Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

Waziri Membe asaini Kitabu cha Maombolezo ya Kifo cha Mhe. Margareth Thatcher

$
0
0
Mhe Waziri Bernard Membe, leo amesaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Uingereza jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Hayati Magreth Thatcher.
Mheshimiwa Waziri Membe akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Dianne Melrose alipowasili Ubalozini.
Waziri Membe akizungumza na Balozi ea Uingereza nchini Tanzania,Mhe Diane Melrose baada ya kusaini kitabu cha maombolezo.
heshimiwa Waziri Membe akisaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Uingereza.

Kontena linapogoma kupiga Nolindaaaa....

$
0
0
 Mchana wa leo katika pita pita za Mdau wa Globu ya Jamii Abdallah Masangu aliinasa taswira hii ya lori lililokuwa likikata kona katika eneo la Mikunguni,Zanzibar, na kushindwa kumaliza kona hiyo baada ya Kontena kuchoropoka na kuanguka chini. Pembeni pale ni mzee wa Feva akiwa amesimama kuhakikisha hautokei msongamano wa Magari Barabarani.
 Mdau akishangaa na kupiga mahesabu ya namna ya kunyanyua huu mzigo
 Kila aliyekuwa akipita eneo la tukio alijikuta akisimama na kuchukua taswira yake hata kama simu yake ni ya kitochi.Wadau tujihadhari sana na malori ya namna hii.

Uwanja wa Maji Maji Songea wahitaji Ukarabati

$
0
0
Moja ya timu zijazotumia uwanja wa Majimaji ikijitupa uwanjani kusukuma gozi. Uwanja umeharibika pitch, sehemu za kukaa, vyoo nk. Unahitaji ukarabati mkubwa. Shukrani kwa Hayati Dr Lawrence Gama kwa kujenga uwanja huu. Alikua bado hajaukamilisha.
Wachezaji wa timu ya Majimaji Kabla ya kupiga mechi ya mwisho ya ligi daraja la kwanza. Hata hivyo wameshindwa kufuzu kucheza ligi kuu msimu ujao Baada ya kuzidiwa point na Mbeya City waliopanda daraja. Majimaji ilikua mshindi wa pili na hivyo Wananchi wa Songea na Ruvuma wataendelea kuisikia ligi kwenye radio na kuitazama kunako TV
eneo la Hightable uwanja wa Majimaji.Picha na Mdau Gerson Msigwa 

TASWIRA YA KUMBUKUMBU

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa katika picha ya kumbukumbu na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Naibu wake Mhe William Ruto pamoja na Ridhiwani Kikwete (shoto mbele) Mhazini wa CCM Mororogo Hassan Bantu (wa pili shoto mbele), Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt Emmanuel Nchimbi (nyuma ya Rais Kikwete, Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt Batilda Burian na mfanyabiashara na Davis Mosha (wa kwanza shoto nyuma) na wadau katika Ikulu ya Nairobi baada ya sherehe za kuapishwa kwa Mhe Uhuru Kenyatta na Naibu wake

introducing Golden Bush FC ya Kinondoni, Dar es salaam

$
0
0

Kuna timu imeibuka katika ligi daraja la nne Wilaya ya Kinondoni inayoitwa Golden Bush FC ambayo ndiyo timu pekee  mpaka sasa haijapoteza mchezo hata mmoja katika mechi nne za mzunguko wa Kwanza. Golden Bush imeshinda mechi zote katika mzunguko wa kwanza ikicheza mechi nne na kujikusanyia alama 12. 
Wadau wengi wa soka Kinondoni wamekuwa wakijiuliza Golden Bush FC, timu ambayo inaonekana imejiandaa vilivyo kwenye hii ligi ya TFF, imetoka wapi na inamilikiwa na nani?  Kama mtakumbuka vizuri kuna timu inaitwa Golden Bush veterans, timu ambayo inaundwa na wachezaji wa zamani waliocheza mpira katika kiwango cha juu kabisa, wachezaji hao ni pamoja na Ally Mayay, Katina Shijja, Madaraka Seleman, Waziri Mahadhi, Athuman Machupa, Nico Nyagawa, Said Sued, Godfrey Bony, Yahaya Issa, Herry Morris, Abuu Mtiro, Wisdon Ndlovu, Steve Marash, Majuto Komu na wengine wengi. 
Wachezaji hawa wa zamani waliocheza mpira katika daraja la juu kabisa Tanzania, ndiyo wanaomiliki timu hii ya Golden Bush FC. Mwenyekiti wa Golden Bush FC ni Ally Mayay, Makamu Mwenyekiti ni Salum Sued, katibu wa timu ni Herry Morris, Kocha mkuu ni Katina Shijja, mkurugenzi wa ufundi ni Maradaraka Seleman, na Meneja wa timu ni Waziri Mahadhi. 
Jopo  hilo la uongozi wakishilikiana na wachezaji wenzao nguli wa zamani na wanaondelea kucheza mpira mpaka leo akiwemo Amri Kiemba, ndiyo haswa waliojitolea kutengeneza timu ya vijana ambayo inashiriki ligi daraja la nne kwa mara ya kwanza kabisa na sasa imeshaanza kuteka vyomba mbalimbali vya habari. 
Timu ya vijana hufanya mazoezi yao siku za kawaida (weekdays) viwanja vya chuo kikuu na siku za mwisho wa wiki na sikukuu hujumuika na wazee wao pale Uwanja wa Kinesi. 
Golden Bush FC ni timu ambayo imejipanga vilivyo ili kuleta ushindani katika sura mpya ya kabisa katika soka la Bongo. Tunawaomba wapenzi wa soka mtuunge mkono kwa namna yoyote ile, mpira wetu unahitaji mapinduzi ya kimawazo, kuanzishwa kwa timu kama Golden Bush FC, ni changamoto tosha katika kuleta maendeleo na mapinduzi ya kweli katika soka la Tanzania.

Mungu ibarika Tanzania, Mungu ibariki Golden Bush FC.

Imetolewa na msemaji wa timu.

Onesmo Waziri “Ticotico”

Huyu nani na anasema nini?

$
0
0

 Ankal habari za kazi, leo katika tembea tembea zangu katika youtube nimekutana na nyimbo ya huyu jamaa. Wimbo nimeupenda beats zake ila sielewi ni nini hasa anasema, naomba uiweke nyimbo hii katika blog yako ili wale wanaojua kifaransa watutafsirie, kadhalika kwa wale waliopo Zanzibar watueleze kama msanii huyu bado yupo huko na kama anazo nyimbo zaidi ya hii,

NENO KUTOKA KWA ERIC SHIGONGO

$
0
0
"Ulijifunza darasani kanuni ya kutafuta mzingo ukaielewa, nami nilijifunza kutoka kwa wazazi wangu kanuni ya kutoa kabla sijapokea! 
Hebu jaribu na wewe kanuni hii uone kama haitakusaidia. Hakuna atayefilisika kwa kusaidia wengine"
ERIC SHIGONGO.

masanja mkandamizaji kazini

$
0
0

Msanii maarufu wa vichekesho nchini ambaye pia ni mwimbaji wa nyimbo za injili Emanuel Mgaya anayejulikanakwa jina maarufu la Masanja Mkandamizaji  akitumbuiza  katika mkutano wa injili wa kuliombea taifa uliofanyika mjini Kigoma jana jioni ambapo wahubiri wa kimataifa kutoka nchini Marekani waliendesha mahubiri. Picha na Editha Karlo

Viongozi mbali mbali wamuenzi Waziri Mkuu wa Zamani,Marehemu Edward Moringe Sokoine

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (mwenye tracksuti ya bluu),Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo,Dkt. Fenela Mukangala (wa tano kulia) na Mbunge wa Jimbo la Simanjiro,Mh. Christopher Ole Sendeka,wakishiriki katika matembezi ya nusu kilomita ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 29 tangu kufariki kwa Waziri Mkuu wa zamani,Marehemu Edward Moringe Sokoine,yaliyofanyika leo huko Kijijini kwao Monduli Juu,Mkoani Arusha.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiweka shada la Maua kwenye Kaburi la Waziri Mkuu wa zamani,Marehemu Edward Moringe Sokoine,aliefariki miaka 29 iliyopita siku kama ya leo.
Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo,Dkt. Fenela Mukangala akiweka shada la Maua kwenye Kaburi la Waziri Mkuu wa zamani,Marehemu Edward Moringe Sokoine.
Wake wa Waziri Mkuu wa zamani,Marehemu Edward Moringe Sokoine wakiweka shada la Maua juu ya kaburi la Mume wao.
Mbunge wa Jimbo la Arusha,Mh. Godbress Lema akishiriki mbio za kumuenzi Waziri Mkuu wa zamani,Marehemu Edward Moringe Sokoine zilizofanyika kijijini kwake Monduni Juu,Mkoani Arusha leo.
Baadhi ya vijana wa jamii ya Kimasai wakikimbia mbio fupi za kumuenzi Waziri Mkuu wa zamani,Marehemu Edward Moringe Sokoine,kijijini kwake Monduli Juu,Mkoani Arusha.

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Ngoma ya 'Ni Wewe Pekee' ya Nguza Viking "Big Sound" enzi za Maquis du Zaile Wana Zembwela si mchezo, Asante Vumbi Dekula kwa kutukumbusha mbali.... Enzi za chini ya mwembe

Mkoko wa Ukweli upo sokoni

$
0
0




Mkoko huu bado ni mpya kabisa na una kilometers 100,500, Bei Tsh 12M, kwa wanunuzi piga simu namba 0789 88 88 82. Mmiliki anauza sababu amepata matatizo ya gafla ambayo yanahitaji pesa kuyatatua. 

Toyota IST Ya Mwaka 2003 Color: Light Blue Automatic Petrol

SUZUKI GRAND VITARA INAUZWA

$
0
0
 Hii gari ni model ya mwaka 2005, Imenunuliwa kutoka DT Dobie brand new by then,so far imetembea kilometres 166,049. Bei ya kuanzia ni 25M ila mazungumzo pia yapo please Kama kuna AMJ isiwatie Shaka gari ni Nzuri, atakayeinunua sasa ndiyo itakuwa second hand.
Contact number is 0715 08 29 57

KUMBUKUMBU YA HAYATI MAREHEMU EDWARD MORINGE SOKOINE KATIKA ENEO LA KIJIJI CHA WAMI SOKOINE

$
0
0
Jana Aprili 12, 2013 , Parokia ya Dakawa , wilayani Mvomero, mkoa wa Morogoro, ilifanya kumbukumbu ya Waziri Mkuu Hayati Marehemu Edward Moringe Sokoine kwa ibada ya misa takatifu iliyoendeshwa na Askofu Telesphor Mkude wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, katika kanisa lilojengewa karibu na mahali alipofia baada ya kupata ajali ya gari Aprili 12, 1984 akitokea mkoani Dodoma kuelekea Dar es Salaam, sehemu alipofia hayato Sokoine ni Wami -Ruhindo,kilometa 40 kabla ya kufika mjini Morogoro na Kanisa alilojengewa na Jimbo Katolikila Morogoro linaitwa Kanisa la Picha ya Sokoine , tangu kufariki kwake dunia ametimiza miaka 29. Habari na picha na John Nditi.
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro  Telesphor Mkude akiwa na mapadre na waumini wakielekea eneo la kutolea maombezi ya kumbukumbu ya kifo cha Sokoine
Askofu Telesphor Mkude akiongoza sala ya maombezi ya kumwombea Marehemu Edward Sokoine baada ya kumalizika kwa ibada
Baadhi ya akina mama na watoto wao wakijumuika kanisani kumwombea Hayati Sokoine
Hapa ndipo alipofia aliyekuwa Waziri Mkuu , Edward Moringe Sokoine , Aprili 12, 1984 akitokea Mkoani Dodoma. Eneo hili ni Wami Ruhindo , kilometa 40 kabla ya kufika mjini Morogoro
Baadhi ya kina mama wa Jamii ya wamaasai wa Kijiji cha Wami Sokoine , wilaya ya Mvomero wakiwa nje ya kanisa wakati wa ibada ya mumwombea marehemu Edward Sokoine
 Kanisa laKatoliki Jimbo la Morogoro limejenga kanisa hili kumuenzi Hayati Sokoine karibu na eneo alipopata ajali na kufariki dunia. Kanisa hilo linaitwa Picha ya Sokoine
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka (wa pili kutoka kushoto) na waumini wengine wakishiriki misa ya kumwombea Hayati Edward Sokoine eneo la Wami Sokoine.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka ( kulia) akifurahia jambo na Askofu , Telesphor Mkude wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro eneo la Makao makuu ya Parokia ya Picha ya Sokoine

mambo ya gado leo

$
0
0

President Kenyatta clarifies on Free Maternity!

UMOJA WA MATAIFA WAIDHINISHA UJENZI WA MAJENGO YA KIMATAIFA TANZANIA

$
0
0
Afisa Ubalozi wa  Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Bw. Justin Kisoka ambaye pia alikuwa Mratibu wa Kamati ya Tano   inayohusika na masuala ya Utawala na Bajeti  akiwasilisha  siku ya Ijumaa, taarifa ya Kamati hiyo mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.  Taarifa  hiyo ilihusisha maazimio  Nane ambayo Baraza Kuu liliyapisha kwa kauli moja, likiwamo lile linaloidhinisha ujenzi wa Majengo ya Taasisi ya Kimataifa ya  Kumalizia Mashauri ya Masalia ya iliyokuwa  Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ( ICTR) Tawi la Arusha. Majengo hayo ya kisasa yatajengwa katika eneo la Lakilaki Jijini Arusha.

Na Mwandishi Maalum
Baraza Kuu la  Umoja wa Mataifa    limepitisha  kwa kauli moja Azimio  linalopendekeza kuidhinishwa  kwa hatua zote za   Ujenzi wa  Mradi wa   Taasisi mpya ya Kimataifa  itakayochukua  majukumu  ya   Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda ( ICTR).
Mradi huo wa majengo ya  kisasa, utajengwa katika eneo la LakiLaki Jijini Arusha-Tanzania na   utahusisha Ofisi, vyumba vya  mahakama, na sehemu ya kutunzia nyaraka na kumbukumbu zote za  ICTR.  Eneo hilo la Laki Laki limetolewa na Serikali ya Tanzania kwa Umoja wa Mataifa.
 Baraza    Kuu limepitisha Azimio hilo katika  mkutano wake uliofanyika siku ya Ijumaa ( April 12),mkutano ambao  pia, Baraza lilipokea na kupitisha  maazimio mengine Nane  yaliyowasilishwa na  Kamati ya Tano inayohusika na masuala ya  Utawala na Bajeti katika Umoja wa Mataifa.
Taasisi hiyo mpya  ijukulikanayo kama  Mfumo wa Kimataifa wa Kumalizia  Mashauri Masalia ya iliyokuwa Mahakama ya  Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari au kwa kimombo (  International Residual Mechanism forCriminal Tribunal )- Tawi la Arusha   pamoja na kuhifadhi nyaraka itasimamia kesi za Masalia ambazo zitakuwa bado hazijakamilia baada ya  ICTR kumaliza muda wake mwakani.
Azimio hilo pamoja na mambo mengine, linamtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, kuweka bayana uwajibikaji na uangalizi wa kina katika ujenzi wa mradi ikiwa  ni pamoja na  kuhakikisha kwamba, sheria, taratibu, kanuni na miongozo yote ya  Umoja wa Mataifa     inayohusu manunuzi/ugavi inafuatwa  ipasavyo katika utekelezaji wa mradi huu.
Gharama za mradi zinatarajiwa kuwa kiasi cha dola za kimarekani 8.78 Milioni ( takribani  Sh.14 Bilioni). Fedha hizi zinalipwa na  Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa. Mradi unatarajiwa kukamilika  kabla ya mwishoni mwa  mwaka 2015.
Aidha kupitia Azimio hilo,  Baraza Kuu  pia limeishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea na jukumu la  kufuatilia kwa karibu mchakato wote unaohusiana na  utekelezaji wa mradi na vilevile katika kuhakikisha kwamba  inashirikiana na Umoja wa Mataifa kufanikisha  Mradi huu.
Halikadharika  kupitia  Azimio hilo, Baraza Kuu limeelezea  kufurahishwa na  maendeleo ya utekelezaji wa mradi hasa kwa kutumia ujuzi wa ndani, (Local knowledge) katika  ubunifu wa majengo (design),   upatikanaji wa  meneja wa mradi na maandalizi ya kina ya gharama za  ujenzi.
Pamoja na pendekezo la  kuidhinishwa kwa hatua za ujenzi wa mradi ,  Baraza pia  kupitia  Azimio hilo , linamtaka KatibuMkuu   kufanya juhudi zote zitakazo pelekea  kupunguza muda wa ujenzi wa mradi .
Katika hatua nyingine,  Baraza  Kuu pia linamtaka Katibu Mkuu  kuanza mazungumzo na Asasi nyingine za Kimataifa ikiwamo ile ya Mahakama Afrika itakayoshughulikia   Haki za Binadamu,  juu ya namna bora ya  kushirikiana katika matumizi ya  miundo mbinu hiyo katika siku za usoni.
Mwaka 2010 Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, lilipitisha Azimio nambari  1966  la kuanzisha Mfumo wa Kimataifa utakaomalizia Mashauri ya Masalia  kwa zilizokuwa   Mahakama za Kimataifa za Mauaji ya Kimbari  yaliyotokea  nchini Rwanda ( ICTR) na Mauaji ya  halaiki yaliyotokea katika  iliyokuwa Yugoslavia ya Zamani ( ICTY).
Katika azimio hilo Baraza Kuu la Usalama lilibainisha wazi  kwamba  Arusha ndiyo itakuwa makao ya  Tawi la mfuno huo mpya na  The Hague ikiwa ni  makao ya Tawi  jingine.





MATATIZO YA KIUFUNDI YAKWAMISHA SUPER WEEK ‘LIVE’

$
0
0

Mechi tano kati ya sita za Super Week za Ligi Kuu ya Vodacom zilizokuwa zioneshwe moja kwa moja (live) na Kituo cha televisheni cha SuperSport cha Afrika Kusini sasa hazitaoneshwa kutokana na matatizo ya kiufundi.

Kwa mujibu wa Mtayarishaji Mtendaji (Executive Producer) wa SuperSport Kanda ya Afrika, Max Tshunungwa ambaye yuko nchini, wameshindwa kuonesha mechi hizo kutokana na matatizo ya kiufundi katika magari yao ya kurushia matangazo (OB van) yanayohudumia Afrika Mashariki- Kenya, Tanzania na Uganda.

Mechi hizo ni kati ya Azam na African Lyon, Yanga na Oljoro JKT, Azam na Simba, Coastal Union na JKT Ruvu na Mgambo Shooting na Yanga itakayochezwa Aprili 17 mwaka huu jijini Tanga.

Tatizo hilo pia limeathiri mechi za Ligi Kuu ya Kenya (KPL) ambazo hazitaonekana wikiendi hii. SuperSport ndiyo yenye haki za matangazo ya televisheni kwa ligi hiyo ya Kenya.

Tshunungwa amekutana na Sekretarieti ya TFF na Kamati ya Ligi kuelezea tatizo hilo. SuperSport kwa kushirikiana na Kamati ya Ligi na TFF watapanga mechi nyingine za Super Week kabla ya ligi kumalizika msimu huu.

Pia TFF, Kamati ya Ligi na SuperSport watakuwa na mkutano mfupi wa waandishi wa habari wakati wa mapumziko kwenye mechi ya leo kati ya Yanga na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa.

Kampuni ya Mabibo yaendelea kula sahani moja na waingizaji wa Bia za Windhoek kimagendo

$
0
0
 Mshauri Mkuu wa Kampuni ya Mabibo Beer,Wines & Spirits Tanzania,James Rugemalira akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya watu wanaohusika na kuuza bia za Magendo za Windhoek ambazo hazina Code No MB 66 ambayo ni Code Maalum ya Kampuni ya Mabibo yenye kibali cha kuuza na kusambaza bia hizo hapa nchini.Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mabibo Beer,Wines & Spirits Tanzania,Benedicta Rugemalira.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mabibo Beer,Wines & Spirits Tanzania,Benedicta Rugemalira akizungumza na kusisitiza umuhimu wa vyombo vya habari katika kuelimisha wananchi kuhusu utumiaji wa bidhaa halala na ambazo zimelipiwa kodi,wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) uliofanyika leo kwenye ukumbi wa East 24,Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Mshauri Mkuu wa Kampuni ya Mabibo Beer,Wines & Spirits Tanzania,James Rugemalira akionyesha code ya MB 66 iliopo kwenye moja ya chupa ya bia ya Windhoek zinazosambazwa na Kampuni ya Mabibo,ambayo haionekani katika bia hizo za Magendo.
 Baadhi ya waandishi wa habari na wadau wa Windhoek Bia wakiwa kwenye mkutano huo leo.

Yalee Yaleeeeeee...........

$
0
0

Katika tukio moja jijini Dar es Salaam katika Mtaa wa Indhira Ghandhi/Mshihiri, Tanki nne (4) za Maji za Lita 5000 kila moja zaanguka kutoka juu ya jengo la ghorofa 13 na kuvunja nyumba ya jirani.

Tanki hizo bado zilikuwa zinafungwa juu ya ghorofa hilo na mkandarasi alikuwa hajaweka vizuizi vya aina yoyote.

Naomba kuuliza wadau, matanki ya lita ngapi zinaruhusiwa kisheria kupandishwa juu ya maghorofa? na kwenya tukio kama hilo nani awajibiishwe, CRB, Mkandarasi, mmiliki wa jengo au…?

Kibao cha Mkandarasi wa Jengo hilo.

Tanki zote chaliiiiii
Sehemu ya Madhara yaliyotokea kwenye nyumba zilizopo jirani na Jengo hilo.
Hili ndio jengo lenyewe.

hii inaitwa Usije Mjini

$
0
0
Hivi ndivyo hali ilivyo katika baadhi ya Mitaa ya Kariakoo Jijini Dar es Salaam hivi sasa,Maana kila mwenye gari anajiona yeye ndie mwenye haki ya kupita kuliko mwenzie.hapa ni magari yakiwa yamegoma kupishana katika mtaa wa Likoma.

taarifa ya msiba

$
0
0
Ndugu Adam Nderumaki anasikitika kutangaza kifo cha baba yake Mzazi kilichotokea usiku wa Jumatano katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. 

Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Mzee Bernard Nderumaki Victoria, Kijitonyama. Ibada ya kuaga mwili itafanyika nyumbani kwa marehemu siku ya Jumapili saa 8 mchana na mazishi yatafanyika siku ya Jumatatu Kilema Moshi.

Bwana ametoa bwana ametwaa jina lake lihimidiwe,

Amen.
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images