Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1033 | 1034 | (Page 1035) | 1036 | 1037 | .... | 3284 | newer

  0 0


  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


  Agizo alilolitoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la kutaka fedha zilizochangwa na wadau mbalimbali kwa ajili ya kugharamia hafla ya wabunge zipelekwe Katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kununulia vitanda na magodoro ya wagonjwa wanaolala chini limetekelezwa.


  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema fedha hizo zimefanikisha kupatikana vitanda 300 vya wagonjwa pamoja na magodoro yake, shuka 600, Baiskeli za kubebea wagonjwa na vifaa vingine na kwamba hivyo vyote tayari vimepelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.


  Balozi Sefue ameuagiza uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha vitanda vyote vinafungwa kesho jumapili na kwamba atakwenda kuvikagua siku ya jumatatu vikiwa tayari vinatumiwa na wagonjwa waliokua wanakosa vitanda vya kulalia na kulazimika kulala chini.


  Wadau mbalimbali walichanga fedha kiasi cha shilingi milioni 225 kwa ajili ya kugharamia hafla ya wabunge baada ya uzinduzi rasmi wa bunge la 11 lakini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli aliagiza fedha hizo zitumiwe kwa kiasi kidogo kisichozidi shilingi milioni 15 na nyingine zipelekwe hospitali ya Muhimbili kutatua tatizo la uhaba wa vitanda.


  Gerson Msigwa

  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano IKULU,


  Novemba 21, 2015.


  0 0
  0 0

  Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa na mkewe Mama Mary Majaliwa wakisalimiana na viongozi wa mkoa wa Morogoro wakati waliposimama kwa muda mjini  Morogoro wakiwa njiani kuelekea Dar es salaam wakitoka Dodoma kwa gari leo Novemba 22, 2015. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Rajabu Rutengwe 
  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

   Balozi mdogo wa china hapa nchini Mhe. Zhang Biao  akizungumza na wandishi wa habari kuhusu mkutano wa pili wa ushirikiano na africa utakaofanyika mwezi ujao Nchini Afrika yakusini ambao Utaongozwa na Rais wa China Xi Jinping  pamoja na wakuu wanchi wapatao hamsini katikakuangalia furusa zinazo tolewa na China katika kuleta maendeo africa
  Mkutano wa pili wa taasisi ya ushirikiano kati ya China na Afrika –FOCAC- utafanyika mjini Johanesburg nchini Afrika kusini mwanzoni mwa mwezi ujao kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya pande hizo. 
  Balozi mdogo wa China nchini ZHANG BIAO amesema hayo wakati akizungumza na wandishi wahabari katika ubalozi wa china hapa nchini nakusema viongozi wakiwemo wakuu wa  nchi zaidi ya 50 na viongozi wa Umoja wa Afrika akiwemo Rais wa China XI JINPING wanatarajia kuhudhuria mkutano huo. 
  Mkutano wa kwanza wa aina hiyo  ulifanyika nchini China na hivi sasa utafafanyika Africa kwa lengo la kukuza maendeleo na kusaidia bara la Afrika kuondokana na matatizo ya kiuchumi pamoja na afya. 

  0 0

  Na RAMADHANI ALI, MAELEZO ZANZIBAR                                    
   Chama cha Wanasheria Mawakili Zanzibar kimepata heshma ya kuwa mwenyeji wa Mkutano wa siku mbili wa mwaka wa Wanasheria Mawakili wa Nchi za Afrika Mashariki utakaoanza  tarehe 27 Mwezi huu katika Hoteli ya Sea Cliff Resort.
  Akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake Bwawani, Katibu Mkuu wa Chama cha Wanasheria Mawakili Zanzibar Omar Said Shaaban amesema mkutano huo utawashirikisha zaidi ya Wanasheria 400 kutoaka Nchi zote wananchama wa Afrika Mashariki na Mataifa mengine Duniani.
  Amesema kwa kawaida Jumuiya ya Wanasheria Mawakili wa Nchi za Afrika Mashariki inawachama wa aina mbili ambao ni wanasheria wenyewe binafsi na Jumuiya za kila Nchi nazo huwa ni mwanachama wa pili.
  Katibu Mkuu wa Wanasheria Mawakili Zanzibar amesema Mkutano huo utakuwa na malengo ya kubainisha kuwa Taaluma ya sheria kama kichocheo cha Biashara na Uwekezaji ambapo mada mbali mbali zitawasilishwa.
  Amezitaja baadhi ya mada zitakazowakilishwa katika mkutano huo ni pamoja na Kada ya Sheria kama biashara, muundo mzima wa Biashara na uwekezaji katika ukanda wa Afrika Mashariki na mada nyengine ni masuala ya rushwa na vipato visivyohalali.
  Ametoa wito kwa wananchi wa Zanzibar kuupokea ugeni huo mkubwa wa wanasheria na kuonyesha ukarimu uliozoeleka kwa wageni na kutumia fursa ambazo zitapatikana kutokana na kuwepo kwao hapa nchini.
  Amesema chama kwa upande wake tayari kimeliarifu Jeshi la Polisi kuhusu ugeni huo kwa lengo la kuimarisha hali ya usalama wakati wote wa mkutano.
  Katibu Mkuu wa Chama cha Wanasheria Zanzibar amesema Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu (pichani) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano huo.

  0 0


  Rift Valley Hotel is an imposing  three-floored hotel with summit, having 42 rooms, Ground floor: Zebra Bar, Restaurant and main kitchen and Lobby. 
  The basement has a sound proof Underground Discotheque. Two separate spacious conference halls on different floors to easily accommodate 100+pax. 
  The Hotel is Located/Situated on Block “E” at the Junction of Jamathkhan and Karume roads. Both roads are of tarmac nature and lead to the heart of the City. 
  The Hotel stands on a Low-density plot measuring 4000 sq meters and also has a separate main spacious outbuilding hosting Weddings named “TAUSI HALL to accommodate 400+ pax,  complete with a parking space to accommodate a fleet of vehicles with a security fence. 
  The hotel is sited adjacent with HOLIDAY IN , COFFEE GARDEN and SOKOINE STADIUM idirectly on the opposite. This neighborhood is characterized by commercial properties built on very low density plots. 
  For more information contact: Ngusekela Mwakyoma/Mansfield 
  Phone 0712055660 and 0754864471

  0 0


  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ambaye ni mlezi wa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWU), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi nje ya chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Taifa ya kuhusu kifo cha utata cha aliyekuwa Katibu wa chama hicho Tanzania, Rashid Saleh kilichotokea hivi karibuni pamoja na ratiba ya mazishi yake yatakayofanyika jijini Mwanza.
   Marehemu, Rashid Saleh
   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ambaye ni mlezi wa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADU), akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Pubrishers LTD, Eric Shigongo (katikati), na wadau wengine kuhusu taratibu za mazishi za katibu huyo.
   Mjumbe wa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWU), Stanley Kilave (kulia), akizungumza na Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho, Clement Masanja (kushoto), pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Pubrishers LTD, Eric Shigongo (katikati), wakati wa taratibu za mazishi zikifanyika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dar es Salaam leo.

   Msemaji wa familia ya marehemu, Jonas Marinyizu (katikati), akitoa shukurani kwa DC Makonda na wadau wengine kwa kuwezesha msiba huo pamoja na utaratibu wa mazishi utakavyo kuwa.

  Mwenyekiti wa Chama hicho, Shaban Mdemu akizungumza katika mkutano na wanahabari

  Na Dotto Mwaibale
  MWILI wa Katibu Mkuu na Msemaji wa Chama Cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWU), Rashid Saleh umesafirishwa jana kwenda kijijini kwao Kayenze wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza kwa maziko.
  Marehemu Saleh alifariki jana Novemba 21 Majira ya saa 8 mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), wakati akipata matibabu ya maradhi ya figo ili kuokoa maisha yake baada ya kile kinachodaiwa kushindwa kufanya kazi ipasavyo.
  Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ambaye pia ni mlezi wa chama hicho, Paul Makonda alisema kuwa wamepata pigo kutokana na umuhimu na umahiri ambao alikuwa nao marehemu hasa katika kutetea haki za madereva wenzake sanjari na kuibua mambo mbalimbali ambayo yatabaki kuwa historia na kumbukumbu kwao.
  "Saleh alifariki jana (Novemba 21) baada ya kusikia anaumwa ambapo hali yake haikuwa nzuri na madaktari walishauri nimlete Muhimbili kwa matibabu zaidi ambapo nilimfikisha lakini baada ya muda mfupi wakati madaktari wanahangaika kumtibu na kuokoa maisha yake alifariki,"alisema.
  Alisema marehemu amekiacha chama sehemu ya mafanikio makubwa zaidi ya mabadiliko na mikataba ya haki za madereva nchi nzima huku akibainisha mazingira ya kifo na kutaka uchunguzi zaidi ili kujiridhisha na kifo chake uliofanywa chini ya uangalizi wa polisi.
  "Hatukuona kama kuna haja ya kumuhifadhi mwili wa ndugu yetu hadi hapo tutakapojua nini chanzo cha kifo chake kwani majibu ndiyo yatatupa picha ya ugonjwa kwani tumehangaika tangu alipokuwa hospitali ya Kairuki ambapo tulipofika hapa ikabainika kuwa figo zake zote mbili hazifanyi kazi,"alisema.
  Aliongeza kuwa marehemu alipelekwa hospitalini hapo kwa kitengo maalum huku akibainisha endapo figo zinashindwa kufanya kazi mzunguko mzima wa damu mwilini nao husimama ambapo madaktari walishirikiana lakini hawakuweza kuokoa maisha yake.
  Mwenyekiti wa Chama hicho, Shaban Mdemu alisema kuwa msiba huo umewasikitisha sana kutokana na mazingira ya kifo chake huku akiitaka mamlaka husika kulisimamia suala hilo la kupatika kwa majibu sahihi juu ya kifo chake.
  "Tunataka uchunguzi ufanyike na majibu yatoke yakiwa sahihi na yanayoridhisha juu ya kifo chake kwani amekufa na madai ambayo yapo ndani yao, hivyo serikali itambue kifo cha Saleh ni katika harakati za kudai haki ambayo tuliyawasilisha mbele ya aliyekuwa waziri mkuu Mizengo Pinda,"alisema. 
  Alisema Saleh ni kiongozi wa taifa zima hivyo alimtaka rais Magufuli kuingilia kati suala hilo kwani kutokana na hali hiyo watamaliza wafanyakazi wote kwa kuwauwa katika mazingira kama hayo sambamba na kutenga siku rasmi kwa ajili ya maombezo ya msemaji huyo.
  Harakati za kudai haki ya madereva
  Marehemu Saleh alizaliwa mwaka 1966 Mwanza, ambapo hadi anafariki alikuwa katika harakati za kudai na kutetea haki za madereva ambapo Oktoba 2, mwaka huu alikaririwa akisema wamechoshwa na yanayoendelea kufanywa na Mamlaka ya Usafirishaji Majini na Nchi Kavu (Sumatra) na Wizara ya Kazi na Ajira kuhusu kufumbia macho kero zinazoitatiza sekta ya usafirishaji hasa kwa madereva wa mabasi ya abiria na magari ya mizigo.

  0 0

  Ankal akila pozi na Mbunge wa Mafinga Mjini Mhe. Cosato Chumi kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma. Globu ya Jamii inampongea sana Mhe. Chumi kwa ushindi wa kishindo alioupata katika kinyang'anyiro cha jimbo hilo, na kumtakia mafanikio katika kuendeleza jimbo katika miaka mitano ijayo. Pia inampongeza si tu kwa kuwa mmoja wa wadau wakubwa wa Globu ya Jamii,  bali pia amekuwa mchangiaji wa mawazo kwa muda mrefu.

  0 0


  0 0

   Mke wa Waziri  Mkuu, Mama Mary Majaliwa  (kushoto) akikaribishwa na mke wa Waziri Mkuu, Mstaafu Mama Tunu Pinda wakati alipowasili nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda katika kijiji cha  Zuzu nje kidogo ya mji wa Dodoma kwa mazungumzo Jumamosi Novemba 21, 2015 

   Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majliwa  akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda wakati alipomtembelea nyumbani kwake katika kijiji cha Zuzu, nje kidogo ya mji wa Dodoma Jumamosi Novemba 21, 2015.

  Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa na mkewe Mary (wapili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu,Mstaafu Mizengo Pinda na mkewe Tunu (kulia) Wakati Waziri Mkuu alipomtembelea Waziri Mkuu Mstaafu, nyumbani kwake katika kijiji cha Zuzu nje kidogo ya mji wa Dodoma Jumamosi Novemba 21, 2015.
  Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0


  Wachezaji wa timu ya Polisi Dar wakipasha misuli moto kabla ya kuanza kwamchezo wa ligi ya shirikisho hidi ya Panone fc mchezo uliopigwa katika uwanja wa Chuo cha Ushirika.


  Wachezaji wa timu ya soka ya Panone fc wakipasha misuli moto kabla ya kuanza kwa mchezo wa ligi ya shirikisho inayodhaminiwana Azam.

  Kocha wa timu ya soka ya Panone fc,Atuga Manyundo akizungumza na Azam TV iliyokuwa ikirusha mchezo huo moja kwa moja.
  0 0

  SWAHILI FASHION WEEK will take place from 4-6 December at Hotel Sea Cliff. The 27 designer Runways shows will take place every evening over the period of three days from 8.30PM onwards. 

  During  Day time there shall be a shopping festival whereby various exhibitors shall display and sell various crafts, art and accessories.

  0 0

  Moja ya heka heka langoni mwa timu ya Panone fc.
  Baadhi ya Mashabiki waliojitokeza katika mchezo huo.
  Vikosi vya timu za Polisi Dar na Panone fc vikiwa tayari kuingia uwanjani.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


  0 0

  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salaam (TUDARCo)-Utawala, Dk. Joyce Peters Chonjo (kushoto), akikabidhi cheti kwa, Stella Jacob mmoja wa washiriki 300 wa mafunzo ya ujasiriamali yaliyoandaliwa kwa ushirikiano kati ya TUDARCo na benki ya NBC. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wa pili kushoto ni Meneja Huduma za Jamii wa NBC, Irene Peter.
  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu ch Tumaini Dar es Salaam (TUDARCo)-Utawala, Dk. Joyce Peters Chonjo (kushoto), akikabidhi cheti kwa, Judith Peter, mmoja wa washiriki 300 wa mafunzo ya ujasiriamali yaliyoandaliwa kwa ushirikiano kati ya TUDARCo na benki ya NBC. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wa pili kushoto ni Meneja Huduma za Jamii wa NBC, Irene Peter.
  Meneja Ukuzaji wa Biashara wa Kitengo cha biashara ndogondogo na za kati wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Jonathan Bitababaje (kulia) akielezea mbinu za kufanya biashara na masuala ya mikopo kwa washiriki wa mafunzo ya ujasiriamali yaliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salaam (TUDARCo) na benki ya NBC. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.


  0 0
 • 11/22/15--06:31: TAARIFA KWA UMMA KUTOKA NHIF

 • 0 0

   Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa alipowasili Fumba Mkoa wa Mjini Magharibi jana katika ziara ya kutembelea maeneo ya ujenzi wa Mji mpya wa Nyumba za kisasa zinazojengwa na Kampuni ya Azam Group kwa kushirikiana Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
   Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na viongozi mbali mbali wakati alipowasili Fumba Mkoa wa Mjini Magharibi jana katika ziara ya kutembelea maeneo ya ujenzi wa Mji mpya wa Nyumba za kisasa zinazojengwa na Kampuni ya Azam Group kwa kushirikiana na Serikali nya Mapinduzi ya Zanzibar
   Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akipata maelezo kwa ufupi kutoka kwa  Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Bw.Said Salim Bakhresa alipowasili Fumba Mkoa wa Mjini Magharibi jana katika ziara ya kutembelea maeneo ya ujenzi wa Mji mpya wa Nyumba za kisasa zinazojengwa na Kampuni ya Azam Group kwa kushirikiana Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,(kushoto) Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitega Uchumi Zanzibar Nd,Salum Khamis Nassor
   Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kwa ufupi kutoka kwa  Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa alipowasili katika eneo linalotarajiwa kujwga kiwanda cha utengezaji wa Lami katika Kijiji cha Fumba Mkoa wa Mjini Magharibi jana katika ziara ya kutembelea maeneo ya ujenzi wa Mji mpya wa Nyumba za kisasa zinazojengwa na Kampuni ya Azam kwa kushirikiana Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakipokea shada la maua kutoka kwa Immaculata Warqaso wa Ofisi ya Waziri  baada ya kuwasili kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam leo Novemba 22, 2015 wakitoka Dodoma kwa gari.Wapili kulia ni Katibu Mkuuwa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt Florens Turuka. 
  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0   Na Emanuel Madafa, Mbeya
  Wachezaji 22 wa mpira wa kikapu Mkoa wa Mbeya, tayari wamefanikiwa kuondoka mkoani humo kwa ajili ya  kushiriki mashindano ya Taifa CUP, yatakayofanyika  Mkoani Dodoma  November 22 hadi November 30 mwaka huu.
  Wachezaji hao walishindwa kusafiri mapema kuelekea mkoani Dodoma
   kushiriki mashindano hayo  kutokana na kukabiliwa na uhaba wa fedha hali iliyofanya kuwepo na maandalizi hafifu.
  Aidha kufanikiwa kwa timu hiyo kunatokana na kujitokeza kwa  Kampuni ya vinywaji baridi ya Coca Cola, Mkoa wa Mbeya pamoja na Kampuni ya Tbl , amboa wamechangia kiasi kidogo cha fedha kilicho fanikisha safari hiyo.

  Akizungumzia juu ya kupokea kwa ufadhiri huo Katibu wa chama  cha mpira wa kikapu mkoani Mbeya ambaye pia ni mwalimu wa timu hiyo  , Yusuf Nyirenda, amesema kuwa wanawashukuru wadau hao kwa kujitokeza   kwa kuchangia kiasi hicho cha fedha.
  Amesema kampuni ya  Coca Cola pekee imechangia kiasi cha shilingi Mil 1.5 ambapo kwa upande wa TBL  wamechangia kiasi cha shilini laki tano   hivyo watajitahidi kutumia kaisi hicho kilicho patikana  ili kushiriki mashindano hayo.
  Amesema, tayari timu imekwisha ondoka   Mbeya November 21, ikiwa na wachezaji 22 kati yao wanawake 11 na wanaume 11 lakini mpaka sasa  wamefanikiwa kupata shilingi milioni 2  kati ya milioni 4,700,000 zinazohitajika.
  “Kiasi cha shiringi milioni 4,700,000 zinahitajika kwa ajiri ya usafiri wa kwenda na kurudi, chakula, malazi na ada ya kushiriki mashindano haya,”alisema.
  Amesema kwa dhati kabisa anaipongeza kampuni ya Coca cola kwani ndio kampuni pekee ambayo imekuwa ikijitoa mara kwa mara kusaidia timu hiyo .
  Amesema kutokana na mazingira hayo baadhi ya wachezaji watalazimika kujigharamia wenyewe katika eneo la usafiri   hivyo, amewaomba wadau  na mashabiki wa mpira huo, kuendelea kjitokeza kwa wingi katika kuichangia timu hiyo ili iweze kushiriki mashindano hayo.

  ( Imeandaliwa na Mtandao wa 
  www.jamiimoja.blogspot.com Mbeya 0759406070)

  0 0
  0 0


older | 1 | .... | 1033 | 1034 | (Page 1035) | 1036 | 1037 | .... | 3284 | newer