Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1014 | 1015 | (Page 1016) | 1017 | 1018 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Balozi Dora Msechu  amekutana na watanzania wanaoishi kwenye Jimbo la Fyn nchini Denmark na kuwapongeza kwa kutimiza miaka 10 ya Umoja wao. na kuwashukuru kwa mchango mkubwa wanaotoa kwenye maendeleo ya nchi yetu. Amewaasa waendeleze mshikamano wao na kuwahakikishia kuwa  milango ya Ubalozi ipo wazi katika kuwahudumia na kushirikiana kwa  karibu na watanzania wote wanaoishi kwenye nchi za Nordic na Baltic.
  Sherehe hiyo iliandaliwa na Jumuiya ya Watanzania Jimbo la Fyn kwa kushirikiana na familia ya Bibi Dorthe Nielsen, rafiki mkubwa wa Tanzania na mtoto wa aliyekuwa Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Denmark, marehemu Robert Andersson.

  0 0

  Logo ya Zadia
  Jumuiya ya Wazanzibari Waishio Nchini Marekani (ZADIA), imekuwa ikifuatilia kwa karibu na makini zaidi zoezi zima la Uchaguzi Mkuu visiwani Zanzibar na Tanzania kwa ujumla. Kwa kiasi kikubwa mchakato wa uchaguzi ulifanyika kwa njia za amani na utulivu. Hata hivyo ZADIA imeshtushwa mno na tamko la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Mh. Jecha Salim Jecha la kutangaza kuufuta Uchaguzi Mkuu Zanzibar na matokeo yake.

  Ama kwa hakika kitendo hicho hakikuwa cha busara na kinapelekea kurudisha nyuma maendeleao ya demokrasia Zanzibar, na vilevile hakiashirii mustakbali mwema kwa nchi yetu tuipendayo. Wazanzibari wameelezea maoni na matakwa yao kwenye visanduku vya kupigia kura, na maoni na matakwa yao hayo yanapaswa kusikilizwa na kuheshimiwa.

  Kwa hivyo, ZADIA inatoa wito kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar, kumalizia mchakato mzima wa kuhesabu kura kwa majimbo yaliyobakia na kutoa matokeo ya mwisho ya Uchaguzi na kumtangaza mshindi ili kuiepusha Zanzibar yetu tuipendayo kuingia katika hali ya mtafaruku na mifarakano isiyokuwa na tija bali kuleta hasara.

  ZADIA pia inaungana na jumuiya zote za kimataifa ambazo zimetoa msimamo wao juu ya uchaguzi wa Zanzibar, hasa ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, ambao ni kiungo madhubuti kati ya Wazanzibari walioko Zanzibar na wenzao wanaoishi nchini Marekani.

  Aidha, tunapenda kumkumbusha Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dakta Ali Mohammed Shein kuwa Wazanzibari walimpa amana kubwa ya kuwaongoza, na kwa hivyo ni wajibu wake kuienzi amana hiyo kwa kuchukuwa hatua za kiungwana za kuitoa Zanzibar kwenye mgando huu wa kisiasa. Hali hii iliyopo sasa inaleta wasiwasi miongoni mwa raia na imekua ikiathiri maisha yao ya kila siku, na ikiachwa kuendelea huenda ikaathiri pia mustakbali maisha yao kwa jumla.

  ZADIA pia inamtolea wito Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kutumia mamlaka yake aliyonayo kuhakikisha Zanzibar inatoka kwenye mkwamo huu wa kisiasa na kwamba anaondoka madarakani akiiacha Zanzibar ikiwa katika hali ya amani na utulivu. Kwa kufanya hivyo atauthibitishia ulimwengu kuwa kweli Tanzania ni kisima cha amani.

  Na mwisho tunawaomba Wazanzibari, wapenzi wa Zanzibar, na Watanzania wote kwa ujumla popote pale walipo, wajitahidi kufanya mawasiliano na Jumuiya nyengine za Kimataifa ili ziingilie kati suala hili kabla nchi yetu haijaingia kwenye mtafaruku mkubwa wa kisiasa na kijamii na hata kupelekea kuhatarisha amani ya nchi yetu.
  Mungu Ibariki, Zanzibar.

  0 0
 • 10/31/15--00:51: MAPITIO YA MAGAZETI LEO
 • Wasomi wamchambua Dr. John Magufuli undani wa habari hii inapatikana katika magazeti ya leo  Octoba.31.2015; https://youtu.be/DrYYX3PzFiY 

  Simba yaitega Azam, Mbeya City wamefanya kweli. Ndivyo gazeti  la Mwanaspoti linavyojinadi katika kurasa zake siku ya leo; https://youtu.be/ljShGJxMUo0

  Magufuli awapasha wanafiki,  Vijana wa UKAWA waachiwa kwa dhamana, Tume ya uchaguzi yamaliza kazi rasmi. Pitia dondoo za magazeti; https://youtu.be/iZRIy7ugwsI

  35 waliochoma maboksi ya kura Mbagala Kortini. Pata habari za kina zilizopewa kipaumbele katika magazeti hapa Simu.tv; https://youtu.be/GX8dtQr8QNQ

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri Mkuu wa India Dr. Narendra Moodi walipokutana kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Stadium Indiragandi mjini New Delhi India jana, wakati Makamu wa Rais alipohudhuria na kuhutubia mkutano wa tatu wa mahusiano ya India na Afrika kwa Wakuu wa Nchi hizo uliolenga na kujadili suala la kuendeleza fursa za kimahusiano katika Nyanja za Biashara, Sayansi, Teknolojia, Afya na Kilimo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri Mkuu wa India Dr. Narendra Moodi walipokutana kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Stadium Indiragandi mjini New Delhi India jana, wakati Makamu wa Rais alipohudhuria na kuhutubia mkutano wa tatu wa mahusiano ya India na Afrika kwa Wakuu wa Nchi hizo uliolenga na kujadili suala la kuendeleza fursa za kimahusiano katika Nyanja za Biashara, Sayansi, Teknolojia, Afya na Kilimo. (Picha na OMR)

  0 0

  Ujumbe wa maafisa wanane kutoka Tanzania ulioko nchini Malawi kwa ziara ya kimafunzo umemtembelea Mhe. Victoria R. Mwakasege, Balozi wa Tanzania nchini Malawi, ofisini kwake mjini Lilongwe. 

  Ujumbe huo wenye maafisa kutoka taasisi mbalimbali za Serikali ikiwemo Ofisi ya Rais –Utumishi, Ofisi ya Waziri Mkuu -Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Wizara ya Fedha, Clinton Health Access Initiative (CHAI), na Mpango wa Taifa wa Kuthibiti UKIMWI (National Aids Control Programme - NACP), uko nchini Malawi kujifunza namna ambavyo Serikali ya Malawi inachukua hatua mbalimbali kuboresha huduma za afya katika jamii kwa kutumia wahudumu wa kujitolea (Health Surveillance assistants). 

  Mpango huo unatumika katika nchi mbalimbali zikiwemo Malawi, Tanzania, Ghana, Ethiopia na Rwanda kwa lengo la kuboresha huduma za afya na hatimaye kupunguza vifo vya akina mama na watoto katika jamii.
  Mhe. Balozi Victoria R. Mwakasege wa sita kutoka kushoto akiwa na ujumbe wa maafisa kutoka Serikali ya Tanzania walipofika ofisini kwake tarehe 29 Oktoba, 2015 kumtembelea. Kushoto ni Afisa Ubalozi Bw. Wilbroad A. Kayombo
  Mhe. Balozi Victoria R. Mwakasege wa sita kutoka kushoto akiwa na ujumbe wa maafisa kutoka Serikali ya Tanzania walipofika ofisini kwake tarehe 29 Oktoba, 2015 kumtembelea. Kushoto ni Afisa Ubalozi Bw. Wilbroad A. Kayombo  0 0


  0 0

  Juma Pinto Mwenyekiti TASWA
  CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA), kinatoa pongezi za dhati kwa Dk. John Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano ya Tanzania. 
  TASWA imepokea kwa furaha ushindi huo wa Dk. Magufuli, ikiamini atawapa furaha wanamichezo katika masuala mbalimbali kama alivyofanya mtangulizi wake Rais, Jakaya Kikwete ambaye anamaliza muda wake wa kuwatumikia Watanzania kwa mujibu wa katiba na ataanzia pale mtangulizi wake alipoishia kuhusiana na michezo kwa ujumla. 
  Kutokana na hali hiyo tunampongeza Rais Mteule Dk. Magufuli na Makamu wake, Samia Suluhu Hassan, ambaye atakuwa mwanamke wa kwanza Tanzania kushika wadhifa wa Makamu wa Rais hapa nchini. 
  Tunaamini watakuwa tumaini kubwa la wanamichezo na tunaahidi kuwapa ushirikiano wa kutosha ili watekeleze majukumu yao ipasavyo upande wa michezo. 
  Pia TASWA inawapongeza wadau wote wa michezo waliochaguliwa kwa nafasi mbalimbali za Ubunge na Udiwani na tunaamini ushindi wao utakuwa mwanzo mzuri katika kusaidia michezo hapa nchini. 
  Tunawapongeza pia wale ambao si wanamichezo, lakini walitumia mgongo wa michezo na wanamichezo kutafuta uongozi wa kisiasa katika nafasi za Ubunge na Udiwani, wakiahidi watasaidia michezo. Nao tunawapongeza na tunasubiri utekelezaji wa ahadi zao. 
  Wanasiasa ndiyo wanaounda Serikali, tena wao ndio wanaofanya uamuzi kutokana na nafasi zao. Watendaji ni wataalamu, na kazi yao ni kushauri au kutoa ushauri. Ushauri ni kitu kimoja, na ushauri kufanyiwa kazi ni kitu kingine pia. 
  Hivyo basi tunaamini wanasiasa walioingia wakitokea kwenye michezo wanajua matatizo yaliyoko huko kwa kiasi kikubwa kuliko mwingine yeyote, hivyo wanaweza kusaidia kwa kiasi fulani mawazo ili michezo ipige hatua.
  Ahsanteni,
   Juma Pinto
  Mwenyekiti TASWA
  30/10/2015

  0 0

  Mshambuliaji wa Simba, Peter, Mwalyanzi akiwatoba wachezaji wa Majimaji ya Songea katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam ambapo Simba iliibuka na ushindi wa bao 6-1. (Picha na Francis Dande)
  Wachezaji wa Simba, Hamis Kiiza na Irahim Hajibu wakishangilia kwa pamoja moja ya bao lililofungwa na Hajibu.
  Ibrahim Hajibu wa Simba akiifungia timu yake bao la kichwa.
  Wachezji wa Majimaji ya Songea baada ya kufungwa.
  Hamis Kiiza akimiliki mpira.

  0 0


  Serikali imezindua bodi ya usimamizi wa miundombinu ya reli nchini yenye wajumbe 8 itakayo jihusisha na usimamizi na uangalizi wa miundombinu.https://youtu.be/EYQxEBqN5ao

  Wakazi wa Moshi mkoani Kilimanajaro wamtaka raisi mteule kutekeleza ahadi zake alizoaahidi kipindi cha kampeni. https://youtu.be/PJajLOlGUAY
  Umoja wa vijana wa CCM (UVCCM) waitaka serikali ya Zanzibar kuunda tume huru ya uchunguzi wa zabuni za upatikanaji wa zabuni za vifaa vya uchaguzi.https://youtu.be/CSh7KkatLwA

  Wananchi wilayani Meatu watakiwa kuweka tofauti zao pembeni na badala yake washirikiane katika kuijenga Tanzania kwa uchaguzi umekwisha.https://youtu.be/L74yNDjcVzE

  Tanzania yaelezwa kuendelea kukumbwa na tatizo la watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi huku mikoa kadhaa ikiongoza. https://youtu.be/JXgsweRmvt4

  0 0

  CCM Zanzibar yaiijia juu ZEC, Matokeo darasa la 7, CCM Zanzibar yajiandaa na marudio ya uchaguzi.Tazama uchambuzi wa magazeti. https://youtu.be/6R-bt6q2Jd0

  UVCCM yataka uchunguzi zabuni za uchaguzi Zanzibar,Ufaulu darasa la 7,pata habari hizi na nyingine nyingi kupitia uchambuzi wa magazeti. https://youtu.be/dRdEfw8FHh4

  0 0

   Mtu mmoja amenusurika kifo kufuatia ajali ya gari alilokuwa anaendesha mchana huu kwenye milango ya saa 8.10. katika kijiji cha Kibele, Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja kwa kile kilichoelezwa kuwa ni mwendo kasi wa dereva huyo ambaye alishindwa kuidhibiti gari ndogo aina ya Toyota Spacio yenye namba za usajili Z 511 FG na gari  kuacha barabara na kugonga mnazi ambao uliangukia gari na baadae gari kuwaka moto. 
  Dereva huyo, ambaye jina halikuweza kupatikana mara moja, alitolewa ndani ya gari akiwa amebanwa na air bags zilizofyatuka na kuokoa uhai wake. 
  Alipata majeraha madogo ya kuchubuka kwenye mikono yake iliyokuwa inavuja damu. (kutokana na  maadili ya taaluma ya habari sikuwaletea picha ya dereva ambaye alikuwa peke yake ndani ya gari hiyo ila gari ni kama inavyoonekana kwenye hizo picha. Picjha na mdau Hassan S.
   Sehemu ya nyuma
   Sehemu ya ubavuni
  Sehemu ya mbele

  0 0
 • 11/01/15--05:02: IN LOVING MEMORY
 • THE LATE THERESIA RUTAHAKANA 

  Today is exactly 3 years from the time when you left us.
  Remembering you is easy as we do it every day. 
  But always there is an ache in our hearts.

  0 0


  Mtoto Careen Modest Kassuw pichani, ana umri wa mwaka mmoja, amezaliwa ana tatizo la Moyo ukiwa na matundu mawili na valvu zake nyembamba  zimebana kiasi  hivyo analazimika kusafirishwa kwenda India kwa matibabu.

  Wazazi wa mtoto huyo wanaomba msaada wako wewe Mtanzania kwa atakayeguswa ili wafanikishe gharama za matibabu ya mtoto Careen ambayo ni Shilingi Milioni 30 zinahitajika ili kuokoa maisha yake.
  Ewe Mtanzania, ewe mzazi tunaomba mchango wako wa hali na mali, kwa atakayeguswa tunaomba utume mchango wako kwa mama mzazi wa mtoto huyo Eunice kwa namba0713 034866 au kwa namba 0715 083055
  Mungu awabariki wote mtakaochangia kwa njia moja au nyingine.

  0 0

  On-going Construction work
  on 1st phase of the airport
  BAM International has received the instruction to proceed with phase 2 of the design and construct contract of the new Terminal 3 of Julius Nyerere International Airport in Dar es Salaam, Tanzania, by Tanzania Airports Authority. The contract value of phase 2 is over €100 million. The contract value of phase 1, awarded to BAM in 2013, was more than €130 million.

  The new terminal is designed for the anticipated growth of international air traffic, leaving the existing international Terminal 2 to cater for domestic flights. Phase 1 of the scope of work comprises the construction of the main terminal building – facilitating 3.5 million annual passengers – including parking lots, access roads, platforms and a taxiway. 
   This second phase will provide further capacity to facilitate six million annual passengers and includes a total terminal building area of approximately 60,000 m2.
  Artist impression of the airport after completion.

  0 0

  Mke wa Mbunge Mteule Bi Sarah Abdallah akitoa shukrani kwa wananchi wa kata ya Choma kwa kazi nzuri waliyoifanya.
   Mbunge mteule katika Jimbo la Manonga wilaya ya Igunga mkoani Tabora , Seif Khamis Gulamali (CCM) akiwapungia mkono pamoja na kuwashukuru wananchi wa kata ya Mwashiku kwa kuonesha upendo wa dhati baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo ilo
  Hakika ilikuwa ni siku ya furaha kwa wakazi wa jimbo la Manonga.

  0 0


  0 0

   Mshambuliaji wa Azam FC, Didier Kavumbagu akitafuta mbinu za kumtoka veki wa Toto African,  Hamis Seleman katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Francis Dande)

  Beki wa Toto African, Salum Chuku (katikati) akichuana na mshambuliaji wa Azam FC, Didier Kavumbagu (wa pili kushoto) wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam jana. Azam ilishinda 5-0. 
   Kipre Tchetche akimiliki mpira huku beki wa Toto African akijaribu kumzuia.
  Wachezaji wa Azam FC wakishangilia baada ya kupata bao.

  0 0


  0 0


  0 0

older | 1 | .... | 1014 | 1015 | (Page 1016) | 1017 | 1018 | .... | 3283 | newer