Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

TFF YAVITAKA VILABU KUHESHIMU TARATIBU

0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limevitaka vilabu vyote nchini vya Ligi Kuu (Vodacom), Ligi Daraja la Kwanza (StarTimes), na Ligi Daraja la Pili (SDL) kuheshimu utaratibu uliowekwa wa usajili na utekelezaji wake, kwani TFF haitapendelea klabu yoyote katika suala hilo.

TFF inachukua fursa hii kuwakumbusha viongozi wote wa vilabu kuhusu kalenda ya mwaka ya usajili ambayo ina vipindi viwili,

(i)  Dirisha Kubwa la Usajili  (Juni 15 – Agosti 20)

(ii)  Dirisha Dogo la Usajili (Novemba 15 – Disemba 15)

Baada ya usajili hufuatia kipindi cha pingamizi ambacho kuchukua wiki moja, kisha Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji ya TFF kupitia mapingamizi hayo na kupitisha usajili wa wachezaji wote waliosajiliwa.

Kipindi cha usajili wa dirisha dogo ulifunguliwa Novemba 15 na utafungwa kesho Disemba 15, kipindi hichi hutumika kwa ajili ya uhamisho, kutangaza wachezaji wanaoachwa kwa mujibu wa kanuni, kutangaza wachezaji waliositishiwa mikataba, na kipindi cha pingamizi Disemba 16 – 22, na kuthibitisha usajili Disemba 23, mwaka huu.

TFF inaviomba vilabu kufuata utaratibu uliopo kikanuni katika shughuli za uendeshaji wa mpira wa miguu nchini.

TAMASHA LA MITIKISIKO 2015 LAACHA HISTORIA MKOANI IRINGA

0
0

Msaani maarufu wa bongofleva, Linex akifanya vitu vyake katika uwanja wa Mlandege mjini Iringa juzi kwenye tamasha la muziki (Mtikisiko) lililoandaliwa na redio Ebony FM ya mjini Iringa kwa udhamini wa kampuni ya simu za mkononi Tigo. Tamasha hilo hufanyika kila mwaka katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

Msaani maarufu wa Hip hop,Darasa akifanya vitu vyake katika uwanja wa Mlandege mjini Iringa juzi kwenye tamasha la muziki (Mtikisiko) lililoandaliwa na redio Ebony FM ya mjini Iringa kwa udhamini wa kampuni ya simu za mkononi Tigo. Tamasha hilo hufanyika kila mwaka katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini

Umati wa wananchi wa Iringa waliojitokeza  katika uwanja wa Mlandege mjini Iringa juzi kwenye tamasha la muziki (Mtikisiko) lililoandaliwa na redio Ebony FM ya mjini Iringa kwa udhamini wa kampuni ya simu za mkononi Tigo. Tamasha hilo hufanyika kila mwaka katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini

Msaani maarufu wa Hip hop, Roma Mkatoliki akifanya vitu vyake katika uwanja wa Mlandege mjini Iringa juzi kwenye tamasha la muziki (Mtikisiko) lililoandaliwa na redio Ebony FM ya mjini Iringa kwa udhamini wa kampuni ya simu za mkononi Tigo. Tamasha hilo hufanyika kila mwaka katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini

TEASER JOTO LA ASUBUHI LA 93.7 EFM KUANZIA SAA 12 ASUBUHI

DK. KIGWANGALA AFANYA ZIARA ZA KUSHTUKIZA KATIKA KITUO FOREPLAN CLINIC KINACHOMILIKIWA NA DK. MWAKA

0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala leo majira ya jioni amefanya ziara ya kushtukiza katika kituo kinachotoa tiba mbadala cha Foreplan Clinic kinachomilikiwa na Dk. Mwaka Juma Mwaka kilichopo Ilala Bungoni na kujionea hali halisi ya kituo hicho. Mara baada ya kufika alianza kufanya ukaguzi kuanzia sehemu ya Mapokezi mpaka kwenye vyumba vya matabibu lakini katika vyumba vyote hakuna daktari aliyekuwa anatoa huduma.

Akizungumza na wagonjwa waliokuwa wakisubilia tiba alisema kuna waliofika katika kituo hicho ili kutibiwa lakini kituo hicho hakina uwezo wa kuwahudumia wagonjwa hao. Na kuwataka wagonjwa hao waende kwenye hospitali ili wapate matibabu yanayoendana na magonjwa wanayoumwa.

Akizungumza msaidizi wa Dk. Mwaka, Bi Teddy L. Mbuya alisema yeye hawezi kusema kuhusu kituo hicho maana yeye sio msemaji mkuu bali alimwomba Naibu waziri kufanya ukaguzi katika kituo hicho pamoja na kuwaliza maswali wahusika mbalimbali wa vitengo vya ktuo hicho.

Baada ya ukaguzi wa kituo hicho Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala amemwagiza Mkurugenzi Msaidizi Tiba Asilia na mbadala Dk.Paul Mhame ndani ya wiki moja kufanya ukaguzi kwa kituo cha Dk. Mwaka na aletewe taarifa iliyokamilika kuhusu taaruma yeke pamoja na washirika wake na pia dawa anazozitumia kama ni rafiki kwa wananchi wanaotumia dwa hizo pamoja na kufanya ukaguzi wa vituo vyote vinavyotoa tiba mbadala na tiba asilia kama Dk. Ndodi, Dk. Rahabu nk. ili kuwabaini wanaowalaghai wananchi. 

Pia amesema Dk Mwaka Juma Mwaka amekuwa akijitangaza kupitia vyombo mbalimbali hapa nchini ambavyo ni kosa la kutangaza kama unafanya kazi za tiba tabibu. Alisema madaktari wana miiko na katika miiko hiyo ambayo inatumika na mojawapo ikiwa ni kutojitangaza. Naibu waziri aliendelea kusema kuwa Dk. Mwaka amekuwa akijiita Dokta na amekuwa akichambua mwili wa binadamu kama vile ameusomea udakitari wakati sheria ya tiba asilia na tiba mbadala hairuhusu watu wa tibaAsilia na Tiba Mbadala kutumia maneno ya tiba ya kisasa.

Pia Naibu Waziri amamtaka Dk. Mwaka Juma Mwaka kufika wizarani kesho saa mbili asubuhi akiwa na nyaraka zake zote zinazohusu utoaji wa huduma ya Tiba Mbadala kwani amekuwa akijiita majina ya tiba za kisasa na pia kutibu kwa njia ya kisasa badala ya kutibu kwa njia ya Asilia au Tabibu.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akiwasili katika kituo cha Foreplan Clinic kinachotoa tiba mbadala kilichopo Ilala Bungoni, jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho leo jumatatu kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Tiba Asilia na tiba Mbadala Dk.Paul Mhame kutoka wizara ya Afya na Ustawi wa jamii.
Masaidizi wa Dk. Mwaka, Bi Teddy L. Mbuya akimtolea ufafanuzi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala kuhusu huduma zitolewazo katika kituo cha Foreplan Clinic mara baada ya kuanza kukagua kituo hicho kinachotoa Tiba 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala akikikagua kifaa kinachotumika kufanyia vipimo kwenye kituo cha Foreplan Clinic wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho leo jioni siku ya jumatatu.


RAIS MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA JAPAN NCHINI

0
0
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida aliyefika Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo. Katika Mazungumzo hayo Balozi Yoshida amempongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa kuiongoza Tanzania katika awamu hii ya tano na pia amezungumzia miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Japan hapa nchini.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mmoja wa Maofisa walioambatana na Balozi Yoshida Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Kalenda kutoka kwa Balozi wa Japan hapa  nchini Mheshimiwa Masaharu Yoshida mara baada ya kumaliza mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kulia akiagana na Balozi wa Japan Nchini Mheshimiwa Masaharu Yoshida mara baada ya kumaliza mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU. 

WAZIRI MKUU, MAJALIWA AITISHA KIKAO CHA KAZI CHA BARAZA LA MAWAZIRI LEO

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mawaziri na Naibu Mawaziri katika kikao cha kwanza cha kazi cha Baraza la Mawaziri alichokiitisha Ofisini kwake jijini Dar es salaam Desemba 15, 2015.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama wakati alipomkaribisha kuzungumza katika kikao cha kwanza cha baraza la kazi la Mwaziri, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Desemba 15,2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

ITC, EAC LAUNCH NEW PROJECT TO BOOST AFRICAN TRADE

0
0
The International Trade Centre (ITC) and the East African Community (EAC) yesterday announced that the two organizations are launching a new, joint project to boost intra-African trade.

The Trade and Regional Integration Project (TRIP) for EAC was announced by the EAC Secretary-General Amb. Dr. Richard Sezibera and ITC Executive Director Arancha González on the margins of the World Trade Organization’s Ministerial Conference taking place in Nairobi, Kenya from 15-18 December 2015.

The new initiative aims to strengthen existing efforts by East African Partner States for closer economic integration, including the East African Customs Union and the EAC Common Market.

The TRIP for EAC project also sets out to support the African Union’s Action Plan for Boosting Intra-African Trade and the recently agreed tripartite free-trade agreement among the Common Market for Eastern and Southern Africa (COMESA), the EAC and the Southern African Development Community (SADC).

Specifically the project aims to boost the competitiveness of EAC-based small and medium-sized enterprises (SMEs), enabling them to step up intra-and inter-regional trade. The project will have a strong focus on women’s economic empowerment, and will also support wider private-sector development in the EAC to spur deeper economic integration, including in agriculture, information and communication technologies (ICT), and tourism.

“Regional integration led by the private sector is a powerful vehicle for boosting growth, creating jobs and promoting economic development,” Ms González said. ‘Enabling the private sector and policymakers to take advantage of trade opportunities is at the heart of what ITC does. We are looking forward to doing this in collaboration with the EAC, and to ensuring sustainable growth for East African countries and their SMEs.”

Amb. Sezibera said: ‘This cooperation will contribute to improve the global competitiveness of our region and to trigger sustainable economic growth.’Implementation of the five-year US$ 8.5 million TRIP for EAC project is set to begin in January 2016. The Government of Finland has pledged to provide initial funding.

ITC and the EAC will intervene at three levels to provide integrated solutions to problems of SME competitiveness. At the enterprise level, they will work to enhance the competitiveness of SMEs in selected sectors, with a strong focus on women entrepreneurs.

At the institutional level, they will work to strengthen trade and investment support institutions, enabling them to better serve their SME clients, especially on export development and international marketing services.

Finally, at the trade policy level, the project will aim to enhance the business environment through improving trade facilitation and public-private dialogue to ensure that reforms correspond to business needs.

MKUU WA MKOA WA DODOMA AFUNGUA MASHINDANO YA TUSA

0
0
Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Mh. Chiku Gallawa akisalimia na wachezaji wa timu ya Zanzibar Univestity wakati wa ufunguzi wa mashindano ya shirikirisho la vyuo vikuu Tanzania (TUSA) yatakayojumuisha michezo mbalimbali ambayo yanafanyika Katika chuo kikuu cha Dodoma.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Mh. Chiku Gallawa akizungumza wakati akifungua mashindano ya shirikirisho la vyuo vikuu Tanzania (TUSA) yatakayojumuisha michezo mbalimbali ambayo yanafanyika Katika chuo kikuu cha Dodoma.
washiriki mbalimbali wa mashindano ya shirikirisho la vyuo vikuu Tanzania (TUSA) yatakayojumuisha michezo mbalimbali ambayo yanafanyika Katika chuo kikuu cha Dodoma.

Balozi Mulamula afungua Mkutano wa Asasi za Kiraia wa Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu

0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akizungumza wakati akifungua rasmi Mkutano wa siku mbili wa Asasi za Kiraia kutoka Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu uliofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo uliwashirikisha wenyeviti wa asasi za kiraia kutoka nchi wanachama wa Ukanda wa Maziwa Makuu.
 Sehemu ya Wajumbe wakifuatilia ufunguzi wakati Katibu Mkuu, Balozi Mulamula akizungumza (hayupo pichani)
Sehemu nyingine ya wajumbe wakifuatilia ufunguzi.
Wajumbe wengine wa mkutano.

VODACOM TANZANIA YAJA NA KAMPENI YA"LIFE IS BETTER"

0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(watatu toka kushoto)akiwa ameshikana mikono na baadhi ya viongozi wa taasisi zilizowezeshwa na Kampuni hiyo kufanya wanajamii maisha yao kuwa murua.Wakati wa hafla ya Uzinduzi wa kampeni mpya ya kampeni hiyo ya“Life is better” inayolenga kuendelea kunufaisha jamii kwa kutoa intanet yenye kasi zaidi kwa kutuma na kupokea pesa kwa M PESA kwa haraka na salama zaidi,Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto katika picha Msimamizi wa kituo cha Mabinti Centre,Katia Geurts,Mmoja wa akina mama aliyepona Fistula Cherry Msangi,Mkurugenzi wa walemavu katika Hospitali ya CCBRT,Brenda Msangi na Mkuu wa Vodacom Foundation,Renatus Rwehikiza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(kushoto)akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa walemavu wa hospitali ya CCBRT,Brenda Msangi wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni mpya ya kampeni hiyo “Life is better” inayolenga kuendelea kunufaisha jamii kwa kutoa intanet yenye kasi zaidi na kutuma na kupokea pesa kwa M-PESA kwa haraka na salama zaidi ,Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa akina mama aliyetibiwa na kupona Fistula katika hospitali ya CCBRT, Cherry Msangi akitoa ushuhuda kwa waandishi wa habari wakati wa Uzinduzi wa kampeni mpya ya Vodacom Tanzania ya” Life is better” inayolenga kuendelea kunufaisha jamii kwa kutoa intanet yenye kasi zaidi na kutuma na kupokea pesa kwa M-PESA kwa haraka na salama zaidi,Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam,Wengine katika picha ni Msimamizi wa kituo cha Mabinti Centre,Katia Geurts na Mkurugenzi wa walemavu katika Hospitali ya CCBRT,Brenda Msangi(kulia).
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao akiongea na waandishi wa habari pamoja na wadau mbalimbali(hawapo pichani)wakati wa hafla ya Uzinduzi wa kampeni mpya ya kampuni hiyo ya “Life is better inayolenga kuendelea kunufaisha jamii kwa kutoa intanet yenye kasi zaidi na kutuma na kupokea pesa kwa M-PESA kwa haraka na salama zaidi,Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.

NAIBU KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI ALIASA JESHI LA MAGEREZA KUPUNGUZA MATUMIZI YA FEDHA ZA SERIKALI YASIYO MUHIMU

0
0
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. John Mngodo akihubia Baraza la Wafanyakazi raia wa Jeshi la Magereza lililofanyika leo Desemba 15, 2015 katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi raia wa Jeshi la Magereza kutoka vituo mbalimbali hapa nchini wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi kama wanavyoonekana katika picha.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua rasmi Baraza la Wafanyakazi raia wa Jeshi la Magereza lililofanyika leo Desemba 15, 2015 katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Maafisa Wandamizi wa Jeshi la Magereza kutoka Mikoa yote Tanzania Bara, Makao Makuu ya Jeshi hilo, Wakuu wa Vyuo vya Magereza wakifuatilia majadiliano katika Baraza hilo.

TPDC: Gesi asilia ipo na ziada

0
0
Mkurungezi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, Dkt. James Mataragio, amesema hali ya uzalishaji wa gesi asilia nchini ni nzuri, alieleza kuwa mitambo ya kuchakata gesi asilia kule Madimba Mkoani Mtwara na Songo Songo Mkoani Lindi inao uwezo wa kuzalisha futi za ujazo milioni 240 za gesi asilia, huku gesi anayo tumika ikiwa futi za ujazo milioni 146 za gesi asilia. 

Dk. Mataragio ameongeza kuwa mchanganuo huo wa uzalishaji wa gesi unazidi mahitaji yetu kwa sasa na hivyo kuwa na gesi ya ziada takribani futi za ujazo milioni 94 za gesi asilia kwa siku (94mmscfd).
Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, Dkt. James Mataragio, akizungumza na waandishi katika mkutano huo, wengine ni Mkurungezi wa Usafirishiji na Usambazaji wa Gesi Asilia Dk. Wellngton Hudson (wa pili kulia) na Meneja Mawasilino-TPDC Marie Msellemu (wa kwanza kulia) wakiwa katika mkutano.

FA CUP KUENDELEA LEO

0
0
Michezo ya mzunguko wa pili wa Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) inaendelea leo katika viwanja vitatu tofauti, huku kila timu ikisaka ushindi na kuweza kusonga katika hatua inayofuata itakayochezwa mwakani Januari, 2016 na bingwa kuwakilisha nchi mwaka 2017 katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika (CC).

Leo katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam, African Lyon watawakaribisha Ashanti United, mjini Tabora Polisi Tabora watacheza dhidi ya Rhino Rangers na uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Sabasaba FC watawakaribisha Burkinfaso FC.

Kesho Jumatano kutachezwa michezo miwili, Friends Rangers watawakaribisha KMC katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam, huku katika uwanja wa Sheihk Amri Abeid jijini Arusha, Madini FC watacheza dhidi ya maafande wa JKT Oljoro.

Alhamisi michuani hiyo itaendelea kwa michezo mitatu, Panone FC watawakaribisha Kiluvya FC uwanja wa Ushirikia mjini Moshi, Lipuli FC watacheza dhidi ya Kurugenzi uwanja wa Wambi – Mafinga, huku Mbao FC wakiwakaribisha  Geita Gold kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

Waziri wa Mambo ya Nje akutana na Waziri wa Nchi wa Mambo ya Nje wa Japan

0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) (kulia) akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Nchi wa Mambo ya Nje wa Japan yaliyofanyika katika Ofisi ya Wizara hiyo leo.
Walioshuhudia mazungumzo hayo kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Mbelwa Kairuki, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi, Mindi Kasiga na Katibu wa Waziri, Bw. Thobias Makoba.
Maofisa kutoka Serikali ya Japan.


MBUNGE WA JIMBO LA UBUNGO, SAED KUBENEA AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR LEO.

0
0
 Mbunge wa jimbo la Ubungo,(Chadema) Saed Kubenea amefikishwa mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam mapema hii leo akielekea katika  chumba cha kusomewa shtaka la kutoa lugha chafu dhidi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
 Mbunge wa jimbo la Ubungo,(Chadema) Saed Kubenea akiwa na wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo, leo mara baada ya kusomewa shitaka lililokuwa likimkabiri katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo. 
 Mbunge wa jimbo Ubungo,(Chadema) Saed Kubenea akizungumza na waandishi wa habari katika mahakama ya kisutu jijini Dar es Salaam leo.

Hata hivyo, Kubenea amekana kufanya kitendo hicho na kesi yake imeahirishwa hadi Desema 29, mwaka huu.Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

MUONEKANO WA ENEO LA JANGWANI BAADA YA MVUA KUNYESHA LEo

WAZIRI MKUU AKUTANA NA KATIBU MKUU WA CCM LUMUMBA JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkaribisha kwenye Makao Makuu ya Chama, Ofisi Ndogo CCM Lumumba,Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Mhe.Majaliwa Kassim Majaliwa.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro nje ya Ofisi Ndogo,Lumumba katikati ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimiana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka wilaya ya Simanjiro Mhe. Christopher Ole Sendeka nje ya Ofisi Ndogo, CCM Lumumba.

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha wageni cha Ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Martha Mwaipaja, Jesca BM, Mwahangila kupanda jukwaa la Krismasi

0
0
WAIMBAJI nyota wa muziki wa Injili hapa nchini Martha Mwaipaja, Jesca BM na Christopher Mwahangila wanatarajia kupanda katika jukwaa la Tamasha la Krismasi linalotarajia kufanyika Desemba 25 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Waimbaji hao wanaungana na wenzao waliotangulia kuthibitisha kushiriki tamasha hilo ambalo lina mlengo wa kurudisha Shukrani kwa Mungu baada ya kufanikisha uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 kwa amani na utulivu.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama aliwataja wengine ambao watakuwa sambamba na wenzao siku hiyo ni pamoja na Sifael Mwabuka sambamba na Kwaya ya Yombo KKKT.

Msama alisema tamasha hilo linadhaminiwa na gazeti la Dira ya Mtanzania ambako alitoa wito kwa mashirika na kampuni mbalimbali kujitokeza ili kufanikisha tamasha hilo.

Aidha Msama aliwataja wengine waliothibitisha kupanda jukwaa la tamasha hilo ni pamoja na Rebeca Malope, Eiphraim Sekeleti, Solomon Mukubwa, Faustine Munishi, Upendo Nkone, Christina Shusho, Joshua Mlelwa na Kwaya ya Wakorintho Wapili.

Msama anaweka bayana kauli mbiu ya tamasha hilo ni Njooni wote tumsifu Mungu kwa pamoja, tumuinue Mungu kwa nyimbo na kucheza mbele yake.

KAMPUNI YA TINGATINGA IMEINGIA MKATABA NA KAMPUNI YA BRICOLEUR HOLDINGS Co.LIMITED YA JAPAN.

0
0
Na Zainabu Hamis,Globu ya Jamii. 
CHAMA Cha Wasanii wa uchoraji picha aina ya Tingatinga imeingia mkataba wa miaka tano (5) na kampuni ya Bricoleurholdings Co.Limited ya nchini Japan, kwa ajili ya kuwatafutia soko nchini Japan 

Makabidhiano ya Mkataba huo yamefanyika leo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. 

Mwakilishi wa Kampuni ya Bricoleurholdings Co.Limited, Shoji Tsuchiya amemkabidhi mkataba huo Mwenyekiti wa Chama Cha Tingatinga, Zack Chimwanda, amesema kuwa kazi hii ya uchoraji wa picha aina ya Tingatinga imeanza nchini Tanzania ikiwa na mwanzilishi wake Edward Said Tingatinga ambaye alifariki dunia mwaka 1970 na jina la hilondipo lilipopatikana kutokana na yeye. 

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Hakimiliki Nchini (Cosota) Doreen Sinane,amesema kuwa kampuni ya BricoleurholdingsCo,Limited itakuwa inafanya kazi ya kuuza na kutafuta soko la picha zinazotengenezwa na wanachama wa Tingatinga. 

Kwa upande wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Godfrey Ngereza, amesema kuwa sanaa ya uchoraji ni kazi kama kazi nyingine pia ni biashara inayomfanya msanii kupata kipato pamoja na kuliingizia taifa mapato.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan, Bi. Yu Shiran (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu kushirikiana kufanya kazi za sanaa na Kikundi cha Sanaa cha Tingatinga, leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO). Kulia ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Sanaa Tingatinga, Bwana Zachi Chimwanda na kushoto ni Mkurugenzi pia wa Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan, Bwana Shoji Tsuchiya.
Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bwana Godfrey Mngereza akiwa na wanakikundi cha Sanaa cha Tingatinga na wajapani wakonyesha vibao vilivyochorwa na kikundi cha Sanaa cha Tinga Tinga jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan Bwana Shoji Tsuchiya (kulia) wakibadilishana mikataba na kupeana mikono na Mwenyekiti wa Kikundi cha Sanaa cha Tingatinga, mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam katika wa mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO). Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ya Japan Bi. Yu Shiran. 
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Helpage international happy with new cabinet, say New Ministry Dealing with Older People is Momentous and Opportune

Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images