Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

TAARIFA YA MWENENDO WA MIFUMO YA HALI YA HEWA NA MVUA ZA MSIMU WA VULI 2015


WADAU WA MUZIKI WAMLILIA MMILIKI WA BENDI YA FM ACADEMIA

MISA YA MAREHEMU MAMA GREN JUDICA MOSHI Washington DC

$
0
0
Ndugu, jamaa na marafiki mbalimbali, jana (Novemba mosi 2015) walijumuika na wanafamilia katika misa na kusherehekea maisha ya Mama Gren Judica Moshi iliyofanyika hapa Washington DC
Watoto wawili wa Marehemu Donald na James Moshi, na ndugu wengine, waliungana kwa misa hiyo iliyofanyika alasiri na kufatiwa na chakula cha pamoja

Mchungaji kiongozi wa Kanisa la The Way of the Cross Gospel Ministries Ferdnand Shideko, akiwakaribisha watu waliohudhuria misa hiyo

Mch John Kadyolo akifungua misa kwa maombi. 

Utambulisho wa kipindi kipya cha Televisheni cha Kiswahili Washington DC

$
0
0
Mwakilishi wa balozi, ambaye pia ni Mkuu wa utawala na Fedha wa ubalozi, Swahiba Mndeme, akisalimia wageni wakati wa utambulisho
Mkuu wa utawala na Fedha wa ubalozi, Swahiba Mndeme akitambulisha rasmi kipindi hicho

Mmoja wa washiriki wa Jambo Show Radio inayotayarishwa na Swahili Media Network, Sala Damali
Mwanzilishi wa Jambo Show Steven Mghaza akielezea kipindi hicho kwa wageni waalikwa
Meneja masoko wa CBC Radio hapa Washington DC R.J Trzaska akielezea umuhimu wa radio kwa jamii yetu na muelekeo wake.
 Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

JOTO LA ASUBUHI LA EFM 93.7 NOVEMBER 3, 2015 JUMANNE

TICKETS ON SALE NOW FOR THE ST. ANDREW'S BALL @ the Hyatt Regency Hotel in Dar es salaam

$
0
0
Book your tickets NOW for the St Andrew's Ball 2015 - tickets sell out fast for this great Scottish event -Held at the Hyatt Regency Hotel in Dar es salaam on  Saturday  28th November this year from 6.45pm
 
Lots of great food (of course with HAGGIS) with beer, wine and whisky on the table. Our fantastic Scottish Band all the way from Bonny Scotland, Jigging until the wee small hours of the morning. Party on after the Ball at ROUGE Night club in the Hyatt - plus Amazing raffle prizes to be won

TANZANIA HOTTEST MODELS COMPETITION YAJA

$
0
0
Neema  Modelling  Agency, wanakuletea  TANZANIA  HOTTEST  MODELS  COMPETITION. Ni    shindano  la  kumtafuta  mwanamitindo  wa  kike , mwenye   mvuto  kuliko  wote  Tanzania
SIFA  ZA  WASHIRIKI.
1.    Awe  msichana  mwenye  umri    usio pungua  miaka  kumi  na  nane  na  usio  zidi miaka  thelathini.
2.    Elimu  ya  kuanzia  kidato  cha  nne  na  kuendelea.
3.    Uwezo  wa  kuzungumza  kwa  ufasaha  lugha  za  Kiswahili  na  kiingereza.
4.    Awe  maridadi na  mwenye  mvuto
5.    Awe  raia  wa Tanzania  anaye  ishi  mahali  popote  ndani  au  nje  ya  Tanzania.
6.     Awe  na  passion  na  kazi  ya  mitindo.

UTARATIBU  WA  KUSHIRIKI.
Tuma  CV yako  pamoja  na  picha  zako  kumi  za  rangi  ( Full)  ulizo  piga  hivi  kaibuni, kwenda :neemamodelling@gmail.com.

Mwisho  wa  kupokea  maombi  ya  kushiriki  katika  shindano  hili  ni  tarehe  30 NOVEMBA  2015  saa  nane  kamili  mchana.
Shindano  kuzinduliwa rasmi  tarehe  05  DESEMBA  2015.
Kwa  maelezo  zaidi  kuhusu  shindano  hili, tembelea  kila  siku : www.neemaherbalist.blogspot.com
 Kwa  maulizo  zaidi  wasiliana  nasi  kwa  simu  0765  10  30  80.
Au  fika  katika  ofisi  zetu  zilizopo  Ubungo  Dar  Es  salaam, karibu  na  Shule  Ya  Msingi  Ubungo  National  Housing, nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA jijini Dar es salaam.
 HII  NI  FURSA    YA  PEKEE  KWA  WANAMITINDO  CHIPUKIZI, KUONYESHA VIPAJI  VYAO  VYA  MITINDO.

This Weekend "Karibu Music Festival, Bagamoyo 2015"

$
0
0
 The long wait is almost over, The Karibu Music Festival 2015, is taking off this weekend (Friday 6th Nov. To Sunday 8th November) Three days of extreme Music, Arts, and Cultural experience.

Headlining one of Africa's most popular musician and prominent in world music, PAPA WEMBA, and a variety of International Musicians from KENYA, UGANDA, TOGO and SOUTH AFRICA  to NORWAY, PAKISTAN and JAMAICA. 

With the a variety of Tanzanian Musicians, More than 20 Groups from Tanzania, ranging from Cultural groups, Ngoma Dances, Zouk, RnB, Fusion, Reggae, Hip Hop and Bongo Flava.

Want to Be part of the Adventure?

Tickets can be bought online through: 
and 

Also physically at the following places:

1. Robby One Fashion (Sinza and Kinondoni)
2. Born To Shine (Mwenge)
3. Big Daddy Store (Biafra)
4. Didis (Oysterbay)



SHEREHEKA NA MICHUZI ep 5

$
0
0
Kama unataka kusherekea sherehe yako na MICHUZI TV piga simu namba 0714471474 au 0712426666 Pia usisahau kujiunga(Susscribe) na MICHUZI TV Youtube.

Ngoma azipendazo ankal:FM ACADEMIA WAZEE WA NGWASUMA -HESHIMA KWA WANAWAKE

Mgahawa wa Chef issa mjini Trollhatan, sweden, walisha waombolezaji 1000 baada ya mazishi ya mwafrika aliyeuwawa kibaguzi

$
0
0
Mnamo tarehe 22/10/2015 kijana mmoja wa Kiswedish alivamia shule ya Krona iliyopo mji wa Trollhatan uliopo jirani na mji wa Goteborg ambao ni mji wa pili kwa ukubwa nchini Sweden.
Kjjana huyo alivamia shule hiyo akiwa amevalia mavazi ya Halloween na kuanza kuchoma visu watoto . Alifanikiwa kuchoma visu walimu wawili na watoto wawili na maaaskari  wawili kabla ya polisi kumpiga risasi na na kumuua dunia hapo hapo. Watu aliowajeruhi walikimbizwa hospital ambapo mwalimu mmoja na mwanafunzi mmoja walifariki dunia na wengine wailipona.

Baada ya kumpekua, Polisi walikuta barua yenye maelezo na sababau ya huyo muuaji kuamua kufanya hivyo. Aliandika kuwa nimeamua kufanya mauaji haya kwa sababu  sikubaliana na serikali yangu kwa sasa kukubali wimbi la wahamiajai kuongezeka. Hali kwa sasa imekua ni tete ambapo karibu  kila wiki kwa nyumba wanayoishi wahamiaji  imekua ikichomwa moto au kambi waliyokua wamehifadhiwa wakimbizi toka sirya.

Tarehe 13/10/2015 ndio yalikua mazishi ya kijana huyo wa Kiafrika aliyeitwa Ahmed Hassan aliyefariki katika mauaji hayo ya kibaguzi na kuzikwa na maelfu ya watu toka ndani na nje ya Sweden.

Baada ya mazishi na huduma za chakula cha mchana kilichoandaliwa na Tanzanian Restaurant kwa wageni maalumu tu ambao walifikia 1000. Mgahawa huu wa Chakula cha Kiafrika unaendeshwa na Executive Chef Issa Kipande, ambaye pia ni blogger nguli na mwanachama hai wa Tanzania Bloggers Network (TBN).
 Chef Issa akiwa na Gustav Fridolin waziri wa elimu wa Sweden wakati wa chakula cha mchana amvcho kilihudumiwa na mgahawa wake anaoendesha wa Tanzanian restaurant kwa wageni maalumu tu ambao walifika 1000.
 Akiwa na Paul Akerlund Meya wa jiji la Trollhattan
 CHef Issa akiwa na mmoja wa watu mashuhuri waliofika kutoa rambi rambi na kulaani kitendo hicho ni pamoja na Bw. Mohamed Adulahi Mohamedi almaarufu  kama "Farmajo' ambaye  alikua waziri mkuu wa Somalia kati ya mwaka 2010 na 2011, 
 Chef Issa akiwa na Monica Hanson, Meya msaidizi wa jiji la Trollhattan
 Eneo la tukio mnamo tarehe 22/10/2015 ambapo kijana mmoja wa Kiswedish alivamia shule hii ya Krona iliyopo mji wa Trollhatan uliopo jirani na mji wa Goteborg ambao ni mji wa pili kwa ukubwa nchini Sweden.
Sehemu ya umati wa waombolezaji tarehe 13/10/2015 kwenye mazishi ya kijana huyo wa Kiafrika aliyeitwa Ahmed Hassan aliyefariki katika mauaji hayo ya kibaguzi na kuzikwa na maelfu ya watu toka ndani na nje ya Sweden.

TAWI LA CCM EMPRESS KWA FUNDI MUSA MTAA WA SAMORA WASHEREHEKEA USHINDI WA DK. JOHN POMBE MAGUFULI

$
0
0
1
MBUNGE mteule wa Muleba Kaskazini (CCM) na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Charles Mwijage akisalimiana na Godson Kaligo Mjumbe wa tawi la CCM Epress Social lililopo mtaa wa Samora maarufu kwa Musa Shoeshine alipowatembelea wakati wa sherehe yao ya kusherehekea ushindi wa Rais Mteule Dr. John Pombe Magufuli mara baada ya kushinda katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu nchini kote, Wana CCM hao wamesherehekea kwa muziki na kupata supu ya mbuzi na nyama choma huku wakiwakaribisha wananchi mbalimbali bila kujali itikadi zao kwani Dr John Pombe Magufuli ni Rais wa Watazania wote.(PICHA NA RASHID SHOTI-DAR ES SALAAM)
3
MBUNGE mteule wa Muleba Kasikazini (CCM) na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Charles Mwijage akibadilishana mawazio na Godson Kaligo na wana CCM wa tawi hilo.
4
Katibu wa Tawi hilo Musa Mtulia ambaye pia ni Shoeshine Maarufu mtaa wa Samora akiendelea na kazi yake huku wana CCM wengine na wadau wengine wakiendelea na sherehe hiyo kwa kupata supu.

ngoma azipendazo ankal: Dunia Kigeugeu FM Academia

WADAU WA MUZIKI WAMLILIA BABA WA FM ACADEMIA "WANA NGWASUMA" MAREHEMU MARTIN KASYANJU MSIBANI OYSTERBAY, DAR ES SALAAM LEO

$
0
0

KWA MUJIBU WA TAARIFA ZA FAMILIA YA MAREHEMU MARTIN KASYANJU YANATARAJIWA KUFANYIKA SIKU YA IJUMAA KATIKA MAKABURI YA KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM. HII NI KURUHUSU WATOTO NA NDUGU WA MAREHEMU WALIO NJE YA NCHI NA MIKOANI WAWAHI MAZISHI. 
MAREHEMU KASYANJU, AMBAYE ALIKUWA MMILIKI WA BENDI MAARUFU YA FM ACADEMIA WANA NGWASUMA, ALIFARIKI JANA JIJINI DAR ES SALAAM BAADA YA KUUGUA KWA MUDA MFUPI. MSIBA UKO NYUMBANI KWA MAREHEMU OYSTERBAY JIRANI NA HOTELI YA COLOSSEUM JIJINI DAR ES SALAAM. RATIBA KAMILI YA MAZISHI ITATOLEWA PUNDE

Makala ya Sheria: KUMLAZIMISHA SHAHIDI KUFIKA MAHAKAMANI...

$
0
0

Na Bashir Yakub
Kesi/shauri  lolote  iwe  jinai  au  madai  kuishinda  kwake   mara  nyingi  hutegemea  mambo  makuu  mawili. Kwanza  mashahidi ,pili  ushahidi. Mashahidi  siku  zote  ni  watu.  Hakuna  kitu  kinaweza  kuitwa  mashahidi  halafu  kisiwe  binadamu. 
Hii ni  tofauti  na  ushahidi. Ushahidi   si  lazima  wawe  binadamu.   Vitu hasa  vizibiti(exhibit)  ndivyo  huitwa  ushahidi. Nyaraka, mali,  vifaa,  na  kila  kitu  ambacho  mtu  anaweza kukitumia  mahakamani kuthibitisha  kile  anachokisema huitwa ushahidi. 
Yumkini  yawezekana  wakati  huohuo  mmoja  ukawa  na  vyote  yaani  ushahidi  pamoja na  mashahidi  hapohapo.  Hii  hutegemea namna mtu  alivyojiandaa  katika    kuwasilisha  kesi  yake.


1.SIFA  ZA  SHAHIDI.

Si  kila  mtu  ana  sifa  za  kuwa  shahidi. Shahidi  hutakiwa  kuwa  mtu  mkweli , muaminifu  na  muadilifu.  Lakini  pia  sifa  kuu  ya  shahidi  ni  kuwa  na  akili  timamu.  Mtu  asiye  na  akili  timamu  hawezi  kuwa  shahidi. Lakini  pia  mtu  mwenye  sifa   ya  uongo  hasa  huko  nyuma  kama  aliwahi  kutoa  ushahidi  wa  uongo  mahakamani  na  ikathibitishwa  kuwa  alitoa  ushahidi  wa  uongo   basi  naye  hupoteza  sifa  ya  kuwa  shahidi.  

Pia  sifa  nyingine  kuu  ya  shahidi   ni  muhimu  awe  ni  yule  aliyeona,  kuhisi  kwa  kutumia  moja  kati  ya  viungo  vyake,   au  kusikia .  Hii  ina  maana  shahidi  hutakiwa kuwa yule  anayelijua  tukio  kwa  kulishuhudia  na  si  vinginevyo


2.  IDADI  YA  MASHAHIDI  INAYORUHUSIWA.

Hakuna  idadi  ya  mashahidi  rasmi  inayoruhusiwa  kisheria.  Idadi  yoyote  ya mashahidi  inaruhusiwa.  Suala  la  msingi  hapa  ni  kuwa  kila  shahidi  katika  mashahidi  hao  unaowaleta  awe  na  umuhimu  katika  kesi.  Usilete  watu  ambao   hawahusiki  na  kuisababishia  usumbufu  mahakama. Hii  ni  kwasababu  wingi  wa  mashahidi hauakisi  ushindi  katika  kesi. Hata  shahidi mmoja  tu  kama  ni  wa  muhimu anaweza  kukufanya  ushinde  kesi na kumshinda  mwenye  mashahidi  ishirini.




SHEREHEKA NA MICHUZI ep 6

NAIBU KATIBU MKUU MPYA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AANZA KAZI RASMI NA KUWATAKA WATUMISHI KUTEKELEZA KAULI MBIU YA “HAPA KAZI TU”

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi aliyeteuliwa hivi karibuni, John Mngodo, akijitambulisha kwa Watumishi  mara baada ya kuanza kazi rasmi  katika Wizara hiyo. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Lilian Mapfa na kushoto ni Mwenyekiti wa TUGHE,  Obedi Mbaga.


Mkurugenzi wa Idara ya Sheria katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Marlin Komba akijitambulisha mbele ya Naibu Katibu Mkuu mpya, John Mngodo (hayupo pichani) wakati wa Mkutano kati ya Watumishi na Naibu Katibu Mkuu huyo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara.
Naibu Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, akizungumza na Watumishi mara baada ya kuanza kazi rasmi katika Wizara hiyo.
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu mpya wa Wizara (hayupo pichani) alipofanya mkutano na watumishi hao mara baada ya kuanza kazi rasmi katika Wizara hiyo.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

Imeandaliwa na Kitengo Cha Mawasiliano  Serikalini-Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

KAMPENI YA BINTI THAMANI KUFANYIKA NOVEMBA 17 KATIKAUKUMBI WA KING SOLOMONI JIJINI DAR

$
0
0
Mratibu wa Kampeni ya BINTI THAMANI wa Taasisi ya Don Bosco Net Tanzania, Agnes Mgongo akizunumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO kuhusiana kampeni ya BINTI THAMANI itakayofanyika katika ukumbi wa King Solomoni jijini Dar es Salaam na kampeni hiyo itakuwa inawalenga hasa wasichana ili kufikia malengo yao kwa kutumia fursa zinazotolewa na vyuo vya Don Bosco hapa nchini.
Mkurugenzi wa malezi ya vijana wa Taasisi ya Don Bosco Net Tanzania, Padre, Dustan Haule akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa habari MAELEZO kuhusiana na harakati za kuwakomboa wasichana na uwepo wa kampeni ya BINTI THAMANI ambayo itafanyika katika ukumbi wa King Solomoni jijini Dar es Salaam, pia amewakaribisha wadau na wafadhili mbalimbali katika kufanikisha kampeni ya BINTI THAMANI itakayo wawezesha wasichana ili kufikia maelengo na waweze kujitegemea katika jamii. Aidha alimtambulisha Msanii wa Kizazi Kipya Elias Barnaba (Barnaba Boy Classic) pamoja na Mshereheshaji na Mchekeshaji MC, Pilipili kuwa watakuwepo katika kampni ya BINTI THAMANI  itakayofanyika Novemba 17 mwaka huu katika ukumbi wa King Solomon jijini Dar es Salaam. 

Kutoka kushoto ni Msanii wa Kizazi Kipya Elias Barnaba (Barnaba Boy Classic) na Mshereheshaji na Mchekeshaji MC, Pilipili wakiwa katika mkutano ulioandaliwa na Taasisi ya Don Bosco Net-Tanzania leo katika ukumbi wa Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam.
Msanii wa Kizazi Kipya Elias Barnaba (Barnaba Boy Classic) akizungumza na waandishi wa habari kuwa atatumbuiza katika kampeni ya BINTI THAMANI ambayo itafanyika Novemba 17 katika ukumbi wa King Solomoni  jinini Dar es Salaam. Pia aliwasihi wasichana kujitokeza kwa wingi ili waweze kuwahamasisha wasichana wengi zaidi ili kujipatia mafunzo yanayotolewa na Taasisi ya Don Bosco Net Tanzania.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwasikiliza waandaaji wa kampeni ya BINTI THAMANI itakayofanyika Novemba 17 mwaka  katika ukumbi wa King Solomoni jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

KATIBU MKUU WA UCHUKUZI ATEMBELEA ENEO INAPOJENGWA RELI MPYA YA KISASA YA STANDARD GAUGE

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka,akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu Rwanda, Rwakunda Christian,wakati walipotembelea ujenzi wa reli mpya ya kisasa, iliyoanza kujengwa Mkoani Pwani, katika eneo la Soga.
 Muonekano wa ujenzi wa reli mpya wa kisasa Standard Gauge, ambayo inaendelea kujengwa katika eneo la soga mkoani Pwani.

 Muonekano wa ujenzi wa reli mpya wa kisasa Standard Gauge, ambayo inaendelea kujengwa katika eneo la soga mkoani Pwani.
IMG 5841     Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka (wa tatu kutoka kulia), akiwa katika picha pamoja na Uongozi wa Taasisi inayosimamia usafirishaji katika Ukanda wa Kati pamoja na Viongozi wa Nchi zinazotumia ukanda wa Kati, wakati walipotembelea ujenzi huo hivi karibuni, katika eneo la Soga, Pwani.
   Muonekano wa Vituo vya Reli hiyo Mpya ya kisasa ya standard Gauge, itakapokamilika.

(Habari Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)

Zantel staff meets with Benoit Janin new CEO

$
0
0
 

Dar es Salaam-November 2,2015: Zantel Tanzania, welcomed Benoit Janin new Chief Executive Officer taking over the reigns from Pratap Ghose.
A 17-year telecom industry veteran, Benoit is best known for his tenure as a Tigo Chad CEO, where he successfully led Tigo Chad to experience a significant double-digit growth to become the unchallengeable market leader and also launching 3G and 4G services.

Prior to joining Millicom Group Benoit has worked for almost 3 years in Vimpelcom group as the CCO of their Cambodia operation and before that, he worked for 10 years within Orange Group in various consultant and then C-level roles.

Speaking of his new role, Benoit said he is excited to join Zantel and looks forward to work together with the Zantel team to reenergize the Zantel brand.
"I am motivated by the challenge in creating the new era for Zantel where we are going to leverage the current brand status, increase the quality of service, improve mobile money services and expand areas of Corporate Social Responsibility ’ said Benoit.

Benoit has a Master of Science (MSc) degree in Business Administration and Management from the ICN High Business School in France. 

He also has a Leadership program certificate from Stanford Business School, together with a Post-Graduate degree in Foreign languages (DEUG LEA in English & German) from Aix-en-Provence University.

In Zantel he would be responsible for enhancing market share and margins along with growth of alternate revenue streams including 4G, Data, Ezypesa and value added services, taking Zantel to next phase.
Mr. Beneth Kagoro receiving “Long service awarded” handed over to him by CEO, accompanied by Mrs. Joanitha Mrengo HR Director on the right.
CEO addressing Zantel staff during the event.
Flash mob dancers performing during the event. 
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images