Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1048 | 1049 | (Page 1050) | 1051 | 1052 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Mtunzi mahiri na mkongwe wa riwaya za kusisimua nchini SAM KITOGO amekuja kivingine na kitabu chake kipya 'OPERESHENI KIGALI' ambacho ni moto wa kuotea mbali. Ukihitaji nakala rejareja ama kwa jumla mpigie kwa namba +255 655 711515

  0 0

  Wahitimu wa Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya Zanzibar wamehimizwa kuwa tayari kufanya kazi popote watakapopangiwa ambapo watakuwa na wajibu wa kuthamini na kuchangia jitihada zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali katika kupambana na maradhi mbali mbali yanayoisumbua jamii Nchini. 
  Himizo hilo limetolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein kwenye Mahafali ya 22 ya Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya Zanzibar yaliyofanyika kwenye Kampas ya chuo hicho yaliyopo Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. 
  Jumla ya wahitimu 440 wa kada saba walihitimu na kufanikiwa kupata stashahada mwaka huu wa masomo kukiwa na ongezeko kubwa mara mbili ikilinganishwa na wahitimu 280 wa mwaka 2014. 
  Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein ambae Hotuba yake ilisomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idii alisema wapo baadhi ya baadhi ya wahitimu wanaoajiriwa na Wizara ya Afya wanapiga chenga kufanya kazi Kisiwani Pemba wakisahau kwamba Wananchi wa kisiwa hicho wanahitaji kupata huduma zao. 
  Alisema watumishi wa Umma wakiwemo wa sekta ya afya wanapaswa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria na taratibu za kazi na miongozo ya sehemu wanazoajiriwa na inapendeza zaidi wawe mfano wa tabia njema kwa kushikamana katika kutekeleza maadili ya kazi zao. 
  Aliupongeza Uongozi wa Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya Zanzibar kwa kutoa mchango mkubwa katika utekelezaji wa mipango ya Serikali tokea kilipoanzishwa katika kuimarisha sekta ya afya kwa misingi iliyowekwa na waasisi wa Afro Shirazy Party wakati wa kupigania uhuru wa Nchi hii. Mmoja wa wahitimu hao Faika Karim Zam kwa niaba ya wenzake wameuomba Uongozi wa Chuo hicho kuanzisha mafunzo ya ngazi ya Shahada { Diploma } kwa nia ya kuwapunguzia gharama za kutafuta elimu hiyo nje ya nchi. 
  Mapema Mkuu wa Chuo cha Taalum za Sayansi za Afya Zanzibar Dr. Haji Mwita Haji alisema Uongozi wa Chuo hicho kupitia Baraza lake umeamua kuongeza majengo zaidi ili kuwahudumia vyema wanafunzi wanaoamua kujiunga na chuo hicho sambamba na mahitaji ya ongezeko la Hospitali na vituo vya Afya Nchini. 
  Akimkaribisha Mgeni rasmi katika ufungaji wa Mahafali hayo ya 22 ya Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya Zanzibar, Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Mahmoud Thabit Kombo aliwaomba wauguzi kufuata maadili ya kazi zao ili kupunguza au kuondosha kabisa malalamiko yanayotolewa na wananchi. 
  Mh. Mahmoud alisema lugha zao kwa wagonjwa ndio kitendo kilichompa wakati mgumu alipokuwa akijibu maswala ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika Vikao vya Baraza hilo vilivyokuwa vikiendelea kwa muda wote wa miaka mitano iliyopita.
   Baadhi ya wahitimu wa Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya fani ya Uuguzi wakisubiri kuhudhurishwa baada ya kumaliza mafunzo yao ya miaka Mitatu katika chuo cha Taaluma za Sayanasi za Afya Mbweni.
   Wahitimu wa Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya fani ya maabara wakifuatilia matukio mbali mbal;I yaliyokuwa yakiendelea kwenye mahafali ya kumaliza mafunzo yao hapo Mbweni.
   Baadhi ya wahitimu wa Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya fani ya Uuguzi wakisubiri kuhudhurishwa baada ya kumaliza mafunzo yao ya miaka Mitatu katika chuo cha Taaluma za Sayanasi za Afya Mbweni.
   Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya Mbweni Dr. Abdulla Ismail Kanduru  kushoto akiteta na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyemuwakilisha Rais wa Zanzibar kwenye mahafali ya 22 ya Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afra Mbweni.
  Balozi Seif akimkabidhi Cheti Maalum Salama Witi Asfau wa Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya akiwa Mhitimu bora wa Fani ya Usanifu wa Vifaa Tiba vya Hospitali kwa mwaka 2015.

  0 0
 • 12/07/15--03:55: NYUMBA INAUZWA
 • Nyumba ya kisasa inayouzwa jijini Arusha, ipo maeneo ya Njiro Block C
  Bei maelewano kwa anayeihitaji.
   Kwa Maelezo zaidi piga simu +255 759 929 271 

  Ni Nyumba ya kuishi familia na iko vizuri kabisa.
  Muonekano wake kwa upande wa juu
  Muonekano wake kwa upande wa pembeni.
  inavyoonekana Ndani.
  Bustani.

  0 0

  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kushoto) akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi na Watendaji Wakuu wa ofisi zilizo chini yake katika kikao cha kuhimiza uwajibikaji kilichofanyika ofisini kwake.

  Na Lilian Lundo-Maelezo
  OFISI ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma imeanza rasmi kutekeleza Ahadi ya Uadilifu kwa watumishi wa Umma nchini ambao ulizinduliwa Agosti Mosi mwaka huu.

  Akiongea na vyombo vya habari leo, Katibu Mkuu Hab Mkwizu amesema utekelezaji huo umeanza rasmi Disemba, 2015 ambapo kila mtumishi wa Umma ataweka saini ya kiapo kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa na mazingira ya Taasisi husika.

  “Utaratibu wa Utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu kwa watumishi wa Umma umetolewa kupitia waraka wa Mkuu wa Utumishi wa Umma Na. 2 wa mwaka 2015 kuhusu utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu kwa viongozi, watumishi wa Umma na sekta binafsi wa tarehe 1 Agosti, 2015.” Alisema Mkwizu.

  Mkwizu aliongezea kwa kusema, uanzishwaji wa Ahadi ya Uadilifu ni muendelezo wa uundwaji wa vyombo vya kusimamia maadili baada ya ongezeko kubwa la ubadhirifu, utoro sehemu za kazi na kushuka kwa nidhamu katika kipindi cha miaka ya themanini na tisini.

  Alivitaja vyombo vingine ambavyo vilianzishwa kusimamia ahadi na uadilifu kuwa ni Sekretariate ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

  Mkwizu alivitaja vipengele ambavyo mtoa ahadi anatakiwa kuvitamka ni, kuwa mzalendo wa nchi yake na kutii Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, kuhudumia Umma na watumishi wenzake kwa heshima, kutimiza wajibu wa kutoa huduma bora kwa umma, kutoa huduma bora kwa usawa kwa watu wote na kutofanya ubaguzi wa dini, siasa, kabila, udugu, ukanda, jinsia, urafiki au hali ya mtu.

  Vipengele vingine ni kutumia rasilimali za Umma kwa manufaa ya Umma, kutotoa siri za Serikali au mteja kwa watu wasiohusika isipokuwa kwa maslahi ya Umma, kufanya kazi kwa nidhamu ya hali ya juu, kutoomba kushawishi, kutoa wala kupokea rushwa na kutotumia madaraka kwa manufaa binafsi ya ndugu, rafiki au jamaa.

  Aidha, Mkwizu ametoa wito kwa waajiri wote kuhakikisha kuwa utekelezaji wa Ahadi na Uadilifu unakamilika ifikapo tarehe 31/12/2015 na kuwasilisha Ofisi ya Rais – UTUMISHI kabla ya tarehe 25/02/2016 na utekelezaji wake kuwa kila ifikapo Juni 30 ya kila mwaka. Fomu za Ahadi ya Uadilifu zinapatikana katika tovuti ya Ofisi ya Rais – UTUMISHI yenye anwani www.utumishi.go.tz.

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza siku ya kupiga kura kwa baadhi ya majimbo ambayo uchaguzi wake ulihairishwa kutokana na sababu mbalimbali

  Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Jaji Mstaafu Damian Lubuva ametaja siku hiyo ya uchaguzi itakuwa Disemba 13, mwaka huu.

  “Natoa rai kwa Wananchi wote waliojiandikisha kama wapiga kura katika Majimbo na Kata husika kujitokeza katika vituo walivyojiandikishia ili kuweza kupiga kura na kuwachagua viongozi wanaowataka” amesema Lubuva.

  Jaji Lubuva aliyataja majimbo hayo ambayo wananchi watapiga kura za kuchagua Wabunge kuwa ni Majimbo ya Arusha Mjini na Handeni Mjini ambapo uchaguzi wa Madiwani katika kata za Mvomero, Ipala na Nyamwilolewa nao utafanyika siku hiyo.

  Aidha, Jaji Lubuva alisisitiza kuwa, taratibu zilizotumika katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015 mwaka ndizo zitakazotumika kwenye uchaguzi kwenye majimbo hayo na kata hizo.

  Kwa ufupi, Jaji Lubuva alikumbushia baadhi ya taratibu hizo zikiwemo za mpiga kura kubeba kadi yake ya kupigia kura pindi aendapo kupiga kura, mawakala wa vyama vya siasa lazima wawepo kwenye kila kituo na pia Maafisa Uchaguzi kufungua kituo na kufunga kwa muda uliopangwa na Tume.

  Katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 25 Oktoba 2015, uchaguzi wa Wabunge na Madiwani wa Majimbo 7 pamoja na Kata 35 ulihairishwa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za vifo na vurugu.
   Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu uchaguzi wa wabunge unaotarajiwa kufanyika Tarehe 13/12/2015 katika jimbo Handeni na Arusha Mjini, (kushoto) ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura Bw.Clarence Nanyaro kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
   Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva(ambaye hayupo katika picha) leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waaandishi wa habari kuhusu taratibu zitakazo tumika katika uchaguzi wa wabunge katika jimbo la Arusha na Handeni.

  0 0

   Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa Efm Radio, Denis Ssebo akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya wasanii zaidi ya 50 wa Bongo Movie akiwamo Steve Nyerere, Wema Sepetu na Vicent Kigosi (Rey) wataungana na kituo cha redio cha EFM na Benki ya DTB kufanya usafi Desema 9 mwaka huu. Usafi huo utaanzia katika barabara ya Morocco hadi Magomeni, mkutano huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mkuu wa Bidhaa na Masoko wa benki ya Diamond Trust Bank (DTB), Sylvester Bahati.
   Mkuu wa Bidhaa na Masoko wa benki ya Diamond Trust Bank (DTB), Sylvester Bahati akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya usafi ni nguzo moja wapo katika benki hiyo na si kwa ajili ya agizo la Rais John magufuli bali ni zoezi endelevu, kulia ni Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa Efm Radio, Denis Ssebo.
  Wandishi wa habari wakimsikiliza Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa Efm Radio, Denis Ssebo, mkutano huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam
  Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii.

  WASANII wa  Bongo Movie zaidi ya 50 akiwamo Steve Nyerere, Wema Sepetu na Vicent Kigosi (Rey) wataungana na kituo cha redio cha EFM na Benki ya DTB kufanya usafi Disemba 9 mwaka huu. 

  Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa EFM, Denis Ssebo, amesema usafi huo utaanzia katika barabara ya Morocco hadi Magomeni. 

  Ssebo amesema katika usafi huo EFM, DTB pamoja na wasanii hao watashirikiana na viongozi mbalimbali walioko madarakani pamoja na wakazi wa Kinondoni chini ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda. 

  Kauli mbiu ya siku hoyo isemayo ‘Naona aibu kuishi na uchafu’ huku tukiunga kauli mbiu ya kinondoni ‘Usafi uanze na mimi’ endapo kila mmoja atatambua umuhimu wa usafi wake, mazingira yake tutaweza kwa pamoja kulimaliza tatizo la uchafu nchini,”amesema Ssebo. 

  Kwa upande wake mwakilishi wa DTB Silvesta Bahati alisema usafi ni nguzo moja wapo katika benki hiyo na si kwa ajili ya agizo la Rais John magufuli bali ni zoezi endelevu.

  0 0

   Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli, Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahmana Kinana kabla ya kuanza kwa Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa jijini Dar es salaam leo Desemba 7, 2015.
    Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa jijini Dar es salaam leo Desemba 7, 2015.
   Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipigiwa saluti na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahmana Kinana kabla ya kuanza kwa Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa jijini Dar es salaam leo Desemba 7, 2015.

  0 0

  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepata mashine mpya na ya kisasa ya Digital X-ray ambayo wataalamu wake hawatalazimika kutumia filamu kusafisha picha kama ilivyozoeleka katika mashine za kawaida.

  Mashine hiyo imegharimu Dola 200,000 za Marekani ambazo zimetolewa na serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambayo ina uwezo wa kusafirisha picha nje ya nchi ili kupata ushauri wa kitaalamu.

  Akilelezea kuhusu maendeleo ya mashine ya MRI na CT-SCAN , Mkuu wa Idara ya Mionzi wa MNH, Dk Florah Lwakatare amesema matengenezo ya mashine hizo yamekamilika na kwamba hadi sasa wagonjwa 148 wamepimwa kwa kutumia mashine ya MRI , wakati wagonjwa 304 wamepimwa kwa kutumia CT-SCAN .

  Katika hatua nyingine Hospitali ya Taifa Muhimbili leo imepokea msaada wa mashuka 200, vyandarua 150 , Televisheni nne , Decoder 4 pamoja na Tv Stand 4.

  Akikabidhi msaada huo ambao umetolewa na Kampuni ya Mr. Uk Electronics Limited ya Dar essalaam, mwakilishi wa kampuni hiyo John Solomon ametoa wito kwa jamii kuwa na moyo wakujitolea na kushirikiana na serikali katika kuboresha huduma mbalimbali za jamii ikiwemo huduma za afya .

  Mkuu wa Idara ya Mionzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Flora Lwakatare akionyesha namna huduma ya kipimo cha CT Scan baada ya mashine hiyo kukamilika.
  Sehemu ya misaada ya shuka 200, neti 150 na Televisheni nne ikipokelewa leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

  0 0

  Bidhaa zinazouzwa katika moja ya eneo la kiwanda cha urafiki yaliyokodishwa na uongozi wa menejimenti ya kiwanda hicho unaolalamikiwa na wafanyakazi kwamba wanajipatia mapato kwenye maeneo ya kiwanda hicho huku wao wakiwalipa kiduchu.
  Mkuu wa Wilaya ya kinondoni Paul Makonda, akiwasili na msafara wake kiwandani hapo kwa ajili ya kuzungumza na wafanyakazi walio katika mgomo. 
  Mkuu wa Wilaya ya kinondoni Paul Makonda akizungumza na wafanyakazi wa Kiwanda cha Urafiki leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Na Mwandishi Wetu

  MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umeamua kutekeleza kwa vitendo agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano, John Magufuli la kufanya usafi nchini siku ya sherehe za Uhuru 9/12/2015 kufagia, kulima, kuzoa taka na kusafisha maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.

  Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema jana Dar es Salaam kuwa usafi huo utaanzia makao makuu yao Ilala Bungoni, soko la Ilala,Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mmachinga Complex, Soko la Mitumba Karume, Kariakoo, Mnazi Mmoja, Soko la Kisutu, Posta ya zamani, soko la samaki Feri mpaka Ikulu.

  Alisema zaidi ya wanachama 300 wa SHIWATA kutoka fani mbalimbali za wanamichezo, wasanii, waandishi wa habari na wadau wamethibitisha kushiriki kufanya usafi huo kutokomeza ugonjwa wa kipundupindu unashika kasi katika maeneo ya jiji la Dar es Salaam.

  Taalib alisema kazi ya usafi huo itaanza saa 1.30 asubuhi kila mmoja aje na fagio, jembe, reki, au zana yeyote ya kufanyia usafi na kuvaa mavazi rasmi ya kufanyia kazi za usafi.


  0 0

  MFUKO wa Pensheni wa PSPF, imeisaidia hospitali ya wilaya ya Temeke, vitanda, magodoro na mashuka ili kusaidia serikali katika juhudi zake za kupunguza uhaba wa vifaa vya hospitali za umma.

  Msaada huo ambao ni utekelezaji wa maombi ya Mbunge wa viti maalum, Angela Kairuki, alioutoa kwa uongozi wa PSPF, baada ya kutembelea hospitali hiyo wakati akiwa naibu waziri wa Sheria na Katiba, na kukuta akina mama wajawazito waliofika hospitalini hapo kujifungua wengine wakilala chini kutokana na uhaba wa viotanda, alisema Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Abdul Njaidi na kuongeza PSPF, kwa kuwa ni Mfuko unaotoa huduma kwa jamii nao hauna budi kutoa sehemu ya faida na kuirejesha kwa jamii kwani wengi wao wanaofika hapo hospitali kwa ajili ya matibabu ni wanachama wa Mfuko na wengine ni wanachama watarajiwa wa Mfuko.

  Kufuatia maombi hayo Mfuko huo umekabidhi vifaa hivyo leo Desemba 7, 2015, ambapo Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Bw. Abdul Njaidi, alikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu.

  Akipokea vifaa hivyo katika hafla iliyohudhuriwa na Mkurugenzi wa Mnaispaa ya Temeke, Photidus Kagimba, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Dkt. Sylvia Mamkwe, na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Temeke, Dkt. Amani Malima, aliishukuru PSPF, kwa moyo huo wa kusaidia jamii.

  “PSPF mmeonyesha moyo wa uungwana kwa kusaidia akina mama zetu wakati wakisubiri kupatiwa huduma wakati wa kujifungua basi wawe na mahala pazuri pa kulala.” Alisema.  Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, (wakwanza kulia), akiungana na Mbunge wa viti maalum, Angela Kairuki, (wapili kulia), mkurugenzi w manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, Photidus Kagimbo, watatu kulia), mganga mfawidhi wa hospitali ya Temeke, Dkt. Amani Malima, (wane kulia) na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Dkt. Sylvia Mamkwe, (wakwanza kushoto), wakati PSPF, ikikabidhi msaada wa vitanda, mashuka na magodoro kwa hospitali hiyo, Desemba 7, 2015. Msaada huo ni utekelezaji wa ahadi ya Mfuko baada ya kuombwa na Mh. Angela Kairuki.Na K-vis Media/Khalfan Said
  Mbunge wa viti Maalum, Angella Kairuki, (wapili kulia), akipokea msaada wa vitanda, kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, kwenye hosptali ya Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam Desemba 7, 2015. Mfuko huo umetoa msaada wa vitanda, magodoro na mashuka ili kuunga mkono juhudi za serikali za kumaliza tatizo la vifaa tiba kwenye hosipatli za umma. Kulia ni .. Muuguzi mwandamizi wa hospitali hiyo. 
  Njaidi (kulia), akiangalia wakati fundi akiunganisha moja ya vitanda hivyo wakati wa makabidhiano hayo.


  0 0


  0 0

  Wadau, 
  Nafasi ya kazi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) itakuwa wazi kuanzia Mwezi Septemba, 2016. Mchakato wa kumpata mrithi wa Bw. George Nyatega (Mkurugenzi Mtendaji wa sasa) umeanza. Kwa mwenye sifa afungue link hii http://www.heslb.go.tz/images/adverts/JOB_POSITION_ED_2015.pdf . Kila la heri.

  0 0


  CEO, Bernard Matthewman
  INTERSWITCH, the leading integrated digital payments and commerce provider focused on Africa has today announced its entry into Tanzania and unveiled its new corporate identity. This marks a new phase inInters witch’s expansionacross Africa with operations now in six (6) countries.
  The entry into East Africa follows the completion of the merger with leading East African e-payments provider Paynet Group.  Effectively, Paynet Tanzanianowbecomes Interswitch.
  Paynetbegun operations  in 2003 and is best known for a number of innovations includinglinking ATMs with M-PESA in Tanzania (Vodacom M-Pesa) and Kenya (Safaricom- M-Pesa), and driving the adoption of EMV Chip cards across Tanzania, Uganda and Kenya.
  Following these announcements, Tanzania becomes the sixth country where Interswitch has re-branded its operations in Africa with its new corporate identity seeking to establish uniform brand values and identity across Africa.
  Speaking during the launch held at the Hyatt Regency- the Kilimanjaro in Tanzania, Interswitch East Africa CEO Bernard Matthewman said the launch of the new brand in Tanzania was a statement of Interswitch’s leading position in the market and reflects its ambition to continue to grow its world class service across the African continent. For more CLICK HERE

  0 0

  Mwenyekiti wa Bodi ya Wataalamu wa Manunuzi na Ugavi nchini(PSPTB)Dk Hellen Bandiho akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Wataalamu unaofanyika kwenye ukumbi wa mikutano ya kimataifa wa AICC jijini Arusha na kusisitiza miiko ya uadilifu katika manunuzi ya umma na sekta binafsi.

  Mjumbe wa Bodi ya Wataalamu wa Manunuzi na Ugavi nchini(PSPTB)Ahmed Kilima akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Wataalamu unaofanyika kwenye ukumbi wa mikutano ya kimataifa wa AICC jijini Arusha.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Manunuzi nchini(PSPTB)Dk Clemence  Tesha  akizungumza jambo na wajumbe wa mkutano wa mwaka wa Wataalamu wa taaluma ya Manunuzi na Ugavi unaofanyika kwenye ukumbi wa mikutano ya kimataifa wa AICC jijini Arusha na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka mikoa mbalimbali nchini na wageni kutoka nchi jirani. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

   .Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya The Dila Africa, Jumba Dickson,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya ufugaji wa sungura unaweza ukawasaidia wakulima katika kujiongezea kipato kwa mbali na kuuza nyama yake lakini pia wana uwezo wa kuuza kinyesi, mkojo pamoja na ngozi yake,katika ziara ya mafunzo kuhusu mradi huo katika eneo la Kivungwi kata ya Vigwaza, Mkoa wa Pwani.
    Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya The Dila Africa, Jumba Dickson, akiwaonesha waandishi moja ya sungura wanaopatikana katika shamba hilo, kulia ni Mjasiriamali na mfugaji wa sungura hao, Gladness Nyange, katika ziara ya mafunzo kuhusu mradi huo katika eneo la Kivungwi kata ya Vigwaza, Mkoa wa Pwani.
   Sehemu ya mabanda ya kufugia Sungura hao.
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya The Dila Africa, Jumba akifafanu jambo kwa Wandishi wa habari  katika ziara ya mafunzo  kuhusu mradi  huo  katika eneo la Kivungwi kata ya Vigwaza, Mkoa wa Pwani.
   Picha na Emmanuel Massaka waGlobu ya jamii


  WATANZANIA wameshauriwa kujihusisha na ufugaji wa sungura ili waweze kujiongezea kipato kutokana na mnyama huyo kuwa na faida nyingi.

  Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya The Dila Africa, Jumba Dickson wakati akizungumza na waandishi wa habari waliokuwa katika ziara ya mafunzo kuhusu mradi huo jana katika eneo la Kivungwi kata ya Vigwaza, Mkoani Pwani.

  Dickson alisema, ufugaji wa sungura unaweza utawanufaisha wakulima katika kujiongezea kipato  mbali na kuuza nyama yake wana uwezo wa kuuza kinyesi, mkojo pamoja na ngozi yake

  “Tunawafundisha wakulima jinsi ya kufuga sungura ili waweze kunufaika, lakini wanaweza kujiuliza ni wapi wanaweza kuwauza wakishafikia hatua ya kuuzwa, sisi tunawapa soko kwa hiyo kikubwa kwa mkulima ni kufuga tu,” Dickson alisema.

  Alisema kampuni yake ina mashamba ya sungura hivyo wanapoingia mkataba na wakulima wanaohitaji kufuga wanakubaliana mambo mbalimbali ikiwemo kuwatafutia masoko ambapo wao wenyewe wananunua sungura hao. 

  Alisema mbali na faida ya kuuza nyama yake lakini pia wanaweza kuuza kinyesi, mkojo pamoja na ngozi yake.                                                                                  

  Naye Mjasiriamali na mfugaji wa sungura hao, Gladness Nyange alisema, kuna umuhimu wa kinamama  kutumia fursa ya ufugaji sungura ili kumudu kuwasomesha watoto wao badala ya kuwategemea waume zao.

  Alisema licha ya kuwa sungura hao wanahitaji uangalizi wa hali ya juu katika kuwafuga lakini amekuwa akihakikisha kuwa waishi katika mazingira mazuri ili waweze kumpa faida.

  “Huu ufugaji kwa kuwa ni mpya watu, wengi wanaweza kujiuliza inakuwaje au masoko watapata wapi...lakini mimi nilipoanza kufuga niliingia mkataba na hii kampuni na wao walinipa masoko ina maana kwa kila sungura wa kilo nne nauza kwa Sh 40,000,” Nyange alisema.

  Nyange alishauri wajasiriamali na hasa wanawake kujiingiza katika ufugaji huo ili waweze kufanya mambo yao mbalimbali bila kuwategemea akinababa ambao wakati mwingine wanakuwa na majukumu memgi.

  0 0
  0 0


  0 0

   Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, (wakwanza kulia), akiungana na Mbunge wa viti maalum, Angela Kairuki, (wapili kulia), mkurugenzi w manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, Photidus Kagimbo, watatu kulia), mganga mfawidhi wa hospitali ya Temeke, Dkt. Amani Malima, (wane kulia) na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Dkt. Sylvia Mamkwe, (wakwanza kushoto), wakati PSPF, ikikabidhi msaada wa vitanda, mashuka na magodoro kwa hospitali hiyo, Desemba 7, 2015. Msaada huo ni utekelezaji wa ahadi ya Mfuko baada ya kuombwa na Mh. Angela Kairuki.
   
   Mbunge wa viti Maalum, Angella Kairuki, (wapili kulia), akipokea msaada wa vitanda, kutoka kwa Afisa Uhusiano  Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, kwenye hosptali ya Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam Desemba 7, 2015. Mfuko huo umetoa msaada wa vitanda, magodoro na mashuka ili kuunga mkono juhudi za serikali za kumaliza tatizo la vifaa tiba kwenye hosipatli za umma. Kulia ni .. Muuguzi mwandamizi wa hospitali hiyo.


older | 1 | .... | 1048 | 1049 | (Page 1050) | 1051 | 1052 | .... | 3286 | newer