Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1030 | 1031 | (Page 1032) | 1033 | 1034 | .... | 3270 | newer

  0 0

  BENKI  ya Barclays hapa nchini inatarajia kuwaletea wapenzi na Mashabiki wa soka kombe la ligi kuu ya Uingereza kwa ajili ya kupiga nalo picha ikiwa mwaka huu ni mwisho wa benki hiyo kudhamini ligi kuu nchini Uingereaza, Pia wananchi wameombwa kujitokeze kufungua akaunti kwa ajili ya mshara katika benki hiyo ili kujishindia tiketi mbili za kwenda kuangalia ligi kuu ya Uingereza.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar,Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Masoko benki ya Barclays, Joe Bendera alifafanua kuwa  "Wapenzi wa soka wajitokeze kwa mujibu wa ratiba ya benki a Barclays kwaajili ya kugipatia picha wakiwa na kombe la benki hiyo ikiwa ni mwaka huu ni wa mwisho kudhamini ligi kuu ya Uingereza iliyokuwa ikijulikana kama Barclays Premier League." Bendera 

  Nae Mkuu wa kitengo cha Bidhaa katika benki ya Barclays, Oscar Mwakyusa  amesema kuwa  Disemba 3 mwaka huu kombe hilo litaanzia katika tawi kuu la benki benki hiyo Posta kuelekea Mwembe yanga kupitia barabara ya Pungu mpaka Temeke Hospitali, Uwanja wa Taifa, kituo cha magari cha Mombasa na kumalizia viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.

  Na Disemba 4 litaanzia kutembezwa kutokea katika benki ya Barclays tawi la Alpha kuelekea ofisi za IPP Media, Mlimani City, tawi la benki hiyo la Slip way Kinondoni Biafra, Mazese Darajani na kuishia katika viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam.

  Aidha Mwakyusa aliyoa wito kwa wapenzi wa soka kujitokeza kwa wingi kwaajili ya kupiga picha na kombe la ligi kuu ya Uingereza ambapo mwaka huu ni mwisho wa benki ya Barclays kudhamini ligi kuu Uingereza.
  Mkuu wa kitengo cha Bidhaa katika benki ya Barclays, Oscar Mwakyusa na Kaimu mkuu wa kitengo cha Masoko benki ya Barclays, Joe Bendera wakiwa wameshika picha ya kombe la mpira ambayo litatembezwa Disemba 3 na 4 mwaka huu jijini Dar es Salaam kwaajili ya wapenzi wa mpira wa miguu kupiga nalo picha ikiwa mwaka huu benki ya Barclays ni mwisho wa kudhamini ligi kuu uingereza.
  Kaimu Mkuu wa kitengo cha Masoko benki ya Barclays, Joe Bendera akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na benki hiyo kutembeza kombe la Barclays premier ligi ya Uingereza kulitemeza jijini Dar es Salaam kwaajili ya wapezi wa soka jijini hapa kupiga nalo picha ambazo itakuwa kumukumbu kwao.Kusoto ni Grace Josef na kulia ni Rhobina Justine wakiwa ni miongoni wa washiriki wa benki hiyo katika kutembeza kombe hilo jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa kitengo cha Bidhaa katika benki ya Barclays, Oscar Mwakyusa akizungumza na waandishi wa habari kuhuriana na ratiba ya kombe hilo litakavyokuwa likizungushwa ili wapenzi wa soka kupiga picha na kombe ikiwa benki ya Barclays ni mwaka wa mwisho kudhamini ligi ya Uingereza.

  0 0

   Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Dianna Melrose (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF), Koshuma Mtengeti (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Wanawake wa Afya, Utafiti na Maendeleo (Forward), Naana Otoo-Oyortey MBE, wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Filamu ya Simulizi halisi ya Ghati na Rhobi ulifanyika nyumbani kwa balozi huyo, Oysterbay Dar es Salaam jana.
   Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Dianna Melrose (kulia), akizungumza kabla ya uzinduzi wa filamu hiyo.
   Mwakilishi kutoka taasisi ya DFID, Jane Miller OBE (kushoto), akizungumza katika uzinduzi huo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF), Koshuma Mtengeti na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Wanawake wa Afya, Utafiti na Maendeleo (Forward), Naana Otoo-Oyortey MBE.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Watoto wawili wa familia moja wakazi wa mkoani Singida wamefariki mara baada ya kuangukiwa na nyumba kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani humo. https://youtu.be/E4vbul_POEc
  Mkuu wa wilaya ya Tarime amewataka viongozi wa halimashauri ya walayani humo kuacha siasa maofisini badala yake wawajibike ipasavyo. https://youtu.be/WeGWoXpvFa8
   Bodi ya Korosho nchini imesema itaendelea kutoa asilimia 7 ya ushuru  wa mauzo ya Korosho nje ya nchi kwa lengo la kuimarisha shughuli za utafiti wa zao hilo; https://youtu.be/X4SDodiqSxQ

  Inaelezwa kuwa mauzo ya hisa katika soko la hisa la Dar es Salaam yaanza kuongezeka baada ya kushuka wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania; https://youtu.be/sketAaFAyPw
  Mfuko wa pensheni wa PSPF imeingia makubaliano na mfuko wa bima wa  taifa wa NHIF kwa lengo la kutoa bima ya afya kwa wananchama wa PSPF. https://youtu.be/CDoSmMTvtIY
  Raisi wa shirikisho la mpira wa miguu nchini,Bwana Jamal  Malinzi amewataka watanzania kuwa wavumilivu na timu yao ya tifa,Taifa Stars. https://youtu.be/zEOIV3pSjxg
  Wabunge wateule wa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania wamemtaka waziri mkuu ajaye kusimamia serikali ipasavyo; https://youtu.be/pf3wnk-ZIfU

  Serikali ya manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam imepiga marufuku uuzaji wa viwanja kiholela kwa lengo la kuepusha migogoro ya ardhi. https://youtu.be/seBn8GURMpE
  Inaelezwa kuwa hukumu inayomkabili katibu wa jumuiya za kiislamu Tanzania Sheikh Issa Ponda imeharishwa adi tarehe 30 mwezi wa 11 mwaka huu. https://youtu.be/Y29MTgmOKV8
  Serikali kupitia wizara ya nishati na madini imeliagiza shirika la umeme TANESCO kuimarisha kitengo chake cha ukaguzi kuongeza mapato. https://youtu.be/VfxKyrTqTuI
  Raisi wa TFF amesema kipigo ilichokipata Taifa Stars haikihusu uongozi wake kwani TFF imewapa wachezaji kila kitu wanachokita; https://youtu.be/afJ-tr4QmbI

  Klabu ya Simba imetangaza kuwaacha wachezaji wawili katika dirisha hili dogo la usajili.https://youtu.be/JZEI5I_m4tY

  [12:09:52 AM] samwel kamugisha: Taratibu za kukabidhi jina la waziri mkuu bungeni zatolewa ufafanuzi na mkuu wa kitengo cha habari,elimu na mawasiliano cha Bunge. https://youtu.be/NlIfe1rLAN8

  Kitendawili cha wawania kiti cha naibu spika chafikia patamu baada ya wanawake wawili kuwekwa hadharani.https://youtu.be/MHLVC72sWzc
  Makamo wa Raisi wa Tanzania Bi.Samia Suluhu aapa kupambana na uzembe hasa katika suala la utendaji serikalini. https://youtu.be/uoyVms8ey0w

  Tanzania yaelezwa kushika nafasi ya kwanza duniani kwa kuzalisha korosho bora lakini cha kusikitisha ni kwamba Tanzania huuza korodho ghafi nje ya nchi. https://youtu.be/LAAjTzlT9Fc
  Shamra shamra zaendelea kutawala katika viwanja vya bunge huku baadhi ya wabunge wakipongezwa na wageni na familia zao. https://youtu.be/275wNDk17j4
  Mwanasheria mkuu wa serikali atoa ufafanuzi juu ya hoja na mambo mbalimbali yaliyoibuliwa na viongozi wa UKAWA kabla ya raisi Magufuli kuhutubia bunge. https://youtu.be/Fjh_jVY3uEg
  Saa chache zijazo jina la atakaye kuwa waziri mkuu wa 11 wa Tanzania litafahamika na kutangazwa bungeni huku baadhi ya watu wakihusishwa. https://youtu.be/QsP5eif6QHY

  0 0

  Waziri Mkuu mpya Mh. Kassim Majaliwa.

  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, muda mfupi uliopita limepitisha jina la Mbunge wa Jimbo la Rwangwa, Mh. Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Serikali ya awamu ya tano baada ya jina lake kupelekwa Bungeni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

  Mh. Majaliwa amepitishwa kwa kura 258 sawa na asilimia 73.5% ya kura zote za ndio.

  0 0


  0 0

  Dkt. Tulia Ackson Mwansasu

  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limempitisha Dkt. Tulia Ackson Mwansasu kuwa Naibu Spika wa Bunge, kwa kuta 250 sawa na 71.2% dhidi ya mpinzani wake, Mh. Magdalena Sakaya aliepata kura 101 sawa na 28.8%. 

  0 0

   Mhandisi wa Manispaa ya Kinondoni, Baraka Mkuya akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salam leo na kuwaomba wananchi wa eneo la Basihaya kata ya bunju kuwa watii wa sheria bila shuruti wakati wa ubomoaji wa majengo yaliyojengwa kwenye sehemu za wazi, pia amewahi wananchi kujua maeneo ya wazi yaliyo karibu nao, pia ameongezea kuwa wananchi wakiona maeneo ya wazi yanajengwa watoe taarifa manispaa ya Kinondoni au wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi.
  Ubomoaji wa maeneo ya wazi katika Mtaa wa Basihaya Kata ya Bunju jijini Dar es Salaam Ukiendelea.
  Wananchi wakiondoa mbao katika eneo la wazi walipokuwa wameziweka ili kupisha ubomoaji uniendelea.
  Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  Meneja Uhusiano wa kampuni ya TTCL, Nicodemus Thomas (wa pili kulia) akimkabidhi sehemu ya vifaa tiba Ofisa Muuguzi Mkuu wa Kituo cha Afya cha Buguruni, Alvera Mtembelea (wa tatu kushoto) vilivyotolewa na kampuni ya TTCL leo kwa Kituo cha Afya Buguruni cha jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Ofisa Uhusiano wa TTCL, Amanda Luhanga akishuhudia zoezi hilo.
  Meneja Uhusiano wa kampuni ya TTCL, Nicodemus Thomas (kulia) akimkabidhi moja ya mashine ikiwa ni sehemu ya vifaa tiba Ofisa Muuguzi Mkuu wa Kituo cha Afya cha Buguruni, Alvera Mtembelea (wa pili kulia) vilivyotolewa na kampuni ya TTCL leo kwa Kituo cha Afya Buguruni cha jijini Dar es Salaam. TTCL leo imetoa msaada wa mashuka 100, vyandarua 100, maboksi ya dawa mbalimbali pamoja na vifaa tiba ili kukabiliana na changamoto anuai za afya zinazokikabili kituo hicho.
  Meneja Uhusiano wa kampuni ya TTCL, Nicodemus Thomas ( wa pili kulia) akimkabidhi moja ya mashuka Ofisa Muuguzi Mkuu wa Kituo cha Afya cha Buguruni, Alvera Mtembelea (wa tatu kulia)  ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa na kampuni ya TTCL leo kwa Kituo cha Afya Buguruni cha jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Ofisa Uhusiano wa TTCL, Amanda Luhanga akishuhudia zoezi hilo. TTCL leo imekabidhi msaada wa mashuka 100, vyandarua 100, maboksi ya dawa mbalimbali pamoja na vifaa tiba vingine li kukabiliana na changamoto anuai za afya zinazokikabili kituo hicho.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0


  0 0

  KAMPUNI ya SBC Tanzania Limited, watengenezaji na wasambazaji wa vinywaji baridi imepunguza bei ya vinywaji vyake kutoka shillingi mia sita (600) hadi mia tano (500) kwa chupa yenye ujazo wa Mililita 350 na 300.

  Hayo yamesemwa na Meneja Mafunzo na Uwezeshaji Bw.Rashid Chenja (Pichani)alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam na kuongeza kuwa lengo la kupunguza bei ni kutokana na hali ngumu ya uchumi iliyopo.

  “Imekuwa vigumu kwa mnywaji kuweza kudumu bei ya kinywaji akipendacho cha pepsi , gharama za maisha zinapanda kila mwaka na soda imekuwa ghali kiasi cha wananchi wa kawaida kushindwa kumudu kununua soda hivyo kampuni imeamua kupunguza bei” alifafanua Meneja huyo.

  Pia amesema kuwa kampuni ya SBC Tanzania imefanya punguzo hilo  kuanzia tarehe 16/11/2015 kwa vinywaji vya Pepsi, Mirinda,7up, Mountain Dew na Evervess na maeneo yatakayo husika na punguzo hilo la bei ni Dar es salaam,Morogoro, Dodoma, Pwani, Tanga, Lindi, Mtwara na Zanzibar.

  “Ni matumaini yetu mtaendelea kutuunga mkono katika biashara yetu kwa kununua soda zetu kwa bei iliyopendekezwa ya shilingi Mia Tano kwa chupa, shilingi elfu tisa mia nne (9,400) kwa kreti moja na faida kwa wauzaji wa rejareja itakuwa ni shilingi 2500 kwa kila kreti” aliongeza Bw. Chenja.  

  Mbali na hayo Kampuni ya SBC Tanzania Limited inawashukuru wateja wake kwa kuwaunga mkono katika biashara yao kwa kipindi cha miaka 14 hapa nchini.

  0 0


  Dkt Hamisi Kigwangalla Mbunge Mteule Nzega Vijijini CCM.


  MBUNGE mteule jimbo la Nzega vijijini  Dkt Hamisi Kigwangalla  (CCM) ametoa ushauri kwa wizara husika juu ya udhibiti wa kuvuja kwa madawa serikalini na kwenda kwenye maduka binafsi.

  Kupitia ukarasa wake facebook Kigwangalla amesema #‎Sasa Kazi Tu Changamoto ya Udhibiti wa Kuvuja Madawa Kutoka Mfumo wa Serikali Kwenda Kwenye Maduka ya Watu Binafsi ni Katika Mambo ambayo mgombea Urais wa CCM, Ndg. John Pombe Magufuli alionesha kuwa yanamkera sana. Hivyo wananchi wanasubiri kuona nini kitafanyika kutatua changamoto hii...kuna 'expectation gap' ambayo ni lazima izibwe ndipo watu wasadiki kushuhudia #‎MabadilikoYaKweli.

  0 0

   Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao (katikati) akimkabidhi jezi mmoja wa wawakilishi wa timu zinazoshiriki ligi daraja la kwanza ya StarTimes (SFDL) wakati wa hafla ya kukabidhi jezi hizo iliyofanyika jijini Dar es Salaam Jumatano. Kushoto akipiga makofi ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bw. Jamal Malinzi. (Picha na mpiga picha wetu).
   Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao (Kushoto) akimkabidhi jezi mmoja wa wawakilishi wa timu zinazoshiriki ligi daraja la kwanza ya StarTimes (SFDL) wakati wa hafla ya kukabidhi jezi hizo iliyofanyika jijini Dar es Salaam Jumatano. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ligi Kuu nchini, Bw. Boniface Wambura. (Picha na mpiga picha wetu)
  Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao (Kulia) akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi jezi kwa timu za Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes (SFDL) iliyofanyika jijini Dar es Salaam Jumatano. Katikati ni ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bw. Jamal Malinzi na wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa TFF, Bw. Selestine Mwesigwa.
   (Picha na mpiga picha wetu).

  Na Mwandishi Wetu.
  KAMPUNI ya Urushaji wa Matangazo Kidijitali ya StarTimes ya Tanzania imekabidhi jezi kwa timu zinazocheza Ligi Daraja la Kwanza nchini Tanzania, ikiwa ni moja kati ya udhamini wa ligi hiyo ijulikanayo kama Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes (SFDL).

  Akizungumza na waandishi wakati wa kukabidhi jezi hizo jijini Dar es Salaam Jumatano, Kaimu Afisa Mkuu Mtendaji wa StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao alisema kuwa angependa kuona jezi hizo zinakuwa kama chachu ya kufanya vizuri kwa timu zote zinazoshiriki ligi hiyo msimu huu.
  “Kwanza napenda Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa ushirikiano huu wanaouonyesha kwetu kama StarTimes, lakini leo hii tunatoa jezi kwa timu za ligi hii ya daraja la kwanza ya StarTimes ikiwa ni sehemu ya udhamini wetu mbali na udhamini wa fedha za uendeshaji.”

  “Jezi hizi sasa ni kama chachu ya timu zote za ligi daraja la kwanza kuongeza bidii na kufanya vizuri katika ligi hii msimu huu ili kuvutia wadhamini wengi zaidi. StarTimes kupitia udhamini huu tunaamini tumefungua njia kwa wengine nao kujitokeza na pia kuinua ari ya timu hizi,” alisema Bw. Liao.
  Bw. Liao alisema kuwa kutokana na jitihada hizo angependa kuona wachezaji wanaocheza katika ligi hiyo wanacheza katika Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ na timu nyingine kubwa kimataifa.

  Kwa upande wake mwakilishi wa Timu zinazoshiriki ligi hiyo, Bw Masao Bwire, aliipongeza kampuni ya StarTimes kwa kujitokeza kuipiga jeki ligi hiyo ambayo imekuwa ikiendeshwa bila udhamini wowote kwa kipindi kirefu.

  Pamoja na hayo pia alilipongeza Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kwa jitihada zake za utafutaji wa wadhamini kwa lengo la kuinyanyua ligi daraja la kwanza nchini ambayo imekuwa ikizalisha wachezaji wanaocheza ligi kuu.

  “Naipongeza kampuni ya StarTimes kwa kujitokeza kudhamini ligi daraja la kwanza. Hii ni hatua kubwa kwa ligi hii, kwa kuwa imekuwa ikienda bila udhamini kwa muda mrefu. Kukosekana kwa udhamini kulikuwa kukisababisha timu kutojiendesha vizuri hasa katika masuala ya vifaa, kulipa wachezaji na viongozi posho, kusafiri mbali kwa ajili ya mechi na usajili. Tunashukuru sana hayo sasa yatabakia historia na tunawaomba wadau wengine wajitokeze kwani bado hitaji ni kubwa. Lakini pia naipongeza TFF kwa jitihada zake kubwa za kutafuta wadhamini ili kusaidia maendeleo ya ligi hii nchini,” alisema Bw. Bwire.

  Naye Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Bw. Jamal Malinzi aliishukuru kampuni ya StarTimes kwa ushirikiano inaoutoa ili kuhakikisha ligi hiyo inasonga mbele na kuziasa timu zinazoshirki ligi hiyo kuongeza jitihada na kufanya vizuri baada ya kupata msukumo huo toka StarTimes.

  “Napenda kuishukuru kampuni ya StarTimes kwa ushirikiano inaotuonyesha ili kuipeleka mbele ligi hii lakini pia naziasa timu zote zinazoshiriki ligi hii ya StarTimes ya Daraja la Kwanza kuongeza jitihada na kufanya vizuri katika msimu huu wa ligi. Pia ningependa kuwataka na nyinyi mfanye juhudi kutafuta wadhamini wengine kwani mnaweza kufanya hivyo ili kufanya ligi iwe na ushindani zaidi.” alihitimisha Bw. Malinzi.

  0 0
  0 0

   Mhe. Magdalena Sakaya akijieleza na kumba kura
   Dkt. Tulia Ackson Mwansasu akijieleza na kuomba kura
  Dkt. Tulia Ackson Mwansasu akila kiapo katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma leo bada ya kushinda nafasi ya  Naibu Spika wa Bunge, kwa kura 250 sawa na 71.2% dhidi ya mpinzani wake Mhe. Magdalena Sakaya aliepata kura 101 sawa na 28.8%. 
  Picha na Sultani Kipingo wa Globu ya Jamii, Dodoma

  0 0


  0 0


  0 0

  To Vote for that whom you think Deserves to win SIMPLY TEXT nominees Code to 15670 or vote via email by Putting the CODE in the SUBJECT and send to vote@swahilifashionweek.com or Simply CLICK on our WEBSITE to vote ONLINE.


  0 0


   Mpambe wa Rais Kanali Mkeremi akiingia bungeni mjini Dodoma leo asubuhi akiwa na bahasha yenye jina la Waziri Mkuu mteule lililowasilishwa  na  Rais Dkt.John Pombe Joseph Magufuli ili kupigiwa kura na hatimaye kuridhiwa na wabunge,
    Mpambe wa Rais Kanali Mkeremi akimkabidhi Spika Job Ndugai bahasha yenye jina la Waziri Mkuu mteule lililowasilishwa  na  Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ili kupigiwa kura na hatimaye kuridhiwa na wabunge,
   Spika Job Ndugai akiinua bahasha kabla ya kusoma  jina la Waziri Mkuu mteule lililowasilishwa bungeni  na  Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ili kupigiwa kura na hatimaye kuridhiwa na wabunge,
   Wakati hayo yakiendelea ndani ya bunge Mbunge wa Rwangwa Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akiwasili viwanja vya bunge akiwa peke yake bila shaka akiwa hana habari kwani usiri wa kupatikana na hatimaye kuwasilishwa jina la Waziri Mkuu Mteule ulikuwa mkubwa sana.
   Bunge linaripuka na wabunge wanampongeza Waziri Mkuu Mteule Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa baada ya jina lake kutangazwa na hatimaye kupigiwa kura na kupita kwa kishindo kwa kura 258 ama asilimia 73.5 ya idadi ya kura zilizopigwa.
  Bunge linaripuka na wabunge wanampongeza Waziri Mkuu Mteule Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa baada ya jina lake kutangazwa
   Waziri Mkuu Mteule Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akimtanguliza  Mwenyezi Mungu kwa kumjaalia nafasi hiyo, akimshukuru Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa imani aliyoonesha juu yake, anawashukuru pia wabunge kwa kumpa kura nyingi, na wapiga kura wake kwa kumchagua tena na kumuwezesha kufika hapo. Picha na Sultani Kipingo.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


  0 0


  Sherehe za kumuapisha Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa (pichani), Waziri Mkuu Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zitafanyika katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Novemba, 2015 kuanzia saa   4.00 Asubuhi. 
  Sherehe hizo zinafanyika siku moja  baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitisha jina lake kwa kura nyingi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia uteuzi uliofanywa na Mhe. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Kwa mujibu wa ratiba ya sherehe hizo, Wageni waalikwa wote wanapaswa kuwasili katika Ikulu ya Chamwino kuanzia majira ya saa mbili asubuhi.


  Sherehe hizo zinatarajiwa kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo  Marais Wastaafu, Mawaziri Wakuu wastaafu na waheshimiwa wabunge.


  Imetolewa na Idara ya Habari MAELEZO

  19 Novemba, 2015

  0 0


  Na Bashir Yakub
  Serikali  mpya  imeanza  kwa  kasi  kubwa kufuta  umiliki  wa  viwanja  nyumba na  kubomoa  yale  maeneo  yote  wanayoona  hayastahili. Upo  umuhimu  wa  kujua  namna  ya  kuepuka  kuingia  katika  janga  hili.


  1.Kifungu cha 45 (2)(i-vi) cha Sheria ya Ardhi kinaeleza sababu za msingi zinazoweza kusababisha mhusika kubomolewa, kufutiwa umiliki ardhi kama ifuatavyo :
  ( a ) Kwanza iwapo eneo limetelekezwa kwa muda usiopungua miaka miwili. Muda usiopungua miaka miwili maana yake ni kuanzia miaka miwili na kwenda mbele. Kutelekeza eneo kwa mujibu wa maana hii hapa ni pamoja na kutoonekana ukishughulika na eneo lako kwa namna yoyote tangu upatiwe umiliki.
  ( b ) Jaribio lolote la kutaka kuuza au kugawa ardhi kwa mtu asiyekuwa Mtanzania. Ni kosa mtu asiyekuwa raia wa Tanzania kumiliki ardhi, hivyo jaribio lolote la kumpatia ardhi linatosha kuwa kosa la kufutiwa umiliki.


  ( c ) Epuka  kujenga  maeneo  ya  wazi, maeneo  yaliyotengwa  kwa  ajili ya  miundo  mbinu, na  huduma  nyingine  za  umma. Kufanya  hivyo  hutafsiriwa  kama  kuukosesha  umma  manufaa  yaliyokusudiwa  na  ni  kinyume  na tamko  namba 6.6.1 la  sera  ya  taifa  ya  ardhi  ya  mwaka 1995.


   ( d ) Jaribio lolote la kutoa ardhi kwa mamlaka nyingine kinyume na namna ulivyoagizwa na mamlaka wakati unapewa eneo husika.
  (  e  ) Kutumia eneo kinyume na masharti yaliyo kwenye hati ikiwa ni pamoja na matumizi yoyote yaliyo kinyume na sheria ya ardhi, sera, miongozo na kanuni zake.
  (  f  ) Pia, Rais kwa mamlaka aliyonayo, anaweza kufuta umiliki wa ardhi ya mtu yeyote kwa sababu zozote zinazohusu maslahi ya umma.

older | 1 | .... | 1030 | 1031 | (Page 1032) | 1033 | 1034 | .... | 3270 | newer