Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1013 | 1014 | (Page 1015) | 1016 | 1017 | .... | 3284 | newer

  0 0  0 0

  Wakati wananchi tukiendelea kufuatilia matokeo ya uchaguzi mkuu wa kuchagua viongozi wa awamu ya tano, ni vema basi kujikumbusha yale ambayo yaliyofanyika katika serikali ya awamu ya nne ya Rais anayemaliza muda Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mtoto wa Msoga.
  Kwa kupitia njia ya muziki bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU-Ughaibuni chini ya uongozi wake mtunzi gwiji kamanda Ras Makunja wameshusha nyimbo mbili za kumuaga Rais Jakaya Kikwete na kuyaimba baadhi ya aliyoyafanya katika awamu ya Nne.
  Pata burudani kwa kusikiliza nyimbo hizi at:


  0 0


  0 0

  Huu ni uchambuzi wa Habari toka vituo mbalimbali vya Televisheni Asubuhi Hii Oktoba 29, 2015.

  SIMUtv: Mwenyekiti wa ZEC Jecha Sakim Jecha jana ametangaza kufuta Matokeo ya Uchaguzi visiwani Zanzibar kutokana na kasoro Lukuki. https://youtu.be/2YWBj1NboRA
  SIMUtv: Chama Cha Mapinduzi CCM kimekusudia kwenda mahakamani  kupinga matokeo ya uchaguzi ya majimbo 4 ya Ndanda, Iringa mjini, kawe na Mikumi. https://youtu.be/WPEDVwm7ckE
  SIMUtv: Baadhi ya wachambuzi wa Masuala ya kisiasa wamesema ufutaji wa Matokeo Zanzibar utatoa fursa kwa Wananchi kuendelea na Majukumu yao. https://youtu.be/-H8umF9i3SI
  SIMUtv: Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC leo inatarajia kukamilisha kutangaza matokeo ya kura za Uraisi wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania. https://youtu.be/XbfizVTZFvA

  SIMUtv: Kutana na mchambuzi wa maswala ya siasa akielezea mwenendo wa uchaguzi  mkuu uliofanyika hivi karibuni;https://youtu.be/Krbe5eu87VA
  SIMUtv: Fuatilia namna wataalam wa siasa wakichambua muenendo wa siasa na wanasiasa katika mjadala wa leo hapa Simu.tv; https://youtu.be/_NqzuwTv1cc

  SIMUtv: Je waangalizi wa uchaguzi mkuu kutoka nje na ndani ya nchi wana mchango gani katika uchaguzi mkuu? Fuatilia mjadala hapa. https://youtu.be/y0oGcVZzs2k
  SIMUtv: Wananchi wamekuwa na maoni tofauti tofauti juu ya kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar na tume ya uchaguzi ZEC; https://youtu.be/avllJRMlUAk

  SIMUtv: Shirikisho la mpira wa miguu duniani(FIFA) limetaja majina saba watakaowania kiti cha uraisi, afrika wakijitokeza wawili; https://youtu.be/Hws7xP8abuI

  SIMUtv: Ligi kuu Tanzania bara, Yanga ya banwa mbavu, Toto African yaibuka kidedea katika uwanja wake wa nyumbani;  https://youtu.be/gsbqcekHgbk  0 0

  Waziri Mkuu wa zamani Kenya Raila Odinga amempongeza Dkt. John Pombe Joseph Magufuli baada yake kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa Urais Tanzania.
  Akiongea katika mahojiano na BBC, Mhe Odinga amemshauri mgombea wa upinzani Mhe. Edward Lowassa Kuwa Kama Hajakubaliana na Matokeo basi Aende Mahakama kushtaki Kama yeye Alivyofanya wakati akigombea Urais Kenya na kushindwa na Rais Uhuru Kenyatta.
  Ameeleza pia matumaini yake kwamba Dkt. Magufuli atahakikisha kuendelea kwa uhusiano mzuri uliopo katia ya Tanzania na Kenya, na kuimarisha Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuendeleza ndoto ya kuelekea kwenye Shirikisho la nchi hizo.

  0 0


  0 0


   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza kwa furaha mshindi wa kinyang'anyiro cha Urais kwa tiketi ya CCM na Rais Mteule Dkt John Pombe Joseph Magufuli wakifurahia matokeo mara baada ya Mwenyekiti wa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva  kutangaza kutangaza rasmi matokeo ya uchaguzi mkuu Ikulu jijini Dar es salaam ambako walifuatilia kwa pamoja matangazo hayo ya moja kwa moja kupitia vituo vya televisheni jioni hii Oktoba 29, 2015

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza kwa furaha mshindi wa kinyang'anyiro cha Urais kwa tiketi ya CCM na Rais Mteule Dkt John Pombe Joseph Magufuli mara baada ya Mwenyekiti wa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva  kutangaza kutangaza rasmi matokeo ya uchaguzi mkuu Ikulu jijini Dar es salaam ambako walifuatilia kwa pamoja matangazo hayo ya moja kwa moja kupitia vituo vya televisheni jioni hii Oktoba 29, 2015

  0 0
 • 10/30/15--01:18: TANZIA

 • Familia ya Bw. Abbas Elias Machimu wa Vijibweni Dar Es Salaam, wanasikitika kutangaza kifo cha baba yao mpendwa Mzee Abbas Elias Machimu (Pichani)kilichotokea siku ya Jumatano tarehe 28/10/2015. Maziko yatafanyika Ijumaa tarehe 30/10/2015 huko Kisiwani Vijibweni. Habari kwa ndugu, jamaa na marafiki popote walipo. Bwana alitoa, bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.
   Amina.

  0 0
 • 10/30/15--01:20: MAPITIO YA MAGAZETINI LEO

 • Ni Magufuli atangazwa rais awamu ya 5.Pata habari motomoto za kisiasa katika magazeti ya leo Octoba 30.2015;  https://youtu.be/8ZvvzkBbuz4


  Utulivu warejea kisiwani Zanzibar.Waangalizi walia na ZEC wataka matokeo yatangazwe.Haki za binadamu wataka kuisaidia ZEC; https://youtu.be/BI16XOK4tAg


  Lowasa apinga urais wa Dr.Magufuli, viongozi wa dini wamshauri Lowasa na UKAWA. Ndivyo magazeti yanavyoandika siku ya leo;  https://youtu.be/WLjkpl61hHc


  Dr.Magufuli atinga ikulu. Watanzania wampa zawadi ya urais siku yake yakuzaliwa.Pitia dondoo za magazeti;  https://youtu.be/ApwuMAGHEho


  Pata habari kemukemu za kina zilizopewa kipaumbele na wahariri wa magazeti mbalimbali hapa nchini; HTTPS://YOUTU.BE/NSVTVP3C8YC

  0 0

  TAWI LA CCM CHINA TUNAKUPONGEZA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI KWA KUCHAGULIWA KWA KURA NYINGI KUWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WA AWAMU YA TANO.TUNAKUTAKIA AFYA NJEMA NA MAFANIKIO KATIKA KIPINDI CHA UONGOZI WA JUU WA NCHI YETU.

  0 0

  The Secretary-General congratulates the people, Government and political parties of Tanzania for the peaceful and orderly manner in which the country held its elections on 25 October 2015. 

  The responsible conduct of the citizens of Tanzania as they cast their ballots and awaited the results was a concrete manifestation of their commitment to democracy, peace and stability. 

  The Secretary-General remains concerned about the situation in Zanzibar and underscores that any disputes related to the electoral process should be addressed through the existing legal framework in a peaceful and transparent manner. 

  The Secretary-General calls on all stakeholders to remain calm, reject the use of violence, and avoid making statements that could further increase tensions. 

  New York, 29 October 2015

  0 0

  Na: Hassan Hamad, OMKR.

  Msajili wa vyama vya siasa Tanzania Jaji Francis Mutungi, amesema kuna umuhimu kwa viongozi wa vyama vya siasa Zanzibar kukutana, ili kutatua mzozo wa kisiasa uliojitokeza.

  Amesema Zanzibar ni nchi amani, hivyo hakuna haja ya kuruhusu migogoro ya aina hiyo ambayo inaweza kupelekea kuvurugika kwa amani na kuipotezea sifa Zanzibar katika jamii ya Kimataifa.

  Jaji Mutungi akiambatana na baadhi ya wajumbe wa ofisi hiyo ya msajili pamoja na msajili wa vyama kwa upande wa Zanzibar Bw. Rajab Baraka, ametoa ushauri huo wakati akizungumza na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, nyumbani kwake Mbweni, nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

  Amesema kuna kila sababu ya kulinusuru taifa kuingia katika migogoro isiyokuwa ya lazima, na kutaka juhudi za makusudi zichukuliwe ili kumaliza tatizo hilo.

  Kwa upande wake Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad ambaye pia ni mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CUF, amesema amekuwa akichukua juhudi binafsi kukutana na wagombea wenzake kuzungumzia tatizo hilo, lakini baadhi yao wanaonekana kutokuwa tayari kulizungumza.

  Amesema hapendi kuona Zanzibar inaingia katika machafuko yanayoweza kuepukwa, na kwamba viongozi wengine pia wanapaswa kufikiria amani na maslahi ya Zanzibar kuliko maslahi binafsi.

  Katika hatua nyengine Maalim Seif amemshutumu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Bw. Jecha Salim Jecha kwa kuiingiza nchi katika migogoro ya kisiasa na kikatiba.

  Akinukuu vipengele vya Katiba ya Zanzibar, Maalim Seif amesema kipindi cha Urais wa Zanzibar ni miaka mitano kuanzia tarehe ya kuapishwa, hivyo kuanzia tarehe 02/11/2015 kipindi cha Urais wa Zanzibar awamu ya saba kitakuwa kimemalizika. 

  Hivyo amesema bila ya kuchukuliwa juhudi za dharura, kuanzia tarehe 02 mwezi ujao kwa mujibu wa katiba, Zanzibar itakuwa haina Rais, Serikali wala Baraza la Wawakilishi.
  Msajili wa vyama vya siasa Tanzania Jaji Francis Mutungi, akizungumza na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, nyumbani kwake Mbweni Zanzibar.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika picha ya pamoja na Msajili wa vyama vya siasa Tanzania Jaji Francis Mutungi (wa pili kushoto) na baadhi ya wajumbe wa Ofisi hiyo. Kushoto ni msajili wa vyama Zanzibar Bw. Rajab Baraka. (Picha na Salmin Said, OMKR)

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
   WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

  JESHI LA POLISI TANZANIA.

         TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

     “PRESS RELEASE” OKTOBA  30,2015.


  ·         WATU WATATU WANAODHANIWA KUWA MAJAMBAZI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA.  ·         WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUMILIKI SILAHA KINYUME CHA SHERIA.

  KATIKA TUKIO LA KWANZA:

  WATU WATATU WANAODHANIWA KUWA NI MAJAMBAZI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. KEFA ISRAEL MDEKWA (40) MKAZI WA MAKAMBAKO 2. EVARISTO MSEMWA (26) MKAZI WA MAKAMBAKO NA 3. KIMESHU KITIPAI (36) MKAZI WA KIJIJI CHA MODELO WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA BAADA YA KUMVAMIA MTU MMOJA AITWAYE ASHERY MPANYAKAVI (32) MKAZI WA MKONDAMI WAKIWA NA SILAHA KISU, PANGA/JAMBIA MBILI NA NONDO WAKIWA NA GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.278 BMJ AINA YA TOYOTA CHASSER.

  TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 28.10.2015 MAJIRA YA SAA 23:50 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA MKONDAMI, KATA YA MAWINDI, TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA, WATUHUMIWA HAO WALIMVAMIA MHANGA AKIWA AMELALA NYUMBANI KWAKE NA ALIFANIKIWA KUPIGA KELELE ZA KUOMBA MSAADA NDIPO WALIJITOKEZA WANANCHI NA KUMSAIDIA. MHANGA ALIJERUHIWA KWA KUPIGWA NONDO MDOMONI HATA HIVYO ALIPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA. HAKUNA MALI/KITU KILICHOCHUKULIWA KATIKA TUKIO HILO. UPELELEZI UNAENDELEA.


  KATIKA TUKIO LA PILI:

  WATU WAWILI WAKAZI WA CHITETE WILAYA YA MOMBA WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA SIMON BENARD (42) NA BONDIA PETER PANDISHA (38) WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA SILAHA/ BUNDUKI MBILI AINA YA GOBOLE NA BASTOLA MOJA ILIYOTENGENEZWA KIENYEJI.


  WATUHUMIWA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 29.10.2015 MAJIRA YA SAA 10:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA CHITETE, TARAFA YA NDALAMBO, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA. SILAHA HIZO ZILIPATIKANA BAADA YA KUFANYIKA UPEKUZI KATIKA NYUMBA YA BONDIA PETER PANDISHA NA KUKUTWA ZIKIWA ZIMEFICHWA KWENYE DARI LA NYUMBA. AIDHA INADAIWA KUWA, WATUHUMIWA HUZITUMIA SILAHA HIZO KUFANYA UHALIFU.


  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUTAFUTA KIPATO KWA NJIA HALALI NA KUJIEPUSHA NA VITENDO VYA UHALIFU KWANI VINA MADHARA KWA MAISHA YAO. 

  AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ZA MTU/WATU WANAOWATILIA MASHAKA KATIKA MAENEO YAO ILI UPELELEZI UFANYIKE IKIWA NI PAMOJA NA KUWAKAMATA.

  Imesainiwa na

  [AHMED Z. MSANGI – SACP]

  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

  0 0
 • 10/30/15--02:53: BEI YA MADAFU HII LEO


 • 0 0

  Kutangazwa rasmi mshindi wa urais 2015 kutokaa ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar Es Salaam;   
   Washiriki wa mbio za urais wa vyama vya siasa pamoja na viongozi mbalimbali katika hafla za kutangazwa mshindi wa urais 2015; Hafla 
  MKurugenzi wa NEC Ramadhan Kailima akitoa tathmini ya mchakato  wa uchaguzi mkuu mwaka  2015;https://youtu.be/Lg8d2m1YwgE 
  STAR TV: Mwenyekiti wa NEC Jaji Damian Lubuva akitoa taarifa za matokeo ya uchaguzi 2015 katika hafla ya kutangazwa mshindi wa urais 2015; https://youtu.be/b-RaifbfLy0
   DR.John Pombe Magufuli  na Samia Suluhu  wa CCM wakipokea chati cha ushindi wa urais na makamu wa urais wa Tanzania 2015; https://youtu.be/i15KeuGkv3Y 
    Anna Mghwira -ACT-Wazalendo aeleza matarajio ya Watanzania kwa uongozi wa Dr.Magufuli ikiwemo katiba ya mpya, usawa, uchumi na kudumisha amani  ya nchi huku akimkabidhi ilani ya chama chake ;https://youtu.be/pJet8rttF8U
  Viongozi mbalimbali wakishiriki kupiga picha za kumbukumbu wakati wa hafla ya kukabidhi washindi wa wagombea urais vyeti; https://youtu.be/nGT8lWgs504

  0 0

  Balozi wa Tanzania nchini Canada na Cuba Mhe. Jack Mugendi Zoka aliwasilisha Hati za Uwakilishi kwa Makamu wa Rais wa Cuba Mhe. Salvador Valdes Mesa katika Ikulu ya nchi hiyo ijulikanayo kama ´Revolutionary Palace´.

  Mhe. Balozi aliambatana na Mama Balozi Bibi Esther Zoka na Afisa wa Ubalozi Bw. Paul Makelele. Sherehe hiyo pia ilihudhuriwa na Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Cuba, Mhe. Balozi Miguel Lamazares Puello na Maafisa wengine kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na ofisi ya Makamu wa Rais.

  Baada ya zoezi hilo, Mhe. Balozi Zoka alipata fursa ya kuwa na mazungumzo na Mhe. Makamu wa Rais. Baada ya zoezi la kuwasilisha Hati na mazungumzo, Balozi alitembelea eneo la kumbukumbu - Memorial Square ijulikanayo kama Jose Marti ambapo aliweka Shada la Maua, kutembezwa na kupewa maelezo ya historia kuhusu ukombozi wa nchi hiyo inayomtambua Jose Marti kama shujaa na muasisi wa ukombozi wa Cuba.
  Balozi wa Tanzania Ottawa-Canada na Mwakilishi nchini Cuba, Mhe. Jack Mugendi Zoka pamoja na ujumbe wake wakiwasili katika Ikulu ya Makamu wa Rais ijulikanayo kama Revolutionary Palace.
  Mhe. Balozi Jack Mugendi Zoka akikabidhi Hati za Uwakilishi kwa Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Valdes Mesa katika Ikulu ijulikanayo kama Revolutionary Palace.
  Mara baada ya kukabidhi hati, yalifuata mazungumzo ya pamoja kuhusu ushirikiano wa nchi za Tanzania na Cuba. Kutoka kushoto ni Mama Balozi, Esther Nyanzila Zoka, Balozi wa Tanzania Ottawa-Canada na Mwakilishi nchini Cuba, Mhe. Jack Mugendi Zoka, Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Valdes Mesa, na maafisa wa Ikulu ya Cuba.
  Picha ya pamoja. Kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania Ottawa-Canada na Mwakilishi nchini Cuba, Mhe. Jack Mugendi Zoka, Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Valdes Mesa, Mama Balozi, Esther Nyanzila Zoka na mshauri wa Makamu wa Rais wa Cuba.
  Mhe. Balozi Jack Mugendi Zoka akiweka shada la maua katika eneo la kumbukumbu (memorial square) kwa heshima ya mwanamapindizu, Jose Marti, shujaa na mhasisis wa Cuba.
  Picha ya kumbukumbu mara baada ya kuweka shada la maua. Kutoka kushoto ni askari wa Cuba mwenye mkumbulu, Balozi wa Tanzania Ottawa-Canada na Mwakilishi nchini Cuba, Mhe. Jack Mugendi Zoka, Mama Balozi, Esther Nyanzila Zoka, Afisa wa Mambo ya Nje, Bw. Paul James Makelele na mshauri wa Makamu wa Rais wa Cuba. Wa nyuma ni maaskari wa Cuba.

  0 0

  Bondia wa ngumi za kulipwa, Francis Cheka atapanda ulingoni mjini Manchester Uingereza Novemba 7 kupambana katika pambano lisilokuwa la ubingwa.

  Akizungumza kwa njia ya simu jana, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Advance Security Limited, Juma Ndambile amesema kuwa Cheka anatarajia kuondoka wiki ijayo kwa ajili ya pambano hilo.

  Ndambile ambaye ni meneja wa Cheka, alisema kuwa tayari msaidizi wake, Rashid Nassoro yupo nchini Uingereza akiwa na mabondia wengine wawili huku akikamilisha maandalizi ya mwisho ya pambano hilo.

  Kwa mujibu wa Ndambile, Cheka anaweza kupambana na mpinzani wake wa awali, Martin Murray au bondia mwingine kutokana na sababu mbalimbali za kiufundi.

   “Maandalizi yanaendelea vizuri na msaidizi wangu, Rashid Nassoro, kwa sasa yupo Uingereza akikamilisha masuala ya pambano hilo, kuna vitu fulani fulani vilikuwa havijakamilika, ila pambano ni Novemba 7 na leo jioni nitajua lini tutaondoka Tanzania,” alisema Ndambile ambaye kwa sasa yupo Kenya kikazi.

  Alisema kuwa Cheka kwa sasa yupo mkoani Morogoro akiendelea kujiandaa na pambano hilo na kama unavyojua, akishinda, atapata ofa kubwa katika mchezo wa ngumi za kulipwa.

  Alisema kuwa Cheka anatakiwa kushinda pambano hilo ili kusaini mkataba mnono wa zaidi ya dola za Kimarekani 25,000 (Sh milioni 50) ili kupigana katika pambano linalofuata la ubingwa “Lengo ni kumfanya bondia bora ili hata akiachana na masumbwi ya kulipwa, awe na maisha mazuri, chini yangu pia nitamfundisha jinsi ya kuwekeza katika biashara na kujipatia kipato, nilisikitishwa sana matatizo aliyopata,” alisema Ndambile.

  Alisema kuwa Cheka amekuwa na heshima kubwa hapa nchini na ghafla heshima hiyo kupotea kutokana na mambo ya ‘kidunia’ na yeye ameakua kumkwamua kabisa.

  Wakati huo huo; Bondia Benki Mwakalebela ambaye alitakiwa kupanda jukwaani jana usiku, hakuweza kufanya hivyo baada ya pambano lake kuhairishwa dakika za mwisho.

  Ndambile alisema kuwa Mwakalebela alitakiwa kupambana na bondia Craig Kennedy na pambano hilo limefutwa kutokana na sababu za kiufundi.

  0 0

  Baada ya wasanii nguli wa muziki wa Bongo Fleva Ali Kiba kutoka Tanzania na Victoria Kimani kutoka Kenya wiki iliyopita kumwaga raha ya burudani  kupitia onyesho la muziki la Coke studio linalorushwa na luninga ya Clouds kila siku ya Jumamosi. Leo nyota wengine wa muziki huo Fid Q kutoka Tanzania na Maurice Kirya kutoka nchini Uganda watawasha moto.

  Wasanii hawa wawili ambao wanatamba kwa muziki wa Bongo Fleva katika ukanda huu wa Afrika Mashariki wamefanya Kolabo matata (Mash-up) katika msimu huu wa Coke Studio unaoendelea.

  Wasanii wengine kutoka Tanzania waliopo kwenye msimu wa tatu wa Coke Studio mwaka huu  ni Ben Pol ambaye alifanya kolabo matata(mash-up) pamoja na  mwanamuziki nguli kutoka Kenya anayejulikana kama Wangechi, ,  Vanessa Mdee amefanya kolabo matata(mash-up) na  mwanamuziki nguli kutoka nchini Nigeria ajulikanaye kama 2Face,na Ali Kiba ameshirikiana na Victoria Kimani.

  Akiongea wakati wa uzinduzi wa onyesho hili hivi karibuni Meneja wa Bidhaa za Coca-Cola Nchini Maurice Njowoka alisema kuwa wasanii nguli kutoka Tanzania wanaungana na wasanii wengine 27 barani Afrika katika msimu wa tatu wa maonyesho ya  burudani ya muziki maarufu kwa jina la  Coke Studio Afrika ambalo linaendelea  kuonyeshwa katika nchi mbalimbali.

  Alisema kolabo ya wasanii 55 itashirikisha wasanii wawili kutoka nchi mbili tofauti kuimba nyimbo mbili za mitindo tofauti. “Mtindo wa Kolabo (Mash –up) uliwahi kutumika hapo awali katika maonyesho ya televisheni,sinema na wakati wa kupiga muziki mchanganyiko lakini safari hii unatumika katika onyesho la Coke Studio na utawawezesha wasanii watakaoshiriki kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika kuwa wabunifu na kuboresha viwango vyao vya sauti za uimbaji”.Alisema

  0 0


  0 0


older | 1 | .... | 1013 | 1014 | (Page 1015) | 1016 | 1017 | .... | 3284 | newer