Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110104 articles
Browse latest View live

TAARIFA KWA UMMA


HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI LEO

$
0
0
SIMU.TV: Wakazi wa kisiwa cha Songosongo Mkoani Lindi wameiomba serikali kufuta nia ya kuwahamisha kisiwani humo na kumpa mwekezaji. 
SIMU.TV: Serikali imesema haina mpango wa kuyafunga maduka binafsi ya dawa yaliyoko katika Hospitali mbalimbali nchini. https://youtu.be/rz9uHSFL63k 
SIMU.TV: Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania TUCTA limekemea na kukataa ukandamizaji unaofanywa na baadhi ya waajiri.   https://youtu.be/ERm7gZJPk6g  
SIMU.TV: Mabondia Francis Cheka na Thomas Machali wamezidi kutunishiana misuli  zikiwa zimebaki siku chache ya pambano lao litakalofanyika Morogoro; https://youtu.be/gFa8JmmFK10
SIMU.TV: Meli ya Mapinduzi yawasili katika bandari ya Zanzibar.Ikiwa ni agizo la Rais Shein kupunguza kero ya usafiri visiwani humo;  https://youtu.be/090PxmIefqQ 
SIMU.TV: Timu ya vijana chini ya miaka 15 imeendelea na mazoezi Jijini Mwanza ikiwa ni maandalizi ya mechi za kimataifa https://youtu.be/h7RdV7qf2Xc
SIMU.TV: Kutana na mtumishi wa Mungu akiwasisitiza wananchi kushiriki  katika agizo la tarehe 9 December na kufanya kazi katika hofu ya Mungu. https://youtu.be/xiduTZ5pbMk 
SIMU.TV: Yajue mengi kuhusu changamoto mbalimbali zinazowakabili watoto na watu wenye mahitaji maalumu katika jamii ya kitanzania. https://youtu.be/6kXq10dqA9s
SIMU.TV: Pata habari kutoka kwa Meneja mkuu wa gesi, akikujuza kuhusu sheria mpya za gesi na mafuta pamoja na faida kwa wanachi wake https://youtu.be/un8cPxVXx08
SIMU.TV:  Ungana na msemaji mkuu wa TANESCO Badra Masoud akikuhabarisha jinsi walivyojipanga katika sekta ya umeme, gesi na mafuta.https://youtu.be/rGG3deNJxHE

UBUNIFU.......

$
0
0
Muhindi yupo kazini katika kusaka hela katika mitaa ya Jiji la Roma nchini Italy, niliipenda sana hii....maana mpaka ugundue kuwa kaweka chuma linalopita mkononi linalopita mgongoni hadi kufika kwenye makalio ambako kuna kitako alichokalia, tayari utakuwa umefurahi sana...utafikiri kweli anaelea elea juu, kumbe ni mbinu na ubunifu tuu za kumpatia riziki.....hapa kupiga picha nae lazima uangushe hela (Euro) hapo chini kwenye kibakuri kidogo kilichopo mbele yake, na kuna mtu pembeni yake anayelinda na kuruhusu upige nae picha, kama hutoi hela anakutimua.

Maisha ni kutafuta sio kutafutana....anajipatia ridhiki yake mdogo mdogo. Hapa ni mitaa ya kati ya Jiji la Roma, majuzi kati nikiwa huko kutembea.
Picha na Mdau Baraka Chibiriti.

INTRODUCING Nkukundie by Mnyambudu

BEI YA MADAFU LEO

Balozi Mero ashiriki Mkutano mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Viwanda Duniani (UNIDO) unaofanyika Vienna, Austria

$
0
0
Balozi Modest Jonathan Mero, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataiafa na Mashirika mengine ya Kimataifa Geneva na Vienna akiwasilisha hotuba ya Tanazania katika mkutano mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Viwanda Duniani ambao unajadili maendeleo endelevu ya viwanda kama njia mbadala ya kuzikwamua nchi maskini. Mkutano huu unafanyika jijini Vienna, Austria kuanzia tarehe 30 Novemba hadi tarehe 4 Desemba 2015.

Katika hotuba yake, Mhe. Balozi Mero, pamoja na mambo mengine aliwaleza wajumbe wa mkutano huo hatua mbali mbali ambazo zimekuwa zikichukuliwa na Serikali ya Tanzania kwa lengo la kukuza viwanda nchini ikiwa ni pamoja na mafanikio ambayo yamefikiwa hadi sasa.

Mhe. Balozi Mero pia alizungumzia juu ya mapitio ya Mpango wa Kitaifa wa Maendeleo wa awamu ya pili (National Development Plan Phase Two) ambao utatekelezwa na Serikali kuanzia 2016/2017 hadi 2020/2021 ambao pamoja na mambo mengine umeweka msisitizo wa kukuza viwanda kwa lengo la kuongeza thamani ya rasimali zetu, kukuza mahitaji ya ndani ya bidhaa za viwandani na kuongeza ajira kupitia viwanda, Sekta nyingine za uzalishaji, huduma duniani.

BALOZI SEIF ALI IDDI AMTEMBELEA RAIS MAGUFULI, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe  Joseph Magufuli kulia akifurahia jambo na makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif  Ali Iddi aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dkt. John Pombe Joseph Magufuli kulia akizungumza na Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefika Ikulu jijini Dar es Salaam kwaajili ya mazungumzo. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dkt. John Pombe Joseph Magufuli  kulia akiagana na makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya kufanya nae mazungumzo ikulu jijini dar es salaam. 

TAFFA WAMFAGILIA MAGUFULI, WATAKA BANDARI KAVU ZIFUTWE

$
0
0
 Rais wa Chama cha Wakala wa Forodha Tanzania (Taffa), Stephen Ngatunga (kushoto), akizungumza kuhusiana na kazi inayofanywa na serikali katika kudhibiti wizi na ukwepaji wa kodi na ushuru unaofanywa na Idara ya Forodha katika Mamlaka ya Mapato (TRA) na wafanyabiashara wasiowaadilifu wakati wa mkutano na waandishi wa habari ofsini kwake, Dar es Salaam jana. Kulia ni Naibu Rais, Edward Urio.
 Baadhi ya wanahabari wakiwa katka mkutano na viongozi wa TAFFA, jijini Dar es Salaam jana. 

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam. 
CHAMA cha Wakala wa Forodha Tanzania (Taffa), kimeitaka serikali kuzuia matumizi ya bandari kavu isipokuwa pale bandarini kunapokuwa hakuna nafasi ili kudhibiti wizi na ukwepaji wa kodi za serikali unaofanywa na wafanyabiashara kwa kushirikiana na wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato (TRA).

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, Rais wa Taffa, Stephen Ngatunga alisema wizi na ukwepaji wa mapato ya serkali ni jambo la muda mrefu sana na serikali imeishapoteza mabilioni ya shilingi hadi hivi sasa na wizi huo unachangiwa na bandari kavu.

Alisema haoni sababu kwanini bandari hizo zisitumike pale tu kunapokuwa hakuna nafasi bandarini na badala yake sasa imekuwa jambo la kawaida makontena na mizigo mingine kuletwa bandari kavu moja kwa moja wakati hivi sasa bandari ni tupu haina msongamano wowote kama miaka ya nyuma.
 “Wizi na ukwepaji wa mapato ya serikali huanzia hapo” alisema na kuongeza kuwa wanajua njia zote ambazo zinatumika kuiba mapato ya serikali isipokuwa hawakuwa na pa kusemea kwa kuwa hata walipokuwa wakitoa taarifa mtandao huo wa uhalfu ulikuwa una mkono mrefu.

Alisema walitumia njia mbalimbali kujaribu kufikisha kwa serikali njama zilizokuwa zinatumika kuiba mapato ya serikali bila mafanikio na hivi sasa wapo tayari kwa lolote kwani mkombozi sasa amepatikana ambaye ni Rais John Magufuli.

“Kutokana na kasi ya utendaji wa viongozi wapya, matuko yaliyojitokeza katika idara ya frodha ya Mamlaka ya Mapati (TRA) tukiwa wadau wakuu, baadhi ya wanachama wetu wameguswa kwa njia moja au nyingine ndo maana tunaongea leo” aisema.

Alibainisha kipindi kirefu waipigia kelele hali hiyo lakini hawakusikiizwa na wizi unafanywa na kundi la watu wachache ambao hawafiki hata 10 ambao walikuwa wamehodhi biashara ya kuingiza na kutoa mizigo bandarini huku wakimiliki bandari kavu katika maenero mbalimbali jijini ambazo wanazitumia sivyo.

Naibu Rais wa Taffa, Edward Urio alisema chama chao hakitakuwa na huruma kwa wakala ambaye amehusika au atakayekamatwa akihusishwa na wizi na ukwepaji kodi unaoibuliwa hivi sasa na akibainika watamfukuza katika chama na picha, jina lake na la kampuni vitachapishwa katka vyombo vya habari iwe fundisho kwa wengine.

WATU WANNE WAMEUWAWA KWA KUKATWA NA MAPANGA MKOANI GEITA

$
0
0
Watu wanne wameuwawa kwa kukatwa na mapanga na watu wasiofahamika mkoani Geita kutokana na imani za kishirikina.

WWF YAIJENGEA UWEZO HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI

$
0
0
Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha, Dk Bakari Salum akifungua mkutano wa Wasaa wa Mazingira (Earth Hour City Challenges) kwa watumishi wa halmashauri ya Jiji la Arusha unaowajengea uwezo kuweka mipango inayoendana na mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika kwenye hotel ya Palace jijni Arusha kushoto ni Mratibu wa mradi wa nishati wa shirika la Utunzaji wa mazingira duniani(WWF- Tanzania)Dk Teresia Olemako.
Mratibu wa mradi wa nishati wa shirika la Utunzaji wa mazingira duniani(WWF- Tanzania)Dk Teresia Olemako akizungumza kwenye mkutano wa Wasaa wa Mazingira(Earth Hour City Challenges).
Watumishi wa halmashauri ya Jiji la Arusha wakifatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa zenye lengo la kulifanya Jiji kuwa la mfano barani Afrika. 

MKUU WA MKOA AZINDUA MTAMBO MAALUM ULIONUNULIWA NA MANISPAA YA KINONDONI

$
0
0

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadick akipanda kwenye mtambo maalum wa kuchimbia mitalo (Scaveter), wakati wa uzinduzi uliofanyika leo jijini Dar,Mtambo huo umenunuliwa na Manispaa ya Kinondoni  kwa  thamani zaidi ya Sh. Milioni 600.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni ,Mussa Natty akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadick baada ya kuzindua scaveter iliyonunuliwa na Manispaa hiyo leo  katika viwanja vya Manispaa , jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii

WAZIRI MKUU AVAMIA TENA BANDARINI NA TRL,AKUTA MAKONTENA 2431 YEMETOKA BILA KULIPIWA KODI.

$
0
0
  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua bandari ya Dar es salaam  Desemba 3, 2015 ambako alikwenda kupata ukweli kuhusu makontena 2,431 yaliyopitia kwenye bandari hiyo bila kulipiwa kodi ya serikali.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mfumo wa kukagua makontena bandarini kwa kutumia scaner huku akipata maelzo kutoka kwa Ofisa wa forodha, January Shauri wakati alipotembelea bandari ya Dar es salaam Desemba 3, 2015  kutaka kujua ukweli wa tuhuma za makontena 2431 yaliyopita bandarini hapo bila kulipiwa kodi ya serikali.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu utoaji bili za kulipia kodi za serikali kwa watumiaji wa bandari ya Dar es salaam kutoka kwa ofisa mwandamizi wa masuala ya fedha , Bw. Sartho Mbuya wakati alipotembelea bandari hiyo  Desemba 3, 2015 kutaka kujua ukweli wa tuhuma za makontena 2431 yaliyopita bandarini hapo bila kulipiwa kodi za serikali. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimwonyesha Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es salaam, Bw. Abel Mhanga (kulia) orodha ya makontena 2,431 yaliyopitia kwenye banda ya Dar es salaam bila kulipiwa kodi wakati alipofanya ziara kwenye bandari hiyo Desemba ,3, 2015. 
 Waziri Mkuu,  Kassim Majliwa  akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli nchini TRL wakati alipotembelea stesheni ya Dar es salaam kukagua uendeshaji wa Shirika hilo Desemba 3, 2015. 
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akitembelea steheni ya reli ya Dar es salaam Desemba 3, 2015.


WAZIRI MKUU ATINGA TENA BANDARINI NA TRL
*Akuta makontena 2,431 yametoka bila kulipiwa ushuru
*Ataka majina yaletwe ofisini leo saa 11 jioni
*Atoa wiki wiki moja kwa mfumo wa malipo kubadilishwa
*Akagua mabehewa, awaweka kiporo TRL

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara nyingine ya kushtukiza bandarini na kukagua mfumo wa upokeaji na utoaji mizigo na utozaji wa malipo baada ya kupewa taarifa kwamba kuna makontena 2,431 yametolewa bila kulipiwa ushuru.

Waziri Mkuu alisema kwa mujibu wa taarifa ya ukaguzi wa bandari ya kuanzia Machi hadi Septemba 2014, makontena hayo yalipita bila kulipiwa kodi kupitia bandari kavu nne (ICDs) ambazo ni JEFAG, DICD, PMM na AZAM.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ni watumishi 10 tu ambao wamesimamishwa kazi kutokana na makosa hayo. “Mmeamua kuwasimamisha kazi watu wadogo na kuwaacha wakubwa wanaendelea na kazi. Hatuwezi kuendelea kuikosesha Serikali mapato namna hii,” alisema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu amemtaka Kaimu Meneja wa Bandari, Bw. Hebel Mhanga amletee ofisini majina ya watumishi wote waliohusika na ukwepaji kodi huo ifikapo leo saa 11 jioni. Pia amempa Meneja huyo wiki moja kuhakikisha kuwa mamlaka hiyo inabadilisha mfumo wa utozaji malipo kutoka kwenye billing system na badala yake kuweka mfumo wa malipo wa kielektroniki (e-payment).

Ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Desemba 3, 2015), wakati akikagua idara mbalimbali za mamlaka ya bandari na kuona ukaguzi wa mizigo unavyofanyika kwa kutumia scanners. Akiwa kwenye chumba cha scanner mojawapo, Waziri Mkuu alikuta manifest moja ikisema kontena limejaa diapers lakini picha ya kwenye kompyuta ya scanner ilionyesha kuwa ndani ya kontena hilo kuna vitu kama vifaa vya umeme.

Kwa mujibu wa Kaimu Meneja Bandari upande wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Ben Usaje ambaye pia ni msimamizi wa kitengo cha scanner, inapobainika taarifa kama hiyo inapaswa itumwe kwa wenye ICDs ili wafanye ukaguzi kwa kulifungua kontena ili kuhakikisha mali zilizomo ndizo zilizoandikishwa kwenye manifest.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa amefanya ziara ya kushtukiza kwenye ofisi za Shirika la Reli (TRL) na kukagua mabehewa yaliyokuwepo kisha akazungumza na baadhi ya wafanyakazi waliokuwepo kwenye stesheni hiyo ambako alibaini madudu kwenye malipo ya mishahara na makato ya michango ya wafanyakazi.

Akizungumza na Mkurugenzi Mkuu TRL, Mhandisi Elias Mshana, Waziri Mkuu alisema amefika kwenye shirika hilo ili kujifunza utendaji wao kazi lakini anazo taarifa za wao kupewa fedha na Serikali kiasi cha sh. bilioni 13.5/- ili waendeleze miundombinu ya reli lakini hawakufanya hivyo. “Nia ya kuwapa fedha hizo ilikuwa ni kuboresha miradi ili muweze kujiendesha kibiashara lakini nyie mkaamua kujilipa wenyewe,” alisema.

“Ninazo taarifa kuwa baada ya hapo, mlikopa sh. bilioni 3 kutoka benki ya TIB ili kuendesha miradi ya shirika lakini badala ya kufanya miradi, fedha hizo mkaamua nazo kujilipa mishahara. Sasa sijui mnarudishaje huo mkopo wakati hakuna mradi wowote uliofanyika,” alihoji bila kupata majibu.

Alipoulizwa wafanyakazi wana matatizo gani hapo TRL, Katibu wa TRAWU, Bw. Boaz Nyakeke alisema wanadai malimbikizo ya makato yao kwenye mifuko ya pensheni, malimbikizo ya makato kwenye SACCOS na malimbikizo ya kuanzia Julai – Novemba 2014.

Waziri Mkuu kwa upande wake alimtaka Mhandisi Mshana asimamie uboreshaji huduma za usafiri wa treni katika Jiji la Dar es Salaam ili hata mabasi ya mwendo kasi yatakapoanza wananchi waweze kuwa na uhuru wa kuchagua aina ya usafiri wautakao.

“Tunataka kujenga yadi kubwa nje ya mji ili watu wenye magari wawe wanayaacha huko na kutumia usafiri wa treni au DART kuja mjini kama njia mojawapo ya kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salaam,” alisema.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
ALHAMISI, DESEMBA 3, 2015.


DIRA YA DUNIA ALHAMIS 03.12.2015

NHIF YAJA NA MPANGO WA BIMA YA AFYA KAYA KWA KAYA

$
0
0
 Mwakilishi wa Kaimu Mkuruegenzi Mkuu wa NHIF, Eugen Mikongoti akifungua kikao kilichowashirikisha wenyeviti wa bodi na makatibu wa Vituo Vya Afya, Zahanati na Hospitali wa Manispaa ya Temeke juu ya mpango wa bima ya afya kwa kayo iliyofanyika leo jijni Dar es Salaam.
 Meneja wa Mkoa wa Temeke wa NHIF, Costantino Makala akitoa maada katika kikao hicho leo latika ukumbi wa Temeke jijini Dra es Salaam.wa katikati ni Mwakilishi wa Kaimu Mkuruegenzi Mkuu wa NHIF,Eugen Mikongoti Kushoto ni Mganga Mkuu wa Manispaa Temeke,Silvia Mamkwe.
Sehemu ya Wenyeviti wa Bodi na Makatibu wa Vituo vya Afya ,Zahanati na Hospitali katika kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umesema mpango wa huduma ya afya katika kaya utasaidia upatikanaji wa huduma bora ya matibabu kwa jamii kutokana na mchango wao wa uanachama.

Akizungumza leo Wenyekiti wa Bodi na Makatibu Afya wa Manispaa ya Temeke, Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Eugen Mikongoti amesema sharia iko tayari kwa ajili ya mpango huo kinachotakiwa ni utekelezaji kwa wananchi katika kupata huduma hiyo.

Mikongoti amesema kuwa kila mtu mmoja katika kaya kwa Manispaa ya Temeke atachangia Sh.50000 ambapo atapata matibabu kwa mwaka mmoja katika Vituovya Afya,Zahanati na Hospitali katika Manispaa hiyo.

Amesema fedha ambazo watachangia zitatumika katika kununua dawa na vifaa tiba katika Manispaa hiyo hivyo kila mwananchi atakayejiunga na mpango huo matibabu kwa kutambua mchango wake na dawa lazima ziwepo pamoja na vifaa tiba.

Mikongoti amesema kuwa fedha zinazochangwa na wanachama katika mpango ho zitatumika kwa malenfo yaliyokusudiwa na serikali itachangia asilimia 50.

Amesema NHIF itahakikisha kila mwananchi anakuwa na bima ya afya ili kuweza kupata matibabu yake wakati akifikwa na magonjwa kwani wakati mtu anaweza kuugua ugonjwa na kuweza kushindwa kupata matibabu kutokana na kutokwepo katika mapango wowote.

“NHIF itakuwa karibu na wananchi kama tunavyofanya nia yetu ni kutaka kila mwananchi anakuwa na bima ya afya ya kumfanya maisha yake yawe  mazuri ya uhakika wa matibabu”amesema Mikongoti.

RAIS MAGUFULI AHUTUBIA VIONGOZI NA WAWAKILISHI WA UMOJA WA SEKTA BINAFSI NCHINI - TPSF IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Viongozi na Wawakilishi wa Umoja wa Sekta Binafsi nchini (Tanzania Private Sector Foundation - TPSF) katika ukumbi wa mkutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 3, 2015 PICHA NA IKULU


SERIKALI YATAKA KILA KAYA KUWA NA CHOO BORA

$
0
0
SERIKALI imewaagiza maafisa  wa  afya nchini  kuhakikisha  kila kaya inakuwa  na choo bora  ikiwa ni hatua ya kuhakikisha  jamii inaepekana  na magonjwa  yanayotokana na uchafu  mazingira , sambamba  na   suala la usafi wa mazingira  kuwa endelevu  kama ilivyoagizwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.  John Pombe Magufuli.
Aidha Serikali imepiga marufuku ulaji wa matunda yaliyomenywa barabarani.

Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donan Mmbando(Pichani),wakati wa mkutano wake na  waandishi  wa habari  uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa  wizara hiyo.

Katibu Mkuu huyo ambaye alikuwa ameambatana na baadhi ya viongozi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na Ofisi ya Waziri Mkuu, wakiwemo wa wizara yake kwa ajili ya kuzungumzia mambo matatu ambayo ni  suala la usafi  wa mazingira  katika kuadhimisha siku ya  Uhuru ,Desemba 9, mwaka 2015, ugonjwa wa kipindupindu na  polio.
“Wakuu wa mikoa na wilaya wanatakiwa kutekeleza agizo hili kwa kujiwekea utaratibu wa kufanya usafi maeneo yao,” alisema Dkt. Mmbando.

 Dkt. Mmbando alisema  ikumbukwe kuwa ugonjwa wa kipindupindu pamoja na magonjwa mengine yanayohusiana na uchafu huenea kwa kasi kutokana na hali duni ya usafi katika maeneo tunayoishi. Hivyo takwimu zinaonesha kuwa kati ya taka ngumu zinazozalishwa ni 50% tu huzolewa na kupelekwa dampo. Kiasi cha taka kinachobaki huzagaa katika maeneo mbalimbali hususani kando kando ya barabara, katika maeneo ya kukusanyia taka (Collection points), chini ya madaraja na katika maeneo ya wazi hali inasayobabisha miji yetu kuonekana michafu. 

TANZANIA YATUNUKIWA CHETI KWA KUTOKOMEZA UGONJWA WA POLIO

$
0
0
(Pichani ni Watoto walioathirika na Polio. Picha kwa hisani ya shirika la WHO).
Na Magreth Kinabo.
TANZANIA imetangazwa rasmi kuwa ni mojawapo ya nchi isiyokuwa na ugonjwa wa polio katika nchi za Afrika katika mkutano wa Tume ya Afrika ya kuthibitishwa kutokomezwa kwa polio(Afrika Regional Certification Commission for Polio Eradication).

Kutangazwa kulifanyika katika mkutano huo uliofanyika nchini Madagascar, Novemba 26, mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donan Mmbando wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu ugonjwa huo ulifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo jijini Dar es Salaam.

“Hii inamaanisha kuwa kwa sasa hatuna ugonjwa wa polio tena nchini kwa sababu tumeweza kuwafikia watoto wengi zaidi kwa kuwapatia chanjo ya polio na hivyo kuongeza kinga kwenye jamii.Kutokana na mafanikio hayo, tunatakiwa bado kuendelea na kutoa chanjo ya polio kwa watoto wote stahiki ili kuongeza kinga kwa jamii pamoja kuimarisha mfumo wa ufutiliaji wa mgonjwa yoyote mwenye ulemavu wa ghafla,” alisema Dkt. Mmbando.

Katibu Mkuu huyo alifafanua kwamba mgonjwa wa mwisho wa polio alipatikana Julai mwaka 1996 hapa nchini.

Aliongeza kuwa ufuatiliaji wa magonjwa yanayokingwa na chanjo uliimarishwa na kufikia viwango vinavyo kukubalika kimataifa na kuthibitisha kuwa watoto wenye umri chini ya miaka 15 waliopata ulemavu wa ghafla wanapatikana na sampuli zao kuchukuliwa mara moja. 

Hivyo kuanzia mwaka 1997 mpaka Oktoba 2015 jumla ya sampuli 6,249 za watoto waliopata ulemavu zilipelekwa kwenye maabara za kimataifa na kuthibitishwa kuwa hakuna sampuli iliyoonesha uwepo wa ugonjwa wa polio.

Dkt. Mmbando aliongeza kwamba wizara yake kupitia Mpango wa Taifa wa Chanjo imekuwa ikihakikisha kwamba watoto wote Tanzania wanapata chanjo zenye ubora ili kuwakinga dhidi ya magonjwa ya milipuko ikiwemo ugonjwa wa polio.

“ Mwitikio wa wananchi kwa huduma za chanjo umeendelea kuwa mkubwa kwa takribani miaka kumi iliyopita na kufikia viwango vya zaidi ya asilimia 90 kwa kila chanjo kitaifa na wilaya zaidi ya asilimia 80 kufanya vizuri katika kutoa huduma za chanjo,” alisema Dkt. Mmbando.

Ugonjwa wa polio ni ugonjwa wa kuambukizwa unaosababishwa na virusi vya polio, unaathiri misuli na mfumo wa fahamu hivyo kusababisha kupooza kwa viungo hasa na miguu na wakati mwingine kusababisha hata kifo .

Alisema ulemavu huo ukishajitokeza huwa ni wa kudumu, waathirika wakuu wa ugonjwa huo ni watoto hasa waliaochini ya umri wa miaka mitano.

Aliongeza kwamba ugonjwa huo unazuilika kwa chanjo ya polio ambayo ni salama na inatolewa bure na Serikali katika vituo vyote vya huduma ya afya.

Dkt. Mmbando alitoa pongezi kwa wananchi wote wakiwemo viongozi na watendaji wa ngazi zote kwa ushirikiano wao ambao umeifikisha Tanzania kwenye ramani ya dunia ya kutokuwa na ugonjwa huo.

Aidha wizara imewashukuru wajumbe wa kamati mbalimbali za kutokomeza ugonjwa huo chini ya uongozi wa Profesa Ester Mwaikambo, watendaji wa Mpango wa Taifa wa Chanjo na wadau wa chanjo, wadau wa mfuko wa pamoja wa Pamoja wa Afya , WHO, GAVI, UNICEF, CHAI, USAID,
REDCROSS NA LIONS CLUB kwa kazi kubwa ya kuhakikisha kila mtoto mlengwa anapata chanjo.

Tanzania ni miongoni mwa nchi nne ambazo zimepata cheti hicho mwaka huu, katika bara hilo.Pia ni nchi ya 33 kati ya nchi 47 za bara hilo ziliowahi kupata cheti hicho. 

Katika bara hilo bado nchi 14 ambazo hazijawahi kupata cheti hicho.

WAFANYAKAZI WA PSPF WATEMBELEA VYOMBO VYA HABARI JIJINI DAR

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu akifafanua jambo kwa Wahariri wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) alipotembelea Makao Makuu ya MCL, Tabata Relini jijini Dar es salaam, kulia ni watendaji wa PSPF
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Bw. Francis Nanai (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugezi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, baada ya kikao kazi kati ya Wahariri wa Mwananchi na Watendaji wa PSPF, kushoto ni Bw. Daniel Mwaijega Meneja Utawala Idara ya Habari na kulia ni Bibi. Matlida Nyalu Afisa wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa PSPF.
 (Picha zote na Abdul Njaidi).


MKURUGENZI Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu aliongoza ujumbe wa watendaji wakuu wa PSPF kutembelea vyumba vya habari vya magazeti ya Mwananchi na Majira, ikiwa ni utaratibu wa PSPF wa kutembelea vyombo vya habari kwa lengo la kufahamiana, kutolea ufafanuzi masuala mbalimbali na kupokea ushauri wa kuboresha huduma za PSPF. 

Katika ziara hiyo iliyofanyika Desemba 2, 2015, Mkurugenzi wa PSPF aliongozana na Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji, Bw. Gabrilel Silayo, Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bibi Neema Muro, Mkurugenzi wa TEHAMA, Bw. Andrew Mkangaa, Meneja wa Mawasiliano, Masoko na Uenezi, Bibi. Costantina Martin, Afisa kutoka Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa PSPF, Bibi. Mathilda Nyallu na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF Bw. Abdul Njaidi. 

Kituo cha kwanza cha safari hiyo ilikuwa katika ofisi za gazeti la Majira wachapishaji wa Gazeti la Majira na Business Times ambapo walikutana na watendaji wakuu wa kampuni hiyo. 

Pia viongozi hao wa PSPF walitembelea ofisi za Mwananchi Communications zilizopo Tabata, ambapo walikutana na watendaji wakuu wa gazeti hilo. Katika maeneo yote watendaji wa PSPF walijibu maswali mbalimbali, walipokea ushauri na kutambulisha huduma ya Bima ya Afya inayotolewa na PSPF kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya. 

“Lengo la ziara hizo ni kuwatembelea wenzetu wa vyombo vya habari kwa lengo la kufahamiana, kutolea ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali ya PSPF na kujifunza kutoka kwao jinsi ya kuboresha huduma zetu, pia kwa sasa tunatangaza huduma yetu mpya ya Bima ya Afya,hivyo tupo katika mpango wa kuwaelimisha waandishi wa habari ili na wao waweze kuelimisha umma juu ya mpango huo ambao ni mkombozi kwa watanzania wengi…huu ni mwendelezo kwani tulianza ziara hizi tangu mwaka jana,” alifafanua Bw. Mayingu.

HUAWEI TANZANIA YAKUTANA NA WADAU WA HABARI JIJINI DAR

$
0
0
Mkuu wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Huawei, Jimmy Jin akizungumza na waandishi wa habari wa Tanzania na China wakati wa mkutano na waandishi hao uliofanyika Makao makuu ya Kampuni hiyo jijini Dar es Salaam mwanzoni mwa wiki wenye malengo ya kuweka mahusiano mazuri na kati ya waandishi wa habari na Kampuni hiyo.

 Kampuni ya Huawei Tanzania leo hii imewakaribisha waandishi wa habari mbalimbali jijini Dar Es Salaam kupata chai ya asubuhi pamoja na mkutano mfupi kuelezea mafanikio yake na mipango yake katika tasnia ya uandishi wa habari. Mkutano huu umefanyika katika ofisi za Huawei zilizoko Golden Jubilee Towers jijini Dar Es Salaam.

Mkutano huu uliwakutanisha waandishi wa Habari wa Tanzania na waandishi wa Habari raia wa China walioko Dar Es Salaam, hii ni kupitia muungano wa Wanahabari na Huawei ujulikanao kama Huawei Media Club. Muungano huu una lengo la kujenga mahusiano ya muda mrefu baina ya kampuni ya Huawei Tanzania na waandishi wa habari, pia kuendeleza mpango wa kampuni ya Huawei Tanzania kuendeleza sekta ya Teknolojia ya mawasiliano (IT) hapa nchini.
Akizungumza katika mkutano huu, Bwana Jimmy Jin, Meneja wa Habari wa Kampuni ya Huawei Tanzania aliitambulisha kampuni ya Huawei kama kampuni inayowajibika vema, yenye lengo la kuchochea ubunifu, kushirikiana na serikali kuwezesha sekta ya Teknolojia ya mawasiliano (IT) nchini Tanzania. Aliwakaribisha wanahabari na kusisitiza mawasiliano baina ya Huawei Tanzania na wanahabari katika mipango tofauti ya kuendeleza sekta ya Habari hapa nchini.

Mwandishi Mkongwe wa Habari za Michezo nchini Willie Chiwango afariki dunia.

$
0
0
Marehemu Willie Chiwango

Taarifa kutoka mtoto wa marehemu, Stephen Chiwango (61), zinasema mauti ya limfika baba yao jana saa 5:30 usiku katika hospitali ya Masana iliyopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam alikokua amelazwa kwa matibabu na alikua akisumbuliwa na matatizo ya kichwa.
Alisema kuwa mauti yalimkuta katika hospitalini hapo akifanyiwa vipimo zaidi ili kujua tatizo la mwandishi huyo ambaye chombo chake cha mwisho kukifanyia kazi ni Tanzania Standard Newspapers (TSN) akiwa ni Mhariri Msanifu wa Michezo Gazeti la Daily News.
Alisema kuwa mwili wa Chiwango bado uko Masana na ndugu wanafanya mipango ili kwenda kuuhifadhi katika chumba cha kuhifadhia mahiti cha hospitali ya Lugalo, Mwananyamala au Amana.
Alisema baada ya kuuhifadhi mwili wa mpendwa wao, ndugu watakutana kwa ajili ya mazungumzo ili kujua mazishi yatafanyika lini na wapi.
Marehemu Chiwango ameacha mke na watoto wawili.
Tulimpenda Chiwango, lakini Mungu Amempenda Zaidi!
Viewing all 110104 articles
Browse latest View live




Latest Images