Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1017 | 1018 | (Page 1019) | 1020 | 1021 | .... | 3286 | newer

  0 0

  nh1
  Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti akifafanua jambo wakati akizungumza waandishi wa habari kuhusu kuvunjika kwa uzio wa jengo la mfuko huo linalojengwa mkoani Mbeya kutokana na kukumbwa na mvua na upepo mkali, amesema jengo hilo liko salama kabisa ila uzio unaosaidia kuwakinga wajenzi ndiyo ulioanguka kutokana na upepo huo. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF,Bw Rehani Athuman.
  nh2
  Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti akifafanua jambo wakati akizungumza waandishi wa habari kuhusu kuvunjika kwa uzio wa jengo la mfuko huo linalojengwa mkoani Mbeya.
  nh3
  Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF,Bw Rehani Athuman akionyesha mchoro wa jengo hilo kwa waandishi wa habari, kushoto ni Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti
  ......................................................................................................
  Utangulizi:
  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) hivi sasa unaendelea na ujenzi wa majengo katika mikoa mbalimbali nchini, kwa lengo la kujitosheleza kwa majengo ya ofisi na kukidhi mahitaji ya wanachama wake na wadau wengine.Moja ya mikoa ambayo inaendelea na ujenzi huo ni Mbeya, ambako Mfuko unajenga jengo la ghorofa kumi na mbili litakalokuwa na nafasi za ofisi na huduma nyingine ndani yake.

  Tukio la Kuanguka kwa jukwaa:
  Wakati shughuli hizo za ujenzi zinaendelea, jana mchana katika hali isiyotarajiwa mvua iliyoambatana na upepo mkali ilinyesha mjini Mbeya. Upepo na mvua hizo vilisababisha kuanguka kwa jukwaa la jengo hilo na kutua juu la paa la jengo la ofisi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoani Mbeya. Kuanguka kwa jukwaa hilo hakukuwa na madhara yoyote kwa maisha ya binadamu, kwa maana kuwa hakuna mtu aliyepoteza maisha au kupata majeraha. 

  Hata hivyo tukio hilo lilisababisha taharuki kwa wafanyakazi wapatao hamsini waliokuwemo ndani ya jengo hilo na hivyo kusababisha kazi kusimama kwa muda. Aidha tathmini ya awali iliyofanyika katika paa la jengo la TANESCO lililoangukiwa na jukwaa hilo inaonyesha kuwa paa hilo ilipata hitilafu ndogo ambayo itafanyiwa marekebisho kwa gharama za Mkandarasi anayejenga jengo la NHIF.

  Hatua za kisualama zilizochukuliwa:
  Kama sheria za ujenzi zinavyoagiza, kabla ya kuanza kwa ujenzi wa jengo hilo Mkandarasi alishajenga uzio kuzunguka jengo zima ili kuhakikisha kuwa shughuli za ujenzi hazileti madhara kwa wapita njia au ofisi zilizo jirani. Umakini wa Mkandarasi huyo katika kuzingatia taratibu za tahadhari katika shughuli za ujenzi, umewezesha jengo hilo la ghorofa kumi na mbili kufikia hatua nzuri ya ujenzi bila madhara yoyote kwa wajenzi wenyewe, wapita njia au ofisi za jirani.

  Aidha kufuatia tukio la Jumatatu 02/11/2015, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umeshamwandikia Mkandarasi anayeendelea na ujenzi katika jengo hilo kuhakikisha kuwa uzio unaozunguka jengo zima unaimarishwa zaidi hususani wakati huu tunapokaribia kipindi cha mvua za masika ili kuepuka uwezekano wa madhara yoyote kwa binadamu wakati shughuli za ujenzi zinaendelea.

  Namna Habari ilivyoripotiwa:
  Tunapenda kuufahamisha umma kwamba habari zilizoripotiwa jana na baadhi ya vyombo vya habari kwamba jengo la NHIF mkoani Mbeya limeporomoka, zilipotosha ukweli wa tukio hilo, kwani kilichoporomoka siyo jengo, bali ni jukwaa.Tunapenda kusisitiza kuwa tukio hilo limesabishwa na mvua kubwa na upepo uliovuma katika mji wa Mbeya, wala siyo uzembe wa Mkandarasi anayejenga jengo hilo.

  Wito kwa Wanachama wa NHIF:
  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya unawaomba wanachama na wadau wake nchini kote waendelee kuwa watulivu na kuvuta subira kwani changamoto ya ufinyu wa ofisi katika mikoa itakuwa imepatwa ufumbuzi baada ya kukamilika kwa ujenzi wa majengo ya unaoendelea hivi sasa katika mikoa mbali mbali nchini.
  Imetolewa na:
  Mkurugenzi Mkuu,
  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA MAWASILIANO SAYANSI NA TEKNOLOJIA 
  TAARIFA KWA UMMA 
  UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI WA KAMPUNI YA SIMU TANZANIA 
          Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Prof. Tolly Salvatory Augustin Mbwette  kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwa kipindi cha miaka miaka mitatu kuanzia tarehe 12 Oktoba 2015. 


  Uteuzi huo ni kwa mujibu wa kifungu Na. 9 (4) (a) cha Sheria Na. 20 ya Mwaka 1993 iliyoanzisha Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Prof. Tolly Salvatory Augustin Mbwette amekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania kwa kipindi cha miaka kumi kuanzia tarehe 13 Aprili 2005 hadi tarehe 13 Aprili 2015. Pia amekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwa taaluma ni Mhandisi ujenzi aliyobobea kwenye maeneo ya Mazingiria, TEHAMA, Utawala na Menejimenti kwa zaidi ya miaka 25 na amesoma Vyuo Vikuu vya Dar es Salaam, Tanzania; IHE Delft, Netherland; na Chuo Kikuu cha London, Uingereza kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza, Uzamili na Uzamivu. Pia ameshirikiana na Vyuo Vikuu mbali mbali duniani kutoka Bara la Ulaya, Amerika, Asia na Afrika katika maeneo ya uhandisi, utafiti, TEHAMA, uandishi wa vitabu na majarida mbali mbali.

  Imetolewa na:


  KATIBU MKUU


  Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia


  0 0

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akipokea ngao yenye picha ya chui ikiwa ni ishara ya tuzo ya Shirika la Nyumba la Taifa kwa Waziri huyo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu kwa kuonyesha utendaji uliokuwa wa kasi usiochoka wakati Waziri Lukuvi alipotembelea katika Shirika hilo kuaga rasmi.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akipokea ngao yenye picha ya chui ikiwa ni ishara ya tuzo ya Shirika la Nyumba la Taifa kwa Waziri huyo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu kwa kuonyesha utendaji uliokuwa wa kasi usiochoka wakati Waziri Lukuvi alipotembelea katika Shirika hilo kuaga rasmi.
  Waziri Lukuvi akizungumza na Wakurugenzi na Mameneja wa Makao Makuu ya Shirika hilo wakati alipotembelea katika Shirika hilo kuaga rasmi kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu.

  0 0


  UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga umewaomba radhi wadau wa soka pamoja na shirikisho la soka nchini (TFF) kwa vurugu zilizotokea


   kwenye mchezo wa baina yake na Mbeya City uliofanyika mwishoni mwa
  wiki uwanja wa CCM Mkwakwani.

  Mchezo huo wa ligi kuu Vodacom ulimalizika kwa  vurugu hadi kikosi cha
  kutuliza ghasia kilipoingilia kati na kutumia mabomu ya machozi
  kuwatawanya mashabiki wa soka waliokuwepo katika uwanja wa Mkwakwani.

  Vurugu hizo zilitokea kufuatia mwamuzi,Erick Enock kutoka Arusha
  kuamuru ipigwe penati kuelekea lango la Coastala union katika dakika
  za majeruhi na kuiwezesha Mbeya City kusawazisha bao hivyo hadi
  matokeo kuwa sare ya fungana bao 1-1.

  Coastal Union iliomba radhi katika barua yake iliyoandikwa na kutiwa
  saini na Mwenyekiti wake,Dr Ahmed Twaha kwenda kwa Katibu mkuu wa TFF
  na nakala kwa Rais Jamal Malinzi,afisa mtendaji mkuu bodi ya ligi na
  katibu wa Chama cha soka mkoa wa Tanga (TRFA).

  Aidha baada ya kutokea tukio hilo,Mwenyekiti huyo alisema alilazimika
  kuitisha kikao cha dharura cha kamati ya utendaji kujadili nini cha
  kufanya na hatua za kuchukua kwa wale watakaobainika kuhusika kwenye
  vurugu hizo.

  Katika kikao hicho alisema kamati ya utendaji imelaani vurugu hizo na
  imeaziamia kuwachukulia hatua waliohusika“Tunaomba radhi kwa TFF na
  TRFA kwa matukio hayo yaliyofanywa oktoba

  31,tunachukua ahadi klabu ya Coastal Union kufidia gharama za
  uharibifu utakaothibitika na kuwachukulia hatu waliohusika”ilieleza  sehemu ya barua hiyo.

  0 0

  Huu ni uchambuzi wa Habari toka vituo mbalimbali vya Televisheni Mchana Huu November 3, 2015.

  Watu 6 wamefariki dunia na 1 kujeruhiwa katika matukio 4 tofauti yaliyotokea mkoani Singida toka oktoba 31 na November 1.

  Mwenyekiti wa Baraza la Vyama Vya siasa nchini Peter Mziray avishauri vyama vya siasa kutumia baraza hilo kutatua Migogoro kwa Njia ya Mazungumzo. https://youtu.be/Z90lI_ga7Mg

  Wahamiaji Haramu raia Wa Ethiopia waliokamatwa wakiwa ndani ya lori wamehukumiwa kutumikia kifungo cha miezi 6 jela au faini ya laki 5  https://youtu.be/xc637Ykh6Mw

  Halmashauri ya wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa imefanikiwa kutatua baadhi Ya changamoto zinazoikabili sekta ya Kilimo kwa kuongeza idadi ya Afisa Ughani. https://youtu.be/nqk4rGU6hvE

  Kamati kuu Ya Chama Cha Mapinduzi CCM imetangaza kurudiwa kwa zoezi la kura za maoni katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Handeni. https://youtu.be/RVTSjWOxPGc

  Aliyekuwa mgombea Uraisi CCK aliyeenguliwa na NEC Dkt. Godfrey Malisa akusudia kuwania nafasi ya Spika wa Bunge. https://youtu.be/m4gnvAcUJn4

  Kukusekana kwa Umeme na Huduma za Maji kumetajwa kukwamisha maendeleo ya wanafunzi wa mchepuo wa sayanzi katika Shule Ya Wel Wel. https://youtu.be/PcmWUOA-v-o
  Raisi Jakaya Kikwete azungumzia ushindi wa ccm kuwa umetokana na kazi kubwa iliofanywa na vijana katika kuhakikisha ushindi wa Kishindo kwa Dkt. Magufuli huku akiviponda baadhi ya Vyombo vya Habari kuegemea Upande wa wapinzani na kunyima Fursa ya wananchi kusikia Sera za Chama Cha Mapinduzi. https://youtu.be/OoQicJcNJAI


  0 0

   Tabibu Gonzaga Marwa akiangalia baadhi ya mkopo ya Dawa jijini Dar es Salaam leo

  TAASISI isiyo ya Kiserikali ya Tanzaone Herbal Clinic chini ya mradi wake wa ‘Tanzaone’ hatimaye imethibitisha pasipo shaka kuwa mmea ujulikanao kama Lozera na bidhaa zitokanazo na mmea huo hazifai kwa matumizi ya binadamu na wanyama.

  Akizungumza na waandishi wa habari, sanjari na kuonyesha majibu ya vipimo vya kitaalamu kutoka Wakala wa Maabara ya Ofisi ya Mkemia Mkuu wa serikali kupitia utafiti uliofanywa chini ya mradi huo, Mratibu wa mradi.

   Tabibu Gonzaga Marwa, amesema  matokeo ya uchunguzi wa sampuli za mmea huo yameonesha una ukuvi yaani ‘fangasi’ aina ya Aspergillus ambao hutoa sumu ya Aflatoxin ambayo huweza kusababisha saratani ya maini.


  Aidha, Tabibu Marwa ameiomba serikali kupitia Wizara ya Afya, na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA, kuhakikisha wanachukua hatua za haraka kunusuru afya za walaji, sambamba na kushauri wadau wa tiba asili nchini kufanya utafiti wa kina wa dawa za mitishamba na bidhaa zake kabla ya kumfikia mlaji.


  Hati ya uchunguzi ya Mradi huo, namba 241/2013, uliopewa jina la ‘Tanzaone Red Tea Juice’ na kudumu kwa miaka mitatu 2010/2013, kwa kushirikisha watuamiaji wakubwa wa Lozera zaidi ya 250 nchini kote, ilichunguzwa, kuidhinishwa na kuthibitishwa na Mkemia Mkuu wa Serikali

  0 0


  0 0
  0 0

  Mhubiri TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations nchini Nigeria  ametua jijini Dar es salaam leo  tayari kwa kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli siku ya Alhamisi.
  Mara tu baada ya kutua uwanja wa Ndeghe wa Kimataifa wa Julius Nyerere, TB Joshua alikwenda Ikulu moja kwa moja kumsalimia Rais Jakaya Mrisho  Kikwete  kumsabahi na kumpongeza kwa kufanikisha uchaguzi mkuu kwa uhuru na amani, huku akiondoka madarakani akiwa mtu mwenye furaha. TB Joshua amepongeza Rais Kikwete pia kwa kupata Dkt Magufuli kama mrithi wake, akimtaja Rais huyo mpya mteule kama Rais wa Tanzania wa Baraka na Fanaka tele katika awamu hii mpya.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki Mhubiri TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations la nchini Nigeria Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii. TB Joshua ametua jijini Dar es salaam  tayari kwa kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli siku ya Alhamisi.


   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mhubiri TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations la nchini Nigeria Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii.
  Picha na Freddy Maro

  Rais mteule wa awamu ya tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli alimpokea Mhubiri wa kimataifa kutoka Nigeria  TB Joshua Uwanja wa ndege Dar jioni hii. Mhubiri huyo aliyekuja na watu 40 kwa ndege yake mwenyewe, amekuja kushuhudia Dkt Magufuli akiapishwa  0 0


  0 0


  0 0  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

  JESHI la Polisi limewataka wananchi kuendelea na utulivu kama walivyoonyesha wakati wa upigaji kura na hatimaye kupatikana katika siku ya uampishwaji wa Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Kamishina wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi hilo, Paul Chagonja amesema kuwa jeshi la polisi limeridhishwa na utulivu uliokuwepo wakati wa upigaji kura, na utulivu huo umeweza kufanya uchaguzi kwenda salama na hatimaye kukaweza kupatikana mshindi.

  Amesema katika suala la Zanzibar liko katika mazungumzo na viongozi wanafanya kazi yao hivyo maandamano hayana nafasi kutokana na taratibu wanazozitumia.

  Chagonja amesema watu waliokamatwa katika vurugu za uchaguzi wamefikishwa mahakamani na huku wengine wakiendelea na uchunguzi.

  Amesema hali ya amani ipo na wananchi wametakiwa kulinda hali hiyo na ikitokea mtu analeta uchochezi walipoti kwa vyombo vya usalama ili hatua zichukuliwe.
  Chagonja ametaka baadhi ya taarifa katika mitandao ya jamii kuupuzwa ,kwani zinatoa taharuki kwa wananchi na zinapotosha.

  0 0

   Kibanda cha kitakachotumika wakati wa kuapishwa kwa Rais Mteule, Dk John Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kesho kutwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
   Askari wa Jeshi la Wananchi akiigiza kama Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davis Mwamunyange na mwingine akiigiza kama Rais anayemaliza muda wake, Jakaya Kikwete wakati wa mazoezi ya sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
   Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange (wa pili kulia), Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Maangu (wa tatu kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick wakipiga saluti ulipokuwa unaimbwa wimbo wa Taifa wakati wa mazoezi ya sherehe za kuapishwa Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

   Kikundi cha sarakasi kikitumbuiza wakati wa maandalizi hayo
   Wasanii kutoka Zanzibar wakicheza ngoma ya kibati wakati wa mazoezi hayo
   Mtu aliyeigiza kama  Rais Jakaya Kikwete, akiwa amesimama alipokuwa akipigiwa mizinga ikiwa ni ishara ya kuagwa kwa rais huyo kabla ya kuapishwa Rais mpya wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli wakati wa mazoezi hayo.
  Mtu aliyeigiza kama Rais Jakaya Kikwete, akielekea kukagua gwaride la heshima la kumuaga wakati wa mazoezi hayo.

  0 0

  By Innocent Mungy
  Geneva, 3 November 2015

  The 2015 World Radiocommunication Conference, the international treaty-making Conference, opened in Geneva yesterday. The treaty-making Conference is expected to allocate spectrum for rapidly evolving ICTs”

  The conference which started yesterday 2nd November to 27 November, will review the international regulatory framework for radiocommunications – the Radio Regulations – and revise them as needed. This process will take into account the rapid evolution of information and communication technologies (ICT), ensuring the global management of the radio-frequency spectrum and satellite orbits, and enabling people to live and travel safely while enjoying high performance radiocommunications.

  During the opening Ceremony, Mr Festus Yusufu Narai Daudu of Nigeria was appointed Chairman of the 2015 World Radiocommunication Conference along with six Vice Chairmen: Mr A. Jamieson (New Zealand), Mr Y. Al-Bulushi (Oman), Mr D. Obam (Kenya), Ms D. Tomimura (Brazil), Mr A. Kühn (Germany), and Mr N. Nikiforov (Russian Federation).
  3800 delegates, representing more than 160 out of ITU’s 193 Member States are attending the 2015 World Radiocommunication Conference (WRC-15). About 100 observers from among ITU’s 700 private sector members along with international organizations also attending the conference.

  ITU Secretary General during the opening ceremony said the 2015 World Radio Conference will set new and better ways to regulate radio services and applications.

  “The 2015 World Radiocommunication Conference will define new and better ways to regulate radio services and applications,” said ITU Secretary-General Houlin Zhao. “In a world where radiocommunications play an increasingly important role in connecting people, I am convinced that the outcome of the conference will contribute towards making the world a better place for all.” He added.

  “With the relentless expansion of wireless services worldwide, all services relying on radio waves are competing for a share of the radio-frequency spectrum to support new applications, growing user numbers and exploding traffic,” said François Rancy, Director of ITU’s Radiocommunication Bureau in his speech during the beginning of the conference.
  “The deliberations at WRC-15 and its outcomes will ensure that we can maintain a stable, predictable and universally applied regulatory environment that secures long-term investments for a multi-trillion-dollar industry.” Said Mr. Rancy.

  Tanzania, an ITU member is participating in 2015 World Radio conference with participants from Ministry of Communications, Science and Technology, Ministry of Infrastructure (Zanzibar Government), TTCL, Tanzania Maritime Agency, TCRA and other stakeholders.

  World radiocommunication conferences (WRC) are held every three to four years. It is the job of WRC to review, and, if necessary, revise the Radio Regulations, the international treaty governing the use of the radio-frequency spectrum and the geostationary-satellite and non-geostationary-satellite orbits. Revisions are made on the basis of an agenda determined by the ITU Council, which takes into account recommendations made by previous world radiocommunication conferences.

  The general scope of the agenda of world radiocommunication conferences is established four to six years in advance, with the final agenda set by the ITU Council two years before the conference, with the concurrence of a majority of Member States.

  0 0

  DSC_0027
  Mwenyekiti wa Mfuko wa Doris Mollel Foundation, Bi. Doris Mollel akiwakaribisha wageni mbalimbali na wanahabari wakati wa utambulisho maalum juu ya tamasha linalotarajiwa kufanyika siku ya Jumapili Novemba 8, katika viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu Idara ya Afya, uzazi na watoto, Bi. Georgina Msemo na kulia kwake ni Dk. Sonal Peter ambaye ni daktari wa watoto (Pediatrician) kutoka Hospitali ya Agha Khan. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).

  Na Andrew Chale, Modewjiblog
  [DAR ES SALAAM] Katika kuadhimisha siku ya watoto njiti duniani, Taasisi ya Doris Mollel Foundation (DMF) imeandaa tamasha la kwanza na la aina yake kufanyika nchini siku ya Jumapili Novemba 8. 2015 kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni kuanzia majira ya asubuhi mpaka saa 12 jioni huku wasanii mbalimbali wakitarajiwa kushiriki kwa ajili ya kuchangisha fedha za kununulia vifaa vya kusaidia watoto wanaozaliwa na uzito pungufu ama watoto njiti.

  Akielezea mbele ya wanahabari jijini Dar es Salaam mapema jana, dhumuni la tamasha hilo ni kuwaleta watanzania pamoja kupata uelewa na mwamko katika kuadhimisha siku hiyo muhimu kwa afya na ustakabali wa mtoto njiti ambapo kulingana na takwimu za Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, takribani watoto 88,128 walizaliwa njiti au wakiwa na uzito mdogo nchini kwa kipindi cha mwaka 2014/2015 pekee.

  “Lengo ni kuhakikisha kupitia Mfuko huu unasaidia watoto njiti hasa kwa vifaa vya kuwawezesha kusaidia maisha yao. Tunataka kufikisha vifaa 10 kwa kila Kanda chache za awali. Karibuni sana watanzania kwa siku ya Jumapili Novemba 8. Kwa kiingilio cha sh 2,000 pekee kama mchango ambapo utapata burudani ya kipekee kutoka kwa wasanii mbalimbali wakiwemo Barnaba Classic, Mwasiti, kundi la The Voice, Miriam, Baraka De Prince, Ruby, Shilole na wengine wengi.” Amebainisha Doris Mollel.

  DSC_0031
  Tukio hilo likiendelea.

  Aidha, Doris amebainisha kuwa, Watanzania watapata fursa maalum ya kuusikia wimbo ulioimbwa na baadhi ya wasanii hao watakaoshiriki katika tamasha hilo.

  DMF imeongeza kuwa, baada ya tamasha hilo, kwa kushirikiana na wadhamini pia itatoa vifaa mbalimbali ikiwemo (Suction machines, Oxygen Concentrators na Feeding tubes) hii ni kwa Hospitali za Mikoa nchini ilikuweza kusaidia watoto hao na vifaa hivyo vinatarajiwa kutolewa katika siku ya kilele cha maadhimisho ya mtoto njiti Duniani huku kwa Tanzania ikitarajiwa kufanyika Mkoani Mbeya.


  0 0
 • 11/03/15--23:03: MAPITIO YA MAGAZETI LEO


 • SIMU.TV; Magufuli aileta dunia Tanzania, Sitta ajitosa tena kuwania uspika. Makamishna ZEC wakaliwa kooni. Pitia udondozi wa magazeti;  https://youtu.be/nanyB8GGQqU

  SIMU.TV; Pata habari kemukemu za magazetini ikiwemo ya UKAWA kubanwa na kauli ya TEMCO juu ya uchaguzi mkuu uliyofanyika nchini;  https://youtu.be/LwY0psFttZQ

  SIMU.TV; TP Mazembe yaimwagia siri Stars, Samatta awania tuzo ya mwanasoka bora Afrika. Habarika na magazeti ya michezo hapa Simu.tv; https://youtu.be/qp0Y_rs67dg

  SIMU.TV;  TB Josua awafuata Lowassa, Magufuli. Marais 8 kushuhudia Dk.Magufuli akiapishwa.Ni katika magazeti ya leo. Novemba 4.2015; https://youtu.be/euRBepbSRD4

  0 0
 • 11/03/15--23:36: BEI YA MADAFU LEO


 • 0 0

  Meneja mauzo Kanda ya Kaskazini wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, Aluta Kweka ( kulia) pamoja na Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Hafsa Mtasiwa (wa kwanza kushoto) akifatia na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe Patricia Andrew Mbigili (katikati) wakiwa na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya mazinde Day wakionyesha vitabu walivyokabidhi na Airtel ikiwa na lengo la kutatua changamoto ya uhaba wa vitabu shuleni hapo. Vitabu hivyo vya sayansi vinathamani ya shilingi milioni 3. 

  KAMPUNI ya simu ya mkononi ya Airtel kupitia mpango wake wa Airtel shule yetu imetoa msaada wa vitabu vyenye thamani ya sh.milioni tatu kwa Shule ya Sekondari ya mazinde Day ya mkoani wa Tanga wilaya ya Korogwe.

  Akikabidhi msaada huo jana Meneja mauzo Kanda ya Kaskazini Aluta Kweka alisema kuwa kwa kutambua umuhimu wa kuendeleza elimu nchini Airtel ililazimika kuanzisha mpango huo ili kuongeza viwango vya ufaulu.

  Alisema kuwa vitabu vilivyotolewa ni vya sayansi hivyo kupitia vitabu hivyo wanafunzi wataongeza bidii kwa kuvisoma na kusaidia idadi ya wanafunzi wanaofaulu katika masomo hayo ambayo awali ilionekana ni masomo magumu kutokana na kutokuwa na vitendeakazi.

  Alisema kuwa utoaji wa vitabu hivyo kwa shule za sekondari ni mmrefu unaofanywa na kampuni yake ili kutimiza dhamira yake ya kurudisha faida wanayopata kwa Watanzania na kuboresha huduma mbalimbali za kijamii.
  Meneja mauzo Kanda ya Kaskazini wa Airtel, Aluta Kweka akimkabidhi vitabu vya sayansi mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Mazinde Day, Bi Jermana Mchome (katikati) ikiwa ni msaada katika kuendeleza elimu na kutatua changamoto za uhaba wa vitabu shuleni hapo. Akishuhudia ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Hafsa Mtasiwa. 

  Alisema kuwa hadi sasa zaidi ya shule 1,300 zimenufaika na mradi huo ambapo umechangia kupunguza changamoto ya ukosefu wa vitabu kwa shule zilizokabidhiwa.

  Akizungumza wakati wa kupokea msaada huo Mkuu wa wilaya ya Korogwe Hafsa Mtasi aliipongeza kampuni hiyo ambapo imekuwa ikisaidiana na serikali katika kuinua kiwango cha elimu nchini.

  "Tunaipongeza Airtel kwa mpango huu kwani umekuwa ukichangia kupunguza changamoto ya ukosefu wa vitabu katika shule za sekondari na ni mfano mzuri wa kuigwa," alisema.

  Naye Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya Mazinde Day,Jermana Mchome aliishukuru Airtel pamoja na kuwasisitiza wanafunzi wa shule zote zilizofaidika kuvitumia vitabu kikamilifu ili kujiendeleza kwa manufaa ya jamii zao pamoja na taifa kwa ujumla.

  "Sasa ni jukumu lenu wanafunzi kutumia fursa hii kusoma kwa bidii ili muweze kusaidia taifa baada ya kisomo chenu, msaada huu mkiutumia vizuri ni nyenzo kubwa sana yakusaidia hata familia zenu kutokana na faida kubwa mtakayopata kutokana na zao la elimu” alisema.

  Kampuni ya simu ya Airtel imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia sekta ya elimu kupitia mpango wake wa Airtel Shule Yetu bado inasaidia vijana mbalimbali hapa nchini kutatua changamoto mbalimbali kupitia mradi wake mpya wa Airtel FURSA Tunakuwezesha
  Meneja mauzo Kanda ya Kaskazini wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, Aluta Kweka (kushoto) pamoja na Mkuu wa wilaya ya Korogwe ,Hafsa Mtasiwa na Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya Mazinde Day, Jermana Mchome (katikati) wakionyesha vitabu walivyokabithi na Airtel ikiwa na lengo la kutatua changamoto ya vitabu shuleni hapo. Vitabu hivyo vya sayansi vinathamani ya shilingi milioni 3.

  0 0


older | 1 | .... | 1017 | 1018 | (Page 1019) | 1020 | 1021 | .... | 3286 | newer