More Channels
Showcase
Articles on this Page
(showing articles 20381 to 20400 of 65435)
- 11/04/15--02:53: _ONESHO LA SWAHILI F...
- 11/04/15--03:13: _VYUMBA VYA KUPIMIA ...
- 11/04/15--03:22: _RAIS KIKWETE AMWAPI...
- 11/04/15--03:48: _MREMA ACHUKIZWA NA ...
- 11/04/15--04:52: _NAMNA YA KISHERIA Y...
- 11/04/15--05:15: _NGOMA AFRICA BAND J...
- 11/04/15--05:23: _MALALAMIKO YA MAHAK...
- 11/04/15--06:14: _Serikali yatoa Ufaf...
- 11/04/15--11:58: _SHIMMUTA YAMPONGEZA...
- 11/04/15--12:15: _TAARIFA KWA WATEJA ...
- 11/04/15--12:27: _Tanzania yapokea Eu...
- 11/04/15--12:30: _NEWS ALERT: ALHAMI...
- 11/04/15--12:30: _RAIS KIKWETE AKUTAN...
- 11/04/15--12:30: _RAIS KIKWETE AKUTAN...
- 11/04/15--12:30: _Viongozi wawasili n...
- 11/04/15--12:31: _SIMU TV: HABARI KUT...
- 11/04/15--19:00: _Ngoma azipendazo an...
- 11/05/15--07:00: _MULTICHOICE TANZANI...
- 11/05/15--14:49: _SIMU TV: HABARI KUT...
- 11/05/15--16:17: _Kipindi cha JUKWAA ...
(showing articles 20381 to 20400 of 65435)
Channel Description:
Most read Swahili blog on earth
Mwanamitindo wa hapa nchini, Mustafa Assanali kulia na Katibu mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania, Godfrey Mngereza wakifungua pazia kuzindua Onesho la Swahili Fashion Week leo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam aambalo litakuwa na mwendelezo wa kuonesha ubunifu wa mitindo kwa siku tatu mfululizo litakalokuwa likifanyika katika hoteli ya Sea Clief jijini Dar es Salaam.
Mwanamitindo wa hapa nchini, Mustafa Assanali akizunguza na waandishi wa habari leo katika mkutano na waandishi wa habar jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na uzinduzi wa onesho la Swahili Fashion week iliyozinduliwa leo ikiwa tunakaribia mwishoni mwa mwaka Mwanamitindo huyo amesema kuwa katika uzinduzi huo kutakuwa na siku tatu mfululizo za wanamitindo mbalimbali wataonyesha mitindo, Urembo na mitindo ya maisha katika onyesho litalokuwa likifanyika katika hoteli ya Sea Clif jijini Dar es Salaam.
Pia amesema kuwa onyesho hilo la mavazi lina nia ya kusisitiza jamii kuwa mitindo ni pato linalozalisha tsinia ya ubunifu pia ni kukuza dhana ya bidhaa ya Afrika ikiwa kwa mwaka huu onesho la Swahili Fashion Week ni la nane tangu lianzishwe hapa nchini.
Kushoto ni Afisa Udhamini na matukio wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, Ibrahim Kaude akizungumza na waandishi wa habari leo katika mkutano wa uzinduzi wa Onesho la Swahili Fshion Week uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Maneja wa masoko wa kapuni ya magari ya Jaguar hapa nchini, Jennifer Gower.

Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
0 |
|
0 |
|
Wawezeshaji wa Sheria katika soko la Mchikichini katika Manispaa ya Ilala, wakiwa na mabango ya mradi wa Mpe Riziki si Matusi baada ya kuzungumza na waaandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi wanaotembelea masoko yaliyopo katika Manispaa hiyo kuona maendeleo ya vita ya kupinga udhalilishaji wa kijinsia katika masoko hayo baada ya Shirika la Equality for Growth linaloendesha mradi huo kutoa mafunzo kwa Wawezeshaji wa Sheria wanaoshirikiana na wafanyabiashara katika vita hivyo.
Mwezeshaji wa Sheria, Eva Kakobe akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya ukatili wa jinsia wanavyokabiliana nayo katika soko hilo.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
Na Dotto Mwaibale
VYUMBA vilivyokuwa vikitumiwa kwa ajili ya kupimia nguo kabla ya kuzinunua katika soko la Mchikichini Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam vinadaiwa vilikuwa vikitumia kudhalilidha wateja hasa wanawake.
Hayo yamebainishwa na Mjumbe wa Bodi ya Sekta ya Kanga na Vitenge katika soko hilo Zainabu Namijojo Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akizungumza na waandishi wa habari ambao wanafanya ziara ya kutembea masoko ya Manispaa ya Ilala kuona jinsi mradi wa Mpe Riziki si Matusi ulivyowakomboa wanawake katika vita ya kupinga udhalilishaji masokoni unaoendeshwa na Shirika la Equality for Growth (EfG).
"Katika soko letu tulikuwa na changamoto kubwa ya udhalilishaji hasa maeneo ya wauza nguo kuu kuu (Mitumba), kwani walikuwa wakitumia vyumba vidogo vya kujaribishia nguo kuwadhalilisha wanawake kwa kuwakamata maungoni na kuwawekea kioo chini ili waweze kuona utupu wao" alisema Namijojo.
Alisema hivi sasa vitendo hivyo vimekoma baada ya shirika hilo kufanya matamasha na semina mbalimbali na kutoa mafunzo kwa baadhi yao ambao sasa ni Wawezeshaji wa Sheria katika soko hilo ambao wamekuwa karibu na wafanyabiashara kufuatilia vitendo vya udhalilishaji.
Mwezeshaji wa Sheria Domitila Ngwada alisema vitendo vya ubakaji na matusi ya nguono yalishamiri sana lakini hivi sasa hali ni nzuri kwani vitendo hivyo vimepungua kwa asilimia 70 ukilisha na hapo awali kabla ya kufikiwa na EfG.
"Tangu kuwepo na wawezeshaji wa Sheria katika soko letu vijana wengi waliokuwa na vitendo vya kudhalilisha wanawake wameingiwa na hofu kubwa hasa kupigwa faini zilizowekwa kuanzia kiwango cha sh.50,000" alisema Ngwada.
Mfanyabiashara katika soko hilo, Ikram Zuberi alisema jitihada za makusudi zinapaswa kufanyika ili kumaliza vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia katika sokjo hilo ingawa kwa kiasi kikubwa vimepungua kwa msaa wa EfG.
Mwezeshaji wa Sheria katika soko hilo Charles Beatus alisema wale wote wanaopatika na makosa ya udhalilishaji wamekuwa wakiadhibiwa kutokana na mwongozo uliopo na kesi zote zinaanza kusikilizwa sokoni hapo na ikishindikana upelekwa ngazi nyingine ikiwemo polisi.
Katibu Tawala Mpya wa Mkoa wa Lindi Bwana Ramadhani Kaswa akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam jana.
Katibu Tawala Mpya wa Mkoa wa Lindi Bwana Ramadhani Kaswaakipongezwa na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam jana.
(Picha na Freddy Maro)
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Agustino Lyatonga Mrema amesema kuwa kushindwa kwake ubunge kulitokana na michezo mchafu uliochezwa na mshindi wa ubunge wa jimbo hilo, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha NCCR-MAGEUZI, James Mbatia
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mrema amesema kuwa mshindi wa jimbo hilo amekuwa akionywa na msimamizi wa uchaguzi kutokana na matumizi ya vipeperushi ambavyo yeye alijipigia kura ya ubunge katika jimbo la Vunjo.
Mrema amesema matokeo ya yaliyompa ushindi Mbatia hakusaini kutokana na kufanya hujuma nyingi ikiwa ni pamoja na kumsema mgombea mwenzake.
Aidha amesema kuwa katika kipeperushi chake Mbatia sehemu ya bendera ya TLP yenye alama ya jogoo ilionekana kifaranga baada ya kuwa na jogoo mkubwa anayewika.
Mrema katika kukutana na waandishi pia alimpongeza Rais Mteule wa CCM, Dk.John Pombe Magufuli kwa kura za kishindo na kutaka kuwa yuko naye.
Amesema kumpigia kampeni Mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli kulitokana na kazi nzuri ya kupeleka barabara katika jimbo lake akiwa Waziri wa Ujenzi.
Mrema katika mkutano wake leo aliambatana na viongozi wa juu wa chama hicho kueleza hujuma alizofanyiwa katika uchaguzi katika jimbo la Vunjo akimhutumu, James Mbatia ambaye ameibuka kidedea katika uchaguzi huo.
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP),Agustino Lyatonga Mrema akizungumza leo na waandishi habari juu ya kufanyiwa rafu katika jimbo la vunjo na kusababisha kushindwa kulitwa kwa mara nyingine kushoto ni aliyekuwa Mgombea Urais wa TLP ,Maxmillian Lyimo , na Kulia Katibu Mkuu wa TLP,Nancy Mricaria.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Agustino Lyatonga Mrema leo jijini Dar es Salaaam.
Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii
NA BASHIR YAKUB -
Unapomdai mtu kupitia mahakanma na hukumu ikatolewa kuwa ni kweli unamdai na anastahili kukulipa basi mtu huyo hustahili kulipa. Lakini mara kadhaa hutokea mtu kusema sina hela ya kulipa au vinginevyo ilimradi tu asilipe deni.
Lakini pia madai hapa si lazima iwe hela tu inayotokana na kukopeshana. Yapo pia madai ambayo hutokana na mtu kushinda kesi. Kwa mfano mwanamke alifungua kesi dhidi ya mme wake akitaka matunzo yake na ya mtoto/watoto. Au shauri limekwisha na mtu aliyeshindwa ametakiwa na mahakama kulipa gharama. Au malipo ya fidia na mengineyo yote ambayo huamuliwa na mahakama kuwa yalipwe. Haya yote unaweza kuyafanya yalipwe kwa kukamata mshahara wa mhusika kwa njia za kisheria .
Hatua hii imeelezwa katika amri ya 21 ya kanuni ya 47 ya sura ya 33 ya sheria ya mwenendo wa mashauri ya madai.
1.HATUA YA KUKAMATA MSHAHARA WA MTUMISHI.
Mahakama inapotoa hukumu ikimtaka mtu fulani kutekeleza jambo fulani au kulipa kiasi fulani kwa mtu fulani amri hiyo hutakiwa kutekelezwa kwa hiari na si vinginevyo.
Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa Band aka FFU-ughaibuni yenye makao nchini Ujerumani ,itatumbuiza mjini Bremen,Ujerumani.
siku ya jumamosi 7 November 2015,katika ukumbi wa Weserterrasse, uliopo
mtaa wa Osterdeich 70b, D- 28205 Bremen kuanzia saa usiku, onyesho hilo limeandaliwa na Pan-African Org tawi la Bremen ambalo linasherekea miaka 10 ya kuanziswa kwake.
Bendi ya Ngoma Africa band kwa sasa wanatamba na CD yao mpya La Mgambo na pia song lao jipya waliloliachia juzi tu
"Mapenzi ya Pesa" nyimbo zote hizo zinapasua anga ya kimataifa
unaweza pia kusikiliza at www.ngoma-africa.com
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (Pichani) amesema wananchi ambao hawajaweza kupata haki zao katika mahakama za mwanzo wanaweza kutumia kamati ya maadili.
Makonda ameyasema leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,Makonda amesema kuwa watu wengine wanakosa haki katika mahakama na hawajui wanaweza kupata haki sehemu gani kutokana na mwenendo wa kesi ilivyoendeshwa.
Makonda amesema kamati hiyo inawajibu wa kuangalia mwenendo wa maadili ya hakimu na ikibanika kamati inaweza kuchukua hatua.
Amesema kuna baadhi ya wananchi wanapewa hukumu za kesi lakini mwenendo wa kesi haujui na mwisho wa siku anakosa haki kutokana na baadhi ya watu kutumia mahakama vibaya.
Makonda amesema sharia ya Usimamizi wa Mahakama Na.4 ya mwaka 2011 sehemu 51(1) kutakuwa na kamati ya mahakama ya wilaya ambayo mwenyekiti wake ni Mkuu wa Wilaya.
Aidha amesema wengine wanaounda kamati hiyo ni Hakimu Mkazi wa Wilaya au msimamizi wa Wilaya ,Katibu wa Tawala wa Wilaya (DAS) ambaye anakuwa Katibu wa Kamati hiyo,Kiongozi wa dini mmoja ambaye atateuliwa na Mkuu wa Wilaya ,mtu mashuhuri wa wilaya ambaye ni mwadilifu.
Hata hivyo amesema katika kamati hiyo maafisa wawili watateuliwa na Jaji anayesimamia .
Kamati hiyo itawajibika kupokea na kuchunguza malalamiko yaliyowasilishwa na wananchi kuhusu mahakama na kuwasilisha ripoti kwa tume.
Na Georgina Misama-MAELEZO
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw. Assah Mwambene amekanusha taarifa za uzushi zinazosambazwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii kuhusu kifo cha Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa.
Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Bw. Mwambene amesema kuwa Mhe. Rais Mkapa ni mzima na mwenye afya nzuri anaendelea na shughuli zake kila siku kama kawaida.
“Mhe. Rais Benjamin William Mkapa ni mzima hajafariki, wala haumwi na si jambo jema kumzushia tukio hilo kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria na nawasihi msiendelee kusambaza ujumbe huo” alisisitiza Mwambene.
Aidha, katika mkutano huo Mwambene aliwashukuru wahariri, waandishi wa vyombo vyote vya habari na mitandao ya kijamii kwa ujumla kwa kuonyesha moyo wa uzalendo katika kipindi chote ambacho Taifa limekuwa katika mchakato wa uchaguzi na mpaka sasa ambapo serikali inaendelea na maandalizi ya sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Awamu ya Tano, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Mwambene amesema mpaka sasa maandalizi ya sherehe hizo yanaendelea vizuri, zaidi ya Marais 15 kutoka nchi mbalimbali wamealikwa baadhi wameshawasili nchini na wengine wanaendelea kuwasili.
Sherehe za kuapishwa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya Tano zitafanyika kesho tarehe Novemba, 5 mwaka huu katika uwanja wa Uhuru.
Katika kufikia ahadi yetu iliyopo kwenye malengona dira ya benki ya kuwa taasisi ya fedha inayopendelewa zaidi nchini kupitia mtandao mpana wa matawi unaotoa huduma kwa gharama nafuu zaidi zenye kumlenga mteja na jamii ya watanzania,
Tunapenda kuwataarifu wateja wetu na umma kwa ujumla kuwa matawi yetu yote yatafungwa siku ya Alhamisi Novemba 5, 2015 ili kupisha sherehe za kitaifa za kuapishwa kwa Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Raisi wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Huduma zitarejea tena katika matawi yetu yote siku ya Ijumaa Novemba 6, 2015 kuanzia saa 2:30 asubuhi.
Ili kuhakikisha kuwa tunaendelea kukupatia huduma bora siku hiyo, njia mbadala za kibenki kama ATM, NMB mobile, NMB Wakala na Internet Banking zitaendelea kufanya kazi kama kawaida kwa masaa 24.
Hata hivyo, kituo chetu cha huduma kwa wateja kitaendelea kuwa wazi mpaka saa 2:00 usiku. Hivyo unaweza kuwasiliana na kituo chetu cha huduma kwa wateja kwa kupiga simu ya bure 0800 11 22 33 kwa msaada zaidi.
Imetolewa na Menejimenti ya NMB
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yasaini mkataba wa jumla ya Euro milioni 158.5 na Serikali ya Ujerumani wenye lengo la kusaidia Bajeti ya Serikali pamoja na msaada wa kiufundi.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelie aliposaini mkataba huo na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bw. Egon Kochanke leo jijini Dar es salaam
Dkt. Likwelile alisema kuwa lengo kuu la fedha hizo zitaelekezwa katika sekta ya Afya, Mazingira, Nishati, Maji na kuimarisha Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Kwa upande wake Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bw. Egon Kochanke alisema kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania kwa kuwa nchi hizo zimekuwa na uhusiano mzuri wa muda mrefu ambao umekuwa na manufaa na tija kwa wananchi baina ya nchi hizo mbili.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile (kulia) akifurahia jambo na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bw. Egon Kochanke (kushoto) wakati wa maandalizi ya kusaini mkataba utakaoipatia Tanzania jumla ya Euro milioni 158.5 kusaidia Bajeti ya Serikali pamoja na msaada wa kiufundi.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile (kulia) akibadilishana mkataba na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bw. Egon Kochanke mara baada ya kusainiwa leo jijini Dar es salaam.
Ujumbe ulioshuhudia utiaji saini utakaoipatia Tanzania jumla ya Euro milioni 158.5 kusaidia Bajeti ya Serikali pamoja na msaada wa kiufundi. Wa pili kutoka mwisho ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile, kulia kwake ni Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bw. Egon Kochanke, Mshauri wa Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bi. Claudia Imwolde-Kraemer, Afisa Msimamizi wa Fedha Wizara ya Fedha Bw. Abdallah Lyangu, Mchumi kutoka Ubalozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bw. Jan-Dieter Gosink na kushoto kwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha ni Mchumi Wizara ya Fedha Bw. Melckzedek Mbise kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa hafla hiyo iliyofanyika Wizara ya Fedha.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akifafanua jambo kwa ujumbe wa Ujerumani mara baada ya kusaini mkataba utakaoipatia Tanzania jumla ya Euro milioni 158.5 kusaidia Bajeti ya Serikali pamoja na msaada wa kiufundi. Kulia kwake ni Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bw. Egon Kochanke, Mshauri wa Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bi. Claudia Imwolde-Kraemer pamoja na Mchumi ubalozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bw.Jan-Dieter Gosink.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameamua na ameitangaza kesho, Alhamisi, Novemba 5, mwaka huu, 2015, kuwa Sikukuu na siku ya mapumziko.
Rais Kikwete amefanya uamuzi huo, ili kuwawezesha Watanzania kushiriki katika sherehe za kuhitimisha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne na kuingizwa madarakani Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muung ano wa Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam leo Jumatano, Novemba 4, 2015 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Yohana Sefue, Rais Kikwete ametoa uamuzi huo kwa mujibu wa mamlaka aliyo nayo chini ya Kifungu cha 3 cha Sheria ya Sikukuu za Kitaifa.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
4 Novemba, 2015.
Rais Jakaya Kikwete ateta na makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Shariff Seif Hamad kuhusu hali ya kisiasa Visiwani leo asubuhi Ikulu jijini dar es Salaam
Wakiwa katika picha ya pamoja.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo Jumatano, Novemba 4, 2015, amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama cha Civic United Front (CUF), Mheshimiwa Seif Shariff Hamad ambaye pia alikuwa Mgombea Urais wa Zanzibar wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu uliofanyika Oktoba 25.
Viongozi hao wawili walikutana kwa kiasi cha saa moja Ikulu, Dar es salaam, kuzungumzia hali ya kisiasa Zanzibar kufuatia ombi la Mheshimiwa Hamad kutaka kukutana na kuzungumza na Rais Kikwete.
Viongozi hao wamekubaliana kuwa mashauriano yaendelee kufanyika baina ya pande zote zinazohusika na hali ya kisiasa Zanzibar.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
4 Novemba, 2015
0 |
|
0 |
|
Afisa Mambo ya Nje Bi. Liliani Kimaro akisalimiana na Rais Mugabe.
Rais Mugabe akikagua Gwaride la Heshima.
Rais Mugabe akiangalia kikundi cha wapiga Tarumbeta huku Waziri Membe akitoa ufafanuzi wa nyimbi iliyokuwa inachezwa.
===============================
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (kushoto) akimlaki Naibu Waziri Mkuu wa Namibia Mhe. Netumbo Nandi - Ndaitwah mara baada ya kuwasili nchini kwa ajili ya kushuhudia Uapisho wa Rais Mteule Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Mhe. Netumbo Nandi - Ndaitwah (wa pili kutoka kulia) akifurahia kikundi cha ngoma kilichopo mbele yao.
================================
Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini pia anayeiwakilisha Tanzania nchini Botswana Mhe. Radhia Msuya (kushoto) akisalimiana na Makamu wa Rais wa Botswana Mhe. Olale Eric Mothibi alipo wasili nchini kwaajili ya kushiriki Sherehe za Uapisho wa Rais Mteule Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Picha na Reginald Philip
0 |
|
0 |
|
Mwanamuiki nyota nchini Tanzania, Nassib Abdul ama Diamond Platnumz akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani). (Picha na Andrew Chale, Modewjiblog).
Na Adndrew Chale, Modewji.
KAMPUNI ya MultiChoice Tanzania mapema jana imezindua ofa kabambe za msimu wa siku kuu huku ikimtambulisha rasmi Mwanamuziki Diamond Platnumz kuwa balozi maalum wa bidhaa za kampuni hiyo ikiwemo kifurushi cha DSTV BOMBA chenye chaneli zaidi ya 65 ikiwemo huduma ya vituo kadhaa vya televisheni za hapa nchini.
Akimtambulusha rasmi Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Furaha Samalu, amemtambulisha Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuwa balozi wa king’amuzi hicho na kutaja gharama zake kuwa ni shilingi 23,500/= kwa malipo ya mwezi na king’amuzi chenyewe kinapatikana kwa shilingi 79,000/= na kuwataka wananchi kuchangamkia huduma hiyo muhimu katika msimu huu wa ofa za sikukuu.
Meneja masoko huyo ameongeza kuwa, kifurushi hicho kimesambaa nchini mbalimbali barani Afrika hivyo wasanii wa filamu, muziki na wengineo ambao watang’aa kwenye vipindi hivyo watakuwa wakionekana pande mbalimbali barani Afrika na hivyo kuwapatia umaarufu na kuwaongezea soko la kazi zao.
Mwanamuziki Diamond Platinumz akisoma kipeperushi chenye maelezo juu ya ofa mbalimbali za DStv wakati wa utambulisho wa ofa za sikukuu pamoja na kutangazwa kwa balozi huyo wa bidhaa za DSTV. Katikati Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu na kushoto ni Meneja Mwendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo.
Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu akifafanua jambo katika mkutano huo na kushoto ni Meneja Mwendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo na upande wa kulia ni msanii Diamond Platnumz balozi wa bidhaa za DSTV.
Meneja mauzo wa DSTV, Bw. Salum Salum akifafanua jambo juu ya ofa hiyo mpya na mahaala wanapopatikana nchini kwa mawakala wote ambapo amewaomba watanzania kuchangamkia ofa ya kuunganishwa haraka huduma bora zaidi za chaneli za kisasa kupitia DSTV.
Baadhi ya wanahabari wakifuatilia mkutano huo wa DSTV.
Mkuu wa wilaya ya Geita awataka madiwani waliochaguliwa hivi karibuni kujenga uhusiano mwema wa kiuntandaji na watumishi wa halmashauri ili kuwaletea maendeleo wananchi. https://youtu.be/1ynKoT77ASg
Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Songea waonyesha matumaini makubwa na raisi mpya katika kubadili mfumo wa utendaji serikalini. https://youtu.be/iOHZUu4XXzU
Mapokezi makubwa yamgonja raisi Dr.Magufuli mkoani Geita huku wananchi wakiwa na amatumaini makubwa juu yake huku wengine wakitoa nasaha zao.https://youtu.be/LNnSnYYy8BU
Wakati raisi mstaafu Jakaya Kikwete ankabidhi madaraka ametoa masamaha kwa wafungwa 4160 nchini kote. https://youtu.be/_68wRnZyaLs
Taifa la Tanzania leo limepata raisi mpya wa awamu ya 5 baada ya Dr.Magufuli kuapishwa na kuanza kazi za kiserikali rasmi hii leo. https://youtu.be/ZtMxPb0k3rs
Wakazi wa Iringa watoa maoni yao juu ya mategemeo kwa raisi wa awamu ya 5 Dr.Magufuli huku wakitoa rai mbalimbali. https://youtu.be/QmUxnIAND80
Wakazi wa visiwa vya Zanzibar wametoa maoni yao kufuatia kuapishwa kwa raisi wa awamu ya 5 Dr.John Magufuli. https://youtu.be/qCFHPanLEVA
Aliwahi kuwa waziri mkuu wa Kenya na kiongozi mkuu wa upinzani wa Kenya aongea machache juu ya raisi wa awamu ya 5 Dr.Magufuli. https://youtu.be/r32j4qsgFno
Baada ya Raisi Kikwete kuhitimisha kipindi chake cha uongozi wa awamu ya 4 raisi huyo mstaafu azumgumzia malengo yake baada ya kustaafu.https://youtu.be/2BMfmtvWSHw
Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali yaihusuyo Tanzania. Wiki hii, tumeangalia zaidi kuhusu mustakabali wa Tanzania baada ya UCHAGUZI MKUU 2015