Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 101 | 102 | (Page 103) | 104 | 105 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kiondoni jijini Dar es Salaam, Jordan Rugimbana, (Aliyesimama), akitoa hotuba kwenye tamasha la kutangaza fao la elimu la Mfuko wa Pensheni wa PPF kwenye viwanja vya chuo cha Ustawi wa Jamii jijini Dar es Salaam Aprili 13. Wengine pichani kutoka kulia, ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, William Erio, Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge, na Meneja wa PPF kanda ya Kinondoni, Zahra Kayugwa.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, akihutubia kwenye tamasha la kutangaza fao la elimu la mfuko wa PPF, Kanda ya Kiondoni jijini Dar es Salaam Aprili 13.
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Jordan Rugimbana (Watatu kulia), akimkabidhi zawadi Mwangalizi wa wanafunzi shule ya sekondari Loyola ya jijini Dar es Salaam, Herieth, wakati wa tamasha la kutangaza fao la elimu la Mfuko wa Pensheni wa PPF, kwenye viwanja vya chuo cha ustawi wa Jamii jijini Aprili 13. Wanaoshuhudia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge (Kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio.
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Jordan Rugimbana (Wapili kulia), akimkabidhi zawadi mwanafunzi wa kidato cha tatu, shule ya sekondari Loyola, ambaye ni mmoja wa wanafunzi wanaosoma kupitia fao la elimu la mfuko huo, Jolen Nyonyi wakati wa tamasha la kutangaza fao la elimu la Mfuko wa Pensheni wa PPF, kwenye viwanja vya chuo cha ustawi wa Jamii jijini Aprili 13. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  NMB inaendelea kupanua mtandao wake wa matawi na kusogeza huduma za kibenki karibu na wateja wake.

  Sasa NMB imekuwa karibu na wateja wa eneo la buzuruga kwa kufungua tawi eneo la Buzuruga Mwanza katika jengo la Buzuruga Plaza lililopo karibu na kituo cha mabasi cha Buzuruga.

  NMB inaendelea kuwa kinara katika ubunifu Tanzania kwa kuanzisha huduma nyingi za kibenki. Hivi karibuni imeungana na Vodacom ili kuwarahisishia wateja kupata huduma za kibenki kwa urahisi. Sasa wateja wanaweza kuweka na kutoa fedha kwenye akaunti ya NMB kutokea M-Pesa. Huduma hii ni ya haraka, salama, unaitumai popote ulipo na wakati wowote.
  Kwa mawasiliano zaidi, wasiliana na:

  NMB Buzuruga;
  S.L.P 1450
  Mwanza
  Tanzania
  Simu: 028 2570483
           028 2570482

  0 0

      Meneja mahusiano wa Airtel-Tanzania akimsikiliza mmoja wa wakazi wa mji wa Chalinze-Mkoa wa Pwani namna anavyoweza kujiunga na kuitumia huduma mpya ya Airtel Yatosha,wakati wa tamasha la uzinduzi wa huduma hiyo yenye bei nafuu ,lililofanyika mkoa wa pwani kwa  siku  wa mbili (Jumamosi & Jumapili),  katika viwanja vya sokoni chalinze.
    Anaitwa Sir Juma Nature a.k.a Kibra akiongoza mashambulizi makali ya kundi lake la TMK-Wanaume Halisi kama umuonavyo jukwaani mbele ya umati mkubwa wa wakazi wa mji wa Chalinze-Mkoa wa Pwani mwishoni mwa wiki,wakati wa tamasha la uzinduzi wa huduma mpya ya  Airtel Yatosha,lililofanyika mkoa wa pwani kwa mda siku  wa mbili (Jumamosi & Jumapili),  katika viwanja vya sokoni chalinze.
   Mmoja wa wasanii mahiri wa Hip hop kutoka kundi la Tip Top Connections,ajulikanaye kwa jina la kisanii,Madee a.k.a Rais wa Manzese akionesha umahiri wake wa kukamua vilivyo jukwaani mwishoni mwa wiki,wakati wa tamasha la uzinduzi wa huduma mpya ya  Airtel Yatosha,lililofanyika mkoa wa pwani kwa mda siku  wa mbili (Jumamosi & Jumapili),  katika viwanja vya sokoni chalinze. 
    Msanii wa miondoko ya muziki wa kizazi kipya,hip hop,Fid Q pamoja na Meneje Mauzo wa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel Kanda ya pwani ,Bwa.Aluta Kweka wakimkabidhi fulana mmoja wa mashabiki wa Chalinze,kwa kuimba vyema mashairi ya msanii Fd Q.
     Sehemu ya wakazi wa mji wa Chalinze-Mkoa wa Pwani wakishuhudia uzinduzi wa huduma mpya ya  Airtel Yatosha,lililofanyika mkoa wa pwani kwa mda siku  wa mbili (Jumamosi & Jumapili),  katika viwanja vya sokoni chalinze.
  Mmoja wa wasanii mahiri wa Hip hop nchini,ajulikanaye kwa jina la kisanii,ney wa Mitego akitumbuiza jukwaani mwishoni mwa wiki,wakati wa tamasha la uzinduzi wa huduma mpya ya  Airtel Yatosha,lililofanyika mkoa wa pwani kwa mda siku  wa mbili (Jumamosi & Jumapili),  katika viwanja vya sokoni chalinze.
   Baadhi ya mawakala wakiendelea kuwasajili wateja wa Airtel kupitia huduma zote zitolewazo na kampuni hiyo,ikiwemo  huduma ya .Airtel Yatosha,ambapo Mteja anajiunga kwenye huduma hiyo kwa kupiga *149*99#.

  0 0

  NEEMA HERBALIST & NUTRTITIONAL FOODS CLINIC ni wauzaji wa dawa mbalimbali za asili. Tunayo dawa nzuri na ya asili ya KUONDOA KITAMBI. Dawa hii ni ya asili “ pure herbal “, haijachanganywa na kemikali yoyote, haina side effect kwa mtumiaji na inaondoa kitambi ndani ya siku kumi na nne tu. Bei yake ni Shilingi Elfu Arobaini Tu ( Tsh 40,000/=)

  Tunapatikana jijini Dar Es salaam, katika eneo la CHANGANYIKENI karibu na CHUO CHA TAKWIMU. Vile vile tunafanya ‘delivery’ kwa wateja wasio weza kufika ofisini kwetu, na kwa wateja wa mikoani tunawatumia kwa njia ya mabasi, wateja waliopo Zanzibar tunawatumia dawa kwa njia ya meli na kwa wateja waliopo nje ya nchi tunawatumia kwa magari, DHL, ama posta kulingana na nchi waliyopo.

  PIA tunayo dawa ya asili iitwayo JIKO ambayo hutibu tatizo la ukosefu na upungufu wa nguvu za kiume.

  Wasiliana Nasi kwa Simu : 0767010756 au 0766538384. 
  Website http://www.neemaherbalist.blogspot.com


  0 0

  Balozi wa Tanzania nchini China Philip Marmo (wa pili kushoto) akisalimiana na Mtanzania Egidius Kabitura katika banda la Tanzania kwenye maonyesho ya utalii ya COTMM 2013 yaliyomalizika jana jijini Beijing China. Wengine kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Nuru Millao na Mkurugenzi wa Idara ya Utalii Ibrahim Mussa.
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Nuru Millao akisalimiana na wakalimani katika katika banda la Tanzania.
  Wadau katika banda la Tanzania.
  Balozi Marmo akijadiliana jambo na wageni waliofika katika banda la Tanzania
  Kutoka kulia: Mbunge wa Ngorongoro Mhe. Kaika Telele; Naibu Katibu Mkuu Nuru Millao; Balozi Philip Marmon a Mkurugenzi wa Utalii Ibrahimu Mussa katika banda la Tanzania. Aliyesimama nyuma ni Meneja Huduma za Utalii wa TANAPA Bw. Johnsone Manase.
  Mgeni huyu alifurahishwa na vazi la kimasai kutoka kwa Egidius Kabitura na kuamua kupiga naye picha katika banda la Tanzania.

  0 0


  Moja ktk  tofauti kubwa iliyopo kati ya bima inayofuta sheria za ki-Islam na ile isiyofuata sheria ya ki-Islam ni kitendo cha wateja kugawiwa faida inayopatikana ktk biashara hiyo.


  Takaful Insurance of Africa Limited (TIA) ni shirika la bima la kwanza nchini Kenya linalofuata sheria za ki-Islam ambalo limetangaza kugawana faida na wateja wake. Ktk kongamano lililohudhuriwa na mashirika yasiyopungua 500 ambayo ni wateja, brokers na mawakala, TIA ilitangaza kugawana asilimia 60 ya faida na wateja wake 4000 ambao hawakudai fidia yoyote ktk kipindi cha mwaka mzima. 

  Alinukuliwa akisema mwenyekiti wa shirika hilo ndugu Abdurahman Sheikh ‘ninayo furaha na heshima kubwa kutangaza kwamba TIA imepata ziada (Surplus) yake ya kwanza ambayo ni sawa na Sh 15.6 million za Kenya na ambazo watagawana na wateja wake’, ktk tukio ambalo ni lakwanza kwa shirika la bima kufanya hivyo Kenya na Africa Mashariki kwa ujumla.


  Akizungumza ktk kongamano hilo Mkurugenzi Mkuu Ndugu Hassan Bashir alisema ‘shirika limekua sana ukilinganisha na lilivyoanzishwa miaka miwili iliyopita, na limeweza kufanya kwa kipindi hicho, kile ambacho mashirika mangine yamekifanya kwa muda usiopungua miaka kumi’. Kwa maelezo zaidi kuhusu bima inayofuta sheria za ki-Islam wasiliana na http://ijuebankyakiislam.blogspot.com

  0 0
 • 04/14/13--23:22: KUMBUKUMBU
 • Marehemu Mwl. Ernestina Kahabuka

  Miaka minne imepita toka ulipotuaga tarehe 15 April 2009 na kuzikwa nyumbani kijiji cha Buhangaruti, Mugana Catholic Parish, Bukoba.

  Unakumbukwa daima na mume wako Dr.F.C.Kahabuka, wanao Anna, Oliva, Mary, Prim, Pelagia pamoja na wakwe zako na wajukuu, ndugu, majirani na marafiki na wote tunazidi kukuombea upumzike mahali pema huko peponi,

  Amina.

  0 0  0 0


  0 0


   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa tatu kushoto) akitoa maelekezo alipotembelea mradi wa ujenzi jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa Dodoma. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa Dodoma Ndg. Rehema Madenge.


  Mafundi wa kampuni ya China Railway Jiachang Engeneering Ltd (CRJE Co. Ltd) inayojenga Jengo la ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wakiendelea na kazi kama walivyokutwa na Katibu Mkuu Kiongozi (hayupo pichani) mwishoni mwa wiki alipotembelea mradi huo.


  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amewataka watumishi wa serikali kutambua kuwa wanawajibu mkubwa wa kujenga taswira nzuri ya utumishi wa umma hapa nchini kupitia utendaji uliotukuka.

  Balozi Sefue alieleza hayo mwishoni mwa wiki alipokutana na watumishi wa sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma ambapo alisisitiza kuwa watendaji na viongozi wote wa umma kuanzia ngazi za chini za uongozi na utumishi wanatakiwa kuhakikisha wanatimiza wajibu wao ipasavyo na kuondoa taswira mbaya inayouandama utumishi wa umma.

  Katika hatua nyingine baada ya katibu Mkuu Balozi Sefue kuona tatizo la ukosefu wa ofisi kwa watumishi wa sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma na kutembelea mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma unaokwenda taratibu kutokana na upatikanaji wa fedha, balozi Sefue amesema serikali inawajibu wa kuhakikisha mradi huo unakamilika haraka iwezekanavyo.

  Vilevile ameahidi katika mwaka wa fedha ujao 2013/14 serikali inaweza kutoa mara mbili ya fedha zilizoombwa na sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya uendelezaji wa ujenzi wa mradi huo wa ofisi ambapo jumla ya shilingi bilioni tatu ziliombwa kwa ajili ya kuendeleza ujenzi katika bajeti ya mwaka 2013/14.

  Kwa upande wake katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Ndg. Rehema Madenge alibainisha kuwa pamoja na tatizo la ofisi ya Mkuu wa Mkoa kutokuwa na jrngo lake la ofisi, matatizo mengine yanayoikabili sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma ni pamoja na Ufinyu wa bajeti kwa ajili ya miradi ya maendeleo na fedha kidogo za kuendeshea ofisi wakati gharama za uendeshaji zinapanda.

  Aidha uchache wa watumishi hasa kwenye kada za afya ni tatizo linguine lenye kuhitaji utatuzi na kumuomba katibu mkuu kiongozi kutoa vibali kwa maombi yote ya kuajiri yatayomfikia mezani kwake na kuiomba serikali itenge bajeti ya kuajiori watumishi wa kada zenye upungufu ili sekretarieti za Mikoa ziweze kuajiri na kuziba nafasi wazi.

  Akiwakilisha watumishi wengine, Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Hospitali ya Mkoa wa Dodoma Dr. Lucy Mkandawile alisema kuwa matatizo mengine yanayogusa watumishi moja kwa moja ni pamoja na uchelewaji kupanda vyeo, malimbikizo ya Mishahara baada ya kupanda vyeo, malipo ya nauli za likizo na matibabu, fedha kwa ajili ya sare za kazi, ufadhili wa masomo kwa watumishi kwa ajili ya kujiendeleza na mishahara midogo.

  Akijibu hoja hizo katibu Mkuu alieleza kuwa serikali inazifahamu baadhi ya changamoto zilizoelezwa na inazichukua zote pamoja na zile mpya zinazoendelea kuibuliwa na kuahidi kuwa serikali itaongeza jitihada katika kuzishughulikia lengo likiwa kuzidi kuboresha mazingira ya utumishi wa umma na hali za maisha za watumishi.


  0 0
 • 04/15/13--00:40: Article 7


 • 0 0
  0 0

  Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na UNDP kupitia mradi wa Legislative Support Project, imeandaa semina ya kuwapa Uelewa waheshimwa Wabunge kuhusu Changamoto zinazowakabiri Watu wenye Ulemavu wa Ngozi (Albinism) ili kuwa na uwelewa mpana kuhusu changamoto zinazowakabili albino. Semina hii ni mwendelezo wa semina za kutoa elimu kwa waheshimiwa Wabunge na Watumishi wa Ofisi ya Bunge kupitia Mradi wa Legislative Support Project, ambao upo chini ya Shirika la Maendeleo Duniani (UNDP) ili kuwajengea wabunge na watumishi katika kutekeleza majukumu yao ya Kibunge, hususani, uwakilishi wa wananchi pamoja na kuisimamia na kuishauri serikali.
   Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii Mhe. Margareth Sitta (MB) akitoa neno la Utangulizi wakati wa Ufunguzi wa Semina hiyo jumamosi
   Mwenyekiti wa Chama cha Maalbino Nchini Ndg. Ernest Kimaya akitoa utambulisho kwa baadhi ya wajumbe kutoka Chama cha Maalbino waliofika katika Semina hiyo.
   Mwakilishi wa Mradi wa Legislative Support Project uliochini ya UNDP Bi. Anna Hovhannesyan akitoa maelezo mafupi kuhusu Mradi wa Legislative Support Project kwa Waheshimiwa Wabunge
   Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akifafanua baadhi ya changamoto zinazowakabiri maalbino kabla ya kumkaribisha  Waziri Mkuu kufungua rasmi Semina hiyo
   Mbunge wa Lindi Mjini Mhe. Salum Barwani ambaye nae ni mlemavu wa ngozi akitambulishwa katika semina hiyo.
  Washiriki wengine wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika semina hiyo.
   Mwakilishi wa Mradi wa Legislative Support Project uliochini ya UNDP Bi. Anna Hovhannesyan akiteta jambo na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda wakati wa Semina hiyo jumamosi.
   Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Kayanza Pinda akifungua rasmi semina kuhusu Changamoto zinazowakabiri Maalbino kwa waheshimiwa wabunge katika Ukumbi wa Msekwa, Dodoma
  Waheshimiwa Wabunge wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika semina hiyo.

  0 0

  Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza ushindi wa Tuzo ya Bia Bora Barani Afrika kwa bia ya Safari Lager ilioupata,ambapo pia Hatua hii itafuatiwa na safari ya kupeleka kikombe hiki cha ushindi Bungeni siku ya Alhamisi wiki hii. Kama tunavyofahamu, wabunge ni wawakilishi wa wananchi wote hivyo itakuwa fursa nzuri kufikisha kombe hili ambapo Bunge litatoa baraka zake nasi tutaanza kulizungusha kombe katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu. Ujumbe mkuu katika ziara hii utakuwa ni kuutangaza ushindi huu mkubwa wa Bia hii ya Kitanzania, inayotengenezwa na Watanzania.Kulia ni Mratibu wa Ziara hiyo,Innocent Melleck.
  Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akionyesha vikombe hivyo.
  Baadhi ya waandishi wa habari waliokuwepo kwenye mkutano huo.

  0 0

  Waendesha pikipiki zinazopakia abiria maarufu kama Boda Boda wako juu ya sheria na hakuna mtu anayeweza kutia fyoko, Globu ya Jamii inaweza kuthibitisha. Waendesha Boda Boda jijini Dar es salaam na hata mikoani wameanzisha himaya yao inayoonesha hata vyombo vya dola havina ubavu kuidhibiti, hata kama ni kuchukua sheria mikononi watakavyo na kuvunja sheria za usalama barabarani. 

  Wananchi wengi tuliowahoji wametahadharisha kwamba endapo vyombo vya dola vitaruhusu hali hii iendelee, usalama na amani nchini vinaweza kuwa rehani kimoja. Wamehoji kwa nini hawa waendesha BodaBoda wamekuwa wajeuri na wababe dhidi ya wananchi tena mbele ya dola? "Bwana mwandishi ka ma unabisha hebu mgonge kwa gari Bodaboda mmoja uone jioni wenzie toka kila kona watakavyokutanika na kukushambulia na kukudhuru", anasema Mwananchi mmoja, akiendelea kushangaa pale Bodaboda wanapoachiwa kuvuka wakati taa za barabarani kuwa nyekundu. 

  Globu ya Jamii jana Jumapili ilishuhudia Bodaboda wakitawala barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam wakati wakisindikiza gari linalosadikiwa kuwa na mwili wa mwenzao aliyefariki dunia, akipelekwa maeneo ya Ukonga kwa maziko. Kwenye makutano ya njia inayoelekea Uwanja wa Ndege wa kimataifa ya Julius Nyerere, ambapo pana taa za barabarani, umati huo wa Bodaboda ulifanya ubabe kupita wakati taa zilikuwa zinawaka nyekundu na hata askari trafiki aliyekuwepo pale alidharauliwa na badala yake mmoja wao ndio akawa anaongoza magari. 

  Pia Daladala moja lililojaa abiria  lililazimishwa kibabe na kwa matusi kupaki pembeni ili msafara wa Bodaboda upite, na dereva alipotaka kungoja taa ziwake za kijani ili aendelee akazingirwa na Bodaboda kibao hadi akasalimu amri. Hali hii inazidisha maswali kwani hawa watu ni kina nani wafanye watakacho bila kujali sheria halali za nchi? 

  Wananchi wametoa wito kwa wahusika kutathmini hali hii ambayo wameitaja kama bomu linalofukuta, na kisha kuchukua hatua haraka sana kabla hali haijawa mbaya zaidi ya ilivyo sasa. Vile vile wameshauri kuwepo namna ya kuwaelimisha Bodaboda namna bora ya kuendesha shughuli zao kwani kwa mfano mdogo tu wengi hawana utaalanmu wa kuendesha pikipiki, hali inayopelelea kukuta majeruhi wengi katika hospitali zote hivis sasa ni Bodaboda. 

  "Hawa wanahitaji elimu ya namna ya kuendesha pikipiki ama sivyo tutapoteza vijana wetu kila siku" kasema mwananchi mwingine, akitolea mfano wodi ya Sewa Haji ya Taasisi ya Mifupa (MOI) iliyoko Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo kwa uchache tu waendesha Bodaboda 15 hulazwa pale kwa majeraha kwa siku.
  Bodaboda wakiteka barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam
  Mpita njia amepigwa butwaa kuona Bodaboda wanalazimisha Daladala lipaki pembeni ili wao wapite
  Wengi ni vijana wadogo wa umri kati ya miaka 15 na 30.
  Daladala likilazimishwa kupaki pembeni
  Abiria wanashangaa kuona Bodaboda wakifanya watakalo
  Gari walilokuwa wanalisindikiza likipita
  Daladala limezingirwa na Bodaboda
  Mmoja wa waendesha Bodaboda akielekeza pikipiki zipite huku daladala likiwa limesalimu amri na kupaki pembeni

  0 0


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, katika utekelezaji wa kazi za Wizara hiyo katika Ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi,( kulia) Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi,pia Katibu Mkuu Kiongozi Dk.Abdulhamid Yahaya Mzee.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, (katikati)akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, katika utekelezaji wa kazi za Wizara hiyo katika Ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi, (wa tatu kulia) Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamadi. [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

  0 0
 • 04/15/13--03:38: IN LOVING MEMORY
 • ‘’ It is by grace of God the almighty that we are marking the 5th anniversary of your passing since 20th April 2008, when you left such a deep empty void in our hearts, We are thinking of you all the time JOSEPH. Although life has to move on, your memories continue to live on and your presence is still very much living in our hearts. We remember your charm, smile, kindness, politeness and so many more things you shared with us. As we celebrate your life on 20th April 2013.

  We thank God for the gift of your presence in our lives which was truly the greatest gift of all. Although the thoughts of you gone still hurt us but we believe you are in a much better place watching down to us. Your deeply missed and fondly remembered by your wife Flora, kids Maurice, Malcolm & Johnson, your Dad, sisters, relatives and friends. We always pray that God grants your soul in eternal peace till the end of time when we meet again by the grace of God. Eternal rest grant onto him, o Lord & let perpetual light shine upon him, may he rest in peace , Ameen’’

  Thanks giving mass will be held at his father’s place Ilemela Mwanza on 20th April 2013 at 10:00 a.m.
  Regards,

  Flora

  0 0

  Meneja Biashara wa Nokia Nchini Tanzania Samson Majwala, Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde na menjeja masoko wa Airtel Edwin Byampanju kwa pamoja wakionyesha simu za rangi tofauti za Nokia Lumia 620 wakati wa wakati wa uzinduzi wa Nokia Lumia 620 kwa ushirikiano kati ya Airtel na Nokia utakaowawezesha wateja wa Airtel na watanzania kupata simu ya Nokia Lumia 620 yenye technologia ya kisasa na offa kabambe ya Muda wa Maongezi wa dakika 275, sms bila kikomo na internet ya 3GB kwa muda wa mienzi mitatu.
  Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde akiongea wakati wa uzinduzi wa simu Nokia Lumia 620 , ushirikiano kati ya Airtel na Nokia utakaowawezesha wateja wa Airtel na watanzania kupata simu ya Nokia Lumia 620 yenye technologia ya kisasa na offa kabambe ya Muda wa Maongezi wa dakika 275, sms bila kikomo na internet ya 3GB kwa muda wa mienzi mitatu.
  Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde akiongea wakati wa uzinduzi wa simu Nokia Lumia 620 , ushirikiano kati ya Airtel na Nokia utakaowawezesha wateja wa Airtel na watanzania kupata simu ya Nokia Lumia 620 yenye technologia ya kisasa na offa kabambe ya Muda wa Maongezi wa dakika 275, sms bila kikomo na internet ya 3GB kwa muda wa mienzi mitatu.
  Meneja Biashara wa Nokia Nchini Tanzania Samson Majwala, Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde na menjeja masoko wa Airtel Edwin Byampanju kwa pamoja wakionyesha kipeperushi cha Nokia Lumia 620 wakati wa wakati wa uzinduzi wa Nokia Lumia 620 kwa ushirikiano kati ya Airtel na Nokia utakaowawezesha wateja wa Airtel na watanzania kupata simu ya Nokia Lumia 620 yenye technologia ya kisasa na offa kabambe ya Muda wa Maongezi wa dakika 275, sms bila kikomo na internet ya 3GB kwa muda wa mienzi mitatu.
  Meneja Biashara wa Nokia Nchini Tanzania Samson Majwala( kushoto) akimkabidhi simu ya Nokia Lumia 620 Batuli Chombo mwandishi wa habari wa Sikuba kwenye bahati nasibu wakati wa uzinduzi wa Simu hiyo kwa ushirikiano kati ya Airtel na Nokia utakaowawezesha wateja wa Airtel na watanzania kupata simu ya Nokia Lumia 620 yenye technologia ya kisasa na offa kabambe ya Muda wa Maongezi wa dakika 275, sms bila kikomo na internet ya 3GB kwa muda wa mienzi mitatu. Wakishuhudia ni Afisa Uhusiano Jane Matinde akifatana na menjeja masoko wa Airtel Edwin Byampanju.

  0 0
 • 04/16/13--00:51: KIJIWE CHA UGHAIBUNI

older | 1 | .... | 101 | 102 | (Page 103) | 104 | 105 | .... | 3284 | newer