Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1007 | 1008 | (Page 1009) | 1010 | 1011 | .... | 3278 | newer

  0 0

  FAMILIA ya Josef Antoni Mloka inatangaza kupotelewa na kijana wao Edimund Josef (Pichani) mwenye umri wa miaka 23 mara ya mwisho aliondoka nyumbani  Julai 3 mwaka huu akiwa amevaa fulana ya rangi ya kijani na modo ya jinsi ya rangi ya bluu tangu siku hiyo tunamtafuta bila mafanikio.
  Edimund Josef ni mrefu wa wastani kwa rangi ni maji ya kunde anaupungufu wa akili alikua anaishi Kimara Bonjokwa kwa Mashiringi mtaa wa mjumbe Ally Wila jijini Dar es Salaam. 

  Amesoma shule ya Msingi Ukombozi-Mazese alimaliza shule hiyo 2007.


  Kwa yeyote atakaye muona sehemu yoyote ile  (Hata kama kwa mtu kwa jirani, jalalani, au akiokota takataka au akiombaomba) tunaomba atoe taarifa kituo cha Polisi cha Urafiki, pia kituo cha Polisi cha Stakishari Ukonga,au kituo chochote cha Polisi kilichopo karibu nawe.

  Au unaweza kuwasiliana na Baba mzazi wa kijana huyo Josef Antoni kwa simu namba 0654790019 Au kaka yake Felix Josef  kwa namba 0657536219.

  TUNAOMBA USHIRIKIANO WAKO.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akifungua hafla ya kumuaga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe iliyoandaliwa na watumishi wa Wizara hiyo na kufanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere
  Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa waliohudhuria hafla hiyo
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Hassan Simba Yahya akitoa muhtsari wa shughuli chache ambazo Waziri Membe alizisimamia kwa umahiri mkubwa katika kipindi chake cha miaka 9 ya Uwazi wa Mambo ya Nje. Waliokaa ni Mhe. Membe na Balozi Mulamula ambao wanasikiliza kwa maikini shughuli zilizotekelezwa na Mhe. Waziri Membe.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.


  0 0
 • 10/22/15--03:26: BEI YA MADAFU HII LEO


 • 0 0

  Katibu wa Kamati ya Taifa Stars, Teddy Mapunda leo amefanya makutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Karume, ambapo ametumia nafasi hiyo kutangaza namba za simu za uchangiaji kwa Watanzania kwa ajili ya timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.
  Akizungumza na waandishi wa habari, Teddy amesema watanzania wanaweza kuichangia Taifa Stars kiasi chochote cha fedha kuanzia shilingi mia moja (TZS 100) kwenda namba 0654-888868 (Tigo Pesa) na 0789-530668 (Airtel Money) ambazo zitatumika kwa ajili ya motisha kwa wachezaji, uhamasishaji/masoko na maboresho ya kambi za ndani na nje ya nchi.
  Aidha Teddy amesema Kamati ya Taifa Stars inaandaa utaratibu kwa ajili ya washabiki watakaotaka kusafiri kuelekea nchini Algeria katika mchezo wa marudiano, waweze kuchangia gharama za usafiri ili waweze kwenda kuipa sapoti Stars katika mchezo wa marudaiano Novemba 17, 2015.
  “KamatI inaendelea na mchakato wa kukamilisha suala la kambi ya Taifa Stars, na mpaka sasa tunasubiri majibu kutoka katika vyama vya soka vya vya nchi tunazotaka kuweka kambi ambazo ni Afrika Kusini, Dubai na Oman kabla ya kutangaza rasmi kambi itakapokuwa” Alisema Teddy.
  Kamati inawaomba watanzania, wadau, washabiki na wapenzi wa mpira miguu nchini kuichangia timu ya Taifa kupitia namba zilizotolewa na pia kujitokeza kwa wingi kuujaza uwanja wa Taifa siku ya mchezo wa tarehe 14 Novemba, 2015

  0 0

   Mkuu wa Hazina Benki ya Exim Tanzania Bw. George Shumbusho (Kushoto) pamoja na  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya STE BPS (COTE DIVOIRE) S.A LTD Bw. Vijayan Vetharethinam kwa pamoja wakifungua shampeni wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Benki hiyo kwa ajili ya wateja wake Mkoani Mtwara hivi karibuni.
  Mkuu wa Hazina Benki ya Exim Tanzania Bw. George Shumbusho (wa pili kulia) akibadilishana mawazo na  Bw. Anoop Kumar  pamoja na  Bw  Prasoon kutoka kampuni ya Regal Holdings Ltd wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Benki hiyo kwa ajili ya wateja wake Mkoani Mtwara hivi karibuni. Wengine ni pamoja na Meneja Masoko Msaidizi wa Benki hiyo Bw.  Abdulraham Nkondo (kushoto) na Meneja Msaidizi Mauzo Hazina, Bi Glynis Stambuli (kulia).

  0 0


  Mahujaji wengine wawili kutoka Tanzania ambao walikuwa hawaonekani tokea ajali ya kukanyagana kwa mahujaji ilipotokea Makkah nchini Saudi Arabia tarehe 24 Septemba 2015 wametambuliwa kuwa, ni miongoni mwa mahujaji waliofariki dunia.

   Kutambuliwa kwa mahujaji hao kunafanya idadi ya mahujaji wa Tanzania waliopoteza maisha katika ajali hiyo kufikia ishirini na saba (27). Majina kamili ya mahujaji hao ni Bw. Juma Yussuf Bakula na Bw. Ahmad Awadh Namongo kutoka Kikundi cha Ahlu Dawaa.

  Hadi sasa mahujaji kumi na tatu (13) kutoka Tanzania bado hawajulikani walipo na jitihada za kuwatafuta bado zinaendelea.

  Kwa upande wa mahujaji wanne ambao walikuwa wanapatiwa matibabu kutokana na kuugua au kujeruhiwa, mmoja wao ni Bw. Mustafa Ali Mchina ambaye alikuwa amelezwa katika chumba cha wagonjwa mahututi katika mji wa Maddinah alifariki dunia tarehe 17 Oktoba 2015 na kuzikwa Maddinah siku hiyo hiyo. 

  Bi. Mahjabin Taslim Khan ambaye alijeruhiwa katika ajali hiyo na kusababisha kukatwa mguu wake amepata nafuu na alirejea nchini tarehe 20 Oktoba 2015. Mwingine ni Bi. Hidaya Mchomvu ambaye alijeruhiwa pia bado yupo hospitali akiendelea kupatiwa matibabu.

   Hujaji wanne ni Bw. Ahmed Abdallah Jusab ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo alifanyiwa upasuaji wa kumuwekea kifaa cha kuongeza mapigo ya moyo tarehe 19 Oktoba 2015 na alitarajiwa kurejea nchini tarehe 21 Oktoba 2015.

  Serikali ya Saudi Arabia inaendelea kutoa taarifa zaidi za kuwatambua mahujaji waliofariki dunia au kujeruhiwa katika ajali hiyo na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa itaendelea kutoa taarifa kwa umma kuhusu wahanga wa ajali hiyo kadri itakapokuwa inazipokea.
  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
  Dar es Salaam
  22 Oktoba, 2015

  0 0

   Mhe. John Lugalema  Kahyoza akila kiapo mbele ya Rais Jakaya kikwete baada ya kuteuliwa kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufaa mapema hii leo Ikulu jijini Dar es Salaam, awali mhe. Kahyoza alikuwaMsajili Mahakama Kuu ya Tanzania.
   MheKatarina Tengia Revocati akila kiapo mbele ya Rais Jakaya kikwete baada ya kuteuliwa kuwa Msajili Mkuu  wa Mahakama  mapema hii leo Ikulu jijini Dar es Salaam, awali  Mhe. Katarina alikuwa Msajili wa Mahakama ya rufani.
  Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na majaji wanawake waliohudhuria sherehe za kuapishwa wa heshimiwa John Lugalema  Kahyoza na Bi. Katarina Tengia Revocati mapema hii leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Picha zote na Eliphace Marwa – Maelezo.

  0 0

    Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akionyesha waandishi wa habari leo (hawapo pichani) kitabu cha maadili ya uchaguzi kilichosainiwa na viongozi wa vyama vya siasa waliosimamisha wagombea katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25.

   Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Jeshi la Polisi leo Mkuu wa Jeshi hilo IGP Ernest Mangu amesema kuwa ulinzi utaimarishwa maeneo yote kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha kuwa taifa linapita salama katika kipindi hiki cha kupiga kura, kuhesabu na kutangaza matokeo ya uchaguzi.

   Ametoa rai kwa wananchi kujitokeza kupiga kura siku  hiyo bila wasiwasi wa aina yoyote ili kuweza kutumia haki yao ya kikatiba kuchagua viongozi.
  (Picha na Francis Dande)
    Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akionyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) kitabu cha maadili ya uchaguzi kilichosainiwa na viongozi wa vyama vya siasa waliosimamisha wagombea katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 ambapo amewataka watu wote kutii sheria bila shuruti wakati wa uchaguzi.
    Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akifafan jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).

  0 0

   Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati Airtel ilipozindua  smartifoni mpya ijulikanayo kama Magnus Bravo Z10zitakazopatikata katika maduka yote ya Airtel zikiwa zimeunganishwa na ofa ya Smartifonika  kutoa  muda wa maongezi wa dakika 150, 150MB na SMS 150 kwa kipindi cha miezi sita. Kulia ni bi Anethy Muga meneja masoko wa Airtel. Hafla ya uzinduzi imefanyika jana katika makao makuu ya Airtel Dar es salaam
   Meneja Masoko wa Airtel Bi Anethy Muga akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati Airtel ilipozindua  smartifoni mpya ijulikanayo kama Magnus Bravo Z10 zitakazopatikata katika maduka yote ya Airtel zikiwa zimeunganishwa na ofa ya Smartifonika  kutoa  muda wa maongezi wa dakika 150, 150MB na SMS 150 kwa kipindi cha miezi sita. Kushoto ni Afisa Matukio wa Airtel Bi, Dangio Kaniki wakati wa Hafla ya uzinduzi iliyoyika jana katika makao makuu ya Airtel Dar es salaam.
   Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki (kushoto) akiwa na  Meneja masoko wa Airtel Anethy Muga (kulia) wakionyesha simu mpya zilizoingizwa sokoni zikiwa na ofa ya Airtel smartifonika aina ya Mgnum Bravo Z10 wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika makao makuu ya Airtel leo
  Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki akijaribu kupiga picha kwa kutumia kamera ya mbele ya simu mpya aina ya Magnus Bravo Z10 inayopatikana katika maduka ya Airtel kuanzia sasa ikiwa na ofa ya Smartifonika, uzindunzi wa kuingiza sokoni simu hii yenye uwezo wa kutumia  laini mbili umefanyika jana katika makao makuu ya Airtel.

    AIRTEL  Tanzania leo imezindua smartifoni mpya na yenye ubora zaidi ijulikanayo kama Magnus Bravo Z10 ambapo zinapatikata sasa hivi  kwenye maduka yote ya Airtel nchini zikiwa zimeunganishwa na ofa ya Smartifonika  inayompatia mteja muda wa maongezi wa dakika 150, 150MB na SMS 150 kwa kipindi cha miezi sita.

  Akiongea na waandishi wa habari Meneja masoko wa Airtel Tanzania Aneth Muga amesema “Airtel tumekuletea Simu mpya ya Magnus Bravo Z10 ili kukuwezesha mteja wetu kuendelea kufurahia huduma zote za Airtel na zile huduma zote za kisasa za smartifoni ukiwa mahali popote
   “Magnus Bravo Z10 toka Airtel inatumia laini mbili, ina radio, kioo (screen) kubwa ili kukupa raha zaidi kuona vyema unapokuwa unaitumia, pia imewekewa kamera zenye uwezo mkubwa mbele na nyuma za 5mp ili kukupa taswira au picha nzuri utakazopiga karibu au mbali ukiwa na ndugu, jamaa na marafiki” alielezea Bi Muga
  “Vilevile ili  uweze kufurahia huduma zote za mitandao, Airtel tumehakikisha tayari simu hii inamitandao yote ya kijamii kama facebook, Instagram, twitter na mingine mengi” . Alisema Bi Muga
  Simu hii inapatikana sasa katika maduka yote ya Airtel nchini kwa gharama nafuu kuliko zote ya sh. 75,000  tu.

  0 0  0 0

  Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mariado na walimu iliyopo Usa River ,wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha wakiwa katika picha ya pamoja waliposhiriki maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu barani Afrika katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu iliyofanyika Oktoba 21 na kudai haki za wenye ulemavu wa ngozi(Ualibino) kulindwa kama wananchi wengine

  Mwanafunzi Kelvin wa shule ya Mariado akiimba wimbo Umoja wa Afrika(AU)ambao ni maalumu wakati wa shughuli za umoja huo zinapofanyika.

  Kamishna wa Tume ya Haki Binadamu na Utawala Bora,Zanzibar ,Mohamed Khamis Hamad akizungumza katika maadhimisho hayo.

  Imeandaliwa na www.rweyemamuinfo.blogspot.com

  0 0
 • 10/22/15--06:43: KUFUNGA KAMPENI CCM


 • CCM inapenda kutoa taarifa kuhusu masuala kadhaa kwa wanachama, wapenzi na mashabiki wake na kwa umma wa Watanzania.

  Kufunga Kampeni
  CCM itafunga kampeni zake kwa utaratibu mpya na kwa kishindo.  Kampeni za CCM zitafungwa Kitaifa kwa mikutano mikubwa ya kampeni katika mikoa mitano. Mikutano hiyo itaongozwa na viongozi wa CCM Kitaifa waliopo madarakani na wastaafu. Mikoa hiyo na viongozi watakaoongoza mikutano hiyo ni kama ifuatavyo:

   1.    Mwanza – Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, Mwenyekiti wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, Mgombea Urais, na Ndugu Samia Hassan Suluhu, Mgombea Makamu wa Rais
   2.    Tanga – Ndugu Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM
   3.    Mbeya – Ndugu Benjamin William Mkapa, Mwenyekiti wa CCM Mstaafu
   4.    Mtwara – Ndugu Ali Hassan Mwinyi, Mwenyekiti wa CCM Mstaafu
  5.    Kigoma – Ndugu Philip Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM
  6.    Kilimanjaro – Ndugu Yusuf Makamba, Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu
  7.    Mara – Ndugu Joseph Warioba, Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu  Mstaafu
  Kati ya leo na kesho, maeneo mengine yanaweza kuongezeka. Mikutano hii itaanza saa sita mchana na itarushwa, yote kwa pamoja, kwa matangazo ya moja kwa moja ya vituo vya televisheni vitano na vituo vya redio 67. Vilevile, watakaohudhuria katika mikutano hii wataunganishwa moja kwa moja na mkutano wa Mwanza, alipo Mwenyekiti, Mgombea na Mgombea Mwenza, na wataweza kusikiliza hotuba ya Dkt. Magufuli moja kwa moja kupitia screens zitakazokuwa katika viwanja vyote hivi saba.
  Namna hii ya ufungaji wa kampeni itakuwa ni ya kihistoria, na inadhihirisha nguvu ya CCM inayoiwezesha kufanya mikutano mikubwa ya kampeni kwa siku moja katika maeneo mbalimbali nchini.  Lakini pia tutaweka historia katika tasnia ya utangazaji wa televisheni hapa nchini kwa kutangaza na kuunganisha kwa pamoja matukio saba kwa wakati mmoja.
  Kwa upande wa Dar es Salaam, tutafanya mkutano mkubwa wa ufungaji wa kampeni za Mkoa wa Dar es Salaam, katika Uwanja wa Jangwani, kesho, Ijumaa, tarehe 23 Oktoba 2015. Siku ya Jumamosi, tarehe 24 Oktoba 2015, Wagombea Ubunge katika majimbo ya Mkoa wa Dar es Salaam watafunga kampeni katika maeneo ya majimbo yao kwa namna mahsusi.

  Tathmini ya Kampeni
  Kama Chama, tumeridhika na ubora na ukubwa wa kampeni tulizofanya licha ya changamoto za hapa na pale. Dkt. Magufuli na Ndugu Suluhu wamefanya kazi kubwa, na kwa bidii kubwa, na maarifa makubwa. Wamekuwa barabarani kwa siku 57 wakifanya mikutano kati ya 8 hadi 12 kwa siku.  Imani yetu ya ushindi inatokana na kazi kubwa waliyofanya. Pia, CCM inawashukuru viongozi, wapenzi wa washabiki wake – wa makundi mbalimbali ya kijamii - kote nchini kwa kazi kubwa ya kampeni waliyoifanya.
  Kutokana na kazi kubwa na nzuri iliyofanyika, na kutokana na mwenendo wa tafiti huru na tafiti zetu za ndani, CCM inategemea ushindi wa asilimia zisizopungua 69. 

  Uchaguzi wa Amani
  CCM haitachoka kuendelea kusisitiza uchaguzi wa amani na utulivu. Sisi kama chama kikubwa cha siasa nchini, chenye wafuasi wengi zaidi, na chenye dhamana ya uongozi wa dola, tutatimiza wajibu wetu wa kuhimiza utulivu kwa wapenzi, washabiki na wanachama wetu. Tunawataka na wenzetu wafanye hivyo.
  Kauli za wenzetu kwamba kura zitaibiwa ni kauli za kutojiamini na kujiandaa kufanya vurugu. Kauli za kwamba washabiki wa UKAWA wakishapiga kura wabaki vituoni kulinda kura si kauli za wanaotaka uchaguzi wa amani.
  Kwa utaratibu wetu wa uchaguzi, utaratibu wa pekee kwa Chama kulinda kura zake ni kwa kupitia wakala wa vyama waliopo kwenye kila kituo cha kupiga kura na wenye nguvu na mamlaka ya kisheria ya kushuhudia zoezi zima, kuanzia kupiga kura, kuhesabu kura hadi kutangaza matokeo. Kura zinapigwa na kuhesabiwa vituoni mbele ya Wasimamizi wa Uchaguzi, Mawakala wa vyama na Waangalizi wa Uchaguzi wa ndani na nje ya nchi. Mawakala wa vyama na Wasimamizi wa Uchaguzi wanaweka sahihi kwenye fomu za matokeo, na matokeo hayo yanatangazwa na kubandikwa kwenye kituo. Kwenye kituo kikuu cha Tume cha kujumlisha matokeo, mawakala wa vyama pia huwepo na Tume hujumlisha matokeo kutoka kwenye fomu za matokeo za vituo vya nchi nzima zilizosainiwa na mawakala wa vyama kwenye kila kituo.  Kwa viongozi wa UKAWA kuwaambia watu waingie barabarani au kuvizunguka vituo vya kupigia kura eti ili kulinda kura hakuna maana yoyote zaidi ya kutafuta namna ya kuhalalisha fujo, vurugu na uporaji na kuwazuia watu wengine, hasa wanawake, kupiga kura. Tunaviomba vyombo vya ulinzi na usalama vizuie hili jambo kwa sababu halina nia njema.
  Mkakati wa UKAWA ni kufanya vurugu baada ya kushindwa na kutengeneza mazingira ya mgogoro wa kisiasa ili Jumuiya ya Kimataifa iingilie kati na kupendekeza kugawana madaraka. Mkakati huo hautafanikiwa. Tunaviomba vyombo vya ulinzi na usalama vihakikishe ulinzi na usalama wa watu wote na mali zao siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi. 
  CCM haitakubali hata kidogo ushindi wake kuhojiwa au kutiliwa shaka kwa sababu tu ya vurugu zilizoanzishwa na watu wengine.
  Siku ya Jumamosi, CCM itatangaza namba maalum za simu kwa Watanzania wote ili siku kabla ya Uchaguzi, siku ya Uchaguzi na mara baada ya uchaguzi, waweze kupiga simu au kutuma ujumbe pale watakapokuwa wanabaini au kushuhudia vitendo vya kuvuruga amani na kuvuruga utaratibu mzima wa Uchaguzi. 

  Kupokea Matokeo
  CCM imeweka utaratibu wa kupokea matokeo kwa kutumia Mawakala wake moja kwa moja vituoni na kupitia mtandao wa Chama. CCM inategemea kuwa na matokeo ya Uchaguzi nchi nzima ifikapo saa nne usiku, siku ya Uchaguzi, tarehe 25 Oktoba 2015. 
  Imetolewa na:                                           

  January Makamba
  MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
  MJUMBE WA KAMATI YA KAMPENI
  22 OKTOBA 2015

  0 0


  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wafanyakazi wa mgodi mara baada ya kuwasili eneo la mgodi wa urani katika mradi wa mto mkuju wilaya ya namtumbo mkoa wa ruvuma Oktoba 21,2015.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua mgodi wa urani mkoani Ruvuma jana.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelekezo mara baada ya kuzindua mgodi wa urani mkoani Ruvuma jana.

  0 0  Serikali imetoa ufafanuzi kuhusu ukomo wa madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mwisho wa uhai wa Baraza la Mawaziri kwa kadri Tanzania inavyoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu unaofanyika Jumapili, Oktoba 25, mwaka huu, 2015.

  Taarifa iliyotolewa jioni ya leo, Jumatano, Oktoba 21, 2015, Ikulu, Dar es Salaam na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Yohana Sefue imesema kuwa Serikali imetoa ufafanuzi huo kuwasaidia wananchi kuelewa maelekezo na matakwa ya Katiba na Sheria kuhusu ukomo wa madaraka ya Rais na mwisho wa Baraza la Mawaziri kufuatia mijadala ya karibu katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.


  Taarifa hiyo imekariri Ibara ya 42(3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ambayo inasema kuwa ukiacha sababu nyingine, mtu anayechaguliwa kuwa Rais atashika madaraka ya kiti cha Urais hadi Rais Mteule atakapoapishwa.


  Ibara hiyo ya 42(3) inasema: ”Mtu anayechaguliwa kuwa Rais, atashika kiti cha Rais hadi – (a) siku ambako mtu anayemfuatia katika kushika kiti hicho atakula kiapo cha Rais.”


  Taarifa hiyo imesema: “Hivyo, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais anaendelea kuwa Rais, akiwa na madaraka na mamlaka yote na kamili yanayoambatana na nafasi hiyo, hadi Rais Mteule anakapokula kiapo cha Urais. Hivyo, ni vyema wananchi waelewe kuwa hakutatokea wakati wowote ambapo hakuna Rais na Amiri Jeshi Mkuu mwenye mamlaka kamili na aliye tayari kuyatekeleza mamlaka hayo. Lengo ni kuhakikisha kuwa haitokei wakati wowote nchi yetu ikakosa Rais na Amiri Jeshi Mkuu.”


  Imesisitiza taarifa hiyo: “Madaraka na mamlaka ya Rais yapo, na hayapugui kwa namna yoyote ile, hata baada ya Uchaguzi Mkuu, mpaka Rais Mteule atakapoapishwa.”


  Kuhusu ukomo wa Baraza la Mawaziri, taarifa imefafanua kuwa kwa mujibu wa Ibara ya  57(2) ya Katiba, Waziri na NaibuWaziri ataendelea kushikilia mamlaka ya nafasi yake hadi, ukiacha sababu nyingine, Rais mteule atakapoapishwa.


  Ibara hiyo 57(2) inatamka: “Kiti cha Waziri au NaibuWaziri kitakuwa wazi litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo – (f) Ukiwadia wakati wa Rais Mteule kushika madaraka ya Rais, basi mara tu kabla ya Rais Mteule hajashika madaraka hayo.”


  Taarifa hiyo imeongeza kuwa Mawaziri na NaibuMawaziri wanaendelea kushikilia nafasi zao, wakiwa na madaraka na mamlaka kamili yanayoambatana na nyadhifa zao hadi mara tu kabla ya Rais Mteule hajashika madaraka.


  Imemalizia taarifa hiyo: “ Naomba vyombo vya habari, vyenye jukumu la kuelimisha jamii, kuwaelewesha Watanzania kuhusu utaratibu huu wakubadilishana madaraka kati ya awamu moja ya uongozi wa nchi na nyingine. Madaraka na mamlaka ya Rais yapo, na hayapungui kwa namna yoyote ile, hata baada ya uchaguzi Mkuu mpaka Rais Mteule atakapoapishwa.”


  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu,

  DAR ES SALAAM.


  21 Oktoba, 2015


  0 0

   Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akipungia mkono kuwaaga wananchi baada ya kumalizika kwa mkutano wa kampeni za CCM katika viwanja vya Shule ya Msingi Bunju  A, Jimbo la Kawe, Dar es Salaam
   Dk Magufuli akiondoka kwenye viwanja hivyo huku ulinzi ukiwa umeimarishwa kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Binju A, Jimbo la Kawe, Kinondoni Dar es Salaam.
   Wananchi wa Kata ya Mlandizi, Jimbo la Kibaha Vijijini, wakishangilia kwa furaha baada ya kumuona Dk Magufuli.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  DSC_2410
  Moja ya eneo lililoaribika kutokana na hali ya mabadiliko ya tabianchi (Climate Change) katika fukwe ya Kilindoni, katika Kisiwa cha Mafia, Mkoani Pwani, nchini Tanzania. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).
  Afisa Mazingira Mafia
  Afisa Mazingira wa Wilaya ya Mafia, Bw. Gideon Zakayo.
  Na Andrew Chale, Modewjiblog
  [MAFIA-ISLAND] Kisiwa cha Mafia kijografia kipo karibu na mlango wa Mto Rufiji kusini mwa Tanzania.

  Hata hivyo, Kisiwa hichi ambacho ni Wilaya moja wapo ya Mkoa wa Pwani inakabiriwa kwa kiwango kikubwa na changamoto za Mabadiliko ya tabianchi hasa baada ya wananchi wake wengi kutopata elimu hiyo sahihi.

  Imeelezwa kuwa, elimu juu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika Kisiwa cha Mafia ambacho pia kinaunda visiwa vidogovidogo zaidi ya vitano, wananchi walio wengi katika kisiwa hicho bado hawajapata elimu sahihi ya kukabiliana na mabadiliko ya kimazingira (Climate Change).

  Mtandao huu ambao ulipiga hodi katika kisiwa hicho cha Mafia ili kupata habari za mabadiliko ya tabianchi na namna ya Mabadiliko ya tabianchi yanavyo athiri Kisiwa hicho (How Climate Change effects Mafia Island in Tanzania) ambapo iliweza kuzungumza na maafisa Ardhi, Mazingira na wananchi wa Wilaya hiyo, na kueleza haya:

  Kwa upande wa Afisa Mazingira wa Wilaya hiyo, Gideon Zakayo (pichani juu) amebainisha kuwa, Kisiwa cha Mafia kinakabiliwa na changamoto mbalimbali za Kimazingira ikiwemo hali ya Mabadiliko ya tabianchi huku suala la elimu kwa wananchi likiwa dogo kutokana na kutokuwa na fungu la kutosha.

  0 0


  Soud Rajab.
  Na Dotto Mwaibale
  MGOMBEA ubunge Jimbo la Mbagala kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Soud Rajab (pichani kushoto), amewaomba wananchi wa Jimbo la Mbagala wamchague ili aweze kuwaletea maendeleo waliyoyakosa kwa muda mrefu.  Rajab alitoa maombi hayo kwa wananchi hao Dar es Salaam jana wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wake wa kampeni wa lala salama kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika nchi nzima kesho.  "Ndugu wananchi nawaombeni sana msifanye makosa ambayo mtakuja kuyajutia kwa kipindi cha miaka mitano nawaombeni nichagueni niweze kuwaletea maendeleo mliyoyakosa kwa muda mrefu" alisema Rajab  Alisema jimbo la Mbagala kwa muda mrefu limesahulika kimaendelea hasa zile za kijamii nichagueni kupitia changu makini cha ACT-Wazalendo niweze kuwatumikia.  Rajabu alisema endapo atachaguliwa atahakikisha anapunguza gharama za  huduma za jamii zikiwemo za hospitalini.  Alitaja gharama hizo kuwa ni zile zinahusisha wajawazito wanaokwenda kujifungua kwa kupata mahitaji muhimu kwani hajaona umuhimu wa kwenda na mabegi ya nguo wakati wa kujifungua pamoja na kupunguza foleni kwa asilmia 80.  Alisema katika kuboresha afya za wananchi hao atahakikisha anaboresha hospitali zilizopo katika jimbo hilo kutolewa huduma zake zinazofanana na hospitali ya Temeke.  "Ninafahamu mazingira ya watu wa mbagala hivyo nahitaji kutatua kero zenu za barabara, kwa kutanua barabara za mitaa ikiwa ni kuondoa foleni kupungua kwa aslimia 80,"alisema.  Alisema kutokana na kutanua barabara hizo pia atajenga kituo kikubwa cha kisasa cha sanjari na kila kata kuwa na kituo cha afya na kuongeza kuwa kutokana na wananchi wa jimbo hilo kuwa wengi hali ambayo haina uwiano na huduma muhimu kama masoko ataboresha na kuwa la kisasa.  "Soko la Zakhem serikali inasema ni mali yao huku wafanyabiashara wa sokoni hapo wanalipa kodi ya sh.30,000, nikipata nafasi ya ubunge soko hilo litakuwa mali ya umma ili liwaletee uchumi wananchi,"alisema.   (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii

  0 0


   Rais Kikwete (Kushoto) na Ridhiwan Kikwete (Kulia).

  MKAZI wa mjini Moshi, Kyefa Joachim Makundi (33), amepandishwa kizimbani akikabiliwa na mashitaka ya kumtukana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya  Kikwete.

  Mbali na shitaka hilo, mshitakiwa huyo amesomewa shitaka lingine la kumtukana Ridhiwan Kikwete ambaye ni mtoto wa Rais Kikwete ambaye pia ni Mbunge wa Chalinze anayemaliza muda wake.

  Mshitakiwa huyo amefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya mkoa Kilimanjaro, Joachim Tiganga na kusomewa mashitaka hayo na wakili wa Serikali Kanda ya Moshi, Agatha Pima.

  Wakili Pima amedai mahakamani kuwa Oktoba 17 mwaka huu katika baa ya Harambee iliyopo katikati ya mji wa Moshi, mshitakiwa alitumia lugha ya matusi dhidi ya Rais Kikwete na mwanae Ridhiwan.

  Ingawa matusi hayo hayakuandikwa kwenye hati ya mashitaka, lakini wakili Pima amedai kitendo hicho ni kinyume cha kifungu 89(1) (a) cha kanuni ya adhabu kama kilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

  Chini ya kifungu hicho, mtu yeyote anayetumia lugha ya matusi, kuudhi, au kudhalilisha dhidi ya mtu mwingine katika hali ambayo inaweza kusababisha uvunjifu wa amani anatenda kosa la jinai.

  Adhabu inayotolewa kwa mtu anayepatikana na hatia katika kosa hilo ni kifungo cha miezi sita jela.

  Hata hivyo, mshitakiwa amekana shitaka hilo ambapo mahakama imesema dhamana ilikuwa wazi ikiwa mshitakiwa atakuwa na wadhamini wawili watakaosaini hati ya dhamana ya Sh1.5 milioni kila mmoja.

  0 0

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi, Charles Mkumbo
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi, Charles Mkumbo.

  JESHI la Polisi mkoani Mwanza, limesema halipo tayari kukipendelea chama chochote kile cha siasa katika kipindi hiki cha uchaguzi utakaofanya Oktoba 25 mwaka huu.
  Kauli hiyo imetolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi, Charles Mkumbo, wakati akizungumza na wanahabari.

  Mkumbo amesema kuwa katika kipindi hiki, jeshi halitakuwa tayari kukipendelea chama cha siasa kwani lipo kwa ajili ya kutenda haki na kulinda raia.

  Amesema kuwa wananchi wamekuwa na dhana na imani potofu ya kwamba Polisi hupendelea baadhi ya vyama vya siasa, ambavyo ndivyo sivyo na kwamba Wananchi wanapaswa kuwa na imani na Jeshi hilo.

  “Tutafanya kazi kwa kufuata sheria na pale tutakapo ona uvunjifu wa amani unatoweka hatusita kuongeza nguvu ya Polisi.

  “Kama ulivyoniuliza kwamba kuna upendeleo wa chama tawala, kitu hicho hakitakuwepo sasa hivi, hata juzi pale Nyegezi wafuasi wa Chadema na CCM walitaka kuleta fujo tulifika na kudhibiti,” amesema Mkumbo.

  Sanjali na hayo pia Mkumbo aliyaonya makundi ya watu yatakayofanya fujo siku ya uchaguzi kuacha Mara moja kwani hayatafumbiwa macho, yatachukuliwa hatua za kisheria.

  Mkumbo amesema kuna vikundi vichache vilivyoandaliwa na baadhi ya vyama vya siasa ili kuwafanyia fujo wazee na wanawake siku ya uchaguzi na kwamba wanaendelea kufanya uchunguzi ili kuyadhibiti mapema. 

  0 0

  Mke wa Mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa, Regina Lowassa akiwa katika mkutano wa hadhara
  Mke wa Mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa, Regina Lowassa akiwa katika mkutano wa hadhara.

  BARAZA la Wanawake la Chama Cha Demokrasia (Chadema) Taifa, Bawacha, limewataka wanawake nchi nzima kupiga kura na kukaa mita 200 ili kulinda kura zao kwani ni haki yao kisheria.
  Kauli hiyo imetolewa jana na Naibu Katibu Mkuu wa Bawacha Kunti Yusuph wakati wa mkutano na wanawake, uliofanyika katika ofisi za Chadema kanda ya ziwa Victoria jijini hapa.

  Kunti ambaye ni mratibu wa mikutano ya kukutana na wanawake ya mke wa Mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa, Regina Lowassa, amesema kuwa kupitia wanawake wa Mwanza, wanawake nchi nzima wanapaswa kupiga kura na kulinda kura zao.

  Amesema endapo wanawake na watanzania kwa ujumla watapiga kura na kuondoka watakuwa wamevunja sheria ya nchi hivyo amewaomba kulinda kura zao kwani ndio maisha yao.

  Hata hivyo Regina aliwaomba wanawake na watanzania kwa ujumla kupiga kura kuanzia ngazi ya Udiwani, Ubunge na nafasi ya Urais kwa maendeleo ya Taifa. 

older | 1 | .... | 1007 | 1008 | (Page 1009) | 1010 | 1011 | .... | 3278 | newer