kinana na Ujumbe wake wa CCM wako ndani ya Wilaya ya Gairo katika ziara ya kuimarisha chama cha CCM mkoani Morogoro sambamba na kuangalia shughuli mbalimbali za maendeleo.
Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi-CCM,Nape Nnauye akizungumza jambo mbele ya wakazi wa Chakwale mara baada ya shina la kata hiyo kuzinduliwa mapema leo mchana,ndani ya wilaya ya Gairo.
Baadhi ya Wazee waasisi ndani ya CCM-Kata ya Chakwale wakionesha kadi zao za chama cha CCM walizonazo tangu kuanzishwa kwa chama hicho,kwenye shughuli fupi ya kuzindua shina la kata hiyo.
Kijana aliyekuwa Mwanachama wa CHADEMA akiwa ameinyanyua kadi ya chama chake cha awali,na kukabidhiwa kadi ya chama cha CCM,akiwa mmoja wa wanachama wapya waliojiunga na chama hicho cha CCM.
Baadhi ya Vijana wakiwa kwenye ajira ya kujitegemea,kama waonekanavyo pichani wakitumia mashine aina ya Trekta kupukuchua mahindi.PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

JAMII YAFAIDIKA NA MAFAO YA NSSF

$
0
0
 Ofisa Uhusiano Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Maife Kapinga akifafanua jambo kuhusu huduma ya mafao ya matibabu wakati wa maonesho ya Huduma za Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam jana.
Ofisa wa Matibabu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Yasinta Shibola akitoa ufafanuzi kwa watu mbambali waliotembelea banda la NSSF wakati wa maonesho ya Huduma za Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam leo ambapo NSSF ni moja ya taasisi zinazoshiriki katika maonesho hayo. 
 Baadhi ya watu waliojitokeza katika banda la NSSF wakipata maelezo ya huduma mbalimbali za NSSF.

Na Mwandishi Wetu

WATANZANIA wametakiwa kujiunga na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), ili kufaidika na huduma za bure katika mafao yanayotolewa na shirika hilo.

Wito huo umetolewa leo na Ofisa wa matibabu wa NSSF, Yasinta Shibola, jijini Dar es salaam katika maonesho ya siku tatu ya Muhimbili kutimiza miaka 13 toka kupandishwa hadhi ya kuwa hospitali ya Taifa tangu mwaka 2000.


Shibola alisema kuwa NSSF hawatoi mafao ya kustaafu pekee bali wana mafao mengine ambayo hutolewa bure kwa mwanachama aliyejiunga na mfuko huo.


“Mafao yetu yamejikita kusaidia wateja wa sekta binafsi na wa serikali, lakini pia hata wale wanaofanya kazi kwa kujitegemea kama atakuwa mwanachama wetu atapatiwa fao hilo kama wengine tena katika hospitali atakayochagua yeye mwenyewe katika zile ambazo tumeingia nazo mkataba na kupewa fao hilo kama wengine wote, hakuna upendeleo hapo,”alisema


Naye Ofisa habari wa NSSF, Maife Kapinga, alisema kuwa fao la matibabu (SHIB) ni bure na linahudumia watu wanne katika familia moja.

Aidha alisema kuwa maonesho hayo yamekata kiu ya wafanyakazi wa Muhimbili pamoja na wagonjwa kwani wengi walikuwa hawana elimu ya namna shirika hilo linavyofanya kazi japo ni wanachama.


Kapinga alitoa wito kwa watanzania kujiunga na shirika hilo ili wafaidike na mafao yanatolewa bure.

UDHALILISHAJI WANAWAKE KIJINSIA UNAENDELEA KAMA MBINU YA KIVITA

$
0
0
Pichani na sehemu ya raia wakiwamo wanawake, watoto na wanaume wakikimbia machafuko katika eneo la Mashariki ya Kongo, siku ya Jumatano, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, lilikuwa na majadiliano ya siku nzima kuhusu ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama. Katika Majadiliano hayo, ilidhihirisha wazi kwamba licha ya juhudi mbalimbali ambazo zimekuwa zikichukuliwa na Jumuiya ya Kimataifa katika kupigania na kutetea haki na usalama wa wanawake katika maeneo yenye vita, bado wanawake, watoto na hata wanaume, wanaendelea kudhurumiwa utu na hadhi yao kwa kufanyiwa ukatili mkubwa ikiwa ni pamoja na kubakwa, mbinu inayoendelea kutumiwa kama mbinu ya kivita. Ukatolewa wito wakati wa majadiliano hayo wa kuendelea kuwachukulia hatua za kisheria wale wote wanaobainika kuhusika na ukatili huo ikiwa ni pamoja na kutafuta namna ya kuwafidia waliodhulumiwa utu wao.

RAIS KIKWETE AONGOZA MAMIA KWENYE MAZISHI YA BI. KIDUDE UNGUJA LEO

$
0
0
jeneza lenye mwili wa Msanii Mkongwe wa Muziki wa Mwambao (taarab) hapa nchini,Marehemu Fatma Bint Baraka (Bi Kidude) likitolewa katika msikiti wa Mwembeshauri aliposaliwa mchana wa leo,tayari kwa kwenda kwenye Mazishi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania , Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Msanii mkongwe wa Taarab Tanzania, Fatma Baraka (Bi Kidude) katika makaburi ya Kitumba Wilaya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akiweka udongo katika kaburi la Msanii mkongwe wa Taarab Tanzania, Fatma Baraka (Bi Kidude) katika makaburi ya Kitumba Wilaya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif akiweka udongo katika kaburi la Msanii mkongwe wa Taarab Tanzania, Fatma Baraka (Bi Kidude) katika makaburi ya Kitumba Wilaya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said sadiq akiweka udongo katika kaburi la Msanii mkongwe wa Taarab Tanzania, Fatma Baraka (Bi Kidude) katika makaburi ya Kitumba Wilaya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akiweka udongo katika kaburi la Msanii mkongwe wa Taarab Tanzania, Fatma Baraka (Bi Kidude) katika makaburi ya Kitumba Wilaya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Nasibu Abdul Juma (Diamond) akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya Msanii mkongwe wa Taarab Tanzania, Fatma Baraka (Bi Kidude) katika makaburi ya Kitumba Wilaya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Taratibu za Mazishi zikiendelea.

Vodacom yazindua maduka mawili mapya jijini dar

$
0
0
Ofisa Mkuu wa Usambazaji na mauzo wa Vodacom Tanzania, Hassan Salleh, akitoa huduma kwa wateja waliofika wakati wa uzinduzi wa duka jipya la huduma kwa wateja lililoko katika mtaa wa India Posta jijini Dar es Salam, Vodacom imezindua maduka mawili yanayotarajiwa kupunguza msongamano katika maduka mengine ya kampuni hiyo.
Ofisa Mkuu wa Usambazaji na mauzo wa Vodacom Tanzania, Hassan Salleh, akimkabidhi funguo, Meneja Miradiwa Vodacom Tanzania, Sharon Rwekola, mara baada ya kuzinduliwa kwa duka jipya la kampuni hiyo lililoko mtaa wa India posta jijini dar es Salaam, Maduka hayo yanatarajiwa kupunguza msongamano kwa wateja wa kampuni hiyo.
Ofisa Mkuu wa Usambazaji na mauzo wa Vodacom Tanzania, Hassan Salleh, akitoa huduma kwa wateja waliofika wakati wa uzinduzi wa duka jipya la huduma kwa wateja lililoko katika makutano ya barabara ya morogoro Posta jijini Dar es Salam, Vodacom imezindua maduka mawili yanayotarajiwa kupunguza msongamano katika maduka mengine ya kampuni hiyo.
Meneja wa Duka la Vodacom lililoko mtaa wa Morogoro Posta Jijini Dar es Salaam, Sayed Shadab, mapema baada ya uzinduzi wa duka hilo, anayeshuhudia ni Ofisa Mkuu wa Usambazaji na mauzo wa Vodacom Tanzania, Hassan Salleh, Vodacom imezindua maduka mawili yanayotarajiwa kupunguza msongamano katika maduka mengine ya kampuni hiyo.
Meneja wa Duka la Vodacom lililoko mtaa wa Morogoro Posta Jijini Dar es Salaam, Sayed Shadab, mapema baada ya uzinduzi wa duka hilo, anayeshuhudia ni Ofisa Mkuu wa Usambazaji na mauzo wa Vodacom Tanzania, Hassan Salleh, Vodacom imezindua maduka mawili yanayotarajiwa kupunguza msongamano katika maduka mengine ya kampuni hiyo.

HUKUMU YA PONDA YAAHIRISHWA HADI MEI 9

$
0
0
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda (kulia) akiwa na mshtakiwa mwenzake Saleh Mkadamu wakielekea  kupanda basi la magereza baada ya hukumu ya kesi yao ya uchochezi kuahirishwa hadi Mei 9. Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49 wanakabiriwa na makosa matano ya kula njama na kuingia kwa jinai katika uwanja namba 311/3/4 kitalu T uliopo Markaz Chang'ombe na wizi wa vifaa mbalimbali vya ujenzi vyenye thamani ya Shs milioni 59 mali ya kampuni ya Agritanza.
 Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda akipanda basi la magereza.
 Askari wakiimarisha ulinzi nje ya Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Wafuasi wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda wakiwa wamekusanyika nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo wakati hukumu ya kesi yake ilipoahirishwa leo.
Viewing all 110137 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>