Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1012 | 1013 | (Page 1014) | 1015 | 1016 | .... | 3270 | newer

  0 0


  0 0

  Katikati ya mwezi September 2015 tuliipata good news kwenye kiwanda cha Muziki Tanzania, East Africa na Africa kwa ujumla ambapo list ya wakali wa muziki wanaowania Tuzo za MTV EMA 2015 ilitangazwa, kilichoongeza furaha ilikuwa kushuhudia majina ya mastaa kama AKA toka South AfricaYemi Alade na Davido toka Nigeria na pia mkali toka Bongo +255, Diamond Platnumz nae alikuwemo pia kwenye list hiyo.
  Good news nyingine ni kwamba Diamond Platnumz amefanikiwa kuibuka na ushindi wa Tuzo moja ya  Best Worldwide Act usiku wa October 25 2015 Jijini Milan Italy.

  0 0

  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu, Damian Lubuva (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari na waangalizi wa kimataifa wakati akitangaza matokeo ya awali ya urais Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhan Kailima.
   Waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa wakiwa kwenye mkutano huo wa kutangazwa matokeo ya awali.
   Waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa wakiwa kwenye mkutano huo wa kutangazwa matokeo ya awali.
   Jaji Lubuva akijiandaa kutangaza matokeo hayo ya awali.
   Maofisa wa NEC wakiwa kwenye mkutano huo.
   Wadau wa siasa wakiwa kwenye mkutano huo.  Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
  (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com

  0 0
 • 10/26/15--11:48: MATOKEO RASMI MAJIMBO 10
 • 0 0

  Photo Credits: dw.com/sw

  Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015
  Na leo, tulizungumzia Tanzania baada ya Uchaguzi wa jana Oktoba 25, 2015

  0 0

  Na Mwandishi Maalum, New York 
   Imeelezwa kwamba michezo ya aina yoyote ile kuanzia mpira wa miguu hadi mchezo wa bao, ikutumiwa vema na kwa uzito unaostahili ni moja ya eneo ambalo linaweza kuchangia katika siyo tu kuchochea kasi ya maendeleo bali hata katika kudumisha Amani, upendo na mshikamano miongoni mwa na baina ya mataifa. 
  Ni kwa sababu hiyo jana ( Jumatatu) Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, limepitisha kwa mara nyingine Azimio ambalo pamoja na mambo mengine linasisitiza ujenzi wa ulimwengu bora na wenye Amani kupitia michezo ikiwamo michezo ya Olimpiki. 
   Azimio hilo na ambalo hupitishwa kila baada ya miaka miwili na ikiwa ni miezi michache kabla ya kuanza kwa michezo ya Olimpiki ya majira ya kiangazi, majira ya baridi na Olimpiki ya watu wenye ulemavu ( Paralympic). 
  Miongoni mwa mambo yanayosisitizwa ni kuachana vitendo vya vyenye viashiria vya fujo, ugomvi au kubaguana siku saba kabla ya michezo kuanza na siku saba baada ya michezo kumalizika. Michezo ya Olimpiki kwa majira ya kiangazi itafanyika mwakani (2016) huko Rio de Janairo,Brazil. Na kwa kupitia azimio hilo, nchi wanachama wameipongeza Brazil kwa kuwa mwenyeji wa michezo hiyo pamoja na Olimpiki ya walemavu. 
  Azimio hilo pia limeitambua terehe 6 Aprili ya kila mwaka kuwa siku ya Kimataifa ya Michezo kwaajili ya Maendeleo na Amani. Tanzania ni miongoni mwa Nchi wanachama 150 zilizounga mkono azimio hilo lililopita kwa kauri moja. Akizungumza kwa niaba ya Tanzania wakati wa upitishaji wa Azimio , Afisa wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Bw. Noel Kaganda, amesema, Tanzania ilianza kutambua umuhimu wa michezo katika ujenzi wa taifa mara tu ilipopata uhuru wake.
   Akasema, Tanzania, inaamini kwamba, michezo ni kiungo muhimu katika ujenzi wa umoja wa kitaifa, kuleta usawa wa kijinsia, uwezeshwaji wa wanawake, fursa za elimu ,afya, maendeleo pamoja na kuzuia machafuko na utafutaji wa suluhu na kwamba azimio hili limekuja wakati muafaka ambapo Jumuiya ya Kimataifa imepitisha Ajenda 2030 na ikiadhimisha pia miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa. 
   Na kuongeza , tangu kuanzishwa kwa Taifa la Tanzania, Serikali kuanzia ile ya muasisi wa Taifa hili , Mwalimu Julius Nyerere michezo imepewa muhimu wa aina yake kwa kutungiwa sera na sheria mbalimbali ikiwa pamoja na kuwa na Wizara yake. 
   Akaeleza zaidi kwamba, michezo pia inafanyika mashuleni kuanzia shule za msingi, sekondari hadi elimu ya juu kwa kutoa mfano wa kama SHIMIWI ikiwa ni sehemu ya kuvumbua vipaji kwa wanafunzi wote bila ya kubagua jinsia zao Akabinisha zaidi kuwa michezo kama ya Bao, mchezo ambao Baba wa Taifa aliuenzi sana na kuuendeleza ni baadhi ya michezo kati ya mingine mingi ya kiasili ambayo kwayo imekuwa ni kielelezo na nembo ya utaifa wa watanzania. 
   Aidha akasema, katika kuhakikisha kwamba vijana wanaanza kupata fursa ya kuanza kuonyesha vipaji vyao tangu wakiwa wadogo, hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amefungua kiwanja cha kisasa cha michezo kwa ajili ya vijana, kiwanja ambacho kimejengwa kwa ushirikiano na Kampuni ya Symbion ya Marekani na Sunderland A.F.C ya Uingereza. 
  Tanzania imesema, inakaribisha ubia na ushirikiano kama huo katika kuendeleza michezo pamoja na kubadiliashana maarifa na uzoefu Akizungumza dhana ya kuheshimiana, kuvumulia na kutokubaguana kwa misingi yoyote ile kama inavyosisitizwa kupitia Azimio hilo, Bw. Noel Kaganda amesema, Tanzania inasikitishwa na kuendelea kuwapo kwa vitendo vya kibaguzi na ubaguzi wa rangi wakati wa michezo hususani michuano ya kimataifa. 
  Akaeleza kuwa tabia hizo zinakwenda kinyume na dhana ya maudhui na misingi ya Katiba ya Umoja wa Mataifa na Katika ya Olimpiki. Na hivyo Tanzania inatumia nafasi hiyo kuiomba Jumuiya ya Kimataifa kukemea vitendo hivyo kwa nguvu na kwa kauli moja.
   Akagusia pia kwamba pamoja na umuhimu wa michezo katika ujenzi wa taifa na kama moja ya nguzo muhimu katika kuleta Amani, bado mataifa mengi hasa yale yanayoendelea yapo nyuma katika eneo hilo kutoka na sababu mbambali mbali zikiwamo za ukoloni . Awali akizungumza kabla ya kupitishwa kwa Azimio hilo, Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki, Bw. Thomas Bach, amelitaarifu Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwamba, Kamati hiyo imeamua kuwaalika wakimbizi wenye vipaji vya hali juu kuwa miongoni mwa washiriki 11,000 wanaoshiriki michuano ya Olimpiki mwakani huko Brazil. 
  Amesema wakimbizi hao ambao watashiriki bila ya bendera za nchi zao wala kupigiwa nyimbo za mataifa yao, watakimbia kwa bendera ya Olimpiki na wataimbiwa wimbo wa Olimpiki lengo ni kuwafanya au kuwapatia wakimbizi hao fursa ya kuonyesha vipaji vyao lakini kubwa zaidi kuwaonyesha upendo.
   Bw. Noel  Kaganda, Afisa wa Uwakilishi wa Kudumu wa  Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  akizungumza kwa niaba ya Tanzania wakati wa  upitishaji wa Azimio kuhusu nafasi ya michezo katika ujenzi  wa ulimwengu  ulio bora na wenye amani. Azimio hilo  limepitishwa siku ya Jumatatu na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Kabla ya  kupitishwa wa Azimio,  Wajumbe wa Baraza Kuu  walifanya mkutano mfupi wa kumuenzi na kumkumbuka, Bw. Ali Treki mwanadiplomasia wa  Libya na aliyewahi kuwa Rais wa Baraza  Kuu la  64 la Umoja wa Mataifa. Bw. Treki alifariki Octoba 19 huko Misri.
   Michezo kama hii ya  Bao,  inaweza kuwa     njia moja  wapo ya vijana hawa kama wanavyoonekana pichani kutambua  vipaji vyao,  kuimarisha uwezo wao wa kufikiri,  lakini kubwa zaidi  kujenda maelewano, ushirikiano na kupendana kupitia mchezo huu na mingine mingi.
  Bw. Benedict Msuya Pichani Afisa   Mambo ya Nje,  akizungumza kwa niaba ya Tanzania  wakati wa majadiliano ya Kamati ya Sita ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa,  kuhusu  umuhimu wa  programu ya mafunzo ya Sheria ya Kimataifa kwa nchi zinazoendelea. Tanzania  imezishukuru  baadhi ya nchi wanachama  wa Umoja wa  Mataifa kwa kutoa michango yao  ya hiari ambayo imekuwa ikisaidia sana katika uendeshaji  mafunzo kuhusu  Sheria  ya Kimataifa.  Mafunzo hayo ambayo hutolewa  Kikanda na ambayo baadhi ya wanasheria na wanadiplomasia kutoka Tanzania wamekuwa wakinufaika    yanakabiliwa na  uhaba mkubwa wa rasilimali fedha kutoka na  kutotengewa bajeti  na Umoja wa Mataifa licha ya umuhimu wa mafunzo hayo hususani kwa nchi zinazoendelea. Anayefuatilia majadiliano hayo nyuma ya  Bw.  Msuya ni Bi. Jamila Illomo kutoka Idara ya Uhamiaji, Wizara ya Mambo ya Ndani.

  0 0


  Hatimaye Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa chama cha demokrasia na maendeleo -Chadema Bw. Wilfred Lwakatare ameibuka kidedea leo hii kuwa Mbunge wa Bukoba Mjini akiibuka kidedea dhidi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini kwa tiketi ya CCM, Khamis Kagasheki. Matokeo hayo yametanga usiku huu punde na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukoba mjini Bw. Aron T. Kagurumjuli. Kura za Udiwani Chadema/ Ukawa imeshinda Kata zifuatazo: Kahororo, Kagondo, Kibeta, Kitendaguro, Nshambya, Hamugebe, Kashai, Bakoba na Bilele. CCM imepata Kata ya Rwamishenye, Buhembe, Miembeni, Nyanga na Ijunganyondo. 

  Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukoba mjini Bw. Aron T. Kagurumjuli akitoa matokeo usiku wa kuamkia leo saa 2:30 na kumtangaza Lwakatare kwamba ndie mshindi na Nafasi hiyo ya Ubunge Bukoba Mjini. 
  Bw. Aron T. Kagurumjuli(Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukoba mjini) akiendelea na zoezi la kutangaza matokeo usiku huu.
  Mshindi wa nafasi ya Ubunge wa Bukoba Mjini Bw. Wilfred Lwakatare kupitia Chama cha CHADEMA akifurahia baada ya kuibuka kidedea katika kinyang'anyiro hicho baada ya kumwangusha mgombea mwenza aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo la Bukoba Mjini kwa tiketi ya CCM, Khamis Sued Kagasheki usiku huu. Picha na Faustine Ruta, Bukoba.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


  0 0
 • 10/26/15--22:00: CCM KIDEDEA JIJINI MWANZA
 • Stanslaus Mabula akiongea na wanahabari baada ya kutangazwa mshindi wa Ubunge Jimbo la Nyamagana (CCM)

  Na George Binagi-GB Pazzo
  Mgombea wa Chama cha Mapinduzi CCM Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza ameibuka mshindi wa kiti cha Ubunge katika jimbo hilo kwa kupata kura 81,017 na hivyo kumbwaga aliekuwa mbunge wa jimbo hilo Ezekiel Wenje kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema aliepata kura 79,280.
  Matokeo hayo yalitangazwa na Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi Jimboni humo ambae pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Tito Mahinya huku kukiwa na Ulinzi Mkali wa vyombo vya ulinzi na usalama katika viunga vya ofisi za Jiji hilo.
  Akitakangaza matokeo hayo majira ya saa saba usiku wa kuamkia leo, Mahinya alibainisha kuwa pia CCM imeibuka kidedea kwa upande wa Madiwani ambapo kati ya Kata 18, imeshinda Kata 14 na Chadema Kata Nne.


  Kwa upande wa Wagombea wengine, Chacha Okong’o (ACT Wazalendo) alipata kura 161, Faida Potea (CUF) amepata kura 1,005, Ahmad Mkangwa (NRA) kura 104, Mohamed Msanya (Jahazi Asilia) kura 175 na Ramadhan Mtoro (UDP) amepata kura 68.
  Hata hivyo kabla ya matokeo hayo kutangzwa, Mgombea kutoka Chadema Ezekiel Wenje alikataa kusaini karatasi ya wagombea na kubainisha kuwa demokrasia haikutumika katika zoezi zima la uhesabuji wa kura katika uchaguzi huo na kwamba atafuata hatua zaidi za kisheria katika kupinga matokeo hayo.
  Kwa upande wake Mshindi wa Uchaguzi huo Stanslaus Mabula alisema kuwa tangu awali alitarajia ushindi huo na kwamba suala la demokrasia limezingatiwa.
  Katika hatua nyingine Mabula alibainisha kuwa atahakikisha anatatua changamoto zinazolikabiri Jiji la Mwanza ikiwa ni pamoja na kuwaunganisha wakazi wa Jiji katika shughuli mbalimbali za uzalishaji ili waweze kujitegemea kiuchumi.
  Ezekiel Wenje akiongea na wanahabari muda mfupi kabla ya matokeo kutangazwa
  Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi Jijini Mwanza Titho Mahinya akitangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu Jijini Mwanza
  Kushoto ni Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana akiwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (kulia) muda mfupi kabla ya matokeo kutangazwa
  BINAGI MEDIA GROUP, KWA PAMOJA TUIJUZE JAMII

  0 0

  User comments Baadhi ya vijana hao wakiwa darasani wakifurahia masomo wanayopatiwa ya kujiandaa na elimu ya sekondari katika kituo hicho cha Furahini mkoani Kilimanjaro.
  Na Mwandishi wetu
  TAASISI ya misaada ya Mo Dewji Foundation imekubali kufadhili mradi wa kituo cha mafunzo cha vijana cha Furahini (FYLC) wenye lengo la kuboresha upatikanaji wa elimu katika kijiji cha Kisangara mkoani Kilimanjaro.

  Imeelezwa kuwa taasisi hiyo ya bilionea Mo Dewji imetoa shilingi milioni 7 kusaidia ujenzi wa miundombinu inayotakiwa na kituo hicho chenye lengo la kuboresha elimu kwa watoto wa kijiji hicho.

  Baadhi ya watoto hao ni wawafanyakazi wa mashamba ya Mkonge ya MeTL yaliyopo jirani na kijiji hicho.

  Ufadhili huo unaenda sambamba na sera za MeTL za urejeshaji wa faida yake kwa wananchi kama sehemu ya wajibu wake kwa jamii, wenye lengo la kuimarisha ustawi wa jamii inayochangia biashara za kampuni hiyo.

  Taasisi ya Mo Dewji ambayo ndiyo inatekeleza wajibu wa kundi la makampuni ya MeTL la kurejesha faida kwa umma, kwa ufadhili huo kwa kikundi cha Furahini wametanua wigo kutoka katika shughuli mbalimbaliw alizokuwa wakufadhili mkoani Singida.

  Lengo la ufadhili huo ni kuwezesha jamii yenye kipato cha chini kabisa kuweza kumudu mikiki ya elimu ili kukabili umaskini.

  Toka mwaka 2000 kundi la makampuni ya MeTL imekuwa ikitanua mazingira ya urejeshaji wa faida kwa umma kutokana na shughuli zake mbalimbali. Katika kipindi cha miaka mitano taasisi ya Mo Dewji imetumia zaidi ya dola za Marekani milioni 3 kusaidia miradi mbalimbali ya jamii.
  User comments 
  Baadhi ya vijana hao wakiwa darasani wakiendelea na masomo katika jengo la kituo hicho cha Furahini ambacho kinatarajiwa kukabaratiwa na kwa msaada wa Mo Dewji Foundation.

  Tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo, shughuli mbalimbali zimedhaminiwa na kufadhiliwa. Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa shule, uchimbaji wa visima, ugawaji wa vyandarua, usambazaji wa unga wa mahindi kwa wananchi waliokumbwa na baa la ukame kwa mwaka 2005-2006,ufadhili kwa wanafunzi wa sekondari,afya kw awale waliozidiwa kiafya, kujenga kitengo cha macho katika hospitali za mkoa,kuweka taa katika mitaa, msaada wa chakula kwa waliokumbwa na ugonjwa wa ukimwi, ununuzi wa vifaa vya michezo na vifaa vya wakulima.
  Kwa mujibu wa mratibu wa kituo hicho cha Furahini (FYLC) Bw. Msuya Isiaka, wazo la kuanzishwa kwa kituo lilitokana na uzoefu wa muda mrefu wa ufundishaji katika eneo hilo la mahusiano ya jamii.


  0 0

  Magufuli azidi kungara katika matokeo ya awali katika majimbo 13. Mawaziri waanguka majimboni. Yote haya utayapata katika magazeti; 
  Mzee ‘sawasawa’ ajitangaza  mshindi Zanzibar, Polisi yakamata 169 kwa kuingilia tume. Pata dondoo za habari za magazetini;  https://youtu.be/mGoDo1XC_Ts

  Polisi wazima vurugu Zanzibar. Aeleza sababu ya matokeo jimbo la Ukonga kuchelewa. Pata undani wa habari hizi katika magazeti;  https://youtu.be/3jfyH1rEnjQ

  Ulinzi waimarishwa Zanzibar, wasimamizi wa uchaguzi wanusurika kifo. Pitia dondoo za magazeti hapa Simu.tv;https://youtu.be/n_vmWxE0dyM

  Pitia udondozi wa habari kemukemu za kisiasa zilizotawala magazeti ya leo Octoba 27.2015 hapa Simu.tv;https://youtu.be/ntk9bzkfQKE


  0 0


  WAKATI wakisubiri matokeo ya uchaguzi ya rais huku Tume ya Uchaguzi ikitangaza kura za wagombea wabunge na uwakilishi katika majimbo ya uchaguzi Zanzibar, Jeshi la Polisi limelazimika kuzima fujo na vurugu kutoka kwa wafuasi wa CUF waliotanda mitaa ya Mji Mkongwe na barabara kuu ya Darajani.


  Vurugu zimezuka baada ya mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad kufanya tathmini na kutangaza matokeo ya ushindi wa chama chake katika uchaguzi wa juzi kwa asilimia 52.87. 

  Maalim Seif alitoa tathmini hiyo mbele ya waandishi wa habari katika Ofisi Kuu ya CUF Mtendeni mjini Unguja na kuitaka Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kutangaza matokeo hayo.

  Katika tathmini hiyo inaonesha kwamba mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa tiketi ya urais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amepata ushindi kwa asilimia 47.13. 

  Maalim Seif alidai matokeo waliyonayo yamekusanywa na mawakala waliopo katika vituo vya uchaguzi vilivyopo Unguja na Pemba kwa kufanya majumuisho. Hatua hiyo ilizusha shangwe na furaha kwa wafuasi wa CUF na kuanza kutembea barabarani huku gari zikipiga honi.

  Baadhi ya mitaa ikiwemo Darajani na Mlandege, polisi waliweka vizuizi ambavyo vilisaidia kuwazuia wafuasi hao kuingia barabarani. Aidha, ofisi za Serikali zilizopo katika eneo la Mji Mkongwe pamoja na taasisi za kibenki, zilifungwa baada ya kuibuka kwa mazingira ya fujo na vurugu.

  Kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mkadam Khamis Mkadam alithibitisha Jeshi la Polisi kudhibiti maeneo mbalimbali zaidi yaliyopo Mji Mkongwe pamoja na eneo la Darajani ambalo ni ngome ya upinzani.

  “Tumefanikiwa kudhibiti vurugu za watu waliofanya fujo na vurugu katika maeneo mbali mbali ya mji wa Unguja na hali ni shwari kwa sasa,” alisema Mkadam. Kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ni kosa la jinai kwa mtu yeyote au mgombea wa chama cha siasa kutangaza matokeo ya urais. Mapema, CCM Zanzibar ililaani kitendo kilichofanywa na Maalim Seif kujitangazia ushindi katika uchaguzi huo.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alisema kitendo hicho ni sehemu ya vitendo na matukio ya uchochezi yanayotakiwa kudhibitiwa kwa ajili ya kuimarisha amani na utulivu. Vuai aliitaka ZEC kuchukua hatua za kisheria na kinidhamu kwa mgombea huyo kwa kauli zake ambazo lengo lake kuingiza nchi katika machafuko katika kipindi hiki kigumu cha uchaguzi.

  Hata hivyo, viongozi watendaji wa ZEC hawakuwa tayari kulizungumzia suala hilo, ambapo maofisa wote walikuwa wapo katika mchakato wa kupokea na kutangaza matokeo ya uchaguzi wa majimbo. 

  0 0


  0 0

  Photo Credits: dw.com/sw

  Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015
  Na leo, tulizungumzia Tanzania baada ya Uchaguzi wa jana Oktoba 25, 2015

  0 0


  Wakazi Wa Kata Ya Saranga jijini Dar Jana wamefanikiwa  kupiga kura ya mbunge na Raisi baada ya kuahirishwa kwa zoezi hilo Oktoba 25. https://youtu.be/vIOP_RKkwuU

  Matokeo ya uchaguzi katika jimbo la Mtwara mjini Yametangazwa na msimamizi wa jimbo hilo huku kukiwa na hali ya Vurugu. https://youtu.be/CY2Y2WnYkaM

  Jeshi la polisi Visiwani Zanzibar limelazimika kutumia mabomu ya machozi kutawanya wafuasi wa CUF waliokusanyika katika ofisi za CUF. https://youtu.be/944jzWlWh6k
  Mwenyekiti wa Tume Ya Taifa Ya Uchaguzi NEC Jaji. Damian Lubuva akemea baadhi ya watu wanaotangza Matokeo katika Mitandao ya Kijamii. https://youtu.be/Zg-spuDs1Ks

  Haya ndiyo matokeo ya Uchaguzi mkuu ya Uraisi Mkoani Pwani jimbo la Chalinze ambapo mgombea Uraisi CCM akipata asilimia 69.70 na Lowassa akipata asilimia 28.53. https://youtu.be/HsdD_2j3w_8

  Haya ndio Matokeo halali ya Uraisi Mkoa wa Kusini Pemba Jimbo la Chwanga visiwani Zanzibar. https://youtu.be/OKEVQQ_WZno
  haya ndio matokeo halali ya Nafasi Ya Uraisi Mkoa Wa Mjini Magharibi jimbo la Chumbuni visiwani Zanzibar. https://youtu.be/u6lwnYXuBSI
  Haya ndio matokeo halali ya Nafasi ya Uraisi mkoa wa Mbeya Jimbo la Ileje kama ilivyotangazwa na Tume Ya Taifa Ya Uchaguzi NEC. https://youtu.be/13vTh4vVWXQ
  Oscar Rwegasira Mukasa wa CCM aibuka mshindi wa nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Biharamulo Magharibi. https://youtu.be/q_LAhUNBeSc

  Musoma mjini jimbo lililokuwa likishikiliwa na Vicent Nyerere limetwaliwa na Ndg. Vedastus Manyinyi wa CCM kwa kishindo cha asilimia 55.https://youtu.be/oKt6jChBHSs

  Zitto Zuberi Kabwe aibuka kidedea kwa ushindi wa asilimia 52 katika jimbo la Kigoma Mjini Uchaguzi mkuu. https://youtu.be/W3rx9Cw969g

  Ndg. Daniel Nsanzugwanko ambwaga Moses Machali wa ACT kwa asilimia 52 na kunyakua jimbo la Kasulu mjini mkoani kigoma. https://youtu.be/zawE1FlbXfk
  Haya ndio matokeo halali ya Nafasi ya Uraisi mkoa wa Kaskazini Unguja Jimbo la Kijini kama ilivyotangazwa na Tume Ya Taifa Ya Uchaguzi NEC. https://youtu.be/BT_9iEvy8tA
  Haya ndio matokeo halali ya Nafasi ya Uraisi mkoa wa Mkoa wa Tanga Jimbo la Kilindi kama ilivyotangazwa na Tume Ya Taifa Ya Uchaguzi NEC.https://youtu.be/NQFWV2JWQd8

  Haya ndio matokeo halali ya Nafasi ya Uraisi Mkoa Wa Tanga Jimbo La Korogwe Mjini Tanga kama ilivyotangazwa na Tume Ya Taifa Ya Uchaguzi NEC.https://youtu.be/AH3_q7X8Gi4
  Haya ndio matokeo halali ya Nafasi ya Uraisi Mkoa Wa Mjini Magharibi Kwahani kama ilivyotangazwa na Tume Ya Taifa Ya Uchaguzi NEC. https://youtu.be/VT8Q3C7RwZI

  Tume ya taifa ya uchaguzi NEC leo itaendelea kutangaza matokeo ya uraisi katika ngazi ya majimbo nchini kote kuanzia saa 3 asubuhi. https://youtu.be/AEOM3qkVvTU
  Matokeo Ya Uchaguzi Mkuu Uliofanyika oktoba 25 yameendelea kutangazwa huku yakionesha mchuano mkali kati Chama Cha CCM na CHADEMA.https://youtu.be/UnAp-4RP9C8

  0 0
  0 0
 • 10/27/15--04:43: BEI YA MADAFU HII LEO


 • 0 0

  Timu ya Taifa Tanzania ya Wanawake ya Mpira wa Miguu (Twiga Stars) inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Taifa ya Wanawake ya Malawi Novemba 7, 2015 jijini Dar es salaam.
  Mchezo huo wa kirafiki ni sehmu ya kujipima kwa Twiga Stars inayonolewa na kocha Rogasian Kaijage, ambayo ilishiriki Fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) mwezi Agosti – Septemba nchini Congo – Brazzavile.
  Awali Twiga Stars ilikua icheze mchezo huo nchini Malawi Oktoba 24, kabla ya chama cha soka nchini humo (FAM) kuahirisha mchezo huo, na sasa mchezo huo utacheza nchini Tanzania Novemba 07, 2015.

  0 0

   DAR ES SALAAM, 27th October, 2015 - Over the past ten years (2005-2015), Tanzania has managed to boost its economy through the tourism sector especially as it is a significant contributor to progress in terms of increasing employment and foreign exchange and in uplifting the total GDP of a country. 
  In 2014, the Tanzanian travel and tourism industry’s total contribution to GDP was 14% which equals to TZS 8252.7bn and this is estimated to rise by 1.3% by the end of 2015 and only 6.6% by the end of 2025. This sector has not done well compared to input and output contributions when the natural resources and tourism attractions are considered. 
  The tourism sector created over a million employment opportunities in 2014, some obstacles could rise up to reduce these opportunities by 3% by the end of 2015 but opportunities could also increase  2% by 2020. (World Travel & Tourism Sector, 2015). 
  Andrea Guzzoni, Country Manager of JovagoTanzania explained that, "Tourism is the most essential sector after agriculture in the contribution to GDP growth, but the outcomes remain below target as it is projected to be able to drop in 2025 if poaching continues - failure to control corruption and the lack of patriotism for domestic tourism will still remain as a challenge".


  To boost the GDP for the next ten years with the new government,  there is a need to control uneven tax collections from investors, “there has been an increase in tariff collections and  this causes foreign investors and allies evade the payment of taxes added, Andrea Guzzoni.


  However, the sector is also facing a lack of knowledge in terms of tourism, most of the employers only master one language, which is their mother tongue and only a few can master international languages. Also, there is a need to strongly control poaching and take other measures to promote all the heritage sites that exist in Tanzania and not only some of the most popular destinations like Zanzibar and Arusha. 
  About Jovago


  Jovago.comis an online hotel booking service with offices in Nairobi (Kenya), Lagos (Nigeria), Dakar (Senegal), Doula (Cameroon), Abidjan (Ivory Coast) and Dar es Salaam (Tanzania). The company is founded by Africa Internet Holding and has MTN as one of the investors. Jovago.com, Africa’s No.1 booking portal, facilitates the booking process for its users to provide them with the best hotel booking experience with fast, transparent and easy-to-use services. Jovago.com has over 25,000 local hotel listings across Africa and over 200,000 hotels around the world.


  0 0


  0 0

   Makamu Mwenyekiti Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Hamid M. Hamid (wa pili kushoto) akisoma matokeo ya wagombea nafasi ya Urais leo jijini Dar es Salaam katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu,anayemfuata kulia ni Mwenyekiti  wa Tume Jaji  Mstaafu Mhe. Damian Lubuva na Mkurugenzi wa Uchaguzi Mhe. Kailima Ramadhani
   Baadhi ya waandishi wa Habari wa Ndani na  Nje ya nchi wakifuatilia zoezi la kutangazwa kwa matokeo ya wagombea Urais  katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu  leo katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.
   Msaidizi wa Mkurugenzi wa Uchaguzi Chadema Bw. Matson Chiizi akihojiwa na mwandishi wa habari wa Idhaa ya Kiswahili, Sauti ya  Ujerumani (DW) Bi.Hawa Bihoga  kuhusu namna gani analiona zoezi la utangazaji wa matokeo linafanyika.
   Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  Jaji Mstaafu Damian Lubuva  wanne kushoto kwa waliyokaa katika picha ya pamoja kwa baadhi na waangalizi wa uchaguzi kutoka nchi za  Jumuiya ya SADC walipotembea ukumbi unaotumika kutangazia matokeo ya wagombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu leo jijini Dar es Salaam.

  Mwandishi wa habari kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw.Edward Kondela akimhoji mmoja wa waangalizi wa uchaguzi ambaye ni  Mwenyekiti wa SADC nchini Malawi Bw.Justice Mbendera  alipotembelea ukumbi wa kutangazia matokeo ya urais leo jijini Dar es Salaam. Picha na Anitha Jonas – MAELEZO.

older | 1 | .... | 1012 | 1013 | (Page 1014) | 1015 | 1016 | .... | 3270 | newer