Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1039 | 1040 | (Page 1041) | 1042 | 1043 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Mkoa wa Dodoma umeanza rasmi kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli lililotaka kufanyika kwa usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya nchi siku ya tarehe 9 Disemba, 2015 kama mojawapo ya maadhimisho ya siku ya uhuru na kuwataka viongozi na wataalamu kusimamia utekelezaji wa agizo hilo. 

   Uongozi wa Mkoa umeamua kuanza mapema zoezi la ufanyaji usafi pasipo kusubiri tarehe 9 Disemba na umepanga kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu likihusisha usafi wa kila siku na usafi wa siku zote za Jumamosi kuanzia saa 1:00 hadi saa 3:00 asubuhi. 

  Taasisi mbalimbali zilizopo Mkoani Dodoma zimetumia Jumamosi ya jana Novemba 28, 2015 kushirikiana na wananchi kufanya usafi kwenye maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dodoma ambapo Viongozi na Watumishi wote wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Ofisi ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika na Manispaa ya Dodoma wamefanya usafi eneo la Bahi Road kuelekea Nkuhungu kwa kuondoa taka na michanga kwenye mitaro ya maji ya mvua, kufyeka na kuchoma taka eneo la makaburi ya Kizota. 

   Kwa mujibu wa Ratiba ya usafi iliyotolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Mamlaka ya majisafi na usafi wa Mazingira mjini Dodoma-DUWASA ilifanya usafi eneo la kuanzia ofisi za waziri mkuu (Mtaa wa Mahakamani) hadi ofisi za hazina ndogo. 

  TANESCO Mkoa wa Dodoma walisafisha eneo la kituo cha kuuzia mafuta cha BP Capital hadi soko la Sabasaba. Taasisi nyingine ni pamoja na jeshi la Magereza ambapo lilifanya usafi kuanzia mzunguko wa barabara ya kuelekea Bahi hadi maeneo ya magorofa mengi wakati mabenki yalisafisha mitaa na barabara zinazopita mbele ya majengo yao ya benki na Wakala wa Barabara TANROADS wao walisafisha kuanzia kituo cha mabasi ya mikoani hadi soko la Sarafina. 
  Kwa upande wa wananchi walioshiriki zoezi hilo la kufanya usafi, wamepongeza utaratibu na kusema utasaidia kuweka mji katika mazingira safi. 

  Akiwawakilisha wananchi walioshiriki zoezi hilo, Mkazi wa Dodoma Onesmo Stephano alielezea kuwa utaratibu huo wa viongozi wa Mkoa na watumishi wa serikali kushiriki kufanya usafi unawatia hamasa kubwa wananchi nao kushiriki pale wanapoona viongozi wao wanashiriki kufanya nao usafi. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa alibainisha kuwa siku ya tarehe 9 Disemba itakuwa siku ya kutathimini kazi ya usafi inayoendelea kufanyika ndani ya Mkoa, pia utafanyika usafi kwenye maeneo ya huduma za jamii kama masoko na Hospitalini. 

   Maagizo yaliyotolewa wakati wa kupanga mikakati ya utekelezaji wa agizo la kufanya usafi kwenye Mkoa wa Dodoma ni pamoja na mamlaka za serikali za mitaa katika ukaguzi na usimamizi wa zoezi la usafi kwenye maeneo ya makazi na shughuli mbalimbali wafanye ukaguzi wa vyoo. Vilevile ukaguzi kwa kazi iliyofanyika ya usafi wa mazingira ya makazi, maeneo ya huduma za jamii, maeneo ya utupaji taka. 

  Maelekezo mengine ni pamoja na matumizi ya sheria ndogo kama kutoa ILANI, Makatazo na adhabu za Faini kwa makosa ya uchafuzi wa mazingira. Uongozi wa Mkoa wa Dodoma umeelezea kuwa zoezi hili la kufanya usafi wa mazingira kila siku na usafi wa pamoja wa kila siku za jumamosi utasaidia kupunguza magonjwa mengi yatokanayo na uchafu wa mazingira kama vile kipindupindu, kuhara na magonjwa mengine ya milipuko na kwa sasa wanasubiri Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma kutoa ratiba ya zoezi la usafi la Jumamosi 


  Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Ndg. Rehema Madenge (kulia walioingia mtaroni) na watumishi wengine wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wakishiriki zoezi la kusafisha mitaro ya maji ya mvua eneo la Bahi Road mapema leo ikiwa ni mwanzo wa utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais la kutumia siku ya uhuru 9 Disemba kufanya usafi wa mazingira.
  Watumishi wa Manispaa ya Dodoma wakishiriki zoezi la kufanya usafi kwa kufyeka magugu eneo la makaburi ya Bahi Road mapema leo ikiwa ni mwanzo wa utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais la kutumia siku ya uhuru 9 Disemba kufanya usafi wa mazingira.
  Wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Tume ya Maendeleo ya Ushirika wakijiorodhesha baada ya kumaliza zoezi la usafi wa mazingira mapema leo ikiwa ni mwanzo wa utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais la kutumia siku ya uhuru 9 Disemba kufanya usafi wa mazingira, orodha hiyo itatumika kuwabaini watumishi ambao hawajashiriki zoezi la usafi.


  0 0

  Na Dotto Mwaibale

  BOHARI ya Dawa (MSD) imejiimarisha na kuhahikisha inatekeleza kwa wakati agizo la Rais Dk. John Magufuli la kuweka maduka ya dawa katika hospitali za rufaa na kanda nchini.

  Katika kutekeleza agizo hilo MSD imeanza kwa kasi kubwa ya kukarabati jengo la duka la dawa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), ambalo linatarajiwa kufunguliwa kesho.

  Mwandishi wa habari hii alishuhudia jana kasi kubwa ya mafundi ujenzi wakikarabati jengo hilo ambalo awali lilikuwa likitumika kama stoo ya kuhifadhi vitu mbalimbali vya hospitali hiyo.

  Akizungumza na vyombo vya habari hivi karibuni kuhusu ufunguzi wa maduka hayo, Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laureane Bwanakunu alisema agizo la Rais la kuitaka MSD kuanzisha duka la dawa karibu na hospitali limekuja wakati muafaka kwani kwenye mpango mkakati wa miaka sita wa MSD tayari ilikuwa na mpango wa kufungua maduka hayo kwa ajili ya kusogeza huduma karibu a wananchi.

  Alisema maduka ya MSD ambayo yatafunguliwa kwenye hospitali za rufaa na kanda yatafanya kazi masaa 24 na kuuza dawa na vifaa tiba chini ya bei ya soko pia yatahudumia watu binafsi na wale waliopo kwenye taratibu za Bima ya afya kote nchini.

  "Ili kudhibiti watumishi wasio waaminifu kuiba dawa MSD inafanya kazi za uagizaji, uhifadhi na usambazaji kwa kutumia mfumo wa mtandao wa E9 na tangu mwaka wa fedha uliopita tumeanza kuziwekea alama ya GOT bidhaa zetu ikiwa ni pamoja na vidonge." alisema Bwanakunu.

  Alisema vidonge ambavyo tayari vimewekewa nembo ya GOT vipo 45 na wanaendelea kuwapa maelekezo wazabuni ili vyote viwekwe alama hizo..,nembo ya serikali inaonekana kwenye dawa za serikali kama Diclofenac, moxillin, iprofloxacin, Contrimoxale,paracetamol, na magnesium.
   
  Alisema wanatarajia kuanzisha huduma ya kutoa taarifa kwa njia ya simu pale wananchi watakapoona kuna wizi wa dawa za serikali na kwamba wananchi wanaelimishwa kutoa taarifa pale wanapoona dawa za serikali mitaani.

  Alisema, pamoja na serikali kuanza kupunguza deni lake linalodaiwa na MSD bado inadaiwa Sh.bilioni 53.

  Mafundi wakikarabati jengo ambalo Bohari ya Dawa (MSD), itafungua duka la dawa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MSD) Dar es Salaam jana kwa ajili ya kuhudumia wananchi kwa karibu zaidi vikiwemo vifaa tiba. Duka hilo linatarajiwa kufunguliwa kesho kutwa.
  Fundi akitoboa ukuta sehemu litakapo fungwa beseni la kunawia katika duka hilo.
  Mafundi wakiendelea na ukarabati wa jengo hilo lililopo jirani na wodi ya Kibasila linalotizamana na maegesho ya magari.


  0 0

   Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Ziwa, Godwin Zakaria(kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama cha Mitumbwi kanda ya Ziwa, Richard Mgabo,moja vikombe vitakavyoshindaniwa katika mashindano ya  za mbio za Mitumbwi wakati wa uzinduzi huo uliofanyika jijini Mwanza mwishoni mwa wiki kwa udhamini wa bia ya Balimi Extra Lager.

   Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Ziwa, Godwin Zakaria(kushoto) akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama cha Mitumbwi kanda ya Ziwa, Richard Mgabo,moja vikombe vitakavyoshindaniwa katika mashindano ya  za mbio za Mitumbwi wakati wa uzinduzi huo uliofanyika jijini Mwanza mwishoni mwa wiki kwa udhamini wa bia ya Balimi Extra Lager.

  Mwenyekiti  wa mitumbwi Kanda ya Ziwa, Richard Mgambo(katikati),akinyanyua juu moja ya kikombe mara baada ya kukabidhiwa na Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Ziwa, Godwin Zakaria kulia kwake atakalokabidhiwa bingwa wa mbio za makasia  mara baada ya uzinduzi wa mashindano hayo yaliyofanyika TBL Mwanza mwishoni mwa wiki kwa udhamini wa bia ya Balimi Extra Lager.Wengine  ni viongozi wa mikoa katika maeneo ambako fainali zitafanyika.

  0 0

   Ofisa Mtendaji wa Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (Dawasco), Mhandisi Cyprian Luhemeja, akizungumza katika mkutano na wafanyakazi uliofanyika hivi karibuni Makao Makuu ya Dawasco jijini Dar es Salaam kuhusu utendaji kazi wa kazi.
   Wafanyakazi wa Dawasco wakimsikiliza Ofisa Mtendaji 
  Mkuu wao.

  Na Dotto Mwaibale
  Ule usemi maaarufu wa "Hapa kazi tu"unaendelea kuimbwa na kufanyiwa kazi na Watanzazia wengi hususani watumishi wa Umma na serikali ili kuendana na kasi ya awamu ya Tano ya Raisi Magufuli. Kauli mbiu hiyo imekumbushwa tena na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati wa kikao cha pamoja na  wafanyakazi wa shirika hilo mapema wiki hii.
  “Lazima tuendane na kasi na speed ya Mheshimiwa Rais, tabia ya kufanya kazi kwa mazoea, kutojali malalamiko ya Wateja sasa ni mwisho” alisisitiza Mhandisi Luhemeja.
  Aliwataka wafanyakazi kujali muda wao wa Kazi kwa kutenda yale ambayo yataondoa kero ya Maji kwa Wateja hususani kuziba mivujo ya Maji katika maeneo mengi ya Jiji pamoja na kupambana na wizi wa Maji ili kila mwananchi apate huduma ya Maji kihalali.
  Alimalizia kwa kuwataka wafanyakazi wa DAWASCO kutekeleza kauli ya Rais aliyoitoa mapema wakati akifungua Bunge katika sekta ya Maji pale aliposema “LAZIMA TUWATUE KINA MAMA NDOO KICHWANI” kwa kuhakikisha huduma ya Maji inamfikia mwananchi na kuondokana na malalamiko ya upatikanaji huduma hiyo kwa maeneo stahili.  0 0

   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Maliasili Dr. Bakar Ased akimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar umuhimu wa eneo ya hifadhi ya Misitu la Muyuni kwa ustawi  bora ya maisha ya wananchi wa ukanda wa Kusini Unguja.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kati kati akitembelea msitu wa hifadhi Muyuni kuangalia maeneo ambayo baadhi ya watu wameamua kulima kilimo chengine mchanganyiko. Kushoto ya Balozi Seif ni Waziri wa Kilimo na Maliasili Mh. Sira Ubwa Mwamboya na kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dr. Idriss Muslim Hijja.

  Othman Khamis Ame
  Tamaa za baadhi ya watu katika kutaka kujimilikisha maeneo ya ardhi kwa nia ya kupata utajiri wa haraka hapo baadaye ndio chanzo kikuu kilichosababisha uchafuzi wa mazingira katika hifadhi ya msitu wa Muyuni Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja. .
  Kauli hiyo ilitolewa na baadhi ya wana Kamati na wananchi wa shehia ya Muyuni “B” ambayo ilionyesha mgongano baina yao wakati wakimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefika katika Msitu huo kuangalia maeneo ya Hifadhi ya Msitu ambayo baadhi ya wahusika hao wameamua kuyatumia kwa kuendeleza  kilimo.
  Eneo hilo la ardhi lililokubalika kutumiwa kuwa hifadhi ya Msitu na Wananchi wote wa  Shehia  Tatu za Muyuni A,B na C kwa takriban miaka 10 limekuwa na mgogoro  wa matumizi kwa miaka minane sasa tokea kutolewa uamuzi wa kila shehia iunde Kamati yake ya Uhifadhi badala ya ile ya pamoja ya shehia hizo.
  Wana Kamati hao pamoja na wananchi ambao mpaka ziara hiyo inamazliza wakihitilafiana walisema baadhi yao wamekuwa na malengo ya kuyatumia maeneo hayo na baadae kuyauza kwa vile tayari yamekuwa rasilmali kubwa katika masuala ya uwekezaji vitege uchumi vya sekta ya Utalii.
  Walisema tabia ya baadhi ya wananchi wenzao ya kuanza kilimo cha minazi na miti mengine ya matunda na biashara pamoja na kisingizio cha sababu za kushutumiana kwa itikadi za kisiasa imechangia  kuvuruga eneo kubwa la hifadhi hiyo muhimu kwa hatma yao na vizazi vijavyo.
  Akitoa nasaha zake kwa wana Kamati pamoja na Wananchi hao wa Muyuni “ B “ Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itatoa ushauri kuhusiana na mgogoro huo wa hifadhi ya Msitu wa Muyuni hapo baadaye.
  Balozi Seif alisema utaratibu maalum utaandaliwa katika kulitafutia ufumbuzi  tatizo hilo kwa kuhusisha Viongozi wa Taasisi za Kilimo, Ardhi na Maingira ambapo wahusika hao watakuwa na uamuzi wa kuwaita watu waliohusika na mgogoro huo katika kuwahoji na kutaka ufafanuzi.
  Alisema nia ya Serikali Kuu ni kuona hifadhi ya Msitu wa Muyuni inaendelea kubakia kwa maslahi ya Wananchi wa eneo hilo pamoja na Taifa zima kwa vile eneo hilo tayari limeshatangazwa ndani ya Gazeti la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaeleza  Wananchi hao kwamba Zanzibar ikiwa niongoni mwa baadhi ya Mataifa ya Bara la Afrika imebahatika kuwa na rasilmani nzuri za maumbile lakini baadhi ya watu wamekuwa na tabia mbaya ya kuharibu kwa makusudi rasilmali hizo.
  Mapema Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Mali asili Zanzibar Dr. Bakar Ased alisema eneo hilo la hifadhi hivi sasa baadhi ya sehemu linatumika kwa shughuli za kilimo kinyume na lengo lililokusudiwa kwa makubaliano ya Wananchi wenyewe na idhini ya Serikali.
  Dr. Ased aliwatanabahisha Wananchi hao kwamba licha ya eneo hilo kulengwa kuwa hifadhi ya misitu  lakini pia wataalamu wa mazingira na hali ya hewa wamefanya utafiti na kutoa ripoti iliyoeleza kwamba  Ukanda wa Kusini ni eneo zima lenye Hewa safi.
  Alisema kuvurugwa kwa  hifadhi hiyo  kwa shughuli nyengine za kilimo kunaweza kukasababisha kuwa  chanzo cha uchafuzi wa hali ya mazingira na matokeo yake ni athari kwa viumbe hapo baadaye.
  Kuna sehemu kubwa ya Eneo la hifadhi ya misitu la Muyuni ambayo kwa sasa in atumika kwa shughuli za kilimo mchanganyiko kama miembe, Minazi, Mivinje ,Migomba pamoja na mazao madogo madogo ya mizizi.
    
  Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
  29/11/2015.
  0 0

  Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U15) leo hii imekabidhiwa bendera ya Taifa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel katika hosteli za TFF zilizopo Karume jijini Dar es salaam.
  Akiongea wakati wa kukabidhi bendera kwa timu hiyo ya vijana, Ole Gabriel amewashukuru TFF kwa kuwekeza katika soka la vijana, na kusema mafaniko yote yanandaliwa chini, hivyo analipongeza Shirikisho kwa kuamua kuwalea na kuwaendeleza vijana hawa wenye vipaji kwa manufaa ya taifa ya baadae.
  Ole Gabriel amewataka vijana waliochaguiwa katika kikosi hicho, kuitumia nafasi hiyo adimu ipasavyo kuwawakilisha watanzania, kujituma katika mafunzo wanayopewa na waalimu wao, nidhamu ndani na nje ya uwanja na kuonyesha uzalendo wao wanapoiperesuha bendera ya Taifa.
  Kikosi hicho cha vijana wenye umri chini ya miaka 15 kinatarajiwa kuondoka kesho alfajiri (Jumatatu) kuelekea jijini Mwanza kwa mchezo wa kirafiki na kombaini ya mkoa wa Mwanza (U17), kisha kuelekea mkoani Kigoma kwa michezo miwili ya kirafiki dhidi ya kombaini ya mkoa wa Kigoma (U17) na timu ya Taifa ya Burundi (U17).
  Baada ya michezo ya mkoani Kigoma, U15 itaelekea Kigali Rwanda kwa michezo na timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, kisha Jinja kucheza na timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ya Uganda, Nairobi itacheza na timu ya taifa ya Kenya (U17) na kumalizia jijini Arusha kwa kucheza na kombaini ya mkoa wa huo (U17).
  Timu inatarajiwa kurejea jijini Dar ess alaam Disemba 24 baada ya kuwa imecheza michezo kumi ya kirafiki, mechi hizo zitampataia nafasi kocha mkuu Sebastiani Mkomwa kuona maendeleo ya vijana wake, wakiajiandaa kucheza michezo ya kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika U17 mwaka 2017 nchini Madagascar. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

  Angalia webisode mpya ya Ubongo Kids "Rafiki wa Macho" BURE kupitia YouTube! Kibena, Kiduchu, Koba na Baraka wanakutana na Bundi na wanajifunza kuhusu sayansi ya mwanga!

  0 0

  Habari zilizosambaa mitandaoni kuhusiana na mabunda ya noti za dola ya Kimarekani kuwa zimekutwa nyumbani kwa mmoja wa watuhumiwa wa mtandao wa wizi bandarini na TRA sio za kweli, Globu ya Jamii inaweza kuthibitisha.
  Ukweli ni kwamba mabunda hayo ya noti yalikamatwa huko jijini York, Portland, Marekani Mwezi Septemba mwaka 2010, na sio hapa Dar es salaam, Tanzania kama ambavyo wadau wengi wa mitandao hasa ya Whatsapp na Instagram wanavyovumisha.
  Tumelazimika kutoa habari hii ili kuokoa wadau wetu wengi katika vuguvugu hili la uvumi wa mitandaoni ambayo hupelekea kazi kuwa ngumu kwa wengi wetu tunaotafuta na kutoa taarifa za uhakika na ukweli. Maana samaki mmoja akioza wote huonekana wameoza.
  Vile vile hii ni kuwafumbua wale wote wanaohusika kusimamia na kutekeleza sheria ya mitandao wawe macho na kuanza kuchukua hatua madhubuti ili kupunguza kama si kuondoa kabisa tabia hii mbaya ya kusema uwongo kila kukicha.
  0 0

   Waziri  Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa  akisalimiana na baadhi ya viongozi wa kanisa la Africa Inland Church  wakati alipohitimisha maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo katika Dayosisi ya Pwani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa PTA katika uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere Kilwa Road jijini Dar es salaam Novemba 29, 2015.


   Waziri  Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa  akizungumza  wakati alipohitimisha maadhimisho ya miaka 20 ya Kanisa la Africa Inland Church Dayosi ya Pwani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa PTA katika uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere Kilwa Road jijini Dar es salaam Novemba 29, 2015
   
   Waziri  Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa  akiwa meza kuu na  viongozi wa kanisa la Africa Inland Church  wakati alipohitimisha maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo katika Dayosisi ya Pwani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa PTA katika uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere Kilwa Road jijini Dar es salaam Novemba 29, 2015.
   Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim majaliwa akiwash moja ya pikipiki tatu ili kuashiria mkaka ti wa kueneza injili wakati alipohitimisha  maadhimisho ya miaka 20 ya kanisa la Africa Inland Church Dayosisi ya Pwani kwenye  ukumbi wa PTA katika uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere, Kilwa Road jijini Dar es salaam Novemba 29, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  TUMEDHAMIRIA KUWATUMIKIA WATANZANIA - MAJALIWA

   *Asema Serikali hii siyo ya watu wapole

  WAZIRI MKUU Majaliwa Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuhakikisha kila kinachokusanywa kama mapato ya nchi kinatumika kwa maslahi ya Watanzania wote na si kwa manufaa ya wachache.

  Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumapili, Novemba 29, 2015) wakati akifunga maadhimisho ya miaka 20 ya Dayosisi ya Pwani ya Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) kwenye ukumbi wa PTA, viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. 
  “Serikali imeanza kukabiliana na upotevu wa mapato ya Serikali na kuepuka matumizi yasiyo ya lazima ya fedha za umma. Nia yetu ni kuhakikisha kila kinachopaswa kukusanywa kama mapato ya nchi, kikusanywe na kitumike kwa masuala ya msingi kwa ustawi wa Watanzania wote na si kwa watu wachache,” alisema. 
  Akifunga maadhimisho hayo kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri Mkuu alisema Serikali imedhamiria kupambana na maovu yote na kuondoa kero zinazowaumiza wananchi wa kawaida. “Wako watu wanaoamini kwamba hatuwezi, nawaomba waondoe hiyo dhana. Wako watu wanaodhani kwamba kwamba utawala huu ni wa watu wapole, nao pia waondoe hiyo dhana,” alisema huku akishangiliwa na mamia ya waumini waliohudhuria sherehe hizo zilizoanza Novemba 27, 2015. 
  “Tunawaomba Watanzania wote mtuunge mkono kwenye vita hii na mtuwezeshe kuifanya kazi hiyo. Tunaomba waumini wote mtuombee katika sala zenu za kila siku ili tuweze kuongoza kwa haki na kuwaletea Watanzania wote maendeleo,” aliongeza. 
  Akinukuu kitabu cha Mithali sura ya 29 mstari wa pili, Waziri Mkuu alisema: “Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi, bali mwovu atawalapo, watu huugua. Mtuombee viongozi wenu tuwe waadilifu na wenye kutenda haki. Nasi tutaendelea kuwa waadilifu ili watu wetu wasigue,” alisema.

  Aliwataka viongozi wa kanisa hilo waendelee kuisaidia Serikali katika kujenga kundi la watu wenye maadili mema ili walisaidie Taifa kuwa na watu waadilifu na hivyo kupunguza kero nyingi zinazoikabili jamii.

  Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na waumini wa kanisa la hilo kutoka mikoa mbalimbali, Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT, Askofu Silas Kezakubi alisema Kanisa hilo litaendelea kumuombea Rais Dkt Magufuli na viongozi wenzake ili wawe na afya njema, wawe na hekima na kuahidi kwamba wataendelea kuwaweka chini ya ulinzi wa Mungu siku zote.

  Alisema wao kama kanisa wanaamini kwamba Serikali ya awamu ya tano ina nia ya kuwatumikia wananchi kwa bidii na uadilifu lakini akasisitiza kuwa siri ya bidii na uadilifu inapatikana kwenye neno la Mungu.

  Akisoma risala ya kanisa hilo, Askofu wa AICT Dayosisi ya Kibaha, Askofu Charles Salalah alisema kanisa halina budi kushirikiana na Serikali kwa sababu wote wanawahudumia watu walewale isipokuwa katika malengo tofauti. 
  Alisema kanisa hilo linahubiri maadili mema na bidii katika kazi kwa vile linaamini kuwa maendeleo hayadondoki kutoka juu wala hayaoti kama uyoga bali yanapatikana kwa watu kufanya kazi. 
  Akisisitiza kuhusu uadilifu, aliwataka wazazi kudumisha ndoa zao ili watoto wapate malezi mema kutoka kwa baba na mama na kwamba baba na mama wasipokaa vizuri, watoto hawawezi kuwa waadilifu. 
  “Wazazi tunao wajibu wa kupanda mbegu bora ya uzalendo kwa watoto wetu. Endapo tutapanda mbegu mbaya ya kuwagawa watoto wetu kwa itikadi tofauti, ni lazima tujue kuwa tutavuna tunachopanda.”

  “Tukumbuke kuwa tunalo Taifa moja tu la Tanzania. Hata kama watoto wetu watakuwa na upenzi na vyama vyao, ni lazima tuwalee katika misingi ili wakue wakijua Taifa letu ni moja tu. Ndiyo maana tunaweka mkazo kwenye familia kwa sababu maadili mema yanaanzia nyumbani,” alisisitiza.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S.  L. P. 3021,
  11410 DAR ES SALAAM
  JUMAPILI, NOVEMBA 29, 2015.  0 0

  Na  Ghalib Nassor Monero

  Asalaam Alaykum Warahmatullahi wabarakatu, 
  Alhamdulilah....

  Kwa Niaba ya wakazi wa kijiji cha Mlamleni , kitongoji cha kimbangulie , wilaya ya Mkuranga  Mkoa wa Pwani ninatoa shukran za dhati kwanza Ma Admin wote wa blogs mlioshirikiana nasi katika kulitangaza jambo hili la kheri.
  Pili tunawashukuru wale wote wadau ambao wameshirikiana nasi kwa hali na mali katika Ujenzi wa Jengo hili la msikiti kutoka Nyasi Mpaka kuwa katika Muonekano mpya kama mnavyo ona katika picha, Mwenyezi Mungu awalipe thawabu nyingi, awasimamie katika mambo yenu, awape rizki kunjufu za halali na kila ya kheri mnayo yatamani myapate kwa haraka. Msikiti umekwisha na tumekwisha kabidhi kwa wahusika.

  Kwa sasa mahitajio  yaliyobaki kama nilivyopokea kwa njia ya Risala waliyonisomea waumini wa huko wakati wa ufunguzi rasmi wa msikiti huo na ambayo pia ni Maombi kwenu: 


  1. Kisima cha Maji, 2.Solar power na 3.Uwezweshaji wa kununua eneo jirani na msikiti ili wapate jenga Madrasa. Na mwisho pia wanatuomba kila mazuri ambayo twaona yanafaa kwao na wao tuwasogezee.


  Nikiwa kama msimamizi wa PROJECT hii  , Napenda kusema kuwa tunaweza hivyo basi kuisha kwa hii Project ya kwanza ndio muendelezo wa Project No2. ambayo inakusanya:1.Msikiti, 2.Madarasa vyumba vitatu n.k, 3.Nyumba ya walimu na wanafunzi (bado kujengwa).


  Tafadhali ninaomba kuleta kwenu ombi la vifaa vifuatavyo :-

  1.Cement - mahitaji Mifuko 150 na kuendelea, 2.Mchanga  (mahitaji loli 3 kubwa), 3.Kokoto, 4.Nondo, 5.Bati ( tunapokea kwa uwezo wa mtu ) na 6.Mbao na kila kifaa cha Ujenzi.Tunapokea kuanzia kimoja viwili na zaidi.

  ACHA MATUMIZI YASIYO NA LAZIMA TENGENEZA PEPO YAKO KWA DARAJA UNAYO ITAKA HAPA DUNIANI KWA KUTOA SADAKA YENYE KUENDELEA ( Sadaqatul jaalia ) .

  Kwa mawasiliano zaidi Tafadhali wasiliana , au tuma Mchango kwa Tigo pesa au Airtel Money kwa Namba zifuatazo.

  +255715800772 (Whatsapp)
  +255673800772
  +255685800772
  +255689604780 (Whatsapp)

  Kwa wale walio nje ya nchi Western union & Money gram

  Receiver name :- GHALIB NASSOR MONERO.

  Shukran , wabilahi taufiqh 
   Muonekano wa  Msikiti wa zamani ulivyokuwa katika kijiji cha Mlamleni katika kitongoji cha Kimbangulile wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani kabla ya kujengwa upya kwa nguvu za michango ya wasamaria wema wa ndani na nje ya nchi baada ya kuona matangazo yake kupitia blogs mbalimbali.
    Muonekano wa  Msikiti wa zamani ulivyokuwa katika kijiji cha Mlamleni katika kitongoji cha Kimbangulile wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani kabla ya kujengwa upya.     Muonekano wa  leo wa msikiti wa kijiji cha Mlamleni katika kitongoji cha Kimbangulile wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani baada  ya kujengwa upya     Maandalizi ya ufunguzi rasmi wa msikiti huo

  Muonekano wa  ndani ya msikiti wa kijiji cha Mlamleni katika kitongoji cha Kimbangulile wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani baada  ya kujengwa upya. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


  0 0


  0 0

    Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu (CCM) (mwenye kofia) akimkabidhi nahodha wa timu ya Ferry Beach Boys, Selemani Ally 'Kaseja' nyaraka za  Pikipiki aina ya GSM ayowaahidi wakati wa Kampeni zake, jijini Dar es Salaam leo .(PICHA NA  KHAMISI MUSSA)
   Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu (CCM) (mwenye kofia) akimkabidhi nahodha wa timu ya Ferry Beach Boys, Selemani Ally 'Kaseja' namba ya Pikipiki hiyo, Dar es Salaam leo.  

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (wa kwanza kulia) akizungumza na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mara baada ya kuwasili katika kituo cha kuzalisha umeme wa maji cha Mtera ili kukagua kituo hicho na kuzungumza na wataalam.Wa Tatu kulia ni Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, Mhandisi Hosea Mbise), na wa Nne kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Sheria Wizara ya Nishati na Madini, Justus Mulokozi.
  Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (katikati) akikagua kituo cha kuzalisha umeme wa maji cha Mtera mara baada ya kufanya mazungumzo na watendaji wa Tanesco wanaosimamia kituo hicho. Wa Kwanza Kushoto ni Kaimu Meneja wa Kituo cha Mtera, Eng. Manfred Mbyallu na kulia ni Meneja Uzalishaji Umeme wa Maji nchini, Antony Mbushi.
  Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Omar Chambo (wa kwanza kushoto waliokaa) akiwa katika chumba cha kuongozea mitambo ya uzalishaji umeme katika kituo cha kuzalisha umeme cha Kidatu mkoani Morogoro wakati alipofanya ziara katika kituo hicho. Katikati (waliokaa) ni Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, Mhandisi Hosea Mbise na Wa Kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Sheria Wizara ya Nishati na Madini, Justus Mulokozi.


  0 0

  Wakazi mbalimbali mkoani Lindi wajumuika katika kufanya usafi wa mji huo huku msanii Mrisho Mpoto akiunga mkono juhudi hizo kwa kushiriki. https://youtu.be/mBCEkJQZauA  

  Mkazi mmoja mkoani Lindi afariki dunia baada ya kuangukiwa na udongo wakati akichimba mchanga na kupelekea mkuu wa wilaya hiyo kusitisha shughuli za uchimbaji. https://youtu.be/LKuZvVb_arU   

  Umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi UWT wawaomba wananchi na viongozi wote wa dinizote nchini kumuombea Raisi Magufuli ili aweze kuendelea na hatua anazochukua ili kuleta tija kwa wananchi.

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,John Mngodo,akizungumza na wajumbe wa mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Idara ya Jeshi la Polisi(hawapo pichani),wakati alipoalikwa kufunga mkutano huo uliofanyika Chuo cha Taaluma ya Polisi,Kilwa Road,jijini Dar es Salaam.
  Naibu Katibu wa Baraza la Wafanyakazi,Stanford Busumbiro(kulia) akimpongeza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,John Mngodo, muda mfupi baada ya kumaliza kufunga mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Idara ya Jeshi la Polisi uliofanyika katika Chuo cha Taaluma ya Polisi,Kilwa Road,jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi,DCP Ally Lugendo,akizungumza wakati wa kufunga mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Idara ya Jeshi la Polisi uliofanyika Chuo Cha Taaluma yaPolisi,Kilwa Road, jijini Dar es Salaam.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ,John Mngodo(katikati),akiwasili Chuo cha Taaluma ya Polisi kilichopo Kilwa Road, jijini Dar es salaam kufunga mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Idara ya Jeshi la Polisi.wengine waliongozana na Naibu ni viongozi wa Baraza hilo.(Picha zote na Abubakari Akida,Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

  0 0

  WAZIRI MKUU Majaliwa Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuhakikisha kila kinachokusanywa kama mapato ya nchi kinatumika kwa maslahi ya Watanzania wote na si kwa manufaa ya wachache.

  Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumapili, Novemba 29, 2015) wakati akifunga maadhimisho ya miaka 20 ya Dayosisi ya Pwani ya Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) kwenye ukumbi wa PTA, viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

  “Serikali imeanza kukabiliana na upotevu wa mapato ya Serikali na kuepuka matumizi yasiyo ya lazima ya fedha za umma. Nia yetu ni kuhakikisha kila kinachopaswa kukusanywa kama mapato ya nchi, kikusanywe na kitumike kwa masuala ya msingi kwa ustawi wa Watanzania wote na si kwa watu wachache,” alisema.

  Akifunga maadhimisho hayo kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri Mkuu alisema Serikali imedhamiria kupambana na maovu yote na kuondoa kero zinazowaumiza wananchi wa kawaida. “Wako watu wanaoamini kwamba hatuwezi, nawaomba waondoe hiyo dhana. Wako watu wanaodhani kwamba kwamba utawala huu ni wa watu wapole, nao pia waondoe hiyo dhana,” alisema huku akishangiliwa na mamia ya waumini waliohudhuria sherehe hizo zilizoanza Novemba 27, 2015.

  “Tunawaomba Watanzania wote mtuunge mkono kwenye vita hii na mtuwezeshe kuifanya kazi hiyo. Tunaomba waumini wote mtuombee katika sala zenu za kila siku ili tuweze kuongoza kwa haki na kuwaletea Watanzania wote maendeleo,” aliongeza.

  SOMA ZAIDI HAPA

  0 0


  0 0

  Kumekuwa na taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa kampuni ya Bakhresa inahusika na upotevu wa Makontena 349 yaliyoripotiwa hivi karibuni kuwa yametolewa bandarini bila kulipiwa ushuru. Taarifa hizo zilitolewa na Waziri Mkuu wakati wa ziara yake ya Bandari ya Dar es salaam hivi karibuni.

  Uchunguzi wetu umeonyesha kuwa si kweli kuwa kuna makontena yenye bidhaa zilizoingizwa na kampuni hio ama ni miongoni mwa makontena yaliyohusika katika sakata hilo. Isipokuwa kumetokea upotevu wa makontena yaliyoingizwa nchini na baadhi ya wafanyabiashara katika eneo la kuhifadhia makontena(ICD) linalomilikiwa na kampuni hiyo la Azam ICD.


  Aidha imebainika kuwa kuna uchunguzi unaofanywa na mamlaka ya mapato nchini TRA, huku kukiwa na ushirikiano na uongozi wa Kampuni hiyo (SSB Group of Companies) kuhakikisha wale wote wanaohusika na upotevu huo wanachukuliwa hatua na kodi yote ya serikali inalipwa na wamiliki wote wa makontena yaliyohusika katika upotevu huo wanawajibishwa.


  SSB Group of Companies

  Corporate Affairs Department

  November 29, 2015

  0 0


older | 1 | .... | 1039 | 1040 | (Page 1041) | 1042 | 1043 | .... | 3272 | newer