Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live

INTRODUCING DULLY SYKES' NEW HIT SINGLE "DODOMA"


Matokeo ya mtihani wa Kitaifa wa Darasa la Saba 2015

0
0
Baraza la Mitihani Tanzania - NECTA limetangaza matokeo ya mitihani ya darasa la saba iliyofanyika September 9 na 10 mwaka huu ambapo mikoa ya kanda ya ziwa imefanya vizuri ikilinganishwa na mikoa mingine nchini. 
Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dk. Charles Msonde amesema jijini Dar es salaam kuwa  jumla ya watahiniwa 51,8034 kati ya 76,3602 wamefaulu sawa na asilimia 67.84, ambapo kati yao wasichana wamefaulu kwa asilimia 64.60 na wavulana asilimia 71.58 huku kiwango hicho cha kikiongezeka kwa asilimia 10.85 ukilinganisha na ufaulu wa mwaka jana wa asilimia 56.99. 
 Dk. Monde amezitaja shule zilizofanikiwa kuingia kumi bora kitaifa mwaka huu ni pamoja na shule ya Waja Springs ya Geita iliyoshika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Enyamai ya Mara na Twibhoki pia ya Mara katika nafasi ya tatu huku zikifuatiwa na shule nyingine 7 zote kutoka mikoa ya kanda ya ziwa. 
Shule ya Mwashigini ya mkoani shinyanga imetajwa kushika nafasi ya mwisho. 
 Katika hatua nyingine Dk. Msonde amezungumzia pia kukamilika kwa maandalizi ya mitihani ya kidato cha nne ambayo itafanyika kuanzia nov mbili hadi 27 mwaka huu na kuwataka wasimamizi pamoja na watahiniwa kujiepusha na vitendo vya udanganyifu ili kuepuka kufutiwa mitihani hiyo. Kwa kuwa mitihani hiyo inafanyika tanzania bara na visiwani Dk Msonde amewatoa hofu watahiniwa wa Zanzibar ambako kuna hofu ya uvunjifu wa amani kutokana na masuala ya kisiasa kuwa mitihani hiyo itaendelea kama kawaida kwani suala la ulinzi limeimarishwa. 
BOFYA jina la Mkoa kupata matokeo yake
ARUSHADAR ES SALAAMDODOMA
IRINGAKAGERAKIGOMA
KILIMANJAROLINDIMARA
MBEYAMOROGOROMTWARA
MWANZAPWANIRUKWA
RUVUMASHINYANGASINGIDA
TABORATANGAMANYARA
GEITAKATAVINJOMBE
SIMIYU

Introducing Samatwizzy's new Song "WARM UP"

Maadhimisho ya siku ya walimu wa Mkoa wa Manyara

0
0
Baadhi ya walimu wa Mkoa wa Manyara wakishikana mikono kwa lengo la kuonyesha umoja na mshikamano daima kwenye maadhimisho ya siku ya mwalimu ambapo kwa mkoa huo zilifanyika mji mdogo wa Mirerani.
Mwenyekiti wa chama cha walimu nchini (CWT) Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Abraham Kisimbi akizungumza kwenye sherehe za siku ya mwalimu ambapo kwa mkoa huo zilifanyika mji mdogo wa Mirerani.
Walimu wa Mkoa wa Manyara, wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Mahamoud Kambona wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya mwalimu ambayo kimkoa ilifanyika mji mdogo wa Mirerani.
Mwenyekiti wa chama cha walimu nchini (CWT) Mkoani Manyara, Qambos Sulle akizungumza kwenye sherehe za siku ya mwalimu ambapo kwa mkoa huo zilifanyika mji mdogo wa Mirerani.
Mwenyekiti wa chama cha walimu nchini (CWT) Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Abraham Kisimbi akizungumza kwenye sherehe za siku ya mwalimu ambapo kwa mkoa huo zilifanyika mji mdogo wa Mirerani.

Joto la asubuhi la 93.7 EFM Jumatatu Novemba 2, 2015 kuanzia saa 12 hadi saa tatu

MAALIM SEIF NA MKWAMO WA KISIASA ZANZIBAR

0
0
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na waandishin wa Habari katika ofisi za CUF Mtendeni kuhusiana na maendeleo ya “mkwamo” wa kisiasa Zanzibar. Picha na Salmin Said, OMKR

Na Hassan Hamad (OMKR)
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesema jitihada za kuutafutia ufumbuzi mkwamo wa kisiasa Zanzibar uliotokana na tamko la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Bw. Jecha Salim Jecha baada ya kutangaza kufuta uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba 2015, zinaendelea vizuri.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za CUF Mtendeni mjini Zanzibar, Maalim Seif ambaye pia ni mgombea Urais kupitia Chama hicho amesema ana matumaini kuwa suala hilo litapatiwa ufumbuzi wa haki unaoheshimu maamuzi ya wapiga wa Zanzibar waliyoyafanya tarehe 25 mwezi uliopita.
Amefahamisha kuwa jitihada hizo zimekuwa zikifanywa na taasisi mbali mbali za ndani na nje ya nchi zikiwemo Umoja wa Mataifa pamoja na nchi kadhaa ambazo ni marafiki wa Tanzania zikiwemo zilizoleta waangalizi wa kimataifa katika uchaguzi huo.
Amesema jitihada pia zimekuwa zikifanywa na viongozi wakuu wastaafu, viongozi wa dini na Msajili wa vyama vya siasa Tanzania Jaji Francis Mutungi.
Ameeleza kuwa Chama Cha Wananchi CUF kimetiwa moyo na imani kutokana na jitihada hizo, na kwamba ufumbuzi wa haki wa suala hilo utapatikana katika kipindi kifupi kijacho.
Maalim Seif ametumia firsa hiyo kuwataka Wazanzibari waendelee kubaki watulivu na kuitunza amani ya nchi, na kuwaaachia viongozi wao kulifanyia kazi suala hilo kwa kushirikiana na watu mashuhuri pamoja na Taasisi za kitaifa na kimataifa.
Amewaomba wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kufanya juhudi kuhakikisha Zanzibar inabaki katika hali ya amani na utulivu, na kutokubali kutumiwa na wanasiasa kufanikisha mbinu chafu ambazo zinaleta taharuki na hofu miongoni mwa raia.
Maalim Seif amewahakikishia viongozi na wanachama wa CCM na Wazanzibari wote kwamba iwapo atatangazwa mshindi wa uchaguzi huo hakutokuwa na ulipizaji wa kisasi, na kwamba atafanya kazi kwa ushirikiano chini ya muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa maslahi ya Zanzibar.

SIKU YA MARUHANI ("Halloween") DUNIANI

0
0
Na Swahilivilla blog.  Washington D.C
Jana ililkuwa ni "Siku ya Maruhani" nchini Marekani. Siku hii ijulikanayo kama "Halloween" husherehekewa kila tarehe 31 Oktoba, na ina historia ndefu.
Siku ya Maruhani ilianzia huko barani Ulaya kiasi miaka 2,000 iliyopita ikifungamana na imani za kishirikina. Wazungu walipoyavamia mabara ya Amerika walihamia pia na utamaduni mila, desturi, dini, na silka zao - na sema upendavyo. Miongoni mwa hayo ilikuwa ndiyo hii siku ya Maruhani ambayo jina lake la asili ni "Samhein".
Sherehe za Maruhani  Photograph by treasuredragon/iStock.

Tuyaachie ya historia kwa wanahistoria, lakini kwa ufupi hii iliaminika kuwa ni siku ambayo pepo, majini, maruhani, mazimwi na mizimu au mizuka ya watu waliokufa hurejea hapa duniani katika maeneo yao ya asili na kujichanganya na watu waliohai.
Maudhui kuu ya siku hii ni kutisha, kuadhibu na mauti, ingawaje katika enzi zetu za leo imekuwa ni siku kuu ya watoto zaidi kuliko watu wazima. Sherehe zake hufanyika kuanzia familia, mitaa, makazini na hadi kufikia Ikulu yenyewe. 

STATE HOUSE STATEMENT

0
0


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone:255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz              

Fax: 255-22-2113425



RESIDENT’S OFFICE,
      STATE HOUSE,
              1 BARACK OBAMA ROAD,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 


STATE HOUSE STATEMENT


The State House has learnt, with regret, claims by the Secretary General of the Civic United Front (CUF) and its Presidential candidate in this year’s General Elections in Zanzibar, Honorable Seif Shariff Hamad, that he has been ignored and his request for an appointment with President Jakaya Mrisho Kikwete, to discuss the political situation in Zanzibar, turned down.

The State House would like to categorically deny that it has received any request from Honorable Hamad for him to meet President Kikwete since voting day in Zanzibar on Sunday and subsequent nullification of the election process in Zanzibar by the Zanzibar Electoral Commission (ZEC) Chairman Jecha Salim Jecha on Tuesday.

What President Kikwete has received, are complaints by CUF about some actions from some sections of the Police Force in Zanzibar and a request for him to facilitate a conversation between Honorable Hamad and the Chief of the Armed Forces (CDF) General Davis Mwamunyange.

Subsequently, President Kikwete, who is also Commander-in–Chief, has instructed the Inspector-General of Police Ernest Mangu to investigate these claims by CUF and report back to him. Accordingly, he has also instructed his office to facilitate a conversation between General Mwamunyange and CUF officials. 

The State House would like to confirm that President Kikwete is as concerned about the political and security situation in Zanzibar as every Tanzanian is, and has been working tirelessly and consulting widely over the last few days to find amicable and peaceful resolution to the situation in Zanzibar.

While the matter remains firmly in the hands of an independent electoral body in Zanzibar, President Kikwete would like to express his readiness to do whatever is in his powers to regularize the situation in Zanzibar.


ISSUED BY THE DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

STATE HOUSE

DAR ES SALAAM.

1 NOVEMBER , 2015





Taarifa rasmi ya Serikali ya Zanzibar kuhusu vifungu vya sheria juu ya uhalali wa Rais kuendelea kuwepo madarakani

0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitoa taarifa rasmi ya Serikali kuhusu vifungu vya sheria   juu ya uhalali wa kuendelea kuwepo madarakani Rais wa Zanzibar.
Na Othman Khamis Ame, OMPR
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imewahakikishia Wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kwamba Rais aliyepo madarakani hivi sasa ataendelea kushika madaraka ya Urais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi mpaka pale utaratibu wa Kikatiba na Kisheria wa kumpata Rais utakapokamilika.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akitoa Taarifa ya Serikali akisisitiza Taarifa ya awali ya Serikali iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuhusiana na kauli za kupotosha zinazotolewa na baadhi ya Viongozi wa vyama vya Kisiasa kuhusu uhalali wa kuendelea kuwepo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliyopo madarakani pamoja na Serikali yake.
Balozi Seif aliwaomba Wananchi wazipuuze kauli za upotoshaji zinazotolewa zikiashira zaidi uvunjifu wa amani na kuwataka waendee kuwa watulivu na kudumisha amani iliyopo Nchini.
Alisema Kifungu cha 28 Mbili {a} cha Katiba ambacho kimekuwa kikitumika katika kutoa tafrisi potofu kwa Wananchi  kwamba Rais aliyopo madarakani atamaliza muda wake wa miaka mitano kuanzia Tarehe ambayo alipokula kiapo cha uaminifu na kiapo cha kuwa Rais.
Balozi Seif alieleza kwamba ni dhahiri kwamba dhamira ya kifungu hicho cha Katiba ilikuwa kuweka bayana kuwa kama uchaguzi Mkuu utafanyika na msindi wa kiti chja Urais atatangazwa rasmi na Tumen ys Uchaguzi, hivyo muda wake wa kuendelea Mtu kuwa Rais ungemalizika kwa kufuatana na masharti ya Kifungu hicho.
Alifafanua kwa kuwa Tume ya Uchaguzi haikumtangaza mshindi wa kiti cha nafasi ya Urais ni dhahiri masharti ya kifungu hicho hayataweza kusimama na hivyo masharti ya Kifungu cha 28 {1} {a} cha Katiba kitakuwa na nguvu za Kikatiba kumpa uwezo wa Rais aliyopo madarakani kuendelea na madaraka ya Urais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Alisema Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi anapatikana  kwa mujibu wa masharti ya Kifungu cha 27 cha Katiba ambacho Rais anachaguliwa kufuatana na Katiba Hiyo na kwa mujibu wa Sheria yoyote itakayotungwa na Baraza la Wawakilishi hukusu Uchaguzi wa Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Balozi Seif alifahamisha kuwa ili Rais wa Zanzibar apatikane kwa mujibu wa Katiba na sheria ya Uchaguzi nambari 11 ya Mwaka 1984, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar inapaswa kuendesha uchaguzi na hatimae kumtangaza mshindi wa nafasi ya Urais ambae atashika madaraka hayo pale ambapo atakuwa ameapishwa rasmi kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Katiba ya Zanzibar.
Alisema Kifungu cha 28 {1} {a} cha Katiba kinaweka utaratibu kuhusu muda wa kuendelea kuwa kuwa Rais, na kwamba kwa kufuatana na kifungu hicho, mtu aliyechaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ataendelea na dhamana hiyo mpaka pale ambapo Rais anayefuata ale kiapo cha kuwa Rais.
Alieleza kwamba kwa msingi huo wa Kikatiba ni vyema Wananchi wakafahamu na kuelewa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Braza la Mapinduzi ataendelea kuwepo madarakani mkapa pale Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar itakapomtangaza mshindi wa kiti cha Urais na Rais Mteule atashika madaraka hayo baada ya kuapishwa rasmi kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Katiba.

SIMU TV: UCHAMBUZI WA HABARI ZA MAGAZETINI

0
0

Gwajima ageuka nguzo ya chumvi, Polisi yasema serikali ya Zanzibar bado ipo yawataka  wananchi kuacha kusikiliza uvumi mitandaoni; https://youtu.be/B5RJMxqLmoM 
Azam FC yaua, yarudi kileleni. Pluijm aandaa utatu hatari Yanga.Kerr akingiwa kifua kila kona. Haya yote utayapata katika magazeti ya leo; https://youtu.be/IuJ4uNambBk 
Kippi amkomalia Mdee, Nyalandu asema tumeangusha mbuyu wa ujangili nchini. Pata habari za kina zilizotawala magazeti ya leo; https://youtu.be/8MuTBSao0jU

SHINDANO KUBWA LA KUSAKA VIPAJI VYA KUCHEZEA MPIRA 'FREESTYLE FOOTBALL CHAMPIONSHIP' KUANZA HIVI KARIBUNI

0
0
IMG_20151022_190217
Tanzania Freestyle football championship (TFFC2016) ambalo ni shindano la kutafuta/kusaka vipaji vya kuchezea mpira yaani freestyle soccer/Freestyle Football wengi hupenda kuita hivyo ambalo linatarajiwa kuendeshwa kama vile mashindano mengine ya kutafuta vipaji kwa njia mbalimbali ikiwemo ile ya TV show.
Waweza wasiliana nao kupitia anuani hapa +255 654 955 825/ +255 655 049 647
IMG_20151010_014924
IMG_20151010_022504

HAFLA YA JUMUIYA YA WANAFUNZI WA TANZANIA WUHAN-CHINA (WUTASA) KUWAKARIBISHA WANAFUNZI WAPYA MWAKA WA MASOMO 2015/16

0
0
1
Picha ya pamoja ya wanafunzi wapya na wazamani. Walioketi mbele kutoka kushoto ni viongozi wa Wutasa, Gelas Rubakula (Naibu Katibu), Ally Salum (Katibu), Rajab Jafar (Makamu Mwenyekiti), Abel Masanja (Mwenyekiti) na Thomas Mtaki (Mwenyekiti Mstaafu).
2
Picha ya pamoja ya wanafunzi wapya. Walioketi mbele kutoka kushoto ni viongozi wa Wutasa, Gelas Rubakula (Naibu Katibu), Ally Salum (Katibu), Rajab Jafar (Makamu Mwenyekiti), Abel Masanja (Mwenyekiti) na Thomas Mtaki (Mwenyekiti Mstaafu).
3
Mpiganaji wa Daily News na Mdau wa Blog hii, Abdulwakil Saiboko (kulia) ambaye pia ni mwanafunzi huko Wuhan akiwa kwenye pozi na mwanafunzi mwenzake, Dr Rama kwenye  hafla hiyo.

Vijana moro wachangamkia mradi wa Airtel Fursa wiki hii

0
0
Afisa Masoko wa kampuni ya simu mkoa wa Morogoro, Aminata Keita akizungumza jambo wakati wa mafunzo ya ujasiliamali ya airtel fursa kwa vijana yenye lengo la kuwapa elimu ya usajiliamali ili kujiendeleza kibiashara na kujikimu kiuchumu yakishirikisha vijana 250 wenye umri wa kuanzia 16 hadi 26 na kufanyika ukumbi wa Veta mkoani Morogoro.
Mkufunzi kutoka Veta kanda ya mashariki na kati, Marthin Mollel akitoa mafunzo ya ujasiliamali ya airtel fursa kwa vijana yenye lengo la kuwapa elimu ya usajiliamali ili kujiendeleza kibiashara na kujikimu kiuchumu yakishirikisha vijana 250 wenye umri wa kuanzia 16 hadi 26 na kufanyika ukumbi wa Veta mkoani Morogoro.
Baadhi ya vijana walioshiriki mafunzo ya ujasiliamali wakimsikiliza mkufunzi (hayupo pichani) wakati akitoa mafunzo ya ujasiliamali ya airtel fursa kwa vijana yenye lengo la kuwapa elimu ya usajiliamali ili kujiendeleza kibiashara na kujikimu kiuchumu yakishirikisha vijana 250 wenye umri wa kuanzia 16 hadi 26 na kufanyika ukumbi wa Veta mkoani Morogoro.

UWANJA WA KAITABA BUKOBA WAANZA KUWEKWA NYASI RASMI LEO.

0
0
Na Faustine Ruta, Bukoba.

Uwanja wa Kaitaba Bukoba Umeanza kuwekwa nyasi bandia rasmi leo hii jumatatu 2 Novemba, 2015 na kutokana na maelezo ya wawekaji wamesema utachukuwa muda wa siku 14 tu. 


Wakaazi wa Mji wa Bukoba na Vitongoji vyake sasa kuanza kushuhudia kipute live bila Chenga katika Uwanja huo wa Kaitaba. Timu ya Kagera Sugar nayo inatarajiwa kurudi katika Uwanja huo ambao uutumia kama Uwanja huo ambapo mpaka sasa tangu msimu uliopita wamekuwa wakitumia Viwanja vingine kwa michezo yao ya Nyumbani na Ugenini pia. 

Uwanja huu umejengwa kwa   ufadhili wa FIFA chini ya mpango wa misaada wa Goal Projects.

Uwekwaji Nyasi ukiendelea katika Uwanja wa Kaitaba leo hii.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

TWIGA YAENDELEA KUJIFUA KUWAVAA MALAWI

0
0
Timu ya Taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’ inayonolewa na kocha mkuu Rogasian Kaijage imendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Timu ya Taifa ya Wanawake ya Malawi utakaochezwa Novemba 07, mwaka huu jijini Dar es salaam katika uwanja wa Azam Chamazi.

Twiga Stars iliingia kambini Oktoba 29, katika hosteli za Shirikisho zilizopo Karume, ina kikosi cha wachezaji 22 wanaofanya mazoezi asubuhi na jioni katika uwanja wa Karume.

Mchezo dhidi ya Malawi ni mchezo wa kirafiki wa kimataifa, ambao kocha Kaijage atautumia kuangalia maendeleo ya wachezaji wake kwa ajili ya maandalizi ya micheo ya kimataifa.

Wachezaji waliopo kambini ni Asha Rashid, Estha Chaburuma, Fatuma Bushiri, Fatuma Omari, Mwajuma Abdallah, Mwanahamis Omar, Fatuma Khatibu, Amina Ally, Fatuma Issa, Belina Julius, Happines Hezron na Donizia Daniel.

Wengine ni Maimuma Hamisi, Stumai Abdallah, Anna Hebron, Anastazia Anthony, Shelder Boniface, Wema Richard, Tumaini Michael, Jane Cloudy, Saada Ramadhani na Sofia Mwasikili.

WAKAGUZI WATAKIWA KUZINGATIA WELEDI

0
0
Mkurugenzi wa msaidizi (Mafunzo) Bibi Felister Tirutangwa akizungumza wakati wa mafunzo ya program ya TEAMMATE kwa ajili ya wakaguzi kutoka NAOT na Wizara ya Fedha. Mafunzo hayo yanafanyika mkoani Morogoro kuanzia tarehe 02 hadi 06 Novemba, 2015.
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) na Wizara ya Fedha wakifuatilia kwa umakini mafunzo  ya program ya TEAMMATE. Mafunzo hayo yanafanyika mkoani Morogoro kuanzia tarehe 02 hadi 06 Novemba, 2015.
Mgeni rasmi wa mafunzo ya program ya TEAMMATE kwa ajili ya wakaguzi kutoka NAOT na Wizara ya Fedha, Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bibi Wendy Massoy akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wanaohudhuria mafunzo hayo.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WAKUTANA

0
0
Msajili wa vyama vya siasa nchini,Jaji Mstaafu ,Francis Mtungi akiarisha mkutano wa vyama vya siasa ulioandaliwa kwa ajili ya kumuaga Rais Dk.Jakaya Kikkwete leo jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa Mgombea Urais wa TLP,Maxmillian Lymo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Phillip Mangula( Kushoto) akizungumza na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Labour Patry (TLP), Agustino Lyatonga Mrema  (kulia ) na katikati Mgombea Urais, Maxmillian Lymo  jijini Dar es Salaam.

                                             KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

UCHAMBUZI WA HABARI TOKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI NOVEMBA 2,2015

0
0
Huu ni uchambuzi wa Habari toka vituo mbalimbali vya Televisheni Mchana Huu November 2, 2015.

Chama cha mapinduzi mkoani Lindi kimewataka watanzania kuungana pamoja katika kujenga nchi ili kusaidia utekelezaji wa Dkt. Magufuli.
Hali ya kisiasa Visiwani Zanzibar inaendelea shwari huku wananchi wakiendelea na shughuli zao za kila siku kama ilivyo kawaida. https://youtu.be/WcX-Npbsmbg

Mitihani ya kidato cha nne imeanza kufanyika leo nchini kote ambapo watahiniwa 448, 358 wamesajiliwa kufanya mitihani hiyo. https://youtu.be/j79mEH18jcI
Raisi wa Misri Abdelk Fatah El Sisi atoa wito kwa watu kusubiri matokeo ya uchunguzi wa kubaini sababu ya kuanguka kwa ndege Ya Urusi. https://youtu.be/0KAV7il8mbA
Baadhi wa wanasiasa walioshindwa uchaguzi mwaka huu watakiwa kuwa na busara au kutumia njia ya amani ili kudai haki zao https://youtu.be/hztuHb6k9gY

Watanzania wametakiwa kuacha uvivu wa fikra na badala yake wajishughulishe kama wanataka maendeleo ya nchi yao https://youtu.be/zwzl7mk2-ug
Polisi  jamii mkoani mwanza imetajwa kuwa chachu ya amani na utulivu katika kipindi cha uchaguzi mkuu wa Tanzania; https://youtu.be/hZZe53utKOM
CCM Iringa yawataka wanachama wake kuwa watulivu hasa wale majimbo yao yaliyokuwa na dosari katika kipindi cha uchaguzi; https://youtu.be/uFtW2RiwDlQ
Mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo jijini mwanza yasababisha ndege kutofanya safari zake  kwa mda kutokana na maji kujaa; https://youtu.be/k37x2D6UKBE


WATAALAM WA TAKWIMU KUTOKA OFISI ZA TAKWIMU BARANI AFRIKA

0
0
Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Afrika Kusini Risenga Maluleke akizungumza leo na waandishi wa habari kuhusu madhumuni ya mkutano wa watalaam wa takwimu kutoka nchi mbalimbali barani Afrika ambapo wamekutana kujadili Mfumo wa Uongozi Bora katika Ofisi za Takwimu pamoja na Uboreshaji wa Mitaala ya Ufundishaji wa Masomo ya Takwimu. Mkutano huo ni wa siku tano na unafanyika katika hoteli ya Golden Tulip iliyopo Jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumza leo na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa siku tano ambao umekutanisha watalaam wa takwimu kutoka nchi mbalimbali barani Afrika kujadili Mfumo wa Uongozi Bora katika Ofisi za Takwimu pamoja na Uboreshaji wa Mitaala ya Ufundishaji wa Masomo ya Takwimu. Mkutano huo unafanyika katika hoteli ya Golden Tulip iliyopo Jijini Dar es Salaam. 
 Baadhi ya wakuu wa Ofisi za Takwimu kutoka barani Afrika wakifuatilia kwa makini majadiliano wakati wa mkutano wa kujadili Mfumo wa Uongozi Bora katika Ofisi za Takwimu pamoja na Uboreshaji wa Mitaala ya Ufundishaji wa Masomo ya Takwimu. Mkutano huo ni wa siku tano na unafanyika katika hoteli ya Golden Tulip iliyopo Jijini Dar es Salaam.
 (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO)

VIONGOZI wa Ofisi za Takwimu barani Afrika leo wamekutana kujadili Mfumo wa Uongozi Bora katika Ofisi hizo pamoja na Uboreshaji wa Mitaala ya Ufundishaji wa Masomo ya Takwimu katika nchi za Afrika.

Wakizungumza katika mkutano wa wataalam wa takwimu ulioanza leo Jijini Dar es Salaam, viongozi hao wamesema ili takwimu bora zipatikane kwa wakati, ni lazima kuwepo na mfumo bora wa uongozi pamoja na wataalamu waliobobea katika fani ya takwimu.

HANDENI MJINI KURUDIA KURA ZA MAONI KESHO

0
0
 Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Sekretarieti, Makao Makuu ya CCM Ofisi Ndogo Lumumba.


Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM iliyokutana leo, Novemba 02,2015 chini ya Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete imejadili kwa kina mapendekezo ya wana CCM walioomba ridhaa ya kugombea ubunge katika jimbo la Handeni mjini.


 Kamati Kuu imetengua mapendekezo ya awali na kuagiza kurejewa kwa mchakato wa kura za maoni kwa wana -CCM wawili walioongoza kura za maoni za awali.


Wana- CCM hao watakaopigiwa kura za maoni tena kesho Novemba 03,2015 ni pamoja na Omari Abdallah Kigoda na Hamis Hamad Mnondwa.


Aidha Kamati Kuu imeteua wajumbe watatu kusimamia zoezi hilo ambao ni Dk. Maua Daftari, Dk.Emmanuel Nchimbi na Alhaji Abdallah Bulembo.

Viewing all 109570 articles
Browse latest View live




Latest Images