Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

GADO LEO


WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI YAFUTA VYAMA VYA KIJAMII 1,268

$
0
0
 Msemaji wa Wizara Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaac Nantanga akizungumza na waandishi wa habari leo juu ya ufutaji wa vyama vya kijamii vilivyoshindwa kuendesha pamoja na kushindwa kulipa ada, kushoto ni Mwanasheria wa wizara hiyo, Berious Nyasembwa.
Waandishi wa habari wakifatilia taarifa ya Msemaji wa Wizara Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaac Nantanga leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.


Na Zainabu Hamisi, Globu ya Jamii.
WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi imefuta vyama vya Kijamii 1,268 kutokana na kushindwa kutekeleza majukumu yao na sheria zilizowekwa katika uendeshaji wa vyama pamoja na mashirika yasiyo ya Kiserikali (NG’0s).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Isaac Nantanga amesema kuwa kufutwa kwa vyama hivyo ni kutokana na kukiuka masharti ya uwendeshaji wa taasisi ikiwemo kutolipa ada kwa mujibu wa sheria.

Katika ufutwaji wa vyama hivyo chama kimojawapo kilichofutwa ni chama cha wapiga picha nchini ambacho kimeshindwa kukidhi vigezo vya uendeshaji na kushindwa hata kuendesha vikao vyake.

Nantanga amesema kuwa vyama vingine 1,406 vimepewa kusudio la kufutwa na baada siku 21 kuanzia leo, kama havitatoa kusudio la kujitetea basi navyo vitafutwa.

Amesema kufuatana na kanuni ya vyama inayoundwa na kifungu cha 38 cha sheria ya vyama vyote vya kijamii vinapaswa kulipa ada ya kila mwaka.

Aidha, amesema kanuni ya 6 za vyama za kijamii inayosomwa pamoja na kifungu cha 22 cha sheria ya vyama inavitaka vyama vya kijamii kuwasilisha taarifa za kila mwaka za hesabu zilizokaguliwa za mapato na matumizi ya vyama kwa msajili wa vyama.

Aliongeza kuwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inatoa angalizo kwa vyama vyote vya kijamii kuendesha shughuli zake kwa kufuatana na sheria zilizoanzisha vyama hivyo.

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AFUNGA MAFUNZO YA ZIMAMOTO NA UOKOAJI CHUO CHA UONGOZI JKT KIMBIJI

$
0
0
Gwaride la Wahitimu wa Mafunzo yaKozi ya Awali ya Sajini na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji likipita mbele ya mgeni Rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (hayupo pichani) wakati wa kufunga mafunzo hayo katika Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akisalimiana na Uongozi wa Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji pamoja na Maofisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakati alipowasili Chuoni hapo kufunga mafunzo ya Sajini na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kozi ya Awali yaliyofanyika hayo Chuoni hapo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, akikagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa na Wahitimu wa Mafunzo ya Awali ya Sajini na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yaliyofanyika katika Chuo cha yaliyofanyika katika Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji, jijini Dar es Salaam.
Muhitimu wa Mafunzo ya Kozi ya Awali ya Sajini na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Semeni Daudi Chiunda, akipokea zawadi kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, kutokana na kuwa Mhitimu Bora katika kipingere cha Ukakamavu wakati wote wa Mafunzo yaliyofanyika katika Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Abubakari Akida, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

EAC SECRETARY GENERAL CAUTIONS ON CLIMATE CHANGE

$
0
0
The Secretary General of the East African Community, Amb. Dr. Richard Sezibera has cautioned the international community that the world was at a crossroads and the outcome of the Paris Climate Conference shall either bequeath a better, safer planet to future generations “or destroy our common heritage and our shared humanity”.

Speaking at the 21st Session of the Conference of Parties (COP21) to the United Nations Framework Convention on Climate Change (UNFCCC), also serving as the 11th Meeting of the Parties to the Kyoto Protocol (CMP11) currently underway in Paris, France, the Secretary General expressed the wishes and expectations of the East African citizens on the Paris Climate Change Talks and reckoned that the Agreement must take into consideration the interest of the vulnerable and poor by ensuring that adaptation is equally prioritized and differentiated responsibilities of developed and developing countries reflected in the Agreement.
(L-R) The EAC Deputy Secretary General for Productive and Social Sectors, Hon Jesca Eriyo, Secretary General of the East African Community, Amb. Dr. Richard Sezibera and Mr. Jean Baptiste Havugimana, Director of Productive Sectors following the proceedings of the conference.

READ MORE HERE

JIJI LA MBEYA LAPATA MEYA MPYA DAVID MWASILINDI (CHADEMA) DIWANI KATA YA NZOVWE

$
0
0
Meya Mteule wa jiji la Mbeya Diwani wa Kata ya Nzovwe(CHADEMA) Ndugu David Mwasilindi ambaye aliibuka kidedea kwa kupata kura 34 dhidi ya Mpinzani wake wa CCM aliyepata kura 14 katika uchaguzi uliofanyika Desemba 10 katika ukumbi wa Mkapa jijini humo.
Wajumbe wa baraza la Madiwani Halmashauri ya jiji la Mbeya wakifuatilia kwa umakini majadiliano katika mkutano huo.
Baadhi ya watumishi wa jiji la Mbeya wakiteta jambo katika mkutano huo wa baraza la Madiwani la Halmashauri ya jiji la Mbeya ambalo liliketi na kumchagua Meya na Naibu wa jiji hilo ambaye ni David Mwasilindi (CDM) baada ya kupata kura 34 dhidi ya mpinzani wake wa CCM aliyepata kura 14.

BENKI YA CRDB YAKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA SHINDANO LA 'TUMA PESA NA SIMBANKING SHINDA PASSO'

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa promosheni ya ‘Tuma Pesa na SimBanking Shinda Passo’ iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 (Picha na Francis Dande).
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia) akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Bodi, Martin Mmari.
Zawadi za washindi.

Wafanyakazi wa Benki ya NBC walivyoadhimisha Uhuru Day

$
0
0
Meneja wa Tawi la Corporate la Benki ya NBC, Geoffrey Ndossa (kushoto), na Meneja Masoko wa benki hiyo, Alina Maria Kimaryo wakifanya usafi eneo la ufukwe wa salender jijini Dar es Salaam kuadhimisha Siku ya Uhuru ambapo wafanyakazi wa NBC waliungana na watanzania wengine kuitikia wito wa serikali ya awamu ya tano kusafisha mazingira
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya NBC wakifanya usafi eneo ufukwe wa salander jijini Dar es Salaam kuadhimisha Siku ya Uhuru ambapo wafanyakazi hao waliungana na watanzania wengine kuitikia wito wa serikali ya awamu ya tano kusafisha mazingira.
Wafanyakazi wa benki ya NBC wakifanya usafi kuadhimisha Siku ya Uhuru ili kuitikia wito wa serikali ya awamu ya tano wa kusafisha mazingira wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Tanganyika.

Idara ya uhamiaji kanda ya Dar es Salaam imewakamata wahamiaji 15 raia wa Ethiopia waliongia nchini kinyume na sheria


MWANAMUZIKI ROBERTO AMARULA KUTOKA ZAMBIA KUTUMBUIZA DAR ES SALAAM, DODOMA KATIKA TAMASHA LA INSTAGRAM WIKIENDI HII

$
0
0


Mwanamuziki na mtangazaji wa redio, Roberto Chindaba Banda 'maarufu Roberto Amarula kutoka nchini Zambia (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana , kuhusu onyesho lake atakalolifanya leo  katika fukwe za Escape One Mikocheni jijini Dar es Salaam na kesho ukumbi wa Ngalawa Pub mkoani Dodoma katika Tamasha la Instagram Party Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Freconic Ideaz, Fred Ngimba ambao wamemleta msanii huyo hapa nchini kwa kushirikiana na Kampuni ya C&G Solutions na kulia ni Mwanamuzi David Banda 'General Ozzy kutoka Zambia.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Freconic Ideaz, Fred Ngimba (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
Meneja Mawasiliano wa Freconic Ideaz, Krantz Mwantepele (kushoto), akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema kampuni yao itaendelea kuleta wanamuziki wengine kutoka pande mbalimbali za dunia kama walivyofanya kwa Robarto Amarula. 

 Mwanamuzi David Banda 'General Ozzy kutoka Zambia (kulia), akizungumza na wanahabari.

 Mwanamuziki na mtangazaji wa Redio, Roberto Chindaba Banda 'maarufu Roberto Amarula kutoka nchini Zambia, akifanya vitu vyake mbele ya wanahabari.
  Mwanamuzi David Banda 'General Ozzy, akiimba mbele ya wanahabari. Mwanamuziki huyu atamsindikiza Roberto Amarula wakati wa shoo yao.
Mwanamuziki, Clinton Nyirongo kutoka Zambia naye atakuwepo kutoa burudani.
Na Dotto Mwaibale

MWANAMUZIKI wa Zambia anayetamba na wimbo maarufu wa Amarula, Robert Banda ‘Roberto Amarula’, kesho anatarajia kufanya shoo kubwa na ya aina yake katika Ufukwe wa Escape One uliopo Mikocheni, jijini Dar es Salaam kabla ya kufanya hivyo mjini Dodoma kesho kutwa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Roberto Amarula, ameahidi kutoa burudanio ya aina yake kwa wakazi wa Dar es Salaam na Dodoma, akiwataka mashabiki wa muziki na burudani kujitokeza kwa wingi kwenye shoo zake hizo.
“Nimefurahia sana kuja Dar es Salaam na ninaahidi kutoa shoo ya aina yake kesho (leo) na Dodoma ili kuwaburudisha Watanzania, lakini pia nitatembelea vituo vya watoto yatima ili kuwafariji na kuwapa nguvu wajione nao ni sehemu ya jamii ya Watanzania na Afrika kwa ujumla,” alisema aliyeambatana na wasanii wenzake wa Zambia, David Banda ‘General Ozzy’ na Clinton Ntirongo ‘Mandela’.
Kwa upande wake, Mkugenzi wa Freconic Ideaz, Fred Ngimba, alisema kuwa shoo ya leo itawahusisha pia wasanii wa Tanzania kama Ben Pol, Roma Mkatoliki, Fred Swag, Msouth na wengine wengi na kwamba onyesho la Dodoma litafanyika kwenye ukumbi wa Ngalawa Pub, ikiwa ni sehemu ya tamasha la Instagram Party.  
Kwa upande wake, Meneja Mawasiliano wa Frecon Ideaz, Krantz Mwantepele, alisema: “Tunafahamu kiu ya Watanzania katika suala zima la burudani ndio maana tumewaletea msanii huyu ambaye kwa sasa ni maarufu mno Afrika na kwingineko tukiahidi kuwaleta wasanii zaidi wakubwa Afrika na hata Marekani ili kukata kiu ya mashabiki wa muziki hapa nchini.”
Ziara ya Roberto Amarula ambaye ni mshindi wa tuzo za uandishi bora, mwanamuziki, mtayarishaji muziki na mtangazaji wa redio, iliyoratibiwa kwa pamoja na Freconic Ideaz na C&G Solutions, imedhaminiwa na Millard Ayo, Morena Hotel, Shabiby Bus Service na Clouds FM.


MAHAFALI CHUO CHA UHASIBU KURASINI JIJINI DAR

$
0
0
Wahitimu wa Shahada ya Uhasibu(BAC) katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA)Felister Kulaya,Janeth Maleto,Eliza Hollo na Oscar Uwesu wakiwa katika picha ya pamoja wakijiandaa kuanza mahafali yao ya kuhitimu Shahada Hiyo leo Katika Taasisi hiyo yaliyofanyika katika makao makuu ya Taasisi yaliyopo kurasini Jijini Dar es Salaam.
 Wahitimu wa Stashahada ya Uhasibu (DA) katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Janet na Edna wakiwa katika picha ya pamoja wakijiandaa kuanza mahafali yao ya kuhitimu Stashahada Hiyo leo Katika Taasisi hiyo yaliyofanyika katika makao makuu ya Taasisi yaliyopo kurasini Jijini Dar es Salaam.

 Wahitimu wa Shahada ya Ugavi(BPLM) katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA)wakiwa katika picha ya pamoja wakijiandaa kuanza mahafali yao ya kuhitimu Shahada Hiyo leo Katika Taasisi hiyo yaliyofanyika katika makao makuu ya Taasisi yaliyopo kurasini Jijini Dar es Salaam.
 Wahitimu wa Shahada ya Uhasibu(BAC) na Ugavi (BPLM) katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA)Josephat Mwashimaha,Steven Lucas,Evelyn Ngachengo na Agness mchaa wakiwa katika picha ya pamoja wakijiandaa kuanza mahafali yao ya kuhitimu Shahada Hiyo leo Katika Taasisi hiyo yaliyofanyika katika makao makuu ya Taasisi yaliyopo kurasini Jijini Dar es Salaam.
 Wahitimu wa Shahada ya Rasilimali watu (BHRM) katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA)Anna Masimba,Tumaini Mwalyoga,Beatrice Shoo,Flora Katanzi,Nuru Makumulo na Abdi Katanzi wakiwa katika picha ya pamoja wakijiandaa kuanza mahafali yao ya kuhitimu Shahada Hiyo leo Katika Taasisi hiyo yaliyofanyika katika makao makuu ya Taasisi yaliyopo kurasini Jijini Dar es Salaam.
Wahitimu wa Shahada ya Uhasibu (BAC) katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA)Hassan Msakamali,Joseph Paschal,Amri Ngoi na Richard LIfa wakiwa katika picha ya pamoja na Mhadhiri wao Dkt.Kato Mpanju Rugaitika wakijiandaa kuanza mahafali yao ya kuhitimu Shahada Hiyo leo Katika Taasisi hiyo yaliyofanyika katika makao makuu ya Taasisi yaliyopo kurasini Jijini Dar es Salaam. Picha zote kwa hisani ya Masama Blog...

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AFUNGA MAFUNZO YA ZIMAMOTO NA UOKOAJI CHUO CHA UONGOZI JKT KIMBIJI

$
0
0
Gwaride la Wahitimu wa Mafunzo ya Kozi ya Awali ya Sajini na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji likipita mbele ya mgeni Rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (hayupo pichani) wakati wa kufunga mafunzo hayo katika Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akisalimiana na Uongozi wa Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji pamoja na Maofisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakati alipowasili Chuoni hapo kufunga mafunzo ya Sajini na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kozi ya Awali yaliyofanyika hayo Chuoni hapo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, akikagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa na Wahitimu wa Mafunzo ya Awali ya Sajini na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yaliyofanyika katika Chuo cha yaliyofanyika katika Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji, jijini Dar es Salaam.
Muhitimu wa Mafunzo ya Kozi ya Awali ya Sajini na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Semeni Daudi Chiunda, akipokea zawadi kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, kutokana na kuwa Mhitimu Bora katika kipingere cha Ukakamavu wakati wote wa Mafunzo yaliyofanyika katika Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Abubakari Akida, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Ardhi waliofanya Vizuri wanyakua Tuzo mbalimbali

$
0
0
 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi Prof. Idrisa Mshoro akimkabidhi cheti mmoja wa wanafunzi wa mwaka wa nne aliyefanya vizuri katika masomo yake kwa mwaka 2014/2015  wakati wa leo jijini Dar es salaam.
 Naibu Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia masuala ya Taaluma wa Chuo Kikuu cha Ardhi Prof. Gabriel Kassenga akizungumza na wanafunzi na wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya utoaji wa Tuzo kwa wahitimu wa chuo hicho waliofanya vizuri leo jijini Dar es salaam.
  Baadhi ya Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Ardhi, wawakilishi wa Makampuni na Taasisi mbalimbali waliochangia tuzo mbalimbali na Wahitimu wa miaka ya nyuma wa Chuo hicho wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa hafla fupi ya utoaji wa Tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri leo jijini Dar es salaam.
  Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Ardhi waliofanya Vizuri waendelea kupokea tuzo zao. Takribani wanafunzi 126 wamepata Tuzo na zawadi mbalimbali wakiwemo wanafunzi kike 61 waliofanya vizuri katika masomo ya Sayansi.
 Wanafunzi na Wageni mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo
 Mwanafunzi Bora wa Kike wa Chuo Kikuu cha Ardhi katika fani ya Upimaji wa Ardhi ( Geomatics) Bi. Lilian Kato akipokea zawadi yake ya mashine ya kupimia Ardhi (Total Station) yenye thamani ya shilingi milioni 15 aliyozawadiwa na Kampuni ya High Tech Systems kwa kuwa mwanafunzi bora wa kike wa mwaka wa nne kwa mwaka 2014/2015
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

DIRA YA DUNIA YA BBC SWAHILI IJUMAA DEC 11

Kampuni ya Mawakili ya Yakubu & Associates Chamber yatwaa tuzo mbili

$
0
0
 Kampuni ya Mawakili ya Yakubu & Associates Chamber usiku wa jumamosi wamezawadiwa tuzo mbili za Mwajiri Bora wa Mwaka 2015 na Chama cha Waajiri Nchini (ATE). Pichani juu ni vikombe vilivyozawadiwa kwa Yakubu & Associates Chamber kama Mwajiri Bora wa Mwaka 2015 Biashara za Kati
 Wadau wa Kampuni hiyo, Meneja wa Fedha, Husna Mkony,Naibu Mtendaji Mkuu (Biashara) Dr Timothy Kyepa(kati) na Meneja Utumishi na Rasilimali watu Ibrahim Pius,
Wakili Mtendaji, Saidi Yakubu akinyanyua juu vikombe walivyoshinda kama Mwajiri Bora wa Mwaka 2015. Picha kwa hisani ya Yakubu Chambers.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc ashinda Tuzo ya Biashara 2015

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc, Ineke Bussemaker (kulia) akipokea tuzo ya Mfanyabiashara Bora wa Kike wa Mwaka 2015 (Business Women of the Year 2015) kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Quality Group Limited, Arif Sheikh (kushoto) katika hafla ya Tuzo za viongozi (Tanzania LeaderShip Awards) iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency Dar Es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc, Ineke Bussemaker (kulia) akitoa neno la shukrani mara baada ya kukabidhiwa tuzo ya Mfanyabiashara Bora wa Kike wa Mwaka 2015 (Business Women of the Year 2015) katika shindano la Tuzo za viongozi (Tanzania LeaderShip Awards) jana kwenye Hoteli ya Hyatt Regency Dar Es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Quality Group Limited, Arif Sheikh aliyemkabidhi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc, Ineke Bussemaker (kulia) akipokea tuzo ya Mfanyabiashara Bora wa Kike wa Mwaka 2015 (Business Women of the Year 2015) kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Quality Group Limited, Arif Sheikh (kushoto) katika hafla ya Tuzo za viongozi (Tanzania LeaderShip Awards) iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency Dar Es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc, Ineke Bussemaker (kushoto) akikabidhi tuzo mbalimbali kwa baadhi ya washindi katika nafasi anuai kwenye hafla ya Tuzo za viongozi (Tanzania LeaderShip Awards 2015) iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency Dar Es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc, Ineke Bussemaker (kushoto) akikabidhi tuzo mbalimbali kwa baadhi ya washindi katika nafasi anuai kwenye hafla ya Tuzo za viongozi (Tanzania LeaderShip Awards 2015) iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency Dar Es Salaam.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Mhe. Anjela Kairuki Aanza Kazi rasmi Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora

$
0
0
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjella Kairuki (Mb) (wa pili kutoka kushoto) akiwasili ofisini na kulakiwa na watendaji wa ofisi yake mara baada ya kuapishwa. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Bw. Tixon Nzunda.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjella Kairuki (Mb) akiweka saini katika kitabu cha wageni baada ya kuwasili rasmi katika ofisi yake leo Jumamosi.
 Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- Utumishi na Utawala Bora Bw. Tixon Nzunda (aliyesimama) akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjella Kairuki (wa kwanza kutoka kulia) kuongea na watendaji wa ofisi yake baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjella Kairuki (Mb) (kulia) akizungumza na watendaji wa Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora mara baada kufika ofisini kwake kuanza kazi leo Jumamosi. Picha na James Katubuka Mwanamyoto

KAMPUNI 15 ZASHINDWA KULIPA KODI ZA KONTENA 329 ZILIZOTOROSHWA KATIKA BANDARI KAVU YA AZAM

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

KAMPUNI 15 zimeshindwa kulipa kodi za kontena zilizotoroshwa katika bandari kavu ya Azam inayomilikiwa na Said Salim Bakhressa na kodi iliyokuwa imekwepwa kwa kampuni 43 ni zaidi ya Sh. Bilioni 12.

Kodi iliyolipwa ya Kontena 329 hadi jana ambayo ndio ilikuwa ulipaji wa hiari kwa ndani ya siku saba za Rais Dk. John Pombe Magufuli ni zaidi ya sh. bilioni 10 pekee.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Kamisha Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Dk. Philip Mpango amesema kuwa kampuni hizo zinatakiwa kulipa kodi hiyo kwani ulipaji wa hiari wa siku saba za Rais Dk. John Pombe Magufuli umeisha jana  hivyo hatua zitachukuliwa kuhakikisha wanalipa kodi hiyo ya Watanzania.

Mpango amesema kuwa kampuni 13 tu ndio zimeweza kumaliza kodi  yote iliyokuwa imekadiriwa na TRA kwenye Kontena 329 zilizotoroshwa katika Bandari Kavu ya Azam (ICD).
Kaimu Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Dk. Philip Mpango akizungumza na waandishi habari (hawapo pichani) juu ya hatua za ulipaji wa kodi iliyokwepwa katoka katika kontena 329 katika bandari Kavu ya Azam,leo jijini Dar es Salaam.

Amesema kampuni 15 zimelipa sehemu ya kodi na wanaendelea kuwadai licha ya kuisha kwa siku saba hivyo wanawajibu kulipa kodi iliyobaki katika Akaunti ya TRA iliyofunguliwa Benki Kuu (BoT) yenye namba 9921169 785.

Mpango amesema  kuwa wafanyabiashara ambao wameshindwa kulipa katika hicho hatua zitachukuliwa na wasubiri cha moto.
Amesema watumishi 36 wa TRA wanatuhumiwa kushiriki katika upotevu wa kodi kutokana na kontena 329  kuondoshwa bandarini kinyume cha taratibu za forodha na hivyo kusababisha serikali ikose mapato.

Mpango amesema kuwa TRA inawaomba wananchi taarifa juu mali za kifisadi na mwenendo mbaya wa baadhi ya watumishi wa mamlaka hiyo.

Amewataka watumishi kuwasilisha tamko za mali wanazomiliki pamoja na fedha zilizo katika benki na mwisho wa kufanuya hivyo ni Desemba 15 mwaka huu..
Waandishi wa habari wakifatilia taarifa kwa Kaimu Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Dk. Philip Mpango leo jijini Dar es Salaam.

DEREVA MZEMBE AHUKUMIWA MIAKA MITATU JELA MKOANI MBEYA

$
0
0


Na Ezekiel Kamanga, Mbeya

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya imememhukumu kwenda jela miaka mitatu Martin Mhina Dereva wa basi la Majinja kwa kuendesha gari kwa uzembe.

Waendesha Mashitaka wa Serikali Hannarose Kasambala na Catherine Gwatu wameiambia Mahakama kuwa Dereva huyo aliendesha Basi la Kampuni ya Majinja kwa uzembe mapema mwaka huu majira ya saa 12 asubuhi kwa kuigonga gari aina ya Toyota Hilux na kusababisha kifo cha mtu mmoja.

Mawakili hao wameiambia Mahakama kuwa Kesi hiyo namba 46/2015 ambapo Dereva huyo alitenda kosa hilo kinyume cha Sheria ya usalama barabarani namba 40(1),63(2)(a),27(1)(a)III(c) kifungu cha 168 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Akijitetea mbele ya Mahakama Martin ameiomba Mahakama kumsamehe kwa kuwa hilo ni kosa lake la kwanza na kwamba anayo familia inayo mtegemea hivyo imwonee huruma kutokana na kosa hilo.

Baada ya kupitia ushahidi uliotolewa Mahakamani na Upande wa Mashitaka na utetezi wa Mshitakiwa Hakimu Zawadi Laizer alimtia hatiani kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela ili iwe fundisho kwa madereva wasifuata sheria za usalama barabarani.

Tume ya Haki za Binadamu yalaani hatua za Viongozi kuwaweka rumande watumishi wa umma kwa makosa ya kinidhamu

$
0
0
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bahame Nyanduga 

WADAU WAPONGEZA FILAMU MPYA YA "GOING BONGO"

$
0
0

Rais wa Shirikisho la Filamu Simon Mwakifamba akiongea na vyombo vya habari wakati wa uzinduzi filamu ya ‘Going Bongo’ uliofanyika katika ukumbi wa cimema wa Cinemax jana Ijumaa jijini Dar es salaam

WADAU mbalimbali waliofika kwenye onyesho la kwanza la filamu ya Mtanzania anayeishi nchini Marekani wametoa sifa kemkema kuhusu filamu hiyo inayokwenda kwa jina la ‘Going Bongo’ na wamewataka wasanii wa hapa nchini waige mfano wake.

Wakizungumza baada ya kutoka kuaitazama ndani ya ukumbi wa cimema wa Cinemax Ijumaa usiku mkongwe katika filamu Ibrahimu Banane almaarufu kwa jina la ‘Mzee Katembo’ alisema kwamba mtunzi wa filamu hiyo amewashtua wasanii wa hapa nyumbani na Afrika Mashariki kwa ujumla.

“Ametushtua sisi kwamba tutunge filamu na kuzicheza katika kiwango cha kimataifa na tuchukue muda mrefu ili kuweza kutunga na kurekodi filamu zetu kama tunataka kulikamata soko hilo na kujitangaza kwa ujumla endapo tu tutafuata nyayo za mtunzi wake Ernest Napoleon.” alisema Katembo.

Alisema m ameiangalia filamu hiyo inayokwenda kwa jina la ‘Going Bongo’ ni nzuri kila muigizaji amesimama katika nafasi yake na kuuvaa uhusika vilivyo na endapo wasanii wa hapa nyumbani watataka kutengeneza filamu nzuri wasiogope kuingia gharama kama jinsi filamu hiyo inavyoonesha muandaaji alivyoingia gharama kwamba aimerekodiwa katika nchi mbili tofauti.

“Hapa nyumbani sisi tumezoea kuona kwamba msanii anafyatua filamu mbili ndani ya mwezi mmoja jambo ambalo hupunguza ubunifu kwani ni vigumu kichwa kimoja kuweza kutoa kitu kizuri ndani ya mwezi mmoja” alisema Katembo.

Msemaji wa Waigizaji nchini Massoud Kaftani aliimwagia sifa filamu hiyo na kusema kwamba wamepata somo kutoka kwa Ernest hivyo wanashukuru pia kwa kupata nafasi ya kuishuhudia filamu hiyo na kuahidi wkamba watafanyia kazi changamoto mbalimbali zilizo ndani ya tasnia ya filamu na maigizo nchini.

Wakati huohuo Rais wa Shirikisho la Filamu Simon Mwakifamba aliongeza kwa kusema kuwa yeye binafsi amevutiwa na filamu hiyo kutokana na kuzingatiwa kwa vina na mpangilio mzuri, “hili ni jambo la kujivunia kama watanzania pia tunatoa wito kwa watanzania wengine wanao ishi nje ya nchi kujipanga na kuibua vipaji vyao kimataifa kama jinsi alivyotuonesha Ernest hivyo huko waliko nina imani na wao wameifuatilia filamu hii ya Going Bongo ilete chachu kwa watanzania wanaoishi ughaibuni na wa hapa nyumbani wote tujipange kwa pamoja katika kuikuza na kuiendeleza tasnia hii” alisema Mwakifamba.

Filamu hiyo ilishuhudiwa na wadau mbalimbali akiwamo Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ huku akiitoa maneno ya kuisifa gfilamu hiyo na kusema kuwa muandaaji ametoa somo kwa wasanii wahapa nchini.

Filamu hiyo inayokwenda kwa jina la ‘Going Bongo’ ilioneshwa kwa mara ya kwanza kwenye ukumbi wa sinema wa Century Cinemax uliopo Mlimani City, Jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na mashabiki wengi ambao wengi wao walikiri kuvutiwa nayo.

Filamu hiyo ambayo mpaka sasa imetwaa tunzo kadhaa, pamoja na tunzo ya Ziff ina maudhui ambayo yanonyesha maisha ya Daktari aliyejitolea kwenda kufanya huduma nchini Tanzania kwa muda wa mwezi mmoja huku mtunzi na muandishi pia aliyeisimamia katika kuitengeneza na kuigiza filamu hiyo ni Ernest Napoleon .

Filamu hii imerekodiwa majiji makubwa mawili ambayo ni Dar es Salaam na California Marekani, inaelezea sehemu ya maisha ya kweli aliyonayo Daktari mwenye asili ya nchini Ufaransa aliyeondoka Ulaya na kwenda kufanya kazi barani Afrika.


Kati ya tuzo ambazo filamu hii imeshinda ni pamoja na, Filamu Bora Afrika Mashiriki katika tamasha la Zanzibar International Film Festival (Ziff) na Filamu Bora ya Kimataifa katika tamasha la ‘Black Entertainment Fashion’, ‘Film and Television Awards’ (BEFTA)
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images