Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109606 articles
Browse latest View live

HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

0
0

Wananchi zaidi  ya 500 wa kata ya Nyarugusu Mkoani Geita waandamana hadi zahanati ya kata hiyo wakishinikiza kuondolewa kwa wahudumu wa zahanati hiyo kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mama mjamzito.https://youtu.be/kF6wJDt_BIo
Hatua ya kwanza ya upanuzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere yaelezwa kukamilika kwa asilimia 65. https://youtu.be/Z-PW1LOT9bA

Zaidi ya shilingi bilioni 3 zimetumika katika ujenzi wa stendi mpya Kisasa ya Msamvu Mkoani Morogoro na kupelekea mradi huo kukamilika kwa asilimia 50. https://youtu.be/L05t_EvTLbU

BOFYA HAPA KUONA ZAIDI

Mtandao wa Wanawake na Katiba Waiomba Serikali ya Dk Magufuli

0
0
MTANDAO wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi umeitaka Serikali ya Awamu ya Tano iliyopo chini ya Rais Dk. John Pombe Magufuli ijenge misingi imara itakayoondoa mazingira kandamizi kwa jamii ya chini hasa kwa akinamama. 

Aidha umeitaka serikali kuhakikisha inasimamia ipasavyo suala zima la uwajibikaji na kupambana na vitendo vya kifisadi ambavyo ndivyo vinavyowakandamiza wananchi. Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na jopo la viongozi wanaounda mtandao huo likiongozwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Mtandao, Profesa Ruth Meena walipokuwa wakitoa tathmini juu ya mtazamo wa mtandao huo baada ya Uchaguzi Mkuu na suala zima la usawa wa jinsia kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari. 

 Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Wanawake Tanzania, Mary Rusimbi ambaye ni mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi alisema serikali ya awamu ya tano ina kila sababu ya kumjali mwanamke na kutambua kuwa anamchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi. 

 Alisema Serikali hainabudi kujenga misingi imara ya uwajibikaji wa kweli na kutambua makundi mbalimbali ya jamii kwa jinsia zote. "...Tunataka haki yetu iwe haki kweli kweli na itambulike huku ikiwa nautekelezaji wa vitendo na kwa uhakika," alisisitiza Bi. Rusimbi.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi, Profesa Ruth Meena (kushoto) akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania. Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi, Profesa Ruth Meena (kushoto) akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania.Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Wanawake Tanzania, Mary Rusimbi (kushoto) ambaye ni mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi, Profesa Ruth Meena. Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Wanawake Tanzania, Mary Rusimbi (kushoto) ambaye ni mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi, Profesa Ruth Meena.
Mjumbe wa Mtandao huo, Dk. Ave-Maria Semakafu (kulia) akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam. Mjumbe wa Mtandao huo, Dk. Ave-Maria Semakafu (kulia) akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

SIMU TV: UCHAMBUZI WA HABARI ZA MAGAZETINI

0
0

SIMU.TV:  Spika Ndugai awaeleza wabunge kuwa wao ndio watakaomfanya awe mzuri au mbabe. Mwesiga asema ana imani na Mh.Majaliwa;https://youtu.be/mL0sBHXF0cM  
 SIMU.TV:  Rais Magufuli akata Sh.Mil. 235 za sherehe na kuagiza zipelekwe Muhimbili. Awapasha UKAWA, amfagilia Zitto; https://youtu.be/6QlhJ2XQHmw 
 SIMU.TV:  Elias Maguri auzwa TP Mazembe kwa Shillingi milioni 100. Yanga yapiga mtu 10, Mkwasa ashitakiwa FIFA; https://youtu.be/KuTKm1n4SGU 
 SIMU.TV:  Pata habari motomoto za kisiasa zilizotawala katika magazeti ya leo Novemba 21.2015 hapa Simu.Tv; https://youtu.be/LdJpmYtb7ZY

TASWIRA MBALIMBALI ZA RAIS MAGUFULI ALIPOLIHUTUBIA BUNGE MJINI DODOMA

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akihutubia Bunge la Jamhuri kama ishara ya kuzindua Bunge la 11.
Kabla ya Rais Dkt. Magufuli kuzindua Bunge, Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju aliomba Bunge likubali kutenguliwa kwa kanuni za Bunge ili kuruhusu wageni kuingia ndani ya Bunge hilo.
Wabunge walionesha kuridhishwa na hotuba ya Mhe. Rais Makufuli, wakipiga meza kuunga mkono hotuba hiyo.
Mhe. Rais Dkt. Magufuli (wa pili kushoto) akiwa na Marais Wastaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa pili kulia), Benjamin Wiliam Mkapa (kulia) na Alhaj Ali Hassan Mwinyi (kushoto).

Jengo la tatu la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere lakamilika asilimia 65

0
0
Jengo la tatu la abiria (TB III) linalojengwa katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Jijini Dar es Salaam limekamilika kwa asilimia 65 na linavutia.

Jengo hilo lenye uwezo wa kuchukua abiria milioni 6 kwa mwaka limewavutia wahandisi ujenzi  kutoka mkoa wa Pwani waliolizuru leo na  wadau wa usafiri wa anga jana.

Akizungumza kwa niaba ya Wahandisi wenzake leo, Mhandisi Michael Mrema amesema, mradi huo ni mkubwa, mzuri na wenye tija kwa uchumi wa nchi na kwamba wamefurahi kupata nafasi ya kujifunza ulivyo.

Meneja Mradi wa Bam International ya Uholanzi inayojenga jengo hilo, Eric Van Zuthem amesema leo, wamefurahi kupata fursa ya kuwajengea Watanzania hasa wadau wa usafiri wa anga jengo hilo la aina yake.

“Jengo hili litakuwa la kimataifa kutokana na vifaa vya usalama vitakavyofungwa hasa ukizingatia hivi sasa kuna matukio ya ugaidi kama yaliyotokea Ufaransa karibuni. Ni furaha kufanya kazi na TAA na wadau pia kuwajengea Watanzania, jengo zuri litakalovutia wageni.’ amesema.

Mkurugenzi wa Mradi wa TB III, Mhandisi Mohammed Millanga amesema, mradi huo unaotekelezwa kwa awamu mbili, utakamilika mwaka 2017. Amesema awamu ya kwanza inatarajiwa kukamilika Juni 2016.

Amewaeleza Wahandisi hao kuwa Mkandarasi, Bam International alipewa zabuni moja ya kujenga kwa awamu mbili ambapo awamu ya pili inatarajiwa kuanza hivi karibuni baada ya Serikali kuridhia kutolewa fedha.

Amewaeleza wahandisi hao jengo hilo linajengwa kwa gharama ya Euro milioni 235 (sh. Bilioni 518). Awamu ya kwanza inagharimu Euro milioni 133.2 (sh. Bilioni 293) na ile ya pili itagharimu Euro milioni 102 (sh. Bilioni 225).Kati ya fedha hizo, asilimia 85 inagharamiwa na Benki ya HBSC ya Uingereza kupitia mkopo unaodhaminiwa na Serikali ya Uholanzi na asilimia 15 Benki ya CRDB za mkopo unaodhaminiwa na Serikali ya Tanzania. Tayari Uholanzi imetoa fedha za awamu ya pili ili kazi ianze.
Mbali ya kuchukua abiria milioni 6, jengo hilo litakuwa na miundombinu ya madaraja makubwa ya abiria matano ya kuegesha ndege 18 na ndege moja kubwa aina ya  Airbus 380. Pia litakuwa na migahawa, sehemu za kusali, watoto kucheza na theluthi moja yake  ni sehemu za biashara.

Jana wadau kutoka mashirika ya ndege, wauza tiketi za ndege, wauzaji vifaa vya ujenzi, mawakala wa mizigo ikiwemo Swissport, maofisa ubalozi walizuru jengo hilo na kusifu ubora wake, miundombinu na viwango vyake.

Kutokana na abiria wanaotarajiwa kuongezeka baada ya jengo hilo kukamilika, Mhandisi Millanga amesema TAA inafikiria kuongeza njia za kurukia ndege ziwe mbili ili kukidhi mahitaji ya ongezeko la ndege zirukazo JNIA.


Amesema TAA inafikiria kuongeza njia hiyo ili moja itumiwe na ndege ndogo tu na nyingine kubwa. Kwa sasa JNIA ina njia moja ya kurukia ndege na abiria wanaopita jengo la pili la abiria, wanakadiriwa kuwa milioni 2.5. 

Sehemu ya mbele
Sehemu ya  nyuma
Ubavuni

Wateja wa Airtel kupata ofa ya simu bomba kupitia SMARTIFONIKA Bazaar

0
0
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa mara nyingine imekuja na ofa kabambe kupitia SMARTFONIKA Bazaar na kuwawezesha wateja kupata simu mbalimbali za kisasa katika msimu huu wa sikukuu

Gulio la simu yaani smartphone Bazaar litakuwa katika maeneo ya Mlimani City na Quality Center kuanzia siku ya Ijumaa, Jumamosi na Jumapili. Watanzania watapata nafasi ya kuchagua na kununua simu za aina ya smartphone inayokidhi mahitaji yao kwa bei nafuu. Ofa hii pia itapatikana katika maduka ya Airtel nchi nzima.

Akiongea kwa niaba ya Airtel, Meneja Uhusiano wa Airtel , Jackson Mmbando alisema” Tunayo furaha kutambulisha ofa hii kabambe katika msimu huu wa siku kuu itakayowawezesha wateja wetu kununua simu kwa matumizi yao binafsi na kwaajili ya wapendwa wao kwa bei nafuu kuliko zote sokoni.

Simu zitakazopatikana katika Smartphone Bazaar ni pamoja na simu aina ya Magnus Bravo Z10 inayokuja na kifurushi cha kuanzia cha bure chenye dakika 150 za kupiga simu, SMS 150 pamoja na kifurushi cha internet chenye ujazo w MB 150 kila mwezi kwa muda wa mienzi 6 kwa gharama ya shilingi 75,000/=. Magnus Z10 ni simu yenye screen kubwa inayomuwezesha mteja kuona taarifa mbalimbali kwa urahisi zaidi battery yake inadumu kwa muda mrefu

Sambamba na simu ya Magnusa Bravo Z10 wateja wetu watapata simu mbalimbali za kisasa za aina ya Samsung, Huawei, Tecno na Star times ambapo wateja wakinunua watapata ofa kabambe kutoka Airtel.

“Tunaamini simu hizi zitakuwa simu muafaka kwa watumiaji wa mara ya kwanza wa simu aina ya smartphone kuweza kupata uzoefu tofauti na kufurahia huduma mbalimbali ikiwemo huduma ya internet toka Airtel.

Natoa wito kwa wateja wetu kuwa wakwanza kupata simu hizi za kisasa kwa kutembelea maduka yetu na gulio la simu katika maeneo ya mlimani city na Quality center kila mwisho wa wiki.” Aliongeza Mmbando
Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando akionyesha simu aina ya Magnus Bravo Z10 iliyo na ofa ya kifurushi cha kuanzia cha bure chenye dakika 150 za kupiga simu, SMS 150 pamoja na kifurushi cha internet chenye ujazo w MB 150 kila mwezi kwa muda wa mienzi 6 katika uzinduzi wa Smartphone Bazaar iliyopo Mlimani City. Pichani ni wafanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja wa Airtel
Moja ya wateja waliotembelea Smartphone Baazar Mlimani City akijipatia simu yake aina ya Magnus Bravo Z10 iliyo na ofa ya kifurushi cha kuanzia cha bure chenye dakika 150 za kupiga simu, SMS 150 pamoja na kifurushi cha internet chenye ujazo w MB 150 kila mwezi kwa muda wa mienzi 6 toka kwa watoa huduma wa Airtel Bi Zainab Hamidu. Airtel imezindua Smartphone Bazaar katika msimu huu wa sikukuu ili kuwawezesha watanzania kupata simu bomba za kisasa kwa bei nafuu.
Meneja kitengo cha huduma za Internet na simu , James Kagashe (wa kwanza kushoto) akiongea na wateja mbalimbali waliotembelea Airtel Smartphone Bazaar katika eneo la mlimani city kujipatia simu bomba na za kisasa zenye ofa za vifurushi vya muda wa maongezi, sms na intaneti kwa gharama nafuu.

Mwinyi awaasa wanafunzi kuchangamkia fursa ya kupata taaluma Chuo Kikuu cha Kampala

0
0
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kampala International cha jijini Dar es Salaam,Rais Mstaafu wa Tanzania Mheshimiwa Ali Hasani Mwinyi amewataka watanzania kuchangamkia fursa za masomo ya taaluma mbalimbali nanayotolewa na Chuo Kikuu cha Kampala kilichopo eneo la Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.

Akiongea wakati wa mahafali ya tatu ya chuo hicho kwa upande wa Tanzania jana ambapo wahitimu walitunikiwa shahada ,stashahada na vyeti vya kufuzu fani mbalimbali alisema chuo hicho kinatoa elimu bora kwenye fani mbalimbali na kuwataka watanzania kuchangamkia fursa za kujiendeleza ili wapate maarifa ya kuwawezesha kupambana katika soko la ajira ikiwemo kupata maarifa ya kuwawezesha kujiajiri kutokana na elimu watakayokuwa wameipata.

Alipongeza wawekezaji kwenye sekta ya elimu na kuiomba serikali kushirikiana nao li nchi iweze kupata wataalamu wa kutosha “Napongeza kwa uwekezaji huu na tunaomba serikali izidi kuunga mkono wawekezaji katika sekta ya elimu ili Taifa liweze kupata wataalamu wa kutosha.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Mohamed Ndaula alisema kuwa chuo kimejipanga kuendelea kutoa elimu bora kuanzia kwenye miundombinu na walimu waliobobea katika fani mbalimbali na uzoefu mkubwa wa kufundisha vyuo vikuu sehemu mbalimbali duniani.

Pia alisema kuwa Chuo hicho kimefanikiwa kupata leseni ya kujiendesha nchini badala ya kuwa Chuo Kikuu kishiriki cha Chuo Kikuu Cha Kampala kilichopo nchini Uganda.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kampala International cha jijini Dar es Salaam, Rais mstaafu wa Tanzania Mh.Ali Hassan Mwinyi akiongozana na wahadhiri wa Chuo Kikuu hicho wakielekea kwenye uwanja wa hafla ya mahafali yaliyofanyika chuoni hapo eneo la Gongo la Mboto jana.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kampala International cha jijini Dar es Salaam, Rais mstaafu wa Tanzania Mh.Ali Hassan Mwinyi (watatu kutoka kulia) na viongozi wa chuo hicho wakiwa wamesimama wakati unaimbwa wimbo wa Taifa kabla ya kuanza hafla ya mahafali ya 3 yaliyofanyika chuoni hapo eneo la Gongo la Mboto jana jana ambapo wahitimu walitunukiwa shahada,stashahada na vyeti katika fani mbalimbali.
Sehemu wa wanafunzi waliohitimu chuoni hapo jana.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Kampala Internatinal cha Dar es Salaam Profesa Mohamed Ndaula akitoa hotuba wakati wa mahafali 3 yaliyofanyika chuoni hapo eneo la Gongo la Mboto jana jana ambapo wahitimu walitunukiwa shahada,stashahada na vyeti katika fani mbalimbali.

KONGAMANO LA MABADILIKO YA TABIANCHI LAFANYIKA KATIKA KIJIJI CHA MAKUMBUSHO,JIJINI DAR

0
0
ASASI za Kiraia nchini zikiwemo Oxfam Tanzania, Forum CC na Norwegian Church Aid Actalliance  zafanya kongamano  la Kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa Chakula nchini.

Akizungumza  Afisa Miradi Msaidizi wa Shirika la Forum CC,Jonathan Sawaya alisema asasi hizo zimeona ni vema kuwakilisha sauti za wakulima  kwa serikali katika kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.

Alisema  asilimia kubwa ya wakulima wengi hasa wanawake ambao karibia asilimia 70 wamekuwa wakiathirika na Mabadiliko hayo wakati wanapolima.

Sawaya alisema  wananchi wanapaswa kuhifadhi mazingira na kutunza vyanzo mbalimbali vya maji  ili kupunguza athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.

"Kwa kushirikiana  na shirika la Oxfam pamoja na Norwegian Church Aid  tumeamua kufanya kongamano hili ili kupaza sauti za wakulima na wafugaji katika suala zima la kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na serikali kutilia mkazo katika kusimamia suala hili kwa kuongeza bajeti,"alisema Sawaya
Aidha alisema asilimia kubwa ya wanawake wameonyesha juhudi mbalimbali za kukabiliana na athari hizo kutokana na wao kujihusisha katika uzalishaji wa chakula.

"Tuwaunge mkono wazalishaji wa chakula wadogo,wafugaji pamoja na wavuvi  katika suala hili kwa kuwaunganisha na masoko na kuwapa mikopo,"alisema

Aidha Kongamano  hili limehusisha wadau mbalimbali wakiwemo watendaji wa serikalini,wakulima pamoja na wafugaji katika kuhakikisha mabadiliko ya tabia nchi yanatokomezwa.

"Kongamano hili ni sehemu ya maandalizi ya  Mkuu wa  21 wa Mkutano wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi unaotarajia kufanyika Novemba 30 nchini Ufaransa,"alisema Sewaya.
 Eva Mageni  ambaye ni Rais wa wakulima wanawake vijijini na alikuwa mshiriki wa shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015, akifungua kongamano la Mabadiliko ya Tabianchi ambapo alizungumzia kwa kifupi kuhusu mkutano wa COP21 ambao utafanyika Paris Ufaransa hivi karibuni.
 Edward Tunyone kutoka Forum CC akieleza maana zaidi ya Mabadiliko ya Tabianchi ambapo alielekeza mazungumzo yake katika majanga asilia, mito kupotea kutokana na shughuli za wanadamu kama kulima jirani na maeneo hayo, mwisho alisisitiza swala la mabadiliko ya Tabianchi ni jukumu la kila mtu na taasisi zinazohusika na mamswala hayo tu.
Baadhi ya washiriki katika Kongamano la Mabadiliko ya Tabianchi.


MTEMVU AFUNGUA KESI YA KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI JIMBO LA TEMEKE

0
0
 Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, (hawapo pichani), ambapo aliwaeleza kuwa amefungua kesi ya kupinga matokeo ya ubunge wa Jimbo la Temeke,ili haki ipatikane. Kushoto ni Katibu wa Jimbo la Temeke,  Kassim Kiame.
Walioshitakiwa ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, ambaye pia ni Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Temeke, Protidas Kagimbo Mbunge aliyeshinda, Abdallah Mtolela na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, (PICHA NA KHAMIS MUSSA)

RAIS ATEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO MJINI UNGUJA

0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa  Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka ya Mji Mkongwe wa Zanzibar Nd,Mussa Awesu Bakari wakati alipokuwa akiangalia ramani ya Mradi wa ujenzi wa Ukuta wa Forodhani Mjini Unguja leo akiwa katika ziara maalum ya kutembelea maendeleo ya Miradi mbali mbali Mjini
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akimuuliza sualaKaimu Mkurugenzi wa mamlaka ya Mji Mkongwe wa Zanzibar Nd,Mussa Awesu Bakari wakati alipokuwa akiangalia   Mradi wa ujenzi wa Ukuta wa Forodhani Mjini Unguja leo akiwa katika ziara maalum ya kutembelea maendeleo ya Miradi mbali mbali Mjini
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akipata maelezo ya ramani ya ujenzi wa Mtaro wa maji ya Mvua katika viwanja wa mnazi mmoja kutoka kwa Mhandisi wa Manispaa ya Zanzibar Mzee Khamis Juma wakati alipotembelea mradi huo wa ujenzi unaojengwa na kampuni ya CRJ kutokaChina
 Wajenzi kazini
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akipata maelezo ya ramani ya ujenzi wa Mtaro wa maji ya Mvua katika viwanja wa mnazi mmoja. Picha na Ikulu, Zanzibar

MSAADA WAHITAJIKA KWA MAPACHA WALIOUNGANA

0
0
Hawa watoto Zahra na Zarina wamezaliwa pacha walioungana tarehe 16/11/15  mama yao Bi Tausi Hageze akiwa njiani kwenye boda boda akitokea kijiji cha Nyarurema Tarafa ya Rulenge Wilaya ya Ngara akielekea hopitali ya misheni Rulenge. Alipopata uchungu wa kuzidi alimuomba bodaboda asimame akaweza kujifungua kwa shida mbele ya mumewe anaeitwa Hamdani hapo njiani.
Baada ya hapo wakapelekwa hospitali ya misheni Rulenge. Mama na watoto wako salama, kama unavyo ona katika picha wameungana kiunoni. Msamaria  amekutana na changamoto hii hapo hospitali na kuamua kuwasaidia kuchangisha iliwapelekwe Mwanza Bugando Hospital walipo hivi sasa. 
Inaelezwa na ma daktari hapo wameshauri watoto wapelekwe India kwa upasuji na matibabu zaidi.
Msamaria anaewasaidia Bi Sabra Said Salum wa namba ya simu +255767220099 anaomba yoyote atakae guswa na kadhia hii afikishe mchaango kwake ili aweze kuwafanyia safari hii muhimu kuokoa maisha ya mapacha hawa.
Baba Hamdani Sibhoro na mama Tausi Hageze wote ni wakulima wa jembe la mkono hawana uwezo hata wa kufika Dar.  Bi Sabra kachangisha na kuweza kuwafikisha Bugando, kuwalipia mahitaji ya hapo.

Mungu awabariki

TAARIFA YA KAIMU MKURUGENZI WA UCHAGUZI TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI NDG. EMMANUEL KAWISHE KUHUSU UPIGAJI KURA KATIKA UCHAGUZI UTAKAOFANYIKA TAREHE 22 NOVEMBA, 2015 KATIKA MAJIMBO MAWILI NA KATA SITA

0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa taarifa kuhusu upigaji kura katika uchaguzi utakaofanyika kesho tarehe 22 Novemba, 2015 katika majimbo mawili na kata sita ambapo uchaguzi wake ulihairishwa.
Akitoa taarifa hiyo leo jijini Dar es salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi, Tume ya Taifa ya uchaguzi Bwa. Emmanuel Kawishe amesema kuwa Tume ilitoa taarifa kwa kuhairishwa kwa Uchaguzi katika Jimbo ya Lushoto mkoani Tanga, Jimbo la Ulanga Mashariki mkoani Morogoro, kata ya Muleba, Uyole, Bukene, Msingi, Bomang’ombe pamoja na kata ya kasulo kutokana na vifo vya wagombea.
“Kesho ni siku ya kupiga kura ya kuchagua Mbunge katika majimbo mawili na kuchagua Diwani katika kata sita, natoa rai kwa wale wote mliojiandikisha kama wapiga kura katika majimbo na kata hizo kujitokeza kwenye vituo mlikojiandikisha ili kuweza kupiga kura na kuwachagua viongozi mnaowataka bila hofu, woga wasiwasi au ushawishi” aliongeza Kaimu Mkurugenzi huyo.
Hata hivyo Bwa. Kawishe alisema kuwa vituo vitafunguliwa kuanzia saa moja asubuhi na kufungwa saa kumi jioni  na kuwakumbusha wapiga kura kubeba kadi yake ya mpiga kura.
“Kipaumbele kitatolewa kwa wagonjwa, watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali, wanawake wajawazito au wenye watoto wachanga na wazee ambao hawatatakiwa kujipanga kwenye foleni”
“Wakati wote wa kupiga kura na kuhesabu kura, mawakala wa vyama vya siasa wawepo kwenye vituo na wajibu wao ni kulinda maslahi ya vyama vyao na wagombea hivyo hawatakiwi kuingilia masuala ya utendaji ambayo yamekabidhiwa kwa msimamizi wa kituo” alifafanua Bwa. Kawishe.
 Mbali na hayo Tume ya Taifa ya Uchaguzi amewapongeza wananchi kutoka majimbo na kata zinazofanya uchaguzi kesho kwa uvumilivu waliouonyesha katika kipindi chote cha kusubiri siku ya kupiga kura kumchagua Mbunge au Diwani wao.

WAZIRI MKUU MAJALIWA KASSIM MAJALIWA KWENYE MCHAPALO WA KUZINDUA BUNGE

0
0
 Waziri  Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa  akizungumza na  Mke wa Rais Mstaafu wa  Awamu ya Nnne , Mama Salma Kikwete katika hafla fupi  iliyoyofanyika kwenye viwanja vya Bunge mjiniDodoma  baada ya Rais John Magufuli kuzindua Bunge Novemba 2015
 Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  akisalimiana na  Rais Mstaafu wa  Zanzibar, Aman Abeid Karume katika hafla fupi  iliyofuatia  kuzinduliwa kwa Bunge na Rais John Magufuli kwenye  mjini Dodoma Novemba 20, 2015. Hafla hiyo ilifanyika kwenye viwanja vya Bunge
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akifurahia jambo katika mazungumzo na Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde (kushoto) na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Abdallah Bulembo katika hafla fupi ya kuzindua bunge iliyofanyika kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Novemba 20, 2015.
  Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza na  Spika wa Bunge Job Ndugai (kushoto) , Mkewe Mary  (wapili kushoto) na  Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilila  (wapili kulia) katika hafla ya  kuzindua Bunge iliyofanyika kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Novemba 20, 2015
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Kassim  akizungumza na baadhi ya wabunge  na waalikwa waliohudhuria hafla fupi  iliyofanyika kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma  baada ya Rais John Magufuli kuzindua Bunge Novemba  20, 2015. Picha na PMO

TASWIRA MBALIMBALI LEO KATIKA UJENZI WA TAIFA, KIBAHA MKOANI PWANI

0
0
  Wazee wa kazi wakiwa katika kazi ya ujenzi wa Taifa (a.k.a Zege halilali) leo walipo naswa na kamera ya Mtaa kwa Mtaa Kibaha Mkoani Pwani.
Wanamama ambaye jina lake halikupatikana mara moja akiwa katika ubora wake wa kuchanganya zege ili lisilale kama alivyonaswa na kamera ya Mtaa kwa Mtaa leo Kibaha mkoani Pwani. 
Hapa kazi tuu walisikika wakisema.

KAMPENI YA NSSF KWANZA YAWAFIKIA WATU WENGI MKOANI MBEYA

0
0

Wananchi wa Kijiji cha Igamba ambao ni wakulima wa Kahawa wakipiga picha ya pamoja baada ya kupata elimu na kujiunga na NSSF kama wanachama wa Hiari chini ya Mpango wa Wakulima Scheme ambao utawasaidia Kupata Matibabu bure na Kujipatia Mikopo ya pembejeo.
Maafisa wa NSSF mkoa wa Mbeya wakiwaandikisha watu kutoka Sekta binafsi waliokusanyika kwenye kituo cha mabasi cha mbalizi kwenye kampeni maalum ya NSSF ya kutoa elimu na kuandikisha wanachama Mkoani mbeya ili kuongeza wigo wa wanachama.
 Meneja wa NSSF Mkoa wa mbeya, Robert Kadege akimsaidia mmoja wa Madereva wa Bodaboda kujaza fomu ya NSSF kwa ajili ya Kumuandikisha kujiunga na NSSF.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Magufuli zawadi ya Mungu kwa Watanzania

0
0


Na mdau Ruger Kahwa

Awali ya yote napenda kumpongeza Mh. Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tangu alipokuwa waziri wa ujenzi alikuwa anonyesha dhahiri kuwa ana nia ya dhati ya kuwatumikia watanzania, na sio maslahi yake mwenyewe na familia yake. 
Chama chetu cha CCM kilitambua hilo na kumpendekeza kuwa mgombea urais wa Tanzania. Naamini ndani ya chama kuna watu walikuwa na kiu na shauku ya kuwa marais kwa ajili yao na marafiki zao, lakini Mungu wetu hakuruhusu hili litokee. 
Hakurusu hilo litokee kwa sababu Mungu anayajua matatizo ya watanzania na ametupa mtu sahihi ili atukumboe. Katika kipindi kifupi tangu alipoapishwa kuwa Rais ameonyesha kasi ya ajabu na nia ya dhati ya kutaka kuwasaidia watanzania. 
Ziara zake za kushtukiza na jana kuamuru mamilioni ambayo yangetumika kwa party ya wabunge yapelekwe Muhimbili kununua vitanda ni ushahidi tosha wa nia yake ya dhati ya kuwasaidia Watanzania. 
 Mheshimiwa Rais, umeanza vizuri sana, na naomba uwabane watendaji wa ngazi zote kuanzia mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya, makatibu wakuu,wakurugenzi,makatibu tarafa na kata na hata watendaji wa vijiji wafanye kazi , kwani wengi wao wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea na kufanya siasa tu. 
Wananchi katika ngazi za wilaya, kata na vijiji wana shida nyingi. Na asilimia zaidi ya tisini ya shida hizo zinasababishwa au zinachochewa na watendaji wabovu au wazembe wanaofanya kazi kwa mazoea na manufaa yao binafsi. Nimeona wananchi wanadhulumiwa mali zao vijijini(hasa yatima na wajane), wanabambikiwa kesi. 
Watu wenye pesa wamekuwa wakinunua haki. Kwa kweli inaumiza sana. Mabaraza ya usuluhishi ya kata ndio kabisa, haki haipatikani ni posho kwa kwenda mbele. Kwa mtindo huu mtu maskini hapati haki. Hali ni ngumu. 
Wananchi tuna imani kubwa sana na wewe na kama ulivyosema hutatuangusha na sisi tunasema watendaji wako wasikuangushe. Kwa mantiki hiyo basi , itakuwa vyema ukapangua na kupanga safu yako vizuri hasa ngazi ya chini ya wakuu wa wilaya. Tukipata watu wa zuri na waaminifu katika ngazi hizo tutaanza na mwanzo mzuri . Katika ngazi hiyo tunataka watu wachapa kazi na sio wapiga siasa mchana kutwa. 
 Mungu ameipenda Tanzania na kutupatia kiongozi kama wewe, mcha Mungu,mchapakazi, mkweli na hanayechukia unafiki. 
Na sasa Mh. Rais tunaomba utupangie safu ya watu wacha Mungu, wachapa kazi, wakweli na wanaochukia unafiki, kwani msema kweli ni mpenzi wa Mungu. 
 Hata ikibidi ubadilishe asilimia tisini ya wakuu wa wilaya na viongozi wengine ni sawa tu, ili mradi watanzania wafaidike na matunda ya nchi yao wenyewe. Wewe ni zawadi kutoka kwa Mungu. Na wapenda haki wote tuko nyuma yako. 
 Asante

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

0
0


 SIMU.TV: Rais Magufuli ametaja vipaumbele atakavyovizingatia wakati wa kutekeleza majukumu yake kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.https://youtu.be/QvzOHNI9u88
 SIMU.TV: Hofu ya kipindupindu imetanda kwa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Hai Kilimanjaro kutokana na vyoo kujaa. https://youtu.be/jMHD9Zc5ovE
 SIMU.TV: Yafahamu na kuchambua mengi hapa kuhusiana na vyombo vya habari jinsi walivyochambua uteuzi wa Maspika na Waziri mkuu: https://youtu.be/cYK0dC9zeKQ
 SIMU.TV: Mtandao wa Wanawake, katiba na Uchaguzi umelaani kitendo cha baadhi ya Wabunge kumzoea naibu spika wakati akijielezea. https://youtu.be/gG-PKOP5CgY
 SIMU.TV: Fahamu mengi hapa kuhusiana na masuala mbali mbali ya utendaji wa viongozi na sifa muhimu anazotakiwa kuwa nazo kiongozi bora:https://youtu.be/O6sX2LBm8fE
 SIMU.TV: Chambua na kuyajua mengi hapa kutoka kwa wadau wa michezo kuhusiana na michuano ya Mashindano ya kawambwa mjini bagamoyo:https://youtu.be/MIYTRh6B5Hk
 SIMU.TV: Yajue mengi hapa kuhusiana na magezeti mbali mbali jinsi walivyochambua habari za uteuzi wa waziri pamoja na hotuba ya kwanza ya Rais:https://youtu.be/H0jGtBTLOdc
 SIMU.TV: Fahamu mengi hapa kuhusiana na masuala mbali mbali ya utendaji wa viongozi na sifa muhimu anazotakiwa kuwa nazo kiongozi bora:https://youtu.be/O6sX2LBm8fE

Habari zaidi BOFYA HAPA

WAKULIMA WA KAROTI WALIA NA BEI YA ZAO HILO

0
0
Kiroba cha karoti ambacho kwa huko shambani kinauzwa kwa shilingi elfu tano tu fedha ambazo inasemekana ni kidogo ikilingamishwa na uzalishaji wa zao hilo
 Wakulima mashuhuri wa mbogamboga ikiwemo karoti katika kijiji Ndabwa wilaya ya Lushoto mkoani Tanga, Rehema Shegulio  (kushoto) na Hadija Shabani wakiwa wameshikilia karoti zao ambazo ni kubwa mithili ya mihogo. Picha na Vedasto Msungu 

ONLY IN TANZANIA: RAIS MAGUFULI AKIWA NA MARAIS WASTAAFU BUNGENI DODOMA

0
0
Andika caption ya taswira hii kwenye sehemu ya maoni. Ikivutia  zaidi ya zote utapata zawadi ya fulana ya #HAPAKAZITU.
Mwisho wa kutuma caption ni Kesho Jumapili saa sita usiku.

WADAU ARCHBOLD NA AGNESS WAMEREMETA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 Wadau waandamizi wa Globu ya Jamii Archbold Josaphat Kiwia na Agnes Samwel Likongo wamemeremeta leo katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam. Wadau hawa, ambao ni wafanyabishara maarufu wa mbao, hivi sasa wanaelekea hoteli ya Serena kwa mnuso wa nguvu waliouandaa. Globu ya Jamii inawatakia Archbold na Agness maisha mazuri na ya furaha!
 Bwana harusi amvisha pete mkewe
 Bi Harusi amvisha pete mumewe 
 Archbold akimwaga wino
Agness naye anamwaga wino
Viewing all 109606 articles
Browse latest View live




Latest Images