Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1006 | 1007 | (Page 1008) | 1009 | 1010 | .... | 3285 | newer

  0 0
 • 10/21/15--02:29: BEI YA MADAFU HII LEO


 • 0 0  0 0

  Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania Mkoa wa Mjini Bi Waridi Juma akisoma risala ya Wanawake wa Mkoa wa Mjini wakati wa mkutano na Mke wa Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, Mama Mwanamwema Shein, uliofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya Mkoa wa Mjini Amani Zanzibar.
  Viongozi wa UWT Mkoa wa Mjini Unguja wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, wakati wa mkutano wake na Viongozi hao uliofanyika Afisi ya CCM Mkoa Amani Zanzibar.
  Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Salama Aboud Talib akizungumza wakati wa mkutano huo na kuwakaribisha Viongozi wa Ujumbe wa Kampeni ya Mama Mwanamwema Shein, kuzungumza na Viongozi wa UWT Mkoa wa Mjini Unguja. 
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Wizara hiyo, jijini Dar es salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  Ndugu Waandishi wa Habari, Mabibi na Mabwana,
  Kama mnavyojua tarehe 25 ya mwezi huu wa Oktoba mwaka 2015 siku ya Jumapili katika nchi yetu kutafanyika Uchaguzi Mkuu kwa ajili ya kuchagua rais, wabunge na madiwani zoezi ambalo litawashirikisha watanzania wote waliojiandikisha kupiga kura kwa mujibu wa sheria.


  Zoezi hili kwa mujibu wa sheria za uchaguzi litasimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi yaani NEC kama ambavyo imekuwa ikifanyika katika chaguzi mbalimbali zilizopita ama kuwahi kufanyika katika nchi yetu.


  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inalo jukumu kubwa la kuhakikisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao unaimarishwa kabla, wakati na baada ya zoezi hilo la Uchaguzi Mkuu katika maeneo yote ya nchi yetu, ili wananchi waweze kuwa salama na kuendelea na maisha yao ya kila siku.

  Ndugu Waandishi wa habari,


  Kumekuwepo na taarifa mbalimbali za vitisho zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na hata mitaani na watu wasio na nia njema kwa taifa letu,  zikiwataka wananchi wanunue mahitaji yao mbalimbali ikiwemo vyakula na kuvihifadhi kwa ajili ya kuja kuvitumia wakati na baada ya uchaguzi kwa ubashiri wa kuwepo kwa vurugu wakati ama baada ya uchaguzi.


  Taarifa hizi zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na mitaani kwa ujumla ni taarifa potofu ambazo zinalenga kuwajengea wananchi hofu na mashaka, wasiwasi na vitisho pasipo sababu zozote zenye tija kwa taifa letu.

  Ndugu zangu Waandishi wa habari,

  Nitoe rai kwa Raia wote waishio hapa nchini yaani Watanzania na Wageni kupuuza taarifa zote zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na mitaani kwa kuwa taarifa hizo si za kweli, na wala hazilengi kulinda amani iliyopo nchini kwetu.  

  0 0


  0 0

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Makame Mbarawa, kwa pamoja wakifunua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa Kituo cha kutunzia kumbukumbu cha Taifa (National Internet Data Centre) Kijitonyama, leo Okt 21, 2015. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Makame Mbarawa (kushoto) na Mwakilishi wa Ofisi ya Uchumi na Biashara ya Serikali ya China, nchini Tanzania, Lin Zhiyong,  kwa pamoja wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kituo cha kutunzia kumbukumbu cha Taifa (National Internet Data Centre) Kijitonyama, leo Okt 21, 2015.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa hafla ya uzinduzi huo baada ya kuzindua rasmi leo Okt. 21, 2015 Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.
  Picha na OMR

  0 0

  Huu ni uchambuzi wa Habari toka vituo mbalimbali vya Televisheni 
   Oktoba 21, 2015.

  Chama Cha soka Jijini Mwanza Kwa kushirikiana na wanamichezo wamefanya mazoezi maalumu  kwaa lengo la kutoa elimu Juu Ya Amani Na Upigaji Kura.  https://youtu.be/Pb-8yIRPV1w
      
  Upungufu Mkubwa wa Damu Katika benki ya Hospitali ya Taifa Muhimbili wachangia mrundikano wa wagonjwa hasa wa upasuaji. https://youtu.be/zhI0gAASoSo
      
  Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi toka Jumuiya Ya Afrika Mashariki EAC imezinduliwa jijini Dar na kuahidi kufanya kazi kwa kufuata misingi ya Sheria za nchi. https://youtu.be/mJv-qJF7p_0

  Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wameendelea na uhakiki wa majina yao katika daftari la wapiga kura huku baadhi ya makaratasi kuchanywa. https://youtu.be/dO23f6qH184

  Ligi Kuu soka Tanzania Bara Inatarajiwa kuendelea leo ambapo Klabu Ya Yanga itamenyana na Toto Africans Ya Mwanza uwanja wa Taifa Dar. https://youtu.be/Qy6kNPakAKo

  Kutana na mabalozi wa amani Christina Shusho pamoja na Mrisho Mpoto  wakizungumzia swala zima la amani kuelekea uchaguzi mkuu;  https://youtu.be/6WJLNbNd3L8

  Je uwepo wa viwanja vipya  utasaidia kukuza vipaji katika michezo mbalimbali nchini? Fuatilia mjadala hapa;https://youtu.be/Zb9Xt-C6hWc

  Leo hii katika mjadala wachambuzi wanaangaliza habari kuu zilizopewa vipaumbele katika taarifa za habari; https://youtu.be/xKyPA5UdOqo
  Je ahadi za wagombea zinazotolewa kwenye majukwaa zinatekelezeka? Fahamu zaidi kupitia mjadala wa leo; https://youtu.be/6WYVHA9qnJc

  Fahamu chama cha  APPT Maendeleo na mikakati ya chama hicho katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika jumapili tareh 25 Octoba, https://youtu.be/Iq7qQpu4x70
  0 0

  Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi iliyofanikisha upatikanaji wa Gari  la zimamoto, Mussa Bibose akitoa maelekezo kwa wananchi waliohudhuria shughuli ya kukabidhi gari hilo Kibada,Kigamboni  Jijini Dar es salaam. 

  Mwenyekiti wa Umoja wa wananchi wa Kibada, Kigamboni Jijini Dar es salaam Bwana Lagano Mwampetu akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya gari moja ya zimamoto iliyopatikana kwa Juhudi za umoja huo na kukabidhi kwa  Kamishna wa Operation Jeshi La Zimamoto na uokoaji Tanzania CF, Rogatus Kipali.

  Kamishna wa Operation Jeshi La Zimamoto na uokoaji Tanzania CF, Rogatus Kipali akiangumza na wananchi waliojitokeza wakati wa kukabidhi Gari hilo ambapo amewapongeza wananchi wa Kibada kwa juhudi kubwa za kuhakikisha kuwa wanaleta maendeleo katika maeneo yao.

  Mwenyeikiti wa umoja wa wananchi wa Kibada, Kigamboni Jijini Dar es salaam Lugano Mwampeta akimpa maelekezo kamishna wa Operation jeshi la zimamoto na uaokoaji Tanzania CF, Rogatus Kipali wakati wa shughuli ya kumkabidhi gari moja la kuzima moto lililofanyiwa matengenezo kwa nguvu ya wananchi wa kibada kwa ajili ya kuwasaidia wakazi hao na majanga ya moto,makabidiano hayo yaliyofanyika Kigamboni Kibada Jijini Dar es salaam.

  Gari la Jeshi la Polisi la zimamoto lilofanyiwa matengenezo na wananchi wa Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam.


  0 0

   Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano  kongamano la kuchochea uzalishaji mali, Prof.Leonard  Mwaikambo akizungumza na waandishi wa habari juu ya lengo la kongamano ni kutoa fursa kwa watanzania kwa jumla kuelewa malengo na mwelekeo wa taifa letu kufikia uchumi wa kati .
  Waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano  Profesa,Leonard  Mwaikambo.

  Na Emmanuel  Massaka ,Globu ya Jamii
  RAIS Dk. Jakaya  Kikwete   anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano la kuchochea uzalishaji mali katika kuinua kipaato cha mtanzania  wa kawaida kufikia malengo ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 litakalofanyika kesho katika Ukumbi Diamond Jubilei jijini Dar es Salaam.

  Hayo ameyasema leo  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano  Prof.Leonard  Mwaikambo kongamano hilo litakuwa na watoa maada mbalimbali na wataalam katika sekta ambazo zitafanya kufikia uchumi huo.

  Profesa Mwaikambo amesema kuwa wakati huu kutokana na harakati za uchumi kunahitajika wataalam ambao wamebobea kwa kuleta  maendeleo hayo ambayo watanzania  wanayoyataka kwa kukuza kipato.

   Amesema kongamano hilo linagusa nyanja zote katika sera za vyama hivyo ni muda mwafaka wa kujadili masuala ya uchumi ni ya msingi katika ukuza ji kipato kwa wananchi.

  Aidha amesema  wanataaluma hao watatoa mchango wao katika maswala ya kijamii na sekta mtambuka , Utawala Bora ,na Mawasiliano ya kielektroniki kwa ukuzaji wa maendeleo watanzania ,Miundombinu ,Afya ,Maji, Elimu pamoja na ujenzi .

  Majadiliano yataongozwa na Waziri Mkuu Mstaaf,Jaji Mstaafu,Joseph Sinde Warioba na neno la shukrani litatolewa na Waziri Mkuu,Mstaafu, John Malecela .

  0 0

   Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini . Jaji Francis S. K  Mutungi akizungumza na Waangalizi wa  uchaguzi Mkuu  kutoka Bunge la Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi hiyo jana Oktoba 21,2015.
   Baadhi ya Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Bunge la Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)
  kushoto ni Msajili Msaidizi Usajili wa Vyama vya Siasa Bw. Sisty Nyahoza akielezea utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa , kulia ni Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji francis Mutungi.
  Picha ya pamoja ya Jaji  Francis S.K Mutungi , Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Bunge la Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na baadhi ya watumishi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

  0 0

   Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akizungumza na waandishi wa habari leo baada ya taasisi hiyo kufanikiwa kuwafanyia upasuaji watoto 37.
   Mkuu wa Kitengo cha Moyo cha Watoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Godwin Shirau akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matatizo mbalimbali ya moyo.
   Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakimsikiliza Profesa Mohamed Janabi leo katika hospitali hiyo. 

  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) kupitia Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (Jakaya Kikwete Cardiac Institute  (JKC) imefanikiwa kuokoa zaidi ya Shilingi mIlioni 800 baada ya kuwafanyia upasuaji wa moyo watoto  37 wenye matatizo ya moyo .


  Operesheni hiyo imefanyika kuanzia Oktoba  10 hadi 19 mwaka huu kwa kushirikisha timu ya wataalam  18 kutoka nchini Italy na  Marekani  pamoja na madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka taasisi hiyo.


   Kaimu Mkuu wa taasisi hiyo Profesa Mohamed Janabi amewaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kwamba  endapo wagonjwa hao wangetibiwa nje, kila mmoja yangegharimu kati ya Dola za Kimarekai 10,000 hadi 15,000, gharama ambazo Watanzania wengi hawawezi kuzimudu.

  Kwa mujibu wa Profesa Janabi,  changamoto inayowakabili ni upatikanaji wa damu  na upungufu wa watalaam.


  Alifafanua kwamba hivi sasa kuna orodha ya watu 500 ambao wanasubiri kufanyiwa upasuaji wa moyo, na kwamba desemba mwaka huu, wanatarajia  kupokea wagonjwa wenye matatizo ya moyo  kutoka nchini Zambia.


  Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Moyo cha Watoto, Dk. Edwin Shiran amesema watoto 17 wamefanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na wengine 20 wamewekewa kifaa maalum kwa ajili ya kuziba matundu na kuzibua  mishipa ambayo  imezibana  na kwamba kati ya hao watoto wawili wametokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).


  Tangu Januari mwaka huu tayari wamekwishafanyiwa upasuaji wa moyo watoto 122 na watu wazima 132 .

  0 0
 • 10/21/15--21:04: IJUE NAMNA YA KUKATA RUFAA.
 • NA  BASHIR  YAKUB -
  Unaposhindwa  kesi  sio  mwisho  wa kusaka  haki. Hii  ni  kwasababu  kushindwa  kesi  kunatokana  na  sababu  nyingi . Si  kweli  kuwa  kwakuwa  umeshindwa  kesi  katika  mahakama  fulani  basi  maana  yake  ni  kuwa  ulikuwa  huna  haki. Yawezekana  kabisa  haki  ilikuwa  yako  isipokuwa  umeshindwa  tu  kutokana  na  sababu  nyingine  za  kiutaratibu na  kimbinu (procedures & technicalities).  Pia  waweza  kuwa  umeshindwa  kutokana  na  uwezo  mdogo  wa  kujieleza  na kushindwa  kugusa  nukta  muhimu  ambazo  kimsingi  ndizo  zilizokuwa zinabeba   shauri  lako. 

  Lakini  pia  waweza  kuwa  umeshindwa  kwasababu  ya  hila  na  mbinu  chafu. Na  hii  wakati  mwingine  huwahusisha  hata  waamuzi yaani mahakimu  na  majaji.  Basi  ifahamike  kuwa  ni  sababu  hizi   zilizopelekea  kuwepo  utaratibu  wa  rufaa  ili  yule  anayehisi  kutotendewa  haki  aende mbele  ili  kuona  kama anaweza  kupata  haki  yake  huko.


  1.RUFAA  NININI.
  Rufaa  ni  hatua  ya  kisheria  ya  kupeleka  malalamiko  katika  hatua  ya  mahakama  ya  juu  zaidi  baada  ya  mmoja  wa  wahusika  katika  kesi  iliyoisha  kutoridhishwa  na  hukumu/maamuzi. Ili  ukate  rufaa  ni  lazime uwe  ulikuwa  mhusika  katika  kesi  iliyoisha  na  uwe  na sababu  za  kwanini  unadhani hukuridhishwa  na  maamuzi.  Sababu  yoyote ya  msingi  inakubalika.


  0 0

  Mpango kwa ajili ya watoto wadogo ipo mstari wa mbele katika vita dhidi ya umasikini. Watoto katika jamii zilizo masikini sana wamo katika hatari kubwa za kupata maradhi na utapiamlo na hawafanyi vizuri shuleni. 

  Mipango jumuishi ya watoto wadogo inayolenga watoto walio masikini sana huzisaidia familia kuwa na mwanzo mzuri wa watoto wao na husaidia kupunguza pengo kati ya masikini na matajiri. Uwekezaji kwa watoto wadogo una faida mara saba na una thamani kuliko kuwekeza kwenye mipango ya kunusuru maisha ya mtoto hapo baadaye.

  Wazazi fukara wapatiwe msaada wanaohitaji ili kuhakikisha kuwa watoto wao wanakuwa na mwanzo mzuri zaidi katika maisha. Msaada kwa ajili ya miradi ya kijamii ya kulea watoto na ya maendeleo na makuzi ya awali ya watoto itasaidia katika kuhakikisha kuwa watoto wanakua wakiwa na afya, wanapata lishe bora na wametayarishwa vizuri kwenda shule.

  Maendeleo ya watoto wadogo yaingizwe katika muhtasari wa mafunzo kazini ya walimu. Yaanzishwe mafunzo kazini ya kitaifa kwa wote wanaohudumia watoto wadogo. Wale wanaofanya kazi katika jamii fukara wapewe kipaumbele katika mafunzo haya.

  Zianzishwe kamati za kijamii katika ngazi ya wilaya na kata ambazo zitafuatilia upatikanaji wa huduma na kusaidia uboreshaji wa vituo vya kumwendeleza mtoto akiwa mdogo.

  #AjendaYaWatoto

  0 0

  Ndugu  Issa BAtenga wa Dar es salaam anapenda kuchua nafasi hii kwa niamba ya familia kutoa tangazo kuwa Mwili wa Marehemu wa mama/shangazi/bibi yetu TAMALI LEBI MWAKYOMA.unawasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam alasiri ya leo Jumatano saa 9 kutoka India  na ndege ya Emirates. 

  Utaratibu ni kwamba Mwili huo utapelekwa moja kwa moja kwenye Hospitali ya Aghakhan kwa ajili ya kuhifadhiwa na Maandalizi..
  Taarifa hii ni kutokana na Kuvurugika kidogo kwa Ratiba za ujio wa watoto wa Marehemu waishio Marekani ambao utasababisha kukawia kwao kuwasili Tanzania, kwa kuzingatia haya na pia endapo watawasili siku ambazo hazitaendana na ratiba tulizozipanga hapo awali, ni dhahiri kwamba mwingiliano wa safari ya kwenda Mbeya-Tukuyu, mazishi na safari ya kurudi Dar es Salaam kabla ya Jumapili itakuwa imewakosesha waombolezaji na wafiwa haki zao za msingi za kupiga Kura siku ya Jumapili 25/10/2015. 


  kwa hivyo na kwa kuzingatia haya, Tumeona ni busara tutoe tamko rasmi kwa kauli moja la kuahirisha Mazishi haya hadi tarehe ya karibu ambayo tutaipanga baada ya Uchaguzi.

  Kwa ramani, Msiba upo barabara ya Rose Garden Mikocheni. kwa kutumia njia ya kutokea kwa Mwalimu Nyerere ni baada ya uzio wa TPDC/ Njia iendayo Data vision. Kuna kibao. 


  Na kwa Barabara ya kutokea Maji Machafu/Sayansi, ni kwenye njia mita 100 kandokando ya je go la Tume ya Vyuo Vikuu (Commision of High learning Institutions) 
  Tunawashukuru kwa uvumilivu na kwa kutufariji kila siku. 
  Mungu Awabariki na awape nguvu wafiwa.

  0 0


                                                                             
    2.0Taarifa hii si ya ukweli na ni ya upotoshaji,Mhe Jaji Mkuu hajawahi kuzungumzia chochote kuhusu sheria hiyo ukitilia maanani kesi hiyo iko Mahakama Kuu shauri Namba 37 ya 2015 iliyofunguliwa na Bi. Amy Kibatala dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Mkurugenzi wa Uchaguzi (DE) na itatolewa maamuzi kati ya tarehe 22 au 23 mwezi huu. Hivyo, kwa mujibu wa sheria Mhe.Jaji Mkuu asingeweza kuzungumzia chochote kuhusu sheria hiyo kwa kuwa suala hilo liko MAHAKAMANI.                                                                                

    3.0 Tulimwandikia Mkurugenzi wa Habari MAELEZO nakala East Africa Television na kufuatilia kwenye Baraza la Habari (Media Council) kuomba maelezo ya kina na usahihi wa taarifa hiyo,  tarehe 21/10/2015 tumepokea barua Kumb Na EATV/ADMN/096/10/2015 ilyosaniwa na Bi Regina Mengi Mkurugenzi Mtendaji wa East Africa Television akiomba msamaha kuhusu taarifa hiyo potofu na kuwa watatoa maelezo ya ziada kuwa, taarifa hiyo haikutolewa na Mhe.Jaji Mkuu wa Tanzania

      Tunashukuru kwa ushirikiano mkubwa tulioupata toka uongozi wa juu kabisa wa East Africa Television kwa kuomba radhi mapema na Tunamini kuwa, vyombo vya Habari na Wananchi kwa ujumla vitasitisha usambazaji wa taarifa hii iliyokuwa si sahihi.

                                                                                                                                   Barua ya kuomba radhi imeambatanishwa:


   Imetolewa na:                     
  MTENDAJI MKUU WA MAHAKAMA

                                                
  MAHAKAMA                                                                   YA TANZANIA  0 0

  Kesi ya mita 200 moto, Lowasa sasa atishia kushtaki jeshi la polisi ICC. GP Hamdan awaonya waoandaa vurugu. Ni katika magaazeti ya leo Octoba 22.2015;https://youtu.be/TkIYjEUaJyw
   Yanga acha kabisa, Chipukizi Simba kutimukia Ubelgiji, Ndemla afunguka. Nyoso atafutiwa mbadala. Kwa habari hizi na nyingezo za michezo utazipata katika udondozi wa magazeti hapa Simu.tv ; https://youtu.be/yL4C4fUOPgo
   Rais Kikwete asema wanaimarisha jeshi ili kulinda mipaka ya nchi, NHIF yapania makubwa. Pata habari za kina hapa Simu.tv; https://youtu.be/eE10aUBwMHU

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (kulia) akimkaribisha Balozi mpya wa Misri, Mhe. Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf katika ofisi yake. Balozi Mpya wa Misri alikuja ofisini kwa Mhe. Waziri kwa ajili ya kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mpya wa Misri, Mhe. Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0  OFISI Usambazaji na Ugavi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Eliud Njaila akiwaonyesha waandishi wa habari vizimba vya kupigia kura siku ya uchaguzi. 
  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema wapiga kura waliopoteza kadi zao za kupigia kura hawataruhusiwa kupiga kura katika uchaguzi utakaofanyika nchini kote siku ya Jumapili.

  Akizungumza katika mkutano wa vyama vya siasa na NEC mjini Dodoma leo, Ofisa Mwandamizi wa tume hiyo William Kitebi, amesema watu hao hawataruhusiwa hata kama majina na taarifa zao zipo kwenye Daftari la Wapiga Kura (BVR).

  “Hakuna jinsi ya kuwasaidia watu waliopoteza kadi zao za kupigia kura ,”amesema Kitebi
  Hata hivyo, Kitebi amesema kutokana na kasoro zilizojitokeza kwenye BVR  kuna baadhi ya mambo NEC wameyawekea utaratibu ili watu waweze kupiga kura.

  Amesema watu ambao namba za kadi zinatofautiana na zile zilizopo kwenye BVR  lakini taarifa nyingine ni sahihi wataruhusiwa kupiga kura.

  “Kuna wale ambao picha zao hazionekani kwenye daftari lakini kadi za kupiga kura wanazo, hawa wataruhusiwa kupiga kura,”amesema.
  Kuhusu wale wapiga kura walioathiriwa na mipaka ya utawala, Kitebi amesema maamuzi ya tume kuwa watu hao watapiga kura kwenye kata walizopo.

  “Kuna maeneo kulikuwa na mabadiliko ya mipaka ya kiutawala baada ya zoezi la uandikishaji kama Kishapu (Shinyanga) na Kaliuwa (Tabora), wao wataruhusiwa kupiga kura kwenye maeneo yao mapya,”amesema.

  Kwa upande wa wapiga kura ambao wanakadi za kupigia kura lakini hawaonekani kwenye BVR, Kitebi amesema hao wamewekewa utaratibu utakaowawezesha kupiga kura.


  “Kama kule Mbarali (Mkoa wa Mbeya), kuna watu kama 6,000 ambao hawaonekani katika daftari lakini wanakadi na fomu zao zimejazwa na kuwasilishwa tume  hawa wanaruhusiwa kupiga kura,”amesema.

  0 0

   Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Saz Salula, akizungumza kutoa shukurani wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa ajili ya Mhe. Makamu wa Rais kuagana na Watumishi wa Ofisi yake. Hafla hiyo ilifanyika juzi Okt 20, 2015 kwenye Makazi ya Dkt. Bilal
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Katibu Mkuu wa Ofisi yake, Saz Salula, wakati wa hafla fupi ya kuagana na watumishi wa ofisi yake, iliyofanyika Oysterbay jijini Dar es Salaam, juzi Okt 20, 2015.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib BIlal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Ofisi yake baada ya hafla hiyo.
   Picha na OMR
  MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal amewashukuru watumishi wa ofisi yake kwa ushirikiano waliompa katika kipindi chote cha miaka mitano kiasi cha kuweza kutekeleza majukumu ya msingi ya ofisi hiyo ya kudumisha Muungano na uhifadhi wa mazingira kwa ufanisi mkubwa.

  Akizungumuza katika hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika jana jijini Dar es salaam Dkt. Bilal alisema kuwa, anayo furaha kufikia kipindi hiki na kwamba alifanya majukumu yake vema kutokana na kuwa na wasaidizi mahiri na waliojitoa kufanya kazi zao kwa weledi na uvumilivu mkubwa muda wote.

  “Natumia nafasi hii kuwashukuru Watanzania wote. Walinisaidia sana katika kipindi nikifanya kazi ya kuitumikia nchi yangu. Niwashukuru ninyi wafanyakazi wa ofisi yangu, mlifanya kazi kwa kujituma sana na majukumu yetu kwa mujibu wa taratibu tuliyatekeleza kwa ufanisi,” alisema 

  Mheshimiwa Makamu wa Rais na kuongeza:
  “Nakutakieni kila la kheri katika utendaji wenu. Jitahidini kufanya kama mlivyofanya kwangu kwa yule atakayekuja baada yangu. Nakushukuruni kwa zawadi hasa ya vitabu maana mimi ni muumini wa kusoma, nitavisoma”.

  Dkt. Bilal aliwaambia watumishi hao kuwa ushirikiano waliompa katika utendaji wa kazi umewezesha  kuzipatia ufumbuzi hoja mbali mbali za muungano na kusema hoja zilizobaki zinafanyiwa kazi na zitapatiwa ufumbuzi katika serikali ijayo.

  Hoja ambazo zipo katika hatua mbalimbali za kutafutiwa ufumbuzi ni pamoja na Hisa za SMZ zilizokuwa katika Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki na Mgawanyo wa Mapato yatokanayo na Faida ya Benki Kuu; Usajili wa vyombo vya moto, Uchimbaji na Utafutaji wa Mafuta na Gesi Asili na Mapendekezo ya Tume ya Pamoja ya fedha.

  Kwa upande wa mazingira alisema katika kipindi chake Tanzania ilipata nafasi ya kuwa Mwenyekiti wa Masuala ya Mazingira kwa viongozi wa Bara la Afrika jambo ambalo limewezesha nchi kutoa mchango mkubwa katika suala zima la uhifadhi na usimamizi wa mazingira katika Bara la Afrika.

  Hata hivyo, Dkt. Bilal alionyesha wasiwasi wake katika eneo la usafi wa mazingira na kuwataka watumishi wa ofisi hiyo kushirikiana na taasisi nyingine katika kuhakikisha usafi wa mazingira unapewa kipaumbele katika maeneo yote nchini.

  Mapema, akizungumza katika hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula alimshukuru Makamu wa Rais kwa uongozi wake ambao umekuwa mwongozo kwa watumishi katika utendaji wao wa kazi na kumtakia kila la heri katika kipindi cha kustaafu kwake.

  Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
  Dar es salaam.

  0 0

  Huu ni uchambuzi wa Habari toka vituo mbalimbali vya Televisheni Asubuhi Hii October 22, 2015.

  SIMUtv: Fuatilia mwenendo na uchambuzi wa kampeni za vyama mbalimbali za lala salama baada ya kusalia masaa 48 kuelekea uchaguzi Mkuu mwaka  huu

  SIMUtv: Katibu wa chama cha madereva TADU, Rashid  saleh akizungumzia vitendo vya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji kuwaadhibu madereva: https://youtu.be/ne2li6v5HN8

  SIMUtv: Tambua namna ambayo Nchi imejiandaa kulinda amani siku ya uchaguzi zikiwa zimesalia takribani masaa 48 kuifikia siku hiyo maalumu: https://youtu.be/dK2fdWR1jS0
    
  SIMUtv: Fuatalia mazungumzo na viongozi wa dini wakihamasisha amani  katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu ikiwa zimesalia siku 2: https://youtu.be/-JyP0slzlIc
    
  SIMUtv: Fuatilia vipaumbele vinavyotiliwa mkazo zaidi na mgombea udiwani kata ya Mwananyamala jijini Dar es salaam kupitia chama cha ACT https://youtu.be/61OyRSbdgEI

  SIMUtv: Mamlaka ya Chakula Na Dawa TFDA imezindua mfumo mpya wa utoaji na usajili wa vibali kwa njia ya kieletroniki.   https://youtu.be/EKpX7i9iUpg
     
  SIMUtv: Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kesho itatoa maelekezo maalumu juu ya Madai Ya Upinzani  kukaa Mita 200 kusubiri matokeo. https://youtu.be/NniBsA0A4uA
    
  SIMUtv: Mgombea Uraisi CCM Bi. Samia Suluhu awaahidi wananchi wenye ulemavu kushirikiana na serikali katika shughuli za kimaendeleo. https://youtu.be/YpieDVjInjo

   SIMUtv: Serikali imesema itaimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao kabla, wakati na baada ya uchaguzi utakaofanyika oktoba 25. https://youtu.be/MIxU_FaGfQs
    
  SIMUtv: Mgombea Uraisi CHADEMA Mhe. Edward Lowassa aahidi kurudia upya mchakato uliotumika kubadili matumizi ya Fedha kwa ajili ya kuboresha bandari ya Tanga. https://youtu.be/pN50aOZzqr8
    
  SIMUtv: Mgombea Uraisi CCM Dkt. Magufuli amewaahidi wananchi wa Dar es Salaam kushughulikia mradi mkubwa wa maji na kuondoa kero hiyo. https://youtu.be/-Zb1ocoEOjo

  SIMUtv: Siku 3 zimesalia kabla ya uchaguzi mkuu wa wabunge na madiwani  kufanyika  lakini kasi ya wananchi yaelekezwa katika Wagombea Uraisi pekee https://youtu.be/AGUCEprc9pc


older | 1 | .... | 1006 | 1007 | (Page 1008) | 1009 | 1010 | .... | 3285 | newer