Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1057 | 1058 | (Page 1059) | 1060 | 1061 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Habari na picha na Ismail Ngayonga - MAELEZO
  SERIKALI imewataka watumishi wa sekta ya afya nchini kutofanya kazi kwa mazoea na badala yake kufanya kazi kwa bidii na uadilifu ili kufikia malengo yaliyowekwa. Hatua hiyo inaelezwa itasiaidia kurahisisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi kwa kutoa huduma bora na zinazofikiwa kwa wakati. 
  Akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema kila mtumishi wa umma anapaswa kutekeleza kwa bidii ilani ya Chama Tawala ya mwaka 2015. 
  “Sekta ya Afya imeingizwa kwenye mpango wa Tekeleza kwa Matokeo makubwa sasa, ili tuyakifia matokeo makubwa sasa pamoja na mambo mengine tunahitaji kubadilika sana katika utendaji wetu wa kazi” alisema Mwalimu. 
   Aidha Waziri huyo alisema alisema pamoja na mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa katika sekta ya afya, Wizara hiyo hiyo hiyo haina budi kuakabiliana na chyangamoto mbalimbali zinazojitokeza ikiwemo vifo vya akina mama wajawazito wakati wa kujifungua. 
  Kwa mujibu wa Waziri Mwalimu aliwataka watumishi wa Wizara hiyo kutekeleza kwa vitendo maagizo yaliyotolewa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika hotuba yake ya kuzindua Bunge la 11, kwani hotuba yake ni dira ya maelekezo rasmi ya masuala muhimu yanayopaswa kutekelezwa na kusimamiwa katika kipindi cha miaka mitano. 
   Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donald Mmbando alisema katika kutekeleza mpango wa tekeleza kwa matokeo makubwa sasa, Serikali imeanisha maeneo 4 ya utekelezaji ili kuboresha huduma bora za afya kwa wanachi. 
  Dkt. Mmbando alianisha maeneo hayo kuwa ni pamoja mgawanyo wa watumishi wa kada ya afya, upatikanaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi, ubora wa huduma pamoja na kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto. 
  “Katika kutekeleza haya, wiki ijayo tutazindua mpango mkakati wa miaka 5 wa sekta ya afya (2016-20), ambapo tutahakikisha kuwa yote yaliyoanishwa katika Ilani ya Chama Tawala tunaweza kuyafikia na kuyatekeleza” alisema Dkt. Mmbando
   Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (aliyesimama) akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo (15.12.2015) Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donald Mmbando na wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Hamis Kigwangalla.

   Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (aliyesimama) akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo (15.12.2015) Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donald Mmbando na kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Hamis Kigwangalla.

   Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo (15.12.2015) Jijini Dar es Salaam.

  1.    Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa nne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii mara baada ya kulifungua Baraza hilo leo (15.12.2015) Jijini Dar es Salaam. Wengine  pichani ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Hamis Kigwangalla (wa tano kutoka kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donald Mmbando.   

  0 0

  wanafunzi waliosoma zamani shule za St Joseph's Convent School na Forodhani Secondary School (St Josephs and Forodhani ALUMNI) washerehekea tarehe12 December kwa kuwapelekea wagonjwa 360 wa kansa hospitali za Ocean Road na Muhimbili sabuni za kufulia na kuogea, miswaki na dawa za kusafishia meno. Mkuu wa msafara Collins Rutenge, amesema tarehe 9 Disemba walikuwa wakifanya usafi kila mmoja alipo. 
   Kama kukindi waliamua kupeleka vifaa vya usafi kwa wagonjwa wa kansa waliolazwa hospitali za Ocean Road na Muhimbili ili na wao wapate vifaa vya kufanyia usafi wa mwili.
  Ndani ya kituo. Tuna kutana na Mlezi Eunice (aliopiga goti)  na kutupokea vizuri
  Wanafunzi waliosoma St Joseph Convent School na Forodhani Secondary School kwa mara nyingine tena wamejitolea kwa kuadhimisha siku ya UHURU kwa kupeleka sabuni za kuoga na za kufulia, miswaki na dawa za kusafishia meno kwa wangonjwa 300 waliolazwa katika Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es es Salaam .  Hapa ni kikundi kiliofika hospitalini kwa niaba ya 

  Kiongozi wa msafara ( kushoto)  amesema wameitikia wito wa Rais Magufuli ya USAFI kwa hivyo wameleta sabuni za kuogea na za kufulia miswaki na dawa za kusafishia meno.


  0 0


  Mkurugenzi wa Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, (UNCDF) nchini Tanzania, Peter Malika akizungumza na wageni waalikwa wakati wa makabidhiano ya misaada kwa miradi ya maendeleo iliyodhaminiwa na UNCDF Tanzania.
  Naibu Katibu Mkuu Tamisemi, Kagyabukama E.Kiliba akisoma hotuba yake wakati wa kukabidhi hundi kwa mashirika binafsi na ya umma kwa ajili ya kuendeleza miradi ya maendeleo.
  Naibu Katibu Mkuu Tamisemi, Kagyabukama E.Kiliba (katikati) akimkabidhi hundi bilioni moja na milioni sabini (1,070,000,000) Mkurugenzi wa Mji wa Kibaha, Bi. Jennifa C. Omolo (kulia) na kushoto ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, (UNCDF) nchini Tanzania, Peter Malika.DSC_0211
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, Bw. Jeshi Godfrey Lupembe (kushoto) akikabidhiwa hundi ya shilingi milioni mia tano na tisa (509,000,000/=) na Naibu Katibu Mkuu Tamisemi, Kagyabukama E.Kiliba (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, (UNCDF) nchini Tanzania, Peter Malika.
  Naibu Katibu Mkuu Tamisemi, Kagyabukama E.Kiliba pamoja na Mkurugenzi wa Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, (UNCDF) nchini Tanzania, Peter Malika wakiwakabidhi masisita hundi ya milioni miamoja na saba (107,000,000/=) wa kwanza kulia ni Msimamizi wa Mradi wa Umeme wa Lupali, Sister Imakulata Mlowe na Sister Helga Silinu ambaye ni fundi umeme katika mradi wa Lupali. 
  Habari na picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0  0 0


  Mshitakiwa namba moja katika kesi ya kuhujumu uchumi, aliyekuwa Naibu Kamishna wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), Tiagi Masamaki (Kulia) akiwa na wenzake aliyekuwa Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja, Habibu Mponezya na Bulton Mponezya wakiwa katika Mahakama Kuu Tanzania jijini Dar es Salaam leo wakisomewa shtaka linalowakikabili  la makosa ya jinai na uhujumu uchumi.

  Watuhumiwa watatu wa uhujumu uchumi wakisindikizwa na Polisi wakitoka mahama kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kupewa dhamana. Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

  0 0


  The Attorney General of the United Republic of Tanzania, Mr George Masaju (pictured right) has today seriously advised lawyers to refrain from practicing as private advocates while still serving in public service as such actions can attract very strong disciplinary measures to be taken against the relevant lawyer.  
  The AG made this remark when addressing the 144 newly admitted advocates to the Bar in Dar es Salaam, at an event held at Karimjee grounds today.  This is because such practices are against the rules and regulations that govern the legal profession.  The AG has otherwise advised lawyers to choose between practicing as a private advocate, in which case, the sky will be the limit for them or choosing to practice and render legal services to the public service institutions in order to avoid any conflict of interest.

  As the Attorney General of the United Republic of Tanzania, and head of the Bar, Mr Masaju has pointed out that public access to justice, is one of his  top priorities and that it continues to be the focus of the Attorney General`s Chambers. 
  He therefore urged d lawyers to must always remember that, as they are privileged to be lawyers and advocates, there are many others in our society who are less privileged than they are, and have no access to legal services, because of ignorance or poverty.  
  In regard he reminded lawyers that they have a moral obligation to assist the poor when they seek justice in the course of their career, since we are all potential victims of poverty or ignorance and that we cannot choose our fate. Therefore lawyers have significant role to play in promoting access to justice for all, through legal aid, pro bono work, and the like.

  “So please, consider the poor and you will always be blessed accordingly by the Lord”. Noted the AG.

  On a different note, the AG has strongly encouraged all of the newly admitted lawyers, and who shall proceed as private advocates, to be ready and willing to work in any part of the country, as ways to consider in creating self employment. He further noted that self employment is one of the priorities of the Government that lawyers should be ready to open up Law Firms and offices in both urban and rural areas rather than concentrating in big cities alone. That is how, they will be able to take their services closer to the people and make themselves more viable, and being prepared to lead their destiny, as well. 
  Mr. Masaju has further elaborated what it means to be an advocate and how to be engaged as one, in either private capacity or otherwise where he noted that, “Indeed, after your enrolment to the bar, most of you will start looking for new jobs, especially in the public service. 
  Whether you get to be employed in the public or private sector is entirely your own choice. But for those who are already employed in the public sector or aspire to be employed there, you should make sure that you observe the practising rules and procedures governing advocates who serve in public service institutions”

  In Tanzania, advocates are mainly regulated by the Advocates Act, Cap 341 of the laws of Tanzania, the Tanganyika Law Society Act as well as Rules of Professional Conduct and Etiquette of the Tanganyika Law society. Under the Advocates Act, an advocate is defined as any person whose name is duly entered as an advocate upon the Roll. Once lawyers have been registered in accordance with the law, they are required to discharge their duties in an ethical manner, short of which a complaint can be filed against them under the Act.  

  Mr. Masaju has conclusively urged lawyers not to refrain from further learning, always be students, be disciplined and honest as such self discipline should inform their work, habits and emotions and that in the face of provocation they should observe rules of conduct for lawyers.  
  He further insisted on lawyers adjust to change and be dynamic, and to always remember that we live in the 21stcentury, in a technological world hence be prepared to handle diverse legal matters and emerging issues from not only the surrounding society but also from the technological world of internet and what have you. So everyone should always find ways of being proactive and creative in order to cope with the pace and efficiency typical of the 21st century.
  The AG has thus reminded lawyers that they are committed to the rule of law in a democratic society, where advocates are also committed to an independent Bar and an independent Judiciary as such an independent and vibrant legal profession is also essential for the proper functioning of the administration of justice.


  0 0

  Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande amewataka Mawakili kote nchini kufanya kazi zao kwa kuzingatia weledi na maadili ya taaluma ya Sheria na kwamba wasisite kuwaeleza ukweli wateja wao wanaopeleka mashauri Mahakamani ili kuepuka kupoteza muda na gharama katika masuala yanayoweza kupatiwa ufumbuzi nje ya Mahakama. 
   Akizungumza na Mawakili wapya 104 waliohitimu Shule ya Sheria kwa mwaka 2015 wakati wa hafla ya 53 ya kuwapokea na kuwaapisha iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee leo jijini Dar es salaam amesema kuwa msingi mkubwa wa kazi yao umejengwa katika uzingatiaji wa maadili ya taaluma ya sheria. 
   Amewataka Mawakili hao kubadilika kifikra kwa kuwa Mawakili Bora ili kujenga imani na uaminifu kwa jamii wanayoihudumia na kuongeza kuwa sasa wameingia kwenye utaratibu wa kutambuliwa rasmi na Mahakama ya Tanzania kwa kuwezeshwa kufanya shughuli za uwakili kwenye mahakama ya Tanzania maeneo mbalimbali nchini. 
   “Naomba mtambue kuwa kila Wakili ni Ofisa wa Mahakama hivyo mnao wajibu na jukumu la kusoma, kufuatilia mashauri mbalimbali ili kuwa na uhakika wa kesi mnazosimamia kuliko kuzitegemea Mahakama” 
   Aidha, ameeleza kuwa yapo mambo ambayo yamekua yakifanywa na baadhi ya Mawakili wasio waaminifu yanayochafua sura ya Taaluma ya Sheria ikiwemo kutumia nyaraka za kughushi, kuvunja Kanuni na Maadili ya Taaluma huku baadhi yao wakijikuta wakiingia katika mgogoro na Mamlaka zinazosimamia kitaaluma taaluma hiyo. 
   “Nawataka mzingatie sheria, kanuni na Maadili ya Uwakili, hata hivyo tuna chombo kinachosimamia maadili yenu, wapo takribani 176 waliokiuka maadili na hawa wanashughulikiwa kwa mujibu wa Sheria ili kulinda maadili na utendaji wa taluma yenu” Amesisitiza Mhe. Othman. Amewataka watimize wajibu wao kwanza kwa wananchi watakaouhudumia pamoja na Mahakama ya Tanzania ambayo inawataka kufanya kazi zao kwa kuzingatia Sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa. 
   Mhe. Othman amefafanua kuwa Mahakama ya Tanzania inaendelea na Mkakati wa kupunguza mrundikano wa Kesi Mahakamani kwa kuhakikisha kuwa kesi zote zinazofikishwa Mahakamani zinamalizika katika kipindi cha chini ya mwaka 1 Ameeleza kuwa silimia 47 ya kesi zaidi ya 200 zilizokuwepo Mahakama Kuu katika kipindi cha miaka 4 iliyopita zimeendelea kusisikilizwa kwa ubora na sasa zimebaki asilimia 17 ya kesi hizo jambo linaonyesha kuongezeka kwa ufanisi wa Mahakama. 
   Kwa upande wake Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju akiwakaribisha Mawakili hao katika familia ya sheria Tanzania amesema kuwa katika jamii wanao mchango mkubwa katika kuhakikisha Haki na Usawa vinadumishwa nchini. 
   Amesema mawakili hao kabla ya kuapishwa na kuingizwa kwenye utaratibu wa kutambuliwa kuwa Mawakili wamepitia na kufauru vigezo vya kitaaluma vilivyowekwa ili kulinda heshima ya Taaluma ya sheria nchini. 
   Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande akiongoza maandamano ya Majaji na Watendaji wa Mahakama wakati wa hafla ya 53 ya kuwapokea na kuwaapisha Mawakili wapya 104 iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee leo jijini Dar es salaam.

   Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande akizungumza na Mawakili 104 walioapishwa leo jijini Dar es salaam. Mhe. Chande amewataka Mawakili hao kufanya kazi zao kwa kuzingatia weledi na maadili ya taaluma yao.

   Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande (katikati) akiongoza akiwa na Majaji na Watendaji wa Mahakama wakiendelea na zoezi zoezi la kuwaapisha Mawakili wapya 104 katika viwanja vya Karimjee leo jijini Dar es salaam.

   . Mawakili wakiwa wamesimama mbele ya Jaji Mkuu kabla ya kuapishwa.

  Mawakili walioapishwa wakiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mkuu Mhe. Othman Chande na Watendaji wa Mahakama ya Tanzania. 
  Picha na Aaron Msigwa MAELEZO.  

  0 0

  Image result for KOSA La jinai

  Na Bashir Yakub
  Makosa  ya  jinai  ni  makosa  yote  yaliyoorodheshwa  katika  sura  ya  16  ya  kanuni  za  adhabu  pamoja  na  yale  yaliyo  katika  sheria  nyingine  kama  ile  ya  uhujumu  uchumi.  Pamoja  na  kuwapo  sheria nyingine  ambazo huorodhesha  makosa  ya  jinai   bado  Kanuni  za  adhabu  inabaki  kuwa  sheria  kuu  inayoorodhesha  makosa  ya  jinai.  Kwa  ujumla  katika  sheria tunayo makosa  makuu  ya  aina mbili. 
  Kwanza  ni  hayo  ya  jinai  na  pili  ni  ya  madai.  Kwa  kusema  makosa  ya  jinai  na  madai  unajikuta  umeongelea  karibia  makosa  yote unayoyajua  na  usiyoyajua.  Kila  kosa  unalolijua  kichwani  mwako  lipo  katika   moja  ya makundi  haya.
  Kwa  mifano  tu  makosa  ya  jinai  ni  kama  kupiga,  kutukana, kuendesha  kwa  uzembe( ulevi, kuongea  na simu, mwendo  kasi,kuzidisha  abiria n.k), kudhalilisha, kuiba, kubaka, kuua, utapeli, kughushi, ufisadi, rushwa, matumizi  mabaya  ya  ofisi  ya  umma, kulawiti, kumiliki  madanguro, ukahaba, dawa  za kulevya( kutumia au kuzimiliki), kuzuia  mahakama  au  mamlaka  za  kisheria  kutekeleza  wajibu, kuharibu  mali  ya  mtu, kuvamia eneo  la  mtu  kwa  nia ovu, manyanyaso  ya  jinsia  na  mengine  mengi. Kusoma zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi,Utumishi na Utawala bora George Simbachawene amewaagiza wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurungenzi wote wa halmashari nchini kuhakikisha wanazoa taka zote zilizokusanywa wakati wa siku ya uhuru kabla ya tarehe 20 mwezi huu. 
   Kauli hiyo aliitoa wakati alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa Wizara hiyo wakati wa kikao cha kumkaribisha katika ofisi ya Tamisemi mjini Dodoma. 
   Alisema kuwa hataki kuona hadi ifikapo tarehe 20 ya mwezi huu kuwa uchafu wa siku ya uhuru bado unaendelea kulalamikiwa na watu kuwa bado haijaondolewa katika maeneo uliokusanywa. “Hadi ifikapo tarehe hiyo sitaki kusikia uchafu bado haujaondolewa katika maeneo ulipokusanywa toka siku ya uhuru lakini pia unapoondolewa huo kuna uchafu mwingine unakuja hivyo basi watendaji wanaohusika wa hakikishe kuwa wanaanda maeneo ya kuupeleka”alisema Simbachawene. 
   Aidha aliwataka watumishi wa Tamisemi kubadilika katika utendaji wa kazi zao na kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwani awamu ya tano ya haitaendelea kuwalea watendaji wavivu.
   Kwa upande wake,Naibu Waziri wa wizara hiyo Suleiman Jaffo, aliwataka watumishi wa Tamisemi kubadilika katika utendaji wao wa zamani ili waweze kuongeza ukusanyaji wa mapato na kuweza kuboresha maisha ya wananchi.
   WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi,Utumishi na Utawala bora George Simbachawene akipokelewa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Jumanne Sagini alipowasili makao makuu ya ofisi hizo mjini Dodoma.
   Naibu waziri  nchi ofisi ya Rais Tamisemi,Utumishi na Utawala bora, Selemani Jaffo akipokelewa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Jumanne Sagini alipowasili makao makuu ya ofisi hizo mjini Dodoma.
   wafanyakazi wa wizara ya ofisi ya Rais Tamisemi,Utumishi na Utawala bora wakimsikiliza waziri wao  George Simbachawene.

   WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi,Utumishi na Utawala bora George Simbachawene akizungumza na wafanyakazi wa wizara hiyo mjini Dodoma.


  0 0


  Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha (Taffa), Stephen Ngatunga (kulia), akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na njia zinazotumika kuiba mapato ya serikali bandarini na katika Idara ya Forodha, Jijini Dar es Salaam jana. kushoto ni maofisa waandamizi wa chama hicho. Picha na Mpigapicha Wetu


  Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha (Taffa), Stephen Ngatunga (kushoto), akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na njia zinazotumika kuiba mapato ya serikali bandarini na katika Idara ya Forodha, Jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Ofisa Mwandamizi wa chama hicho, Ernest Kallaghe.


  Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

  CHAMA cha Mawakala wa Forodha nchini (TAFFA) kimesema kuwa wizi wa kontena bandari ya Dar es Salaam na kusababisha serikali kukosa mapato ni tatizo la muda mrefu ambalo ni limekuwa likisababishwa na watumishi wa bandari.
  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Rais wa TAFFA, Steven Ngatunga amesema tatizo lilojitokeza ya uondoshaji wa kontena 329 katika bandari Kavu ya Azam ilitokana na baadhi ya watumishi wa baadhi ya benki na Bandari kuingilia taarifa katika mfumo na kusababisha serikali kukosa mapato. 
  Ngatunga amesema kuwa tatizo la serikali kukosa mapato katika bandari ya Dar es Salaam walishagundua lakini serikali ilishindwa kuchukua hatua mpaka serikali ya awamu ya tano kugundua hilo na hatua zimechukuliwa kwa wale waliohusika.
  Amesema TAFFA itatoa ushirikiano kwa kile ambacho wanakiona katika bandari ya Dar es Salaam juu ya watu wanaosababisha serikali kukosa mapato kwa maslahi yao binafsi.
  Aidha amesema kuwa kuna kampuni zilionekana kuwa zipo kwa ajili ya kukwepa kodi ya serikali ambazo chama kiliona na kupeleka malalamiko ambayo mwisho wa siku kukawepo urasimu wa kukutana viongozi ambao wanaweza kushughilikia hilo.
  Amesema baadhi ya mawakala walilipia kontena lakini wanaambiwa malipo hayakufanyika huku wakiwa na kumbukumbu za malipo na kusababisha kutilia shaka juu ya uadilifu wa watumishi wa benki pamoja na bandari.
  TAFFA imesema haiko tayari kwenda na mawakala ambao wanaharibu taaluma hiyo na kusababishia serikali kukosa mapato ambayo ndio ya kufanyia maendeleo nchini.

  Amesema kuwa kuna kampuni 73 zimefungwa wakati hawahusiki katika katika uondoshaji wa kontena katika bandari na bandari kavu kutokana na kampuni hizo kuwa kulipia kontena zinazodaiwa kukwepa kodi.


  0 0
 • 12/16/15--03:10: BEI YA MADAFU LEO


 • 0 0

   Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na Viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) walipimtembelea ofisini kwake.
  Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiwasikiliza Viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) walipimtembelea ofisini kwake.
   (Picha na Benjamin Sawe –WHUSM)

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula amesema kuwa Serikali imeweka mazingira rafiki ya uwekezaji, hivyo alitoa wito kwa wafanyabiashara kutoka Qatar kutumia fursa lukuki za uwekezaji zinazopatikana hapa nchini. 

  Balozi Mulamula aliyasema hayo kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Taifa ya Qatar iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regence, Kilimanjaro jijini Dar es Salaam jana.

  “Tanzania imeweka mazingira wezeshi ya uwekezaji katika sekta mbalimbali kama vile kilimo, madini, uchukuzi, elimu, afya, nishati, wanyamapori, mafuta na gesi, hivyo natoa wito kwa ndugu zetu wa Qatar watumie fursa ya uhusiano mzuri tulionao kuja kuwekeza nchini”, Balozi Mulamula alisema. 

  Balozi Mulamula aliendelea kusema kuwa Serikali inaelekea katika uchumi wa gesi na ina matumani makubwa ya kufaidika na uzoefu wa mshirika wake Qatar ambayo ni mmoja wa wazalishaji wakubwa wa gesi duniani. 

  Suala lingine ambalo Katibu Mkuu aliligusia ni umuhimu wa Tanzania na Qatar kuunganisha nguvu ili kutumia rasilimali fedha na ardhi zilizopo kuimarisha sekta ya kilimo kwa madhumuni ya kuodoa changamoto za usalama wa chakula kati ya nchi hizi mbili.

  Kwa upande wake, Balozi wa Qatar nchini, Mhe. Abdulla Jassim Al Maadadi pamoja na mambo mengine, aliongelea suala la Qatar kuwa mwenyeji wa mashindano ya mpira wa miguu wa Kombe la Dunia kwa mwaka 2022. Alisema miradi mingi kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo inatarajiwa kukamilika mwaka 2020. Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa barabara, mtandao wa reli, viwanja vya mpira, viwanja vya ndege na nyumba za makazi.

  Alisema miradi hiyo ni mikubwa hivyo inahitaji wafanyakazi wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani na aliahidi kuwa watu watakaokwenda kufanya kazi nchini humo, haki zao zitalindwa.
  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Liberata Mulamula akizungumza kwenye hafla ya kuadhimisha ya Siku ya Taifa la Qatar kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Augustine Mahiga. Katika maadhimisho hayo, Balozi Mulamula alisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Qatar hususan katika sekta za kiuchumi na biashara. 
  Sehemu ya Mabalozi na wageni waalikwa wakimsikiliza Balozi Mulamula (hayupo pichani) 
  Balozi wa Qatar nchini, Mhe. Abdallah Jassim Mohamed Al-Maadadi naye akizungumza katika maadhimisho hayo. 
  Sehemu ya watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bw. Hangi Mgaka (wa kwanza kulia), na Bw. Batholomeo Jungu (wa pili kutoka kulia) nao wakimsikiliza Balozi Al-Maadadi (hayupo), katika maadhimisho hayo. 


  0 0

  Mkurugenzi wa maendeleo ya Utamaduni Profesa. Hermas Mwansoko akizungumza na watumishi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni wakati akiwaaga rasmi jana ofisini kwake. Mkurugenzi huyo anastaafu rasmi kuanzia tarehe 25 Desemba 2015.
  Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Utamaduni sehemu ya Sanaa Bibi. Leaha Kihimbi akielezea jambo wakati wa hafla ya kumuaga Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni anayemaliza muda wake Profesa Hermas Mwansoko (kulia) jana jijini Dar es Salaam.
  Afisa Utamaduni wa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Msami akitoa neno kwa niaba ya watumishi wa Idara ya Utamaduni wakati wa hafla ya kumuaga Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni anayemaliza muda wake katika utumishi wa umma Profesa. Hermas Mwansoko jana jijini Dar es Salaam.


  0 0

   Waziri wa Kilimo Uvuvi na Mifugo Mwigulu Lameck Nchemba atoa saa 48 kwa kampuni ya Sparkway ltd kuwalipa wakulima wa korosho wa Mkoa wa pwani, kiasi cha Bilioni 3.4 za mauzo ya korosho kufuatia agizo hilo,Wakulima waliouza Korosho  wataanza kulipwa jumatatu ya Desemba 21, mwaka huu.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Kilimo Uvuvi na Mifugo Mwigulu Lameck Nchemba wakati akizungumza mkoani Pwani leo.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya akifungua semina ya kuwaelimisha na kuwahamasisha watumiaji wa Huduma za Mawasiliano iliyoandaliwa na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA-CCC) katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya Desemba 15 -2015.
  Wananchi na baadhi ya watumishi wa serikali na mashirika binafsi wakisikiliza kwa Makini Hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro katika semina ya kuwaelimisha na kuwahamasisha watumiaji wa huduma za Mawasiliano Mkoa wa Mbeya Desemba 15 mwaka huu katika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.
  Picha ya pamoja na Meza Kuu. 
  Na Emanuel Madafa, Mbeya(jamiimojablogu).

  0 0
 • 12/16/15--04:26: Article 18


 • 0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akialimiana na Mjumbe maalum wa Waziri Mkuu wa Japan Seiji Kiara Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mjumbe maalum wa Waziri Mkuu wa Japan Seiji Kiara mara baada ya kufanya nae Mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi Kamal Ismail Waziri wa Nchi anayeshughulikia Mambo ya nje na Mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Sudan.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mjumbe maalum wa Waziri Mkuu wa Japan Seiji Kiara mara baada ya kufanya nae Mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc Ineke Bussemaker akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu mfumo wa kisasa wa utunzaji wa taarifa za mikopo uliozinduliwa na Benki hiyo. Mfumo huo utatutumika kwenye kanzi data ya Mikopo ya Benki hiyo ( CRB's) na kuwawezesha wateja wakubwa na wadogo wa wanaoomba mikopo kutoka NMB kuipata ndani ya siku 1 hadi 4 kutokana na taarifa zao za mikopo kuendelea kuwepo kwenye mfumo wa Benki hiyo.
  Afisa Mkuu Udhibiti wa Hasara wa Benki ya NMB Bw. Tom Borghols (wa pili kutoka kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) namna Benki ya NMB inavyoongoza katika utoaji wa mikopo kwa makundi mbalimbali.
  Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Wadogo wa Benki ya NMB Bw. Abbdulmajid Nsekela( kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu kuanzishwa kwa mfumo wa kisasa wa utunzaji wa taarifa za mikopo kwa wateja uliozinduliwa na Benki ya NMB na jinsi utakavyoongeza ufanisi kwa kuwawezesha wateja kupata mikopo kwa haraka. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc Ineke Bussemaker.

  0 0

   Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt Tulia Ackson akimshuhudia Balozi wa Cuba nchini Mheshimiwa Jorge Lopez Tormo akisaini kitabu cha wageni wakati alipomtembelea ofisini kwake jiiji Dar es salaam.
  Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt Tulia Ackson akifafanua jambo wakati akizungumza na Balozi wa Cuba nchini Mheshimiwa Jorge Lopez Tormo aliyemtembelea leo ofisini kwake jijini Dar es salaam.
  Balozi wa Cuba nchini Mheshimiwa Jorge Lopez Tormo akifafanua jambo wakati akizungumza na Naibu Spika Mhe. Dkt Tulia Ackson alipomtembelea leo ofisini kwake jijini Dar es salaam.
  Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt Tulia Ackson akiagana na Balozi wa Cuba nchini Mheshimiwa Jorge Lopez Tormo mara baada ya kufanya mazungumzo naye ofisin kwake jijini Dar es Salaam.
   (Picha na Ofisi ya Bunge).

older | 1 | .... | 1057 | 1058 | (Page 1059) | 1060 | 1061 | .... | 3278 | newer