Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1043 | 1044 | (Page 1045) | 1046 | 1047 | .... | 3272 | newer

  0 0

   Mkurugenzii Mkazi wa Taasisi ya kimataifa inayojishughulisha na masuala ya kidemokrasia na utawala bora (The international Republican Institute) Bi. Robina Namusisi akisalimiana na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai alipomtembea Ofisini kwake Dar es Salaam leo kuelezea mipango ya taasisi yake inayokusudia kushirikiliana na Bunge katika kutoa mafunzo ya kidemokrasia kwa Wabunge vijana na wanawake.
   Mkurugenzii Mkazi wa Taasisi ya kimataifa inayojishughulisha na masuala ya kidemokrasia na utawala bora (The international Republican Institute) Bi. Robina Namusisi akimweleza Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai mipango ya taasisi yake inayokusudia kushirikiliana na Bunge katika kutoa mafunzo ya kidemokrasia kwa Wabunge vijana na wanawake. Bi. Namusisi alimtembea Mhe. Ndugai Ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.
   Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akifafanua jambo wakati wa mazungumzo na Mkurugenzii Mkazi wa Taasisi ya kimataifa inayojishughulisha na masuala ya kidemokrasia na utawala bora (The international Republican Institute) Bi. Robina Namusisi alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.  Taasisi hiyo inayokusudia kushirikiliana na Bunge katika kutoa mafunzo ya kidemokrasia kwa Wabunge vijana na wanawake.
  Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya kimataifa inayojishughulisha na masuala ya kidemokrasia na utawala bora(The international Republican Institute) Bi. Robina Namusisi (kulia kwake)alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.  Taasisi hiyo inayokusudia kushirikiliana na Bunge katika kutoa mafunzo ya kidemokrasia kwa Wabunge vijana na wanawake.  Wengine katika picha ni maafisa kutoka taasisi hiyo. Picha na Hassan Silayo, Idara ya Habari Maelezo.

  0 0

  Serikali imewahakikishia Watanzania kwamba mashine ya Magnetic Resonance Imaging (MRI) pamoja na Computerized  Tomography Scan (CT-SCAN) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)  hazitakwama kufanya kazi kwa kuwa imeweka utaratibu mzuri wa kuzitengeneza.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Donan Mmbando amesema serikali imezungumza na Philips na wamekubaliana kwamba mashine hizo hazitakwama na endapo litatokea tatizo la kiufundi watashughulikia mara moja.

  “Mwaka ujao ni mwaka wa bajeti  serikali itatenga fedha kwa ajili ya kutengeneza mashine za CT-SCAN na MRI,  lakini mtambue kwamba si tu mashine hizo zinapaswa kutengenezwa bali na mashine nyingine.”amesema Dk Mmbando.

  Pia, Dk Mmbando  amefungua duka la dawa  la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) ndani ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kueleza kwamba kufunguliwa kwa duka hilo kutasaidia wananchi kupata huduma haraka na kununua dawa kwa gharama nafuu  na huduma hiyo itatolewa kwa saa 24.

  Akifafanua  kuhusu mashine za MRI na CT-Scan, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Lawrence Mseru amesema Novemba 25, 2015  alifika fundi kutoka Afrika Kusini ambaye pia ni fundi wa MRI na kuitengeneza na kuanza kufanya kazi tangu Novemba 26 mpaka Disemba 2, mwaka huu. Wagonjwa 152   wamepimwa na kwamba wengi wagonjwa wa dharura.

  Amesema hivi sasa mafundi wanafunga mashine ya Digital X-Ray iliyotolewa na serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambapo  usimikaji unatarajiwa  kukamilika mwishoni mwa juma hili.

  Akielezea utekelezaji wa agizo la wagonjwa wanaolala chini kupatiwa vitanda, Profesa Mseru amesema ili kuondoa wagonjwa wote waliolala chini, serikali kupitia MSD ilileta vitanda 300 pamoja na magodoro yake, vitanda hivyo vyote vilipelekwa kwenye Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) na tayari MOI imeanza kuhamisha wagonjwa waliokuwa wamelala chini kutoka wodi za MNH walizokuwa wanazitumia, mpaka sasa wagonjwa 120 wamehamishwa.

  Novemba 9, mwaka  huu Rais John Magufuli alifanya ziara MNH na kutoa maagizo kwamba ndani ya wiki mbili mashine ya MRI na CT-SCAN ambazo zilikuwa zimeharibika ziwe zinafanya kazi, wagonjwa waliolala chini wawe wamepata vitanda  na Bohari Kuu ya Dawa (MSD) ifungue duka la dawa ndani ya hospitali ili kuondoa ukosekanaji wa dawa.

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho 
  Maonesho ya utamaduni wa watu wa China yalifanyika jana usiku maeneo ya Makumbusho ya TaifaJijini Dar es salaam baada ya ufunguzi rasmi wa Kituo cha Utamaduni wa watu wa China uliofanyika mchana. 
  Maonesho hayo yalifunguliwa na Mkurugenzi wa kituo hicho cha Utamaduni wa watu wa ChinaTanzania Bwana GAO Wei ambapo alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wageni waalikwakuangalia utamaduni wa wachina kupitia muziki wao. Hafla hiyo ilipambwa na wanamuziki mahiri wa kundi la watafiti wa muziki wa asili linaloitwa Zijincheng kutoka Chuo Kikuu cha Sanaa cha China kilichopo Beijing. 
   Wanamuziki hao walianza kwa kupiga vyombo vyao vya muziki kwa pamoja bila kuimbachochote na baadae kila mmoja wa wanamuziki hao alipiga chombo kimoja cha muziki ilikuwaonyesha wageni waalikwa sauti na mdundo wa kila chombo cha muziki.
   Mwishoni walipiga vyombo vyao kwa pamoja kwa kupiga mapigo ya wimbo wenye asili yakitanzania unaoitwa ‘Malaika Nakupenda’. 
  Kituo cha Utamaduni wa China nchini Tanzania ndio kituo cha kwanza kufunguliwa kwa Afrika Mashariki. Kimefunguliwa rasmi jana saa nne kamili asubuhi.Kituo hicho kipo Barabara ya Hassan Mwinyi maeneo ya Upanga Jijini Dar es Salaam.
  Msanii wa kundi la Zijincheng  kutoka Chuo Kikuu cha Sanaa cha China Yang Jing akionyesha umahiri wa kutumia vifaa vya muziki wakati wa Tamasha la Forbidden City Chamber Orchestra lililofanyika katika ukumbi wa maonyesho wa Makumbusho ya Taifa jana jijini Dar es Salaam.Tamasha hilo lilikuwa maalumu kufuatia kuzinduliwa rasmi kwa Kituo cha Utamaduni wa watu wa China hapa nchini
  Msanii wa kundi la Zijincheng  kutoka Chuo Kikuu cha Sanaa cha China Di Yang akionyesha umahiri wa kutumia vifaa vya muziki wakati wa Tamasha la Forbidden City Chamber Orchestra lililofanyika katika ukumbi wa maonyesho wa Makumbusho ya Taifa jana jijini Dar es Salaam.Tamasha hilo lilikuwa maalumu kufuatia kuzinduliwa rasmi kwa Kituo cha Utamaduni wa watu wa China hapa nchini.
  Mkuu wa Kituo cha Utamaduni wa Watu wa China nchini Tanzania Bw. Gao Wei (watano kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wanamuziki wa kundi la Zijincheng  kutoka Chuo Kikuu cha Sanaa cha China. Kundi hilo linaundwa na wanazuoni na watafiti wa muziki wa asili nchini China.

   Picha na Frank Shija, WHVUM

  0 0

  Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Amos Makalla akiwa kwenye ukaguzi wa kiwanda cha sukari cha TPC kilichopo Moshi, mkoani humo, kama sehemu ya kuangalia hali ya uzalishaji wa sukari kwenye kiwanda hicho. Picha na Mpigapicha wetu.

  Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro

  MKUU wa Mkoa Kilimanjaro, Amos Makalla, amefanya ziara katika kiwanda cha Sukari cha TPC kilichopo Moshi, mkoani Kilimanjaro ili kujionea hali ya uzalishaji wa sukari kwenye kiwanda hicho. RC Makalla alijionea hali halisi ya kiwanda hicho ambacho sasa kinazalisha sukari tani 105,000 baada ya kubinafsishwa, tofauti na uzalishaji wa tani 35,000 tu hapo zamani.
  Ziara inaendelea kiwandani hapo.
  Akizungumza katika kiwanda hicho, RC Makalla alisema kwamba amefurahishwa na hali ya uzalishaji wa sukari kwenye kiwanda hicho, huku akiahidi kushirikiana na uongozi wa Mkoa wa Tanga kudhibiti sukari inayoingia kutoka nje ya nchi. Alisema atashirikiana na serikali ya Mkoa wa Tanga kudhibiti sukari hiyo ya nje, akiamini kuwa kutasababisha kiwanda hicho kupiga hatua kwa kuuza sukari yao nchini.
  Majadiliano yanaendelea kiwandani hapo dhidi ya RC Makalla
  “Kilio cha kiwanda hiki ni uingizwaji wa sukari kutoka nje, hivyo Kilimanjaro tutashirikiana kwa karibu na wenzetu wa Tanga ili kuweka ulinzi mkali kwa ajili ya kudhibiti sukari inayoingia kutoka nje kwa kupitia mkoani Tanga.


  “Naamini tukifanya hivyo tutaweza kukiweka kiwanda hiki katika hali nzuri, ukizingatia kuwa viwanda vyetu ili viweze kujiendesha vinapaswa kuuza bidhaa zao vizuri na si kupata changamoto zinazoweza kuwaathiri kama suala hili la sukari nyingi kuingia kutoka nje wakati wao pia ni wazalishaji,” alisema Makalla.


  Kwa wiki kadhaa sasa RC Makalla amekuwa akifanya ziara mbalimbali mkoani Kilimanjaro pamoja na kufanya vikao muhimu vyenye lengo la kuhakikisha kwamba wanaenda mchaka mchaka ili kwenda sambamba na kauli ya hapa kazi ya Dr John Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  0 0

   Mratibu wa Kitaifa wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa yasiyopewa Kipaumbele, Dkt. Upendo Mwingira akielezea jinsi Serikali inavyojitahidi kupambana na magonjwa hayo, ambayo   baadhia yake  ni Matende, Mabusha, Minyoo ya Tumbo, Kichocho, Trakoma na Usubi kwa baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari  katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii leo jijini Dares Salaam.
  Mratibu wa Kitaifa wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa yasiyopewa Kipaumbele, Dkt. Upendo Mwingira akielezea jinsi Serikali inavyojitahidi kupambana na magonjwa hayo, ambayo   baadhia yake  ni Matende, Mabusha, Minyoo ya Tumbo, Kichocho, Trakoma na Usubi kwa baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari  katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii leo jijini Dares Salaam.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Mkuu wa Shirika la Bandari Mbarouk Hamadi Mbarouk (wa pili kushoto) wakati alipotembelea Eneo la Ujenzi wa Bandari Mpya ya kisasa Mpigaduri Maruhubi Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi itakayojengwa Kampuni ya CHINA HARBOUR ENGINEERING COMPANY LTD (CHEC) kutoka Nchini China,(kushoto) Naibu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Issa Haji Ussi.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akifuatana na Naibu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Issa Haji Ussi (kushoto) Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Dkt.Juma Malik Akili (wa pili kulia)akifuatia Mhandisi Mkuu wa Shirika la Bandari Mbarouk Hamadi Mbarouk (katikati) wakati alipotembelea Eneo la Ujenzi wa Bandari Mpya ya kisasa Mpigaduri Maruhubi Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi itakayojengwa Kampuni ya CHINA HARBOUR ENGINEERING COMPANY LTD (CHEC) kutoka Nchini China.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akiuliza jambo alipokuwa akipewa maelezo na Mhandisi Mkuu wa Shirika la Bandari Mbarouk Hamadi Mbarouk (kushoto) wakati alipotembelea Eneo la Ujenzi wa Bandari Mpya ya kisasa Mpigaduri Maruhubi Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi itakayojengwa Kampuni ya CHINA HARBOUR ENGINEERING COMPANY LTD (CHEC) kutoka Nchini China.Picha na Ikul, Zanzibar.

  0 0


  0 0


  0 0


  0 0

  Mwanamuziki Kasongo Mpinda Clayton (anayeimba) ametutoka leo jioni baada ya kuugua kwa muda mrefu. Kasongo atakumbukwa kama mwimbaji mwenye sauti ya kipekee toka alipoibukia ghorofa ya saba pale New Africa Hotel jijini Dar es salaam akiwa na MK Group, wana Ngulupa Tupa Tupa na baadaye Maquis du Zaire 'Wana Kamanyola' akikonga nyoyo washabiki wa muziki, na baadaye Wazee Sugu chini ya King Kikii. 
  Badhi  ya nyimbo zilizompandisha chati Marehemu Kasongo ni 'SEYA' , 'ANGELOU', 'MUME WANGU MWENYEWE' na 'NSONONEKA' katika mtindo wa 'Ogelea piga mbizi' . Cheza hizo video nne umsikie Kasongo Mpinga....
  Marehemu Kasongo anatarajiwa kuzikwa kesho saa 10 Kinondoni. Msiba upo nyumbani kwake Kinondoni karibu na jengo lenye Benki ya Akiba Commercial Bank jijini Dar es salaam.

  0 0
 • 12/02/15--12:30: SPANISH CULINARY WEEKEND


 • 0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaabani Mwinjaka (katikati) akikata utepe pamoja na Balozi wa Zambia nchini Tanzania Judith Kapijimpanga (kushoto) na Mwakilishi wa Balozi wa China nchini Tanzania, wakikata utepe kuashiria kukabidhiwa kwa kwa mabehewa 18 na vichwa 4 kutoka Serikali ya China.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaabani Mwinjaka na Balozi wa Zambia nchini Tanzania Judith Kapijimpanga, wakielekea kupanda kwenye treni ya kichwa na mabehewa mapya ya TAZARA.
  Moja ya mabehewa mapya.


  0 0

  SIMU.TV: Kortini kwa njama za kumuua Jaji Lubuva. TAZARA ni mshikemshike, serikali yaagiza ifikapo Juni waanze kujilipa mishahara wenyewe.TPA yakomalia wamiliki wa makontena 9 Dar;https://youtu.be/Fl7fkzvEi6U

  SIMU.TV: Serikalini hapakaliki, kasi ya Rais Magufuli yazua hofu kwa wafanyakazi. Wafanyabiashara taharuki tupu. Wizara tano kuhamia Dodoma; https://youtu.be/mZnlcnvVQ_I

  SIMU.TV: Kamishna TRA afunguka tuhuma za ufisadi Uingereza. Mashine za CT-Scan zaanza kazi Muhimbili. Meli mpya yawasili Zanzibar; https://youtu.be/SS7LLyvZC-I

  SIMU.TV: Canavaro, Haji Mwinyi waanza tizi. Waziri Mkuu amtimua Benzema. Pluijm ampa mikoba Ngoma. Pata dondoo za habari za michezo zilizotawala magazetini leo; https://youtu.be/PeMK7pB8qak

  SIMU.TV: TUKTA yavutiwa na Rais Magufuli, yasema inaunga mkono kasi ya kutumbua majipu. Kigogo TRA kizimbani kwa rushwa ya mil.1.5; https://youtu.be/EqDFKiLWa0M

  0 0

  EALA has today debated and adopted the Report of the Committee on the Audited Accounts of the EAC for the Year ended 30th June 2014.

  During debate, Members called for improvement on the financial performance of the Community, review of procurement procedures and adherence to the set regulations.  They further want the absorption of funds by the Community enhanced and reimbursement of all unclaimed Value Added Tax (VAT) followed.

  The report presented to the House by the Chair of the Accounts Committee, Hon Jeremie Ngendakumana, covers the Committees findings arising from the report of the Audit Commission and is divided into seven main parts.  It includes the audit findings on the financial statements of the EAC Secretariat and its Organs and Institutions.  They include the Lake Victoria Basin Commission, the Lake Victoria Fisheries Organisation and the Inter-University Council for East Africa (IUCEA).  The Audited Financial Statements of the Civil Aviation Safety and Security Oversight Agency (CASSOA) are also presented.
  Hon Jeremie Ngendakumana presents the Report of the Accounts Committee to the House.


  The recommendations state that all planned activities should ideally be carried out within the agreed timeframe and to avoid further delays in the implementation of planned activities.  The Report further wants follow-up on disbursement of donor funds and calls on the EAC to comply with all requirements concerning funds in time and at all times.

  On planning, the Committee is of the view that EAC experienced a slow start in implementing the planned activities during the year especially in the first quarter due to limited financial resources as the percentages of remittances by Partner States were low.  As a result, a number of activities were not implemented in good time.

  On Information, Communication and Technology (ICT) matters, the Committee urges the Council of Ministers to ensure the ICT Strategy is implemented at the EAC.  It further wants the Assembly to direct the Council to hire additional staff in the ICT Sector to ensure financial information security of the Assembly.    It also wants due diligence to be undertaken and that EAC adheres to all laid procurement Procedures. 

  Hon Shyrose Bhanji takes the floor during debate on the Accounts Report.

  In his contribution, Hon Yves Nsabimana called for recruitment of staff to enable effective implementation of tasks.  He further called for the implementation of the decisions and directives of the Council of Ministers.  Hon Nsabimana also cited the operationalization of the Protocols as an area that can be better co-ordinated and said it was time for the EAC to inculcate a system that effectively ensures Protocols are enforced.


  0 0

  Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori akizungumza na Afisa Mwandamizi Matekelezo wa NSSF, Theopista Muheta (kulia) na Afisa Masoko na Uhusiano wa NSSF, Aisha Sango wakati wa maonesho ya 16 ya wajasiriamali wa Sekta isiyo rasmi Afrika Mashariki yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
   (Na Mpigapicha Wetu).
  Afisa Matekelezo Sekta Binafsi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Edwin Kafanabo akitoa maelezo jinsi ya kujiunga kwa hiari uanachama wa NSSF wakati wa maonesho ya 16 ya wajasiriamali wa Sekta isiyo rasmi Afrika Mashariki yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. 
  Afisa Matekelezo Sekta Binafsi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Edwin Kafanabo akitoa maelezo jinsi ya kujiunga kwa hiari uanachama wa NSSF wakati wa maonesho ya 16 ya wajasiriamali wa Sekta isiyo rasmi Afrika Mashariki yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. 

  0 0

  Marehemu Hellen Stephen Mbebha wakati wa uhai wake.
  Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai (Mb) akiweka shada la maua juu ya kaburi la aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi Shughuli za Bunge Marehem Hellen Mbebha.
  Katibu wa Bunge la Tanzania Dkt. Thomas Kashilillah akitoa heshima za mwisho kwa kwa mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi Shughuli za Bunge Marehem Hellen Mbebha ambapo mazishi yake yalifanyika katika kijiji cha Kung’ombe wilayani Bunda mkoa wa Mara tarehe 01/12/2015. Aliyesimama ni Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge Bi. Nenelwa Wankanga.
  Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Bunge Mhe. Kangi Lugola na Mhe. Abdulkadir Shah wakiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Hellen Mbebha.


  0 0

  Mwenyekiti wa Muda  wa Jumuiya ya Wanafunzi waliowahi kusoma katika shule ya Sekondari Enaboishu Renalda Shirima akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam juu mkutano wao wa  kwanza utafanyika katika matawi mawili ya mkoa wa Arusha na Dar es salaam kwa ajili ya kuangalia fursa mbalimbali ambazo wanaweza kushirikiana katika kuleta maendeleo ya taaluma katika shule yao ya zamani kwa kuboresha mazingira ya wanafunzi na walimu ya kujifunzia na kufundishia. Kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Zawadi Msalla na kushoto ni Mjumbe wa Jumuiya hiyo George Msonde.

  Na Zawadi Msalla-MAELEZO
  WANAFUNZI waliowahi kusoma katika shule ya Sekondari Enaboishu ya jijini Arusha wanatarajia kukutana tarehe 5 Desemba 2015 ili kujadili masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kuisaidia shule hiyo katika kuboresha maendeleo ya taaluma.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Muda  wa Jumuiya hiyo ya Enaboishu Renalda Shirima alisema mkutano huo wa kwanza utafanyika katika matawi mawili ya mkoa wa Arusha na Dar es salaam. 

  Ambapo katika mkoa wa Dar es salaam utafanyika katika ukumbi wa Triple Seven eneo la Kawe  na Arusha katika club ya AICC Kijenge. 

  Renalda alisema jumuiya hiyo ina malengo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuangalia fursa mbalimbali ambazo wanaweza kushirikiana katika kuleta maendeleo ya taaluma katika shule yao ya zamani kwa kuboresha mazingira ya wanafunzi na walimu ya kujifunzia na kufundishia.

  “Tutaweza kufahamiana kwa karibu zaidi kwa watakao hudhuria na pia kupata mawasiliano ya wale ambao hawata hudhuria, hii pekee ni chachu ya kuleta maendeleo” alisema Renalda.

  0 0

  Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam,(DAWASCO), limeanza rasmi kutumia bei zake mpya za ankara ya Maji, ikiwa ni siku chache tu baada  ya Mamlaka ya Udhibiti wa huduma ya  Nishati na Maji (EWURA) kupitisha  mapendekezo ya kupandisha gharama hizo zilizotolewa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) ili kusaidia kuboresha  huduma ya Majisafi na salama jijini Dar es salaam, Kibaha, na Bagamoyo mkoani Pwani.

  Gharama hizo mpya ambazo zimeanza rasmi kutumika Disemba 01, zimepanda kutoka kiasi cha shilingi 1098 kwa unit 1 ya ujazo wa Maji ambayo ni sawa na lita 1000, hadi kufikia shilingi 1663  ambazo ni sawa na ongezeko la asilimia 51%. 

  Ilielezwa kuwa Kupitishwa kwa mapendekezo hayo kutaongeza uwezo wa DAWASCO kufanya maboresho ya huduma za Maji na kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo kwa wateja na kuwafanya wateja hao kuwa na uhakika wa huduma hiyo kwa kukamilisha miradi mbalimbali mikubwa ya Maji ambayo tayari ipo katika hatua zake za mwisho.

  Wakizungumzia gharama hizo mpya za Maji wakazi wa jijini  Dar es salaam, wametoa maoni yao kuhusu ongezeko hilo jipya la bei za maji, ambapo wengi wao wameonesha kuridhika na bei hiyo mpya lakini wameiomba Dawasco kuhakikisha inawapatia huduma hiyo kulingana na mahitaji yao huku ikiendana na gharama iliyoongezwa. 

  “Sisi hatuna shida kabisa na hiyo bei, tunachotaka ni maji, Dawasco wahakikishe wananchi tunapata huduma hiyo bila usumbufu wowote, sio mnaongeza bei halafu maji yenyewe hatupati, hapo hatutakubali kabisa” alisema Bi. Penieli Tenga mkazi wa Mwananyamala.

  Mkazi mwingine wa Kinondoni Bi. Agness Mbwana ameonesha kuridhika na gharama hizo japokuwa hapo awali hakuwa na taarifa za ongezeko hilo la maji, mkazi huyo ameiomba Dawasco kutoa taarifa mapema ili wanapopata bili zao wasishangazwe na kiasi cha bili kilicholetwa.

  Kwa upande wa DAWASCO, Kaimu Meneja Uhusiano Bi Everlasting Lyaro alisema bei hiyo mpya imeanza kutumika rasmi desemba mosi na wanaendelea kuwaelimisha wananchi wa maeneo mbalimbali juu ya ongezeko hilo ili kuepuka usumbufu wakati wa ulipaji wa bili.

  “tumeanza bei mpya rasmi ya Maji juzi (01/12/2015) kwa sh 1663 kwa unit moja ya Maji ambayo ni sawa na lita za ujazo 1000. Tulishawaandaa wateja wetu kuipokea bei hiyo kwa kuwaelimisha na pia kupitia njia za mawasiliano za shirika kama vile Tovuti, Magazeti na hata ujumbe mfupi wa simu ya Mkononi ili wajue kiasi cha Maji watakachochajiwa kwa mwezi huu wa disemba” alisema Lyaro.

  Mnamo Mwezi novemba 2015. Mamlaka ya udhibiti wa huduma ya Maji na Nishati (EWURA) ilipitisha bei pendekezi ya Maji kwa watumia Maji wa Jiji la Dar es salaam kama ilivyoombwa na Mamlaka ya Majisafi na Majitka Dar es Salaam (DAWASA) kutoka sh 1098 hadi Tsh 1663 kiwa ni ongezeko la ziaid ya asilimia 50 ya bei ya awali.

  0 0

   Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na uvuvi Bi Judith Mhina akifafanua kwa waandishi wa habari kuhusu mradi wa udhibiti wa uvuvi na maendeleo shirikishi Kusini Magharibi mwa bahari ya Hindi “SWIOFISH” leo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano na waandishi wa habari. Kulia ni Mkurugenzi  Msaidizi Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi   Bi Fatma Sobo.
   Afisa Uvuvi kutoka  Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Bw. Silas William akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuwainua wavuvi wadogo hapa nchini ili kushiriki katika kukuza uchumi wa Taifa. Kushoto ni Mkurugenzi  Msaidizi Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi   Bi Fatma Sobo.mwisho kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na uvuvi Bi Judith Mhina.
  Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mkutano kati yao na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ambao pamoja na mambo mengine ulibainisha kuwa Serikali imejipanga kukomesha uvuvi haramu hapa nchini hasa kwa kutumia mabomu kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais,Wizara ya Mali asili na Utalii, Wizara ya Nishati na Madini,Wizara ya mambo ya Ndani na ile ya Katiba na Sheria.
  (Picha na Frank Mvungi-Maelezo)

  0 0

   Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli Mhandisi, Hosea Mbise akizungumza katika mkutano wa tatu wa wawekezaji na wadau wa nishati ya umeme ujulikanao kwa jina la  Powering Africa uliodhaminiwa na kampuni ya Wind East Africa. 
  Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa kampuni ya Wind East Africa John Chaggama akifafanua jambo kuhusiana na uwekezaji wao wa Umeme wa Upepo uliopo mkoani Singida. Chaggama alisema mradi huo utatatua tatizo la nishati hiyo hapa nchini mara utakapoanza rasmi uzalishaji mwishoni mwa mwaka 2017. 
  Wadau na wawekezaji mbali mbali wa nishati ya umeme wakimsikiliza Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli Mhandisi, Hosea Mbise hayupo pichani wakati wa ufunguzi wa mkutano wa tatu wa wawekezaji na wadau wa nishati ya umeme ujulikanao kwa jina la  Powering Africa uliodhaminiwa na kampuni ya Wind East Africa.

  Na Mwandishi wetu
  WAKATI Serikali ikibainisha kuliondoa Shirika la umeme nchini (Tanesco) katika uzalishaji wa umeme, kampuni ya kuzalisha umeme wa upepo (Wind East Africa) imesema itaanza uzalishaji wa nishati hiyo mwishoni mwa mwaka ujao.

  Wakizungumza katika mkutano wa kimataifa wa uwekezaji katika sekta ya umeme, Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli Mhandisi, Hosea Mbise na Mwanzilishi na Mkurugenzi wa wa kampuni ya Wind East Africa, Rashid Shamte walieleza mkakati uliopo katika kuboresha sekta ya umeme nchini ambapo baada ya muda, Tanesco itakuwa na kazi ya usafirishaji tu huku kazi ya uzalishaji ikifanywa na kampuni kama Wind EA.

  Mbise alisema kuwa alisema uzalishaji wa umeme unahitaji uwekezaji wa hali ya juu ikiwamo kutoa fursa kwa kampuni mbalimbali kuanza kuzalisha umeme kwa manufaa ya Taifa.

  Kwa mujibu wa Mbise, hatua za awali za kuliondoa Shirika hilo la umeme nchini kuwa mzalishaji wa nishati hiyo umeanza na ifikapo 2022, Shirika hilo halitajihusisha na uzalishaji wa umeme zaidi ya kazi ya usafirishaji tu.

  "Kwa utaratibu huu, Tanesco sasa itaondoshwa katika mchakato wa kuzalisha umeme na kubaki kuwa msambazaji, hatua tayari zimeanza kwa kuangalia madeni yaliyopo Tanesco na jinsi ya kuyafuta sanjari na kuwachukua watumishi wa Tanesco.

  "Ifikapo 2022 hatutakuwa na Tanesco katika uzalishaji wa umeme bali umeme utazalishwa na kampuni mbalimbali na mkakati uliopo ni kwamba hadi kufikia 2030, asilimia 70 ya Watanzania wawe wamefikiwa na huduma ya umeme," alisema Mbise.

  Kwa upande wake, Shamte alieleza kuwa mradi wa umeme wa upepo wa Singida kwa sasa upo katika maandalizi ya kina kuanza na mwaka ujao watakamilisha taratibu mbalimbali kwa mujibu wa sheria za uwekezaji.

  Shamte alisema kuwa mradi huo ambao utazalisha 100 Mega Watts mbali ya kutatua tatizo la umeme, utaufanya mkoa wa Singida kubadilika kwa kupata maendeleo makubwa kiuchumi, biashara na hata kijamii.

  Alisema kuwa mkataba mikataba ya kumalizia uwekezaji wamradi huo itasainiwa mwanzoni mwa mwezi ujao (Januari 2017).
  Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa kampuni ya Wind East Africa, John Chagama alisema, mradi wa umeme wa upepo utakapokamilika utawanufaisha Watanzania hasa wakazi wa Singida ambako mradi huo unaanzishwa.

  "Kwanza utasaidia kutoa ajira kwa wakazi wa Singida, lakini pia utawanufaisha Watanzania hasa wa kipato cha chini kwani umeme utakuwa wa gharama nafuu," alisema.
  Chagama alisema kuwa umeme wa upepo ni mradi wa kudumu na utawafanya watanzania kupunguza gharama za maisha kwani bei ya umeme itashuka.

older | 1 | .... | 1043 | 1044 | (Page 1045) | 1046 | 1047 | .... | 3272 | newer